Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Answers to supplementary Questions by Hon Omary Juma Kipanga (360 total)

MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini pia ningeomba niende mbele zaidi kwa sababu uhalisia unaonesha wanafunzi wanaosoma shule za binafsi hawapati mkopo either wote au kiasi, lakini pia kwa sababu ya umuhimu wa baadhi ya fani kama udaktari na gharama kubwa ya kusomesha watoto kwenye fani hizo, Serikali inaonaje kuwa na mpango wa muda mrefu ili wanafunzi wote wameweze kupata mikopo kwa asilimia mia moja?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, kama ilivyotokana na jibu langu la msingi, Serikali inaendelea kupanua wigo wa bajeti katika Bodi yetu ya Mikopo. Kwa hiyo naomba nilichukue suala la Mheshimiwa Mbunge kwa vile kutoka mwaka 2017, Serikali imeweza kuongeza bajeti katika bodi ya mikopo kutoka bilioni 427 mpaka hivi sasa tuna bilioni 460. Kutokana na hivyo basi, wanufaika ni wengi na wanaendelea kuongezeka kutoka wale laki moja katika kipindi cha mwaka 2015 mpaka kufikia laki moja na arobaini mwaka 2021.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tunapoongeza bajeti hii tuna hakika tunaweza kufanya coverage kubwa ya wanafunzi. Naomba kutoa taarifa katika waombaji wa mwaka huu wale wa mwaka wa kwanza maombi yote yalikuwa 66,000, lakini waliopata jumla karibu walikuwa 55,000. Kwa hiyo tunaendelea kuongeza ule wigo kwa lengo kuhakikisha kwamba wanufaika wanakuwa wengi zaidi.
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini pia ningeomba niende mbele zaidi kwa sababu uhalisia unaonesha wanafunzi wanaosoma shule za binafsi hawapati mkopo either wote au kiasi, lakini pia kwa sababu ya umuhimu wa baadhi ya fani kama udaktari na gharama kubwa ya kusomesha watoto kwenye fani hizo, Serikali inaonaje kuwa na mpango wa muda mrefu ili wanafunzi wote wameweze kupata mikopo kwa asilimia mia moja?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, kama ilivyotokana na jibu langu la msingi, Serikali inaendelea kupanua wigo wa bajeti katika Bodi yetu ya Mikopo. Kwa hiyo naomba nilichukue suala la Mheshimiwa Mbunge kwa vile kutoka mwaka 2017, Serikali imeweza kuongeza bajeti katika bodi ya mikopo kutoka bilioni 427 mpaka hivi sasa tuna bilioni 460. Kutokana na hivyo basi, wanufaika ni wengi na wanaendelea kuongezeka kutoka wale laki moja katika kipindi cha mwaka 2015 mpaka kufikia laki moja na arobaini mwaka 2021.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tunapoongeza bajeti hii tuna hakika tunaweza kufanya coverage kubwa ya wanafunzi. Naomba kutoa taarifa katika waombaji wa mwaka huu wale wa mwaka wa kwanza maombi yote yalikuwa 66,000, lakini waliopata jumla karibu walikuwa 55,000. Kwa hiyo tunaendelea kuongeza ule wigo kwa lengo kuhakikisha kwamba wanufaika wanakuwa wengi zaidi.
MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa elimu ya mafunzo ya ufundistadi hapa nchini ni nini commitment ya Serikali katika kuhakikisha inaongeza msukumo wa pekee ili vijana wengi wa kike na wa kiume kupata elimu hiyo hususan katika Mkoa wetu wa Manyara? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Regina, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Manyara peke yake VETA ina vyuo vifuatavyo: tuna Chuo hiki cha Mkoa cha Manyara, tuna Chuo cha Ufundi Simanjiro, vile vile tuna Chuo cha Ufundi Babati kilichopo Babati Vijijini ambacho kinaitwa Gorowa. Vile vile tunafanya upanuzi katika Chuo cha Wananchi cha Tango ambacho baada ya upanuzi huo zaidi ya wanafunzi 228 wanaweza wakapata udahili. Katika vyuo hivi vyote nilivyovitaja ambavyo viko katika Mkoa wa Manyara jumla ya wanafunzi 1,000 ambao wanaweza kuchukua kozi za muda mrefu na muda mfupi wanaweza wakapatiwa mafunzo katika maeneo haya.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Serikali vile vile kupitia bajeti yake ya mwaka 2019/2020, imepeleka fedha jumla ya shilingi bilioni 48.6 kwa ajili ya kujenga vyuo mbalimbali vya VETA nchini kwa lengo la kuhakikisha kwamba elimu hii ya ufundi inawafikia wananchi wengi na vijana wengi kwa lengo la kupeleka Serikali au nchi yetu katika uchumi wa kati. Ahsante.
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mpango gani wa kujenga chuo cha VETA katika Kata ya Chamazi eneo ambalo limetolewa bure na UVIKYUTA zaidi ya ekari 30 ili kuwawezesha vijana wengi wa Kitanzania kuweza kujiajiri na kuweza kupata ajira katika fani mbalimbali?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza katika jibu langu la msingi Serikali ina mpango mkakati wa kuhakikisha kwamba katika kila mkoa na katika kila wilaya tunakuwa na Chuo cha VETA. Katika awamu ya kwanza tumefanya ujenzi ambao mpaka hivi ssa unaendelea katika wilaya 29, lakini katika awamu ijayo tunatarajia katika kila wilaya kupeleka vyuo hivyo. Kwa hiyo, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba katika kila wilaya tutafikia kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, wakati mimi nilipokuwa nasoma chuo tulikuwa tunapata ziara za mafunzo (study tours) mara kwa mara kwenye maeneo ambayo kazi zilikuwa zinatendwa kwa vitendo. Hata hivyo, utaratibu huo ulikoma na tukabakiwa tu na utaratibu wa mafunzo viwandani (industrial practical training) sasa ili kuzalisha vijana mahiri, wabunifu na wenye uwezo wa kuhamisha maarifa ya kisayansi katika uzalishaji. Je, Serikali haioni haja ya kuongeza utaratibu wa study tours pamoja na huu uliopo wa mafunzo viwandani? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, niishukuru Serikali na niipongeze kwa kutambua mchango wa wataalam wanawake wa kisayansi mpaka wameamua kupanga kujenga shule za masomo ya kisayansi kila mkoa. Je, Serikali inaweka utaratibu gani sasa kuhakikisha wasichana waliofaulu vizuri masomo ya sayansi wanapata mikopo na fursa nyingine za elimu ya juu bila kuhangaika na usumbufu wowote kama ambavyo imetoa hivi karibuni?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ulenge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli katika utaratibu wa kawaida vyuoni tunakuwa na program zile za practical training baada ya kumaliza mwaka husika wa masomo, lakini tumekuwa na utaratibu wa zamani ule wa kufanya study trip. Hata hivyo, kutokana na uhaba wa bajeti program hizi zilisimama.

Naomba kulithibitishia Bunge lako tukufu, hivi sasa tunakwenda kuimarisha na kuboresha bajeti yetu katika maeneo haya ya elimu, especially, katika vyuo vikuu na utaratibu huu sasa wa hizi study tour unaweza ukarejea.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la pili ambalo ni wasichana; kama mnavyofahamu Mheshimiwa Rais wakati anahutubia Bunge hili alizungumza hapa kwamba tunakwenda kujenga shule 26 katika kila mkoa kwa lengo la kuhakikisha kwamba wasichana wanakwenda kupata study za masomo ya sayansi katika maeneo haya. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kwamba wasichana hawa pindi watakapomaliza masomo yao haya tunakwenda kuwa-absorb kwenye vyuo ili sasa tuweze kupata wataalam wasichana na wanawake wengi katika masomo haya ya sayansi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kipaumbele chetu kama Serikali na katika mikopo yetu ya elimu ya juu tutahakikisha kwamba masomo haya ya sayansi yanapewa kipaumbele, hasa kwa wasichana wetu hapa nchini. Ahsante.
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika swali langu la msingi nimesema kwa kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi imefanya kazi nzuri ya kutoa elimu bure katika shule za msingi mpaka sekondari; na kwa kuwa Waraka wa Serikali Namba 5 wa 2015 unasema, elimu bure ni kutoka shule ya msingi mpaka sekondari; na kwa kuwa kidato cha tano na kidato cha sita ni sekondari, ni kitu gani kinazuia Serikali kutoa elimu bure kwa kidato cha tano na cha sita kwa sababu ni sekondari hiyohiyo ambayo inazungumzwa?

Mheshimiwa Spika, umesikia Wabunge wengi wanasema hapa, Mheshimiwa Oliver, Mheshimiwa Sanga na wengine kwamba imetajwa katika Waraka kwamba elimu bure ni shule ya msingi mpaka sekondari, kidato cha tano na cha sita ni sekondari. Sasa ni lini Serikali itatoa elimu bure kwa kidato cha tano na cha sita?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, tumezungumza humu mara nyingi sana na hili swali naliuliza kama mara ya tano sasa, Shule ya Sekondari za Unyali, Mkomalilo, Mihingo, Esparanto, Makongoro, Wamamta, Salama, hazina walimu wa sayansi. Watu wanachanga, tumejenga majengo mazuri watoto wanasoma lakini hawana walimu. Lini Serikali itapeleka walimu kwenye shule hizi?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Getere, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Waraka Namba 5 wa mwaka 2015 wa Elimu Msingi, unaelekeza kwamba itakuwa elimu bure kuanzia elimu ya awali mpaka kidato cha nne. Mheshimiwa Mbunge anauliza kwa nini kidato cha tano na cha sita hakipo katika mpango huo. Ni kweli, kidato cha tano na cha sita hakipo kwenye mpango huu lakini naomba nilieleze Bunge lako tukufu kuwa tunaendelea kuboresha bajeti yetu ya Serikali, mpango huu unaweza kufikiwa iwapo tu bajeti ya Serikali itakuwa imekaa sawasawa.

Mheshimiwa Spika, kama mnavyofahamu, baada ya kupata fursa hii ya kutoa elimu bure usajili wetu wa wanafunzi, tuchukulie mfano wa darasa la kwanza, umeweza kuongezeka kutoka wanafunzi 1,300,000 mwaka 2014 mpaka wanafunzi 2,070,000 mwaka 2016/2017. Utaona kuna ongezeko hilo kubwa kutokana na Sera hii ya Elimu Bure. Kwa hiyo, upatikanaji wa fedha utatupeleka kuhakikisha kwamba kidato cha tano na cha sita tunawaingiza katika mpango huu.

Mheshimiwa Spika, halikadhalika napenda kueleza kwa zile kaya ambazo ni maskini tuna mpango wetu wa TASAF ambapo kwa mwanafunzi wa shule ya msingi anapata shilingi 12,000/= kwa mwezi na wale wa sekondari wanapata shilingi 16,000/= kwa mwezi. Hawa wanaweza wakasaidiwa katika mpango huu ili kuhakikisha kwamba tunaweza kufikia yale malengo ya kulipi hiyo ada ndogo ambayo inalipwa katika kidato cha tano na cha sita.

Mheshimiwa Spika, katika swali la pili, shule alizozitaja na hasa kuhusu wale walimu wa sayansi, Mheshimiwa Waziri Mkuu hapa ametoka kujibu swali kama hilo katika kipindi kifupi kilichopita, Serikali tayari imeshaanza mpango wa kuajiri walimu. Katika mwaka 2020 tumeajiri zaidi ya walimu 8,000 wameshapelekwa shuleni. Sasa hivi Serikali iko kwenye mchakato wa kuajiri tena walimu 5,000 ambao katika kipindi kifupi kijacho tunaamini shule hizi alizozitaja zinaweza zikapata hao walimu wa sayansi.

Mheshimiwa Spika, ahsante.
MHE. MRISHO M. GAMBO: Mheshimiwa Spika, Mkoani Arusha kuna shule ya St. Jude, ni shule ambayo inasomesha watoto wenye mazingira magumu na kwa kupitia misaada ya watu mbalimbali huko duniani. Siku za karibuni TRA imeenda kwenye account ya shule hiyo imechukua fedha na kusababisha shule hiyo kupata misukosuko na kufungwa kiasi ambacho watoto wenye mazingira magumu wamekosa nafasi ya kwenda kusoma pamoja. Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa ahueni kwa shule hii ili suala la elimu ambayo ni kipaumbele chetu liweze kupewa mstari wa mbele?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama alivyobainisha uwepo wa shule hiyo na changamoto zilizotokea kuhusiana na wenzetu wa TRA, suala hili naomba tulichukue twende tukalifanyie kazi na badaye tutaweza kutoa majibu muafaka kwa Mheshimiwa Mbunge na Mkoa wa Arusha kwa ujumla. Ahsante.
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, wakati Mheshimiwa Naibu Waziri anajibu maswali amezungumzia neno elimu bure, lakini najua anajua tofauti kati ya elimu bure na elimu bila kulipa ada. Nazungumza hivi kwa sababu kinachofanyika mashuleni huko wanafunzi na wazazi wanatozwa fedha ama za kulipa mlinzi ama za kulipa maji ama za kulipa walimu wa sayansi ambao wanawatafuta wa ziada ama masomo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nataka Serikali iweke hoja wazi kabisa hapa mezani, kinachofanyika ni elimu bila kulipa ile ada ya Sh.20,000 na Sh.70,000 na siyo elimu bure, ili wazazi wanapochangia huko wajue kwamba wao kwenye mchakato wa elimu ya Tanzania wana-stake yao ya kuchangia na Serikali ina stake yake ya kuchangia. Kwa hiyo, aweke wazi hapa ni elimu bila ada na sio elimu bure. Sasa kwa tafsiri ya kamusi bure ina maana yake na ada ina maana yake. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Halima, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwenye majibu yangu ya msingi, Waraka Namba 5 wa mwaka 2015 ulikuwa unaeleza kwamba elimu bila malipo kwa elimu ya awali mpaka kidato cha nne.

Mheshimiwa Spika, lakini kuna michango ambayo huenda ikawa inatokea huko ambayo ni michango ya hiari…

SPIKA: Ngoja Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa hiyo, ni elimu bila malipo siyo elimu bure.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, elimu bila malipo. (Makofi)

SPIKA: Nisikuwekee maneno mdomoni Mheshimiwa Naibu Waziri, nilitaka tu uweke vizuri, hebu rudia wewe mwenyewe.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, nilikuwa nazungumzia Waraka Namba 5 wa mwaka 2015 unaeleza kwamba elimu ya awali mpaka elimu ya kidato cha nne itakuwa ni elimu bila malipo, tafsiri yake ni elimu bure. Kwa hiyo, waraka huo unaeleza hivyo.

Mheshimiwa Spika, katika muktadha huo, amezungumzia kwamba kuna michango wazazi wanachangishwa ya walinzi, usafi au ya vitu vingine, naomba nilieleze Bunge lako Tukufu kuwa Serikali katika Waraka ule imebainisha wazi kwamba michango ile yote ambayo mzazi alikuwa anachangia katika kipindi cha nyuma katika maeneo haya ya elimu ya awali kwa hivi sasa haipo na gharama hizo zinakwenda Serikalini.

Sambamba na hilo, nadhani keshawahi kusikika Mheshimiwa Waziri wa Elimu lakini Mheshimiwa Rais ameshawahi kuzungumza mara nyingi sana, kama mzazi au mlezi ana mchango wa aina yoyote ambao anaona bora au inafaa mchango huo autoe ni vema aufikishe au auwasilishe kwa Mkurugenzi ambapo yeye atapanga kitu gani cha kufanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mpango mzuri wa kuwawezesha wanafunzi hao ambao wameshindwa kufaulu mitihani ya darasa la saba na kidato cha tano, lakini ikumbukwe kwamba wanafunzi tunaowazungumzia ni wale ambao wazazi wao wameshindwa kulipa ada ya 20,000 na kwa maana hiyo Serikali imewapa elimu bila malipo. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuanzisha mafunzo maalum ya bure kupitia Mfuko wa Uwezeshaji wa Vijana chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ili wanafunzi hao ambao wanashindwa mitihani na wanarudi nyumbani na kuwa tegemezi kwa taifa waweze kupata mafunzo hayo na hatimaye waweze kujiajiri? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, tunayo Idara ya Elimu ya Watu Wazima lakini idara hii haijafanya vizuri kwa muda mrefu. Kutokana na wahitimu kuongezeka sababu ya mpango wa elimu bila malipo nchini wanafunzi wengi wanahitaji kupata elimu hii ya ziada. Je, Serikali sasa ipo tayari kutoa elimu ya watu wazima bure ili kuwawezesha wanafunzi ambao wanashindwa mitihani ya kidato cha nne na darasa la saba kupita kwenye mfumo huu ambao siyo mfumo rasmi wa elimu nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Husna, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani maswali yote aliyouliza Mheshimiwa Husna ni mapendekezo ambapo anapendekeza kwa jinsi yeye anavyofikiri. Kwa hiyo, naomba maswali hayo yote mawili kwa pamoja tuyachukue na tuweze kwenda kuyaongeza kwenye mipango pamoja na Sera yetu ya Elimu na kuweza kuangalia namna gani ya kufanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri sana yaliyotolewa na Mheshimiwa Naibu Waziri, nikirejea swali la Mheshimiwa Mbunge na hasa ushauri wake, kupitia Programu ya Ukuzaji Ujuzi ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, alikuwa anafikiri kwamba Vyuo hivi vya Maendeleo ya Jamii vingeweza pia kutumika kuwafundisha na kuwasaidia vijana kukuza ujuzi katika skills ambazo zinatumika kwenye mazingira husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuliarifu Bunge lako tukufu kwamba program hizo zinaendelea na Serikali imekwisha kutenga bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 tutaendelea kutenga hiyo bajeti lakini kwa mwaka wa fedha 2020/2021 tayari tunavyo Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, ambavyo mwezi huu wa nne vitaanza kutoa mafunzo ya ujuzi kwa vijana, kuwasaidia vijana kuweza kupata ujuzi katika maeneo mbalimbali, lakini asilimia kubwa ya malipo ya ujuzi huo yatagharamiwa na Serikali. Tutakwenda kuangalia vyuo vyote ambavyo vinaweza kutoa mafunzo hayo, tutafanya tathmini yake kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, kuona vile ambavyo vina uwezo wa kufanya kazi hiyo tutaendelea kuvijumuisha kwenye mpango na vitaendelea kutoa mafunzo hayo na kuwafikia vijana wengi wa Tanzania kwenye programu hiyo maalum ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa elimu ya vyuo vya kati na vya chini ni kiungo muhimu katika ujenzi wa uchumi na kupunguza umaskini nchini. Kwa kuwa watoto wengi wanaosoma katika hivi vyuo vya chini ni wa maskini. Je, Serikali ina mpango gani wa ku-extend ule Mfuko wa Mikopo wa Elimu ya Juu ili hawa watoto wa maskini wanaotaka elimu katika vyuo vya chini waweze kupata mikopo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu swali Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tumekuwa na utaratibu wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu lakini siyo hawa wa level ya elimu ya kati. Tukiangalia gharama za vyuo hivi kwa mwaka, Serikali inachangia au inagharamia kwa kiasi kikubwa sana. Kwa Vyuo vyetu vya FDC ada yake ni Sh.250,000/= kwa wanafunzi wale wanaokaa bweni na Sh.145,000/= kwa wanafunzi wa kutwa lakini kwa vyuo vyetu vya VETA, vina gharama ya Sh.120,000/= kwa wale wanafunzi wa boarding na Sh.60,000/= kwa wale wanafunzi ambao wako day. Hata hivyo, tunarudi pale pale kulingana na wigo na bajeti ilivyo, nadhani Serikali tutaangalia kitu gani cha kufanya lakini mpaka hivi sasa Serikali inatoa ruzuku ya kutosha kabisa kuhakikisha kwamba vyuo hivi vinakwenda na kuwapunguzia mzigo wananchi wa kulipa gharama hizi kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Kwa kuwa Serikali inatoa elimu bila malipo kuanzia chekechea mpaka kidato cha nne, wanafunzi wachache ambao hawajabahatika kwenda kidato cha tano wanaenda vyuo vya ufundi. Vyuo vya ufundi, Mheshimiwa Naibu Waziri amesema wanalipia ada ya Sh.60,000/= na Sh.120,000/= kwa wale wa boarding. Je, Serikali haioni haja sasa kuondoa ada pia kwenye vyuo vya ufundi ili kuwawezesha watoto wengi kuweza kupata ujuzi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sima, Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama nilivyoeleza katika majibu yangu ya mwanzo kwamba Serikali inatoa ruzuku ya kutosha. Kwa hiyo, hili alilolileta Mheshimiwa Sima ni pendekezo, tunaomba twende tukalifanyie kazi tuweze kuangalia namna gani aidha kwa kupunguza au kwa kuondoa wakati huo huo tukiangalia wigo wa bajeti ya Serikali unavyokuwa.
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwepo na malalamiko mengi ya wanafunzi wenye sifa za kupata mikopo ya elimu ya juu lakini hawapati hiyo mikopo; na mimi ni shuhuda kwa kuwaleta wanafunzi wa jimbo langu, kwenda Bodi ya Mikopo lakini hawakuweza kufanikiwa kupata Bodi ya Mikopo, zaidi ya wanafunzi 20.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa swali je, serikali ni lini itahakikisha kwamba wanafunzi wenye sifa hakika wanapata mikopo badala sasa takwimu zinaonesha wanapata lakini uhalisia hawapati mikopo hiyo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa wale waliofanikiwa kupata mikopo, kwa maana ya ukimaliza umeweka kanuni ama utaratibu kwamba mwanafunzi akimaliza chuo kikuu mara tu baada ya kumaliza aanze kurudisha huo mkopo na baada ya miezi 24, kwa maana ya miaka miwili, asipoanza kurudisha huo mkopo mmeweka kanuni kwamba atatozwa riba ya asilimia 10.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali, kwa wanafunzi ambao hawajapata ajira na sasa ajira ni changamoto, pengine miaka mitano, mingine kumi, wengine 20 na wengine hawapati kabisa; Serikali imejipangaje kuhakikisha kwamba wanawawezesha kwanza hao wanafunzi kuwa-link na mashirika na taasisi ili fedha zilizokopwa na wanafunzi hawa zisipotee? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Mwakibete kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza kwenye swali langu la msingi,, kwamba Serikali imekuwa ikitoa mikopo hii kwa walengwa na wale ambao wamefikia sifa hizo. Kwa hiyo nichukue hoja ya Mheshimiwa Mbunge; lakini Serikali inaendelea kuboresha bajeti yake ya mwaka hadi mwaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, mikopo yetu imepanda kutoka bilioni 427 kwa 2017/2018 mpaka shilingi bilioni 464 2020/2021; na mwaka ujao wa fedha tunatarajia kutoa mikopo hii kwa jumla ya shilingi bilioni 500. Kwa hiyo tunaamini katika kuongeza wigo huu wa bajeti tunaweza tukawafikia walengwa wengi na changamoto hii ya vijana wetu kukosa mikopo inaweza ikatatulika. Hata hivyo tunarudi palepale, kwamba vigezo vya uhitaji ansifa zeke lazima viziingatiwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye hili eneo la pili la hizi asilimia; na hili naomba tulibebe kwasababu yamekuwa ni malalamiko ya wanufaika wengi na ni malalamiko ya muda mrefu, tuweze kwenda kuliangalia na kufanya review halafu tutaleta hoja hapa katika Bunge lako Tukufu kwamba namna gani tunaweza kwenda kuzishughulikia hizi tozo ambazo zimekuwa ni kero.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala la hawa vijana sasa la kuwa-link kwenye taasisi na maeneo mengine ya ajira ni kwamba, jukumu la Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ni kutoa taaluma kwa vijana, sio jukumu lake kutafuta ajira kwa vijana. Sasa hili tunaomba tulibebe kama serikali tuweze kuangalia vijana wetu wanapomaliza namna gani tunaweza kuwa-link na maeneo mengine ya kuweza kupata ajira ili fedha hizi ziweze kurudishwa kwa haraka ili na wanufaika waweze kuwa wengi zaidi. Ahsante.
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Mimi ningependa kuuliza swali la nyongeza kama ifuatavyo:-

Kwa nini Serikali isipunguze riba kwa hao wanaolipa deni lote kwa mkupuo kwa wakati mmoja ikatoka asilimia kumi au asilimia mbili au tatu au na vile vile kupunguza- retention fee ambayo ni kubwa na haipo kwenye mkataba wanaojaza wakati wa kukopa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza katika majibu yangu yaliyopita, kwamba tunaenda kufanya review ya tozo hizi pamoja na riba na kuweza kuangalia namna gani tunaweza tukazipunguza au kuziondoa kulingana na uhitaji kutokana na malalamiko yaliyopo.
MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa hii ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, liko kundi kubwa sana la wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wanakosa mkopo licha ya kuwa na sifa zote alizozitaja Mheshimiwa Naibu Waziri, na baada ya kukosa mkopo hupitisha bakuli maeneo mbalimbali wakichangisha fedha na wanabahatika kwenda vyuo vikuu lakini baadaye wanakatisha masomo yao kwa kushindwa kupata fedha za kuendelea.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwatambua wanafunzi hao ambao wame-drop out na kuweza kuwasaidia ili waweze kuhitimisha elimu yao na kufikia ndoto zao? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza awali kwamba Serikali tunaendelea na kuongeza wigo wa bajeti ili kuweza kuwafikia walengwa wengi zaidi. Kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi, katika mwaka 2020/2021 waliojaza fomu ni zaidi ya 66,000 lakini tulioweza kuwapa mikopo ni 55,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, jawabu kwamba kuna zaidi ya wanafunzi 11,000 ambao walikidhi vile vigezo lakini hatukuweza kuwapa. Majawabu ya Wizara kupitia Serikali tunakwenda kuongeza wigo wa bajeti ili kuweza sasa kuwafikia walengwa wengi zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeeleza hapo mwanzoni kwamba bajeti yetu ya mwaka 2017/2018 ilikuwa ni bilioni
427. Bajeti ya 2020/2021 ilikuwa 464, lakini bajeti yetu ya mwaka 2021/2022 inakwenda kuwa bilioni 500. Tunaamini kwa kadri tutakavyokuwa tunaongeza bajeti yetu itaweza kuwafikia walengwa wengi na vijana wetu wengi wataweza kunufaika na mikopo hii.
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikijinasibu kwamba mikopo hii inalenga kusaidia watoto wa familia maskini lakini kimsingi mikopo hii inakuwa ni mzigo kwa watoto wa familia maskini. Muuliza wa swali msingi amezungumzia asilima 15 ya makato kila mwezi, amezungumzia asilimia 10 ya interest rate kwa watu ambao ndani ya miezi 24 wameshindwa kulipa, kuna asilimia 6 ya interest kwa watu ambao wanalipa. Sasa matokeo yake ni kwamba badala ya kuwa ni mkopo wa kusaidia watoto unakuwa ni mkopo wa kibiashara.

Sasa ni lini Serikali italeta hapa Bungeni mabadiliko ya kisheria ili kile kinachosemwa kusaidia watoto maskini kithibitike kwa maneno na kwa vitendo na isiwe lugha za kisiasa?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Halima kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, katika urejeshaji wa mikopo hii mnufaika anapaswa kukatwa asilimia 15 katika gross salary yake ambayo makato haya yalipitishwa katika Bunge lako hili Tukufu. Lakini vilevile kuna hizo alizozitaja Mheshimiwa Mbunge kwamba kuna hiyo asilimia 10 kwa wale watakaochelewa na asilimia sita.

Lakini kama nilivyojibu katika maswali ya nyongeza yaliyopita, kwamba tunakwenda kufanya review ya kanuni hizi na kuweza kuangalia namna gani tunaweza aidha kuondoa au kupunguza. Kwa hiyo, tunaomba tuachie ili jambo hili tukalifanyie kazi; na tuwe watulivu ili kuhakikisha mikopo hii haiendi kuwa kero kwa watumishi wetu maskini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza na mpongeza sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri na kwa maswali mengi ambayo yameelekezwa na ameyajibu kwa ufasaha. Jambo dogo tu nilikuwa nataka niweke kumbukumbu ili kwenye Hansard ikae vizuri.

Nilikuwa nataka tu kueleza kwamba, katika mkopo wa mwanafunzi analipa asilimia sita kama tozo ya kutunza thamani, lakini hakuna riba ya asilimia 10 kama ambavyo ilikuwa imeelekezwa, na hiyo asilimia 6 ndiyo hiyo ambayo tunaifanyika kazi. Nilikuwa ninaomba kumbukumbu zikae vizuri. Asilimia 15 ni makato ya mshahara kila mwezi, lakini ile riba iliyokuwa inatajwa ya asilimia 10 niombe niweke kumbukumbu vizuri hiyo haipo. Ahsante sana.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa hii ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili ufaulu mzuri uweze kupatikana inategemea sana mazingira ya kujifunzia na kufundishia hasa ikama nzuri ya walimu.

Je, Serikali haioni kwamba sio haki kuwashindanisha au kushindanisha Halmashauri za Mjini na Vijijini ambako kuna mazingira magumu ya kujifunzia na kufundishia na kuna uhaba mkubwa wa walimu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, Serikali haioni ni wakati sahihi sasa kutazama upya vigezo hivi vya kuzingatia katika kupanga madaraja haya ya ufaulu kwa kuwa kwa kuzingatia maeneo hayo ya mjini na vijijini ambako shule za vijijini zina mazingira magumu sana ya kujifunza na kufundishia ukilinganisha na shule za mjini?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Sekiboko kwa niaba ya Mheshimiwa Shangazi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu kwamba tuna changamoto kubwa ya walimu kwenye shule zetu na mwaka jana mwezi Novemba, Serikali kupitia Wizara ya TAMISEMI ilifanya uajiri wa walimu zaidi ya 8,000 na maeneo makubwa ambayo yali-focus au walipelekwa walimu wale ni maeneo ambayo yenye changamoto kubwa sana ya walimu hasa hasa kule vijijini na maeneo ya pembezoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa suala la ikama ya walimu nipende tu kusema kwamba Serikali bado tunafanyia kazi, kuna walimu wengine zaidi ya 5,000 ambapo kupitia Wizara ya TAMISEMI tunaratajia hivi punde walimu hao watasambazwa kwenye maeneo hayo ili kuweza kusawazisha ile ikama na kuondoa changamoto hii ya upungufu wa walimu kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala la utaratibu wa madaraja, utaratibu huu wakupanga madaraja katika ngazi ya shule na kwa wanafunzi wetu imezingatia vigezo vya kitaifa, kikanda na kimataifa. Kwa hiyo tukisema kwamba leo hii tuweze kubadilisha vigezo hivi kwa sababu tu kuna shule ambazo hazina ikama ya walimu itakuwa hatutendei haki kwenye eneo letu hili la kutoa elimu kwa vijana wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nadhani eneo kubwa la kujikita ni pale kwenda kuhakikisha kwamba ikama ya walimu inapatikana, lakini kwa upande wa vigezo hivi vilivyowekwa imezingatia sana ubora wa elimu yetu na katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa. Naomba kuwasilisha.
MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali.

Kwa kuwa mazingira ya jiografia ya Wilaya ya Ukerewe yanaathiri sana ufaulu wa Watoto wa kike, kwa nini sasa Serikali isione umuhimu wa kujenga shule maalum ya bweni katika Wilaya ya Ukerewe?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nipende kujibu swali la Mheshimiwa Furaha kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tuna changamoto za watoto wa kike sio tu kwa upande wa Ukerewe bali kwa maeneo mengi ya nchi yetu. Nipende kumfahamisha Mheshimiwa Mbunge kwamba tuna programu mbalimbali ambazo zitawezesha sasa kwenye maeneo mengi ambapo tuna changamoto ya vijana wetu kutembea umbali mrefu kuweza kupata shule za bweni katika maeneo hayo.

Kwa hiyo, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge Serikali iko mbioni sasa katika mpango wake wa P4R kuhakikisha tunaweza kwenda kujenga shule kwenye maeneo ambayo yana changamoto kama hizi ili kuweza kupata ufumbuzi wa kudumu, ahsante.
MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kuuliza swali la nyongeza, kigezo kikubwa cha ufaulu cha wanafunzi kwenda kidato cha kwanza au kwenda kidato cha tano imekuwa ni zile grade aidha A,B,C ambazo zinatumika sasa katika ufaulu, lakini kwenye midterm reviews za wanafunzi hasa mitihani Serikali imekuwa na utaratibu ambao tumeendelea nao nadhani tulirithi kwenye ukoloni kwa kutoa wa kwanza mpaka wa mwisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili limekuwa lina- affect watoto kisaikolojia na mtoto anakuwa na alama A, lakini ni wa kumi na ukimuuliza ulikuwa wangapi darasani anakwambia nilikuwa wa kumi lakini ana A; je, Serikali haioni jambo hili linaathiri watoto kisaikolojia na katika maisha mtu kujiona kwamba yuko grade ya mwisho? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nollo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hatuna uhakika sana kama kuwapanga watoto wa kwanza mpaka wa mwisho kuna haribu saikolojia ya watoto bali inaonesha ushindani na namna gani watoto wanaweza wakashindana ili kuweza na yeye kujisukuma kuweza kufika hapo juu, lakini nadhani ni suala ambalo linahitaji kufanyiwa utafiti kwamba je, kupangwa watoto katika utaratibu huo kuna athiri kisaikolojia. Hili naomba tulibebe tukalifanyie utafiti na kama tukiona kama kweli lina tija tunaweza tukaja kutoa majibu mbele ya Bunge lako tukufu.
MHE. BENARDETHA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, ninayo maswali mawili.

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Kagera ni mkoa mkubwa, una watu zaidi ya 3,000,000 lakini hadi leo hauna Chuo kikuu hata kimoja. Vipo vyuo vikuu vilikuwa vimeanzishwa na Mashirika ya Dini, moja ni Lutheran, walianzisha kile cha Joshua Kibira; Roman Catholic walianzisha branch ya Saint Augustine lakini vyote Serikali ilivifunga: Kwa kuwa Serikali inasema kuanzisha Vyuo Vikuu ni gharama, badala ya Serikali kuvifunga, haioni ingekuwa ni vizuri wakaendelea kuvijenga, kuvipa miongozo na kuviwezesha hivi vilivyoanzishwa badala ya kuvifunga? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; miaka ya nyuma huko Mkoa wa Kagera ulikuwa unawika kwenye elimu, uko katika the best three, lakini sasa hivi haiko hivyo: Je, Serikali haioni kwamba sasa wakati umefika, angalau waanzishe tawi moja la Chuo Kikuu cha Serikali kama Sokoine, kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mkoa wa Kagera ili kuchochea maendeleo ya Mkoa huo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Benardetha Mushashu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Kagera tulikuwa na vyuo vikuu binafsi viwil,i hivyo alivyovizungumza Mheshimiwa Mushashu; hicho cha Kadinali Rugambwa na kile cha Kibira alichokizungumza. Nikuthibitishie mbele ya Bunge lako Tukufu, Chuo hiki cha Kadinali Rugambwa hakikufungwa, badala yake walihamisha usajili kutoka ule wa TCU kwenda ule wa NACTE. Kwa hiyo, chuo hiki kipo, kinaendelea kutoa huduma pale, ingawa hazitoi zile kozi za degree, badala yake zinatoa zile kozi za kawaida, za chini, lakini bado kinaendelea kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, kwenye hiki chuo cha pili cha Kibira, wenyewe wamiliki wa chuo hiki waliomba kifungwe kutokana na kushindwa wao wenyewe kuendesha chuo hiki. Kwa hiyo, nimshawishi tu Mheshimiwa Mbunge aweze kuwasiliana na wamiliki wa chuo hiki waweze kujipanga vizuri ili sasa waje kufanya maombi upya kama upo uhitaji wa kukifungua chuo hiki kama wataona inafaa, nasi tuko tayari kupokea maombi yao.

Mheshimiwa Spika, kwenye eneo la pili la vyuo vyetu hivi vikuu kuanzisha matawi kwenye eno hilo, ni suala ambalo linakubalika, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, lakini inatakiwa sasa ifanyike ile needs assessment kwa vyuo hivi vyenyewe kwa sababu wana mamlaka ya kufanya hivyo kama wanaona uhitaji huo wa kuanzisha branch hizo uko katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tutawafikishia ujumbe huu waweze kuja Kagera wafanye market analysis pamoja na needs assessment ili kuona kweli kama upo uhitaji wa kuanzisha branch kwenye maeneo hayo, waweze kufanya hivyo. Ahsante. (Makofi)
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo majibu ya Serikali yameweza kukiri kwamba, mfumo wa sasa wa elimu bado haujakuwa suluhisho la vijana wengi wanaomaliza na kwenda kujiajiri wao wenyewe.

Je, ni lini hasa Serikali itakamilisha mchakato wa mabadiliko haya, ili tuweze kwenda na mfumo kama ambavyo Serikali imeweza kukiri kwamba, hatuko kwenye mfumo wa kidunia, hatujaweza kukimbizana nao?

Je, Serikali ni lini itakamilisha mchakato huo ili kuwasaidia vijana wengi wanaotoka kwenye shule waweze kwenda kujiajiri wao wenyewe? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi kwamba, sasa tuko katika mjadala wa kitaifa wa kuhakikisha kwamba, tunaboresha mitaala yetu hii, ili kuingiza stadi za kazi, lakini vilevile kuingiza mambo yote yanayoonekana ni muhimu kuhakikisha kwamba, tunajenga umahiri wa vijana wetu. Mchakato huo tumeanza na tumeanza katika Mkoa wa Dar es Salaam, lakini vilevile tulifanya mjadala mpana hapa Dodoma na tuna website ya kuhakikisha kwamba, tunakusanya maoni hayo.

Mheshimiwa Spika, tutaendelea na mchakato huu wa kukusanya maoni. Na ndani ya mwaka huu wa fedha tunakadiria au tunakusudia kuhakikisha mchakato huu uweze kukamilika, ili tuweze kupata mitaala ile ambayo nchi yetu inayohitaji. Ahsante.
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kupata nafasi:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa sisi wakati tunasoma miaka ya 70 sekondari tulikuwa na mchepuo wa needle work na cookery.

Mheshimiwa Spika, naomba niwaambie Waheshimiwa Wabunge kwamba, kwa needle work niliyoisoma miaka ile ya 70 nimeweza kushona kibiashara mpaka leo nafanya hiyo kazi. Hivi Serikali kweli hamuoni ni muhimu sana kuwafanya akinamama waweze kupata kitu ambacho watakibeba mpaka wakiwa watu wazima?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Malecela, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Malecela, kama nilivyozungumza mwanzo kwamba, tuko kwenye mjadala, mjadala ambao utawahusisha vilevile Wabunge. Ninyi Waheshimiwa Wabunge ndio ambao mtaamua kwamba, vitu gani tuweke kwenye mitaala yetu kwa lengo la kuhakikisha tunatengeneza jamii, tunatengeneza kizazi ambacho kitakwenda kujitegemea katika nyanja hizo ambazo tunazihitaji.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, wakati huo utakapofika Waheshimiwa Wabunge tutaomba tupokee maoni yenu na sisi bila tatizo lolote tutaingiza kwenye mitaala hiyo, ili kuhakikisha tunatengeneza Taifa lenye kujitegemea. Ahsante.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo ameyatoa na niongeze tu dogo kwamba, pamoja na maboresho ambayo tunayafanya, lakini hata sasa somo la needle work na cookery linafanyika, lakini kwa shule chache.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilikuwa nataka tu pia ifahamike hivyo kwamba, linaendelea kutolewa, lakini sio somo kwa wote. Kwa hiyo, tutazingatia kuona kuna umuhimu na tunakubaliana kwamba, kuna umuhimu wa kuhakikisha vijana wengi wa kitanzania wanapata ujuzi huo. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, jambo hili ni zito linalowakuta wasichana wetu hawa, linavuruga maisha yao utaratibu wao na kuleta simanzi na huzuni katika familia japokuwa kaja kiumbe lakini kaja vipi na atahudumiwa namna gani. Je, Serikali haioni kwamba ni wakati muafaka wa kuwarudisha wasichana hawa wakaendelea na masomo yao baada ya kujifungua kuliko kuwapeleka kwenye vituo nje ya mfumo rasmi. Kwa kuwa mimba siyo maradhi ya kuambukiza wao walikuwa wakazane kuleta mitaala juu ya ngono, uzazi. (Makofi)

Swali la pili Je, Serikali haioni kwamba kuzuia watoto wa kike waliopata mimba kuendelea na masomo yao na kuwaachia watoto wa kiume waliohusika kuendelea kama vile hawajafanya chochote siyo ubaguzi wa kijinsia?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, waliofanya makosa watu wawili, bakora anapigwa mtu mmoja kweli hiyo ni haki? (Makofi)
WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asha.

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo Mheshimiwa Naibu Waziri amelizungumza ni kweli tumeweka huo utaratibu na kama unakumbuka kupitia mradi wetu wa SEQUIP ambao karibu tunaanza kuutekeleza tumeweka pia kipengele cha kuangalia Watoto wanaopata ujazito wakiwa shuleni na tutaenda kuimarisha vituo vyao ambavyo tumevieleza katika jibu la msingi.

Mheshimiwa Spika, jambo hili limekuwa linazungumzwa kwa muda mrefu na kwa sababu sasa ndiyo tunaanza kutekeleza mpango mahsusi ambao tumeuweka ningeomba tutekeleze angalau kwa kipindi cha mwaka huku Serikali ikiendelea kutafakari maoni ambayo yamekuwa yanatolewa na wadau ili tuone namna bora zaidi ya kutekeleza hayo maoni ambayo yamekuwa yakitolewa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili kwamba kwanini anayehusika asichukuliwe hatua. Utakumbuka kwamba mwaka 2016 Bunge lako Tukufu lilitunga sheria ambayo inatoa adhabu kali kwa mtu yeyote ambaye anajihusisha na masuala ya mapenzi shuleni kwa wanafunzi au mtu ambaye anakatiza ndoto ya watoto wa kike ya kupata elimu. Yeyote ambaye anabainika kwa mujibu wa sheria hiyo iliyotungwa mwaka 2016 anapata adhabu ya kifungo cha miaka 30. Nashukuru kwa nafasi.
MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana ningependa nimuulize maswali mawili madogo ya nyongeza.

Kwanza ningependa kujua katika bajeti yao ya mwaka huu wa 2021 ni wanufaika wangapi ambao wataweza kunufaika na mikopo hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili nilikuwa napenda niulize Serikali ina mpango gani wa kuwezesha wanafunzi ambao wako vyuo vya kati ambao wale ndio wenye mahitaji makubwa zaidi ya hii mikopo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimwa Naibu Spika, ahsante na napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Chumbuni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama tulivyoeleza katika bajeti yetu wakati tunapitisha katika Bunge la Bajeti kwamba bajeti ya Bodi ya Mikopo imeweza kupanda kutoka shilingi bilioni 464 mwaka 2021 mpaka shilingi bilioni 570 mwaka 2122 na kwa hali hiyo basi wanufaika wa bodi watapanda kutoka 149,000 wale ambao walinufaika katika kipindi kilichopita mpaka kufika 160,000 katika mwaka 2021/2022 katika mchanganuo kwamba wale wanaoendelea 98,000 watakuwa wanaoendelea 62,000 tunakadiria katika watakaodahiliwa katika mwaka wa kwanza. Kwa hiyo kwa ujumla wao watakaonufaika tunakadiria kuwa watakuwa sio chini ya 160,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la pili amezungumzia kuhusiana na suala la wanafunzi wa vyuo vya kati. Kutokana na ufinyu wa bajeti yetu bado hatujaweza kuwafikia wanafunzi hawa wa vyuo vya kati kwa hiyo naomba tulichukue kama Serikali jambo hili wakati tunaboresha bajeti yetu kama Serikali, lakini ninyi Wabunge ndio ambao tunapitisha bajeti hapa, basi tunaweza kulileta mezani kwa ajili ya mjadala ili tuweze kuona namna gani tunaweza kuwafikia wale wa kada ya kati. Lakini kwa mujibu wa sheria sasa hivi bodi hii inashughulikia wale wa elimu ya juu peke yake, ahsante.
MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na Serikali ya kugharamia elimu kutoka chekechea mpaka kidato cha nne na utaratibu unaofanywa na Serikali wa kutoa mikopo kwa elimu ya juu bado hapa vijana wa kidato cha tano na sita kuna tatizo la kugharamia elimu.

Ni lini Serikali itaweka sasa utaratibu ili kuwahusisha vijana wa kidato cha tano na sita katika utaratibu wa elimu bila malipo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimwa Naibu Spika, napenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Nape kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli vijana wetu wa kidato cha tano na sita wanatakiwa kugharamia kwa maana ya ada kwa wale wa kidato cha tao na sita ambao kwa wanafunzi wetu wa bodi kulipa shilingi 70,000 na wale wa
day kulipa shilingi 35,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii tunaiona kwamba ni affordable au inaweza sana Watanzania wengi kuilipa lakini kwa vile Mheshimiwa Mbunge ameielezea hapa acha basi tulibebe jambo hili tuweze kwenda kuliangalia kwa kina kama Serikali, kwa vile Serikali sasa imeanza kutoa elimu bila malipo kutoka elimu ya awali mpaka kidato cha nne basi na hili tuliingize kwenye mjadala tuweze kuliangalia katika kipindi kijacho kama tunaweza kama Serikali tukaweza ku-wave na kuweza kuondoa ada hii kwa upande wa kidato cha tano na sita, aHsante.
MHE. ALLY A. M. JUMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana; Serikali kama kawaida imekuwa ikifanya kazi kubwa sana kwenye elimu. Sasa hivi imetokea wanafunzi wanaotoka kidato cha nne wanachaguliwa moja kwa moja kwenda kwenye vyuo.

Sasa nilitaka kuuliza na wengine hawana uwezo kabisa na wazazi wao wameshindwa kuwalipia na utakuta ana division one au two. Sasa nilitaka kuuliza je, Serikali inawasaidiaje hawa vijana ambao wanashindwa uwezo wa kwenda huko vyuoni kwa ajili ya kuwasaidia wafike huko vyuoni?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimwa Naibu Spika, napenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Jumbe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Jumbe anazungumza kwamba wapo wanafunzi ambao wanafaulu lakini nafasi za kujiunga kwenye elimu ya juu zimekuwa ni changamoto na suala kubwa hapa ni kuweza kufanya upanuzi. Nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Jumbe na Wabunge wote kwamba tumesaini sasa mkopo kutoka Benki ya Dunia katika mradi wetu wa HIT ambao zaidi ya dola za Kimarekani milioni 425,000 ambazo zinakwenda kufanya upanuzi mkubwa pamoja na ukarabati wa miundombinu katika vyuo vikuu. Tutakapofanya ukarabati huu tunaamini tutaongeza nafasi za udahili na kuondoa changamoto hii ya wanafunzi wengi ambao wamefaulu vizuri lakini kuachwa kwenye vyuo vyetu. Nafasi hizo zitakapoongezeka tunaamini wanafunzi hawa wote ambao watakaofaulu wataweza kupata nafasi ya kwenda kuingia katika vyuo vyetu, asante sana.
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri, lakini niseme ukweli kwamba mikopo inayotolewa ni mikopo na si zawadi. Sasa kuna kitu ambacho kimejitokeza kwamba watu wanaosoma shule binafsi au watoto wa watumishi wa Serikali hawapati mikopo huo ndio ukweli tusiseme uongo.

Je, wako tayari kama itajirudia tena hiyo kitu walete sheria Bungeni ibadilishwe ili itamke wazi kwamba watakaopewa mikopo ni watu waliosoma Serikalini na sio waliosoma kwenye shule za watu binafsi au watoto wa watumishi wa Serikali? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimwa Naibu Spika, ahsante na napenda kujibu swali dogo la Mheshimiwa Ndakidemi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi mikopo hii inaratibiwa kwa ile Sheria Namba 178 ya Bodi ya Mikopo ambayo imebainisha vigezo na vielelezo vya mwanafunzi gani na mwenye sifa zipi wa kupata mikopo hiyo na ambayo haibainishi kwamba amesoma shule gani na alikuwa analipa ada gani katika hizo shule za nyuma zilizopita. Lakini kwa vile yeye Mheshimiwa Mbunge amelieleza jambo hili hapa, tunalichukua tunakwenda kulifanyia kazi na kama kulikuwa na mchezo fulani ambao unachezwa nimwahidi tu kwamba katika kipindi hautatokea na mikopo hii itawafikia wote wenye uhitaji wa kupata mikopo hii.
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, nina swali moja dogo la nyongeza:

Mheshimiwa Spika, kwa vile sasa Wizara ipo kwenye mchakato wa kukusanya maoni ya kurekebisha mtaala. Je, Serikali haioni sasa kuwa ipo haja ya kuweka mtaala mmoja wa elimu ya msingi kati ya Tanzania Bara na Zanzibar? (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Maryam nakupa nafasi tena, sasa uulize swali lako ukiniangalia, usipige chabo. (Kicheko)

MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, kwa vile Serikali sasa ipo kwenye mchakato wa marekebisho ya mtaala. Je, Serikali haioni kwamba ipo haja sasa ya kuweka mtaala mmoja wa elimu kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Bara? (Makofi/ Kicheko)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Maryam Azan Mwinyi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwa upande wa Elimu ya Msingi kuna tofauti ya mitaala kati ya Tanzania Bara na Visiwani. Kwa sababu kwa upande wa Tanzania Bara tunawapeleka watoto shule miaka saba kwa upande wa shule za msingi, lakini kwa wenzetu wa Tanzania Zanzibar wao wanakwenda kwa kipindi cha miaka sita. Kwa hiyo kuna utofauti wa namna hiyo.

Mheshimiwa Spika, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge na nilitaarifu tu Bunge lako Tukufu kwamba, Taasisi yetu ya Elimu Tanzania (TET) na ile ya Zanzibar (ZIE) zinafanya kazi kwa karibu sana kuhakikisha kwamba utekelezaji wa mitaala unakwenda sawasawa lakini na majadiliano ya karibu kuhakikisha kwamba changamoto zote zinazotokea kwenye utekelezaji wa mitaala zinapatiwa ufumbuzi.

Mheshimiwa Spika, ni kweli pasipokuwa na shaka kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanza sasa kufanya mapitio ya Sera ile ya Elimu ya Zanzibar ya mwaka 2016 na wataangalia sasa namna gani tunaweza kuhusianisha miaka hii ya Elimu ya Msingi kuhakikisha kwamba tunakwenda sawasawa.

Mheshimiwa Spika, kama tunavyofahamu kwamba tuna mjadala mpana wa kitaifa kuhakikisha kwamba mwenendo au mfumo wa elimu yetu uwe vipi.

Kwa hiyo, katika majadiliano haya tunaamini changamoto hizi zote anazozungumza Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge humu ndani zinaenda kupata ufumbuzi ikiwemo na hili la kuwa na mtaala mmoja kuanzia Elimu ya Msingi.

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)
MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, lakini kabla sijauliza, niseme tu kwamba sijapata majibu kamili ya swali langu kwa sababu nilitaka kujua kwamba elimu ya viziwi itatolewa lini kwa wanafunzi wote wa shule zetu nchini ili kuweza kuondoa hicho kizingiti cha mawasiliano; lakini naona mjibu swali, Serikali inaonekana ina-focus katika kutengeneza mtaala wa kuboresha elimu kwa wale ambao ni viziwi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo naomba niulize maswali haya madogo ya nyongeza; swali la kwanza;

Je, katika nchi yetu tuna shule ngapi zinazotoa elimu kwa viziwi kwenye ngazi ya Msingi, Sekondari na Vyuo?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili ningependa kujua kwamba kwa kuwa katika nchi yetu lugha rasmi zilizo, zinazotumika kwa mawasiliano ni Kiswahili lugha yetu ya taifa nani ya kimataifa pia na kingereza; nikitaka kupata kitabu au Mtanzania akitaka kupata kitabu cha sign language kwa kiingereza na sign language ya Kiswahili atavipata wapi? Ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Kiruswa katika nchi nyingine wanafundisha hivyo compulsory kwa wanafunzi wote kusoma lugha ya alama?

MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa Spika, kwanza ni-declare interest kwa sababu mimi nimekuwa nikisaidia watoto viziwi kusoma. Nina wachache wanasoma Kenya, nina watatu wanafikia kidato cha nne mwaka huu, na kitabu wanachotumia kinaitwa Kenya Sign Language. Lakini pia nilipokuwa nasoma Marekani nimeona American Sign Language; lakini hapa kwetu nafahamu shule moja ya msingi ambayo inasomesha viziwi iko Moshi -Kilimanjaro - Himo na wale wanasoma kwa Kiswahili. Sasa kunakuwa na crush, kwamba wale watoto walioko Kenya wakija wakikutana na hawa viziwi walioko Tanzania wengine wanaongea sign language ya Kiswahili lakini wenzao wanaongea sign language ya kiingereza. Sasa nilikuwa nataka kujua jinsi ambavyo tungeweza kuwa na hivyo vitabu vya sign language…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana, haya ahsante.

MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: …katika lugha hizo ili tuweze kutoa hiyo…

SPIKA: Haya, ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri eneo hili nyinyi ndio wataalam, majibu tafadhali Mheshimiwa Juma Kipanga. (Kicheko)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Kiruswa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ameuliza suala la shule maalum mahsusi kwaajili ya wanafunzi wetu hawa wenye ulemavu wa usikivu. Tuna shule za msingi 14 ambazo ni mahsusi kabisa kwa ajili ya wanafunzi wetu hawa ambao wana matatizo ya usikivu. Pia shule za sekondari zipo 25, lakini vile vile tunachuo cha ualimu maalum kabisa ambacho kiko Patandi.

Mheshimiwa Spika, katika majibu yangu ya swali la msingi nilizungumza kwamba hivi sasa tunaboresha au tuko kwenye mikakati ya kuhakikisha kwamba tunakwenda kutoa elimu hiyo kama alivyoshauri Mheshimiwa Mbunge, kuanzia ngazi ya elimu msingi mpaka chuo. Lakini katika muktadha wa vitabu nimezungumza katika majibu ya msingi kwamba tumetunga kamusi ambayo inatumia hiyo lugha ya alama.

Mheshimiwa Spika, lakini wanafunzi hawa jukumu letu kubwa sana ni kuhakikisha kwamba tunapata walimu wa kufundisha lugha hizi za alama. Kwa upande wa vitabu, vitabu vinavyotumika ni vitabu vya kawaida kabisa kwa sababu wao wanaweza kuona suala lililokuwepo ni namna gani ni kuweza kufundishwa au kufundishika. Kwa hiyo jukumu letu tunaoenda nalo hivi sasa ni kuhakikisha kwamba tunatengeneza walimu wa kutosha wa kuweza kutumia lugha ya alama; na katika chuo chetu kikuu cha Dar es Salaam sasa tunatoa stashahada ya mwaka mmoja katika kipengele hiki cha lugha ya alama ili kuhakikisha kwamba tunapata walimu wa kutosha wakuweza kufanya service delivery na kutoa elimu hii kwa wanafunzi wetu hawa. Ahsante.
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza na nishukuru kwa jibu kutoka kwa Wizara ya Elimu. Kutokana na umuhimu wa huduma ya afya na hasa kwa suala zima la kupatikana kwa wahudumu pamoja na madaktari katika kipindi hiki ambacho milipuko ya magonjwa imepamba moto. Je, Serikali haioni umuhimu wa kutumia ardhi ya Taasisi za Serikali zilizopo katika Wilaya ya Mbeya ikiwemo ardhi ya Tanganyika Packers ili iweze kukidhi mahitaji ya chuo hiki?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, hii Ndaki ya Afya ina mkakati au mpango gani wa ziada zaidi ya kufundishia ili tuweze kupata huduma nyingi kutokana na hili eneo kubwa ambalo watakuwa wamepatiwa sasa hivi na Serikali? Nashukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Njeza, Mbunge wa Mbeya Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli anayozungumza Mheshimiwa Mbunge kwamba tuna mkakati wa kupata eneo hilo amelizungumza linalomilikiwa na Tanganyika Packers, ambalo liko chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Wizara yangu ikishirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi lakini vilevile Wizara ya Ardhi pamoja na Menejimenti ya Chuo na Uongozi wa Wilaya tutahakikisha tunakwenda kupata umiliki wa eneo hilo ili kuweza kufanya ujenzi wa chuo hiki.

Mheshimiwa Spika, pindi tutakapopata eneo hili, basi Serikali inaweza kutenga bajeti sasa kuhakikisha kwamba tunakwenda kujenga hospitali kubwa ambayo pamoja na Ndaki hii inaweza kuambatanishwa na Ndaki nyingine ili kuweza kupata wataalam wengi zaidi kwa ajili ya kuhudumia Watanzania.

Mheshimiwa Spika, lakini sambamba na hilo, mkakati wa muda mrefu kama nilivyozungumza mwanzo ni kwamba Serikali inatambua jambo hilo na tutakwenda kushughulikia kwa kadri bajeti itakavyoruhusu. Ahsante.
MHE. JUDITH S. KAPINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza napenda kuishukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini napenda kuwashukuru kwa kuongeza rasilimali fedha katika miradi ya maendeleo ya Wizara. Nina swali dogo la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Fedha katika Bunge la Bajeti la 2019/2020 ilitoa maelekezo kwa Bodi ya Mikopo kuangalia uwezekano wa kufanyia kazi suala hili. Je, Wizara haioni umuhimu wa kufanyia kazi mapendekezo haya ya Wizara ya Fedha ili shughuli hii ya kuendeleza mitaji watu kama Wizara inavyosema iweze kufanyiwa kazi vizuri kwa kuitenganisha na Fungu 46? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Judith, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa vile ilikuwa ni mapendekezo na yalipendekezwa na Wizara ya Fedha na kwa vile yalikuwa ni mapendekezo ambayo yaliletwa kwenye Wizara yetu, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa mapendekezo hayo tutaendelea kuyafanyia kazi na pale muda muafaka utakapofika tutawasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu. Ahsante.
MHE. TECLA M. UNGELE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kazi kubwa ya Wizara ya Serikali kufanya ukarabati wa chuo hiki cha Ualimu Nachingwea, lakini kuna uhaba mkubwa wa samani, yani viti, meza, kwa ajili ya wanafunzi hao, lakini pia chuo hakina uzio. Je, Serikali ipo tayari kupanga bajeti kukamilisha mahitaji hayo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kutokana na jitihada kubwa ya vijana wa Mkoa wa Lindi kuwa na ufaulu mzuri katika kidato cha sita kwa miaka mitatu mfululizo inaonesha kabisa vijana hawa wako tayari kwa ajili ya elimu ya juu.

Je, ni lini Serikali itajenga chuo kikuu Mkoa wa Lindi kwa ajili ya kuchochea maendeleo kielimu, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza katika majibu yangu ya swali la msingi kwamba, Serikali imeendelea kukarabati vyuo hivi kwa kuhakikisha kwamba, tunakwenda kuimarisha, lakini tunakwenda kuongeza nguvu ili kuongeza udahili kutokana na uhitaji mkubwa sana wa walimu. Nikaeleza katika swali lile la msingi kwamba, Serikali bado inakihitaji chuo hiki ili kiweze kutoa taaluma hiyo ya astashahada na stashahada ili kuongeza idadi hiyo ya walimu.

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile katika swali lake ambalo linauliza suala la miundombinu ya samani, kwa takwimu tulizokuwanazo chuo chetu cha Nachingwea kina jumla ya viti 400 mpaka hivi sasa, kwa rekodi tulizonazo, lakini wanafunzi waliopo ni 295. Katika muktadha huo haioneshi kwamba, kuna uhaba wa samani kama viti na meza, lakini sambamba na hivyo tuna computer 30 ambazo zinawezesha vitengo vyetu vile vya kutumia computer kupata mafunzo kwa kutumia computer, lakini tuna projector tano ambazo zimenunuliwa hivi sasa na computer mbili ambazo zilikuwa za zamani.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali imeendelea na juhudi zake za kuhakikisha kwamba, tunatengeneza mazingira mazuri ya kupata walimu wa kutosha. Na katika kipindi kilichopita Serikali imeweza kutumia jumla ya shilingi bilioni 84.1 kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, tunatengeneza miundombinu, lakini vilevile samani zinapatikana.

Mheshimiwa Spika, suala la uzio; Serikali bado inaendelea na mkakati wa kuhakikisha tunaboresha mazingira haya. Na hili sasa tunaliingiza kwenye bajeti kuhakikisha maeneo haya yanapata uzio ili kuweza kutengeneza usalama wa mali pamoja na samani za vyuo.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili kuhusiana na suala la chuo kikuu:-

Mheshimiwa Spika, nipende tu kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa hivi sasa bado vyuo vyetu vilivyopo hapa nchini, vyuo vikuu, vina nafasi za kutosha. Na tunawashauri tu wananchi wa Lindi waweze kuvitumia vyuo ambavyo vipo kwasababu, vyuo havijengwi kwa kufuata mikoa wala kanda, bali vyuo hivi vinakuwa ni vya kitaifa, basi wanafunzi hawa wanaweza kwenda katika vyuo vingine ambavyo pale Mtwara tuna chuo kile cha St. Marius wanaweza kupata taaluma yao pale, lakini tuna matawi ya vyuo vikuu huria karibu katika mikoa yote ikiwemo na Mkoa huu wa Lindi.

Mheshimiwa Spika, lakini katika Chuo chetu cha Dodoma walihitajika kudahiliwa wanafunzi au kuna nafasi 40,000 lakini mpaka hivi sasa wanafunzi waliodahiliwa ni 29,595 kwa hiyo, tuna nafasi za kutosha katika vyuo hivi ambavyo vinatosheleza ku-absorb wanafunzi wote. Ahsante sana.
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniona. Kwanza nipende kuipongeza Serikali kwa kutuletea zaidi ya bilioni 1.9 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kwenye Chuo hiki cha Nachingwea:-

Mheshimiwa Spika, swali langu, chuo hiki ni kikongwe, Je, Serikali sasa haioni haja ya kuanzisha kozi maalum ya masomo ya sayansi, ili tuzalishe wataalam wengi, na hasa kwenye masomo haya ya sayansi kwenye Chuo cha Nachingwe?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, kwa vile ametuletea wazo, basi tunaomba tulichukue twende tukalifanyie utafiti, tuangalie uhitaji wa kozi hiyo katika eneo hilo. Iwapo kama Serikali itabaini kwamba, upo huo uhitaji tutaweza kuingiza kwenye mipango yetu. Ahsante.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu, kutoka Mbulu Vijijini sehemu ya Haydom kwenye Mbulu Mjini ni kilometa 90 na kwenda Babati ni zaidi ya kilometa 130. Kwa majibu yake haoni kwamba atakuwa amewaondolea fursa vijana wa Mbulu Vijijini kupata uzoefu na ufundi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Mbulu Vijijini hatuna kabisa chuo, je, yuko tayari kutenga fedha sasa ili bajeti ijayo tuweze kupata chuo katika Jimbo la Mbulu Vijijini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Flatei, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kutoka Mbulu Mjini mpaka Mbulu Vijijini ni kilometa 90 lakini kama nilivyojibu katika swali langu la msingi kwamba Serikali inafanya juhudi mbalimbali za kutafuta fedha ili kuendelea na mpango wake wa ujenzi wa vyuo hivi vya VETA katika kila wilaya na mkoa. Kwa hiyo, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itakapopata tu fedha tutahakikisha kwamba maeneo yote ikiwemo na Mbulu Vijijini yatajengewa vyuo hivi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivi sasa naomba kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge kuwa tuna vyuo vingi ambavyo viko katika Wilaya ile ya Mbulu kiujumla. Tuna Vyuo vya Ufundi Stadi Mbulu, Haydom, Masieda, Jiendeleze, Integrity na St. Jude Yuda Thadei. Vyuo hivi vyote vinaweza kutumika kwa ajili ya vijana wetu kupata uzoefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, vyuo nilivyovitaja mwanzo vile vya Manyara vina nafasi ya wanafunzi kulala pale pale chuoni. Kwa hiyo, wanafunzi wetu hawa wanaotoka mbali wanaweza kupata fursa ya kupata ujuzi wao pale na kuondoa usumbufu huu wa kutembea au kwenda umbali mrefu.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na shukrani nyingi kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kufahamu juu ya Chuo cha VETA ambacho kimejengwa Wilayani Nyasa. Nafahamu kimeshafikia zaidi ya asilimia 95, ni nini mpango wa Serikali kuanza kutoa mafunzo ili vijana waweze kunufaika na chuo hicho?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Tunafahamu kwamba vyuo hivi ambavyo tayari ujenzi wake umekamilika, tuko katika mpango wa kuanza kutoa mafunzo mara moja. Suala lililokuweko mbele yetu sasa ni kuhakikisha kwamba tuna vifaa kwa ajili ya kufundishia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tuko kwenye mchakato wa manunuzi ya vifaa hivyo na pindi tu manunuzi hayo yatakapokamilika, program zile za ufundishaji katika maeneo haya zitaanza mara moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ina uhaba mkubwa wa walimu kwenye shule zake za msingi, jambo linalosababisha wazazi kuchangishwa kati ya 15,000 mpaka 20,000 kwa ajili ya kuajiri walimu wa kujitolea kwenye Kata ya Mlangali, Mavanga na Lugarawa. Je, ni lini Serikali itapeleka walimu wa kutosha kwenye shule za msingi za Wilaya ya Ludewa ikiwa ni pamoja na kuwaajiri wale walimu waliojitolea kwa muda mrefu?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, shule 23 za sekondari zilizopo Jimboni Ludewa hazijafanyiwa ukaguzi muda mrefu. Je, ni lini Wizara itatoa maelekezo kwa wadhibiti ubora wa elimu walioko pale Ludewa waweze kufanya ukaguzi huo kuliko kuendelea kusubiri wakaguzi kutoka kanda? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Spika, ni kweli tuna changamoto ya uhaba wa walimu katika maeneo mbalimbali nchini. Na kama mnavyofahamu hivi punde tu Mheshimiwa Rais aliagiza kwamba, wale walimu 6,000 ambao wa kuziba nafasi utaratibu wake uweze kufanyika mapema. Lakini kama mnavyofahamu mwaka jana mwezi wa Novemba Serikali ilitoa kibali cha kuajiri walimu zaidi ya 13,000. Tunaamini kati ya wale 13,000 walimu karibu elfu nane walikuwa tayari wameshasambazwa shuleni na walimu 5,000 walikuwa wanaendelea na mchakato.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika magawanyo huu sasa na hawa 6,000 watakaopatikana hivi punde watakwenda kutatua tatizo lile la upungufu wa walimu katika Halmashauri zetu ikiwemo na Halmashauri au Wilaya ya Ludewa.

Mheshimiwa Spika, hili la wazazi kuchangishwa, naomba tulibebe. Tutashirikana na wenzetu wa TAMISEMI tuweze kuangalia namna gani jambo hii linaweza likachukuliwa hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili amezungumzia suala la ukaguzi wa shule, Wizara inaendelea na kuimarisha Kitengo hiki cha Wadhibiti Ubora, ambapo hatua tofauti zimeweza kuchukuliwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2018/2019 mpaka hii 2020/2021. Wizara imeweza kufanya mambo yafuatayo; kwanza, tumeweza kusambaza Wadhibiti Ubora 400 katika Halmashauri zote nchini.

Pia katika kipindi cha mwaka 2018/2019 hadi 2020/ 2021 jumla ya ofisi za Wadhibiti Ubora 100 katika Halmashauri zetu zimeweza kujengwa na mpaka hivi navyozungumza tunaendelea na ujenzi wa ofisi 55 na ukarabati wa ofisi 31. Sambamba na hilo, Wizara yangu tumeweza kununua na kusambaza magari 83 kwenye Halmashauri tofauti tofauti.

Mheshimiwa Spika, lengo la kufanya hayo yote ni ili kuimarisha Kitengo chetu hiki cha Udhibiti Ubora hasa katika Halmashauri zetu. Kwa kufanya hivyo, tunaamini kutokana na ongezeko la shule nyingi ambazo zinahitaji kukaguliwa za msingi na sekondari tutaweza sasa kuzifikia shule hizo kwa umakini mkubwa.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge sasa Wadhibiti wetu wa Ubora hawa wa Wilaya watakwenda kufanya ukaguzi katika shule hizi za msingi na sekondari katika maeneo waliopo badala ya kutumia wale Wadhibiti Ubora wa Kanda ambao walikuwa wanakagua hizi shule katika kipindi kilichopita. Ahsante.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi hii. Hitaji ya chuo cha VETA katika Jimbo la Ludewa linafanana sana na hitaji ya chuo cha VETA katika Jimbo la Manyoni Mashariki.

Je, ni lini sasa Serikali itakuja na mpango wa kuhakikisha kwamba Jimbo la Manyoni Mashariki hususan Wilaya ya Manyoni inakwenda kujengewa chuo cha VETA? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mbunge wa Manyoni, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nimeeleza mara kadhaa katika Bunge lako hili Tukufu kwamba hivi sasa Serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo 29 katika Halmashauri mbalimbali nchini, ambapo jumla ya shilingi bilioni 48.6 zimeweza kutengwa na zinaendelea kutumika kwa ajili ya ujenzi huo. Serikali inaendelea na utaratibu wa kutafuta fedha kwa sababu lengo kuu ni kuhakikisha kwamba katika kila Wilaya na Mkoa tunakuwa na VETA.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishe Mheshimiwa Mbunge mara tu fedha zitakapopatikana tutahakikisha kwamba tunakwenda kujenga VETA katika Halmashauri ya Manyoni lakini na Halmashauri zote ambazo bado hazijafikiwa na VETA nchini. Ahsante.
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa kuwa Naibu Waziri amekiri kwamba anatambua uhitaji wa kuweka life skills na soft skills kwenye elimu yetu Tanzania.

Je, Serikali iko tayari sasa kwa ajili ya kuendana na mabadiliko ya mfumo ya Sayansi na Teknolojia pamoja kizazi kipya kwa sababu generation inabadilika. Serikali sasa ipo tayari kulifanya, kuifanya topic ya soft skills ambayo inafundishwa kwenye somo la civic kwa form one topic ya kwanza form two topic ya kwanza na form three topic ya kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo tayari sasa kufanya topic ya life skills iwe somo maalum sasa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba inatengenezewa utaratibu mzuri wa upimaji wa uelewa na kuhakikisha kwamba vijana wanapata maarifa zaidi kuliko kusoma kwa ajili ya kujibu mtihani?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali la pili, je, lini sasa Serikali itaanza mchakato wa kushirikisha wadau wa elimu wakiwemo wanafunzi wenyewe na watu wa ku-develop mitaala ili kuhakikisha kwamba wanayoyasema yanatekelezwa kwa vitendo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Nusrat kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nilivyoeleza katika jibu langu la msingi kwamba katika mwaka wa fedha 2021/2022 tunakwenda kufanya maboresho na mapitio ya mitaala kama nilivyozungumza hapo awali. Kwa hiyo, suala la kuingiza life skills, suala la kuhuisha mitaala ni suala ambalo lina mchakato mrefu ukiwemo na huo Mheshimiwa Mbunge aliouzungumza.

Kwa hiyo, tutahakikisha tunaenda ku-absolve au kuhusisha na mawazo hayo ambayo ulikuwa nayo maadam tayari hili lilishakuwa ni topic kwenye masomo naweza vilevile tukaifanya kama somo kwa kadri utafiti utakavyotuelekeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini suala kwamba ni lini, kama nilivyoeleza kwenye majibu ya msingi kwamba katika mwaka wa fedha 2021/2022 tutakwenda kuianza kazi hiyo kwa kadri itakavyowezekana. Ahsante.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwanza nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri aliyotoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba katika mwaka ujao wa fedha tutafanya mapitio ya mitaala. Lakini swali la nyongeza la pili la Mheshimiwa Nusrat alikuwa ameomba kwamba wadau washirikishwe. Nilikuwa nataka kumtoa hofu kwamba Serikali inapoandaa mitaala huwa inawashirikisha wadau na hata sasa hivi tutawashirikisha. (Makofi)

Kwa hiyo, nitumie Bunge lako Tukufu kuwaomba Waheshimiwa Wabunge kama kuna mambo yoyote ambayo wanadhani yanapaswa kuingia katika mitaala yetu Wizara ya Elimu tupo tayari kupokea maoni yenu. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na nashukuru Serikali kwa hatua iliyofikia katika kurekebisha masuala ya sera na mitaala kwa pande mbilli za Muungano, hata hivyo na maswali mawili madogo sana ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, muda mrefu sana Baraza la Mitihani lilikuwa likiwasiliana moja kwa moja na vituo vya mitihani vya Zanzibar na mara nyingi Wizara ya Elimu bila kuwa na taarifa. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuunda chombo maalumu cha kisheria ambacho kinatambulika ili kuweza kuunganisha Wizara ya Elimu ya Muungano na Wizara ya Elimu ya Zanzibar?

Mheshimiwa Spika swali langu la pili ni kuhusu elimu ya juu, katika Bunge la Kumi na Moja niliuliza na nikaambiwa linafanyiwa kazi kuhusu vyuo vikuu huria ambapo vilevile vyuo ambavyo vinatumika hapa na kutambulika na NACTE wale watu ambao wamefanya mitihani kupitia vyuo hivyo wanakubalika kufanya kazi Tanzania Bara na pia
wanatambulika kwamba wamesoma na vyeti vyao vinatambulika lakini kwa Zanzibar havitambuliki. Je, suala hili limefikia wapi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Giga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) ni Taasisi ya Muungano ambayo inaendesha mitihani hapa nchini. Baraza la Mitihani lina muundo wa namna ya kuendesha shughuli zake; tunakuwa na Kamati za Mitihani ngazi ya Taifa, Mikoa na Wilaya. Kamati hizi ndizo ambazo zinafanya ule mtiririko wa mawasiliano na mahusiano katika uendeshaji wa shughuli za Baraza la Mitihani. Kwa hiyo, kimsingi vyombo vipo, kwa kutumia Kamati hizi; ndizo ambazo zinaratibu pamoja na kuendesha mitihani kote nchini ikiwemo Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.

Mheshimiwa Spika, Baraza la Mitihani lina watumishi kule Zanzibar na vilevile tuna ofisi pale Zanzibar katika jengo lile la Shirika la Bima Zanzibar. Kwa hiyo, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba Baraza la Mitihani limejipanga vizuri na namna bora ya mawasiliano pamoja na co-ordination ni kama hivyo nilivyoeleza.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la pili, kwamba kuna vyuo ambavyo havitambuliwi na NACTE; naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba vyuo vyote vya elimu ya kati ambavyo vinahusika na masuala haya ya NACTE vimesajiliwa na NACTE na orodha ya vyuo hivyo ipo kwenye website.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, namqomba tu Mheshimiwa Mbunge labda tuweze kukaa na kuangalia kuna changamoto zipi kule Zanzibar ambapo labda kuna vyuo ambavyo havijapata usajili ili tuweze kujua kitu gani cha kufanya. Nakushukuru sana.
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ambayo yamenikatisha tamaa, nimechanganyikiwa, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Serikali ilianzisha Kitengo cha SUA huko Tunduru, Waziri anijibu, je, ni lini tawi hilo litaanza kufanya kazi kama Chuo Kikuu Kishiriki au Centre na twende wote huko tukaone?

Swali la pili, Vyuo Vikuu Vishiriki vya Taasisi ya Dini vilivyopo Kusini kama hicho alichokitaja, Stella Maris na kile kingine kipo pale Songea kinaitwa AJUCO, vimeendelea kuzorota na vingine vimefungwa. Serikali ndio inatakiwa kusimamia hivyo vyuo ili viweze kusimama kwenye sehemu yake. Mheshimiwa Waziri ataniambia wanasaidiaje hivi vyuo ambavyo watoto wanaosoma ni Serikali hii hii ili viweze kusimama na kufanya kazi yake kikamilifu? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Thea, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Chuo chetu cha SUA kilikabidhiwa eneo katika majengo ambayo yalikuwa ya camp ya waliokuwa wanajenga barabara. Serikali imefanya yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli udahili katika chuo hiki cha Tunduru bado haujaanza na kinachokwamisha kuanza udahili pale ilikuwa bado kuna miundombinu ambayo siyo toshelezi. Bado hakuna mabweni pamoja na maabara katika eneo hili. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, katika mwaka wa fedha 2020/2021, Chuo chetu cha SUA kimepanga kuanza kutoa kozi fupi fupi pale katika eneo letu la Tunduru kwa wakulima wetu kwa lengo la kuongeza mnyororo wa thamani kwenye mazao ya korosho, mihogo pamoja na ufuta.

Mheshimiwa Spika, halikadhalika majengo yale yaliyopo kwa hivi sasa yanatumika kwa ajili ya kufanya mafunzo kwa wanafunzi wetu wanaosoma Shahada ya Wanyamapori na Utalii. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Chuo chetu cha SUA kinaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kutosheleza au kujenga miundombinu ili tuweze kuanza kutoa huduma pale mara tu majengo hayo yatakapokuwa yamekamilika.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili, amezungumzia juu ya vyuo binafsi ambavyo vipo katika Kanda hiyo ya Kusini, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali imekuwa inafanya juhudi tofauti tofauti kuhakikisha vyuo hivi vinaendelea kutoa huduma. Serikali imekuwa ikifanya yafuatayo kupitia Tume ya Vyuo Vikuu:-

Mheshimiwa Spika, tumeendelea kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha kama vyuo hivi vinatoa huduma sawasawa na elimu Bora; Tume yetu imeendelea kutoa ushauri wa kitaalam; na Tumeendelea kutoa mafunzo kwa viongozi pamoja na Wahadhiri wa vyuo hivi. Katika mwaka huu fedha, TCU imeendesha mafunzo ya Wahadhiri pamoja na wamiliki zaidi ya 218 kuhakikisha kwamba vyuo hivi vinasimama sawasawa. Ahsante.
MHE. KHALIFA MOHAMED ISSA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuondoa tozo ile lakini pia mpango ambao Wizara ya Elimu inaupanga kuondoa tozo ya asilimia 10 kwa wanufaika baada ya grace period. Hata hivyo nina maswali mawili madogo ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa Serikali inakata asilimia 15 ya gross salary ya mnufaika baada ya kuajiriwa, je, haioni asilimia 15 ni kubwa haiwezi kuipunguza mpaka kufikia angalau single digit; asilimia 5, 6 mpaka 9? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili kwa kuwa mfuko huu unanufaisha wale degree holders haioni sasa wakati umefika kushuka chini katika vyuo vya kati kama vile VETA, FDCs na kadhalika?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba sasa kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Khalifa, Mbunge wa Mtambwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli wanufaika hawa huwa wanakatwa asilimia 15 kutoka kwenye mshahara wao ghafi kwa ajili ya kurejesha mikopo hii. Lengo la kukata asilimia 15 ni ili kuweza kurejesha fedha zile kwa haraka na kwa muda mfupi. Hata hivyo, tupokee mapendekezo ya Mheshimiwa Mbunge ya kuangalia namna gani tunaweza kupunguza eneo hilo. Kwa vile tarehe 4 na 5 ya mwezi huu tuliwasilisha bajeti yetu hapa na miongoni mwa mijadala iliyotokea ni kuhusiana na hii Bodi ya Mikopo na kwa vile tutakuwa na mjadala mpana wa kitaifa, nimuahidi Mheshimiwa Mbunge tunakwenda kulijadili na hili tuweze kuangalia namna gani tunaweza tukalizingatia.

Mheshimiwa Spika, swali la pili anauliza mikopo hii imewalenga sana wale wanaochukua elimu ya juu kwa maana ya degree, ni namna gani tunaweza tukafikia zile kada za vyuo vya kati. Kwa vile tutakuwa na mjadala mpana wa kitaifa juu ya mwelekeo ya elimu katika Taifa letu basi na hili nalo tutakwenda kulijadili kwa kina na ninyi Waheshimiwa Wabunge mtakuwa ni sehemu ya mjadala huo, tunaamini tutapata mawazo endelevu kuona ni namna gani tunaweza nalo hili tukaliingiza kwenye mpango.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa kuweka ulemavu kama kigezo kimojawapo cha upatikanaji wa mikopo kama ambavyo Bunge la Kumi na Moja liliweza kushauri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali hili si mara yangu ya kwanza naliuliza ndani ya Bunge hili, lakini pia mara kadhaa nilipopata kuchangia niliweza kuchangia na jibu limekuwa ni hili. Kama ambavyo jibu limesema kwamba Serikali italifanyia kazi, ni lini Serikali itaanza kulifanyia kazi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SANYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ikupa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwishajibu katika majibu yangu ya swali la msingi kwamba Serikali inaendelea kulifanyia kazi suala hili. Kama nilivyokwishaeleza hapa punde kwamba katika mjadala wetu wa bajeti tulisema kwamba tunakwenda kuwa na mjadala mpana kuhusiana na elimu yetu nchini kwa maana kwamba tunaenda kuangalia Sera yetu ya Elimu ya mwaka 2014, lakini tunaenda kuangalia Sheria yetu ya Elimu ya mwaka 1978. Hili nalo kwenye mjadala huo litakwenda kujadiliwa kwa kina na kuona ni namna gani tunaweza kuyafikia makundi haya badala ya kuwapa mikopo tukatoa ruzuku. Nadhani kabisa katika mjadala huo tunaweza tukayaingiza.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la msingi lilikuwa linalenga kwenye malengo ya mtaala; na malengo ya mtaala kwa mujibu wa sera ni kumwandaa mwanafunzi ili aweze kuendelea na ngazi zinazofuata za masomo. Hii imesababisha wimbi kubwa la wanafunzi wanaoshindwa kupata hiyo nafasi ya kuendelea kuachwa na mfumo wa elimu.

Je, Wizara sasa ina mpango gani wa kuboresha mtaala kwa kuongeza malengo ya kumwandaa mwanafunzi kujiajiri kwenye mazingira yake? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ni lini sasa au ni kwa namna gani Serikali inakwenda kutoa elimu ya lazima hadi Kidato cha Nne. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kama nilivyoeleza katika jibu langu la msingi kwamba tunakwenda kuwa na mjadala mpana ambao utakwenda kuhakikisha kwamba taaluma yetu na nchi yetu wapi tunapotaka kuelekea. Katika mjadala huo mpana tunaamini hayo malengo Mheshimiwa Mbunge anayoyazungumza, tutaweza kuyadadavua, kuyafafanua na kuyaweka kwa namna tunavyotaka yawe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyozungumza awali, kwamba mitaala yetu hii imekuwa ikifanyiwa maboresho na maboresho haya mara nyingi sana huwa yanalenga katika maeneo ambayo yamekuwa na changamoto. Kwa hiyo, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mjadala wetu mpana huu, malengo haya ambayo anayazungumza yatakwenda kuzingatiwa na vilevile maboresho ya mitaala yetu ili sasa vijana wetu wanapohitimu waweze kujiajiri nayo vilevile yanaweza kuzingatiwa. Ahsante.
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante pamoja na majibu haya ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza kwa niaba ya Mheshimiwa Zuberi Kuchauka, Mbunge wa Liwale. Swali la kwanza, je, Serikali inatuahidi nini katika bajeti ijayo?

Lakini swali la pili; je, Mheshimiwa Waziri au Naibu Waziri atakuwa tayari kwenda kuona juhudi za wananchi Liwale lakini wakati wa kwenda au wa kurudi apitie Kilwa Masoko kwa ajili ya kuona changamoto zilizopo katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kassinge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti ijayo kwasababu tuna ujenzi wa vyuo hivi 29 katika Wilaya 29 nchini. Katika bajeti ijayo tumepanga kununua vifaa ambavyo vitakavyowezesha sasa vyuo hivi ifikapo Januari, 2022 viweze kuanza kutoa huduma kwa maana kwamba vianze kutoa huduma ya kufundisha wanafunzi katika maeneo hayo. Hilo ndio lengo letu katika bajeti ijayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hili suala la pili la kuweza kwenda kuona maeneo haya nipo tayari, baada ya Bunge hili la Bajeti tutapanga ziara na hata jana tulikuwa na uwekeaji wa jiwe la msingi katika chuo chetu cha VETA pale katika Wilaya ya Ruangwa kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo pamoja na maeneo mengine na dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha kwamba nafika Liwale, lakini nitafika Ruangwa, lakini vilevile nitafika kwa ndugu yangu Kassinge pale Kilwa Kusini kuweza kuona changamoto zilizopo na kwa namna gani ya kuweza kuzitatua. Ahsante. (Makofi)
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Swali langu lilikuwa, kwanza niwapongeze Makete tumepata Chuo cha VETA ambacho kwa Mkoa mzima wa Njombe kipo Makete tu. Lakini tuna changamoto ya kozi ambazo mnazitoa pale nyingi hazipo kwenye soko kwa mfano; hatuna kozi ya ufundi magari, hatuna kozi ya ufundi umeme majumbani, hatuna kozi ya ambayo inashughulikia masuala ya mabomba kwa maana ya ufundi mabomba.

Je, ni lini Serikali italeta hizo kozi ambazo kwa sasa ziko kwenye soko Tanzania kutokana na hizi ambazo tunatekeleza kwenye Ilani hasa hasa suala la umeme vijijini ambapo wana Makete wengi wangependa wafanye kazi kwenye mazingira hayo lakini kozi hizo hazipo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia naomba nijibu swali la Mheshimiwa Sanga, Mbunge wa Makete kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tuna kozi ambazo ziko standard karibu kwenye maeneo mengi sana na kwa sasa hivi kunaonekana kama kuna uhitaji mkubwa sana kwenye baadhi ya maeneo kwamba tubadilishe kozi kuendana na maeneo yale yalivyo. Mfano, nilikuwa kule Mwanza katika Visiwa vile vya Ukerewe hakuna kozi zinazohusiana na masuala ya uvuvi. Lakini wakasema sasa ni muhimu sana tuweze kuianzisha kozi ile. Nimtoe wasi wasi Mheshimiwa Sanga kwamba jambo hili tunakwenda kulifanyia kazi, tutakwenda kukaa na uongozi wa Mkoa na kuhakikisha kwamba kozi hizi ambazo ni muhimu, lakini vilevile zenye soko kwenye maeneo hayo zinaenda kuanzishwa mara moja. Ahsante.
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Kwanza niipongeze Wizara, Waziri na Naibu wake wanafanya vizuri. Mwezi Januari Naibu Waziri alipita pale alifanya ziara na akatoa maelekezo mwezi wa tatu chuo kikamilike lakini nimefanya ziara Jumamosi tarehe 12 changamoto imekuwa ni kwamba fedha zinakwenda kidogo katika kukamilisha huu mradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba commitment ya Serikali katika kukamilisha fedha ambazo zitaenda kukamilisha huu mradi na kuanza udahili. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ngassa kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kulikuwa na kusuasua kidogo katika kupeleka fedha zile za awamu ya mwisho kuhakikisha kwamba tunakwenda kukamilisha ujenzi katika maeneo haya. Lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, fedha awamu ya mwisho zaidi ya Shilingi milioni 560 tayari zimeshapelekwa katika chuo hiki kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi huo na tutahakikisha kwamba tunasimamia vyema kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ifikapo Julai ili vijana wetu waweze kuanza mafunzo katika eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, uhitaji wa Chuo cha Ufundi VETA ambao unawakabili wananchi wa Wilaya ya Igunga unafanana sana na uhitaji wa chuo hicho katika Wilaya ya Kakonko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lini Serikali itajenga chuo cha ufundi VETA katika Wilaya ya Kakonko? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kamamba Mbunge wa Buyungu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni azma ya Serikali kuwa na Chuo cha VETA katika kila Wilaya hapa nchini. Kwa hiyo, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali iko makini, kwa hivi sasa tunakamilisha ujenzi wa vyuo hivi 29 katika Wilaya hizi 29 nchini.

Baada ya awamu hii kukamilika Serikali tutajipanga vema kulingana na upatikanaji wa fedha tutahakikisha kwamba tunakwenda kujenga chuo katika kila Wilaya hapa nchini. Ahsante.
MHE. JUDITH S. KAPINGA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali moja la nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kutokana na kwamba Sera yetu ya Sayansi na Teknolojia ni ya muda mrefu, ya miaka 25 nyuma, lakini vilevile kutokana na suala kwamba mapitio ya sera hii ili yaweze kuleta tija kwenye ubunifu yamekuwa yakichukua muda mrefu, tangu 2012, jambo linalosababisha programu za ubunifu chini ya COSTECH kutokutengewa fungu na kutegemea zaidi ufadhili na hivyo kukosesha vijana fursa nyingi zinazotokana na ubunifu: Je, Serikali haiwezi kutuambia ukomo wa muda wa mapitio haya ya sera ya kwamba yatakamilika lini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni kwa sababu tumeambiwa maboresho yamekuwa yanafanyika toka 2012 lakini hadi leo hayajafanyiwa kazi. Tunaomba Wizara ituambie ukomo wa muda wa kufanyia maboresho ili programu za ubunifu ziweze kuwa na tija kwa vijana wa Tanzania. Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba sasa kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kapinga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge. Wizara imekuwa ikitenga fedha katika kila bajeti kwa lengo la kuhakikisha kwamba eneo hili la ubunifu linafanyiwa kazi sawa sawa. Nimweleze tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Wizara imetengeneza mwongozo wa mwaka 2018. Vilevile mwongozo huu tunaendelea kuuboresha mwaka huu, tena tunaendelea kuupitia upya ili kuweka mwongozo huu sawa sawa, nimtoe wasiwasi.

Mheshimiwa Spika, pia anataka kujua kwamba ni lini Serikali itakamilisha utungaji huu au mapitio haya ya sera? Ndani ya mwaka huu wa fedha tutalifanya hilo na kuhakikisha jambo hili linakaa sawa sawa. Ahsante. (Makofi)
MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali, nitakuwa na maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; pamoja na kutoa elimu hii katika shule zetu bado suala la mimba za utotoni ni changamoto katika jamii. Je, Serikali haioni umuhimu wa kufanya utafiti tunakosea wapi na wakati masomo yote tunatoa kwa watoto wetu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; ni kuhusu Uraia. Tuna Somo la Uraia kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita, lakini suala la uzalendo limeondoka miongoni mwa wananchi wetu. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuweka mada maalum ya uzalendo kwenye Somo la Uraia?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Najma Murtaza Giga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inaendelea kufanya utafiti na kutilia mkazo juu ya masuala haya ya maadili. Kwa kuliona hilo katika miaka ya nyuma wanafunzi wetu wa shule za msingi walikuwa wanafanya mitihani katika masomo matano, lakini katika mwaka huu katika mitihani ambayo imeanza leo kwa kuona umuhimu wa somo hili la maadili tumeanza sasa kulifanyia mitihani ili kulijengea uwezo na kulitilia msisitizo zaidi. Kwa hiyo nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba tunafanya utafiti na kwa umuhimu wa masomo haya imeonekana ni vyema vilevile nayo yakawa sehemu ya mitihani ya wanafunzi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hili, nitoe wito tu kwa ndugu wazazi na walezi; jukumu la malezi ya watoto ni la jamii nzima, siyo la shule wala Walimu peke yake. Hivi sasa imetokea tabia na mtindo kwamba majukumu sasa ya malezi ya watoto wetu yamekuwa ya shule peke yake. Kwa hiyo tutoe wito kwamba, majukumu haya ni ya kwetu kuhakikisha kwamba maadili ya watoto wetu pamoja na mienendo ya taaluma zao tunafuatilia kwa karibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la pili, kwamba Serikali sasa tuna mpango gani? Nimtoe wasiwasi vilevile Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wote, mchakato tunaoendelea nao sasa wa kuboresha mitaala yetu, mambo haya yote tutayatilia mkazo. Waheshimiwa Wabunge mna nafasi nzuri ya kutoa mawazo yenu ili kuweza kuangalia namna gani tunaweza tukatengeneza maadili, lakini tukaweka taaluma vizuri kwa vijana wetu kuhakikisha kwamba tunahitaji kizazi gani chenye maadili gani cha huko mbele tunakokwenda.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
MHE. PHILLIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Swali langu la nyongeza kwa Wizara ya Elimu, pamoja na Wizara ya Afya ni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, miaka ya nyuma kidogo huko shuleni kulikuwa na utaratibu wa kuwapima mimba wanafunzi kuanzia darasa la sita, la saba na hata sekondari, lakini miaka ya hivi karibuni nimekosa kumbukumbu ni kama suala hilo halipo, kwa sababu na mimi ni mdau wa elimu, labda kama wanapima kwenye shule za Serikali. Je, kwa nini Serikali haioni umuhimu wa kuanza kupima mimba angalau mara mbili kwa mwaka kuanzia darasa la sita, la saba na upande wa sekondari ili kuwaweka wanafunzi wa kike hata wa kiume kuwe na tension fulani kwamba kuna kupima mimba mara mbili kwa mwaka na kuacha mimba za utotoni?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mulugo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu huu kimsingi upo pindi watoto wetu wanapotoka likizo tunafanya utaratibu huo. Sasa nimtoe wasiwasi tu Mheshimiwa Mbunge, labda tuweze kuendelea kuutilia tu msisitizo na mkazo ingawa hatuufanyi in public, unafanyika kule shuleni na kinakuwa kitu ambacho ni cha kishule zaidi kuliko kutangaza, lakini kimsingi ni utaratibu ambao upo unatumika kwenye shule zetu za Serikali, vijana wetu wanapotoka likizo huwa utaratibu huo unakuwepo. Hata hivyo, tuchukue vilevile wazo lake, tuendelee kuliimarisha na kuliboresha tuweze kuangalia namna gani ya kufanya. Ahsante sana.
MHE. ALLY Y. MHATA: Mheshimiwa Spika, kwanza naishukuru sana Serikali kwa majibu mazuri kuhusiana na swali hili, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, Kijiji cha Maneme ambapo ndipo yalipo majengo haya kilishaandika barua kukabidhi majengo haya kwa Serikali. Mimi kama mwakilishi wao niliwasilisha barua yao ya kukabidhi hili eneo kwa Wizara. Kwa hiyo, nataka kupata commitment ya Serikali. Ni lini watendaji hawa wa Serikali watakuja ndani ya wilaya yangu ili kuyahakiki majengo haya? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa suala hili la ujenzi wa Vyuo vya VETA liko ndani ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na sisi wananchi wa Jimbo la Nanyumbu tunayo majengo tayari, je, Serikali haioni haja kwa Mwaka ujao wa Fedha majengo haya yakatumika ili wananchi wa jimbo langu wakanufaika?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mhata, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye majibu yangu ya msingi kwamba tayari timu yangu ya wataalam kutoka Wizara itakwenda eneo hili. Mheshimiwa Mbunge anataka kujua lini, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwa vile tuko hapa Bungeni na Makao Makuu ya VETA yako hapa Dodoma, nimwombe tu Mheshimiwa Mbunge mara baada ya kipindi hiki tuweze kuonana, twende wote kwa Mkurugenzi wa VETA pale ofisini, twende tukaipange vizuri ili tujue wataalam wetu wale lini watakwenda kwenye eneo hili la kuweza kufanya tathmini ya pamoja na kujua kitu gani cha kufanya kule Nanyumbu.

Mheshimiwa Spika, kwenye eneo la pili, kwamba majengo yapo, kuna baadhi ya miundombinu itahitaji kuongezwa; naomba hili tulichukue tuweze kuangalia katika bajeti ijayo iwapo kama itaturuhusu kuweza kuingiza bajeti ya kuongeza miundombinu katika eneo hili. Wakati tathmini hii ikishafanyika itatupa dira ya wapi tunakoelekea, mahitaji gani yatakayohitajika na ni commitment gani itahitajika ya kifedha kuweza kwenda kuongeza miundombinu kwenye eneo hili. Kwa hiyo hili tunaomba tulichukue tutaenda kulifanyia kazi na baada ya tathmini yetu hiyo tutakutana na Mheshimiwa Mbunge kumwonesha kitu gani tunachoweza kukifanya kwenye eneo hili. Ahsante sana.
MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa changamoto ya wananchi wa Nanyumbu inafanana kabisa na changamoto ya wananchi wa Jimbo la Mlimba pale Kata ya Mchombe.

Mheshimiwa Spika, Kata ya Mchombe tayari tuna majengo pale. Huko awali kulikuwa na kituo kidogo cha VETA na vijana walikuwa wakijifunza pale, sasa kituo kile kilifungwa na majengo yale hayatumiki.

Je, Wizara haioni umuhimu inavyoenda kufanya tathmnini Nanyumbu hiyo timu ya wataalamu ikafanya pia tathmini pale Mlimba Mchombe, kwa sababu majengo ya Serikali yanaendelea kuharibika tu?

Mheshimiwa Spika, ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kunambi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama ulivyoeleza kwenye utangulizi wako Mheshimiwa Kunambi nadhani wakati tunaunda hii timu kwa vile barabara ni hiyo hiyo moja ya kwenda Nanyumbu nadhani ni lazima tupite Morogoro, tutaona busara itakavyotutuma nadhani timu hii itapita katika eneo hilo. Ahsante sana.
MHE. JUMANNE A. SAGINI Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, kwa kweli yanaleta matumaini. Hofu yangu ni moja tu, kwamba hizi lugha za mchakato, mchakato wakati mwingine unaweza ikachukua muda mrefu. Wakati nachangia hotuba ya bajeti ya Wizara hii, waliniahidi kwamba mwaka wa fedha utakapoanza utaanza harakati za ujenzi. Lakini hadi leo wanazungumzia mchakato, sasa hebu atuhakikishie hii michakato ya ku- procure huyo consultant ili afanye review ya hizi design zitakamilika lini na ujenzi uweze kuanza? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Jumanne Abdallah Sagini, Mbunge wa Butiama kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika kama nilivyoeleza kwenye jawabu la msingi kwamba taratibu zote sasa zimekamilika; na upatikanaji huu wa fedha kama nilivyozungumza kwamba umeanza mwezi wa Septemba. Tunatarajia kama mambo yote yatakwenda vizuri mpaka kufika mwezi wa Februari shughuli za ujenzi katika eneo hili inawezekana zikawa zimeanza rasmi. Ahsante sana.
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Moja, namwomba Mheshimiwa Waziri aweze kutupa Mpango wa Serikali: Ni kwa muda gani chuo hiki kitakuwa kimekamilika na kuanza kutoa mafunzo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili: Kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Ludewa kwa umoja wao wamechangia fedha na nguvu zao kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya wanafunzi watakaokuwa na ufaulu mkubwa wa Darasa la Saba.

Je, ni lini Serikali katika kutambua jitihada za wananchi na kuunga mkono juhudi zao? Ni lini Wizara itatuma watalaamu kwa ajili ya kwenda kusajili shule ile ili watoto waweze kuanza kusoma pale?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante; naomba sasa kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kamonga Mbunge wa Ludewa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Kamonga pamoja na wananchi wa Ludewa na vilevile Watanzania wengine walioko kwenye Mikoa ya Rukwa, Geita pamoja na Simiyu, kwa sababu katika maeneo ambayo vyuo vya mikoa vinaenda kujengwa ni pamoja na maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala la muda, tunatarajia ndani ya miezi minane kutoka leo vyuo hivi vinakwenda kukamilika kwa sababu fedha hizi zina muda maalumu wa utekelezaji kuhakikisha kwamba miradi hii inafanyiwa kazi sawa sawa. Kwa hiyo, niwahakikishie tu, Mheshimiwa Rais ametoa fedha hizi kwa kuhakikisha katika kipindi hiki kifupi huduma hizi zinaweza kupatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la pili, anazungumzia Shule ya Sekondari; nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Ludewa kwamba taratibu za kufuata zipo wakati wa kufanya ukaguzi na kusajili shule hizi. Namshauri Mheshimiwa Mbunge kupitia Mkurugenzi wa Halmashauri kuweza kuandika barua kupeleka kwenye idara yetu ya Udhibiti Ubora iliyokuwepo katika Wilaya ile ya Ludewa na wataalamu wetu wale wakishapata tu barua na maombi hayo, mara moja wanatakiwa kwenda kwa ajili ya kufanya ukaguzi ili kutengeneza ithibati iwapo viwango vile vimethibitika kuwepo, basi usajili huo utapatikana. Ila kwa vile amelizungumza suala hili hapa Bungeni, tutakwenda kulifanyia kazi kuhakikisha kwamba wiki ijayo wataalamu hao waweze kwenda kwenye eneo hilo la shule ili kuweza kupata usajili ili vijana wetu kama Januari shule hii inaweza kufunguliwa, iweze kufunguliwa na wanafunzi waweze kupata huduma. Ahsante. (Makofi)
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ningependa tu kujua ni lini Serikali sasa itajenga Chuo cha VETA katika Wilaya ya Kilolo ambayo tayari ina ongezeko la vijana na chuo kinahitajika ili nao waweze kujiendeleza kama ilivyo kwenye maeneo mengine? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba sasa kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivi sasa Serikali inaendelea na ukamilishaji wa vyuo vile vya VETA katika wilaya 29 ambazo sasa zinakwenda kukamilisha, lakini siyo tu kukamilisha na kuhakikisha vile vile vifaa kwa ajili ya mafunzo vinaweza kupatikana. Kwa hiyo katika mwaka huu wa fedha, juhudi za Serikali tunajikita kwenye eneo hilo, kukamilisha vyuo hivi vya wilaya 29, lakini na vile vya mikoa vinne. Kwa hiyo, nimhakikishie, baada ya ukamilishaji wa vyuo hivi, Serikali sasa tunajipanga vizuri kutafuta fedha ili kuweza kufikia wilaya zote kama sera yetu inavyosema kwamba kila wilaya ni lazima iwe na Chuo cha Ufundi cha VETA. Ahsante sana.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa fursa hii. Matatizo ya Ludewa yanafanana sana na matatizo ya Wilaya ya Muleba. Wilaya ya Muleba ni kubwa yenye watoto wengi wanaohitimu darasa la saba, form four na kidato cha sita.

Je, ni lini Serikali itatujengea Chuo cha VETA katika Wilaya ya Muleba? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba sasa kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kikoyo, Mbunge wa Muleba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwa upande wa Kilolo, Serikali inaendelea kutafuta fedha baada ya ukamilishaji wa vyuo hivi 29 katika wilaya 29 ambayo tumeanza kwa awamu ya kwanza kuweza kuzifikia wilaya nyingine ikiwemo na Wilaya ya Muleba. Kwa hiyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Kikoyo katika muda mfupi ujao baada ya Serikali kupata fedha tutahakikisha kwamba kila wilaya tunaifikia ikiwemo na wilaya ya Muleba. Ahsante sana.
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa Jiji la Dar es Salaam lina idadi kubwa ya watu zaidi ya milioni sita na tunategemea Chuo cha VETA kimoja tu maarufu cha Chang’ombe na Wilaya ya Ubungo sasa ipo pembezoni na idadi kubwa ya watu na eneo tunalo: -

Je, ni lini sasa Serikali itajenga Chuo cha VETA katika Wilaya ya Ubungo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kutoa jibu dogo kwa Mheshimiwa Mtemvu Mbunge wa Ubungo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza kwenye maeneo mengine, nitoe rai na wito kwa Mheshimiwa Mtemvu, kwa sababu Ubungo ni Jiji na ni eneo kubwa na mapato yake ni makubwa, kwa hiyo, aone umuhimu nalo wa jambo hili. Basi angalau kwenye mapato ya ndani pale kama wanaweza wakatoa kasma kidogo wakaanza mchakato huu wa ujenzi, pindi pale Serikali itakapopata fedha kwa ajili ya vyuo hivi vya wilaya, basi tutakwenda kuongezea nguvu na kukamilisha chuo hicho.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Sasa Mheshimiwa Naibu Waziri naona Wabunge wengi wanauliza vyuo vya VETA huko kwenye maeneo yao, hebu tuambia kwa ujumla mpango wa Serikali kuhusu ujenzi wa vyuo vya VETA. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mpango uliokuwepo hivi sasa kwa mwaka huu wa fedha, bado tunaendelea na ukamilishaji wa vyuo vile 29 na vile vile kununua vifaa. Kwa sababu lengo letu ni kuhakikisha vyuo hivi siyo tunajenga tu majengo, bali vile vile kuhakikisha kwamba tunapeleka pamoja na vifaa ili viweze kufanya kazi na kutoa elimu kwa vijana wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, katika mwaka ujao wa fedha, jukumu la Serikali ni kuhakikisha kwamba sasa tunaweza kutenga bajeti kwa ajili ya awamu ya pili ya ujenzi wa vyuo vingine vya wilaya. Huo ndiyo mpango uliopo mpaka hivi sasa. Ahsante sana.
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza kwenye swali langu la msingi. Kwa kuwa Serikali imewaelekeza wananchi wa Handeni kuendelea kutumia Chuo cha Wananchi cha Maendeleo kilichopo Handeni wakati tukingoja ujenzi wa Chuo cha VETA katika Wilaya yetu: Je, ni lini Serikali itapeleka vifaa vya kufundishia kwenye chuo hiki cha FDC kwa maana ya vitabu, mitambo na mashine? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Je, Serikali haioni umuhimu wa kukiendeleza chuo hiki cha FDC kilichopo ili kifikie kuwa katika hadhi ya Chuo cha VETA? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kwagilwa, Mbunge wa Handeni Mjii kama ifuaavyo: -

Mheshimiwa Spika, tarehe 10/10/2021 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliubainishia Umma kwamba tumepata fedha zile ambazo zinatokana na namna gani tunaweza kuondoa changamoto ya Uviko 19.

Katika fedha hizo, jumla ya shilingi bilioni 6.8 zimetengwa kwa ajili ya kupeleka vifaa pamoja na mitambo ikiwemo na vitabu katika vyuo 34 vya FDC. Miongoni mwa vyuo hivyo 34, kimojawapo ni hiki chuo cha Handeni.

Kwa hiyo, nimtoe wasiwasi kwanza Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga vizuri, tunakwenda kupeleka vifaa pale ili kuhakikisha tunaboresha mazingira ya ufundishaji pamoja na vifaa ili vijana wetu waweze kupata taaluma yao katika eneo lile. (Makofi)

Katika eneo la pili anazungumzia namna gani tunaweza kuboresha chuo kile labda kiweze kuwa na hadhi ya VETA. Vyuo hivi vya FDC vilianzishwa kwa mkakati maalum wa kuhakikisha tunapeleka maendeleo katika maeneo yale. Hatuna sababu ya kuvibadilisha vyuo hivi kwenda kuwa VETA, ingawa bado vinatoa mafunzo haya ya VETA.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwa vile Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba tunakwenda kujenga VETA katika kila Wilaya katika mipango yetu ya baadaye, chuo hiki tutaendelea kukiimarisha ili kiweze kutoa mafunzo na tija katika eneo hili ambalo limekusudiwa na Serikali wakati Serikali inajipanga kutafuta Chuo cha VETA katika eneo hilo. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Naomba niipongeze Serikali kwa majibu mazuri na wameonesha kabisa kwamba mmeongeza vitabu. Pamoja na hayo yote naomba niongeze swali la kuhusu watu wenye uoni hafifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wenye uoni hafifu shuleni wanapata taabu sana, kwa sababu Walimu wengi hawafahamu namna ya kuwafundisha hawa watu ili waweze kuelewa. Wanapata tabu ubaoni na kwenye karatasi kwa sababu maandishi yanakuwa ni madogo. Je, Serikali haioni haja ya kupeleka mwongozo kwenye shule zote na Walimu wote wafahamu namna gani ya kuwafundisha watoto wenye mahitaji maalum, hasa hao wenye uoni hafifu ambao wengi ni wenye ulemavu wa ngozi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, tunafahamu kabisa, katika suala la afya na maradhi watu wenye ulemavu wanapata shida sana na wanapata maradhi kutokana na hali ya usafi na mazingira pale shuleni. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha miundombinu, kuongeza vyoo vya watu wenye ulemavu shuleni ili hawa watu waweze kusoma vizuri? Kwa sababu tunaamini kabisa kwamba elimu ndio ufunguo wa maisha na elimu ndiyo mkombozi wa watu wote wenye mahitaji maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Khadija taya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli anayoyazungumza Mheshimiwa, kwamba wenzetu wenye uoni hafifu, hasa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi wanapata changamoto shuleni. Naomba nimhakikishie Mheshimwia Mbunge pamoja na Bunge lako Tukufu kwamba, Serikali yetu hii ya Awamu ya Sita chini ya Mama Samia Suluhu Hassan tumejipanga vyema katika kuhakikisha kwamba tunakwenda kuishughulikia changamoto hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimweleze tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari Wizara iko mbioni kutekeleza au kukamilisha mwongozo ambao utakwenda kushughulikia eneo hili la wanafunzi wetu wenye changamoto ya uoni hafifu, tukishirikiana na wenzetu wa Shirika Binafsi la Under the Same Sun. Kwa hiyo nimwondoe kabisa wasiwasi, kwamba mwongozo huo uko mbioni kuja na mara utakapokamilika na kusainiwa tutausambaza kwenye maeneo hayo ili kuhakikisha kwamba tunaitatua changamoto hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishie vile vile Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali yetu tayari imeweza kusambaza vitabu vyenye maandishi makubwa kwa ajili ya wenzetu hawa ambao wana uoni hafifu. Kwa hiyo kule kwenye shule zetu zote za msingi pamoja na sekondari mambo yanakwenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili anazungumzia suala la miundombinu. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mgawanyo wa fedha za UVIKO-19, zile ambazo tulizipata kupitia Wizara ya Elimu pamoja na TAMISEMI zaidi ya Shilingi bilioni 2.4 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo zaidi ya 2200 kwa ajili ya wanafunzi wetu wenye mahitaji maalum kupitia hizi za UVIKO-19 na zile za GPE lenses na mchakato huu unaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kupitia mradi wetu wa EP4R umeweza kujenga jumla ya matundu 4,549 kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule zetu za msingi na sekondari. Tunaendelea kuboresha miundombinu hii kwa kuhakikisha na wao tunawatengenezea mazingira wezeshi ili isiwe changamoto kwao katika kupata elimu yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie nafasi hii kuipongeza na kuishukuru sana Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo inazishughulikia changamoto mbalimbali za watu wenye ulemavu ikiwemo changamoto hii ya lugha ya alama; na ikikumbukwa kwamba changamoto hii niliweza kuizungumzia sana katika Bunge la Kumi na Moja, lakini hatimaye leo hii Serikali ya Awamu ya Sita imeanza kulifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii itasaidia jamii yetu, yaani tunandaa kizazi ambacho kitaweza kuwasiliana na viziwi kwa maana ya Polisi, Walimu, Madaktari hata kwenye familia zetu. Kwa hiyo, naipongeza sana Serikali. Sina uwezo wa kupiga magoti, ningepiga magoti kuishukuru Serikali ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza la nyongeza ni kwamba, ni lini sasa mchakato huu utakamilika na hatimaye mitaala hii kuanza kutumika ndani ya nchi yetu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wakati tunasubiri ukamilishwaji wa mchakato huu, Serikali ina njia gani mbadala ya kuinua kiwango cha elimu kwa wenzetu viziwi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza naomba tupokee hizo pongezi za Mheshimiwa Rais kwa niaba yake, lakini tunaamini pongezi hizi zimemfikia na hiyo ndiyo Serikali ya Awamu ya Sita, Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan na huo ndiyo wajibu wetu kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kulitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba mchakato huu wa maboresho ya mitaala yetu ni agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alioutoa tarehe 22 Aprili, 2021. Mara tu baada ya maagizo yale, sisi kama Wizara tulikaa na kuanza kuyafanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchakato huu huwa unachukua muda mrefu, ni kati ya miaka mitatu mpaka mitano. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutajitahidi kuhakikisha kwamba katika kipindi kifupi kisichozidi miaka mitatu na miezi tisa mitaala yetu hii mipya iweze kuwa tayari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilihakikishie Bunge lako Tukufu, ifikapo mwaka 2025 Januari, mitaala yetu mipya itakuwa tayari kuanza kutumika katika maeneo yote kama tulivyokusudia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili amezungumzia juu ya namna gani watoto wetu tunawachukuwa kwa sasa hivi? Nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ipo mbioni na inaendelea kuwahudumia wanafunzi hawa au watoto wetu hawa. Kwanza tuna shule ya msingi ambazo tumejenga kule Mtwara inayoitwa Lukuledi kwa ajili ya kuwachukua wanafunzi hawa wenye matatizo ya uziwi kwa upande wa Shule za Msingi. Vilevile kule Patandi Arusha, tuna Shule ya Sekondari kwa ajili ya wanafunzi hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, katika kipindi hiki tumeweza kutoa mafunzo kwa Walimu kwenye shule ambazo zinachukua wanafunzi wenye uziwi katika shule zetu zote za Sekondari katika kipindi kilichopita; na pia mwezi Machi mwaka huu Walimu wetu wa Shule za Msingi kwa shule zinazochukua wanafunzi hawa, nao vilevile tutawapa mafunzo ya lugha ya alama na kuwapa mbinu za namna ya kuwafundisha wanafunzi hawa. Ahsante. (Makofi)
MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa kuwa kuna uhaba mkubwa sana wa Walimu wa Elimu Maalum nchini Tanzania na hasa katika Mkoa wangu wa Songwe; na sasa hivi Serikali ina-practice inclusive education kwa maana ya elimu jumuishi: -

Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka iwe ni compulsory kwa kila Mwalimu ambaye anasomea masuala ya elimu, kusomea elimu maalum kwa ajili ya watoto wetu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Shonza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu katika majibu yangu ya msingi, amezungumzia suala la inclusive education na nimeeleza, katika kipindi kilichopita tumeweza kutoa mafunzo kwa Walimu wote wa Shule za Sekondari katika shule zile ambazo zinachukua wanafunzi hawa wenye uziwi. Katika mwaka huu tunatarajia mwezi Machi tutafanya mafunzo kwa Walimu wote wa shule za msingi zile ambazo zinachukua wanafunzi hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa vile lengo lake ni kuhakikisha kwamba mitaala yetu inakwenda kuboreshwa ili somo hili liwe compulsory, hili ni eneo ambalo tutakwenda kulifanyia kazi katika uboreshaji wa mitaala hii ili wakati tunapoandaa mitaala, masomo ya lugha ya alama na mbinu za kufundishia wanafunzi wenye uziwi yaweze kuingia kwenye mitaala yetu. Ahsante sana.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba niulize swali dogo la nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili tuweze kuwawezesha vijana wetu waweze kupambana na changamoto za uchumi wa kidigitali. Je, Serikali ina mpango gani wa kuingiza rasmi somo la TEHAMA, hususan kwa vitendo, katika mitaala yetu ya elimu ya msingi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Zaytun Swai, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza kwenye jibu langu la msingi. Kwa vile tunaenda kuboresha mitaala yetu na anazungumzia suala la TEHAMA kuweza kuingia katika mitaala yetu ili liweze kuwa compulsory, huu ndio wakati muafaka. Tunaomba tuyabebe mawazo haya na kwa vile tunaenda kuboresha tunaamini kabisa mtaala tutakaokuja nao ni ule ambao utakwenda kukidhi mahitaji ya Waheshimiwa Wabunge, lakini na Waheshimiwa wananchi wa Tanzania. Nakushukuru sana.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, Shule ya Msingi ya Endakoti katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu ina wanafunzi 40 wa elimu maalum. Shule hiyo iliyojengwa mwaka 1929 inakabiliwa na changamoto ya miundombinu. Je, ni lini Serikali itatekeleza azma yake ya kuteua shule mojawapo kila halmashauri itakayochukua wanafunzi wa elimu maalum ili vitengo hivyo viboreshwe kupata miundombinu na huduma nyingine?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Zacharia, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Zacharia kwa kuona umuhimu wa watoto wetu hawa kuweza kupata mazingira wezeshi na miundombinu wezeshi ili kuweza kufikia ndoto zao. Suala la uboreshaji wa mazingira ni suala endelevu na nadhani tumeona kwenye Serikali yetu kwenye kipindi hiki kifupi kilichopita zaidi ya trilioni 1.3 tulizozipata zimeweza kwenda kwenye eneo kubwa sana la miundombinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika kipindi kijacho, kwa vile sasa tunaandaa bajeti, tutahakikisha kwamba, maeneo haya ambayo yanachukua wanafunzi wetu wenye mahitaji maalum tutakwenda kuyafanyia kazi na kuyapa kipaumbele kuhakikisha kwamba, yanapata miundombinu wezeshi, lakini vilevile na Walimu wa kutosha kwa ajili ya kuwafundisha watoto wetu. Ahsante sana.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kunipatia nafasi ya swali la nyongeza. Kwa kuwa, idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita inaongezeka mwaka hadi mwaka; na kwa kuwa, bajeti yetu na uwezo wetu wa kuwagharimia kupata mikopo sio mkubwa sana. Je, Serikali haioni sasa ni muda muafaka kuanza maongezi na mazungumzo na benki za kibiashara, ili Serikali iwadhamini vijana wetu ambao wanakosa mikopo, ili wapate mikopo kupitia benki za biashara kwa riba nafuu ambayo Serikali itaweza kuwadhamini?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba sasa kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Kikoyo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa vile ametuletea pendekezo, ametuletea wazo. Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge naomba nilihakikishie Bunge lako tunaomba tulibebe pendekezo hili la Mheshimiwa Dkt. Kikoyo twende tukakae chini, tulifanyie kazi, tufanye tathmini ya kina na pindi tutakapoona kwamba, jambo hili linafaa, basi tutakuja kulieleza kwenye Bunge lako Tukufu ni namna gani ya kuliendea jambo hili. Ahsante sana.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kiuhalisia Wizara ya Elimu ni miongoni mwa Wizara ambayo inaonekena inatengewa bajeti kubwa, lakini unakuta pesa nyingi katika Wizara hii ni pesa za mikopo ya elimu ya juu ambayo mara nyingi wanaziweka kama ni fedha za miradi ya maendeleo, lakini kimsingi pesa zile zilitakiwa ziwe kwenye matumizi ya kawaida kwa sababu, zinaenda kuwasaidia vijana wetu pesa za kujikimu. Hii imekuwa ni mapendekezo ya Kamati mbalimbali, ikiwepo Kamati ya Bajeti.

Je, ili kuitendea haki Wizara hii kwa nini hizi pesa za mikopo msiziweke kwenye matumizi ya kawaida ili sasa tujue, kama Bunge, tuna jukumu gani la kutenga pesa za kutosha kwenye miradi ya maendeleo iende kwenye utekelezaji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Ester Bulaya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa vile hili ni wazo la Mheshimiwa Mbunge na amesema kwamba, ni mapendekezo ambayo yalitolewa na Kamati mbalimbali, sisi kama Wizara tutaenda kukaa na Wizara ya Fedha kuweza kuona namna gani jambo hili linaweza kwenda kufanyiwa kazi, lakini kimsingi tunaomba tulibebe. Ahsante.
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Kwa kuwa mitaala pamoja na mikopo huzalisha wahitimu na kwa sababu, Wizara hii ndio Wizara ya kisera. Kwa mujibu wa taarifa ambayo ilitolewa hapa Bungeni na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mwaka, kati ya ajira zilizoombwa za ualimu elfu 10, walioajiriwa kama elfu 10, lakini waombaji walikuwa zaidi ya laki moja. Maana yake ni kwamba, ukiangalia mpaka waliohitimu mwaka jana ukijumlisha pale ni zaidi ya laki moja wako mtaani hawajapata ajira. Sasa swali langu, ni kwa nini Serikali au Wizara hii wasijadili hili suala la ajira ili kuwasaidia, hasa Walimu ambao ni Walimu wa Kiswahili, waende kufundisha Kiswahili kwenye nchi za Afrika Mashariki pamoja na SADC?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Kakunda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ajira ni suala ambalo ni mtambuka na kwa vile Mheshimiwa Mbunge anatoa pendekezo kwamba, tuweze kuangalia namna gani tunaweza tukawasaidia Walimu kwenda kufundisha kwenye nchi hizi za Afrika Mashariki na Kati na Kusini mwa Afrika, tunaomba vilevile suala hili tulichukue, twende tukaangalie hizo fursa ambazo zinatokea kwenye nchi hizo na namna gani tunaweza tukakaa kitako na kuweza kushawishi namna gani Walimu wetu ambao wamehitimu kwenye shahada mbalimbali za ualimu, hasa hizi za Kiswahili kwenye vyuo vyetu, wanaweza kwenda kutumika kwenye maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, tunajua kwamba, masuala ya ajira mara nyingi sana yana-competition zake kwa sababu itakwenda kwenye usaili na watahitajika kwenda kwa ajili ya usaili huo. Kwa hiyo, hatuwezi kutoa guarantee moja kwa moja kwamba, tutafanya hivyo kwa asilimia 100, lakini nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, kwamba tunalichukua, tutaenda kulifanyia kazi na kuweza kuangalia namna gani nafasi hizo zinapatikana na tunaweza kunufaika sisi kama nchi.
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona na kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Katika uendelezaji wa sekta ya afya pamoja na sekta nyingine kuna watumishi ambao wanahitajika sana sasa hivi, kwa mfano clinical officers, wafamasia na hawa hawasomi vyuo vikuu. Kumekuwa na pendekezo la muda mrefu sana la kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati ambalo ni hitaji kubwa sana katika nchi yetu kwa sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali sasa ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba, wanafunzi wanaosoma vyuo vya kati pia wanapata mikopo kwa sababu, ndio mahitaji makubwa katika nchi yetu kulingana na miundombinu tunayoijenga kwenye maeneo ya vijijini ambayo yanahitaji sana hiyo kada ya kati kulitumikia Taifa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli analozungumza Mheshimiwa Mbunge kwamba, uhitaji uko mkubwa sana kwenye vyuo vyetu vya kati, lakini kama tunavyofahamu na kama nilivyoeleza kwenye majibu ya swali la msingi, jambo kubwa hapa ni suala la bajeti. Iwapo kama bajeti yetu inaruhusu tunaweza tukavifikia vyuo vikuu vyote, lakini vilevile pamoja na vyuo vya kati. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge, bajeti itakaporuhusu tutahakikisha tume-cover kwanza eneo lote la vyuo vikuu halafu tutaangalia namna gani sasa mikopo hii inaweza kwenda kuwafaidisha au kuwanufaisha wenzetu wale ambao wako katika vyuo vya kati. Ahsante sana.
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona ili niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa katika majibu yaliyotolewa ya swali la msingi imeonekana changamoto kubwa ni ufinyu wa bajeti kwa mwaka hadi mwaka, pamoja na ongezeko la bajeti tuliyoelezwa, lakini ni ukweli kwamba, wanafunzi wenye sifa wanakuwa wengi na wale wanaokosa nafasi katika mwaka husika wengine wamekuwa wana kiu ya kuendelea na wananchi wamekuwa wakiwasaidia au jamii wanayoishi, sasa wakienda mwaka wa pili na watatu wanaendelea kukosa. Je, Serikali haioni inayo kila sababu sasa katika miaka inayofuatia wale wanafunzi waliosaidiwa katika njia mbalimbali wawaingize katika mwaka wa pili kabla hawajaendelea kuwachukua wengine?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Kibamba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, utaratibu huo upo. Sio kwamba, ukikosa mkopo katika mwaka wa kwanza basi unakuwa hu-qualify kwenye mwaka wa pili, provided ulikuwa umeomba katika ule mwaka wa kwanza. Unachofanya katika ule mwaka wa pili, unakuwa wewe sio mwombaji mpya, unakuwa uko katika dirisha la rufaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, utaratibu huo upo Mheshimiwa Mbunge na tumekuwa tukiufanya na wanafunzi hao wamekuwa wakiwa-absorbed wakati wako mwaka wa pili ikiwa mwaka wa kwanza amekosa au mwaka wa tatu, hali ya mwaka wa kwanza na wa pili akiwa amekosa. Kwa hiyo, nikutoe wasiwasi na jambo hili tutaendelea nalo na ndivyo lilivyo.
MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nasema usajili wa shule zetu, shule za msingi, sekondari na hadi vyuo vya kati hivi kama VETA, kumekuwa na masharti magumu sana katika Wizara ya Elimu. Kinachonishangaza hata shule za Serikali na zenyewe zinawekewa masharti magumu kupita kiasi, inatufanya sisi Wabunge ambao tuko vijijini huku wananchi wetu wanataka elimu, lakini tunapata zuwio kutoka katika Wizara ya Elimu.

Je, nini mpango wa Wizara ya Elimu kurahisisha usajili ili watu wengi waweze kusajili vyuo, kusajili shule zetu za msingi na sekondari? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Tabasam, Mbunge wa Sengerema, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Tabasam anazungumzia suala la usajili. Niwatoe wasiwasi Waheshimiwa Wabunge, suala la usajili wa shule au taasisi hizi, linaanzia kule ambako shule ipo. Tuna watumishi wetu, wataalam wetu ambao wako kwenye maeneo hayo katika wilaya ambao wanakwenda kufanya ukaguzi kwenye maeneo hayo. Baada ya ukaguzi huo mara nyingi sana huwa wanaandika taarifa, ili kuweza kuangalia ile miundombinu wezeshi kwa ajili ya kuanza kutoa elimu kama imefikiwa, basi tuweze kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe wasiwasi vile vile Mheshimiwa tabasam, hivi sasa Wizara iko mbioni kuhakikisha inakamilisha mfumo wa kufanya usajili kwa kupitia mfumo badala ya huu wa sasa wa kutumia makaratasi. Katika mfumo huo tunadhani vitu vingi sana vitakuwa ni rahisi na vyepesi na vitaondoa sana manung’uniko na mizunguko ile ambayo ilikuwa haina tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, katika kipindi hiki kifupi, tuendelee tu kuchukua hili wazo lake, lakini nimtoe wasiwasi, nakumbuka jana tulionana na nikamwambia leo tuonane tuweze kuangalia hayo maeneo yake ambayo anaona yana changamoto, lakini utaratibu kimsingi uko hivyo ni vitu tu vya kufuata utaratibu na fomu zile za kujaza. Tunaangalia zile requirements au yale mahitaji muhimu kwa ajili ya kuanza kutoa elimu kwa sababu, hatuwezi tu kusajili shule kwa sababu iko chini ya mti, ni lazima taratibu na miundombinu wezeshi iwepo. Hata hivyo, tunabeba wazo lake, tutakwenda kufanya maboresho kwenye eneo hili, lakini kwa vile mfumo unakwenda kuanza kufanya kazi, tunaamini maeneo mengi yatakwenda kuboreshwa. Ahsante sana.
MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza. Nitakuwa na maswali mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoelekea, elimu ya Vyuo na Vyuo Vikuu inakuwa ni hitaji la msingi kwa wananchi na tunafahamu kabisa Mikoa ya pembezoni imekuwa inapata changamoto hiyo ya kupata huduma ya Vyuo na Vyuo Vikuu. Tunachofahamu Watanzania wengi ni masikini, hawawezi kwenda maeneo hayo wote na kupata hiyo, lakini tuna watumishi wetu wengi ambao wanahitaji kuendeleza ujuzi wao:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni kwamba, ni kwa namna gani Serikali isione umuhimu wa kuwa na mgawanyo sawa (equal distribution) wa vyuo kwa maeneo yote? Kwa Mikoa yetu kumekuwa na changamoto ya kwanza vyuo vyote vinaenda katika Makao Makuu ya Kanda, lakini kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi, Serikali inao uwezo wa kugawanya kwamba chuo hiki kijengwe sehemu fulani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ambacho nakiona, ni lini Serikali itaweza kuendeleza Chuo cha Miyunga (DIT) kiweze kutoa Shahada katika eneo lile? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Neema Mwandabila kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu katika jibu la msingi ni kwamba Vyuo vyetu Vikuu vinaanzishwa au kupelekwa kwenye maeneo kulingana na uhitaji. Nimkahikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu kwamba ipo miongozo ambayo imewekwa na Serikali na inatekelezwa na wenzetu wa TCU kwa niaba ya Wizara ya Elimu pindi wahitaji au taasisi zinapohitaji kufungua vyuo kwenye maeneo mbalimbali kuonesha maeneo yapi yenye uhitaji wa namna hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hili, kabla ya maeneo haya havijafunguliwa vyuo hivi, mara nyingi sana tunafanya assessment ambayo inaitwa need assessment ya kuhakikisha kwamba kweli tukipeleka chuo kwenye maeneo hayo, uhitaji huo utapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la pili, amezungumzia tawi letu la Miyunga kutoa Shahada. Chuo hiki cha Miyunga au Campus hii ya Miyunga ya DIT ilianzishwa mwaka 2017 ikiwa na malengo mahsusi. Malengo yake makuu ilikuwa ni kuhakikisha kwamba tunapata mafundi stadi na mafundi sanifu katika eneo la Uhandisi pamoja na eneo la uchimbaji wa madini. Masomo yanayotolewa hapa ni yale ya ufundi pamoja na ufundi stadi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge anazungumzia kutoa Shahada, lakini tunafahamu kwamba Taifa letu bado lina uhitaji mkubwa sana wa kada hizi za kati za ufundi pamoja ufundi sanifu. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba dhamira ya Serikali ni kuondoa changamoto ya mafundi sanifu pamoja na mafundi stadi wa kawaida. Kwa hiyo, kwa sasa kwa mwelekeo wetu na dhamira yetu ya Chuo kile ni kuhakikisha kwamba inakwenda kutoa kada hizo na kada ya Shahada bado tutategemea vyuo vingine vilivyopo katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ubarikiwe sana kwa kuniona. Swali langu linahusu Vyuo vya ufundi stadi vilivyopo kwenye Kata zetu kwenye Jimbo la Vunjo Kata ya Mwika, Kata ya Marangu, Kata ya Mamba na Kata ya Makuyuni Pamoja na Kiruavunjo ambavyo vimekufa. Naomba niulize, Serikali ina mpango gani wa kufufua vyuo hivi na kuvipa stadi mpya ambazo zitawawezesha wananchi wa Jimbo lile? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mkakati gani kutuonesha kanzidata ya Vyuo vya Ufundi Stadi ambavyo vipo nchini ili tuweze kuwahamasisha wananchi wetu wakasome huko? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sera ya Serikali ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na vyuo vya ufundi stadi katika kila Wilaya nchini. Vile vile Serikali inajikita kuhakikisha kwamba tunakuwa na vyuo vya ufundi stadi vya Mikoa na Kanda mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu, sasa hivi tumeanzisha vituo, zile center of excellence. Kwa mfano, kwa pale DIT Dar es Salaam tutakuwa na center of excellence katika masuala ya TEHAMA, Arusha eneo la Arusha Technical tuna center of excellence katika masuala ya nishati jadidifu, Mwanza tunaanza center of excellence katika masuala ya ngozi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu kwamba Wilaya zote zitakwenda kupata vyuo hivi kwa sababu tumeona umuhimu na uhitaji wa vyuo hivi nchini. Vilevile tunajikita katika maeneo ya Mikoa sambamba na hivi vyuo ulivyovitaja, kwamba tayari sasa tupo katika tathmini ya kuhakikisha vyuo vyote vile ambavyo vilikuwa vimekufa zamani, tunaenda kuvifufua sambamba na kuanzisha vyuo vipya katika Wilaya zote nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi hii. Kwa kuwa vijana wanaoenda chou kikuu ni wachache, hasa wale wanaomaliza kidato cha nne, ukilinganisha na wale wanaobaki. Je, ni nini mpango wa Serikali sasa wa kujenga chuo cha VETA cha ufundi katika Wilaya ya Manyoni? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Chaya, Mbunge wa Manyoni, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza katika majibu ya swali la msingi na maswali mawili ya nyongeza, pamoja na yale maswali ya Dkt. Kimei; dhamira na nia ya Serikali na Sera yetu inazungumza kwamba, kila wilaya angalau tuwe na chuo kimoja. Tumeanza tayari mkakati huu na tumeanza kutekeleza katika wilaya 29 nchini. Namwomba Mheshimiwa Dkt. Chaya awe na Subira katika kipindi hiki ambacho Serikali inaendelea kutafuta fedha, tutaifikia Manyoni, tumeanza na pale Ikungi na tukitoka Ikungi tutakwenda Manyoni kwa Mheshimiwa Dkt. Chaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Chanya aondoe shaka, Serikali hii ya Awamu ya Sita iko hapa kwa ajili ya kutekeleza mahitaji yao. Tukitoka hapo tutaenda kwa Mheshimiwa Katambi kule Shinyanga kuhakikisha na Shinyanga nayo inapata chuo hiki. Ahsante. (Makofi)
MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Namshukuru Mheshimiwa Waziri na naipongeza sana Serikali kwa kupokea mashauri mengi ya Waheshimiwa na kuyafanyia kazi. Hata hivyo, nina maswali mafupi mawili ya nyongeza. Swali langu la kwanza, ni lini Serikali sasa itaweza kukamilisha mapitio hayo na kazi hii kuwa nzuri zaidi kwa manufaa ya vijana wetu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa vile Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) pamoja na Elimu ya Juu ni masuala ya Muungano: Je, Serikali haioni umuhimu wa kushirikiana na Wizara ya Elimu Zanzibar ili manufaa ambayo watayapata vijana wetu wa Tanzania Bara na Zanzibar waweze kupata? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba sasa kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Giga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, suala la uratibu au upitiaji upya wa mitaala yetu ni agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akihutubia Bunge tarehe 22 Aprili, 2021. Nasi kama Wizara, baada ya maagizo yale, tulianza kuyafanyia kazi kwa haraka. Nimhakikishie Mbunge na Bunge lako Tukufu kwamba kazi ile inaendelea vizuri na tumeanza kukusanya hayo maoni; tulianzia pale Dar es Salaam, baadaye tukaenda Zanzibar na baadaye tulifanyia hapa Dodoma na kazi hiyo bado inaendelea. Kazi hii inatarajiwa kukamilika baada ya miaka mitatu na miezi tisa. Tunatarajia mtaala huu mpya utaanza kutumika ifikapo Januari, 2025. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika eneo la pili ambalo amezungumzia namna gani Wizara hizi mbili katika maeneo haya, namna gani yanaweza kufaidika? Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, eneo ambalo tupo tofauti na wenzetu wa Tanzania Visiwani ni katika eneo la elimu ya msingi; lakini upande wa sekondari tunatumia mtaala wa aina moja na upande wa Vyuo Vikuu tunatumia mtaala wa aina moja.

Mheshimiwa Spika, nimwondoe wasiwasi, wakati tunafanya mapitio ya mitaala yetu hii, tunashirikiana kwa karibu sana na Taasisi ya Elimu ya Zanzibar, nayo vilevile inafanya mapitio ya mitaala hiyo ili basi ile Tanzania tunayoihitaji iweze kufikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushuruku sana.
MHE. JUDITH S. KAPINGA: Mheshimiwa Spika, ahsante na naishukuru Serikali kwa majibu mazuri na nina maswali mawili madogo ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, moja, je, ni bunifu ngapi zimeweza kubiasharishwa kutokana na kupata support moja kwa moja na Serikali kupitia COSTECH?

Mheshimiwa Spika, lakini mbili, mwaka jana Serikali mlituahidi ikifika Disemba, 2021 tutaletewa Sera kuhusiana na sayansi, teknolojia na ubunifu. Sasa ningependa kupata commitment ya Serikali kwa sababu mwaka jana halikufanyika; sasa je, Serikali imejipanga vipi kuhakikisha katika mwaka huu Sera ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu mpya inaletwa kwa sababu tuliyonayo ni ya mwaka 1996 na inahusisha sayansi na teknolojia peke yake, haina ubunifu na hivyo haiwezi kuwasaidia vijana katika kujipambanua katika masuala ya ajira ya sayansi, teknolojia na ubunifu? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante na naomba sasa kujibu kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Judith Kapinga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, amezuungumzia suala la bunifu ngapi; naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako tukufu kuwa kati ya bunifu 200 zilizoibuliwa kwenye mashindano yetu ya MAKISATU, jumla ya bunifu 26 zinaendelea kuendelezwa na Serikali, ili kufikia dhamira ya kubiasharishwa ili kuleta tija katika jamii. Kwa hiyo, ni bunifu hizo 26. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini eneo la pili amezungumzia suala la sera, naomba tukiri kwamba kulikuwa na ucheleweshaji kidogo wa sera hii yam waka 1996, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge hivi sasa Wizara yangu inaendelea na mapitio ya sera hii na ndani ya mwaka wa fedha 2022/2023 tutaileta sera hiyo hapa Bungeni kwa ajili ya kupitishwa. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante na nashukuru kwa majibu ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa nafasi za kufanya mazoezi kwa vitendo kwa wanafunzi bado imekuwa shida sana, inakuwa kama hisani, upendeleo au kujuana kwa mara kadhaa.

Je, ni lini Serikali itaweka muongozo na kanuni ya kuelekeza taasisi za umma na za binafsi na waajiri kuweka utaratibu mzuri wa kuwapokea wanafunzi hawa bila kuhangaika sana? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa vile majibu ya Serikali yameashiria kama hakuna tatizo kubwa kwenye zoezi hili; je, ni kwa nini Serikali isifanye utafiti wa kina wa kubaini changamoto na matatizo yanayowakumba wanafunzi hawa na kuweka utaratibu rahisi wa kupata nafasi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba sasa kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asha Abdullah Juma yenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kufanya ufuatiliaji wa karibu kwenye programu hizi za mafunzo kwa vitendo na katika programu hizo tunajua kwamba tunapambana au tunakabiliana na changamoto mbalimbali.

Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa changamoto hizi tutaendelea kuzifanyia kazi na kuzitatua, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa vile ametoa ushauri, kwa nini tusifanye utafiti, basi naomba sasa tulichukue wazo hili twende tukafanye utafiti ili kwa pamoja kuweza kukabiliana na changamoto hizi. Nakushukuru. (Makofi)
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante, napenda kushukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, majibu yenye matumaini. Lakini nina swali moja tu la nyongeza.

Je, ni lini Serikali sasa itajenga chuo cha VETA katika Wilaya ya Meatu na Wilaya ya Busega? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante, naomba sasa kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Minza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi, kwamba ujenzi wa vyuo hivi unalingana sawa au unaendana sawa na upatikanaji wa bajeti na upatikanaji wa fedha. Lakini naomba nimpe tu taarifa Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako tukufu, hatuishii tu kwenye ujenzi wa vyuo hivi tunakwenda mbali zaidi kwa sababu tukishajenga ni lazima tuweze kuangania namna gani ya upatikanaji wa vifaa lakini vile vile upatikanaji wa walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa Serikali imejikita katika umaliziaji wa vyuo hivi 25 na baadae sasa tutakwenda kwenye mkakati wa kuweka bajeti kwa ajili ya kufikia Wilaya hii ya Meatu, Busega na Wilaya nyingine nchini zilizobaki kwa sababu Wilaya bado ziko nyingi, nakushukuru sana.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante sana, vyuo hivi vya VETA ni muhimu sana kwa sababu husaidia katika kukuza ujuzi lakini pia vinaubua ubunifu, na kwa kufanya hivi husaidia vijana aidha kujiajiri au kupata ajira kwa haraka zaidi, asilimia kubwa ya Wilaya za Mkoa wa Mara hazina vyuo vya VETA. Ningependa kujua ni lini Serikali itajenga vyuo vya VETA walau kwa Wilaya ya Tarime, Rorya na Bunda? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli katika Mkoa wa Mara anaozungumza Mheshimiwa Mbunge kwenye maeneo hayo katika Wilaya hizo alizozitaja bado hatujaweza kuzifikia, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika awamu ijayo maeneo ambayo yatapewa kipaumbele ni yale ambayo hatujayafikia hivi sasa kwa karibu.

Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi katika mgawo unaokuja tutahakikisha kwamba maeneo haya aliyoyataja yanapewa kipaumbele na kuanza ujenzi mara moja. (Makofi)
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa wananchi na Serikali ya Kijiji ya Mwambiti iliyopo Jimbo la Meatu katika Halmashauri ya Meatu imeridhia kutoa eneo lake la ekari mia moja bila fidia kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha VETA; Je, Serikali ipo tayari kupokea hati hiyo ya kieneo ili kukabiliana na vijana wanaokosa fusa zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Leah Komanya kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa hatua hiyo nzuri waliyoichukua ya kutafuta eneo na tayari wameshaandaa mpaka Hati na Wizara tuko tayari kupokea hati hiyo. Kwa sababu wameshapiga hatua moja mbele kwa kupata eneo na tayari wameshatafuta Hati tunaamini katika mchakato unaokuja pindi Serikali itakapopata fedha ina maana atakuwepo kwenye mgawo wa awamu hiyo.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mafupi. Nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Kibondo ni kati ya Wilaya kongwe nchini, Wilaya hiyo haina Chuo cha VETA. Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA katika Wilaya ya Kibondo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Genzabuke, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Wilaya ya Kibondo bado hatujaweza kuifikia kwenye Vyuo vyetu vya VETA, ingawa tuna Chuo kikubwa kilichojengwa Kasulu ambapo ni karibu kabisa na wenzetu wa Kibondo. Kwa sasa tunawashauri wananchi wetu wa Kibondo waweze kupata huduma hii katika chuo chetu kikubwa ambacho tumejenga katika Wilaya ya Kasulu wakati Serikali inaendelea na mchakato wake wa kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi katika eneo hili la Kibondo. Nakushukuru sana.
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, wanafunzi ambao wanamaliza kKidato cha nne Wilaya ya Malinyi ambao hawaendelei na masomo ya Kidato cha Tano wako zaidi ya 600 kila mwaka; na wengi wao kimbilio lao lilikuwa ni kilimo; na sasa kutokana na mgogoro kati ya Wizara ya Maliasili (TAWA na wananchi wa Malinyi) kuna uwezekano mkubwa tukapoteza maeneo ya kulima. Wanafunzi hao wanahitaji ujuzi wa ziada kwa ajili ya kujikwamua nje ya kilimo:-

Je, Serikali haioni haja ya kuiingiza Malinyi katika bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Antipas kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, anayoyazungumza Mheshimiwa Mbunge ni kweli, uhitaji wa vyuo hivi ni mkubwa sana sio tu kwa Malinyi. Kama nilivyozungumza kwenye jibu langu la msingi kwamba tunamalizi ujenzi wa vyuo hivi 25 katika wilaya 25 pamoja na mikoa minne nimuondowe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge katika bajeti ijayo iwapo Serikali tutapata fedha kipaumbele cha kwanza itakuwa ni eneo hili la Malinyi na maeneo mengine ambayo yenye uhitaji mkubwa ukilinganisha na maeneo mengine tayari yanavyuo karibu.
MHE. EDWIN E. SWALLE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kunipa nafasi, lakini pia niipongeze sana Serikali ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuongeza fedha nyingi sana kwa wasomi wa elimu ya juu. Kwa taarifa tu ni kwamba kati ya uamuzi mkubwa na wa kihistoria uliofanywa mwaka jana na Serikali, ilikuwa ni kusitisha tozo ya asilimia sita na riba ya asilimia 10 kwenye mikopo ya elimu ya juu jambo hili lilikuwa ni ni jambo la kheri sana.

Mheshimiwa Spika, ninayo maswali mawili ya nyongeza swali la kwanza; kwa kuwa Serikali ilisitisha fine ya asilimia sita na riba ya asilimia 10, lakini imesitisha kwa kutoa tamko ndani ya Bunge lako na sheria haijafutwa. (Makofi)

Je, Serikali haioni haja sasa ya kuleta hii sheria Bungeni, ili iweze kufutwa kabisa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili; kwa kuwa baada ya tamko hili la Serikali la kusitisha fine na riba ya asilimia sita na asilimia 10, watu wengi wamejitokeza kwenda kulipa fedha kwenye Bodi ya Mikopo. Lakini wamekuwa wakisumbuliwa kwamba walipe na madeni ya nyuma kabla ya tamko hilo la Serikali.

Ninaomba kauli ya Serikali kusitishwa kwa ulipaji wa riba ya asilimia sita na fine ya asilimia 10, inahusu madeni ya kuanzia lini kwa wananchi wa Tanzania? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Swalle, Mbunge wa Lupembe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mbunge kwa kuwapigania Watanzania wote, lakini vilevile tupokee shukurani zake kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuona changamoto ya tozo hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye eneo la kwanza la sheria nimtoe hofu Mbunge na Bunge lako Tukufu pamoja na kwamba Sheria ile bado haijaletwa hapa Bungeni, lakini bado utendaji wake haulazimishi uwepo wa tozo zile. Kwa hiyo, hata kama haitakuja bado katika utendaji wetu kwa sababu kanuni ndio ambayo inampelekea Mheshimiwa Waziri aweze kuweka kiwango gani cha tozo hizo za kulipwa. Kwa hiyo, nimtoe wasiwasi tunakwenda kufanya tathmini ya kina kwenye eneo hilo la sheria, kama tukiona kuna haja ya kuzileta hapa Bungeni tutaweza kuzileta kwa ajili ya marekebisho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini eneo la pili ni eneo la madeni; ninaomba nimhakikishie Mbunge baada ya kauli ile ya kuondoa tozo zile pale pale makato yale yote kwa yule ambaye atakayekuwa hajalipa, hakupaswa kulipa tena na wale ambao wanaokuja baadae nao vilevile hawakupaswa kulipa. Kwa hiyo, kwa namna yoyote ile kama kuna mtu anaona kwamba anadaiwa hayo madeni ya nyuma basi tupate taarifa zake ili tuweze kuzifanyia kazi, lakini kwa mujibu wa sheria pamoja na tamko lile siku ile ile tulipozungumza hapa Bungeni makato yale na madeni yale yali-seize automatically. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, hivi tunavyozungumza chuo hiki hakina mkufunzi hata mmoja wala hakina Mkuu wa Chuo. Wakufunzi wanaotegemewa ni kutoka Chuo cha VETA Tanga ambacho na chenyewe kimeelemewa, kinategemewa chuo hichohicho cha Tanga kitoe wakufunzi kwenda Korogwe. Je, Serikali ina mpango gani wa haraka kuhakikisha kinapata wakufunzi ili hayo malengo ya kuanza mwezi wa Kumi yaweze kutimia? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Hivi tunavyozungumza vifaa vya ufundi havijapatikana kwenye vyuo hivi vya Mkinga wala Korogwe. Serikali ina mkakati gani wa haraka kuhakikisha vifaa hivi vinapatikana ili mafunzo yaweze kufanyika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba sasa kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kitandula Mbunge wa Mkinga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nikiri ni kweli tuna upungufu wa walimu kwenye vyuo vyetu hivi vya VETA hivi sasa tuna Wilaya 77 zenye Vyuo vya VETA vya Wilaya pamoja na mikoa. Lakini nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 Wizara imepata kibali cha kuajiri walimu zaidi ya 514. Kwa hiyo, tayari mchakato huu wa kuajiri walimu uko kwenye hatua za mwisho na tutahakikisha sasa miongoni mwa walimu hawa 514 tunaokwenda kuwaajiri basi waweze kwenda kwenye Chuo cha Mkinga lakini pamoja na vile vyuo 25 vya Wilaya pamoja na vyuo vile vinne vya mikoa ambavyo sasa nakamilisha ujenzi wake.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la pili amezungumzia suala la vifaa vya kufundishia; ni kweli mchakato wa vifaa unaendelea kwa sababu upo kwenye bajeti 2022/2023 ambao tumeanza kuutekeleza hivi sasa na tuko katika quarter ya kwanza. Kwa hiyo, pindi fedha zitakapokuwa zimekaa tayari tunakwenda kununua hivyo vifaa na kuvipeleka kwenye vyuo hivi ambavyo tayari vimekamilika, lakini upande wa samani zote za vyuo vyote 25 viko tayari kwa ajili ya kupelekwa katika maeneo haya nakushukuru sana.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, kwa kuwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameonesha nia na dhamira ya dhati ya kumlinda mtoto wa kike, kwa kuweka elimu bila malipo kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita. Kwa nini sasa Wizara isitoe waraka wa kulinda watoto hawa dhidi ya mimba za utotoni na ndoa za utotoni ili kuwahimiza kuwa shuleni wakati tunasubiri mabadiliko makubwa ya sera?

Mheshimiwa Spika, kwa nini Serikali isitoe kauli dhidi ya watoto walioko mtaani wanaokosa kwenda shuleni ambao wamejiingiza kwenye makundi ya vilevi na uhalifu kama panya road? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Husna Sekiboko, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwenye majibu yangu ya msingi, kwamba sasa Serikali tunafanya mapitio ya Sera pamoja na Sheria yetu ya Elimu. Nimeeleza hapa kwamba rasimu hiyo itakuwa tayari mwezi wa Desemba, 2022. Hata hivyo, uandaaji wa miongozo anayozungumza Mheshimiwa Mbunge pamoja na nyaraka mbalimbali zinategemea vilevile mwongozo kutoka kwenye sera hii. Kwa hiyo namwomba Mheshimiwa Mbunge awe na Subira, kwa vile Desemba sio mbali tutakamilisha rasimu hii na huenda hayo yote anayoyazungumza yakawemo kwenye sera pamoja na sheria yetu.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la pili mwaka jana, 2021, Serikali ilishatoa Waraka Na.2 wa Elimu wa mwaka 2021 ambao unahusu namna gani wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo na hii ya ujauzito wanaweza kurudi shuleni. Kwa hiyo tutoe wito tu na rai kwa wadau pamoja na mamlaka mbalimbali zinazosimamia elimu kuhakikisha kwamba tunakwenda kutekeleza maagizo haya ya Serikali. Nakushukuru sana.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Dunia ya sasa ni ya sayansi na teknolojia, hivyo kama Taifa lazima tuwekeze kuhakikisha kwamba tunakuwa na Walimu wa kutosha kwenye masomo haya ya sayansi na hesabu; na kwa kuwa kuna uhaba mkubwa sana wa Walimu waliopo ni takribani asilimia 33 tu. Je, ni nini mkakati madhubuti na wa haraka wa Serikali wa kuhakikisha kwamba inaajiri Walimu wa kutosha ili kukabiliana na changamoto hii?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; kwa kuwa wahitimu hawa ambao hawajaajiriwa tangu mwaka 2015 ni takribani asilimia 60 na wengi wao wamekuwa wakijitolea kufundisha bila ajira rasmi. Ni kwa nini Serikali isiwape kipaumbele Walimu hawa wanaojitolea kwa kuwaajiri kwenye maeneo ambayo wanajitolea kwa sasa?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Esther Nicholaus Matiko, Mbunge wa Viti Maalum, kwa pamoja kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Matiko kwa ufatiliaji wa karibu wa Walimu wetu wa masomo ya sayansi pamoja na hisabati. Hata hivyo, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu yangu ya msingi kwamba Serikali imeendelea kutoa fursa za ajira kwa Walimu hawa, tunajua changamoto ipo na uhitaji upo ni mkubwa. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba Ofisi ya Rais, TAMISEMI yenye dhamana ya kuomba vibali tayari katika mwaka huu wa fedha imeshaomba kibali cha kuajiri Walimu zaidi ya 42,697 ambapo kipaumbele kikubwa sana tutawapa Walimu wa sayansi pamoja na hisabati na wale ambao wanajitolea katika maeneo mbalimbali nchini. Nakushukuru sana.
MHE. AMOUR KHAMIS MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa hii ya kuuliza maswali ya nyongeza, lakini kwanza napenda nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri sana mimi namuombea dua Mwenyezi Mungu amuongezee katika elimu yake hii. Ninayo maswali mawili.

Swali la Kwanza; Serikali inatumia sheria gani kuweka vigezo vya kuwatambua hawa wavumbuzi?

Swali la Pili; amesema kwamba kati ya wavumbuzi waliotambuliwa ni 2,735. Je, katika hawa Zanzibar wapo wangapi? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Amour, Mbunge wa Tumbe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza kwenye majibu yangu ya msingi kwamba Serikali imekuwa ikifanya mchakato wa kuibua hawa wabunifu, wabunifu hawa wanaibuliwa kwa mujibu wa Sheria Na. 7 ya mwaka 1986 ambayo ilianzishwa na Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili kati ya wabunifu hawa 2,735 tumesema wabunifu 376 wanaendelezwa na Serikali, kati ya wabunifu hawa ni wabunifu 11 wanatoka upande wa Zanzibar. Ninakushukuru. (Makofi)
MHE. MICHAEL M. KEMBAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi Wizara imekuwa ikitoa tamko la kuzuia masomo ya ziada katika Shule za Msingi na ilhali wakijua kwamba muda wa ukamilishaji wa mtaala unakuwa hautoshi. Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba inatenga muda ambao watoto hao watasoma wakamilishe mtaala wao kwa wakati?

Swali la pili, Mheshimiwa Waziri amesema kwamba Walimu wanapaswa kutafuta muda wa kukamilisha mtaala huu kwa mpango kazi ambao wanao. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwapa motisha Walimu hawa ambao wanafanyakazi hii ngumu ya kuhakikisha kwamba elimu inatolewa kwa wakati? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kembaki Mbunge wa Tarime Mjini kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwishajibu kwenye majibu yangu ya msingi kwamba katika mwaka tunazo siku 365, kati ya siku hizo 365 tunatumia siku 194 kwa ajili ya kukamilisha mitaala katika mwaka husika wa masomo. Najua maono ya Mheshimiwa Mbunge kwenye eneo hili, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa vile hivi sasa tunapitia Sheria yetu ya Elimu tunapitia mitaala pia tunapitia sera ya elimu, bado hatujaona changamoto kwa hizi siku 194 kwenye utekelezaji wa mitaala hii kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, kwa vile bado tunaendelea kubeba au kuchukua maoni tunaomba tubebe vilevile maelezo yake haya tuweze kuyaingiza kwenye rasimu yetu ya mitaala inayokuja ili tuweze kuangalia kama hizi siku 194 zitatosheleza au hazitatosheleza au kama kutakuwa na changamoto yoyote tuweze kufanya marekebisho. Hilo eneo la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili la motisha, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge pamoja na Bunge lako Tukufu kwamba Serikali imekuwa ikitoa motisha au kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria. Kama tunavyofahamu katika kipindi kilichopita Mheshimiwa Rais aliongeza mshahara siyo tu kwa watumishi kama walimu, lakini kwa watumishi wote. Kwa hiyo, Serikali itaendelea kufanya hivyo kwa kadri bajeti itakavyokuwa inaruhusu ili watumishi wote waweze kupata stahiki zao kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. (Makofi)
MHE. SUBIRA H. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwanza nimwambie tu Mheshimiwa Waziri kwamba hivyo vishikwambi ambavyo vimetumika kwenye sensa havitaweza kutosha kwa walimu wa nchi nzima kwa sababu waliokuwa wanahesabu sensa na idadi ya walimu ni tofauti kabisa. Sasa: Je, mna mpango gani wa kuhakikisha mnaongeza vifaa na kuweka projector kwenye kila shule ili kuondokana na suala la magonjwa na shingo na mgongo kwa walimu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Mmetoa mafunzo kwa walimu ambao watakwenda kufundisha wanafunzi: Je, mmewaandaa namna gani hawa wanafunzi wanaokwenda kufundishwa kwa sababu somo hili litakuwa ni jipya kwao hasa kwenye maeneo ya vijijini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Subira Mwaifunga Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nimeeleza katika majibu yangu ya msingi kwamba vishikwambi vilivyotumika katika zoezi la sensa ni zaidi ya 205,000 lakini sisi kama Wizara tumeongeza vishikwambi vingine zaidi ya 100,000. Kwa hiyo, nimwondoe hofu kwanza. Idadi ya vishikwambi ambavyo wizara imeweza kuratibu na kununua vitatosheleza kwa walimu wote.

Mheshimiwa Spika, niongezee hapo katika swali lake lingine ambalo anazungumzia habari ya kuwaandaa wanafunzi na vilevile kuandaa walimu. Serikali inaendelea na mchakato wa kuhakikisha kwamba tunakuwa na vifaa toshelezi katika maeneo yote na hata katika bajeti yetu ya mwaka huu 2022/2023 tumeweka fungu kwa ajili ya ununuzi wa vifaa, lakini tutaanza kwanza na kuimarisha vituo vile vya kufundishia walimu, zile TRC zetu.

Mheshimiwa Spika, vituo vile vyote 162 tayari tumevikarabati, tumenunua vifaa pamoja na projector katika vituo hivyo kwa kuhakikisha kwanza walimu tunaweza kwenda kuwafundisha wakiwa kule kule makazini pamoja na uwepo huu wa vishikwambi, itakuwa ni rahisi kuwafundisha.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hiyo, Serikali ipo katika mpango wa kuandaa maktaba mtandao ambapo tunaamini maktaba hii itakapokamilika vitabu vyote vya kiada na ziada vitakuwepo kwenye maktaba hiyo na itakuwa ni rahisi kwa wanafunzi pamoja na walimu kupata mafunzo na mada mbalimbali kutoka kwenye maabara hizo. Nakushukuru sana.
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, Serikali inafanya jitihada kubwa kama ambavyo umeeleza za kuhakikisha inanunua vifaa vya TEHAMA nchini pamoja na kuwafundisha Walimu: Je, ni vipi jitihada hizi zinaunganishwa kuhakikisha kwamba tunaitumia TEHAMA kupunguza au kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi nchini?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye swali lake la msingi, Serikali bado inaendelea na jitihada ya kuzalisha walimu katika masomo ya sayansi nchini. Sambamba na hilo, kama nilivyozungumza ni kwamba tunaendelea na ununuzi wa vifaa vya TEHAMA na mahali tutakapoanzia ni kwenye vituo vyetu vya TRC na lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba vifaa vile tunaweza kwenda kuwafundisha walimu wetu.

Mheshimiwa Spika, lengo kuu la kuanzisha vituo hivi ni kuhakikisha kwamba tuna-absorb walimu wengi zaidi kuweza kuwafundisha katika maeneo hayo ili watakaporudi kule shuleni waweze kufundisha, kwa sababu siyo lazima walimu wa TEHAMA watokane na wale walimu wa sayansi tu.

Tukishawafundisha walimu wetu, hata wale walimu wa masomo ya kawaida bado wanaweza kutumika katika kufundisha somo hili la TEHAMA.
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa swali la nyongeza. Tunaipongeza Wizara kwa jitihada yake inayofanya kwa ajili ya TEHAMA. Kwa wale wanafunzi wanaoona watapewa vishikwambi: Je, kwa wale wanafunzi wenye uono hafifu Serikali itawasaidiaje? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Maryam Mwinyi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na jitihada zake za kuhakikisha kwamba watoto wote wakiwemo na wale wenye uono hafifu na wenye ulemavu wa aina mbalimbali wanaweza kupata vifaa vya kujifunzia na kufundishia. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ina takwimu sahihi za wanafunzi hawa na tutahakikisha nao vilevile katika eneo hili tunakwenda kuwapatia vifaa vya kuwasaidia na wao kuweza kujifunza somo hili muhimu la TEHAMA. Ahsante.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Majibu ya Waziri yameonesha Serikali ina mpango wa kuanzisha Maktaba Mtandao lakini kiuhalisia maeneo mengi nchini hakuna mtandao na umeme. Tunataka kujua ni nini mkakati wa Serikali kushirikiana na Wizara ya Nishati pamoja na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia kuhakikisha kwamba program hii inafika kwa wakati katika shule zetu zote? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Esther Matiko, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli anachozungumza Mheshimiwa Mbunge kwamba tuna changamoto ya mtandao maeneo mengi, lakini nimwondoe hofu kwamba Serikali yetu inaendelea na uimarishaji wa mtandao kwa kujenga mkongo wa Taifa. Nasi kama Wizara tayari tuna mradi mkubwa sana ambao utahakikisha tunakwenda kuziunganisha shule zetu na mkongo huu na vilevile kuziunganisha kwenye mtandao wa internet.

Mheshimiwa Spika, mradi huu utaanza na mikoa 10 katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 na tunaamini mpaka kufika mwaka 2025 basi utakuwa umefikia mikoa yote, lakini shule zote zitakuwa zimeunganishwa na mtandao wa internet kuhakikisha kwamba masomo haya ya TEHAMA yanakwenda kufanyika mpaka kule vijijini. Nakushukuru sana.
MHE. OMAR ALI OMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, naomba niulize swali moja la nyongeza.

Kati ya wanafunzi 1,492 ni wanafunzi wangapi wenye mahitaji maalum ambao walipatiwa mkopo huo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, napenda sasa kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Omar Ali Omar Mbunge wa Wetu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, miongoni mwa vigezo ambavyo vinatumiwa na Bodi ya Mikopo yetu ya Elimu ya Juu ni pamoja na ulemavu, kwa maana ya wenzetu wenye mahitaji maalum pamoja ya uyatima. Kwa hiyo nitatoa takwimu tu za jumla za wenzetu hao kwenye makundi hayo kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha mwaka 2021 wanufaika wote wa Bodi ya Mikopo walikuwa ni 149,389; kwa upande wa Zanzibar wale waliokuwa na mahitaji maalum walikuwa ni 100; na mwaka 2021/2022 yaani mwaka huu tunaoendelea nao jumla ya wanufaika wote ni 177,892 na wale wenye mahitaji maalum kwa upande wa Zanzibar peke yake walikuwa ni 181. Nakushukuru.
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, ni kwa nini sasa Serikali isione haja ya kushirikisha taasisi binafsi za fedha ili ziweze kutanua wigo wa kupata fedha zaidi kwa ajili ya kutoa mikopo na yenyewe ibaki ku-regulate tu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Nusrat Hanje, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge hivi sasa tunaendelea na mazungumzo na taasisi mbalimbali za fedha, lakini katika bajeti yetu ya mwaka 2022/2023 tayari wenzetu wa NMB wameweza kuongeza bajeti yetu ya mikopo kwa ajili ya vijana wetu wa elimu ya juu pamoja na elimu ya kati zaidi ya shilingi bilioni 200. Kwa hiyo kama Serikali tunalifanya hilo na tutaendelea kulifanya.
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza: -

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kutenga na kuanza kujenga vyuo vya ufundi ni jambo jema, lakini ipo haja ya kuhakikisha kwamba vyuo hivi vinaanza kufanya kazi. Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha kwamba vyuo vinapomalizika kujengwa na vifaa vya kufundishia vijana vinakuwa vinapatikana?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa sababu wananchi wa Kalambo wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu ujenzi wa chuo, je, ujenzi huu utaanza lini?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Sinkamba Kandege, Mbunge wa Kalambo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tulikamilisha au tunakamilisha ujenzi wa vyuo 25 katika wilaya 25 pamoja na vile vya mikoa. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imeweza kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa pamoja na samani ili vyuo hivi viweze kuanza kufanya kazi mapema iwezekanavyo. Tunatarajia kama mambo yote yatakwenda sawasawa kunako Januari vyuo vile ambavyo vitakuwa vimekamilika au tunavyokamilisha hivi sasa vitaanza kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili, kwa upande wa kule Kalambo, tayari Serikali tupo katika mchakato wa kutenga fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa chuo hicho. Kwa hiyo nimwondoe wasiwasi, ndani ya quarter hii ya pili tutahakikisha tunapata fedha hizi ili ujenzi wa Kalambo uweze kuanza mara moja. Nakushukuru sana.
MHE. GEOFFREY I. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri, lakini nina maswali mawili nyongeza. Swali la kwanza; ni lini basi Serikali itaona umuhimu katika hivyo vyuo ambavyo imepanga kujenga basi kijengwe pale Masasi kwa sababu tayari kilikuwepo na Serikali ilifanya maamuzi ya kukibadilisha chuo na kuwa shule ya sekondari ili pia ihudumie wananchi wa Masasi na wilaya za jirani?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, ni lini Serikali pia itaona haja ya kufungua matawi vyuo vya elimu ya juu Wilayani Masasi ili kuweza kusaidia watu wa Masasi, lakini pia na watumishi mbalimbali kuweza kujiendeleza kielimu? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mwambe, Mbunge wa Masasi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu katika majibu yangu ya msingi kwamba Serikali inamiliki vyuo 35 na katika vyuo hivi tuna mahitaji ya wanafunzi zaidi ya 25,000 lakini wanafunzi waliopo kwa sasa ni 22,000. Tafsiri yake hapa ni kwamba, hata hivi vyuo vilivyopo bado vina upungufu mkubwa wa kupata wanafunzi. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inaendelea kufanya tathmini ya jambo hili kulingana na mahitaji, kama nilivyozungumza kwenye majibu yangu ya msingi, iwapo kama tutaona kwamba kuna uhitaji wa kujenga chuo, basi Masasi tutaipa kipaumbele katika ujenzi huo.

Mheshimiwa Spika, naomba nimkumbushe Mheshimiwa Mbunge kwamba katika Mkoa wa Mtwara, bado tuna vyuo vitatu vya ualimu, tuna Chuo pale Mtwara Mjini, tuna vyuo viwili kimoja cha ufundi na kile cha kawaida. Vilevile katika Wilaya ya Newala tuna chuo pale Kitangale ambavyo wanafunzi hawa wote wanaweza wakatumia vyuo hivi kuweza kupata elimu yao katika maeneo hayo. Kwa hiyo, kama mahitaji yatatokea basi tutaweza kwenda kujenga katika eneo hili Masasi.

Mheshimiwa Spika, katika eneo lake la pili, kuhusiana na masuala ya matawi ya Vyuo Vikuu, naomba nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, hivi sasa Serikali inakwenda kujenga katika maeneo mbalimbali matawi ya Vyuo Vikuu. Naomba tu nitoe taarifa kwenye Bunge lako Tukufu, pale Mtwara tuna matawi ya Chuo Kikuu Huri ana Chuo Kikuu cha Stella Marius, lakini vilevile tuna tawi la Chuo cha TIAA. Vyuo hivi vyote vinaweza vikatumiwa na wenzetu wa Masasi kwa ajili ya kupata mafunzo yao pale. Vilevile Chuo Kikuu chetu cha Dar es Salaam kiko mbioni kufungua tawi katika Mkoa wa Lindi ambapo ni jirani kabisa na Wilaya ya Masasi. Nakushukuru.
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kutoa pesa za ujenzi wa VETA ya Mkoa wa Simiyu na mpaka sasa ujenzi unaendelea. Kwa kuwa sSera ya Serikali ni ujenzi wa VETA kila Wilaya; ni lini sasa Serikali itajenga VETA katika Wilaya ya Simiyu ambayo haina VETA?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Esther Midimu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni azma ya Serikali kujenga vyuo hivi katika Wilaya ambazo hazina vyuo na hivi sasa tuko katika mkakati au mchakato wa kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa VETA hizi. Mara tu pesa zitakapopatikana tutahakikisha kwamba, tunaanza ujenzi mara moja. Nakushukuru sana.
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi: -

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Rorya ni moja ya Wilaya ambazo na sisi tumeanza mchakato wa muda mrefu sana kwa ajili ya maombi ya kupata Chuo cha VETA, na Mheshimiwa Waziri unakumbuka nimekuwa nikikusumbua sana kwa muda mrefu ili angalau na sisi tuweze kupata chuo cha VETA. Nilitaka nijue sasa kwenye mpango wa bajeti ya mwaka huu katika vyuo vya VETA 63 kama na sisi Wilaya ya Rorya tumo katika vyuo hivyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Chege, Mbunge wa Rorya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika Wilaya zilizobaki ambazo hazina Vyuo vya VETA ni Wilaya 63, tafsiri yake Wilaya ya Rorya nayo imo katika ile orodha. Tafsiri yake tunataka tujenge katika Wilaya zote ambazo hazina vyuo kwa awamu. Kwa hiyo, katika awamu ya kwanza tutaanza kwa Wilaya zote ambazo hazina kwa pamoja katika mwaka huu wa fedha na mwaka unaofuata ina maana tutakuwa na jukumu la kumalizia kazi ile ambayo tutakuwa tumeianza katika mwaka huu wa fedha. Nakushukuru sana.
MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniona.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Singida imeshatenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa VETA na uhitaji ni mkubwa sana kwa wananchi wa Jimbo la Singida Kaskazini kwa ajili ya chuo hiki.

Naomba commitment ya Mheshimiwa Waziri; je, Halmashauri ya Wilaya ya Singida nayo imo katika kupata chuo hiki? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, napenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Ramadhani, Mbunge wa Singida, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Singida ninachofahamu kuna Chuo cha VETA cha Mkoa wa Singida ambacho kipo katika Wilaya ya Singida. Kwa hiyo, maadam tuna chuo cha VETA cha Mkoa ambacho kipo katika Wilaya ya Singida, hatuwezi tena kwenda kujenga chuo kingine katika Wilaya hiyo hiyo. Kwa hiyo, kile Chuo cha VETA cha Mkoa wa Singida ndicho ambacho kitatumika kama chuo cha Wilaya ya Singida. Nakushukuru sana.
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, tunaishukuru Serikali kwa kuwa na azma nzuri ya ujenzi wa Vyuo vya VETA katika Wilaya zote 63. Swali dogo tu la nyongeza, je, ni lini sasa Serikali itaanza ujenzi wa vyuo hivyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, napenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kungu, Mbunge wa Tunduru Kaskazini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoanza kueleza katika swali la mwanzo kwamba vyuo hivi tutajenga vyote kwa pamoja na tunachosubiri sasa ni upatikanaji wa fedha ambazo ndizo tumeshafanya maombi kwa Wizara ya Fedha na Mipango; na mara tu tutakapopata fedha hizi ujenzi huu utaanza kwenye vyuo vyote 63 katika Wilaya zote 63 kwa pamoja. Nakushukuru sana.
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante; katika hesabu ya Halmashauri 63, je, na Mbogwe imo kwenye hesabu hiyo Mheshimiwa Waziri? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, napenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Nicodemas Maganga, Mbunge wa Mbogwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama Mbogwe ni Wilaya, sina uhakika sana kwa sababu kuna Wilaya ambazo zina majimbo mawili. Kwa hiyo, hapa kwenye majimbo mawili ina maana tunapokwenda kujenga ni Wilayani, sasa kama Mbogwe ni Wilaya ambayo inajitegemea itakuwa imo, lakini kama Mbogwe ni jimbo miongoni mwa Wilaya ina maana tutakapokwenda kujenga ni Wilayani ambako na Mbogwe ita-share chuo hicho ambacho kitajengwa katika Wilaya hiyo ambayo Mbogwe ipo kwenye Wilaya husika.
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi, kwanza naomba niishukuru Serikali kwa kujenga Chuo cha VETA pale Uvinza.

Sasa nauliza; ni lini chuo kile kitafanya kazi ili watoto wa pale waweze kuanza kuingia chuoni? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Nashon, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tuna vyuo vyetu 25 vya Wilaya ambavyo tulianza ujenzi wake toka mwaka 2021 na ujenzi ule uko kwenye hatua za mwisho. Hivi sasa tunatengeneza samani au tunasambaza samani pamoja na vifaa vya kufundishia. Ni matarajio yetu katika mwaka ujao, 2023 vyuo hivi 25 vya Wilaya pamoja na vile vinne vya mikoa vitaanza kutoa mafunzo rasmi. Nakushukuru.
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi; elimu ya ufundi ni nyenzo muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yoyote.

Je, Serikali haioni sasa kwamba ni muhimu kubadilisha utaratibu, badala ya kujenga hivi vyuo kiwilaya ijenge kijimbo kwa sababu, kuna Wilaya nyingine ambazo zina majimbo mawili?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Pallangyo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kada hii ya ufundi ni muhimu, naomba tuchukue ushauri wa Mheshimiwa Mbunge, hivi sasa tumeanza katika ngazi ya kanda, mikoa pamoja na ngazi ya Wilaya. Tuangalie baadaye namna gani tunaweza tukafika katika ngazi ya jimbo kama Mheshimiwa Mbunge anavyoshauri.

Kwa hiyo, tunaubeba ushauri wako tunakwenda kuufanyia kazi na tufanye tathmini ya kina. Nakushukuru sana.
MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, namshukuru Waziri kwa majibu mazuri, lakini naomba kumuuliza maswali mawili.

Tunafahamu Serikali inaenda kutekeleza Mradi wa High Education for Economic Transformation (HEET); sasa namuuliza swali; je, mradi huo unatarajia kusomesha wahadhiri wangapi?

Je, Serikali inatuhakikisha kuwa Mradi huu wa HEET utapunguza uhaba wa Wahadhiri katika vyuo vikuu kwa kiasi gani? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba sasa kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Nahato kwa pamoja kama ifutavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali yetu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wetu, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, tumepata mkopo wa jumla ya dola za Kimarekani milioni 425, sawa na shilingi bilioni 972.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mradi huu, pamoja na mambo mengine utakwenda kuimarisha miundombinu kwenye vyuo vyetu vya Umma karibu 14, vilevile utashughulikia masuala ya Wahadhiri pamoja na watafiti katika nchi yetu. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu, katika mradi huu tunatarajia kufanya maendelezo ya Wahadhiri wetu katika Vyuo Vikuu wapatao 831, ambapo katika kada ile ya PhD., ambayo tunaita Uzamivu, ni wahadhiri 444 na wale wa Masters yaani Uzamili ni 387.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi, jambo hili tutakwenda kulifanya na kuhakikisha tunataondoa changamoto hii ya wahadhiri katika vyuo vyetu. Nakushukuru. (Makofi)
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nimesikia majibu ya Serikali ni mazuri na yanaleta moyo katika kupunguza changamoto ya upungufu wa Wahadhiri na hasa Wahadhiri Wabobezi katika Vyuo Vikuu vyetu. Pamekuwa na tafiti chini ya Chama cha Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu (THTU) kwamba kuna upungufu mkubwa sana; utafiti wa 2017, lakini sababu kubwa waliyotoa ni Serikali kutumia sana wataalamu wao katika kujaza nafasi mbalimbali Serikalini: -

Je, Serikali haioni sasa ni wakati mzuri wa kushauri mamlaka za uteuzi kuacha kutumia wataalam hawa, hasa Wahadhiri Wabobezi katika nafasi mbalimbali Serikalini?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mtemvu, Mbunge wa Kibamba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa vile Mbunge ametoa wazo na Mamlaka za Uteuzi zipo, namwomba Mheshimiwa Mbunge tuichukue hoja yake hii ili tuweze kuifikisha kwenye vyombo hivi vya uteuzi ili waweze kufanya evaluation au tathmini toshelezi kabisa iwapo kama wanaona inafaa kufanya hivyo, basi liweze kufanyiwa kazi. Nakushukuru sana.
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa
Mwenyekiti, ahsante sana. Kumekuwa na uhaba mkubwa sana wa Maprofesa katika Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Sokoine, Mandela, Ardhi na Chuo cha Muhimbili. Baada ya kustaafu wakiwa na miaka 65 wanaambiwa waende nyumbani na biashara imeishia hapo, lakini kuna uhaba mkubwa.

Kipi bora, je, tuongeze miaka yao ifike angalau 70 waendelee kuhudumia nchi yetu? Kwa sababu kuna ombwe kubwa sana la ngazi hizi kwenye Vyuo Vikuu. Naomba Serikali ifikirie hawa watu waendelee mpaka miaka fulani hivi ili vijana wetu wapate elimu ya uhakika. Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Profesa Ndakidemi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli anayozungumza Mbunge kwamba tumekuwa na changamoto sana ya Wahadhiri katika kada hii ya Maprofesa kutokana na wao kustaafu. Naomba nimweleze tu Mheshimiwa Mbunge kwamba kustaafu kwa upande wa Utumishi wa Umma ilikuwa ni miaka 60 kwenye maeneo mengine yote, lakini kwa upande wa wenzetu hawa Maprofesa au Wahadhiri wa Vyuo Vikuu ilipandishwa kutoka miaka 60 kwenda miaka 65. Sasa hivi Mheshimiwa Profesa Ndakidemi anasema kwamba angalau tungeongeza ifike miaka 70.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tulibebe wazo hili, ingawa vilevile nimeeleza kwenye majibu yangu ya msingi kwamba katika mradi wetu wa HEET, unakwenda kufundisha katika level ile ya Ph.D ambapo tunaamini wengi sasa wataenda kuwa Maprofesa, ambao tutahakikisha katika eneo hili tunaenda kufanya coverage kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuchukue wazo lake Mheshimiwa Prof. Ndakidemi twende tukalifanyie kazi ili tuweze kuona mtu akifikisha miaka 70 atakuwa na uwezo wa kusimama darasani akafundisha au akasimamia watu kwenye kazi zao? Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu hayo ya Waziri, naomba kufahamu kuhusu wale Maprofesa na Madaktari 203 ambao walistaafu kwa sasa wako wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, sehemu ambayo nguvu zinaisha haziwezi kufanya kazi ni sehemu ya ubongo. Kwa hiyo ina maana kwamba mtu anaweza akafanya kazi hata akiwa na miaka 70 mpaka 75 kama tunavyoona baadhi ya maprofesa humu ndani. Sasa ni lini Serikali kama Waziri alivyoahidi mwaka jana, ni lini Serikali sasa itaruhusu hawa watumishi wanaostaafu kwa miaka 65 waendelee kubaki chuoni mpaka miaka 75?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Ntara kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. Ntara kwa kufuatilia kwa karibu sana maendeleo pamoja na upatikanaji wa watumishi hasa Wahadhiri katika vyuo vyetu. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ni kweli kulingana na miongozo ya Utumishi wa Umma, wenzetu katika vyuo vikuu, Wahadhiri wale pamoja na Maprofesa huwa wanastaafu wakifikia umri wa miaka 65, tofauti na maeneo mengine ya Utumishi wa Umma.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katika kipindi cha miaka mitatu watumishi zaidi ya 203 walistaafu kwenye maeneo mbalimbali ya vyuo vyetu hapa nchini. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Ntara kwamba miongoni hawa watumishi 203 ambao wamestaafu basi watumishi karibu 103 walikuwa wamebakishwa vyuoni kwa mikataba maalum. Miongoni mwao walikuwa ni watumishi 98 ambao walikuwa ni Maprofesa na watumishi karibu watano walikuwa ni Senior Lectures.
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Msalala ni miongoni mwa Halmashauri ambazo hazina Vyuo Vikuu na tayari kupitia mapato ya ndani tumetenga fedha kiasi cha Shilingi Milioni 212 kuanza ujenzi wa Chuo cha VETA. Sasa ni Serikali itatuongezea fedha ili tuweze kumaliza chuo hicho?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Serikali katika sera yetu tunahakikisha kwamba tunakwenda kuwa na Vyuo vya VETA katika kila Wilaya nchini, kwa kuanzia tulianza na Wilaya 29 na hivi sasa vyuo hivyo vinakwenda kumalizika pamoja na Mikoa Minne ambayo haikuwa na Vyuo vya VETA. Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mwaka wa fedha ujao, mambo mengi sana kulingana na upatikanaji wa bajeti vyuo hivi tutakwenda kujenga kwenye maeneo ambayo bado ujenzi haujafanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. DKT. PAULINE D. NAHATO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Je, ni lini kutakuwa na usawa wa jinsia katika uongozi wa juu katika Vyuo vyetu Vikuu kwa sababu kwa sasa hivi katika Vyuo Vikuu hakuna usawa wa jinsia kwa uongozi, ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge Dkt. Nahato kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tuna changamoto sana kwenye usawa wa jinsia kwenye level hiyo ya Vyuo Vikuu na hii ni kutokana tu kwamba wakati tunaendelea na masuala haya ya kusoma, wenzetu hawa wa jinsia ya kike huwa wana drop sana. Lakini nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge jambo hili sasa tunaenda kulizingatia katika taratibu za sasa hivi utumishi maeneo haya ya jinsia yanazingatiwa sana hasa katika mradi wetu ule wa HEET ambao nilizungumza katika kipindi kilichopita, zaidi ya Wahadhiri zaidi ya 600 tunaenda kuwasomesha na miongoni mwao tutaweka ajenda maalum kabisa katika kuhakikisha kwamba jinsia inaweza kuzingatiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana.(Makofi)
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza naishukuru Serikali kwa majibu mazuri yanayotia moyo. Hata hivyo majibu haya hajatoa takwimu; yaani hizi takwimu hazijaja na percent ili tuone ukubwa wa tatizo sisi kama wawakilishi wa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, mimi hapa nina takwimu ya chuo kimoja tu hiki cha MUHAS hapo Muhimbili. Mwaka 2022/2023 udahili, wanafunzi walioomba pale walikuwa 27,540; waliokidhi vigezo 19,287, lakini chuo kile kina uwezo wa kudahili wanafunzi 866 tu, ambayo ni 4% tu ya mahitaji: Je, hatuoni kwa trend hii kwamba tunakatisha tamaa vijana wetu kuendelea kusoma masomo ya Sayansi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kuchauka, Mbunge wa Liwale, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyowaelezakwenye majibu yangu ya msingi, tumeona ukubwa wa tatizo, ndiyo maana Serikali imeingia mkataba wa kuchukua mkopo huu. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari fedha hizi tumeshazipata na zinakwenda kutanua sasa wigo wa vijana wetu kuingia katika Masomo ya Sayansi. Amezungumzia suala la Muhimbili ambayo sana sana ni masomo ya tiba, lakini hapa tunazungumzia sayansi kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa takwimu zilizopo mwaka 2020 waliofanya mtihani wa kidato cha sita walikuwa ni 84,212; mwaka 2021 waliofanya mtihani wa form six walikuwa ni 88,273; na mwaka 2022 waliofanya mtihani wa form six walikuwa ni 94,456.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa takwimu hizi kama zaidi ya 40,000 wanakwenda kwenye masomo ya sayansi, yaani karibu asilimia 50 wanadahiliwa katika nyanja hiyo ya sayansi, bado tumesimama pazuri. Hata hivyo mradi huu unakwenda kutusogeza zaidi ya asilimia 70.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Hivi sasa wanafunzi wa vyuo vya afya nchini kwa ngazi ya cheti na diploma wanasoma kwa ghrama kubwa. Je, ni kwa nini sasa Serikali isione namna ya kuwapunguzia wanafunzi hawa gharama katika masomo yao ya fani ya afya kwa ngazi ya cheti na diploma ili wazazi waweze kumudu gharama zilizobaki?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Issaay, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tukiri kwamba ni kweli kwamba upande wa elimu ya tiba ada zimekuwa ni kubwa, lakini wakati tunatoa bajeti yetu hapa, wenzetu au benki yetu ya NMB ilitoa ufadhili wa zaidi ya shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kada hizi za kati. Kwa hiyo, eneo la kwanza naomba wazazi na walezi wa wanafunzi hawa waweze kuifikia benki hii ili waweze kupata mikopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Serikali tuko katika mpango mkakati wa kuhakikisha kwamba tunafikia kada hii ya kati pindi tutakapoongeza bajeti kwa ajili ya wanafunzi hawa kupata mikopo vilevile.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Katika Jimbo langu la Nachingwea kuna Chuo cha Ualimu lakini hakitoi kozi ya sayansi. Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha kozi ya sayansi katika chuo hiki cha Nachingwea?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Nachingwea, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuna Chuo cha Ualimu pale Nachingwea kwa vile Mheshimiwa Mbunge ametoa ushauri, naomba tuuchukue ushauri huu twende tukaufanyie tathmini ili tuweze kuangalia kama kuna uhitaji wa kuanzisha kozi hiyo ya sayansi katika chuo hicho.
MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, Serikali imeweka mkakati gani wa kuhakikisha malimbikizo hayaendelei tena kutokea katika kipindi kijacho?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, Serikali ipo tayari kulipa riba katika malimbikizo ya malipo yaliyochelewa kulipwa kwa Wahadhiri kama inavyofanya kwa wakandarasi wanaochelewa kulipwa malipo yao? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Paulina Nahato, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza kwenye majibu ya msingi, kwamba Serikali hulipa malimbikizo pamoja na stahiki nyingine za watumishi kulingana na bajeti. Kwa hiyo, mkakati wetu kama Serikali jambo la kwanza ni kuhakikisha kwamba tunaweka bajeti stahiki na toshelezi ili malimbikizo kwanza yasitokee na pili watumishi wanapokuwa na madai yao yaweze kulipwa kwa wakati. Huo ndiyo mkakati wetu kama Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye eneo la pili la riba, naomba nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba malipo haya hulipwa kwa mujibu wa kanuni, sheria taratibu na miongozo na kwa kanuni tulizonazo hivi sasa, hazina eneo ambalo linaonesha kwamba malipo yatakapochelewa yalipwe na riba. Kwa hiyo, halipo na badala yake tunasimamia utaratibu wa kawaida ambao ni bila riba.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
MHE. ORANI M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kwanza kuipongeza Serikali kwa kuanzisha na vile vile kuboresha hii ndaki ya afya ikiwa sehemu ya uboreshaji wa Afya nchini kwetu. Sasa kwa vile kuna ongezeko kubwa sasa hivi la magonjwa yasiyoambukizwa: Je, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na hii ndaki ya afya wamejiandaa vipi kukabiliana na hilo ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, kwa kuwa hiki chuo kinaonekana kuwa kitakuwa na eneo kubwa sana, kwa hiyo, kinategemea kuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi.

Je, kitakuwa na wanafunzi wangapi na pia wafanyakazi wangapi mara kitakapokamilika kujengwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Njeza, Mbunge wa Mbeya Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ilivyo kawaida kwenye vyuo vyetu vikuu, jukumu lao la kwanza ni kuhakikisha kwamba utoaji wa taaluma ya aina mbalimbali au katika maeneo ambayo yanakuwa yameainishwa. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu kwamba chuo chetu cha tiba ya binadamu Muhimbili kinaendelea kufanya utafiti wa magonjwa haya yasiyoambukizwa kwa undani zaidi ili kujua chanzo cha magonjwa haya na namna gani tunaweza kuyaepuka. Kwa hiyo, nimwondooe wasiwasi, na mikakati yetu kama Serikali na kama Wizara ni kuhakikisha kwamba tunaendelea kufanya tafiti hizo za kina.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili ni kuhakisha tunatoa elimu kwa Umma kuhusu namna gani ya kuepuka na kujikinga na magonjwa haya yasiyoambukiza. Kwa hiyo, hilo litakuwa ni jukumu la pili na mkakati wetu wa pili. Eneo la tatu ni kubadili sasa mifumo ya maisha yetu tuliyozoea kuishi ili kuweza kuepukana na magonjwa haya kama vile kubadili milo yetu na kuendelea kufanya mazoezi ya kila siku. Kwa hiyo, hiyo ndiyo mikakati yetu na tutahakikisha kwamba chuo kinaenda ku-emphasize kwenye mikakati ili kuhakikisha kwamba mambo haya yanakaa sawa sawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili linahusiana na suala la takwimu. Ameulizia wanafunzi watakuwa wangapi katika ndaki hii pamoja na watumishi watakuwa wangapi? Kwa vile sasa takwimu hizo sina hapa, naomba Mheshimiwa Mbunge aridhie kwamba tukimaliza Bunge hili tuweze kutafuta takwimu hizi na niweze kumpatia rasmi. Nakushukuru sana.
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza. Kwanza naipongeze Serikali kwa uamuzi wake wa kujenga VETA katika wilaya 63 ikiwemo Nyangh’wale. Naomba niulize maswali mawili: La kwanza, ni kiasi gani cha fedha ambacho kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa VETA katika Wilaya ya Nyangh’wale? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Ni lini ujenzi huo utaanza mara moja? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Amar, Mbunge wa Nyangh’wale, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kiasi kilichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo hiki katika awamu ya kwanza kwa sababu vyuo vitajengwa kwa awamu, tumetenga zaidi ya Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi huu. Suala la lini; hivi sasa tayari Wizara imeshapeleka maombi kwa wenzetu wa Wizara ya Fedha, tunasubiri upatikanaji wa fedha hizo. Mara tu fedha hizo zitakapopatikana kutoka Wizara ya Fedha, basi huo ujenzi utaanza mara moja.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Kwa kuwa Chuo cha VETA kinachojengwa pale Mhula Jimboni Ukerewe kipo kwenye hatua za mwisho kabisa za ukamilishaji, ni lini Chuo hiki kitaanza kutoa huduma? Nashukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Napenda kujibu swali dogo la Mheshimiwa Mbunge wa Ukerewe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Serikali ilikuwa imeanza ujenzi wa vyuo 25 katika wilaya 25 pamoja vile vinne vya mikoa na ujenzi ule upo kwenye hatua za mwisho. Hivi sasa tuko katika ukamilishaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na samani ambazo tutapeleka mle madarasani. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mwaka ujao wa 2023 vyuo hivi 25 vya Wilaya na vile vinne vya mikoa vitaanza kutoa mafunzo rasmi.
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba nimwulize Mheshimiwa Naibu Waziri: Ni lini Wizara ya Elimu itasaidia kwa dharura ujenzi Kituo cha VETA kule Nyamwaga, Nyamungo, kwa sababu fedha zimeshatengwa tangu mwaka 2021 mpaka sasa hivi imekaa inasubiri tu usaidizi wa Wizara yake? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu katika swali langu la msingi kwamba ujenzi wa Vyuo vya VETA katika Wilaya 63 tunatarajia kuanza mara tu fedha zitakapopatikana na miongoni mwa maeneo yatakayofikiwa ni pamoja na wilaya yake. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi, ujenzi huo utaanza mara tu fedha hizo zitakapopatikana. Nashukuru sana.
MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Wilaya ya Ilemela hakuna Chuo cha VETA, lakini wameshaandaa eneo lenye ekari 70.

Je, ni lini Serikali itaanza kujenga Chuo cha VETA katika Wilaya ya Ilemela ili kuondoa changamoto kwa vijana wetu ya kukosa ajira? (Makofi)
NAIBUWAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Mheshimiwa Mbunge anachosema kwamba Wilaya ya Ilemela haina Chuo cha VETA na ni kweli eneo tayari limeshatengwa na tayari tulishakabidhiwa eneo hilo rasmi sisi kama Wizara kupitia wenzetu wa Mamlaka ya VETA. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Wilaya hii ni miongoni mwa zile Wilaya 63 ambazo zitapata mgao huu wa fedha hizi awamu ya kwanza kwa ajili ya kuanza ujenzi katika eneo hilo la Ilemela. (Makofi)

Mhesimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. (Makofi)
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuzingatia ushauri wa Mheshimiwa Waziri wa Elimu, tayari Kijiji cha Mpanga, Kata ya Kisawasawa, Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Wilaya ya Kilombero, imepata eneo la ujenzi wa Chuo cha VETA.

Je ni lini ujenzi wa chuo hicho utaanza?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Asenga, Mbunge wa Kilombero kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spiuka, kama nilivyojibu kwenye majibu yangu ya swali la msingi kwamba Wilaya ya Kilombero ni miongoni mwa Wilaya 63 ambazo zipo kwenye mpango huu wa ujenzi wa vyuo vya VETA. Nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, tunasubiri fedha kutoka Wizara ya Fedha. Mara tu fedha zitakapopatikana, basi Wilaya ya Kilombero ni miongoni mwa Wilaya 63 ambazo ujenzi utaanza rasmi.
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Wilaya ya Tunduru ni kati ya Wilaya ambazo hazina vyuo vya VETA, na eneo la ujenzi wa Chuo tayari tumeshaliandaa na lipo: Je, ni lini Serikali itatujengea Chuo cha VETA katika Wilaya ya Tunduru? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Hassan, Mbunge wa Tunduru, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi kwa wilaya zote 63, ujenzi utaanza mara moja mara tu tutakapopata fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango. Ujenzi huo tunatarajia kuanza kwenye Wilaya zote kwa pamoja ikiwemo na Wilaya ya Tunduru. Nakushukuru sana.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa nia njema Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ilikabidhi Chuo cha VETA pale Mikumi kwa Serikali; na tangu Serikali imekabidhiwa, hakuna ukarabati na Chuo kinaendelea kuchakaa.

Je, ni kanuni au sheria kutowekeza fedha za ukarabati katika vyuo ambavyo Serikali imepewa bure?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Londo, Mbunge wa Mikumi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tuna Chuo cha VETA pale Mikumi ambacho hakijafanyiwa ukarabati na majengo yake ni chakavu. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 tumetenga fedha kwa ajili ya ukarabati pamoja na upanuzi kwenye baadhi ya maeneo ambayo vyuo hivi bado havijakamilika au vina miundombinu ambayo ni chakavu pamoja na hiki Chuo cha Mikumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. NOAH L. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Je, ni lini Serikali itajenga VETA katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha katika Jimbo la Arumeru Magharibi ambayo tayari tumeshawasilisha eneo kwa ajili ya kujenga VETA?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Mbunge wa Arumeru kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza kwenye majibu yangu ya msingi, wilaya 63 ambazo hazina Vyuo vya VETA tunatarajia kuanza ujenzi mara tu tutakapopata fedha ikiwemo na Wilaya ya Arumeru.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza swali la nyongeza.

Je, ni lini Serikali itafanikisha kampasi ya Tunduru kuanza rasmi masomo ya muda mrefu badala ya ilivyo sasa kwa masomo ya vitendo ambayo ni ya muda mfupi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kungu Mbunge wa Tunduru Kaskazini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi kwamba kampasi ile tayari ilishaanza kazi toka mwaka 2018/2019, lakini kozi ambazo zinatolewa pale ni zile za muda mfupi wanafunzi wetu wanapokwenda kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mwaka wa fedha 2021/ 2022 tumetenga zaidi ya Shilingi Milioni 250 kwa ajili ya kuongeza miundombinu kwenye eneo lile. Katika mwaka ujao wa fedha tutatenga tena fedha zaidi ya Shilingi Milioni 300 kwa ajili ya kuongeza miundombinu ambayo itasaidia sasa chuo kile kiweze ku-operate katika masaa 24 kwa muda wote.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge baada ya michakato hii kukamilika tunatarajia baada ya miaka hii Miwili hadi Mitatu tutaweza kuanza kozi pale za muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kisangwa kilichopo Bunda ndicho chuo pekee kinachotoa fani mbalimbali za ufundi na tatizo kubwa pale ni mabweni.

Je, ni lini Serikali itatusaidia kupata mabweni hayo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Maboto Mbunge wa Bunda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tuna changamoto kwenye Vyuo vyetu vya FDC lakini naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 tumefanya ukarabati pamoja na upanuzi wa vyuo hivi vya FDC 54 kote nchini.

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie katika kipindi kijacho tunaendelea na upanuzi huo ambapo tunaamini kabisa, chuo hiki cha Bunda kitazingatiwa katika ukarabati na upanuzi pamoja na haya mabweni tutaweza kuyafikia. Nakushukuru. (Makofi)
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, nashukuru.

Katika Kijiji cha Maneme Wilayani Nanyumbu kuna majengo ambayo yaliachwa na Kampuni ya ujenzi wa barabara na Serikali ya Kijiji iliyakabidhi majengo yale Wizarani.

Je, ni lini Wizara itatekeleza ahadi yake ya kufungua Chuo cha Ufundi katika Wilaya yangu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mhata Mbunge wa Nanyumbu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli eneo hili la Mtambaswala ambapo Kampuni yetu ya ujenzi wa barabara ilikuwa na kambi, tayari imekabidhiwa kwa Wizara ya Elimu kupitia Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA). Mwaka jana mwezi Novemba, 2021 timu yetu ya wataalam ilikwenda kufanya tathmini ya eneo lile namna gani tunaweza tukaboresha, kwa maana kwamba ya kufanya ukarabati pamoja na kuongeza baadhi ya miundombinu ili kiweze kufunguliwa.

Naomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge tayari tathmini tumeshafanya na tunatarajia katika mwaka ujao wa fedha, eneo lile tutakwenda kulifanyia kazi kuhakikisha kwamba Chuo kile kinafunguliwa. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwa kuwa, sasa ni miaka miwili toka Serikali itoe fedha za ukarabati wa Chuo cha Maendeleo Tango - FDC Mbulu na kwa kuwa tayari mradi wa awali umeshatekelezwa.

Je, ni lini Serikali yetu itatoa tena fedha ya ukamilishaji wa majengo hayo ya Chuo cha Tango FDC kwa awamu ya pili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mbunge wa Mbulu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu katika majibu yaliyopita katika Chuo cha VETA kule Bunda ni hivyo hivyo kwa upande wa wenzetu wa Tango.

Mheshimiwa Spika, naomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwanza katika fedha ambazo tulizipata za UVIKO – 19 zaidi ya Shilingi Bilioni 6.8 zimekwenda kununua vifaa kwa ajili ya vyuo hivi vya FDC (54) kote nchini, ambapo Chuo hiki cha Tango nacho vilevile kimezingatiwa.

Mheshimiwa Spika, vifaa hivi tayari tunavipeleka kwenye maeneo haya ya vyuo, vilevile upanuzi wa vyuo hivi tumeuingiza kwenye bajeti yetu ya mwaka ujao wa fedha. Kwa hiyo, maeneo haya yote tutakwenda kuyafanyia kazi kuhakikisha kwamba vyuo hivi vinatoa taaluma ile ambayo inatakiwa katika maeneo husika.
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru: -

Mheshimiwa Spika, je, ni lini sasa chuo cha ufundi VETA kwa Wilaya ya Kilolo kitajengwa kama ambavyo zimekuwa ahadi za Serikali kwa muda mrefu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Nyamoga, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni sera ya Wizara ya Elimu kwamba, katika kila wilaya tunakwenda kujenga chuo cha VETA. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa vile sasa tumekamilisha ujenzi wa vyuo vya VETA katika Wilaya 29 na vile vinne vya Mikoa ambavyo tunakadiria kunako mwezi Mei tutakwenda kumaliza katika mwaka ujao wa fedha tutaendelea na ujenzi katika maeneo ambayo bado vyuo havijaweza kujengwa. Ninakushukuru sana.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru: -

Mheshimiwa Spika, ningependa kujua ni lini Serikali itafungua au chuo kikuu au tawi la chuo kikuu Mkoani Kagera kwa kuwa limekuwa ni hitaji la muda mrefu na ukizingatia tuna ardhi ya kutosha? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Anatropia, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tuna mradi wetu wa heat ambao tunataraji tutaanza kuutekeleza katika mwaka ujao wa fedha, miongoni mwa maeneo ambayo ni focused zone ni katika Mkoa wa Kagera. Kwa hiyo, nikuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge katika maeneo ambayo tunaenda kujenga campus nadhani ilikuweko campus pale ambayo baadae ilikuja kufungwa, tunaenda kuifufua ili kuhakikisha kwamba Mkoa wa Kagera unakwenda kupata chuo hiki.

Vilevile tunafungua chuo kikubwa sana cha VETA katika Mkoa wa Kagera ambapo tunaamini chuo kile kitakuwa na hadhi vilevile ya chuo kikubwa hapa nchini. (Makofi)
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba nimuulize maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, miongoni mwa sababu zilizopelekea wanafunzi wengi kupata ujauzito wakiwa mashuleni ni mazingira ya ukatili, unyanyasaji na umaskini uliokithiri kwa maeneo wanayoishi.

Je, Serikali haioni umuhimu sasa wa kuwaweka wasichana hao katika shule za mabweni ili waweze kupata kusoma kwa utulivu na kuondokana na mazingira yale?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, agizo la kurejesha wasichana waliopata ujauzito mashuleni linatekelezwa chini ya Waraka wa Elimu Na. 2 wa mwaka 2021.

Kwa nini sasa Serikali isitunge sheria juu ya suala hili ili asije kutokea Kiongozi mwingine akataka kubadilisha jambo hili lenye dhamira njema?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nichukue fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uthubutu wake wa kuhakikisha kwamba wanafunzi hawa waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo na hii ya ujauzito wanarudi shuleni. Nini mikakati ya Serikali kwa hivi sasa?

Mheshimiwa Spika, mikakati ya Serikali kwa hivi sasa, Mheshimiwa Rais ameridhia ujenzi wa shule 26 za wasichana katika kila Mkoa ambapo ujenzi huu tunajenga kwa awamu, tayari ujenzi wa shule 10 umeshaanza kwenye Mikoa 10 mbalimbali katika awamu ya kwanza kwa lengo la kuhakikisha kwamba tunapata mabweni kwa ajili ya wanafunzi hawa kukaa katika mazingira mazuri na salama ya kujifunza na kujisomea.

Mheshimiwa Spika, eneo la pili ni ujenzi wa hostel kwenye maeneo ambayo tunaona kwamba kuna umuhimu wa kujenga hostel kwenye maeneo hayo pamoja na mabweni katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, mkakati wa tatu ni kuanzisha vitengo vya elimu, unasihi pamoja na ushauri kwenye shule zetu kwa lengo la kuhakikisha kwamba vitendo hivi havijitokezi kwenye maeneo hayo. Hatua ya mwisho ni kuchukua hatua kwa wale wote waliothibitika kujihusisha kwa namna moja ama nyingine kunyanyasa wanafunzi wetu na kuwakatizia masomo, hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao. Hiyo ndiyo mikakati mikubwa ya Serikali ili kuhakikisha jambo hili tunakwenda kulikomesha kabisa katika maeneo yetu.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili amezungumzia waraka namba mbili wa mwaka 2021. Ni kweli urejeshaji wa wanafunzi katika shule waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali ni waraka ambao umetoka mwaka 2021 na ni mwaka mmoja tu hivi sasa toka waraka huu tuweze kuanza kuutekeleza.

Ninamuomba Mheshimiwa Mbunge aridhie Serikali inaendelea kufanya tathmini ya utekelezaji wa waraka huu ili kuweza kubaini changamoto zilizopo, lakini vile vile na mafanikio yaliyopo katika waraka huu. Ikiwa tutaona kwamba kuna haja ya kutengeneza sheria maalum na kwa vile sasa tunafanya mapitio ya sheria pamoja na sera yetu ya elimu, tunaweza kufanya hivyo.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. HAMIDA M. ABDHALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu hayo yenye matumaini lakini pia nishukuru Serikali kwa kutenga fedha 5.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Lindi. Pia, nimshukuru Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ziara ambayo ameifanya Lindi wiki mbili zilizopita kwa kuja kukagua maeneo haya ambayo yatajengwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Lindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

(i) Kwa kuwa Kampasi hii ambayo itajengwa ya Lindi itakuwa mahususi kwa ajili ya kozi ya ufugaji wa nyuki, kilimo, uchumi na biashara, sayansi na teknolojia. Kwa nini Serikali isipanue kwa kuongeza kozi ya uvuvi pamoja na kilimo cha mwani?

(ii) Ningependa sasa kujua kwa sababu kanda nzima ya kusini tuna uhitaji mkubwa wa chuo hiki cha usafiri na usafirishaji baharini, ni lini sasa Serikali itafanya utafiti kuhakikisha kwamba tunapata ujenzi wa chuo hiki cha usafiri na usafirishaji kwa ajili ya kuongeza ajira kwa vijana lakini kuendelea kukuza uchumi na kuwekeza wataalam kama rasilimali watu katika nchi yetu ili waendelee kukuza uchumi kupitia bahari yetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hamida Mohamed, Mbunge wa Lindi Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wa karibu wa suala hili. Amekuwa akifika Ofisini kwetu mara kwa mara na alikuwa akiliulizia mara kwa mara lakini sasa mwarobaini au majawabu ya suala lake hili linakwenda kufikia ukingoni. Kwa hiyo, nikushukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji huo wa karibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama nilivyojibu kwenye swali la msingi kwamba Serikali inakwenda kujenga Kampasi hii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Mkoa huo wa Lindi na tutaanza na kozi hizo na tathmini tutafanya iwapo kama tutaona uhitaji wa kuanzia hizi kozi za uvuvi pamoja na Kilimo cha Mwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti na Mheshimiwa Mbunge nikutoe wasi wasi baada ya kufanya market survey na need assessment na kujiridhisha kozi hizo zitakapoanzishwa zitapata wanafunzi basi tutakwenda kuzianzisha kozi hizo kwa kadri ya mahitaji yatakavyookuwa yanaruhusu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye swali lake la pili kuhusiana na uanzishwaji wa chuo cha usafiri, nimtoe wasi wasi Mheshimiwa Mbunge kwa vile tunaenda kuanza ujenzi wa chuo hiki katika kampasi hii. Ni utaratibu wa vyuo vyote duniani, tutafanya tathmini ya kuanzisha kwanza kozi za usafirishaji katika chuo hiki au katika Kampasi hii. Badaaye katika upanuzi iwapo kama tutaona uhitaji tunaweza sasa kwenda kuanza majengo au chuo kingine katika maeneo ambayo yatakuwa yanapatikana. Ndiyo utaratatibu wa vyuo vyote duniani hata uanzishaji wa Chuo Kikuu cha Muhimbili ulianzia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Ardhi kilianzia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hata hiki baada ya kuanzisha na kuona kwamba uhitaji unazidi kupanuka tutaweza kufika katika maeneo hayo Mheshimiwa Mbunge anapendekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa
Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi kwa kuuliza swali. Ningelipenda kujua Chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere kinachojengwa Butiama ni lini kitaanza kufanya kazi? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza Mheshimiwa Ishengoma, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tuna Kampasi ya Mwalimu Nyerere kule Butiama na ilianzishwa toka mwaka 2014 lakini bado ilikuwa haijanza kufanya kazi, lakini naomba nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge tulifanya ziara na Kamati yako ya Bunge hili mwezi uliopita na tulikwenda pale kwa ajili ya kufanya tathmini na naomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge, chuo kile kitaanza kufanya udahili katika mwaka huu ili kuweza kuanza kutoa mafunzo katika eneo lile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. BAHATI K. NDINGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa, wameshaanza mapitio ya mitaala, ni kwa namna gani wameweza kushirikisha sekta binafsi katika mapitio ya mitaala hiyo ikiwa wao ndio waajiri wakubwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, tunatambua kwamba elimu ya ufundi kwa sasa ni muhimu ili kuwawezesha wahitimu kujiajiri na kuajiriwa. Sasa Serikali ina mkakati gani kuhakikisha wanaanza kutoa mikopo kwenye vyuo vyetu vya ufundi nchini? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Bahati Keneth, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza katika majibu ya msingi, kwamba kupitia mradi huu wa HEET ambao ni wa zaidi ya Dola milioni 425, tunafanya maboresho makubwa na mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu. Miongoni mwa mapinduzi hayo ni katika kuboresha mitaala yetu iliyopo sasa. Katika uboreshaji wa mitaala hii, ushirikishaji wa wadau, kama nilivyozungumza kwenye jibu la msingi, ni wa kiasi kikubwa ikiwemo na sekta binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge pamoja na Bunge lako Tukufu, ushirikishwaji wa wadau mbalimbali wakiwemo sekta binafsi tunauzingatia kwa kiasi kikubwa na ndiyo maana tunafanya kitu kinaitwa tracer study and needs assessment. Lengo kuu ni kuhakikisha kwamba tunapata mahitaji, lakini vilevile tunawashirikisha wadau.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la pili, nazungumzia suala la mikopo katika kada ya kati. Hili suala tayari tulishalizungumza hapa Bungeni na tulisema wenzetu wa NMB tayari wameshaingia kwenye utaratibu huu. Wametenga zaidi ya Shilingi bilioni 200 katika mwaka huu wa fedha 2022/2023, lakini sisi kama Serikali katika mwaka 2023/2024 tunakusudia sasa kutenga fungu kwa ajili ya mikopo katika kada hii ya kati, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. LATIFA KHAMIS JUWAKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa, sasa Serikali imetuelezea kwamba kuna vyuo mbalimbali ambavyo vinatoa elimu ya juu ambayo inazingatia hiyo principal pass. Je, hamuoni sasa Serikali kuandaa Mpango maalum kupitia TCU ambao ndiyo wadhibiti ubora wetu wa Elimu ili waweze kuwashauri sasa Vyuo Vikuu vyetu waweze kuliingiza ili somo la dini liwe kama ni miongoni mwa Principal pass?

Swali langu la pili, kwa kuwa masomo haya ya dini yanawajenga vijana wetu kimaadili lakini pia yanawajenga wanafunzi wetu wetu kimaadili lakini na kiimani. Je, hatuoni sasa kulitoa hili somo la dini kwamba siyo miongoni mwa principal pass ambazo zitamsaidia mwanafunzi kujiunga na Chuo Kikuu, hatuoni sasa tunawaandaa wanafunzi wengi ambao wakimaliza Vyuo Vikuu watakuwa hawana maadili mazuri kwa sababu wanafunzi hawatalisoma hili kama ni somo la msingi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Latifa Juwakali kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwisha kueleza kwenye majibu ya msingi kwamba masomo haya ya dini yanatumika kwenye baadhi ya Vyuo na kwenye baadhi ya program. Hatuwezi program zote tukasema kwamba ziingize masomo ya dini, kwa sababu itategemea na program gani mwanafunzi anayokwenda kusoma. Kwa hiyo, tumebeba ushauri huo alioutoa lakini ninaomba nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba TCU jukumu lake ni kudhibiti, kufanya Ithibati ya ubora wa masomo yanayotolewa na siyo kupanga kwamba program gani iingizwe na kwa requirement zipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezungumza zile Senate ndizo zenye wajibu wa kupanga namna gani requirements zinazotakiwa kwenye program husika. Kwa hiyo, tunalibeba suala hili la kuona namna gani masomo yetu ya dini yanaweza yakaingizwa kwenye baadhi ya hizo program kwa kadri tutakavyoona inafaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru sana.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza niwapongeze Wizara niwapongeze Wizara ya Elimu kwa kazi nzuri wanazofanya. Kwa kuwa Manispaa ya Kahama ina chuo cha FDC ambacho kinafanya kazi kama ile ile ya Chuo cha VETA: Kwa nini sasa chuo hiki cha VETA kisijengwe katika Halmashauri ya Ushetu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili: Kwa kuwa uhitaji wa Chuo cha VETA kwa wananchi wa Ushetu mkubwa sana kulingana na ongezeko kubwa la vijana ambao wanamaliza vyuo vikuu lakini hawaendelei na masomo ya juu: Kwa nini sasa Serikali isione hili kwa umuhimu kulingana na umbali wa kilometea zaidi ya 113 kutoka Ushetu kuja Manispaa ya Kahama?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Cherehani, Mbunge wa Ushetu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimweleze Mheshimiwa Mbunge kuwa Wizara haipangi maeneo ya kujenga vyuo hivi vya VETA, ni jukumu la Serikali za Mikoa pamoja na Wilaya kupanga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivi vya VETA. Naomba nitoe wito kwa Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakuu wa Mikoa washirikishe Waheshimiwa Wabunge wa maeneo mbalimbali kuhakikisha kwamba wanakwenda kupanga maeneo sahihi ya kuweza kufanya ujenzi wa vyuo hivi vya VETA.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lakwe la pili, tunajua umuhimu wa vyuo hivi na hivi sasa tumeanza katika ngazi ya Wilaya pamoja na Mikoa; baada ya kukamilika zoezi hili katika ngazi za wilaya pamoja na mikoa, tutafanya tathmini ya kina ili kuweza kuona namna gani tunaweza kuzifikia zile Halmashauri ambazo labda ziko mbali na maeneo ambayo yamejengwa katika VETA zile za Wilaya pamoja na Mikoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itakwenda kujenga VETA katika Jimbo la Arumeru Magharibi katika Wilaya ya Arumeru?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Arumeru, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyozungumza katika majibu ya msingi, ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba inajenga vyuo vya VETA katika kila Mkoa na Wilaya nchini na tumeweza kufikia Mikoa yote na hivi sasa tunakamilisha Mkoa wa mwisho ule Mkoa wa Songwe. Katika mwaka huu wa fedha tunakwenda kujenga katika Wilaya 63 ambazo zilikuwa hazina vyuo hivi. Iwapo kama Arumeru ni miongoni mwa Wilaya zile 63 bila shaka tutaifikia wilaya hii na kuhakikisha kwamba tunakwenda kujenga katika Wilaya ya Arumeru.
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Wilaya ya Kishapu ni moja kati ya wilaya ambazo zinatekeleza ujenzi wa miradi hii ya VETA; na mpaka sasa hivi mradi huu una zaidi ya miaka mitatu uko katika ujenzi, lakini bado kuna upungufu wa ukamilishaji wa umeme, furniture, maji, na baadhi ya miundombinu katika maeneo hayo. Ni zaidi ya Shilingi milioni 400 zinahitajika kwa ajili ya kukamilisha mradi huu. Ni lini Serikali itakamilisha suala la kuleta fedha kwa ajili ya kukamlisha mradi huu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mbunge wa Kishapu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge wa Kishapu na Waheshimiwa Wabunge wengine ambao maeneo yao tayari tumeweza kujenga vile vyuo 25. Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwaka huu tayari ameshatoa jumla ya Shilingi bilioni 10.3 kwa ajili ya kukamilisha maeneo yale katika vile vyuo vyote 25. Katika zile kazi ambazo bado hatujakamilisha, na tayari tumeshaanza kuzipeleka kwenye maeneo yale kwa lengo la kukamilisha kazi hizo. Kwa hiyo, muda mfupi ujao tutakuwa tumekamilisha. (Makofi)
MHE. NG'WASI D. KAMANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ilitenga eneo la ekari 50 kuipa Wizara ya Elimu bure kabisa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA: Sasa ni lini chuo hiki kitaanza kujengwa rasmi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Ng’wasi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Ilemela ni miongoni mwa Wilaya 63 ambazo tunaanza ujenzi katika mwaka huu wa fedha.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Nampongeza Mheshimiwa Waziri na Serikali kwa hatua kubwa iliyofikiwa ya ujenzi wa chuo hiki cha VETA.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa dhamira ya Serikali kujenga vyuo vya VETA ni kusaidia vijana wetu kupata taaluma itakayowasaidia kujiajiri au kuajiriwa kulingana na mazingira yao, nataka kujua, ni kozi zipi au aina ipi ya mafunzo itakayotolewa kwenye chuo hiki cha VETA ukerewe?

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mkundi, Mbunge wa Ukerewe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyozungumza kwenye majibu ya msingi kwamba mafunzo tutaanza mwezi wa Nne na tutaanza kwa kozi fupi; na tuliwaelekeza Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya, katika Mabaraza yetu ya Madiwani waweze kuamua au ku-detect na aina ya kozi ambazo tunatarajia kuanza nazo; ziko zile kozi za jumla ambazo tunatarajia kuanza nazo kama za ufundi umeme wa majumbani, uchomeleaji na ufundi wa mabomba; hizo ni kozi muhimu ambazo tunatarajia kuanza nazo katika kipindi hicho kifupi.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa nafasi. Serikali imeahidi kujenga Chuo cha VETA Jimbo la Mbulu Vijijini na tumeandaa ekari 50, na umetuma wawakilishi wako; je, lini mnaanza kujenga Chuo cha VETA Mbulu Vijijini?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Flatei, Mbunge wa Mbulu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza katika swali la mwanzo kwamba ujenzi wa vyuo 63 unatarajia kuanza hivi karibuni, kwa hivi sasa tunaandaa michoro pamoja na kufanya geotechnical survey, topographical survey, pamoja na kufanya estimate kwa ajili ya kuanza ujenzi kwenye maeneo mbalimbali, ikiwemo na Wilaya ya Mbulu. (Makofi)
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Wilaya ya Tarime haina Chuo cha VETA. Mwaka 2022 niliuliza swali hili hili kwa Mheshimiwa Naibu Waziri na akaahidi kwamba wataiweka kwa upande wa Rorya na Tarime. Nataka nijue, katika hivyo vyuo 63 ambavyo mnatarajia kujenga, Wilaya ya Tarime nayo imo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Matiko, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katika kipindi kilichopita Mheshimiwa Mbunge aliuliza hoja hii. Naomba tu Mheshimiwa Mbunge baada ya kipindi hiki cha maswali uje kuangalia orodha iwapo kama Wilaya walioiyoitaja ipo au haipo.
MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa kuwa kumekuwa na matatizo mengi yanayoikabili elimu nchini Tanzania tumeona watoto wengi wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma na kuandika, lakini pia idara nyingi za udhibiti wa elimu nchini Tanzania hazina vitendea kazi.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwanunulia vitendea kazi hususani magari Idara ya Udhibiti Ubora wa Elimu?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, kuna mwongozo wowote ambao umetolewa na Wizara ya Elimu katika kudhibiti hivi vyuo vya watu binafsi?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbogo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la kwanza anazungumzia suala la vitendea kazi; kwanza nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali hii inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeshafanya mambo makubwa sana kwenye udhibiti wa ubora wa elimu nchini hasa kwenye upande wa vitendea kazi.

Mheshimiwa Spika, kwanza Serikali imeshajenga ofisi karibu katika halmashauri zote za wilaya nchini kwa ajili ya maeneo ya ndugu zetu hawa au watumishi wetu kuweza kupata mazingira mazuri na salama ya kutendea kazi zao. Lakini vilevile mwaka uliopita wa fedha Serikali ilinunua magari zaidi ya 184 na kuyasambaza kwenye halmashauri au kwenye ofisi hizi za wadhibiti ubora katika halmashauri zote nchini, lakini juzi juzi hapa baada ya zoezi la Sensa kukamilika tumepeleka vishikwambi katika ofisi hizi kwa ajili ya watumishi hawa katika ngazi hii ya udhibiti ubora.

Kwa hiyo, kwa msingi wa vitendea kazi tayari Serikali tumeshafanya kazi kubwa sana na hivi sasa tupo katika programu za kuwaongezea uwezo kwa maana ya kuweza kuweka programu mbalimbali za mafunzo kwa watumishi hawa ili kuweza kutenda kazi yao sawasawa. Niwaondoe wasiwasi Waheshimiwa Wabunge kwamba tayari Serikali imefanya kazi kubwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la miongozo katika utendaji kazi kwenye udhibiti ubora tunakwenda na kanuni pamoja na miongozo mbalimbali ya elimu, ndio wanayozingatia katika utendaji wao wa kazi wa kila siku. Kwa hiyo miongozo kimsingi ipo kuhakikisha kwamba kazi hizi zinakwenda sawasawa, nakushukuru sana.
MHE. JEREMIAH M. AMSABI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, awali ya yote ninaishukuru sana Serikali na kipekee kabisa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa VETA Wilayani Serengeti.

Mheshimiwa Spika, watu wa Serengeti wamekuwa na uhitaji wa chuo hiki kwa muda mrefu sana jambo ambalo lilipelekea kumfuata mara kwa mara Waziri, Naibu Waziri kuwataka kutusaidia kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa chuo hiki.

Sasa niiombe Serikali itoe kauli ya ni lini chuo hiki wataanza ujenzi wake pamoja na maandalizi yote yanayoendelea, lakini tunataka kujua ni lini ujenzi utaanza? Hilo ni swalila kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kutokana na changamoto za kijiografia pamoja na mahitaji maalumu ya Serengeti, niliiandikia Wizara proposal ndogo ya kuboresha kile chuo ambacho watajenga Serengeti.

Sasa je, Waziri au Naibu Waziri pamoja na wataalam wake wapo tayari kuja Serengeti kuona mazingira na kufanya need assessment kwa sababu proposal hii itahitaji nyongeza ya fedha kidogo na hivyo watapata uelewa mpana na kutusaidia katika proposal hii? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Jeremiah Mrimi, Mbunge wa Serengeti kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nikiri ni kweli Mheshimiwa Mbunge toka mwaka 2021 amekuwa akifika ofisini mara kwa mara, lakini hata hapa Bungeni tukionana mara kwa mara alikuwa akinikumbusha jambo hili, lakini mara kadhaa nadhani amefika kwa Mheshimiwa Waziri pamoja na kupiga simu kufuatilia jambo hili.

Kwanza nikushukuru Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji huo wa karibu kwa kuwafuatilia wananchi wa Serengeti tunakushukuru sana.

Mheshimiwa Spika, kipekee nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, siyo kwa kutenga tu fedha.

Mheshimiwa Spika, naomba nikuhakikishie kwamba hii shilingi bilioni 100 tayari Mheshimiwa Rais ameshaitoa, kwa hiyo, ni jukumu letu sisi kama Wizara sasa kusimamia kwa karibu.

Kwa hiyo, naomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge hivi sasa tuko kwenye maandalizi, hauwezi ukasema tu kwamba utaanza kesho kwa sababu kuna taratibu ambazo lazima tuzifanye. Nimesema hapa maeneo tayari tumeshapata, tumebainisha maeneo yale na hivi sasa tunafanya topographical survey, lakini vilevile lazima tufanye geo-technical survey, lakini vilevile lazima tufanye environment impact assessment ili wakati tunapoanza tusiweze tena kupata changamoto.

Kwa hiyo, nikuhakikishie tu kwamba taratibu hizi zitakapo kamilika ujenzi huu utaanza mara moja.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la pili, kwa upande wa kuja sisi aidha mimi au Waziri na wataalam, naomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge tupo tayari kwenda Serengeti ili kuweza kuona changamoto na namna gani tunaweza kuzifanyia kazi, nashukuru sana.
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, nimesikiliza majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri kuhusiana na Wilaya 63 ambazo mnatarajia kujenga VETA katika mwaka huu wa fedha.

Je, Wilaya ya Kigamboni ni moja ya Wilaya hizo unaweza ukalithibitisha hilo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Kigamboni, kaka yangu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimuondoe hofu Mheshimiwa Dkt. Ndugulile kwamba katika orodha na mimi nimeipitia vizuri na Wilaya ya Kigamboni ni miongoni mwa Wilaya ambazo ziko kwenye mpango wa kujengewa vyuo hivi na bahati nzuri maeneo yameshatengwa kwa ajili ya ujenzi na mimi Mheshimiwa Mbunge baada ya Bunge hili kwa vile niko karibu pale tutakwenda kulitembelea na kuona namna hani tunaweza tukafanya. (Makofi)
MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Spika, kwanza niishukuru sana Serikali kwa kutenga fedha, lakini pia nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kupeleka fedha wilayani kama alivyotuhakikishua Mheshimiwa Naibu Waziri. Sasa nina maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa Serikali sasa imesema miradi hii ya ujenzi wa vyuo vya VETA itaanza mwaka huu kwa Wilaya 63 ikiwemo na wilaya ya Busega. Je, nini mpango wa Serikali wa kumaliza vyuo hivyo kwamba itamaliza lini ili Watanzania waweze kunufaika katika hizi Wilaya 63?

Swali la pili, je Naibu Waziri yuko tayari sasa kutembelea Busega ili tuje tumuoneshe eneo ambalo tayari tumeshatenga kwa ajili ya ujenzi wa VETA?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Simon Songe, Mbunge wa Busega kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu ya msingi kwamba Serikali imetenga fedha na tunaenda kuanza ujenzi huu baada ya taratibu za manunuzi, lakini topographical survey, geo-technical survey pamoja na environment impact assessment kuweza kukamilika. Kwa hiyo nimuondoe hofu na wasiwasi kwamba tunaenda kuanza ujenzi huu.

Mheshimiwa Spika, lakini lini tutamaliza? Kwanza naomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ujenzi huu tutajenga kwa awamu, kwa hiyo katika awamu ya kwanza tunakwenda kujenga majengo tisa ikiwemo na karakana tatu, lakini katika awmu ya pili tunakwenda kujenga majengo nane ili kuweza kukamilisha yale majengo 17.

Kwa hiyo, katika mwaka huu wa fedha tutakadiria kwamba au tunaazimia tutakamilisha yale majengo tisa na katika mwaka ujao wa fedha tutamalizia yale majengo manane yaliyobaki. Kwa hiyo, matarajio ya kumaliza ni mpaka mwaka ujao wa fedha tutakapokamilisha majengo yote 17.

Mheshimiwa Spika, katika swali la pili ameulizia kuhusu suala la kwenda. Hili ni jukumu letu, ni kazi yetu kwa vile tunapeleka fedha kule, fedha nyingi, ni lazima tufanye usimamizi wa karibu na ufuatiliaji wa karibu. Kwa hiyo tuko tayari kama Wizara kwenda kuona maeneo haya ya ujenzi, lakini vilevile kwenda kuratibu taratibu za ujenzi kuhakikisha kwamba unakamilika kwa viwango vinavyohitajika, nakushukuru sana.
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa wilaya zitakazonufaika na mradi wa ujenzi wa vyuo 63 vya VETA, tumeshaandaa eneo katika Kitongoji cha Matapatapa Kijiji cha Njia Nne na pia tumewekeza shilingi milioni 6.5 kwa ajili ya uandaaji wa hati pamoja na kufanya environmental impact assessment.

Je, ni lini ujenzi wa chuo hicho utaanza?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Ndulane, Mbunge wa Kilwa Kaskazini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyozungumza kwenye majibu ya msingi kwamba tutakapokamilisha tu taratibu za manunuzi pamoja na hizi geo-technical, topographical pamoja na environmental impact assessment tunatarajia kuanza. Matarajio yetu kunako kuanzia mwezi wa nne hivi tuweze kuanza ujenzi huu katika maeneo yote nchini. (Makofi)
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, Serikali imekamilisha ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi - VETA kwenye Jimbo la Igunga.

Swali langu kwa Serikali; je, ni lini Serikali itafanya udahili na kuanza kwa wanafanzi kusajiliwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Nicholaus Mbunge wa Igunga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza tulikuwa hatujakamilisha ujenzi kwa asilimia 100, Mheshimiwa Rais mwezi wa kumi na mbili alitoa fedha saidi ya shilingi bilioni 10.3 kwa ajili ya umaliziaji wa vile vyuo 25, fedha hizo tayari tumeshazipeleka kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo na pale Igunga. Kwa hiyo, ujenzi sasa tunaenda kukamilisha na tunatarajia kuanzia mwezi wa nne tuanza kudahili zile kozi za muda mfupi, nashukuru sana.
MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipatia nafasi.

Ni lini Serikali itajenga karakana ngumu katika Chuo cha VETA kitangali karakana ngumu ambazo ni uselemala na welding kwa sababu karakana hizo hazipo katika chuo hicho? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Maimuna Mtanda, Mbunge wa Newala kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli katika chuo chetu cha Kitangali kuna upungufu wa karakana na mimi nilishafika pale, nilifanya ziara mwaka jana kuweza kwenda kuona eneo lile na nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge katika bajeti tutakayoiandaa ya mwaka 2023/2024 tunakusudia kuhakikisha kwamba maeneo yale ambayo kuna upungufu wa karakana ikiwemo pale Kitangali pamoja na Mikumi kwa Mheshimiwa Londo tunatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa karakana kwenye maeneo hayo.
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na mimi nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Ufundi VETA Wilaya ya Chemba kimekamilika zaidi ya asilimia 80; ni lini sasa Serikali itaanza kudahili kwa kozi hizo ndogo ndogo za muda mfupi kwa maana miwili/miezi mitatu ili vijana wetu walipo mitaani waondokane na adha ya ajira na hatimaye waweze kujiajiri? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kunti Majala, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwenye swali la Mheshimiwa Ndulane, Chuo cha Chemba ni miongoni mwa vile vyuo 25 ambavyo vilikuwa bado havijakamilika. Kwa hiyo, kuna snag ndogo ndogo ambazo zilikuwa za kumalizia. Zaidi ya shilingi milioni 400 ilikuwa inahitajika na Mheshimiwa Rais tayari ameshatoa fedha zaidi ya shilingi bilioni 10.3 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyuo hivi 25. Tayari fedha hizi tumeshazipeleka pale Chemba na maeneo mengine na tunatarajia kuanzia mwezi wa nne kozi hizi za muda mfupi tuweze kuanza kudahili na ziweze kutolewa katika maeneo ya Chemba na maeneo mengine vyuo hivi 25 vinapojengwa.
MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri, kwanza nilikuwa na maswali mawili ya nyongeza. Kutokana na mpango huu ambao majibu yake ya Serikali ambayo ameelezea nataka nimuulize Zanzibar inanufaikaje na mradi huu wa High Education Economic?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, napenda kumwuliza, Serikali ina mpango gani sasa wa kuzipandisha hadhi campus za UDSM na Mwalimu Nyerere ili ziwe Chuo Kikuu ili kuondosha tatizo hili? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ussi Pondeza, Mbunge wa Chumbuni, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali yetu ilipata mkopo, kutoka Benki ya Dunia wenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 425. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika mkopo huu, Serikali imetenga zaidi ya Dola milioni 20 kwa ajili ya Chuo chetu cha Taifa cha Zanzibar, kwa ajili ya uongezaji wa miundombinu pamoja na usomeshaji wa wafanyakazi katika eneo lile. Kwa hiyo, eneo hili tunakwenda kulifanyia maboresho makubwa sana kuhakikisha kwamba tunakuwa na miundombinu ya kutosha; na Zanzibar ni mnufaika mkubwa wa mikopo hii pamoja na vyuo vingine vya elimu ya juu nchini.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili, ameulizia kuhusiana na suala la kupandisha hadhi campus zetu. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu, hivi sasa Serikali kupitia mkopo huu wa HIT, tunakwenda kuboresha miundombinu katika vyuo vyetu vikuu na taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa hatuna dhamira ya kupandisha hadhi campus hizi mbili pamoja na campus nyingine za vyuo zilizokuweko pale mpaka miundombinu pamoja na watumishi waweze kutosheleza mahitaji tunayoyahitaji hivi sasa. Nashukuru sana. (Makofi)
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba sasa niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mwongozo huu ulitoka mwaka 2019 na sasa ni mwaka 2022; je, Serikali imefanya tathmini na kugundua changamoto zipi juu ya mwongozo huo, na nini majibu ya Serikali baada ya kugundua changamoto zilizopo katika mwongozo huo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; ni lini Serikali itakamilisha uandaaji wa Sera mpya ya Elimu ya Sekondari ili kumpunguzia kijana wa Kitanzania mzigo wa kukaa muda mrefu shuleni? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asia kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani tunakumbuka Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 22 Aprili, 2021 akihutubia Bunge hili tukufu alituagiza Wizara ya Elimu kuweza kufanya mapitio ya sera, sheria pamoja na mitaala yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, zoezi hilo ndilo ambalo linaendelea hivi sasa na katika mapitio haya ya sera, sheria pamoja na mitaala, suala la miongozo hii kufanyiwa tathmini nalo limeingizwa ambapo tutafanya tathmini ya kina kuona namna gani miongozo hii tunaweza kuirekebisha kulingana na wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili, anauliza muda gani tutatumia; naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa mpaka kufika mwaka wa fedha ujao tutakuwa tumekamilisha utaratibu wa mapitio ya sera, sheria pamoja na mitaala hii ili iweze kuanza kutumika. Nakushukuru sana.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hatua kubwa ya wahitimu nchini wa sekta ya elimu, zaidi ya asilimia 70 ya wahitimu wa vyuo nchini ni walimu.

Je, Serikali haioni kuwa ni wakati mwafaka sasa wa kuhamasisha fani nyingine ili vijana wetu wanapomaliza kidato cha nne waweze kusoma fani nyingine kwa mazingira wezeshi?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Zacharia Issaay kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo ambalo anazungumza Mheshimiwa Mbunge ni kweli, na kama nilivyojibu kwenye majibu yangu ya msingi, kwa vile sasa tunafanya mapitio ya sera, sheria pamoja na mitaala yetu ambayo tunakwenda kuhakikisha kwamba maeneo mengi ambayo yanabeba fani za ufundi tunakwenda kuyafanyia kazi. Kwa hiyo, nimuondoe wasiwasi katika eneo hilo, kwa vile amesema wengi ni walimu hata huko huko kwenye ualimu nako tukiweka na stadi zlie za kazi tunaweza tukaondoa changamoto hiyo ya ajira.
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; kwa sababu Serikali inao mpango wa kutafuta fedha na kuhakikisha vyuo hivi vinajengwa. Wilaya ya Magu imeshatenga zaidi ya hekari 30, ikitegemea Serikali ipeleke fedha kwenye eneo hili na wananchi waweze kufaidika na vyuo hivi vya VETA. Sasa Serikali tunaomba commitment yake kwamba itakapopata fedha, Wilaya ya Magu iwe ya kwanza kwa sababu hata kule Kwimba, wanajenga kituo ambacho kina miaka miwili leo na hakijakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, pamoja na Serikali kuendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kupeleka kwenye ujenzi wa vyuo vingi vya VETA, vyuo vingi vimekuwa havina vifaa vya kufundishia na matokeo yake wanafunzi wengi wanajifunza kwa theory peke yake.

Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kila Chuo cha VETA kinapoanzishwa kilichopo kinakuwa na vifaa vyote stahiki kwa ajili ya kufundishia. Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mabula, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwennyekiti, ni kweli katika sera yetu ya Serikali kwamba tutakwenda kujenga Chuo cha VETA katika kila Wilaya na Mkoa katika Taifa letu. Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge na kumpongeza vilevile kwa ufuatiliaji wa karibu, iwapo Serikali itapata fedha, basi kipaumbele cha kwanza kitakuwa katika Wilaya hiyo ya Magu na Wilaya nyingine ambazo tayari zimeshatenga maeneo kwa ajili ujenzi wa vyuo hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimtoe wasiwasi vilevile katika eneo hili la pili la vifaa. Kama anavyofahamu Mheshimiwa Mbunge katika awamu ya kwanza tunakwenda kujenga Vyuo 25 katika Wilaya 25 mbalimbali nchini, tayari Vyuo hivyo viko mwishoni kabisa katika kumalizika kwake na tunaamini ifikapo Julai, vyuo hivi vinaweza kuanza kutoa huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hili Serikali tayari imeshatenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya vyuo hivi ili basi vitakapofunguliwa pamoja na ufundishaji wa nadharia lakini ufundishaji wa vitendo uwe umepewa kipaumbele zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimuondoe wasiwasi tayari Serikali inafanyia kazi jambo hili na fedha tayari imeshatengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia. (Makofi)
MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri kwa kazi wanayofanya ya kuhamasisha VETA katika nchi yetu.

Nataka kufahamu tu kwa ufupi ni lini Serikali inakwenda kutekeleza ujenzi wa VETA pale Mufindi, ikizingatiwa kwamba sasa tarehe 29 Aprili, Baraza la Madiwani limeamua VETA ikajengwe Nyololo, lini utekelezaji wake unafanyika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kihenzile, Mbunge wa Mufindi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Kihenzile, alikuwa anafuatilia suala hili kwa karibu. Mheshimiwa Kihenzile wewe mwenyewe ni shahidi nadhani tumeshawahi kuonana siyo mara moja, siyo mara mbili na umeshawahi kuja ofisi zaidi ya mara moja kwa ajili ya suala hili. Kwa vile tayari mmeshapitisha kwenye Baraza lenu la Madiwani ambalo ndilo lenye mamlaka ya kupanga wapi chuo hiki kijengwe. Nikuondoe wasiwasi iwapo Serikali itapata fedha, kipaumbele kitakuwepo katika maeneo haya ya Mufindi kwa sababu tunajua kule kuna shughuli nyingi sana ambazo zinahitaji masuala haya ya ufundi kuweza kuzingitiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, nikuondoe wasiwasi nalo hili tunalifahamu tutalitilia mkazo kwa karibu zaidi. Ninakushukuru sana. (Makofi)
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu hayo, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa mpaka sasa Serikali inatoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vitatu ambavyo ni vya Serikali MUST, DIT na Arusha Technical College ambao ni 2,435 pekee. Ni nini sasa maandalizi ya msingi ambayo Serikali imeshafanya mpaka sasa kuhakikisha kwamba inatoa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vya kati ikiwepo wa private? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa nini sasa Serikali isione namna ambavyo inaweza kushirikisha Sekta Binafsi ikiwemo benki ili na wao waweze kushiriki katika kutoa mikopo kwa vyuo vya kati kwa riba nafuu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Nusrat Hanje, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la kwanza anataka kufahamu maandalizi au mkakati wa Serikali kwa upande wa utoaji mikopo katika elimu ya kati. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, eneo la kwanza kama nilivyojibu kwenye swali langu la msingi, tumeendelea au tutaendelea kupeleka ruzuku kwenye vyuo hivi vya elimu ya kati kwa lengo la kuhakikisha kwamba kwanza tunaenda kushusha zile gharama za uendeshaji au ile gharama ya ada ambayo wanafunzi wanalipa.

Mheshimiwa Spika, eneo la pili, tulilofanya kama Serikali, Serikali tayari imeshafanya mabadiliko ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuhakikisha sasa tunaenda vilevile ku-cover elimu ya kati. Kwa hiyo ile Sheria ya Bodi ya Mikopo nayo tayari tumeshaifanyia marekebisho.

Mheshimiwa Spika, eneo la tatu, Serikali inafanya mapitio ya uwezo wa Bodi ya Mikopo namna gani inaweza kuratibu utoaji wa mikopo katika vyuo hivi vya kati.

Mheshimiwa Spika, eneo la nne kama mkakati Wizara sasa inafanya tathmini ya fani gani ambazo tutaanza nazo kwa ajili ya utoaji wa mikopo katika eneo hili la elimu ya kati.

Mheshimiwa Spika, katika swali la pili, anataka kujua mkakati wa Serikali kuhususha Sekta Binafsi, tayari tumeshaanza majadiliano na Sekta Binafsi ikiwemo mabenki na naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari Benki ya NMB imetoa bilioni 200 kwa ajili ya mikopo hii ya Elimu ya Juu pamoja na kati na tunaendelea na juhudi hizo na wadau wengi wameonyesha nia ya kuunga mkono juhudi za Serikali.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nichukue nafasi hii kuishukuru Serikali kwa majibu mazuri nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ukisoma ripoti ya CAG ya mwaka 2021/2022 utaona kwamba kuna upungufu mkubwa wa upatikanaji wa vitabu mashuleni licha ya kwamba Serikali imepeleka fedha katika wizara husika. Kwa mfano ukiangalia Halmashauri Biharamulo ilikuwa na upungufu wa asilimia 45 katika ripoti ya CAG. Ukiangalia Halmashauri ya Bunda takriban vitabu 194,000 havikuwasilishwa mashuleni pamoja na kwamba Serikali imetoa fedha. Sasa je, Serikali haioni kuna haja ya kuzipatia fedha hizi shule husika ili wao wakagiza moja kwa moja kwa wazabuni badala ya utaratibu uliopo sasa hivi fedha hizi kwenda kwenye wizara ambao umekuwa na mlolongo mkubwa sana?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; uwiano kati ya kitabu na mwanafunzi sasa hivi ni kati ya kitabu kimoja wanafunzi watano tofauti kabisa na malengo ya Serikali moja kwa moja. Je, Serikali ina mpango gani wa dharura hasa katika zile halmashauri za pembezoni kuondokana kadhia hiyo katika hoja ya vitabu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Yahya Ally Mhata Mbunge wa Nanyumbu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwenye majibu yangu ya swali la msingi, kwamba Serikali hainunui vitabu badala yake Serikali kupitia TET inaratibu zoezi zima. Kwanza inatunga, inachapa na baadaye kusambaza. Gharama zinazotumika ni zile za kuhakikisha kwamba vitabu vinatungwa, vinachapwa na baadaye kusambazwa kwenye maeneo mbalimbali. Kwa hiyo naomba nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kuwa zoezi hili kupitia mamlaka yetu ya elimu TET tutaendelea kuliafanya kwa uaminifu na uadilifu mkubwa kwa sababu ni jukumu letu la msingi kuhakikisha kwamba vitabu vinafika shuleni kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili amezunguzia suala la uwiano wa vitabu ni kweli uwiano wa vitabu bado hatujafikia katika ile ratio ya moja kwa moja lakini naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tunaendelea na zoezi hili na hivi sasa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa pale Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa kununua mitambo ambayo yenye uwezo wa kuzalisha vitabu vingi kwa siku ambao utatuhakikishia sasa maene yote ambayo yenye upungufu wa vitabu tunaenda kuwafikia ili kuweza kufikia ile ratio ya moja kwa moja.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo sasa hivi tumeanzisha maktaba mtandao ambayo katika yale maeneo ambayo mtandao upo au TEHAMA ipo vitabu hivi vinaweza kuwa accessed na wanafunzi pamoja na walimu kwa urahisi zaidi.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali bado tabia ya kuvujisha mitihani imeendelea. Ni vipi Serikali inaenda kukomesha tabia hii? Nadhani ndiyo swali langu la msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mara nyingi tumeshuhudia wazazi na watoto wasio na hatia kubebeshwa mzigo wa kufutiwa matokeo na muda mwingine shule kufungwa. Ni kwa namna gani Serikali itaondoa mzigo huu kwa wazazi na watoto wasio na hatia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, Ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Husna Sekiboko, Mbunge wa Viti Maalum, nitajibu maswali mawili yote kwa pamoja kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa suala la uvujaji wa mitihani halipo, mara ya mwisho mitihani ilivuja mwaka 2008 na ulikuwa ni mtihani mmoja wa somo la hisabati Kidato cha Nne. Kutoka mwaka 2008 hakujawahi kutokea uvujaji wa mitihani.

Mheshimiwa Spika, kinachotokea ni udanganyifu katika mitihani kwenye baadhi ya maeneo, kwa sababu suala la mitihani ni suala la mchakato ambayo inahusisha utungaji wa mitihani, ufungaji wa mitihani, usafirishaji wa mitihani lakini baadaye tunakwenda kwenye vituo vya kufanyika mitihani. Kwa hiyo, matukio ya udanganyifu kwenye baadhi tu ya maeneo baada ya mitihani kufunguliwa na kuingia kwenye vyumba vya mitihani, vijana au Walimu au Wasimamizi wamekuwa labda wakiingia na nyaraka ambazo hazitakiwi kwenye ufanyikaji wa mitihani, pale ndipo inatokea udanganyifu wa mitihani. Lakini suala la uvujaji wa mitihani tulishalitokomeza kama Serikali na sasa hivi tunapambana na suala hili la udanganyifu wa mitihani ndipo tunaona kwamba wale wanaohusika kwenye udanganyifu ndiyo wanaochukuliwa hatua.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Naomba kuuliza swali moja la nyongeza. Serikali ina mpango gani wa kuongeza posho kwa usimamizi wa mitihani, kwa sababu zoezi la usimamizi wa mitihani ni gumu wakati mwingine linagharimu ustawi wa maisha ya msimamizi husika?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Maimuna Mtanda Mbunge wa Newala kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge. Hivi sasa taratibu za usahihishaji wa mitihani tunakwenda kubadilika kwa sababu tunakwenda kwenye e-marking. Tumeanza kwa mitihani ya Darasa la Saba na sasa hivi tuko kwenye pilot ya mitihani ya Ualimu na baadae tutakwenda kwenye mitihani ya Form Four na Form Six. Kwa hiyo kwanza tutapunguza sana gharama za Walimu kusogea kwenye maeneo yale ambayo tunasahihisha mitihani badala yake mitihani itakuwa inasahihishwa huko huko Mikoani.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo wakati tunakwenda kuboresha mifumo hii ya usahihishaji wa mitihani vilevile tunakwenda kuboresha na posho zile za wasahihishaji wa mitihani na wale wataokuwa wanasimamia mitihani hii. Kwa hiyo nimwondoe wasiwasi hili tayari liko kwenye bajeti zetu na linakwenda kukaa sawasawa. Nakushukuru sana.
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Je, Serikali inachukua hatua gani ya kudhibiti udanganyifu badala ya kusubiri udanganyifu ndiyo mnatoa adhabu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Maryam kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyozungumza kwenye majibu yangu ya msingi jukumu letu kama Wizara, jukumu letu kama Serikali ni kuhakikisha kwamba tunatoa elimu ya kutosha ya athari za udanganyifu wa mitihani kwa wasimamizi vilevile kwa wale wanafunzi ambao kwa namna moja au nyingine wanaathirika kwa kiasi kikubwa kwenye zoezi hili. Kwa hiyo, jukumu letu ni kuhakikisha kwamba tunatoa elimu watu wasifanye udanganyifu katika mitihani kwa sababu athari zake ni kubwa kwa wao wenyewe binafsi lakini na kwa Taifa kwa ujumla. Nakushukuru sana.
MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Serikali inatumia Polisi kusimamia mitihani ya wanafunzi. Je, haioni kwa kutumia Polisi wanafunzi wanapata taharuki na kushindwa kufanya mitihani yao kwa uhuru? ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Yustina kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge. Polisi hawaendi kusimamia mitihani, kwa sababu hakuna Polisi ambaye anaingia kwenye chumba cha mtihani. Polisi ni sehemu ya kikosi kazi au ni sehemu ya Kamati zetu ambazo zinaratibu pamoja na kuhakikisha kwamba usalama wa kituo cha mtihani pamoja na uhifadhi wa mitihani yetu. Lakini hakuna Polisi ambaye anaingia ndani ya chumba cha mtihani na kuanza ku-invigilate wale wanafunzi wakati wanaendelea na mchakato wa mtihani. Lakini wako pale kwa mujibu wa sheria kuhakikisha kwamba usalama wa kituo pamoja na usalama wa mitihani yetu pale inapohifadhiwa pamoja na ufanyikaji inakwenda sawasawa lakini siyo kuingia ndani ya kituo au darasa ambalo mitihani inafanyika.
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. Suala la uvujaji wa mitihani ni ukosefu wa maadili wa kuanzia anayeandaa, mratibu na anayesimamia. Sasa nataka kujua mkakati wa Serikali ambao unaenda kusaidia suala hili la ukosefu wa maadili ni upi? ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Sima kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye majibu yangu ya swali la msingi kwamba uvujaji wa mitihani kwa mara ya mwisho ulitokea mwaka 2008. Na kama alivyozungumza Mheshimiwa Mbunge kwamba suala hili ni suala la kimaadili na sisi kama Serikali wajibu wetu ni kuhakikisha kwamba tunakwenda kutoa elimu kuanzia kwa wale ambao wanaotunga mitihani vilevile wale wanaofunga, wanaosafirisha mpaka wale ambao wanakwenda kusimamia zoezi hili la ufanyikaji wa mitihani.

Kwa hiyo tunafahamu ni suala la kimaadili na tumekuwa tukitoa mavunzo ya athari za uvujaji wa mitihani kwa namna moja au nyingine, lakini nimwondoe wasiwasi kwa kiasi kikubwa na kama tukichukua takwimu kwa mara ya mwisho tukizungumza hilo suala la udanganyifu tu mwaka 2011 udanganyifu ulifanyika kwa wanafunzi 9, 736.

Mheshimiwa Spika, lakini mwaka 2021 ni wanafunzi 393 tu ndio ambao walifanya udanganyifu kwenye mitihani. Kwa hiyo tunaendelea kudhibiti na tunaamini baada ya muda si mrefu tunaweza tukapata achievement kubwa kuhakikisha kwamba hakuna mtu ambaye atajihusisha na udanganyifu wa mitihani.
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakshukuru. Je, udahili wa wanafunzi kuingia VETA mpya iliyojengwa Wilayani Longido Mkoa wa Arusha unaanza lini?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vyuo 25 vya Wilaya, vile ambavyo tulijenga katika mwaka uliopita wa fedha, ambapo ukamilishaji wake hivi sasa ndio tunakwenda kukamilisha, tunatarajia udahili ule wa kozi zile za muda mrefu kuanza mwezi wa Kumi mwaka huu, ila zile kozi za muda mfupi muda wowote kuanzia mwezi wa Sita zinaweza zikaanza rasmi.
MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa kila Wilaya imeandikiwa kupata chuo cha VETA. Je, ni lini Serikali itaboresha chuo cha VETA Buhongwa ili kiwe na hadhi ya chuo cha VETA katika Wilaya ya Nyamagana?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Matondo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni azma ya Serikali kuhakikisha kwanza tunakwenda kujenga kwenye maeneo ambayo hayana huduma au hayana vyuo hivyo, lakini kwenye maeneo ambayo vyuo tayari vipo ni azma vilevile ya Serikali kuhakikisha kwamba, vyuo vile tunakwenda kuviboresha kwa maana ya kufanya ukarabati lakini vilevile kuongeza miundombinu. Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu, kwamba Serikali inaandaa bajeti kila mwaka ile ya kufanya maendelezo kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo na chuo hiki ambacho amekitaja Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi.

Kwa kuwa, Serikali yetu na nchi yetu inajikita zaidi katika matumizi ya teknolojia na TEHAMA. Je, Serikali ni lini itaona ni wakati muafaka wa kuongeza masomo haya ya sayansi ikiwemo hisabati kwa wanafunzi wanaofanya masomo ya HGKL. Ni ni lini ili kuwafanya watu hawa wawe tayari katika soko la ulimwengu na Tanzania?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Asha Mshua kama ifuatavyo: -

Mhehsimiwa Mwenyekiti, masomo ya hisabati pamoja na teknolojia tayari yapo kwenye mitaala yetu lakini naomba tu nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, hivi sasa tunafanya mapitio ya mitaala katika ngazi zote za elimu ambapo tutazingatia hasahasa kwenye maeneo haya ya sayansi pamoja na teknolojia na tunaamini kabisa kwa mwendo huo tunaokwenda nao swali lake litakuwa limepata majibu ya jumla na ya moja kwa moja.
MHE. SYLVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu suala la elimu ni suala nyeti katika Taifa letu, ni muda sasa Serikali imesema ipo kwenye mchakato wa mapitio na watoto wetu wanaendelea kutumia mtaala huu ambao hauna tija kwao. Ni lini hasa utekelezaji utaanza rasmi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, vijana wengi wameathiriwa na mfumo huu ambao hauna tija, wengi wapo mtaani na wanashindwa afanye nini kwa elimu walioipata. Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kuwasaidia vijana hawa ambao tayari ni wahanga wa mfumo wetu huu wa elimu pale tutakapobadilisha mfumo rasmi. Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Sylvia, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu ya swali la msingi kwamba kwa upande wa upitiaji wa mitaala Serikali tayari tumekamilisha rasimu ya mitaala pamoja na sera yetu, hivi sasa tupo katika hatua za kurudisha tena kwa wadau lakini vilevile katika mamlaka mbalimbali ambazo zitathibitisha au zita- approve mitaala hiyo. Mara tu mchakato huo utakapokuwa umekamilika tunataraji mitaala hii itaanza kutumika rasmi kwenye ngazi zote za elimu hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye swali lake la pili, anazungumzia kwamba tayari kuna wananfunzi ambao walitumia mitaala ile ya zamani. Naomba nimuhakiishie tu Mheshimiwa Mbunge, utaratibu wa upitiaji wa mitaala pamoja na sera ni suala endelevu ni suala ambalo linatokea mara kwa mara pale tunapoona tu kuna mahitajji ya mabadiliko ya mitaala pamoja na sera, Serikali imekua ikifanya hivyo ili elimu inayotolewa ilingane au iendane na mazingira halisi ya kazi au mazingira halisi ya dunia inavyokwenda. Vilevile utaratibu wetu au sera yetu ya elimu inampa wasaha yule mhitimu kuweza kujiendeleza au kwenda maeneo mengine na kupata elimu zaidi ambayo itaendana na mazingira yale ambayo anafanyia kazi. Ninakushukuru sana.
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, kwa kuwa kumekuwepo na changamoto katika Shule za Msingi na Sekondari kwa ajili ya watoto kupata chakula shuleni. Nini kauli ya Serikali kuhusu watoto kupata chakula shuleni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba watoto wanakuwa kwenye ufanisi mzuri kiakili na kimwili?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli suala la chakula shuleni kwa watoto ni jambo ambalo ni muhimu, bado kuna changamoto kubwa sana ya upatikanaji chakula mashuleni kwa ajili ya watoto wetu. Serikali tulishatoa mwongozo wa namna gani wazazi au walezi wanaweza kushirikiana na Serikali kuhakikisha kwamba watoto wetu wanapata chakula shuleni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia mwongozo ule unadadavua na unatoa maelekezo mazuri kabisa kwamba kila upande ni namna gani unaweza kushiriki ili wanafunzi wetu waweze kupata chakula wanapokuwa shuleni. Nakushukuru sana.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu lakini vitendo vya ubakaji na ulawiti wa watoto wadogo ni vitendo ambavyo vimekithiri katika nchi yetu na moja ya sheria ni kufungwa kifungo cha miaka 30 jela. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka kwa sababu ubakaji ni uuaji, kuleta mabadiliko ya sheria ili wabakaji na walawiti wa watoto waweze kuhukumiwa kifungo cha kifo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mnzava kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli anayozungumza Mheshimiwa Mbunge kwamba imekuwepo sheria ya miaka
30 lakini inaonekanika kama ni sheria legevu kidogo naye Mheshimiwa Mbunge anatoa mawazo, anatoa mapendekezo kwa nini isiwepo adhabu hiyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba tubebe mawazo yake hayo twende tukayafanyie tathmini tuweze kuangalia namna gani sheria hiyo inaweza kubadilishwa.
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kwamba Majimbo ya Vijijini yana maeneo makubwa sana ya kiutawala lakini yana mahitaji makubwa ya elimu ya VETA.

Je, Serikali haioni sababu ya kuowandolea adha wananchi wa vijijini kutafuta elimu hii kwa umbali mrefu?

Mheshimiwa Spika, kutokana na hoja za swali nililouliza hapo juu, Serikali ni lini itajenga chuo cha VETA angalau kimoja kwenye Jimbo la Lulindi.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ally Mchungahela kwa pamoja kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, lengo la ujenzi wa vyuo hivi katika ngazi za Wilaya ni kusogeza huduma hizi karibu kule Wilaya. Tunafahamu kweli zipo Wilaya ambazo zina maeneo makubwa ya kiutawala, lakini naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba wakati tunajenga vyuo hivi, tunaweka vilevile na huduma ya mabweni. Lengo la huduma za mabweni ni kuhakikisha wanafunzi wote ambao wanatoka mbali kuweza kukaa pale pale chuoni na kuweza kupata huduma hii kwa karibu zaidi. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi, bado tunaweza tukawahudumia wale ambao wametoka mbali kwa sababu watakuwa wanakaa pale pale chuoni.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili, anazungumzia suala la ujenzi kama nilivyoeleza kwenye majibu yangu ya swali la msingi, kwamba kwa sasa tunakamilisha kwanza ujenzi wa vyuo hivi katika wilaya hizi, halafu tutaangalia sasa yale majimbo yenye changamoto ikiwemo labda na jimbo lake pamoja na Jimbo la Nanyamba kule nako kuna malalamiko makubwa sana. Hii itategemea sasa vile vile na upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, ahsante nakushukuru. Serikali mwaka 2021 iliahidi kujenga Chuo cha VETA katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara Kata ya Kisawasawa. Sasa hivi tunapewa taarifa kwamba chuo hakitajengwa katika Halmashauri hiyo kwa sababu kuna Chuo cha Ufundi cha FDC. Chuo kinaenda kujengwa katika Halmasahuri ya Mlimba: -

Mheshimiwa Spika, nataka kujua: Je, kuwepo kwa Chuo cha Ufundi cha FDC ni sababu ya kukosa vyuo vya VETA? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Asenga, Mbunge wa Ifakara, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwenye majibu ya swali la msingi, vyuo hivi tunajenga katika ngazi ya Wilaya, havijengwi katika ngazi ya Halmashari. Ni jukumu la Wilaya kuangalia kwamba vinakwenda kujengwa wapi? Kwa zile Wilaya ambazo zina Halmashauri zaidi ya moja, ni lazima wakae chini Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi ili waweze kuamua wapi chuo hiki kinakwenda kujengwa? Kwa hiyo, sisi jukumu letu ni kwenda kujenga Chuo cha VETA lakini majukumu au wajibu wa kuchagua eneo gani la kwenda kujenga linabakia katika Wilaya husika.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kwamba Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa VETA Wilaya 63 na Wilaya ya Nyang’hwale tayari upembuzi yakinifu umeshafanyika; je, katika Wilaya 63 na Nyang’hwale ikiwemo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Hussein Amar, Mbunge wa Nyang’hwale, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwamba vyuo hivi vinaenda kujengwa kwenye Wilaya na kama tayari tumeshafanya upembuzi yakinifu, tafsiri yake ni kwamba tumeshakuja kufanya Geotechnical Survey, Topographical Survey pamoja na Environmental and Social Impact Assessment. Kama shughuli zozote zimeshafanyika kwenye eneo lako, is likely kwamba chuo hicho kinakuja kujengwa kwenye eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ujenzi wa Chuo cha VETA Chemba umekamilika, nataka kujua ni lini sasa kitafunguliwa ili kidahili wanafunzi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mohamed Monni, Mbunge wa Chemba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli ujenzi wa vyuo 25 vile vya Wilaya awamu ya kwanza pamoja na vinne vya Mikoa, tayari ujenzi umekamilika. Jukumu letu tulilonalo sasa hivi ni utafutaji wa vifaa na kuajiri walimu kwa ajili ya kwenda kufundisha kwenye maeneo hayo. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, mwaka ujao wa fedha kuanzia mwezi Julai tutaanza kutoa kozi za muda mfupi lakini kuanzia Mwezi wa Kumi tutafanya usahili sasa kwa ajili ya kozi za muda mrefu sambamba na upelekaji wa vifaa vya kufundishia kwenye maeneo hayo kwa sababu samani tayari tumeshapeleka.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Wilaya ya Liwale iliahidiwa kujengewa Chuo cha VETA kwenye bajeti hii inayotekelezwa sasa. Mpaka leo hii imebakia miezi miwili bajeti inakwenda kwisha: Je, lini tutapewa fedha hizi tuweze kujenga chuo hicho?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kuchauka, Mbunge wa Liwale, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tayari tumeshapeleka fedha za awali kwa ajili ya mobilization na zile kazi za mwanzo; na kazi nyingine za Geotechnical Survey, Topographical pamoja na ESIA (Environmental and Social Impact Assessment) tayari zimeshafanyika. Kwa hiyo, hivi sasa tunachokamilisha ni kupata matokeo ya tafiti hizi tulizokwenda kufanya. Baada ya matokeo hayo, tayari tutapeleka fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa maeneo yote yale 63 tuliyoyataja.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Halmashauri yangu ya Nanyumbu imepokea fedha za ujenzi wa Chuo cha VETA, lakini cha kushangaza fedha hizi zimekabidhiwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ambayo ipo kilometa 90 kutoka wilayani kwangu: Kwa nini fedha hizi zimepelekwa Masasi wakati Nanyumbu yupo mdhibiti ubora ambaye angesimamia fedha hizi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Yahya Mhata, Mbunge wa Nanyumbu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kweli fedha tumepeleka katika FDC ya Masasi na hatukupeleka kwenye Wilaya ya Nanyumbu moja kwa moja kwa sababu FDC Masasi ndipo ambapo fedha tutazipitishia pale. Tumeona ni muhimu kupitishia hizo pesa pale baada ya kufanya study ile ya ujenzi awamu ya kwanza; Vyuo vyote vya FDC wamesimamia vizuri zaidi vile vyuo vya VETA kuliko zile ofisi zetu za wadhibiti ubora. Kwa hiyo, tumepitisha kule kwa sababu ya kupata usimamizi makini kwa chuo chetu kile na matumizi ya fedha yaweze kuwa sahihi.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kama alivyozungumza kwenye majibu yake Mheshimiwa Naibu Waziri kwa suala la FDC na VETA, kwamba lengo ni kupeleka katika kila Wilaya.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri haona sasa wakati umefika wa ku-engage TAMISEMI katika mlolongo huu wa kwenda kusimamia ili hivi vyuo kuwa endelevu? Serikali haioni wakati umefika wa kumshirikisha TAMISEMI katika usimamizi wa hivi vyuo vya ufundi? Nashukuru.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Londo, Mbunge wa Mikumi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ametoa ushauri wa kwamba tushirikiane, lakini tumekuwa tukishirikiana kwenye eneo hili la utoaji wa elimu kuanzia shule hizi za msingi, sekondari mpaka vyuo. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi kwamba ushirikiano upo, lakini kwa vile ametoa ushauri, ushauri huo tumeuchukua tunaenda kuufanyia kazi. Kwa maana ya ushirikiano, bado tunaendelea kushirikiana na TAMISEMI kwa sababu vyuo hivi viko kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Swali langu kwa Mheshimiwa Waziri ni moja tu kwamba: Kwa kuwa mnakwenda kujenga sasa vyuo kwa wilaya zote, ina maana ya mahitaji ya walimu wa ufundi yanakwenda kuongezeka: Mna mpango gani maalum kama Wizara wa kuzalisha walimu wa kwenda kufundisha elimu ya ufundi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Nyongo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli ujenzi wa vyuo hivi; vile 25 na hivi 63 na hivi vya mikoa unakwenda kuongeza uhitaji wa walimu kwenye eneo hili. Naomba nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, kwanza tuna chuo chetu ambacho kinafundisha walimu wa masuala haya atakayekwenda kufundisha maeneo haya ya vyuo vya ufundi pale Morogoro. Vile vile, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Nyongo, tunakwenda kufanya maboresho ya mitaala pamoja na sera yetu ya elimu. Tutakwenda ku-convert vyuo vyetu vile vya ualimu tulivyokunavyo zaidi ya 35 ili tuingize component au kada ya ufundi mle ndani ili tuweze kupata hiyo supply ya walimu kwenye maeneo haya.

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie vile vile Mheshimiwa Nyongo kwamba, Mheshimiwa Rais tayari alishatoa kibali cha kuajiri watumishi au walimu zaidi ya 571, ambao tunaendelea na mchakato na mpaka kufika sasa walimu 171 tayari tumeshaajiri kwa ajili kuanza kutoa mafunzo kwenye vyuo 25 ambavyo ujenzi wake umekamilika.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. KHALIFA MOHAMED ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Pamoja na mikakati ya Serikali ambayo imeianisha lakini bado kuna changamoto ya ufaulu hasa katika masomo ya sayansi na hisabati. Ni nini mkakati wa Serikali kupandisha ufaulu huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, najua kuna mchakato unaendelea wa kuiangalia mitaala. Je, ni lini hiyo mitaala mipya itatumika katika sehemu zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Khalifa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza, anataka kufahamu juu ya mkakati wa Serikali hasa hasa katika masomo ya hisabati na sayansi. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, Serikali tumejipanga vizuri kwa kufanya mambo yafuatayo: -

(i) Kuweka kipaumbele hasa hasa kwenye ajira za walimu wa masomo haya ya sayansi pamoja na hisabati;

(ii) Kuhakikisha kwamba tunakwenda kujenga maabara katika shule zetu ambazo zinazotoa masomo haya ya sayansi;

(iii) Kuhakikisha kwamba tunapeleka vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa ajili ya ufundishaji wa masomo haya; na

(iv) Kuendelea kuhakikisha walimu wale wa masomo ya sayansi basi tunawapeleka kwenye mafunzo ili kuhakikisha kuwajengea uwezo wa kuweza kufundisha masomo haya kwa umahiri, kwa umahiri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili anataka kufahamu utaratibu wa mitaala. Ni kweli tumezungumza hapa kwamba tunaendelea na uratibu pamoja na maboresho ya mtaala wa mwaka 2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge pamoja na Bunge lako Tukufu, mitaala yetu pamoja na sera tayari tuna rasimu ya nyaraka hizo na hivi sasa taratibu zinazoendelea ni kuendelea kupata maoni ya wadau ikiwemo na ninyi Waheshimiwa Wabunge. Tutaleta rasimu hiyo katika Bunge lako Tukufu ili kuweza kupata ridhaa na baadaye kwenda kwenda kwenye mamlaka zinazohusika na ithibati au kupitisha mitaala hii pamoja na sera ili iweze kuanza kutumika. Kwa hiyo, mara baada ya mchakato huu kukamilika, mitaala hii itaanza kutumika rasmi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. JUSTINE L. NYAMOGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, Ujenzi wa chuo hiki pamoja na kwamba umefikia hatua hizo lakini kuna shida ya huduma ya maji na gharama yake ni shilingi milioni 90. Je, ni lini Wizara itapeleka fedha milioni 90 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa chuo hicho na ili huduma ziweze kutolewa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; tunaishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya kujenga chuo katika Wilaya ya Kilolo. Je, ni lini ujenzi huo utaanza katika Wilaya ya Kilolo ili wananchi waweze kunufaika na huduma za chuo cha VETA.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Justin Nyamoga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza anataka kufahamu swala la maji katika Chuo cha Ngudu. Ni kweli tumepeleka fedha kwa ajili ya ukamilishaji kwa maana ya majengo lakini kwa maana ya uunganishwaji wa maji bajeti ile iliyokuja baada ya kuifanyia tathmini tuliona kwamba iko kubwa sana, ilikuwa inflated kwa kiasi kikubwa. Kwa hiyo, tumeifanyia maboresho na sasa fedha zimekuja kama milioni 57 hivi kipindi kifupi kijacho tutapeleka fedha hiyo kwa ajili ya ukatishaji wa maji katika eneo lile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika swali lake la pili anataka kufahamu ujenzi wa chuo cha VETA Kilolo. Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge tayari timu ya wataalam imeshafika Kilolo na tumeshafanya topographical survey, geotechnical survey pamoja na environmental and social impact assessment na baada sasa ya matokeo haya ya vipimo hivi tutakwenda kuanza ujenzi mara moja, nakushukuru sana.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Waziri, Wilaya ya Busekelo tunaomba sana Serikali itujengee chuo cha VETA na Mheshimiwa Mbunge yuko tayari kusaidia kupata eneo kwa ajili ya kujenga chuo hiko. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa vyuo vya VETA unajengwa katika kila wilaya na wilaya zote zilizobaki ambazo hazina vyuo vya VETA katika kipindi hiki cha 2023/2024, tunakwenda kujenga katika wilaya zote zilizobaki. Kwa hiyo, kama Busekelo ni wilaya ambayo haikuwa na chuo cha VETA nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge tunakwenda kufanya kazi hiyo haraka iwezekanavyo. (Makofi)
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Je, ni lini Chuo cha VETA kilichojengwa Wilayani Lushoto Eneo la Mlola kitaanza udahili?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shekilindi, Mbunge wa Lushoto, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Chuo cha VETA Lushoto ni miongoni mwa vile vyuo 25 vya awamu ya kwanza, ambapo ujenzi wake umeshakamilika kwa asilimia 100. Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kama nilivyokwishajibu kwenye majibu ya swali la msingi vyuo hivi vyote 25 vya awamu ya kwanza, tunapeleka samani, vifaa vya kufundishia pamoja na kuandaa rasilimali watu. Ni matumaini yetu katika mwaka wa fedha 2023/2024 vyuo hivi vyote 25 vya wilaya na vile vinne vya mikoa vinaenda kuanza kutoa mafunzo rasmi.
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Wilaya ya Kigamboni katika Hotuba ya Bajeti ya Mwaka jana ilitajwa kwamba ni moja ya wilaya ambayo mtakwenda kujenga chuo cha VETA na imebakia miwezi miwili. Ni lini sasa ujenzi ule utaanza ili wananchi wa kigamboni waweze kunufaika na chuo hicho?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Kigamboni ni miongoni mwa wilaya 64 zilizobaki katika ujenzi wa vyuo 64 zilizobaki. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba geotechnical survey, topographical survey, environmental impact assessment tayari tumeshafanya. Tunasubiri majibu kwa maana ya results ya tafiti hizo na baada tu ya majibu hayo, tunaenda kuanza ujenzi katika mwaka huu wa fedha, nimuondoe wasiwasi kazi hiyo inakwenda kufanyika.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naipongeza Serikali kwa kujenga vyuo vya VETA lakini kwenye vyuo hivi vingi vya VETA vilivyopita, masomo yanayotolewa mengi hayana soko kubwa kwenye ajira ya sasa lakini kuna masoma kama ufundi bomba, ufundi umeme wa magari, umeme wa majumbani unakuta kozi nyingi hazipo kwenye vyuo vya VETA mathalani Makete. Ni lini Serikali itaanza kuongeza masomo hayo ambayo yanaajira nyingi kwa vijana wetu ili waweze kupata kusoma?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Sanga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimejibu katika swali nadhani namba 96 la kuhusiana na suala la upitiaji wa mitaala. Tumeanza upitiaji wa mitaala katika elimu yetu ya msingi lakini tunafanya mapitio ya mitaala katika elimu ya sekondari, vyuo vya ualimu, vyuo vikuu pamoja na vyuo vya VETA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mapitio hayo ya mitaala vile vile katika maeneo haya ya vyuo vya VETA tunakwenda kuongeza idadi ya masomo lakini vile vile kufanya review ya hata hayo masomo yote tunayoyatoa kuhakikisha kwamba tunakwenda kweli kujibu changamoto za wananchi zile ambazo katika maeneo yao ambao wanahitaji.
MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza niwapongeze Serikali kwa kuchukua mikakati hii maalum kwa ajili ya kuwalinda watoto wetu. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali langu la kwanza, Je, ni hatua gani watachukuliwa ambao hawatatekeleza agizo hilo ama maelekezo hayo ya Serikali?

Swali langu la pili, kutokana na hali ilivyo sasa hivi hapa nchini kwetu na harakati ambazo wazazi na walezi tunazo, kuna umuhimu wa wale wasaidizi wetu ambao wanaishi na watoto wetu majumbani, kuwa na elimu ya ulezi wa Watoto. Mambo haya tayari yanafanyika duniani, ukienda Bara la Amerika yapo, ukienda Bara la Asia yapo, ukienda Bara la Ulaya pia yapo pia na Bara la Afrika kwa mfano, nchi za ya South Africa tayari wana training za child care kwa ajili ya kuwalinda watoto wetu waweze kupata malezi bora.

Je, ni lini Serikali itaanzisha vitengo hivi maalum, hata kama ikiwa ni VETA kuwafundisha wale Dada zetu wanaotoka maeneo mbalimbali ya Tanzania wanaokuja kufanya kazi majumbani ili waweze kupata hiyo training kwa ajili ya kuwalea watoto wetu kwa malezi yanayostahiki? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Najma Giga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza anataka kufahamu mkakati na hatua za Serikali itakazochukua kwa wale ambao watapinga utekelezaji wa waraka huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu, Serikali inaendesha taratibu zake kwa mujibu wa kanuni, sheria, taratibu na miongozo, kwa yule atakayekaidi au kupinga au kwa namna yoyote ile akakataa kutekeleza, basi sheria, kanuni na taratibu ndizo ambazo tutakazotumia kuhakikisha kwamba waraka huu unatekelezwa ili mambo yote yakae sawasawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili, anataka kufahamu mkakati wa Serikali juu ya namna gani tunafanya kwa wale wahudumu wa majumbani. Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu Wizara ya Elimu kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi - VETA tumeanzisha kozi mbalimbali, sasa hivi tumeanza na hizi kozi za housekeeping ambazo zinafundisha hawa wahudumu wa majumbani au house girl na ma-house boy.

Naomba tuchukue ushauri huu wa Mheshimiwa Mbunge ni ushauri mzuri tuende tukaufanyie kazi tuweze kuangalia namna bora ya kuweza vilevile kuingiza kozi hii ya child care training kwa wale wahudumu wa majumbani. Ninakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, tunaishukuru Serikali walau Wilaya ya Kilombero sasa inapata chou cha VETA. Swali la kwanza, mtalifanyia nini eneo Kata ya Kisawasawa mlilopewa na wananchi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, maana wataalam wameshaenda na wameshalichukua hilo eneo?

Swali la pili, kule shamba Nakaguru Mchombe ambako mnakwenda kujenga hicho chuo cha VETA hakuna hata barabara, na fedha milioni 45 ni ndogo sana. Je, ni lini fedha zingine zitaongezwa?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asenga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwisha eleza kwenye majibu ya swali la msingi, wajibu wa kutambua au kuamua ni eneo gani chuo kiende kujengwa ni mamlaka za wilaya pamoja na mikoa. Kwa hiyo nimwondoe wasiwasi kwanza Mheshimmiwa Asenga na Bunge lako Tukufu, kwamba eneo hili la Kisawasawa alilolitaja ambalo labda lilitengwa awali na mamlaka za wilaya au na mkoa na kukabidhiwa Wizara ya Elimu nimwondoe shaka na wasiwasi, Serikali bado ina mipango mingi na mikubwa eneo hili bado tuna uhitaji nalo na tutapanga utaratibu mwingine na miradi mingine ya kimaendeleo inaweza kupelekwa katika eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili, kwamba fedha iliyopelekwa ni ndogo ni kweli, tumepeleka fedha milioni 45 kwa ajili ya kazi zile za awali ambayo ilikuwa ni masuala ya geotechnical survey, topographical survey pamoja na environmental and social impact assessment. Hivi sasa tayari fedha kwa ajili ya kazi zile za substructure pamoja na superstructure ela zake tayari tumeshazipata. Nadhani ndani ya wiki hii au wiki ijayo fedha hizo zitakwenda kule kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi huo wa majengo yale tisa kama tulivyoweka kwenye mpango wetu.
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Je, ni lini Serikali itakikarabati Chuo cha Ufundi Music ambacho kiko Korogwe ambacho ni kikongwe na kimechakaa sana?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Timotheo Paul Mnzava Mbunge wa Korogwe kama ifuatavyo:
-

Mheshimiwa Spika, tunafahamu uwepo wa chuo hiki cha FDC pale Korogwe, na katika nchi yetu tuna vyuo 54 vya FDC ambavyo vingi sana ni vya muda mrefu. Tumeanza kufanya ukarabati tangu mwaka 2020/2021 katika bajeti ile na tumeweza kuvikia vyuo 35 kufanya ukarabati pamoja na upanuzi. Nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, katika bajeti yetu hii ya 2023/2024 tunakwenda kuvifikia vyuo 21 vilivyobaki kikiwemo na hiki cha Korogwe.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Chuo cha VETA Nyasa kina course mojawapo ambayo ni ya udereva lakini chuo hicho hakina gari kabisa ikiwemo ya utawala.

Je, nini mpango wa Serikali kukisaidia chuo hicho?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Manyanya Mbunge wa Nyasa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika bajeti yetu ya mwaka huu 2023 tuliweka azma ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia pamoja na samani kwa ajili ya vile vyuo 25 vya Wilaya vipya pamoja na vyuo vine vya mikoa. Nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Manyanya, katika bajeti yetu ijayo ya 2023/2024 tutaendelea kuweka bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vifaa ikiwemo na magari ya kufundishia pamoja na vifaa mbalimbali vya kujifunzia kwa ajili ya vyuo vyetu vile vya zamani lakini pamoja na hivi vipya.
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona. Jimbo la Kilwa kusini halina chuo cha VETA na hakuna mpango wowowte wa Serikali kujenga chuo hicho isipokuwa tuna Chuo cha Maendeleo ya Wananchi pale Kilwa Masoko ambapo miundo mbinu yake ni ya muda mrefu na imechakaa. Sasa hivi kipaumbele chetu ni kujenga bwalo na tulishaomba.

Je, lini Serikali italeta fedha hizi kwa ajili ya ujenzi wa bwalo pale chuo cha wananchi Kilwamasoko?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kassinge Mbunge wa Kilwa Kusini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Kama nilivyokwisha eleza kwamba mpango wa Serikali ni ujenzi wa vyuo 64 katika wilaya ambazo hazina, miongoni mwa Wilaya hizo ni pamoja na Wilaya ya Kilwa. Sasa utaratibu gani wa eneo gani linakwenda kujengwa, aidha ni Kilwa Kusini au ni Kilwa Kaskazini ni maamuzi ya Wilaya au Mkoa wa Lindi kuamua chuo hicho kinakwenda kujengwa wapi. Tunatambua uwepo wa Chuo cha FDC pale kulwa Kusini na mimi nakifahamu chuo hiki na tunajua kwamba tunauhitaji wa bwalo pamoja na baadhi ya mabweni. Kama nilivyosema kwa upande wa Korogwe katika mwaka ujao wa fedha tutatenga fedha kwa ajili ya kufanya ukarabati wa vyuo vile, kuongeza miundombinu ya mabweni pamoja na mabwalo, kama alivyoomba Mheshimiwa Mbunge. Kwa hiyo nimwondoe wasiwasi katika bajeti ijayo mambo mazuri yanakuja.
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.

Je, ni lini Serikali itajenga karakana ngumu na mabweni katika Chuo cha VETA kilichopo Kitangali ili kuwezesha vija wengi kupata mafunzo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Hokororo Mbunge wa Viti Maalumu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli na mimi nilishawahi kufika pale Kitangali, majengo yale yaliyokuwepo ni machache. Nakumbuka tuliweka kwenye bajeti yetu ya mwaka huu kwamba tuongeze majengo, madarasa na karakana katika Chuo kile cha Kitangali. Namwomba Mheshimiwa Hokororo mara tu baada ya kipindi hiki cha maswali tuweze kuonana tuweze kuangalia kwa nini fedha zile zaidi ya milioni 200 ambazo tulizitenga katika bajeti yetu ya mwaka huu kwa ajili ya kwenda kuongeza miundombinu katika chuo kile cha Kitangali kama hazijakwenda tuweze kuzipeleka kwa haraka.
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa swali la nyongeza. Chuo cha VETA Ulyankulu kimechaka sana na hakina majengo ya kutosha, lakini 2020/2022 kilitengewa bajeti ya shilingi milioni 638; fedha zile zilichukuliwa zikarudishwa Wizarani.

Je, Serikali iko tayari sasa kuzirudisha zile milioni 638 kwa ajili ya kufanya ukarabati wa chuo changu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rehema Juma Migilla, sina taarifa kamili ya fedha hizi labda baada ya kipindi hiki tuweze kuonana na Mheshimiwa Mbunge.
MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mimi ningependa nimuulize swali dogo la nyongeza Mheshimiwa Waziri. Campus ya Marine Science ambayo iko Zanzibar nayo imekuwa na uhaba wa madarasa;

Je, nayo imo katika mpango wa vile vyuo 21 vitakavyopata matengenezo makubwa?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Chimboni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, vyuo 64 tunavyo vizungumza hapa ni kwa upande wa Tanzania bara. Kwa upande wa Tanzania Zanzibar tuna utaratibu maalum ambao tunautumia tukishirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar. Kwa hiyo kwa upande wa ukarabati wakule bajeti itatengwa kwenye Wizara ile ili kuhakikisha maeneo yale ambayo yanahusika na vyuo vya ufundi kwa upande wa Zanzibar yanakwenda kushughurikiwa.
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kama ifuatavyo: -

Pamoja na kuishukuru Serikali kwa kutuanzishia VETA wilayani Irambo, je, ni lini Serikali itatuongezea majengo ili tupate mafunzo ambayo hatuyapati kutokana na uhaba wa majengo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta Mbunge wa Urambo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, vyuo hivi vya zamani viko zaidi ya vyuo 44, na ni kweli kabisa vina uhitaji mkubwa wa majengo, vifaa vya kufundishia pamoja na rasilimali watu. Nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kama nilivyokwisha kujibu maswali yaliyotangulia. Kwa upande wa pale Urambo tunajua kwamba chuo kile kina majengo machache ikiwemo na uhaba wa karakana pamoja na mabweni. Katika bajeti yetu ijayo tutahakikisha kwamba tunatenga fedha ili kuongeza miundombinu hiyo ya maabara, karakana pamoja na mabweni kwa ajili ya Chuo chetu cha Urambo. Kwa hiyo tuwasilinae tu Mheshimiwa Sitta ili tuliweke vizuri hili, nakushukuru sana.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Miongoni mwa Wilaya ambazo hatuna chuo kipya cha VETA ni pamoja na Wilaya ya Bunda;

Je, ni lini sasa Serikali mtatujengea Chuo cha VETA katika Wilaya ya Bunda ili vijana wetu waweze kupata ujuzi na kujiajiri wenyewe?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Bulaya Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwisha eleza kwenye majibu ya swali la msingi, katika mwaka wa fedha 2022/2023, yaani huu tunao endelea nao, tunawilaya 64 na mkoa mmoja ambao hauna chuo cha VETA Mkoa huo ni wa Songwe. Wilaya hizi 64 miongoni mwa Wilaya ya Bunda. Kwa hiyo nikuondoe wasiwasi, katika Mkoa wa Mara tuna wilaya nne ambazo ni Serengeti, Bunda, Tarime, ndizo wilaya ambazo hazina vyuo vya VETA. Katika mwaka huu tayari tumeshapeleka fedha zile za awali na sasa tuna peleka fedha awamu ya pili kwa ajili ya kuanza ujenzi rasmi ikiwemo na chuo hiki cha Wilaya ya Bunda. Kwa hiyo nenda kawaambie wananchi Serikali ya Mama Samia iko kazini inawatendea haki wana Bunda.
MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu ya Serikali, aidha nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, wahitimu wengi wa elimu ya juu wanategemea sana kuajiriwa tofauti na wahitimu wa kada ya kati ambao wanaweza kujiajiri wao wenyewe. Ukweli ni kwamba ajira hazitoshelezi kuajiri wahitimu wote.

Je, Serikali haioni haja ya kuwawezesha wanafunzi wa kada ya kati waweze kupatiwa mikopo ya kugharamia elimu yao kama vile wanavyopatiwa wanafunzi wa elimu ya juu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; Je, Serikali inamkakati gani wa kuboresha mitaala ya elimu ili kuweze kuwa na mafunzo ya msingi ya kuanzisha na kuendeleza biashara ili hawa wahitimu wa elimu ya juu watakapokosa ajira basi waweze kujiajiri wao wenyewe? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Katimba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye majibu ya msingi, upande wa utoaji wa mikopo nimesema kwamba Serikali inaendelea kujipanga lakini nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, wenzetu wa Benki ya NMB tayari imeshaanza utaratibu huo wa utoaji wa mikopo kwa upande wa elimu ya kati ambapo kwa mwaka huu wa fedha imeweza kutenga zaidi ya shilingi bilioni 200 kwa ajili ya utoaji wa mikopo, nasi kama Serikali tunaendelea na uratibu wa jambo hili ili tuweze kuangalia uwezekano wa kutoa mikopo hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwamba Serikali inatoa ruzuku ya kutosha kabisa kwa sababu kwenye vyuo vyetu vya kati wanafunzi hawa kila mwanafunzi mmoja anagharamiwa zaidi ya shilingi milioni moja kwa mwaka kwa ajili ya kusaidia vilevile na kupunguza gharama za ada.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili anataka kufahamu mikakati ya Serikali juu ya maboresho ya mitaala pamoja na sera. Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge tunaendelea na utaratibu wa maboresho wa sera pamoja na mitaala, tumeshapata rasimu ya kwanza ya maboresho hayo na miongoni mwa maeneo ambayo tumeyatilia mkazo sana ni katika stadi za fedha pamoja na biashara ili wanafunzi wetu watakapotoka katika vyuo hivi aidha waweze kujiajiri au kuajiriwa.
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri nikupongeze yaani kwa hilo kwa leo nikupongeze, lakini nina swali moja tu la nyongeza. Chuo cha Dodoma ambacho ni kikubwa Afrika Mashariki, na ni kikubwa kweli, kina pia hizo kozi; na kwa hiyo katika kuendelea kufata hizi Sera za Kimataifa, je, Serikali ni lini itaanza kujenga sasa maana yake mmesema vyuo vingine vitajengwa lakini kwa Chuo hiki cha UDOM ni lini chuo hicho mtaanza kujenga teaching hospital?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKINOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Thea Ntara, Mbunge wa Viti Maalumu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nishukuru kwa pongezi alizotoa Mheshimiwa Mbunge na pongezi hizi moja kwa moja ziende kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu yeye ndiye ambaye amewezesha mambo haya yote kuweza kutokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwisha eleza kwenye majibu ya msingi, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wale ambao wanasoma fani au kozi hizi za tiba, wanafanya mafunzo yao kwa vitendo katika hospitali yetu ya Benjamin Mkapa, ambayo iko karibu kabisa na Chuo hiki cha Dodoma. Lakini vilevile wanafanya mafunzo yao katika Hospitali yetu ya Milembe hapa Dodoma. Pia wanafanya mafunzo yao kwa vitendo kwenye hospitali za mikoa ya Dodoma, Singida Pamoja na Iringa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu, na nilithibitishie hapa kwamba Serikali inaendelea na jitihada za kuona vyuo hivi vinakuwa na hospitali zake zenyewe za kufundishia ikiwemo na chuo hiki cha Dodoma. Kwa hiyo tutaendelea kutafuta fedha ili takwa hili la kimafunzo liweze kufikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
MHE. BONIVENTURE D. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ni miezi miwili sasa tangu fedha hizi zitumwe kule Buchosa. Je, Serikali inaweza kuwaambia wananchi ni lini mkandarasi ataanza kazi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa milioni 45 ni awamu ya kwanza, je, fedha zilizobaki zitatumwa lini ili kuendelea kutekeleza mradi huo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kiswaga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tulipeleka milioni 45 kwa ajili shughuli za awali ambazo zilikuwa kwa ajili ya due technical survey, topographical pamoja na ile ESIAM na tayari shughuli hizi zimekwisha fanyika. Mchakato uliokuwa unaendelea ni kwa ajili ya kutafuta mafundi pamoja na wazabuni wa vifaa mbalimbali kwa sababu utaratibu tutakaotumia katika ujenzi ni ule utaratibu wa force account.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tulikuwa tunaendelea na mchakato huo na hivi sasa mchakato umekamilika, tumekwisha pata mafundi wote kwa ajili ya ujenzi. Lakini vilevile tumepata wazabuni wa kupeleka vifaa eneo hilo. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, fedha zote kwa ajili ya ujenzi tayari ziko wizarani na kwa awamu ya kwanza tunapeleka jumla ya milioni 300 kwa ajili ya kuandaa misingi ili baadae tuweze kupeleka fedha nyingine kwa ajili ya sehemu ya juu ya majengo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba nimhakikishie tu nimuondoe wasiwasi hatutatumia mkandarasi na badala yake tutatumia mafundi kwa sababu tunatumia force account na fedha sasa hivi tunavyozungumza milioni 300 tayari iko Buchosa ili kuendelea na ujenzi wa misingi ya majengo yote tisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru Serikali kwa utekelezaji ambao unaendelea. Nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa vyuo vingi vya VETA vina uhaba wa walimu na vifaa vya kujifunzia;

a) Je, Serikali ina mpamngo gani wa haraka wa kutatua changamoto hiyo?

b) Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba mitaala ya VETA inaendana na shughuli za kiuchumi katika maeneo husika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Nancy, Mbunge Viti Maalum kutoka Iringa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa swali lake la kwanza, anataka kufahamu kuhusu mkakati wa Serikali kwa upande wa walimu na vifaa. Naomba nilithibitishie Bunge lako Tukufu pamoja na Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeshapata kibali kwa ajili ya kuajiri waalimu 514; na mpaka hivi sasa walimu 151 tayari wameshaajiriwa na kuripoti kwenye vile vyuo ambavyo vilikuwa vinaendesha mafunzo na hivi vyuo vipya; na tutaendelea na mkakati na mchakato huo wa kuajiri walimu kwa kadri fedha zitakavyoruhusu.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile katika swali lake la pili kuhusiana na suala la vifaa vya kufundishia na kujifunzia, naomba nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu, kwamba Serikali tayari ilishatoa jumla ya shilingi bilioni 8.6 kwa ajili ya ununuzi wa samani kwenye vyuo vile 25 pamoja na vile vya mikoa na vifaa hivyo tayari vimeshanunuliwa na kupelekwa kwenye maeneo hayo. Lakini kwa upande wa vifaa vya kufundishia naomba nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge, tarehe 22 mwezi wa nne mpaka tarehe 30 mwezi wa nne, timu yetu ya wataalamu kutoka Wizara ya Elimu ikiongozwa na mimi mwenyewe pamoja na watu wa NACTVET pamoja na VETA tulifanya ziara katika nchi ya China kwa ajili ya kufanya venting ya vifaa vya kujifunzia na kufundishia, na Serikali tayari imetenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili kuhusiana na suala la mitaala, naomba nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge tunaendelea na mchakato wa mapitio ya mitaala pamoja na sera yetu ya elimu katika ngazi zote ikiwemo na hii ya VETA. Basi ushauri wake huu wa kuona namna gani tunaweza kuhusisha shughuli za kiuchumi na mitaala yetu tutakwenda kulizingatia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, pamoja na Serikali kutenga fedha za ukarabati kila mwaka, lakini vyumba vya kubadilishia wachezaji ni chakavu, pia chumba cha marefarii kipo karibu sana na chumba cha timu pinzani ambayo inaleta wakati mwingine sintofahamu. Je ni lini sasa Serikali inaweza kutatua changamoto hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je nini mpango wa Serikali kuongeza nguvu katika kujenga Uwanja wa Majengo ambao unajengwa kwa fedha za ndani ili uweze kukamilika mapema? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Malleko, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyokwishaeleza katika majibu ya swali la msingi kwamba ni wajibu wa Serikali kupitia Chuo chetu cha Ushirika kwa maoteo ya bajeti kwa ajili ya ukarabati. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge na nilithibitishie Bunge lako Tukufu tutaendelea kufanya hivyo na hivi sasa tutatupia macho maeneo hayo aliyoyataja katika vyumba hivyo vya kubadilishia nguo pamoja na hiki chumba cha marefarii, tutafanya hayo marekebisho labda katika bajeti ijayo ya fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili, anataka kufahamu vile vile mkakati wa Serikali kuhusiana na Uwanja huo wa Majengo. Naomba nimthibitishie Mbunge kwamba uwanja huo tunafahamu kwamba uko chini ya Manispaa ya Moshi. Kwa hiyo tutashirikiana na wenzetu wa TAMISEMI, lakini vile vile Wizara yenye dhamana ya michezo kuhakikisha kwamba tunatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mbunge wa Segerea, Mheshimiwa Bonnah hajapata majibu na anasumbuliwa sana na wananchi kuhusu Uwanja wa Sigara Tabata, Jimbo la Segerea. Hebu nenda kalifuatilieni hili, mtuambie nani anayemiliki ili mumsaidie Mbunge aweze kuwaambia wananchi wake.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, tumelipokea.
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa mwenyekiti ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa niaba ya Serikali alivyojibu; amejibu vizuri, ahsante.

Swali la kwanza; tuna uhaba wa walimu sita na katibu muhitasi mmoja na uhaba huu unasababisha kwamba mwalimu wa fani moja anapokuwa hayupo hakuna linaloendelea;

Je, Serikali ina mpango gani wa kutuongezea wafanyakazi saba ili shughuli za utoaji wa elimu ya ufundi ziendelee kama zilivyopangwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili jambo muhimu katika mafunzo ya ufundi ni utendaji, yaani practical sasa utendaji au elimu kwa vitendo unahitaji sana vifaa;

Je, Serikali yetu imejipangaje kuhusu upatikanaji wa vifaa ili kweli mafunzo ya ufundi ya vitendo yafanyike?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Margaret Sitta, Mbunge wa Urambo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, Serikali ya Awamu ya Sita imejidhatiti kuhakikisha kwamba vyuo hivi ambavyo vilikuwa havina miundombinu tunaenda kuongezea miundombinu. Na hatukufanya hivi tu kwa chuo hiki cha Urambo peke yake, kuna vyuo kadhaa ambavyo vilikuwa na upungufu wa miundombinu. Tunafahamu upungufu wa miundombinu kwa Mheshimiwa Mwijage kule Muleba, tumeshafanya kazi kule, Mheshimiwa Rais alitoa fedha kwa ajili ya ukarabati pamoja na ujenzi wa miundombinu mingine. Pia kwa Mheshimiwa Dugange kule Wanging’ombe tumefanya hivyo; kwa Mheshimiwa Mtanda Serikali imepeleka fedha vilevile lakini vilevile tumepeleka fedha kule Mikumi kwa Mheshimiwa Londo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, si hicho tu, katika swali lake la kwanza anataka kufahamu mkakati wa Serikali juu ya walimu. Nimuondoe wasiwasi, Mheshimiwa Rais alitoa kibali cha kuajiri wafanyakazi watumishi wakiwemo na hao walimu 571. Mpaka hivi sasa ninavyozungumza walimu 151 tayari wameshaajiriwa na wameshapelekwa kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo na kwenye baadhi ya hivi vyuo ambavyo vilikuwa tayari vinatoa huduma na vile vyuo vytu 25 vya wilaya na vinne vya mikoa. Kwa hiyo tunaendelea na mchakato huu kwa kukamilisha idadi hii ya waaalimu na watumishi 571 tunaamini na Urambo itafikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa vifaa naomba nimtoe wasiwasi Mheshimiwa na Bunge lako tukufu, tumejidhatiti na kujipanga kwa dhati kabisa kuhakikisha kwamba tunapeleka vifaa kwenye vyuo hhivi vile vya zamani lakini na vile vipya ambavyo tunajenga hivi sasa. Katika bajeti yetu hii inayoendelea tuna package ya vifaa lakini vilevile na katika bajeti ambayo tumeanza kuisoma hapa kutakuwa na eneo la fedha ambayo tumetenga kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwa ajili ya vyuo hivi vya VETA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka hapo awali tulikuwa na shule ambazo zilikuwa za wananfunzi wenye vipaji maalumu. Shule hizo zilikuwa Kilakala, Loreza, Tabora Boys, Mzumbe, Iliboru na kadhalika lakini hadi sasa hivi hatuzisikii hizo shule zikizungumziwa au tukipata taarifa kwamba performance yake ya vile vipaji vyao maalum vimetumikaje.

Je, Serikali ina mpango gani basi kuziimarisha hizo shule ilikusudi tuone kwamba huu mtaala ambao unatengenezwa sasa hivi wa mali utaweza pia kuwa na tija katika shule hizi maalum?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; tumeona nchi za wenzetu kama Japan na Uchina wanatilia sana mkazo kwenye kazi za stadi, na matokeo yake ni kwamba zile kazi zinazotengenezwa na wanafunzi zinauzwa wakati wakifanya mahafali ya shule na kuwaalika wazazi ili kusudi wanafunzi wale wapate morali kwamba kweli vile wanavyotengeneza vina maana na wawanye wengine wa shule nyingine wapate moyo kwamba kumbe hizi shule za ufundi zina maana.

Je, Serikali ina mpango gani pia kuanzisha utaratibu ambao hivi vifaa vinavyotengenezwa na wanafunzi hawa wanaokwenda kwenye hizi shule za amali zitakuwa zenye thamani ya kuweza kuuzika ili ziongeze kipato kwenye shule hizi wanazofanyia?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kaboyoka, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli alichozungumza Mheshimiwa Mbunge. Nimuondoe wasiwasi, shule hizi bado zipo. Kwa upande wa wasichana ni kama alivyozitaja; tuna Shule ya Msalato hapa Dodoma tuna Kilakala ambayo ipo Morogoro. Pia tuna Tabora Girls ambayo ipo kule Tabora. Kwa upande wa wavulana tuna shule ya Kibaha Sekondari, tuna Mzumbe, tuna Ilboru pamoja Tabora Boys.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani jambo kubwa alilolizungumza ni kwamba hazisikiki. Tunaomba tuchukue ushauri wa Mheshimiwa Mbunge twende tukaimarishe ufundishaji. Hizi ni shule zetu ambazo tunasema ni maalum kabisa kwa ajili ya kupokea watoto wenye vipaji na vipawa mbalimbali. Tunaendelea kuzihudumia na kuziimarisha, lakini tunaomba tuchukue fursa hii, tubebe ushauri wako ili twende tukaziimarishe zaidi ili ziweze kujitangaza kama ilivyokuwa zamani, zilikuwa zinavuma sawasawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili amezingumzia suala la zile study mbalimbali. Kwa vile tumesema kwamba sasa hivi tunafanya mapitio ya mitaala, mapitio ya mitaala hii itakwenda kuongeza baadhi ya masomo ambayo yatakwenda kufundisha sanasana stadi mbalimbali hasa kwenye skills.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezungumzia suala la kuongeza ubora wa vile vitu ambavyo vitakuwa vinazalishwa ili viende vikapate soko, kwa maana ya tuvibiasharishe iwe kama kitega uchumi cha chuo. Tunaomba tubebe ushauri huo; na kwa vile tunapitia mitaala tutakwenda kuchopeka baadhi ya kozi ambazo tutakwenda kuzungumza au tutakwenda kushughulikia zaidi zile study za mikono na kazi za mikono ambazo tutakwenda kuzipeleka sokoni kwa ajili ya kukuza na kuongea vipato na iwe kama miradi kwenye shule zetu.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; katika Wilaya ya Manyoni tuna uhitaji mkubwa sana wa chuo ambacho kinaweza kikatoa elimu ya afya katika ngazi ya cheti na diploma. Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba, sasa wanasogeza kampasi ya chuo cha afya cha ngazi ya certificate and diploma katika Wilaya ya Manyoni?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa, kuna uhitaji mkubwa sana wa Wahadhiri katika vyuo vikuu vyetu na vyuo vya kati; na kwa kuwa, hivi karibuni Serikali imekuwa ikitumia mfumo wa usaili kuwapata Wahadhiri, hususan Tutorial Assistants, je, Serikali haioni haja ya kurudi kwenye mfumo wa zamani ambapo vijana waliokuwa wakipata first class walikuwa wakibakizwa vyuoni na kuendelezwa? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Chaya, Mbunge wa Manyoni Mashariki, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na jambo la kwanza, swali lake la kwanza analozungumzia suala la chuo cha afya. Naomba tuubebe ushauri wake tuweze kuangalia namna gani ya kufanya upande wa hivi vyuo vya afya, tukishirikiana na wenzetu wa Wizara ya Afya au na taasisi nyingine binafsi, tuweze kuangalia namna bora ya kufanya katika upatikanaji wa vyuo hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Dkt. Chaya, pale katika jimbo lake katika wilaya yake tayari sisi kama Wizara ya Elimu, kama Serikali, tumeshapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha VETA ambavyo huenda baadaye tukatohoa tu na hizo kada za afya vilevile zikaweza kufundishwa katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, anazungumzia suala la wahadhiri. Ni kweli zamani tulikuwa na utaratibu katika vyuo vikuu, wale wanafunzi wanaofanya vizuri huwa wanabaki palepale chuoni kwa ajili ya kuwa Wahadhiri. Utaratibu huu hapa katikati ulisitishwa ili kuweza kuweka ushindani kwanza, lakini vilevile kuondoa upendeleo kwa namna moja au nyingine. Kwa hiyo, mamlaka yale sasa yalikasimiwa au yalipelekwa moja kwa moja kwenye Tume ya Utumishi wa Umma kwa lengo la kutoa vibali vya kuajiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunapokea ushauri huo hata wakati tunakusanya maoni wakati wa mapitio ya mitaala suala hili lilizungumzwa sana. Kwa hiyo, tuachie kama Serikali twende tukalifanyie kazi, ili tuweze kuangalia namna bora ya kurudisha utaratibu ambao utakuwa mzuri na kutoa fursa kwa kila Mtanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niulize swali dogo la nyongeza. Mkoa wa Njombe ndio Mkoa ambao hauna chuo kikuu wala chuo cha juu na Mheshimiwa Rais alipotembelea Mkoa wa Njombe tarehe 9 Agosti, 2022 alipokea ombi la wazee wa Njombe kuhusu kujengewa chuo kikuu katika Mkoa wa Njombe na Mji wa Njombe. Je, Serikali itaanza lini mchakato wa kuhakikisha kwamba na sisi tunapata chuo kikuu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni kweli Mheshimiwa Rais alifanya ziara katika Mkoa wa Njombe, tarehe 9 Agosti, 2022 na miongoni mwa ahadi alizozitoa ni ujenzi wa kampasi mojawapo ya chuo kikuu pale Njombe, ingawa katika mgawanyo huu wa miradi ya HEET katika mikoa ambayo haitapata fursa katika awamu hii ya kwanza ni Mkoa wa Njombe. Kwa vile tayari Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alishatoa hiyo ahadi na sisi kama Serikali ahadi hii ya Mheshimiwa Rais tunaendelea kuifanyia kazi, hivyo, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mwanyika na wananchi wa Mkoa wa Njombe, tuko njiani kuja Njombe na tutahakikisha kwamba, tunaleta taasisi ya elimu ya juu katika Mkoa wa Njombe.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Shule binafsi ni wadau wakubwa sana wa elimu katika Taifa hili la Tanzania lakini imekuwa mara nyingi vijana hawa wakifika elimu ya juu wanakosa mikopo au kupata chini ya 40% hatuoni kwamba tunawaonea, watoto wengine wamesomeshwa kwa msaada wakiwemo yatima, kuwazuia kuendelea na elimu ya juu?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Serikali haioni sasa kuna umuhimu watoto wa nchi hii wote wapate mikopo flatrate yani mikopo ya aina moja bila kugawa kwa asilimia ili watoto wote wapate usawa katika Taifa hili? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge Mwakagenda kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwisha eleza kwenye majibu ya swali la msingi kwamba utoaji wa mikopo yetu hauzingatii mwanafunzi amesoma katika shule gani, iwe shule ya umma au shule ya Serikali ilimradi wamekidhi vile vigezo wanafunzi hao wanawajibika kupata hiyo mikopo.

Mheshimiwa Spika, ni kweli anachozungumza Mheshimiwa Mbunge kwamba kumekuwa na changamoto wakati mwingine wakupata asilimia chache sana ya mikopo hii. Tunafahamu kuwa juhudi za Serikali zakuongeza wigo wa kupata mikopo hii kwa kuzingatia bajeti yetu ya Serika bado zinaendelea.

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako tukufu Serikali imeendelea kuongeza fedha za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kutoka shilingi bilioni 464 mwaka 2021/2022 mpaka shilingi bilioni 738 mwaka 2023/2024. Ni matumaini yetu kuwa ongezeko hili la bajeti litahakikisha kwamba wanafunzi wengi wanapata mikopo na kwa kiasi kikubwa cha mikopo.

Mheshimiwa Spika, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, vilevile Serikali imeendelea kufanya juhudi ya kutafuta wadau mbalimbali wa kuweza kuongeza nguvu. Mpaka sasa tunavyozungumza taasisi yetu ya Benki ya NMB katika mwaka wa fedha uliopita iliweza kutenga shilingi bilioni 200 kwa ajili ya mikopo hii. Na katika mwaka huu vilevile itatenga fedha hizo.

Mheshimiwa Spika, lengo la Serikali ikiwa ni kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi wa elimu ya juu anapata mkopo na anapata mkopo katika kile kiasi ambacho kinahitajika. Nashukuru sana.
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, naomba kuuliza swali dogo la nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itaanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati ambao wanapata diploma na vyeti hapa nchini kwetu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Saputu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika bajeti yetu ya 2023/2024 jambo hili lilizungumzwa bayana katika Bajeti Kuu ya Serikali. Serikali imetenga fedha kwa ajili ya utoaji mikopo kwa vyuo hivi vya kati na programme hii itaanza mwaka huu wa fedha.
MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Mheshimiwa Waziri huoni umuhimu sasa wa Serikali kufanya mapitio ya sheria ya hii Bodi ya Mikopo ili kuweza kutatua changamoto nyingi ambazo watoto wa Kitanzania wanazipata kupata mikopo ya elimu ya juu? Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Tweve kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mradi wetu wa Higher Education for Economic Transformation tumetenga fedha kwa ajili ya kufanya mapitio. Tunafahamu sheria hii ya Bodi ya Mikopo imeanza toka 2004 ni miaka 19 sasa toka sheria hii ianze. Kwa hiyo, hivi sasa tunafanya mapitio ili kuangalia vigezo namna gani ya kuweza ku-update information zetu lakini vilevile namna ya utoaji wa mikopo hiyo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimuondoe wasi wasi Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako tukufu mpaka kufika mwisho wa mwaka huu wa fedha shughuli hii itakuwa imekamilika na bodi yetu sasa itakuwa na sheria pamoja na miongozo ambayo itaendana sawa na kasi ya sasa.
MHE. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi. Je, Serikali haioni sasa kuna umuhimu wa kuwapatia mikopo wanafunzi wote wenye ulemavu wa aina yoyote katika vyuo vyetu vikuu kwa 100%?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Nahato kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hivi sasa kigezo kimoja wapo cha wanafunzi kupata mikopo ni wale wenye ulemavu naomba nimuondoe wasi wasi Mheshimiwa Mbunge watoto wetu vijana wetu wenye ulemavu wanapata mikopo kwa 100% na huo ndiyo mpango wa Serikali.
MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Spika, ahsante, je, ni lini sasa Serikali itaanzisha revolving fund ikiwa na maana kwamba zile fedha zinazokusanywa ziwekwe kwenye mfuko ambao ni fedha lindwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Wambura amezungumzia swala la revolving fund kama nilivyoeleza kwenye swali la nyongeza la Mheshimiwa Tweve nadhani kwamba hivi sasa tunafanya mapitio ya sheria ile. Katika mapitio yale tutakwenda kuangalia hayo mambo yote pamoja na kuangalia kama mfuko unaweza kujiendesha lakini vilevile katika kujiendesha katika taratibu za kibenki ikiwemo na hii revolving fund. Kwa hiyo, nimuondoe wasi wasi jambo hili linafanyiwa kazi.
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Spika, NMB kama mdau wa elimu ameandaa shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu lakini mikopo hii itatolewa kwa wale wanafunzi ambao wazazi wao ni wafanyakazi. Je, kuna mkakati gani wa kuhakikisha wale wanafunzi wanaohitaji mikopo ambao wazazi wao siyo watumishi wanapata mikopo kwa asilimia zote?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Migilla kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli wenzetu wa NMB walitenga fedha shilingi bilioni 200 katika mwaka wa fedha uliopita na mwaka huu watatenga tena kwa ajili ya kuendelea na zoezi hili. Nimuondoe wasi wasi Mheshimiwa Mbunge pamoja na kigezo kile cha mzazi awe ni mtumishi lakini vilevile tumeweka kigezo cha mzazi kuwa mkulima. Ilimradi amejiunga au yupo ndani ya chama cha ushirika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo wazazi wote ambao ni wafanyakazi lakini wazazi wote ambao ni wakulima au wale ambao wako katika vyama mbalimbali wanahusika na mikopo hii na tutakwenda kufanya review kwa kadiri mahitaji yatakavyohitajika, nashukuru.
MHE. NORAH W. MZERU: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina swali moja la nyongeza.

Je, Serikali itawasaidiaje wamiliki wa nyumba za kulala wenye nia ya kubadilisha matumizi na kuzifanya hostel hasa katika suala la tozo za Serikali?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mzeru kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, suala la kubadilisha matumizi ya nyumba pamoja na ardhi yapo kwa mujibu wa sheria, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba taratibu hizo wamiliki wa nyumba pamoja na ardhi wanapaswa kuzifuata, lakini kwa vile wanafanya biashara ni lazima zile taratibu zingine za tozo pamoja na kodi ya Serikali ni lazima zilipwe. Kwa hiyo, ni muhimu kwa wale wamiliki wanapobadilisha matumizi kwenda kwenye mamlaka husika kutoa taarifa ya kubadilisha zile leseni zao za biashara ili waweze kupata tozo ambayo ni sahihi. Ninakushukuru.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Je, Serikali haioni umuhimu wa kutumia utaratibu wa ubia na sekta binafsi katika kujenga mabweni kwenye Vyuo na hata kwenye Sekondari?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Kimei kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kimei ametoa wazo, naomba tulichukue ushauri wake tuende tukaufanyie kazi ili tuweze kuangalia ni nimna gani tunaweza tukajenga hosteli kwa njia ya PPP. Ninakushukuru.
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kwa niaba ya watu wa Tarime naomba niishukuru sana Serikali kwa kutenga fedha ya kujenga VETA kule Tarime Vijijini, hasa Nyamongo, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; napenda kujua kimetengwa kiasi gani cha fedha angalau chuo kianze kufanya kazi kwa hatua ya mwanzo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; nini kauli ya Serikali kwa wananchi pale ambao wengi ni wachimbaji wadogo wadogo, wavuvi karibu na Ziwa Victoria, lakini pia na wakulima wa mazao mbalimbali na Tarime pia mazao yanastawi. Nini matarajio ya wananchi hasa vijana kwa uwepo wa Chuo cha VETA katika eneo langu? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Waitara, Mbunge wa Tarime Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni azma ya Serikali kujenga vyuo hivi katika kila wilaya kama nilivyoeleza awali. Katika awamu ya kwanza hii ya mwaka 2022/2023 Serikali imetenga bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivyo. Tafsiri yake ni nini, katika kila chuo katika awamu ya kwanza tunapeleka bilioni moja na milioni 400 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa majengo tisa ya awamu ya kwanza. Majengo haya tisa ya awamu ya kwanza yatakapokuwa yamekamilika, vyuo hivi bila shaka vitaanza kufanya kazi ya kutoa huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati wetu ni nini? Katika awamu ya pili vilevile tutatenga tena fedha kwa ajili ya kukamilisha majengo mengine tisa. Jumla kuu ya bajeti yote ili chuo kiweze kukamilika ni jumla ya bilioni tatu na milioni mia tano. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan imeweza kutenga katika mwaka huu, lakini vilevile katika mwaka ujao tunakwenda kukamilisha ujenzi huu ambapo vyuo hivi vyote vitakapokamilika ni zaidi ya bilioni 200 tunatarajia kutumia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa pili, upande wa mafunzo yatakayotolewa, tunafanya mapitio sasa hivi ya mitaala ile ya utoaji wa mafunzo ya ufundi wa VETA na hasa hasa tutazingatia zile shughuli za kiuchumi zinazofanyika katika maeneo husika. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi kwenye maeneo ya kilimo kutakuwa na mitaala ya kilimo, kwenye maeneo ya madini kutakuwa na mitaala ya shughuli za madini, kwenye maeneo ya uvuvi, tutakwenda hivyo angalau ku-customize kulingana na shughuli za kiuchumi za eneo husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza naomba niishukuru Serikali niliomba ituletee vifaa vya kufundishia, walituletea katika Chuo chetu cha VETA, Wilaya, lakini pia niliomba gari na wakatuletea kwa ajili ya utawala, tunawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu ni kwamba, kwa kuwa wananchi wamejitokeza kwa wingi, kwa maana kuna wanafunzi wengi katika chuo kile. Je, Serikali inaweza sasa kutuongezea wakufunzi wa masomo mbalimbali wanaosoma pale?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kawawa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Kawawa na Waheshimiwa Wabunge wote, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan tayari alishatoa kibali cha kuajiri watumishi wakiwemo wakufunzi pamoja na walimu. Tumepata kibali cha watumishi 571 na mpaka hivi sasa tunavyozungumza watumishi 151 tayari wameshaajiriwa, tutawapeleka Namtumbo na maeneo mengine ya vile vyuo vya zamani, lakini tuna vyuo 25 vipya na vile vinne vya mikoa watakwenda watumishi hawa na tunaendelea kuajiri.
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na Serikali kujenga vyuo vingi vya VETA na ili kuweza kueta hamasa kwa wanafunzi na wazazi kujiunga kwenye vyuo hivi, Serikali ina mpango gani ama mkakati gani wa kutoa mikopo kwa wanafunzi hawa wanaojiunga na Vyuo vya VETA ama vyuo vya kati? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Sima, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba, tunatoa mikopo katika elimu ya juu na elimu hii ya kati. Tumetengeneza mkakati huo, lakini kwa mkakati wa muda mfupi tumezungumza na wadau ikiwemo benki na taasisi nyingine za kifedha. Wenzetu wa NMB tayari katika mwaka huu wametoa zaidi ya bilioni 200 kwa ajili ya mikopo katika kada ya hii ya kati ikiwemo na wanafunzi wa vyuo vya VETA na sisi kama Serikali tunatengeneza mkakati. Baada ya mapitio ya mitaala tutajua kitu gani cha kufanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Chuo cha VETA, Wilayani Mkuranga, ikizingatia Wilaya ya Mkuranga ni ukanda wa viwanda? Ahsante.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Hawa Mchafu, Mbunge wa kutoka Mkoa wa Pwani, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa mchafu na Wabunge wengine wote wa Mkoa wa Pwani. Katika zile wilaya 64 nilizozizungumza awali ipo Wilaya ya Mkuranga, ipo Wilaya ya Kibiti, ipo Wilaya ya Bagamoyo, ipo Wilaya ya Kisarawe. Kazi imeshaanza na shughuli zinaendelea kule Mkuranga na maeneo hayo mengine niliyoyataja kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi, kazi tayari imeshaanza. (Makofi)
MHE. JUDITH S. KAPINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili madogo ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa dunia ya sasa ipo katika mapinduzi ya nne ya viwanda kuelekea mapinduzi ya tano ya viwanda. Je, mitaala inayoboreshwa itaendana na kasi hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; programu ya mageuzi ya kiuchumi ambayo imepelekea kuanzishwa kwa takribani programu 300 kwenye vyuo vikuu. Je, ni lini programu hizi zitahuishwa na kuanza kufundishwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kapinga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu ya swali la msingi kwamba, sasa tuko katika hatua za mwisho za uboreshaji wa mitaala hii. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika swali lake la kwanza anazungumza kuhusiana na suala la mitaala namna gani litaweza ku-cope na mapinduzi ya viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, mitaala inayoboreshwa inalenga kumpatia mhitimu maarifa, study pamoja na ujuzi utakaomwezesha kukabiliana na mabadiliko ya kisayansi, teknolojia na kiuchumi kwa ujumla. Mitaala hii imesisitiza sana masomo ya TEHAMA pamoja na kompyuta ambayo, tutaanzia katika ngazi ya elimu ya msingi na kwenda katika ngazi zote. Lengo kuu la kufanya maboresho haya ni kujiandaa na mapinduzi haya ya nne pamoja na ya tano ya viwanda ambayo yanahusisha matumizi ya teknolojia pamoja na kompyuta kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili anaulizia kuhusiana na tunaanza lini? Mradi huu wa Higher Education for Economic Transformation ni mradi wa miaka mitano na utekelezaji wake ulianza tokea mwaka 2021/2022 na tunatarajia kukamilisha 2025/2026. Kwa hiyo, kazi hii imeshaanza, wataalam wetu wameshapata mafunzo kwa ajili ya uboreshaji wa mitaala pamoja na programu hizi. Kazi hii inaendelea na kwa vile ni kazi ya miaka mitano, tutakuwa tunaendelea kuifanya mpaka kipindi hicho chote kitakapokuwa kimekamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante; je, ni lini Serikali itatoa pesa au kutenga pesa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA Kilwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; vifaa vilivyopo kwenye Chuo cha VETA Lindi Mjini ni vya kizamani sana; je, Serikali haioni haja ya kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya Lindi Mjini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Maimuna Ahmad Pathan, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwisha jibu kwenye majibu yangu ya swali la msingi kwamba vyuo hivi vinajengwa katika Wilaya 64, na Wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa Wilaya 64 ambazo zinajengewa, na tayari tumeshapeleka shilingi milioni 228 kule Kilwa, na usimamizi wa chuo kile kinachojengwa pale unafanywa chini cha Chuo chetu cha FDC ambacho kipo katika Wilaya hiyo ya Kilwa.

Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, lakini niwaondoe hofu wananchi wa Kilwa, hata pale Kilwa napo ni miongoni mwa Wilaya 64 ambazo zinajengewa vyuo hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la pili, amezungumza suala la vifaa; ni kweli tukiri kwanza katika vyuo vyetu vya zamani tulikuwa na vyuo 45 vya zamani ikiwemo na hiki cha Lindi, lakini tumpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa utashi wake na maono yake, katika kipindi hiki kifupi tumeweza kukamilisha vyuo 29 na hivi sasa tunakwenda kujenga vyuo vingine 65, vyuo 64 katika Wilaya na kimoja cha Mkoa. Hivi sasa Serikali inafanya tathmini kwa vyuo vile vyote 45 vya zamani na hivi 29 ambavyo tulijenga katika mwaka uliopita wa fedha, tathmini ya vifaa pamoja na mitambo mbalimbali kwa ajili ya kujifunzia na kufundishia. Kwa hiyo, tuko njiani kupeleka vifaa hivyo.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Swali langu ni hili; je, Serikali inaweza ikatoa kauli gani kuhusu uwezekano wa kuingia ubia na taasisi za kidini ambazo zilijenga Vyuo vya Ufundi Stadi?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Charles Stephen Kimei, Mbunge wa Vunjo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimtoe hofu Mheshimiwa Kimei, utaratibu huo upo. Naomba tu kwa vile ni suala mahususi, baada ya kikao chetu hiki au baada ya kipindi hiki cha maswali, tunaweza tukakutana ili tuweze kuangalia hilo eneo au hivyo vyuo ulivyovitaja namna gani tunaweza tukatengeneza huo ushirikiano wa kutoa mafunzo kwa pamoja baina ya wawekezaji pamoja na Serikali, nakushukuru sana.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu ya Serikali ni majibu mazuri lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia idadi ya Maprofesa nchini imeporomoka sana kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita. Chuo Kikuu pekee cha Dar es Salaam kinahitaji Maprofesa 161 lakini wapo Maprofesa tisa. Sasa kwa nini Serikali isibadili umri wa kustaafu kutoka miaka 65 mpaka miaka 70 ili kutunza hao wachache tulionao? (Makofi)

Swali la pili, kwa nini Serikali sasa kwa kuwa tunao uhitaji mkubwa wa Maprofesa isitoe package nzuri ili kuwavutia vijana wengi wakajitahidi kufanya research ili waweze kufikia hiyo hatua ya Uprofesa kwa ajili ya kutunza vyuo vyetu vikuu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Kikoyo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi, Serikali imeendelea kuchukua hatua za kukabiliana na upungufu wa watumishi na taaluma katika vyuo vyetu vikuu vya umma nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kufanya mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza, tunaendelea kuongeza nafasi za ajira kwa Wahadhiri pamoja na Wanataaluma katika vyuo vyetu. Jambo la pili, tunaendelea kuruhusu uhamisho wa watumishi wenye sifa kutoka taasisi nyingine za Serikali ili kuweza kuingia katika Vyuo Vikuu na kuhudumu kama Wahadhiri pamoja na kwenda kwenye nafasi za juu za Uprofesa. Jambo la tatu, tunaendelea kusomesha Wahadhiri ndani na nje ya nchi ikiwa na lengo pana la kuhakikisha tunaongeza idadi ya watumishi au wanataaluma hawa katika vyuo vikuu. naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali itaendelea kufanya mambo haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile katika mradi wetu wa HEET wa miaka mitano ambao tunaendeleanao. Serikali inaenda kusomesha Wanataaluma zaidi ya 600 ambapo tunaamini kabisa katika usomeshaji huu tutaweza kupata maprofesa wengi. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi juhudi hizi zinaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika jambo hili la kuongeza umri kwa wanataaluma hawa hasa Maprofesa, uliongezwa kutoka miaka 60 mpaka miaka 65. Mheshimiwa Mbunge hapa anashauri kwamba tuongeza tena iwe miaka 70. Tunachukua ushauri huu, tutakwenda kuufanyia kazi tuweze kuangalia namna bora ya kufanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la pili kuhusu kuongeza maslahi Serikali imekuwa ikifanya hivyo. Serikali hii ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea na jambo hili vizuri kabisa na imeendelea kuboresha maslahi ya watumishi wakiwemo na wenzetu wanataaluma katika vyuo vikuu na tutaendelea kufanya hivyo kwa kadri ya bajeti itakavyoruhusu, nakushukuru.
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Naipongeza sana Serikali kwa majibu mazuri, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Kwa kuwa ziko fedha za uchangiaji wa elimu zinazotolewa na Serikali kupitia kwa Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule na Wakuu wa Vyuo kwenda kwa Wadhibiti Ubora, fedha hizi zimekuwa na usumbufu mkubwa sana, lakini zimekuwa kero kubwa sana kwa Wakuu wa Shule pamoja na Wadhibiti Ubora. Serikali haioni haja sasa kwamba umefika wakati wa kubadilisha miongozo yake na sheria ili fedha hizi zitoke moja kwa moja Hazina na kwenda kwa Wadhibiti Ubora? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Wadhibiti Ubora wanafanya kazi yao vizuri sana; Serikali haioni sasa umefika wakati wa kuwajengea uwezo ili kuongeza ufanisi wa kazi katika majukumu yao? Ahsante sana (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali madogo ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza kwenye majibu ya swali la msingi, Serikali inaendelea kufanya juhudi mbalimbali kuhakikisha kwamba Wadhibiti Ubora wanakuwa kwenye mazingira salama ya kufanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama nilivyosema kwamba tunakwenda kubadilisha muundo wa kada hii ya Wadhibiti Ubora na sasa tunakwenda kuondoa ile Udhibiti Ubora ngazi ya kanda na kupeleka katika ngazi ya mikoa na katika kufanya hivyo tunasogeza huduma karibu zaidi ya wananchi na vilevile tunaimarisha utendaji kazi kwa ufanisi mkubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kufanya haya yote, tutahakikisha vilevile katika eneo hili la uchangiaji tunaenda kulifanyia kazi ili liweze kushuka moja kwa moja kwenda Ofisi za Wadhibiti Ubora badala ya kwenda kwa Walimu Wakuu au kwenda shuleni kule.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la pili la utendaji kazi, tumekuwa na utaratibu wa kuhakikisha kwamba Wadhibiti Ubora wanapata mafunzo ya mara kwa mara ili kuwajengea umahiri na kuwawezesha kufanya shughuli zao za kila siku kwa ufanisi, nakushukuru.
MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niwapongeze Serikali kwa majibu mazuri. Ni kweli Wilaya ya Uyuwi tumepata chuo cha VETA, lakini kutokana na jiografia ya Wilaya ya Uyuwi na kuwepo kwa majimbo mawili, wananchi wa Jimbo la Igalula kwenda kuifata VETA ni zaidi ya kilometa 200.

Je, Serikali haioni haja sasa ya kunipatia upendeleo maalum wa kunipatia angalau hata shule ya ufundi ili niweze kuwa na shule ya ufundi na wanachi wa Jimbo la Igalula wakanufaika na matunda ya Mama Samia Suluhu Hassan?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Venant Mbunge wa Igalula kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti,kama nilivyoeleza kwenye majibu ya swali la msingi kwamba ni azma ya Serikali kujenga vyuo hivi katika wilaya zote ikiwemo Wilaya ya Uyuwi, hivyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali wakati inajenga miundombinu hii vile vile tunatoa huduma za mabweni pamoja na zile za kutwa. Lakini vile vile tunafahamu, inawezekana huduma hizi za mabweni kwa wale wanafunzi wanaotoka mbali zinaweza zikawa sio toshelezi. Serikali vile vile inatambua kwamba kuna Wilaya ambazo ni kubwa na jiografia yake ni kubwa na zina majimbo zaidi ya moja. Nitoe tu mfano wa hiyo Wilaya ya Uyuwi lakini tuna Wilaya ya Bagamoyo, tuna Wilaya ya Lindi kuna Wilaya ya Bariadi kwa hiyo kuna Wilaya nyingi ambazo zinachangamoto aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, tunauchukua ushauri wake. Serikali ina mipango mingi endelevu na Serikali hii ya Mama Samia tunakwenda kufanya mambo makubwa kwa lengo la kusogeza huduma za elimu pamoja na elimu ya ufundi karibu. Kwa hiyo andaa tu eneo kwa ajili ya ujenzi wa hiyo shule uliyozungumza na Serikali ya Mama Samia ni sikivu. Tuna amini baada ya kukamilisha ujenzi wa vyuo hivi tunakwenda sasa katika ujenzi wa shule hizi za ufundi katika maeneo ambayo yamekosa vyuo vya VETA, nakushukuru sana.
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza. Nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa mpango Mkakati wa kujenga Vyuo vya VETA kila wilaya. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kujenga Chuo cha VETA katika Wilaya ya Simanjiro?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Asia, Mbunge kutoka Mkoa wa Manyara, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Simanjiro wenzetu wa Taasisi ya Upendo walijenga chuo kilikuwa hakijakamilika miundombinu yake lakini baada ya kujenga waliikabidhi Serikali. Chuo ambacho kipo katika Wilaya ya Simanjiro kipo katika Kijiji Engalakash katika Kata ya Emboret, lakini kilikuwa kimejengwa kweli na wenzetu wa Upendo na wamekwisha kabidhi Serikali na kilikuwa na miundombinu ifuatayo: Karakana mbili; Madarasa; Bwalo; Mabweni mawili; na Kisima cha maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka huu wa fedha Serikali imepeleka pale milioni 190 kwa ajili ya kuongeza miundombinu ambayo tunakwenda kujenga Bweni moja, tunajenga nyumba za watumishi, lakini kulikuwa na changamoto za umeme. Kwa hiyo, tunasambaza umeme ndani ya majengo pamoja na nje ya majengo na tutaendelea kufanya hivi. Kwa hiyo, sasa hiki ndiyo kitakuwa Chuo cha Wilaya ya Simanjiro kinachomilikiwa na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimwondoe hofu tutaendelea kuongeza majengo kama tunavyofanya katika maeneo mengine kama vile Urambo, Nanyumbu na maeneo mengine ambayo tulikuwa na vyuo vya zamani vilikuwa na miundombinu ambayo sio toshelezi, tutakwenda kujenga miundombinu ili kutosheleza kutoa huduma ile ya VETA katika maeneo yote ya wilaya zote nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa ni azma ya Serikali kukuza kilimo nchini. Je, Serikali haioni sasa kuna umuhimu wa kuwapa kipaumbele kwenye mikopo wanafunzi ambao wanachaguliwa kwenda kusomea masomo ya kilimo hususan katika kampasi zilizopo pembezoni mfano kampasi ya Mizengopinda ya sasa hivi ina zaidi ya miaka mitatu ambayo imejikita zaidi katika kutoa elimu ya nyuki?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa sasa katika Mkoa wa Katavi tuna hiyo kampasi moja. Serikali haioni kuna umuhimu wa kuongeza kamapasi nyingine ili kupanua wigo wa elimu katika Mkoa wetu wa Katavi kwa kuongeza kampasi kama vyuo vya afya pamoja na vyuo vya uhasibu? Nakushukuru.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Martha Mariki Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwenye swali lake la kwanza anataka kufahamu mkakati wa Serikali juu ya mikopo. Naomba kumfahamisha Mheshimiwa Mbunge Serikali imekuwa ikiongeza kiwango au kiasi cha mikopo kwa wananfunzi wa elimu ya juu. Kwa takwimu zilizopo kwa mwaka 2021/2022 tulitenga na kupeleka jumla ya bilioni 570 kwa ajili ya wanafunzi hao. Mwaka 2022/2023 tulipeleka zaidi ya bilioni 554 hela ya kawaida lakini tulikuwa na vile vile bilioni tatu kwa ajili ya Samia Scholarship lakini katika bajeti yetu vile vile tumeweza kutenga jumla ya bilioni 738 kwa ajili ya mikopo katika mwaka ujao wa fedha.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wote kwamba Serikali imejipanga na kujizatiti kuhakikisha kwamba wanafunzi wetu wanapata mikopo kwa wakati wake.

Mheshimiwa Spika, tuna kozi za vipaumbele ikiwemo na hiyo aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge kozi za sayansi lakini zile za uhandishi, kozi za udaktari na kozi hizi za kilimo pamoja na masuala ya nyuki kwa ujumla wake ndizo ambazo tunazizingatia katika utoaji wa mikopo katika kipindi kijacho.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili anataka kufahamu utaratibu gani Serikali itatumia kuongeza idadi ya vyuo. Nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge. Uwepo wa kampasi hii unaweza ukasaidia katika kuongeza aidha ndaki au shule nyingine katika kampasi hii. Kwa sababu tukumbuke hata hiyo University of Dar es Salaam wakati inaanzishwa ilianza na kozi moja lakini imeweza kupanuka mpaka hivi sasa ina kozi mbalimbali. Kwa hiyo, hata kozi hizi hapo baadae tutaangalia uhitaji na namna gani ya kuweza kuangalia kozi nyingine za kuanzishwa katika kampasi hii, nakushukuru.
MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa kuzingatia kwamba Mkoa wa Songwe ni mpya naomba kufahamu Serikali ina mkakati gani wa kutujengea angalau kampasi moja tu ya chuo kikuu cha umma, ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shonza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwisha eleza katika majibu ya swali la msingi kwamba tunakwenda kujenga kampasi 14 katika mikoa kumi na nne nchini. Moja ya Mikoa ambayo tunaweza kujenga ni katika Mkoa wa Songwe ambapo Chuo chetu cha DIT ndicho ambacho kitakwenda kujengwa katika eneo hili la Songwe.

Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako labda ningeweza kusema na mikoa mingine ambayo inaweza kujengewa ili Waheshimiwa Wabunge waweze kujua. Naanza na Mkoa wa Manyara Chuo chetu cha TIA kitakwenda kujenga tawi pale. Singida ni TIA, Kagera University of Dar es Salaam, Lindi University of Dar es Salaam, Ruvuma ni TIA, Shinyanga ni MAMCU, Simiyu ni IFM, Rukwa ni MUST, Tabora ni Julius Nyerere, Kigoma ni MUHAS, Zanzibar ni University of Dar es Salaam, Mwanza ni ARU, Tanga ni Mzumbe na Songwe ni DIT, nakushukuru.
MHE. OMAR ALI OMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Ni masomo gani ambayo yalisahihishwa katika kipindi hicho alichokitaja Mheshimiwa Waziri 2021/ 2022?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; je, Wizara imejipanga kusahihisha mitihani mingapi katika mwaka 2023?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ali Omar kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika utaratibu wa usahihishaji wa mitihani kila kituo kawaida huwa kina sahihisha mtihani mmoja na kwa miaka hiyo niliyoitaja ya 2021/2022 katika kituo hiki cha Zanzibar ni somo la civics ndilo ambalo lilisahihishwa katika kituo hicho.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili anataka kufahamu ni mitihani gani ambayo itasahihishwa. Masuala ya mitihani na masomo gani yatasahihishwa ni jambo la siri. Kwa hiyo, hatuwezi ku-disclose hatuwezi kufungua hapa sasa hivi ni mitihani gani utakwenda kusahihishwa kwenye kituo hiki na ni mapema Sana.

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tarehe 26 Juni, tutaanza kufanya ukaguzi wa vile vituo ambavyo tunalenga sasa mitihani itakwenda kusahihishwa lakini somo gani kwamba linapelekwa katika kituo hicho litaendelea kuwa siri mpaka baada ya kazi hiyo kumalizika, nakushukuru sana.
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na hayo majibu yanayoridhisha kiasi, nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, hawa wanafunzi wanaokwenda kusoma katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, naomba Mheshimiwa Waziri atuhakikishie kwa sababu hawa wa maendeleo ya jamii wanaegemea kwenye upande wa afya na elimu; je, wako katika kundi la kupata mikopo au ni wale wa VETA na vyuo vingine vya afya tu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Thea Medard Ntara, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwisha eleza kwenye majibu ya swali la msingi, ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba inatoa mikopo kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu pamoja na wale wa elimu ya kati. Lakini naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatarajia kuanza kutoa mikopo kwa wanafunzi hawa wa elimu ya kati kama ilivyosomwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka ujao wa 2023/2024 Serikali inatarajia kuanza kutoa mikopo kwa wananfunzi wa elimu ya kati katika kada za ualimu, afya pamoja na sayansi.

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kupanua wigo wa kutoa mikopo hii katika kada nyingine kwa kadri ya upatikanaji wa fedha na uwepo wa bajeti, nakushukuru.
MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa fursa.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wanafunzi wenye ulemavu ambao wanafanikiwa kufika hatua hii ya elimu ya juu ni ndogo sana yaani idadi ya wanafunzi ambao wanafanikiwa kufika hatua hii ya eleimu ya juu ni ndogo sana, na kwa kuwa kundi hili linakabiliwa na changamoto nyingi za kimaisha.

Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa mikopo hii ya elimu ya juu kama ruzuku kwa kundi hili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Stella Ikupa Alex, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba miongoni mwa vigezo au sifa za upataji wa mikopo, mojawapo ni kwa wenzetu wenye mahitaji maalum wakiwepo watu wenye ulemavu. Kwa hiyo, kwanza tumeanza na kipaumbele kwa hawa, lakini tunatoa kama mikopo.

Mheshimiwa Spika, swali la Mheshimiwa Mbunge yeye anataka tufanye kama ruzuku, naomba tulichukue pendekezo lake hili au ushauri wake huu twende tukaufanyie kazi, tufanye tathmini ya wangapi hawa watu wenye ulemavu, na tuweze kuangalia namna bora ya kufanya, kama tulivyofanya kwenye Samia Scholarship, Mheshimiwa Rais alitoa fedha hizi zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa ajili ya watoto waliofanya vizuri. Nadhani na hili la watoto wenye ulemavu linawezekana, nakushukuru.
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, na ninaishukuru Serikali kwa majibu hayo, lakini swali la kwanza; kwa kuwa Ifakara ni katikati ya Wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga, na mahitaji ya kuwepo kwa tawi ama kituo cha mitihani ni makubwa mno: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuanzisha Tawi dogo la Chuo Kikuu Huria?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; endapo halmashauri itatoa eneo kwa sasa: -

Je, Serikali iko tayari kujenga Tawi la Chuo Kikuu Huria ama tawi la chuo kikuu kingine chochote? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Abubakari Damian Asenga, Mbunge wa Kilombero, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwisha jibu katika majibu ya swali la msingi, lakini Mheshimiwa Asenga anataka kufahamu, japo kuwa pale tuna Kituo cha Chuo Kikuu Huria ambacho wanafanyia mitihani bado ana msisitizo huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Asenga; Chuo Kikuu Huria kinao utaratibu wa kuwa na vituo vya mitihani katika ngazi za wilaya pamoja na kata kulingana na uhitaji wa maeneo hayo. Lakini vilevile kina utaratibu wa kuweza kuanzisha matawi au vituo hivyo vya kuratibu mitihani katika makambi yetu ya majeshi pamoja na kambi mbalimbali za wakimbizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Asenga naomba tu nikuhakikishe kwamba Serikali itaendelea kufanya tathmini ya kina katika eneo hilo ulilolitaja la Kilombero, Ulanga na kule Malinyi na maeneo mengine nchini, na kuweza kuona kama uhitaji huo upo ili tuweze kuanzisha ama vituo au matawi ya Chuo Kikuu Huria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la pili, kwanza tuishukuru Halmashauri ya Ifakara, lakini tukushukuru wewe binafsi kwa jitihada zako za kutenga eneo kwa ajili ya Chuo Kikuu Huria. Naomba nikuhakikishie kwamba Serikali itaendelea kufanya tathmini, pamoja na uwepo wa maeneo haya, lakini vilevile kuna uhitaji wa rasilimali fedha pamoja na uhitaji wa rasilimali watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hivi vyote vikichanganywa ndipo tunakwenda kuanzisha matawi haya ya chuo kikuu, lakini vilevile uhitaji wa hilo tawi katika eneo hilo. Kwa hiyo, baada ya tathmini hii tutajihakikishia sasa kama upo umuhimu wa kwenda kuanzisha tawi katika eneo la Ifakara au la, nakushukuru.
MHE. LUCY J. SABU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; je, ni vigezo vipi vinatumika kwa ajili ya kibali maalum kutolewa kwa shule za bweni?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa Waraka wa Elimu Na. 2 wa mwaka 2023 umetoa maelekezo wamiliki kuwa na kibali kwa ajili ya shule za bweni: -

Je, ni hatua zipi zimechukuliwa kwa shule ambazo zimekiuka agizo hili? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Lucy John Sabu, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwisha eleza kwenye majibu ya swali la msingi, kwamba vipo vigezo ambavyo Kamishna wa Elimu anatumia, lakini hivi sasa tunahuisha vigezo hivyo. Na nimesema kuwa Wizara kwa kushirikiana na wadau inakamilisha kuandaa vigezo vitakavyotumiwa na Kamishna wa Elimu katika kutoa vibali hivi maalum. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, tunaendelea kufanya uhuishaji wa vigezo hivi na mara vitakapokuwa tayari basi Umma utajulishwa juu ya vigezo hivi ili iweze kufwata wakati wa kuomba vibali hivyo maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili, anataka kujua hatua zipi zilizochukuliwa; naomba nimhakikihsie Mheshimiwa Mbunge wale wote ambao walikuwa wanaendesha shule hizi kinyume na utaratibu wameweza kupewa notice, lakini vilevile wadhibiti ubora wetu wameweza kutembelea maeneo hayo na kuweza kujiridhisha juu ya huduma ambazo zinatolewa hapo, na baada ya kuona hali ilivyo basi tutachukua hatua mara moja, nakushukuru sana.
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

Je, Serikali haioni haja sasa ya kufanya utafiti kujua watoto wangapi waliopo Bwenini wanafanyiwa ukatili wa kijinsia?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Thea Ntara kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa vile Mheshimiwa Mbunge anaomba Serikali iweze kufanya utafiti, nimwondoe hofu Serikali iko tayari kuchukua ushauri wake tuweze kufanya utafiti wa kuweza kujua athari zinazotokea katika unyanyasaji wa watoto wetu katika maeneo aliyoyataja.
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza nataka kujua hao wanafunzi 1,907 waliorejea shuleni ni asilimia ngapi ya wanafunzi wote ambao walikatisha masomo na walipaswa warejee shuleni?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, nataka kujua kuna haja gani ya kuwaacha watoto nyumbani kwa kipindi cha miezi takribani minane tangu wafanye mtihani wa form four mpaka akajiunge na form five, pale pana muda mrefu; kuna sababu gani ya kuacha huo muda kwa sababu kutoka na matokeo ya sensa inaonesha drop out pia zinatokea hapo kwa kiasi kikubwa kwa sababu watoto wanakaa nyumbani muda mrefu, kwa nini muda ule usipunguzwe?

Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili kama ulivyosema swali la kwanza linahusu takwimu. Naomba Mheshimiwa Mbunge aridhie baada ya kipindi cha maswali hapa Bungeni au baada ya Bunge tuweze kukutana kuweza kukokotoa hii percentage.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili anataka kufahamu mkakati wa Serikali juu ya kupunguza muda wa wanafunzi kusubiri kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vingine.

Mheshimiwa Spika, ni kweli tuna kipindi cha zaidi ya miezi saba baada ya wanafunzi kufanya mtihani wa kidato cha nne ili waweze kujiunga aidha na kidato cha tano au na vyuo vingine vya kati.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki tunafanya mambo kadhaa ndio maana muda unakuwa mrefu, baada ya mithani kufanyika mwezi wa 11 zoezi la ukusanyaji wa zile script ambazo zimetumika kujibia mitihani huwaga zinakusanywa, lakini baada ya hapo tunakwenda kwenye zoezi la usahihishaji, tukimaliza usahihishaji tunakwenda kwenye zoezi sasa la uteuzi wa wanafunzi, lakini baadae hufanya maandalizi kwa ajili ya wanafunzi hawa sasa kuwapokea kwenye vituo vyetu vya shule mbalimbali. Kwa hiyo, shughuli ambazo zinafanywa katika kipindi hicho ni hizo.

Mheshimiwa Spika, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge Serikali imejidhatiti na kujipanga kwa dhati kuhakikisha kwamba tunapunguza muda huu ambapo sasa tumeanza utaratibu wa kufanya e-Marking kwenda kidato cha nne, tulikuwa tumeanza na darasa la saba kwa mithani ya darasa la saba, lakini sasa tunakwenda na hii mithani ya darasa la nne, tumeanzisha mfumo wa e-Marking ambao utapunguza muda wa usahihishaji, lakini eneo la pili katika upanganji vilevile tumeanzisha mfumo ambao unajulikana kama Management Information System ambao nao vilevile utapunguza muda wa upangaji au uteuzi ule wa wanafunzi kujiunga katika maeneo mbalimbali.

Kwa hiyo, tunapokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge wa kupunguza muda huo ili tuweze kuufanyia kazi sawasawa. Ninakushukuru sana.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Kwanza kabisa niipongeze Serikali kwa kuona watoto wengi wamerudi mashuleni, lakini mimi swali langu nilitaka kuuliza; je, Serikali inatoa elimu ya makuzi na malezi kwa hawa watoto ili hili tatizo lisiweze kujitokeza tena katika watoto wengine? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Ritta Kabati, kama ifuatavyo;

Mheshimiwa Spika, ni kweli tunatoa elimu hiyo ya makuzi na malezi, lakini nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge katika rasimu ya mitaala pamoja na sera ambayo tunaendelea nayo hivi sasa, maoni ya wadau mbalimbali yameonesha kwamba kuna uhitaji wa masomo haya ya makuzi na malezi. Kwa hiyo, katika mitaala ijayo mambo haya tunaweza kuyaona kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. (Makofi)
MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, VETA Kitangari inahudumia majimbo mawili; Newala Mjini pamoja na Newala Vijijini, kwa hiyo, inasababisha usafiri wa wanafunzi kutoka kwenye maeneo yao kwenda katika eneo VETA ilipo ni mbali. Ujenzi ambao umetajwa na Serikali hauhusishi bweni la wavulana katika VETA hii.

Je, ni lini Serikali itaweka kwenye mpango ujenzi wa bweni la wavulana katika VETA ile ya Kitangari ili kuleta urahisi wa usafiri?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; linahusu watumishi, katika fani za umeme, ushonaji na uhazili, kuna mwalimu mmoja mmoja kiasi kwamba akipata dharura wanafunzi wale hawasomi.

Je, lini Serikali itapeleka walimu katika fani hizo, angalau mmoja mmoja, ili kuleta ufanisi na usomaji mzuri kwa wanafunzi katika VETA Kitangari? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mtanda, Mbunge wa Newala kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwisha eleza kwenye majibu ya swali la msingi, kwamba katika mwaka huu wa fedha tumetenga shilingi milioni hizo 666 na katika fedha hizi tayari tumeshapeleka milioni 304 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa baadhi ya majengo. Kwa hiyo nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge kwamba ni kweli ujenzi wa bweni ukawa bado kutokana na fedha iliyopelekwa. Lakini naomba nimhakikishie fungu lililobaki kati ya ile milioni 666 tutakapopeleka fungu hili la pili, ujenzi wa bweni hilo utakuwa umeanza na tutaendelea nao kwa kadri ya fedha tutakavyokuwa tunapeleka.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la pili la watumishi, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu; Mheshimiwa Rais alitoa kibali cha kuajiri watumishi 514 katika mwaka huu wa fedha na mpaka sasa tumeshaajiri watumishi 169. Kwa hiyo naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge pamoja na eneo la Newala lakini tunafahamu tuna vyuo vya zamani na tuna vyuo vipya 25 vile vya Wilaya, vinne vya Mikoa tunakwenda kuwapangia walimu maeneo haya ili kuhakikisha kwamba taalum hii inaweza kutolewa katika maeneo hayo kwa uhakika, nakushukuru sana.
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Chuo cha VETA Wilayani Rombo kwa kuwa Halmashauri imeshatoa eneo na wataalam wa ardhi wameshafanya uchambuzi na kuona linafaa?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Zuena kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika ujenzi wa vyuo 68 vya wilaya zilizobaki, Rombo ni miongoni mwa Wilaya ambayo inakwenda kujengewa chuo hicho. Kwa hiyo, nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, kazi kule Rombo tayari imeshaanza. Tumefanya geo technical, topographical, environment impact assessment, na tayari tumeshatambua eneo na shughuli zimeshaanza katika mwaka huu wa fedha.
MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuzingatia idadi kubwa ya wananchi katika Jimbo la Busanda ambayo ni takribani laki saba.

Je, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu wa kujenga Chuo cha VETA kwenye maeneo hayo?

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili, kwa vile jibu la msingi linathibitisha kwamba Chuo hicho kimejengwa Geita Mji na sisi tuko Geita Vijijini.

Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga Chuo cha VETA Geita vijijini badala ya Geita Mji?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Tumaini Magessa kwa pamoja kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwisha eleza kwenye maswali ya msingi kwamba tuna chuo ambacho tumejenga pale Geita; lakini ni sera ya Serikali kwa Awamu hii ya Kwanza kujenga vyuo hivi katika ngazi za Wilaya, na tutakapokuwa tumekamilisha ujenzi huu katika ngazi za Wilaya ambapo mnafahamu Waheshimiwa Wabunge wote katika mwaka huu Mheshimiwa Rais ametoa zaidi ya bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivyo katika zile Wilaya ambazo tumekosa na katika Mkoa mmoja wa Songwe ambao ulikuwa hauna chuo hiki.

Mheshimiwa Spika, sasa baada ya kukamilisha awamu hii, tutafanya tathmini na kuona maeneo yapi yana idadi kubwa ya wananchi au ya wakazi na kuweza kuangalia namna gani tunaweza tukasogeza huduma hii karibu na maeneo hayo likiwemo na hili eneo la Busanda. Vile vile tunaweza kuzingatia katika Halmashauri au Wilaya ambazo zina Majimbo au Halmashauri zaidi ya moja kuweza kuwafikishia huduma hii katika Halmashauri hizo kulingana na upatikanaji wa fedha lakini vile vile na kukidhi kwa sifa za maeneo hayo.
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Mimi nataka kujua tu, Serikali imeweka mkakati gani wa kuondokana na hili daraja sifuri? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mussa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyozungumza katika swali lililopita, suala la ufuatiliaji au suala la elimu ni lazima pande zote ziweze kushiriki, kwa maana ya mwanafunzi mwenyewe, ni lazima atengeneze mkakati wa namna gani anaweza kujifunza na kuhakikisha kwamba anafaulu kwenye masomo yake. Pia kuna sehemu ya walimu na vilevile kuna sehemu ya wazazi. Kwa hiyo, sisi kama Serikali jukumu letu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na miundombinu wezeshi ya kumwezesha mwanafunzi kuweza kusoma na kupata elimu yake sawa sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile lazima tupeleke walimu wa kutosha kuhakikisha kwamba masomo yote yanafundishwa kwa vipindi vyote kwa wakati, kwa maana ya kutekeleza mtaala wetu kwa wakati na sehemu inayobaki ni ya mwanafunzi yeye mwenyewe kujitahidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sisi kama Serikali mkakati wetu ni kuhakikisha kwamba tunakwenda kutengeneza facilities za kuwezesha wanafunzi wetu kufanya masomo yao vizuri, ahsante sana.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri haoni kwamba mtihani wa mwisho wa Kidato cha Nne mwanafunzi anapofanya wakati mwingine anaweza akawa amechanganyikiwa: Kwa nini sasa Wizara isiangalie matokeo yake ya nyuma ijumlishe na yale ya mwisho ili tuweze kumuhukumu kuendelea na maisha yake ya baadaye?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mtihani wetu wa mwisho wa Form Four siyo una-contribute au unaosababisha kuwa na matokeo ya mwisho. Mtihani wetu wa mwisho wa Form Four una maeneo mawili; asilimia 30 inakuwa kwenye maendeleo yake ya elimu, tunaita continuous assessment. Kwa hiyo, asilimia 30 ya zile alama (marks) zinatoka kwenye maendeleo yake yale ambayo ameyafanya kwa kipindi chote cha miaka minne; na asilimia 70 ndiyo ambayo inazingatiwa au inakuwa contributed na ule mtihani wake wa mwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, iwapo amefanya vizuri kwenye maendeleo yake kutoka Form One mpaka Form Four, ile asilimia 30 ina maana itambeba na ule mtihani wa mwisho unachangia kwenye asilimia 70 tu ya mitihani yake. Kwa hiyo, hilo kama Serikali tumeshalizingatia na ndivyo inavyofanyika mpaka hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. MICHAEL C. MAKAMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naishukuru Serikali kwa kunipatia majibu kwenye swali hili la msingi, lakini nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa kutokana na uwekezaji mkubwa wa Serikali kwenye maeneo mbalimbali ya nchi hii kujenga Shule za Kata, kunakopelekea watoto wengi kumaliza Kidato cha Nne kwa alama hizo za Daraja la Nne au Sifuri na kwa vyuo hivyo vinavyotajwa na Serikali ni taasisi za Umma ambavyo vimejengwa kwa malengo ya kutoa elimu hizo kwa vijana wetu:-

Je, Serikali haioni sasa ipo haja ya kuwapangia moja kwa moja kwenye vyuo hivyo badala ya wao kuamua wenyewe?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Michael Mwakamo, Mbunge wa Kibaha Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tubebe ushauri wa Mheshimiwa Mbunge, kwa sababu utaratibu huu sasa haupo wa kuwapangia moja kwa moja wale waliopata division four na zero au wale waliofeli darasa la saba. Kwa vile umetoa ushauri huo, acha tuuchukue kama Serikali twende tukaufanyie kazi, tufanye tathmini ya kina kama iwapo jambo hili linawezekana, basi tutaliingiza kwenye mipango yetu kama Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ili mwanafunzi afikie kupata division zero au four ni pamoja na ufatiiaji hafifu wa masomo yake. Wazazi wanatakiwa wahudhurie mikutano ya shule wanapoitwa nakadhalika: Ni lini sasa Serikali italeta Muswada hapa Bungeni kuhakikisha kwamba tunatunga sheria ya wazazi kufatilia masomo ya watoto wao mashuleni? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Shally Raymond, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la elimu ni suala ambalo linahusu pande karibu tatu; upande wa kwanza ni wanafunzi yeye mwenyewe, upande wa pili ni wa wazazi kama Mheshimiwa Mbunge alivyoshauri na upande wa tatu ni wa walimu au Serikali kwa ujumla. Kwa vile amezungumza hapa suala la kuleta Muswada Bungeni wa kuangalia namna gani tunaweza kuwabana wazazi ili waweze kufuatilia maendeleo ya watoto wao katika elimu, naomba tuubebe ushauri huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo tunafahamu kwamba katika shule zetu kunakuwa na Kamati mbalimbali za kufuatilia maendeleo ya shule pamoja na wanafunzi kwa ujumla. Kwa hiyo, nadhani Kamati zile sasa zinatekeleza wajibu huu, lakini kwa vile ni wazo au ushauri ambao ameutoa, acha tuuchukue kama Serikali twende tukafanye tathmini, halafu kama tukiona kama kuna umuhimu wa kuleta Muswada huo, tuweze kuleta hapa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la ujenzi wa kiwanja hicho umechukua miaka saba, kama kuna hilo tatizo, sijui mgogoro inanishangaza.

Je, Serikali sasa ina mpango gani wa ku-review mkataba huo ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika na kiwanja kinatumika mara moja? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Thea Medard Ntara, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wa karibu wa suala hili. Kabla hajaliuliza hapa bahati nzuri aliwahi kufika ofisini na tulilijadili kwa kina.

Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge katika kikao hiki cha tarehe 4 Machi, 2021 pamoja na mambo mengine kilijadili vilevile kufanya review ya mkataba lakini vilevile kufanya review ya design ya viwanja vile. Kwa hiyo, nimuondoe wasiwasi, review imeshafanyika na mchakato sasa mwingine unaendelea katika kuhakikisha kwamba tunafanya review ya thamani au gharama za ujenzi ili kazi hii iweze kukamilika kwa haraka. Nakushukuru sana.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, baadhi ya vyuo nchini vinakabiliwa na ukosefu wa viwanja vya michezo.

Je, Serikali haioni kuwa ni wakati muafaka Wizara kupita kwenye Wilaya zote na Mikoa kuona viwanja vilivyopo na namna ya kushirikiana na wadau? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Issaay kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tukakubali kwamba kuna changamoto ya viwanja kwenye maeneo yetu ya vyuo, tunaomba tubebe/tuchukue ushauri huu wa Mheshimiwa Issaay ili tuweze kwenda kufanya tathmini namna gani tunaweza kushirikiana na wadau wengine kuweka kufanya maendeleo ya viwanja kwenye vyuo vyetu. Nakushukuru sana.
MHE PHILLIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili ni nyeti sana, mimi ni mtu wa elimu. Suala hili limeulizwa leo ni mara ya pili; mimi kama mlezi wa TAMOSCO, elimu upande wa vyuo na elimu msingi na sekondari napata shida sana pale ambapo kwenye shule za msingi, kwenye shule za sekondari O-level na A-level mitihani ikivuja na hasa kwenye shule za private Serikali inachukua hatua haraka na kuwapeleka mahakamani na kuwapa adhabu na ikiwezekana kufunga shule.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini suala hili limejitokeza Wizara ya Afya kwa NACTE ambao ni watu wa Serikali, liko kimya, ni kimya kimya wanafunzi wamerudia mitihani, wameenda wamefanya kimya kimya na wazazi wamepata adha ya kurudia mtihani na kulipia zile ada mara ya pili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nini kauli ya Serikali kuwapa adhabu Maafisa wote wa Serikali Wizara ya Afya waliohusika na uvujaji wa mitihani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, kwanza nianze kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa hoja yake muhimu ambayo mara nyingi sana na yeye huwaga tunashirikiana na anakuja ofisini mara nyingi. Mheshimiwa Mbunge nikutoe wasiwasi, tunakwenda kuhakikisha kwamba maeneo haya tunakwenda kuyasimamia vizuri kwa mujibu wa kanuni, sheria, taratibu na miongozo iliyopo. Na nikuondoe wasiwasi kwamba jambo lile tayari limeshachukuliwa hatua na liko kwenye hatua za mwisho kabisa kuhakikisha kwamba adhabu inatolewa kwa wale wote waliohusika kwenye jambo hili. Nakushukuru sana.
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Kwa kuwa Serikali imekiri kwamba mitihani hii imevuja na inasimamiwa na Wizara ya Afya. Nataka kujua wajibu wa NACTE katika kusimamia mitihani hii ni nini? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Sima kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, wajibu wa NACTE kwenye uratibu wa zoezi zima la mafunzo katika vyuo vyetu vyetu vya kati ni pamoja na mitihani hii. Lakini kwa upande wa mitihani ile ya muhula wa kwanza, mara nyingi sana inafanyika na kusimamiwa na kuratibiwa na Wizara ya Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nimezungumza kwenye majibu yangu ya msingi kwamba tunakwenda kuanzisha chombo maalum kitakachokuwa kinaratibu masuala haya ya mitihani katika Wizara ya Afya kwa ujumla wake ambayo itashirikiana sasa na NACTE kwa ukaribu. Kwa hiyo, matatizo haya tunakwenda kuyamaliza na kuyaondoa kabisa. Nakushukuru. (Makofi)
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa kuwa tunafahamu wote kama Taifa hatuna Sera ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu lakini pia Sheria ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imepitwa na wakati.

Je, Maonesho ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu MAKISATU yanatekelezwa kwa sera ipi?

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Habari, Mawasiliano ya Habari na Teknolojia ya Habari yote yana masuala ya teknolojia jambo ambalo linasababisha tushindwe kuelewa nani hasa mhusika wa masuala ya teknolojia kwenye Taifa letu. Je, Wizara ipo tayari sasa kuanza kuishauri Serikali kwa vielelezo hatua kwa hatua waanzishe Wizara mpya ambayo itashughulika na masuala ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu; ukizingatia mabadiliko ya sayansi na teknolojia ulimwenguzi lakini mapinduzi ya nne ya viwanda kama ilivyo nchi za Kenya, Afrika Kusini na Rwanda? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Nusrat Shaaban Hanje kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Nusrat kwa ufuatiliaji wake wa karibu wa masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu, lakini kipekee nichukue fursa hii kuwapongeza Wabunge wote ambao waliweza kufika na kutembelea kwenye mashindo yetu ya MAKISATU ambayo yalianza tarehe 16 – 20 Mei, 2022 katika Uwanja wetu wa Jamhuri pale Dodoma.

Mheshimiwa Spika, naomba nimtuoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba dhana hii ya utekelezaji wa mashindano hayo ya MAKISATU ni msimamo au ufuatiliaji wa karibu wa Serikali kuhakikisha kwamba mashindano haya au ubunifu nchini unaweza kuimarishwa.

Mashindano haya yanatekelezwa kwa mujibu wa sera ya ubunifu ya mwaka 1996. Tunakiri kuna mapungufu machache kwenye sera hii, lakini ndio ambayo tunazingatia katika utekelezaji wa mashindano haya.

Mheshimiwa Spika, lakini kama nilivyozungumza katika kipindi kilichopita kwamba, sera hii tunakwenda kuifanyia maboresho makubwa, lakini naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kupitia mashindano haya tumeweza kuibua bunifu zaidi ya 1,785, lakini vilevile zaidi ya bunifu 200 zimeweza kuendelezwa na zaidi ya bunifu 26 zimeweza kuingia sokoni kuona namna gani Serikali inasimamia kwenye eneo hili.

Mheshimiwa Spika, lakini katika swali lake la pili anazungumzia suala la Wizara ya Elimu pamoja na Wizara ya Habari kuwa na suala hili la teknolojia. Ni kweli, tunaomba tukiri kwamba, Wizara ya Habari na Wizara ya Elimu zote zina teknolojia ndani, lakini utekelezaji wa teknolojia hii unategemea na mawanda yale ambayo Wizara imepewa kupitia hati idhini ya uanzishwaji wa Wizara husika.

Mheshimiwa Spika, kwa vile ametoa ushauri namna gani sasa Serikali inaweza kutenganisha maeneo haya ya ubunifu na Wizara hizi; basi tubebe ushauri huo, twende tukaufanyie tathmini na tuweze kuufanyia kazi ili tuweze kuona namna gani tunaweza tukatekeleza.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa nami niweze kuuliza swali la nyongeza. Ugunduzi na ubunifu ni miongoni mwa nyanja muhimu sana katika ukuzaji uchumi na maendeleo. Nini mkakati wa Serikali katika kuendeleza ugunduzi na ubunifu katika nyanja za vijijini na hasa kwa wanawake?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Fatma Toufiq, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu katika majibu yangu ya msingi kwamba, kwanza tuna sera ya namna gani ubunifu na ugunduzi unasimamiwa au unaratibiwa katika maeneo yote. Katika kulisimamia hilo, Serikali baada ya kuona hii sera mwaka 2018 tumeandaa mwongozo wa namna gani masuala haya ya ubunifu yanaweza kusimamiwa na kuratibiwa kuanzia ngazi ya vijiji, kata, Tarafa, Wilaya, mpaka kufika katika ngazi ya Taifa ambako huko watu wote tunaweza tukawakuta.

Mheshimiwa Spika, ukitaka kuangalia kwa umakini kabisa katika mashindano yetu haya ya MAKISATU yameweza kubeba makundi yote, kuna makundi karibu saba tumeweza kuyazingatia tunapokwenda kuwagundua wagunduzi wetu au watafiti wetu katika maeneo yote ya vijijini mpaka katika ngazi ya Taifa. Kwa hiyo, katika eneo hili na wanawake vilevile wanaingia kwa namna moja au nyingine.

Mheshimiwa Spika, Nakushukuru sana.
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa. Je, Serikali ina mkakati gani kusaidia wabunifu kuhatamia teknolojia zao au ku-incubate wakati wakijiandaa kuanzisha viwanda vidogo vidogo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa kaka yangu, Profesa Ndakidemi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nimejibu katika majibu yangu ya nyongeza kwenye maswali yaliyopita kwamba, katika kipindi cha miaka minne iliyopita Serikali ilianzisha mashindano ya MAKISATU ambayo tulianza mwaka 2019 na mwaka huu sasa ni awamu ya nne. Katika mashindano haya zaidi ya bunifu elfu moja mia saba na themanini na kitu yaliweza kuibuliwa na zaidi ya bunifu 200 zimeweza kuendelezwa au kuatamiwa na zaidi ya bunifu 26 tayari zimeshapelekwa sokoni, sasa kitu gani tunachofanya?

Mheshimiwa Spika, baada ya kuwapata hawa wagunduzi au wabunifu tunawapeleka kwenye zile hub zetu, tuna center mbalimbali nchini kote ambazo zinawalea na Serikali sisi tumeweza kupeleka fedha katika maeneo haya. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tumeweza kupandisha bajeti ya kuwalea hawa wabunifu wetu kutoka bilioni 3.0 mpaka bilioni 9.0 katika mwaka ujao wa fedha.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Serikali tayari imeshafanya eneo leke na katika kipindi hiki hizi bunifu tulizozipata katika mashindano haya yaliyopita, zaidi ya milioni 700 tumeshazipeleka tayari kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, hawa tunakwenda kuwaendeleza ili bunifu hizi ziende kuwa biashara na bidhaa ambayo tunaweza tukaipeleka sokoni.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, pamoja na jitihada za Serikali kuongeza miundombinu zinazoendelea, bado kuna baadhi ya kozi hazitolewi hapa nchini.

Je, Serikali haioni haja ya kushirikiana na vyuo vingine nchi za nje ili kutoa kozi hizo hasa katika sekta ya afya.

Swali la pili, pamoja na mkakati huu wa miundombinu, Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza Wahadhiri katika Vyuo Vikuu hapa nchini? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Pauline Nahato kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwenye swali la kwanza, kwanza tukiri kwamba kuna baadhi ya kozi katika Sekta ya Afya ni kweli hazitolewi hapa nchini. Lakini nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, katika kipindi kifupi tumeweza kupata uzoefu kutokana na janga hili la UVIKO-19 kuna wanafunzi wengi sana walirejeshwa hapa nchini, vilevile kama mnavyofahamu mwezi Februari, Machi mwaka huu kutokana na vita vya Ukraine pamoja na Urusi wanafunzi wengi wameweza kurejeshwa miongoni mwao ni wale ambao walikuwa wanachukua kozi ya ambazo hazipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeanza mjadala wa kuangalia namna gani tunaweza kuangalia mashirikiano ya karibu ya kuangalia tunaweza kushirikiana vipi na vyuo vingine vya nje ya nchi ili kozi hizo zinaweza zikatolewa kule kwa ushirikiano vilevile na hapa nchini. Naomba tulibebe wazo hili lakini tubebe ushauri huu wa Mheshimiwa Paulina tuendelee kuufanyia kazi kuweza kuangalia kozi hizi ambazo hazitolewi namna gani tunaweza tukazifanya kwa mashirikiano na vyuo vingine vya nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa eneo la pili la uongezaji wa Wahadhiri, nadhani swali hili nimeshawahi kulijibu hapa Bungeni. Kwanza kupitia mradi wa HEET tunakwenda kusomesha Wahadhiri wapya zaidi ya 1,000. Kwa hiyo, pamoja na uongezaji huu wa miundombinu lakini utakwenda sambamba na kusomesha Wahadhiri katika awamu ya kwanza karibu Wahadhiri 625 tunakwenda kuwasomesha wa kozi ndefu lakini wale kozi fupi zaidi ya Wahadhiri 400. Kwa hiyo, tunaamini tunaweza kupunguza uhitaji huo wa Wahadhiri kwenye vyuo vyetu.

Mheshimiwa Spika, eneo la pili Serikali mara nyingi sana huwa inatoa vibali vya kuajiri walimu wapya, wahadhiri wapya nao vilevile mfumo huo tutautumia. Lakini vyuoni kule kuna mpango vilevile vyuo vyenyewe huwa vinakuwa na mpango wa kusomesha Wahadhiri na kuajiri wale Wahadhiri wa mikataba ya muda mfupi. Kwa hiyo, mipango hii yote tukiijumuisha tunakwenda kuondoa tatizo hili la Wahadhiri.

Mheshimiwa Spika, kama mnavyofahamu Serikali yetu imeweza kuongeza mikopo ile ya elimu ya juu kwa wanafunzi wale ambao wanaoingia katika elimu ya juu, eneo hili kwa vile tutakuwa na udahili mkubwa wa wanafunzi wa elimu ya juu, ni dhahiri kabisa tutaweza kupata wahadhiri wa kutosha kwenye vyuo vyetu hivi ambavyo tunatarajia kuvijenga. Nakushukuru sana.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Spika, kunipa fursa ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa Mikoa mikubwa sana hapa nchini na wenye wanafunzi wengi. Je, ni lini sasa Serikali itaanza ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu katika Mkoa wa Kagera?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza Mheshimiwa Dkt. Kikoyo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, wakati najibu swali la msingi nimezungumza mradi wetu wa HEET, kwamba pamoja na mambo mengine unakwenda vilevile kujenga vyuo katika Mikoa ya pembezoni na miongoni mwa Mikoa ambayo niliitaja ni pamoja na Mkoa wa Kagera. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nadhani Mkoa huu upo na upo kwenye program hii HEET tutakwenda kujenga chuo katika Mkoa huo wa Kagera pamoja na Mikoa mingine ya pembezoni. Nakushukuru sana.
MHE. RASHID ABDALLA RASHID: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Zanzibar imeshatoa eneo kwa ujenzi wa Chuo Kikuu Huria na Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere katika eneo la Mfikiwa. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi huo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Rashid Rashid kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyowaeleza kwenye majibu ya msingi, mradi wetu wa HEET unakwenda ku-cover karibu maeneo mengine sana. Amezungumza hapa suala la Chuo Kikuu Huria pamoja na Chuo chetu cha Mwalimu Nyerere ambayo tayari ina Kampasi kule Zanzibar, kwa hiyo, ni suala tu la upanuzi Kwa vile amezungumza hapa kwamba kuna eneo ambalo tayari limeshatolewa tunaomba tuchukue wazo hili tuweze kuangalia namna gani ile Kampasi iliyopo pale Zanzibar inaweza kupanuliwa kwa ajili ya kwenda eneo hilo ambalo Mheshimiwa Mbunge amelitaja. Nakushukuru sana.
MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya swali la nyongeza. Awali napenda niipongeze na kuishukuru Serikali kwa hatua iliyofikia ya ujenzi wa Chuo cha VETA, kizuri, lakini nina swali moja la nyongeza.

Je, mara tutakapoanza kuchukua wanafunzi na kuwaingiza kwenye masomo, wanafunzi hawa wa chuo hiki watapatiwa mikopo ya Serikali ili masomo yaweze kutolewa vizuri? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Rweikiza, Mbunge wa Bukoba Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivi sasa bado Serikali hatujaanza utaratibu wa kutoa mikopo kwa wanafunzi hawa wa VETA na vyuo vingine vya kati. Kwa hiyo, tunachofanya ni nini sasa kama Serikali? Tunachofanya kama Serikali kwa vyuo hivi vya kati pamoja na VETA, tumejaribu kupeleka ruzuku kwenye maeneo hayo na ndio maana utaona hata ada zake tofauti na vile vyuo vingine vya juu. Ada kwa wanafunzi hawa wa VETA kwa wale wa bweni ni shilingi 120,000 na wale wa kutwa ni shilingi 60,000 ambayo sio thamani halisi ya mafunzo hayo pale, lakini baada ya Serikali kuona umuhimu wa mafunzo haya imeamua kutoa ruzuku.

Kwa hiyo, kwa hivi sasa bado hatujaanza kutoa mikopo. Tunalibeba kama ushauri tuweze kuangalia katika kipindi kijacho kulingana na hali ya upatikanaji wa fedha kama tunaweza tukatoa mikopo katika maeneo haya. Nakushukuru sana.
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Kwanza kabisa tunapenda kuishukuru Serikali kwa kutujengea Chuo cha VETA Mkoa wa Rukwa, chuo cha kisasa, chuo kizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali langu ni lini sasa chuo hicho kitafunguliwa na wanafunzi waweze kupata mafunzo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kulikuwa na mikoa ambayo vyuo vya VETA vya mikoa bado havijakamilika, miongoni mwa mikoa hiyo ni pamoja na Mkoa wa Rukwa na mwingine ni Mkoa wa Njombe, Geita pamoja na Simiyu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ukamilishaji wa majengo yale sasa unakamilika. Katika fedha zile za Uviko-19 tulizopata mwaka uliopita tumeweza kupeleka pale zaidi ya bilioni nne kwa ajili ya ukamilishaji wa chuo kile na tunataraji ujenzi ule unaweza ukakamilika katika kipindi hiki kifupi cha mwezi huu wa Juni na mwezi wa Julai, ili basi ifikapo mwezi wa kumi au mwezi Januari mwakani mafunzo pale yaweze kuanza. Nakushukuru sana.
MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, Jinbo la Buchosa lina watu wanaozidi laki nne, lakini hawana Chuo cha VETA; je, ni lini Serikali itajenga chuo cha VETA katika Halmashauri ya Buchosa ili wananchi wale waweze kupata elimu, lakini pia waweze kujiajiri? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Furaha, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, sera yetu ya elimu na hata katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inazungumza ujenzi wa Chuo cha VETA katika kila Wilaya nchini. Kwa hiyo, nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba, tumeanza. Tulianza na Wilaya 25, lakini Wilaya nne nazo vilevile zilikuwa tayari zimeshajengewa katika mwaka ule uliopita wa fedha na sasa hivi Serikali tuko mbioni katika utafutaji wa fedha, ili basi Wilaya zilizobaki karibu Wilaya 70 tuweze kukamilisha ujenzi huu wa vyuo vya VETA katika Wilaya zote nchini. Nakushukuru sana.
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali ya nyongeza. Kwanza; kwa kuwa changamoto ya miundombinu katika Chuo cha VETA cha Kitangali ni kubwa sana; na kwa kuwa wanafunzi wanaotoka sehemu hiyo wanatoka katika maeneo mbalimbali vijijini. Je, ni lini sasa Serikali itakamilisha mradi huo na kujenga mabweni kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka sehemu mbalimbali ikiwepo wanaotoka kwenye Jimbo la Mheshimiwa Maimuma Mtanda?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa changamoto ya vijana wanaomaliza Sekondari na Shule za Msingi imekuwa ni kubwa, vijana wengi wanamaliza shule na wengi wanatarajia sasa kwenda kwenye vyuo hivi vya VETA kupata elimu. Je, Serikali ina mkakati gani sasa wa kuhakikisha kwenye hivi Vyuo vya VETA vyote nchi nzima wanaweka miundombinu na mabweni ili watoto mbalimbali wanaomaliza shule kutoka vijijini waweze kwenda kwenye Vyuo vya VETA na kupata mafunzo na ujuzi wa mbalimbali? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI YA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza kwenye jibu langu la msingi kwamba katika mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali iliweza kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa baadhi ya mbiundombinu katika chuo hiki; na naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika mwaka wa fedha ujao, tutahakikisha kwamba maeneo haya ambayo ameyataja hasahasa katika hiki Chuo cha Kitangali kupitia mapato ya ndani ya VETA tutakwenda kuongeza miundombinu katika eneo hili ikiwemo pamoja na mabweni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye swali lake la pili, ni kweli tukiri kwamba tunajenga VETA katika wilaya zote Tanzania, lakini focus yetu kwanza ilikuwa ni ujenzi wa miundombinu ya vyuo hivi na tumeweza sasa kukamilisha karibu katika Wilaya 77 nchini. Kuna wilaya chache ambazo bado hatujazifikia, tunaamini katika kipindi kijacho kwanza tutakwenda kukamilisha kwenye wilaya hizi ambazo hazina Vyuo vya VETA, lakini vilevile kuhakikisha kwamba haya maeneo ambayo yana upungufu wa mabweni nao vilevile tunaweza kuwafikia kwa ajili ya kukamilisha miundombinu hii ili wanafunzi wetu, vijana wetu, waweze kupata mafunzo katika maeneo hayo.

Mheshimwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa sera ya Serikali ni kuwa na VETA kila wilaya. Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA Wilaya ya Maswa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Midimu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu ya swali la msingi, kwamba Sera yetu kama Serikali ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na Chuo cha VETA katika kila wilaya nchini ikiwemo na Wilaya ya Maswa. Namwomba tu Mheshimiwa Mbunge awe na subira katika hiki ambacho Serikali tunaendelea kutafuta fedha na tunaamini katika mwaka ujao wa fedha tutaweza kuzifikia baadhi ya wilaya lakini tutaipa kipaumbele vilevile Wilaya ya Maswa; kuhakikisha kwamba miongoni mwa vile vyuo vichache ambavyo vitapata fedha basi tuweze kutekeleza mradi huo katika Wilaya ya Maswa. Nashukuru sana.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa fursa hii ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati Chuo cha Ufundi Stadi cha Mangaria kilicho kwenye Kata ya Mamba Kaskazini na kukipa vifaa vya kufundishia?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Kimei kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyokwishaeleza awali kwamba Serikali bado tunaendelea na mchakato wa utafutaji wa fedha; kwanza tuweze kufanya ujenzi kwenye wilaya ambazo hazina hivi vyuo. Hata hivyo, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Dkt. Kimei, kwa vile ametaja suala la ukarabati katika Chuo hicho cha Mamba, nitamwomba tu baada ya kikao hiki cha leo tuweze kuonana baadaye ili kwanza tuweze kutuma timu yetu ya wataalam kwenda kule Mamba, iende ikafanye tathmini ya kina, tuweze kujua gharama za ukarabati ukaohitajika pale ni kiasi gani ili tuweze kuingiza kwenye mipango yetu na tukipata tuweze kukipa kipaumbele cha ukarabati chuo hiki. Nakushukuru sana.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Mwaka 2014 tuliweza kubadilisha Sheria ya Skill Development Levy ambapo zilikuwa asilimia nne zote ziende VETA kwa ajili ya kuboresha ujuzi na miundombinu ya VETA, lakini 2014 tulibadilisha kwa sababu by then tulikuwa hatuna VETA nyingi na sasa hivi Serikali imejenga VETA nyingi sana.

Je, Serikali sasa haioni ni wakati muafaka warudishe ile sheria tuibadilishe, hizi asilimia mbili ambazo zilipelekwa Bodi ya Mikopo kwa ajili kukopesha wanafunzi wa elimu ya juu ziweze kurudishwa VETA; zitumike kama ilivyokuwa imedhamiriwa awali?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Esther Matiko, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nishukuru kwa swali lake la msingi na kuona umuhimu wa taaluma hii ya VETA katika nchi yetu. Hata hivyo, kwanza nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Esther kwanza Serikali imekuwa ikipeleka ruzuku kwenye vyuo hivi, ruzuku zile za uendeshaji, ndiyo kwa maana unaona hata zile ada zake ziko chini sana kwa wanafunzi wa kutwa ni Sh.60,000 na kwa wale wa mabweni ni Sh.120,000. Kwa vile Mheshimiwa amezungumza habari ya sheria kwamba tuirejeshe hapa Bungeni ili tuweze kuirekebisha ili basi ile asilimia nne iweze kwenda kuongeza nguvu kwenye eneo lile la VETA.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tubebe ushauri wake Mheshimiwa Matiko twende tukaufanyie kazi, tufanye tathmini ya kina, tukiona kuna haja ya kuleta hiyo sheria hapa ili tuweze kubadilisha, tuweze kufanya hivyo. Nakushukuru sana.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Chuo cha VETA Mikumi ni chuo ambacho kilijengwa na Irish people kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na kwa nia njema kabisa Chuo kile tuliikabidhi Serikali. Tangu tumeikabidhi Serikali hakuna jitihada zozote za kujenga ama kukarabati miundombinu ya chuo kile hasa ukizingatia kwamba hali yake ni mbaya na hakina mabweni. Sasa nini kauli ya Serikali kuhusiana na ujenzi wa miundombinu hasa mabweni katika Chuo cha VETA?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la kaka yangu Mheshimiwa Londo, Mbunge wa Mikumi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Londo kwa ufuatiliaji wa karibu wa chuo hiki, siyo mara moja wala mara mbili tumeshawahi kukutana.

Mheshimwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Londo aridhie baada ya kikao hiki tuweze kukutana ili kuangalia kitu gani cha kufanya na vilevile tuweze kutuma timu kwenye eneo hili kwa ajili ya kufanya tathmini kama tutakavyofanya kwa Mheshimiwa Kimei, tuweze kufanya vilevile na kwake, kuangalia thamani ya ukarabati pamoja na uongezaji wa miundombinu kwenye eneo lile ili tuweze kutekeleza kwa wakati.

Mheshimwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa maelezo yake mazuri na vijana wetu wanasikia kwamba vipi uteuzi huo unavyoelekea. Baada ya maelezo hayo ningeomba kujua, makubaliano yao yanakuwa baina ya SMT na SMZ na wanateua hao vijana. Je, huduma za vijana hao kutoka Zanzibar hadi kufika chuoni huwa zinafadhiliwa na nani SMT au SMZ? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; vijana ambao tayari huwa wanawateua percentage kubwa ni wanaume kuliko wanawake na wanawake kwa kipindi hiki wanachacharika katika kupata elimu. Je, mtazamo huo unakuwa uko namna gani hata vijana wanawake wanakuwa kidogo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Fakharia, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye majibu yangu ya msingi; ufadhili kwa wanafunzi hawa wanaokwenda nje unafadhiliwa na nchi zile ambazo wanafunzi hawa wanakwenda na siyo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wala siyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo taratibu zote zile za kugharamia yale masomo huwa zinafanywa na zile nchi husika; ingawa sasa hivi sisi kama Serikali tumetoa fursa kwa Bodi yetu ya Mikopo kuweza kuwa na ile partial scholarship. Kuna baadhi ya wanafunzi ambao wanafadhiliwa kupitia Bodi zetu ile Zanzibar pamoja na hii ya Tanzania Bara kwa kupata partial scholarship; kwa hiyo utaratibu wake unakuwa hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili amezungumza habari ya wanaume kuwa wengi kuliko wanawake. Kwanza tukiri kwa sababu takwimu zinaonesha hapa wanaume ni asilimia 71 na wanawake ni asilimia hiyo 29. Hii inatokana na zile sifa kwa sababu hawa wanapochaguliwa kwenda kufanya masomo kwenye nchi hizi za nje kuna sifa ambazo zinaorodheshwa pale pamoja na ufaulu. Kwa hiyo, hii nadhani inatokana na ile namna gani wanaume wanafaulu kuliko wanawake.

Mheshimwa Naibu Spika, kwa vile Mheshimiwa Mbunge amelileta jambo hili hapa, basi sasa labda katika ugawaji hata zile nchi tutaziambia angalau ziweze kufanya fifty fifty ili na wanawake wengi waweze kupata fursa hii. Nakushukuru sana.
MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Nataka kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri mwelekeo wa Serikali kutafuta scholarship ni katika maeneo gani hususan ambayo inataka wanafunzi wetu waende kusoma. Vilevile ukiangalia idadi ya wanafunzi 400 kwa Taifa hili ni kidogo sana ambao wamepata scholarship. Je, mpango wa Serikali ni upi hasa wenyewe makusudi kutafuta scholarship nje ya nchi ili iweze kuongeza idadi ya Watanzania wengi waweze kwenda kusoma nje ya nchi? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, ingawa amezungumzia maeneo mawili ambayo kipaumbele ni vipi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie kwamba nchi hizi zinapotoa ufadhili kwenye hizi scholarship ni nchi zenyewe ndizo ambazo zina-detect, zinazoamua kwamba kozi gani ziende zikasomewe; lakini maeneo mengi sana yamekuwa ni maeneo ya Udaktari pamoja na Uhandisi. Pia naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika mwaka ujao wa fedha, sisi kama Serikali kwanza tumeviagiza vyuo vyetu vikuu viweze kuandaa au kupendekeza maeneo ambayo wanafunzi wa Kitanzania watakwenda kufanya masomo yao nje ya nchi.

Mheshimwa Naibu Spika, vile vile kama nilivyoeleza katika swali la nyongeza ni kwamba, Serikali kupitia Bodi ya Mikopo tumekuwa tukifadhili baadhi ya scholarship kwa kupata partial mikopo kwa ajili ya vijana wetu ambao wanakwenda kusoma nje. Kwa hiyo, huo ndiyo mkakati wetu kama Serikali na tutaendelea kufanya hivyo wakati upatikanaji wa fedha utakapokuwa mzuri. Nakushukuru sana.
MHE. LATIFA KHAMIS JUWAKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nikushukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya Serikali nilikuwa na swali moja la nyongeza.

Je, Serikali inatoa tamko gani sasa kuhakikisha kila muhitimu anapewa kipaumbele anaporudi au anapomaliza au anapohitimu katika elimu yake ya elimu ya juu ili aweze kupata mikopo katika halmashauri waweze kujiajiri na ili kuweza kurejesha mikopo kwa wakati? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Latifa Khamis Juwakali, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye majibu yangu ya msingi kwamba halmashauri zetu zimekuwa zikitenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo ambayo ni kwa ratio ya 4:4:2 asilimia nne kwa vijana, asilimia nne kwa wanawake na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikopo ile inatolewa kwa mujibu wa sheria na zipo kanuni ambazo tumekwenda kuzifanyia marekebisho mwanzoni ilikuwa vijana ni lazima wawe vijana 10 katika kikundi lakini hivi sasa ni vijana tano tu wanaunda kikundi wawe na shughuli maalum ya kufanya na mikopo ile wanaweza kupata.

Kwa hiyo, sisi kauli kama Serikali ni kuwahakikishia tu vijana kwamba wajiunge kwenye vikundi ambavyo ni vya ujasiriamali na sasa hivi haihitajiki kwamba iwe tayari umeshaanza kufanya shughuli hata kama una wazo tu lakufanyakazi fulani au shughuli fulani mikopo ile unaweza kupata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kauli yetu kwa vijana hawa wajiunge kwenye vikundi na kutumia kanuni zile zilizopo kuhakikisha kwamba halmashauri zetu zinawapata mikopo hii ili waweze kukidhi maisha yao, lakini waweze kurejesha mikopo ile elimu ya juu waliyoichukua. Nakushukuru sana.
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, majibu ya Serikali yamejikita kwenye mfuko mmoja tu ambao ni asilimia 10 ya mapato ya halmashauri, lakini Serikali inamifuko zaidi ya 45 ya kuondoa umaskini.

Je, haioni sasa ni wakati muafaka wa kuanza kuwakopesha wanafunzi kwa kutumia dhamana ya vyeti vyao ambavyo wamevipata vya kitaaluma ili kuondoa hili tatizo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Rashid Shangazi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Mheshimiwa Shangazi amezungumza suala la vyeti na mwanafunzi akishapata cheti haitwi tena mwanafunzi anaitwa muhitimu. Kwa hiyo, naomba nilifanyie marekebisho hapo namna gani wahitimu wetu sasa wanaweza kutumia vyeti vyao kuweza ku-access hiyo mikopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tuchukue ushauri wa Mheshimiwa Shangazi, twende tukaufanyie kazi tuufanyie na tathimini ya kina kwasababu sasa ni suala mtambuka si suala la Wizara ya Elimu peke yake hapa itaingia Wizara Fedha, lakini Wizara ya Vijana na Wizara nyingine ambazo zinashughulika na mambo ya vijana na mikopo kwa ujumla.

Kwa hiyo, naomba tuchukue ushauri wa Mheshimiwa Mbunge twende tukaufanyie tathimini ya kina ili tuweze kuangalia je, hivi vyeti vinaweza vikatumika kama bond ya kuwapatia mikopo vijana wetu. Nakushukuru sana.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kuna baadhi ya wizara kama Wizara ya Kilimo mbali ya kwamba kuna mikopo kwenye halmashauri na mifuko mingine wao wamekuwa wakitoa motisha kwa vijana ambao wana invest kwenye kilimo. Unapozungumzia tatizo la ajira kwa graduate ni kwenye Wizara yako.

Je, hamuoni kwamba kama wizara mnapaswa kuwa na fungu maalum kwa ajili ya kuwasaidia vijana graduate wanaoenda kujiajiri wenyewe kama Wizara kama ambavyo mnavyofanya kwenye Bodi ya Mikopo na maeneo mengine? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Ester Bulaya kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye swali la Mheshimiwa Shangazi, sisi Wizara ya Elimu jukumu letu ni kuhakikisha kwamba tunaratibu utaratibu wa utoaji wa elimu nchini. Wanafunzi wakishahitimu linakuwa si jukumu la Wizara ya Elimu, lakini ni jukumu la Serikali.

Kwa hiyo, kwa vile umezungumza habari ya motisha kwa vijana wetu wanaokamilisha masomo yao na kuangalia namna gani tunaweza tukaratibu taratibu zao za kuweza kujiajiri au kupata ajira, tuchukue ushauri huo, lakini Mheshimiwa Ester nadhani baada tu ya kikao hiki kuna umuhimu wa kukaa. Kwa sababu sasa hivi tunafanya mapitio ya mitaala yetu huenda kuna kitu kinakosekana nadhani na wewe unaweza kuwa na input na Mungu akipenda tarehe 13 tutakuwa na kongamano kubwa sana pale Dar es Salaam la kuhakikisha kwamba mitaala yetu ile inakwenda kujibu maswali ya Waheshimiwa Wabunge juu ya suala hili la ajira pamoja na suala la umahiri kwenye masomo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tuubebe ushauri wako twende tukaufanyie kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo tuweze kuangalia namna gani bora ya kuweza kulifanyia kazi jambo hili. Nakushukuru sana.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niulize swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa sasa hivi kuna malalamiko mengi sana kwa baadhi ya wanafunzi wanufaika wa hii mikopo ya vyuo vikuu wamekuwa wakimaliza madeni yao lakini bado mfumo unaendelea kukata madeni yao.

Je, Serikali inasemaje kuhusiana na hawa wanafunzi ambao bado wanaendelea kukatwa wakati wameshamaliza madeni?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Kabati kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niweze kumpongeza Mheshimiwa Kabati kwa ufuatiliaji wa karibu wa jambo hili nadhani ameshakuja ofisini si chini ya mara moja/mara mbili kwa ajili ya kufuatilia jambo hili.

Mheshimiwa Kabati kwanza nikuondoe wasiwasi, sasa hivi utaratibu wetu kila mnufaika wa mikopo ile ana akaunti yake na katika akaunti ile inakuwa inaonyesha kwamba kiasi gani amelipa na kiasi gani kilichobaki kwamba hajalipa. Kwa mantiki hiyo iwapo kama kuna wanufaika ambao wanaendelea kukatwa wakati wameshamaliza ile mikopo, tuna dawati letu la malalamiko la kuonesha kwamba yeye amekamilisha, lakini bado anaendelea kulipwa au anaendelea kukatwa kwenye mishahara au kwenye mafao yake mengine.

Kwa hiyo, hili suala tunaendelea kulifanyia kwa sababu ni suala la kimfumo, lakini nikuondoe wasiwasi wale wote ambao wamekatwa kwa namna moja au nyingine tumekuwa tukizirudisha fedha hizi baada tu ya kuleta hayo malalamiko ili kuweza kuwarudishia wao wenyewe. Nakushukuru.
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwanza naomba nishukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.

Kwa kuwa mahitaji ya Chuo cha VETA ni ya muda mrefu sana katika Jimbo la Vwawa na katika Mkoa wa Songwe, ni lini zabuni za ujenzi wa chuo hicho zitatangazwa ili kuhakikisha kwamba kwa kweli chuo hicho kinakamilika katika mwaka huo wa fedha?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa vijana wengi wa Jimbo la Vwawa na Mkoa wa Songwe wamekuwa wanahitaji sana hiki chuo na inaweza ikachukua muda mrefu sana kukimalisha kukijenga.

Je, Serikali itakuwa tayari kutumia majengo mbadala kutoa mafunzo hayo kwa vijana ambao wanahitaji mafunzo hayo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Japhet Hasunga, Mbunge wa Vwawa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye ujenzi tunakuwa na taratibu au models tofauti tofauti sana za ujenzi. Tuna model hii ya sasa hivi ambayo Serikali tunaitumia ya force account, lakini tuna model ile ya zamani ya kutumia wakandarasi. Kwa hiyo kwamba ni lini Serikali itatangaza zabuni itategemea na model ambayo tutakayotumia na mara nyingi sana kwa ujenzi wa vyuo vyetu vya VETA huwa tunatumia force account. Kwa hiyo, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge mara tu Mwaka wa Fedha ujao utakapoanza mwezi Julai, taratibu za ujenzi zitaanza kwa sababu sasa hivi tunaandaa zile tittle kwa ajili ya kumilikisha lile eneo kwenye Wizara ya Elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini eneo la pili amezungumza utayari wa kutumia majengo. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge baada ya Bunge hili tukufu tuweze kufanya ziara na timu yetu ya wataalam. Twende tukafanye tathmini ya hayo majengo anayoyazungumza ambayo tunaweza tukayatumia katika kipindi hiki kifupi wakati tunaendelea na ujenzi. Tutakapofanya tathmini hiyo na tukajiridhisha kwamba majengo hayo yanajitosheleza katika utoaji wa huduma hii, basi tunaweza tukafanya hivyo. Nakushukuru sana.
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni miaka mitatu sasa toka wananchi wa Tarafa ya Chamriho wameahidiwa kujengewa VETA na wameshatoa eneo bure ekari 55. Ni lini sasa hiyo VETA ya Tarafa ya Chamriho itajengwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Getere, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa juhudi za wananchi za kutenga eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA. Lakini nimuondoe wasiwasi na niwaondoe wasiwasi Waheshimiwa Wabunge wote ambao maeneo yao bado Vyuo vya VETA vya Wilaya havijajengwa, katika mwaka wa fedha ujao dhamira ya Serikali kama ilivyo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi, lakini kama ilivyo kwenye Sera kwamba tunakwende kujenga Chuo cha VETA katika kila Wilaya ikiwemo na Wilaya hii ya Mheshimiwa Getere katika mwaka ujao wa fedha tunaamini kabisa tutaweza kuanza ujenzi katika eneo hili. Nakushukuru.
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, katika Jimbo la Kilwa Kaskazini hakuna chuo chochote ambacho kimewahi kujengwa na Serikali. Je, ni lini Serikali itaweka mkakati wa kujenga Chuo cha VETA katika Jimbo la Kilwa Kaskazini?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Kilwa Kaskazini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyozungumza katika majibu yaliyopita ni Sera ya Serikali na ipo vilevile kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi, lakini ipo vilevile kwenye Dira ya Maendeleo ya Miaka Mitano na Dira ya Maendeleo ya Mwaka Mmoja kuhakikisha kwamba tunafikisha Chuo cha VETA katika kila Wilaya nchini ikiwemo na Wilaya ya hii ya Kilwa. Nimuondoe wasiwasi kaka yangu, ndugu yangu, katika eneo la Kilwa Kaskazini katika mwaka ujao wa fedha tunaamini chuo hiki katika eneo hili tunaweza kuanza ujenzi ili kuhakikisha vijana wetu katika eneo hili wanapata huduma hii ya elimu. Nakushukuru sana.
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya swali la nyongeza. Nishukuru commitment ya Wizara kuja kujenga Chuo cha VETA katika Wilaya ya Kilwa ambayo ina Majimbo mawili ya Kaskazini na Kusini. Pale Kilwa Kusini tuna Chuo cha Maendeleo ya Wananchi ambacho ni chakavu, kuna baadhi ya miundombinu inahitaji maboresho. Nini kauli ya Serikali katika eneo hili?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kassinge, Mbunge wa Kilwa Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, katika mwaka huu wa fedha unaoendelea kwenye vyuo hivi vya FDC Serikali ilitoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa zaidi ya bilioni 6.8. Lakini vilevile katika mwaka uliyopita wa fedha tumeweza kufanya ukarabati pamoja na ujenzi wa miundombinu.

Kwa hiyo, nikuondoe wasiwasi mchakato huu au taratibu hizi bado zinaendelea, tunaamini kabisa vifaa hivi vitafika Kilwa. Lakini tunaamini katika mwaka ujao wa fedha kwa vile programu ya kufanya ukarabati na ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika vyuo vya FDC navyo vilevile tunaendelea kufanyia kazi tunaweza kufika eneo lile na kuweza kufanya kazi vizuri. Nakushukuru sana.
MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi. Wilaya ya Mbinga pamoja na ukongwe wake haina Chuo cha VETA. Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA Wilaya ya Mbinga?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kapinga, kaka yangu, Mbunge wa Mbinga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tukiri kweli Wilaya ya Mbinga ni Wilaya kongwe, lakini nikuondoe wasiwasi kaka yangu nazani ulishawahi kufika mpaka ofisini kwa ajili ya kufuatilia suala hili na Mheshimiwa Mbunge nadhani nilikueleza mpango wetu kama Serikali ni kuhakikisha kwamba Wilaya zile ambazo hazijafikiwa na ujenzi huu wa Vyuo vya VETA katika mwaka ujao tunahakikisha kwamba tunazipa kipaumbele hasa hasa zile Wilaya kongwe ambazo zina miundombinu hafifu lakini vilevile ni ngumu sana kufikika. Kwa hiyo, nikuondoe wasiwasi eneo hili la Mbinga tunakwenda kulifanyia kazi na tunahakikisha tunajenga chuo katika eneo hilo.
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kuniruhusu na mimi niulize swali la nyongeza.

Ni lini Serikali itamalizia Kituo cha VETA kinachojengwa pale Iskizya, Uyui muda mrefu hakijakamilika?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Maige, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge katika fedha tulizozipata za UVIKO-19 zaidi ya bilioni 20 zilipelekwa kwenye maeneo ya vyuo vile 25 vilivyokuwa vinaendelea na ujenzi. Na ujenzi huo unaendelea, kama kutatokea mapungufu machache sisi kama Wizara tutakwenda kukamilisha eneo hilo la ujenzi. Kwa hiyo, nimuondoe wasiwasi ndani ya kipindi hiki kifupi kijacho tunakwenda kukamilisha ujenzi katika chuo kile cha Uyuwi. Nakushukuru sana.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwa kuwa Chuo cha VETA Nyasa ni chuo malkia kwa sababu Wilaya nzima haina chuo kingine zaidi ya kile na kile bado hakijaanza shughuli zake. Ni lini shughuli hizo zitaanza kwa sababu wananchi wanakiulizia sana?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Manyanya, Mbunge wa Nyasa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Manyanya kwa ufuatiliaji wa karibu, lakini nimuondoe wasiwasi katika kipindi cha mwaka huu wa fedha Serikali imetoa zaidi ya bilioni 8.8 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwenye vyuo vinne ambavyo vilikuwa vya Wilaya vilivyokuwa vimekamilika ambavyo ujenzi wake ulikamilika, lakini vifaa kulikuwa hakuna ikiwemo na chuo hichi cha Nyasa, Chuo cha Ruangwa, Chuo cha Kasulu pamoja na Chuo hiki cha Kongwa. Kwa hiyo, vifaa hivi tayari vimeshanunuliwa na tunaamini mara tu vifaa vitakapofika katika eneo hili la Nyasa ufundishaji au ufunguzi wa chuo hiki utaanza kwa kozi fupi lakini ifikapo Januari mwakani tutaanza kwa zile kozi ndefu. Nakushukuru sana.
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, iko dhamira ya Serikali ya kujenga vyuo hivi vya VETA katika Halmashauri zetu.

Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA katika Halmashauri ya Itigi?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Massare, Mbunge wa Itigi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tufanye marekebisho, vyuo hivi havijengwi kwenye Halmashauri, vyuo hivi vinajengwa katika Wilaya. Kwa hiyo, zipo Wilaya ambazo zina Halmashauri zaidi ya moja, kwa hiyo, naomba nifanye marekebisho madogo kwenye eneo hilo kwamba hatujengi kwenye Halmashauri, lakini tunajenga katika Wilaya. Kwa hiyo, nimuonde wasiwasi Mheshimiwa Mbunge katika Wilaya ya Itigi napo vilevile tutafikia eneo hili kuhakikisha kwamba tunajenga chuo katika eneo hilo kwa sababu ni Wilaya muhimu kujengewa chuo.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yenye matumaini makubwa, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa chuo cha VETA, Nyasa wakati huo kilikuwa na changamoto kubwa ya ulipaji wa fidia na kwa sababu kipo maeneo ambayo ni ya kimkakati, kwa hiyo eneo lake ni dogo kiasi kwamba uendelezaji wa chuo hicho unakuwa mgumu kwa hatua zinazofuata. Hakuna kiwanja cha mpira, lakini pia kwa fani nyingine kama za utalii ni ngumu kuendeleza hapo. Je, serikali ina mpango gani wa kuweza kuongeza eneo la chuo hicho?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; naomba kwa kuwa Wizara ni hiyo hiyo moja kupitia mradi wa EP4R, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilijenga jengo la utawala na maktaba ya ghorofa katika Shule ya Sekondari Mbamba Bay ambayo kila siku nalisemea hilo jengo.

Je, ni lini jengo hili litaweza kukamilika na ikibidi Mheshimiwa Waziri sasa ifikie mahali wakatembelee wakaone hali halisi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Manyanya, Mbunge wa Nyasa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala la eneo la chuo chetu cha VETA kuwa dogo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge mimi pamoja na timu yangu ya wataalam wa VETA tutafanya ziara katika chuo hicho ili kujiridhisha na ukubwa wa hilo eneo. Kama kutakuwa na uhitaji wa kuongeza eneo, nimwondoe hofu, tulishalifanya jambo hilo katika Chuo chetu cha Kipawa ambacho kilikuwa na eneo dogo, tumeweza kuongeza eneo, basi na hapa katika Chuo chetu hiki cha VETA tutafanya ziara lakini vilevile tutahakikisha kwamba kama kutakuwa na eneo linahitajika kuongeza, Serikali itaweza kuongeza eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali la pili katika shule hiyo aliyoitaja ya Sekondari ya Mbambabay kwamba Serikali ilishapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu. Pia, kuna hili jengo la utawala ambalo halijakamilika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Wizara yangu kwa kushirikiana na wenzetu wa TAMISEMI, tutafanya ziara katika eneo hilo. Vilevile, tumuagize Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyasa kuweza kufanya tathmini ya jengo hilo, kuona ni kiasi gani cha fedha kinahitajika ili basi Serikali iweze kupata tathmini hiyo na kuweza kuifanyia kazi ili jengo hili liweze kukamilika, nakushukuru.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niulize maswali mawili. Kwa kuwa Chuo hiki tayari kina technical na academics staff zaidi ya 231 wakiwemo zaidi ya Maprofesa 70. Pia huduma mbalimbali toshelezi wapo mpaka wanafunzi wenye mahitaji maalum. Ni kwanini sasa Serikali isitoe kibali chuo hiki kijitegemee na muda maalum wa uwangalizi wa vigezo hivyo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kuwa Mheshimiwa Rais wetu alipokuja katika Mkoa wa Iringa alipoongea na Wazee aliahidi kutoa fedha kupitia Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu kwa ajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali ya chuo.

Je, ni lini sasa Serikali itatimiza ile ahadi ya Mheshimiwa Rais kwa sababu hiki Chuo kinatakiwa kiwe fanisi katika Nyanda za Juu Kusini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ritta Kabati kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika ni kweli Chuo chetu kina Watumishia hao aliowataja Mheshimiwa Mbunge zaidi ya 231 wakiwepo Maprofesa hao 70 lakini kwa vigezo hivi siyo vigezo pekee ambavyo vinatumika kwa ajili ya kupandisha hadhi chuo hiki na naomba nimpe taarifa tu Mheshimiwa Mbunge, Maprofesa hawa waliopo wengi wao ni wale ambao wameazimwa kutoka katika Chuo Mama kile Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Kipekee wale ambao walioajiriwa na Chuo Kikuu cha Mkwawa pale kwa upande wa Maprofesa hatuna hata Profesa mmoja ambaye ameajiriwa kama Mwajiriwa wa chuo kile pale.

Mheshimiwa Spika, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwanza tumebeba ushauri wake, lakini naomba nimuhakikishie Serikali hivi sasa tumepata Mradi wa HEET ambao unakwenda kusomesha Maprofesa na Maprofesa wasaidizi zaidi ya 100 ambao tutahakikisha sasa baada ya mafunzo yao hawa, chuo hiki kinaweza kupandishwa hadhi kuwa Chuo Kikuu kinacho jitegemea.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la pili la upande wa majengo. Tumshukuru sana Mheshimiwa Rais lakini tumshukuru vilevile Waziri wa Fedha kwa upande wa mapato yetu ya ndani mwaka uliopita wa fedha na mwaka huu wa fedha tumeweza kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi pale wa majengo na mpaka hivi ninavyozungumza Wakandarasi wawili wako pale site ambae ni SUMA JKT pamoja na Salimu Construction. Salimu Construction anafanya ujenzi pale wa hostel na SUMA JKT wanafanya ujenzi wa library.

Mheshimiwa Spika, vilevile katika Mradi wetu wa HEET tumeishapeleka pale jumla ya dola za kimarekani milioni nane kwa ajili ya kuongeza miundombinu pamoja na majengo mbalimbali kukifanya Chuo kile kiwe na hadhi ya kupandishwa kuwa Chuo Kikuu kamili, nakushukuru.
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Nataka kuuliza Je, Serikali katika hivyo vyuo 36 itakavyojenga na Wilaya ya Ubungo nayo imo katika orodha hiyo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ambazo hazina vyuo hadi hivi sasa ni Wilaya 62 na katika bajeti yetu ijayo Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi katika Wilaya 36, ni ukweli usiokuwa na shaka kwamba siyo wilaya zote zitakazoweza kupata kwa hiyo tunaweka vigezo na vielelezo vya demand analysis ili kuhakikisha yale maeneo yenye uhitaji mkubwa ndio tunaweza kujenga kwanza halafu vingine tutakwenda kujenga katika mwaka ujao wa fedha, nakushukuru sana.
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa Wilaya ya Siha ina vijana wengi sana ambao hawajapata nafasi ya kuendelea na masomo ya juu.

Je, Serikali ina mpango gani katika hivi vyuo 36 na yenyewe kupata nafasi ya kujenga Chuo cha VETA? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Mbunge Viti wa Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza kwamba ujenzi huo unakwenda kwa awamu, kwa hiyo kuna maeneo tutayafikia na kwa vile tutaweka vigezo, cha msingi tutaangalia ule uhitaji mkubwa katika maeneo tutakayoyaainisha. Kwa hiyo nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwenye hili, kwa vile Wilaya ya Siha ina uhitaji mkubwa na vijana pale ni wengi kwa vyovyote vile Wilaya ya Siha tutaipa kipaumbele, nakushukuru sana.
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza naishukuru sana Serikali kwa majibu mazuri, niliomba kujengewa chuo na sasa ujenzi umeanza, naishukuru sana Serikali. Nina maswali mawili madogo ya nyongeza:

Mheshimiwa Naibu Spika, majengo ambayo yameanza kujengwa katika chuo kile ni majengo Tisa kati ya majengo mengi ambayo yatajengwa katika eneo hilo; Je, ni lini majengo hayo ambayo yapo katika mpango huo yataaanza kujengwa?

Swali la pili; ni lini ujenzi sasa utakamilika ili wananchi wa Wilaya ya Kakonko ambao wanasubiri chuo hiki kwa hamu sana utakamilika na mafunzo yaweze kuanza? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kamamba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli ujenzi wa vyuo hivi unagharimu zaidi ya shilingi bilioni tatu, kwa awamu ya kwanza tumetenga zaidi ya bilioni 1.5 kwa ajili ya majengo ya awamu ya kwanza ambayo ni majengo tisa na ujenzi huo umeanza mwezi wa Nane mwaka huu na ni ujenzi ambao tunatarajia utachukua kati ya miezi nane mpaka 12. Kwa hiyo, ni matarajio yetu ifikapo mwezi wa Sita au wa Saba mwakani majengo haya Tisa ya awamu ya kwanza yatakuwa yamekamilika na yatakapokamilika kwa sababu tumejenga kimkakati, tutahakikisha kwamba majengo haya yatakapokamilika chuo kiweze kuanza kutoa huduma hapohapo wakati tunaendelea na ujenzi wa awamu ya pili. kwa hiyo ujenzi wa awamu ya kwanza unatarajiwa kunako mwezi wa Sita, ama mwezi wa Saba mwakani utakuwa umekamilika then tutaanza ujenzi wa awamu ya pili kwa kadri ya upatikanaji wa fedha utakavyoruhusu. Nakushukuru
MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nitumie fursa hii kuipongeza sana Serikali kupitia Wizara ya Elimu, kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini, hususan katika masuala ya kazi ya masomo ya kazi za mikono.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la nyongeza ni moja tu. Kwa vile Baraza la Taifa la Mitihani pamoja na Elimu ya Juu ni masuala ya Muungano au ni mambo ya Muungano, na kwa madhumini ya kuwajengea msingi wa aina moja, vijana wetu wote wa Kitanzania. Je, Serikali ya Muungano kupitia Wizara ya Elimu inashirikiana vipi na Wizara ya Elimu Zanzibar ili kuhakikisha kwamba misingi yao ya elimu inakuwa ya aina moja na waweze kufanya mitihani ya aina moja? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Giga Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu kwamba wakati wa uandaaji wa mitaala hii, uratibu ulifanyika kwa kutumia taasisi zetu zote mbili ile Taasisi ya Elimu Zanzibar pamoja na Taasisi ya Elimu ya Tanzania Bara. Vilevile Wajumbe wa Kamati waliohusika katika marekebisho ya mitaala hii walitoka katika pande zote mbili za Muungano, kwa maana ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile maoni juu ya mtaala huu yalipokelewa katika pande zote mbili za Muungano. Tulifanya makongamano pamoja na mikutano kule Zanzibar, vilevile tulifanya makongamano na mikutano mbalimbali huku Tanzania Bara. Kwa hiyo, nimuondoe wasiwasi hili limezingatiwa kwa kiasi kikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, tuliweza kuwasilisha rasimu hii ya mitaala kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kabla ya mitaala hii haijaenda kwenye ithibati nyingine. Nimwondoe wasiwasi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tutaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania Bara katika kuhakikisha kwamba mitaala hii inatekelezwa na wenzetu vilevile wa Zanzibar nao vilevile wafanye mapitio ya mitaala yao, ndiyo itakayokwenda kutekelezwa na tutakuwa sasa tunakwenda pamoja. Nakushukuru sana.
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa majibu ya Serikali; pamoja na majibu ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

(a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwabaini wale watanzania wenye umri wa zaidi ya miaka 35 ambao hawako katika programu ya Re-Entry na zile programu afua zingine wasiojua kusoma na kuandika ili waweze kufikiwa?

(b) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikishwa kwamba, shule za msingi na shule za sekondari zote zinakuwa na maktaba ili kusudi wanafunzi waweze kujisomea?)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza la Mheshimiwa Toufiq, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwisha kueleza katika majibu ya swali la msingi. Serikali inazo kwanza takwimu za kutoka NBS zinazotuthibitishia uwepo wa watu wasiojua kusoma na kuadika. Ongezeko hili la watu wasiojua kusoma na kuandika limekuwa likipungua kutoka asilimia 78 mwaka 2012, mpaka asilimia 83 katika Sensa ya mwaka 2022.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo naomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa vile tayari sasa tunafahamu idadi hii au takwimu hizi, Serikali kupitia mpango mikakati hii ambayo nimeitaja ikiwemo na mpango wa Serikali wa Uwiano katika Elimu ya Watu Wazima na Jamii unaojulikanika kama MKEJA, ndio ambao utahakikisha sasa idadi hii ya Watanznaia wasiojua kusoma na kuandika, wale wenye umri zaidi wa miaka 35 tunaweza kuwafikia.

Mheshimiwa Spika, pia katika eneo la pili la suala la shule zetu za msingi na sekondari kuwa na maktaba, suala hili tayari Serikali imeshalifanyia kazi. Katika miundombinu ambayo inajengwa sasa hivi katika Shule zetu za msingi pamoja na sekondari ni lazima kuwe na jengo la maktaba, nakushukuru sana.
MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Spika, kwa maelezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri tuna zaidi ya asilimia 16 ya Watanzania ambao hawajui kusoma na kuandika. Sasa nilitaka kujua Mkakati wa Serikali wa kuhakikisha tunatenga bajeti kwenda kuhudumia Watanzania ambao wanapata elimu kutoka kwenye mfumo usio rasmi kama vile, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ambao kwa sasa hawapati ruzuku, nakushukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante na naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Tweve, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Tweve anatoa ushauri kwamba, Serikali tuweze kupanga bajeti kupitia Taasisi yetu ya Elimu ya Watu Wazima. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa, tutakwenda kufanya tathmini ya kina namna gani tunaweza kutenga bajeti kwenye Taasisi yetu ya Elimu ya Watu Wazima, ili kuweza kulifikia kundi hili la watu wasiojua kusoma na kuandika.
MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Serikali, upi sasa mkakati wa haraka zaidi kuhakikisha tunawanusuru watoto wadogo ambao wanapatikana hususan katika jamii za wafugaji na wavuvi ambao hawajui kabisa kusoma na kuandika, kuweza kuwanusuru watoto hao ili waweze kujua kusoma na kuandika?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Martha, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika maboresho ya mtaala ambayo tuliyapitisha mwaka jana, unakwenda kuchukua ngazi zote za watoto wetu kuhakikisha kwamba wanakuwa shule. Katika sera pamoja na mitaala hii ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha kwamba, yule mtoto ambaye tayari ameshafika umri wa kwenda shule aweze kwenda shule.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, nitoe tu maelekezo kwa Wakurugenzi wetu wote wa halmashauri, Wakuu wa Wilaya ambako ndiko hawa watoto waliko, iwe eneo la wafugaji au iwe eneo la wavuvi, kuhakikisha vijana wetu ambao tayari wameshafikia umri wa kwenda shule waweze kuandikishwa na kuweza kukaa shuleni kwa ajili ya kusoma, nakushukuru.
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na naomba kwanza kwa ruhusa yako niishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kwa kutuletea fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya yetu ya Namtumbo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali; kwa kuwa mradi huu wa majengo yale ya mabweni ukikamilika katika Chuo chetu cha VETA utaweka wanafunzi wengi pale katika Chuo cha VETA na watahitaji maji ya kutosha; je, Serikali katika component ya bajeti inayokuja inaweza ikaweka mradi wa kuchimba kisima kwa ajili ya matumizi ya chuo kile pale cha VETA Namtumbo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa Serikalini kuna magari ambayo yamepata ajali yanaweza kutengenezeka Serikalini na Taasisi za Serikali na yanakaa tu bila kufanyiwa maamuzi yanaharibika; je, Serikali inaweza ikafanya uamuzi wa kupeleka katika Vyuo vya VETA yakawa magari hayo ni ya kufundishia wanafunzi wanaofanya ufundi wa utengenezaji magari katika maeneo ya panel beating, urekebishaji wa muundo wa ufundi wa umeme wa magari lakini pia na ufundi wa injini na vifaa vinginevyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni azma ya Serikali hasa hasa Serikali hii ya Awamu ya Sita kuhakikisha kwamba huduma zote muhimu zinakuwepo katika vyuo vyetu vile vya zamani, lakini pia hivi vipya ambayo tunavyovijenga.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu kwamba tayari Wizara imeshawasiliana na wenzetu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira kule Namtumbo na UWASA na kuwaomba watuletee bajeti ya uchimbaji wa kisima hicho na tayari wameshatuletea bajeti hiyo ambayo inagharimu shilingi milioni mia moja, laki mbili na arobaini na nane laki tano na sabini na sisi pasipokuwa na shaka tutaweza kuingiza sasa katika bajeti inayokuja 2024/2025 ili wakati majengo haya yakikamilika basi na hiki kisima kiweze kuwa tayari.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili amezungumza suala la magari. Mheshimiwa Mbunge naomba nikuhakikishie na Bunge lako Tukufu kwamba Wizara inayo utaratibu huu, ina utaratibu wa kupeleka magari haya yaliyochakaa, lakini vilevile hata magari mapya na kwa vile amezungumzia habari ya magari hapa utaratibu huo upo na magari haya hupatikana kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo zile za TASAF, TANROADS na taasisi nyingine za Serikali. Kwa hiyo, tutafanya kwa kadri itakavyokuwa imewezekana, nakushukuru.
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itapeleka fedha zaidi katika Chuo cha VETA cha Urambo ili tupate majengo zaidi tuongezee stadi zaidi za ufundi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mama Margaret Sitta, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, chuo chetu kile cha VETA, Urambo katika mwaka wa fedha ule uliopita tulipeleka fedha pale kwa ajili ya kuongeza baadhi ya miundombinu lakini vilevile kufanya ukarabati. Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Margaret Sitta kwamba katika mwaka huu tena unakuja wa 2024/2025 tutatenga fedha kama tulivyofanya mwaka uliopita kwa ajili ya kuongeza miundombinu lakini vilevile kufanya ukarabati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi hii tunaifanya kwa Vyuo vyote pale Urambo tumefanya, lakini Wanging’ombe pale tumepeleka fedha, Newala kule napo vilevile tumepeleka kwa hiyo tutafanya kama tulivyofanya mwaka uliopita wa fedha, nakushukuru sana.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi; je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa bweni la Songwe Girls Secondary School ambayo inachukua wanafunzi wa majimbo sita ndani ya Mkoa wa Songwe?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, hii ya shule na ujenzi wa bweni kidogo naomba nilichukue hili la Mheshimiwa Sichalwe kwa sababu ni ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari.

NAIBU SPIKA: Wewe mjibu tu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru na naomba nijibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Sichalwe, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna utaratibu wa ujenzi wa mabweni katika shule zetu na tunafahamu kwamba tuna mradi wetu mkubwa sana wa SEQUIP ambao ni mradi ambao una zaidi thamani ya zaidi ya trilioni 1.1.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa vile mgao wa awamu inayofuata bado haujafika nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika ugawaji huo tutazingatia mahitaji ya bweni hilo pale na mimi bahati nzuri nilifanya ziara nikaenda nikaona nimhakikishie kwamba tutajitahidi kuweza kuweka fedha kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali imewekeza kwenye ujenzi wa Vyuo vya VETA, lakini kwa uzoefu nimeona masomo mengi yanayotolewa ni yale masomo ambayo ni ya ushonaji, ujenzi na ufundi seremala; lakini ni upi mkakati wa Serikali kuongeza idadi ya masomo yenye soko la sasa kama ufundi wa magari ya umeme, ufundi wa mabomba plumbing na mambo mengine ili iweze kusaidia Watanzania walio wengi na vijana waweze kupata soko kwenye Taifa letu? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru na naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sanga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tuna course zile ambazo ni za general course ambazo katika kila chuo kinatoa, lakini mpango wetu wa sasa kama Serikali tumewaagiza wenzetu wa VETA kuhakikisha kwamba tunakwenda ku-customize zile course kulingana na shughuli za eneo husika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mpango huo tunao na hivi sasa au tuko mbioni kuhakikisha kwamba tunaandaa mitaala ambayo inaendana na shughuli za jamii mahali vyuo vilipo, nakushukuru sana.
MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, napenda kufahamu mkakati ambao Serikali inao katika kuajiri watumishi ambao sio walimu. Kwa mfano, pale chuoni hakuna matron, hakuna patron, hakuna dereva wala wapishi, mkakati ukoje ili huduma ziweze kutolewa kwa ukamilifu katika chuo kile?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili. Kupitia majibu ambayo Serikali imeyatoa, imeonesha kwamba fani ziko tatu, na ni kweli fani tatu tu ambazo zinatolewa kati ya fani nyingi ambazo tunatarajia zitolewe ili wanafunzi wengi au wananchi wengi wapate nafasi ya kupata ujuzi. Mfano, hakuna fani ya mafundi magari, hatuna fani ya ujenzi, hatuna fani ya uunganishaji wa vyuma pamoja na mabomba. Mpango wa Serikali wa kuongeza fani nyingine ukoje ili kuwakwamua wananchi wa Newala ambao wanahitaji fani hizi ili waweze kujiendeleza kimaisha? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, nikijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Maimuna kuhusiana na suala la watumishi wasiokuwa walimu, naomba nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Maimuna kwamba kunapo mwezi wa Tatu mwaka huu, 2024 tayari tulishatangaza nafasi za watumishi wasiokuwa walimu kwa vyuo vyetu vyote vya VETA. Kwa hiyo, mara tu baada ya mchakato huu kukamilika, baadhi ya watumishi watakaopatikana tutawapeleka katika chuo hiki cha Kitangari. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la pili kuhusiana na suala la kuongeza fani, Mheshimiwa Maimuna nadhani anafahamu kuna maboresho ambayo tunaendelea pale kwa maana ya ujenzi wa mabweni na ukarabati wa karakana pamoja na madarasa. Kwa hiyo, tutaendelea kuboresha kwanza miundombinu na baada ya uboreshaji huo wa miundombinu, utaratibu wa kuongeza fani sasa tutaweza kuufanya ili uweze kuendana na miundombinu iliyopo katika eneo hilo. Ahsante.
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri. Kwa kuwa mafunzo ya VETA yamekuwa ni mkombozi kwa vijana waliokosa kuendelea na masomo ya juu na kwa wale wasikuwa na ajira, kwa nini, Serikali isiondoe mzigo huu wa ada kwa hawa wanyonge?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Serikali imeweka utaratibu gani wa kuhakikisha kwamba, wenye nia ya kupata mafunzo haya wanapata mafunzo haya bila kubugudhiwa licha ya kuwa wamekosa ada?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, nikijibu maswali mawili ya nyongeza kwa pamoja ya Mheshimiwa Mchungahela kama nilivyoeleza kwenye majibu ya swali la msingi ni kwamba, tumeweza kutoa ruzuku kwenye mafunzo haya na kupunguza ada kwa kiasi kikubwa, lakini kwa vile Mheshimiwa Mbunge anatoa ushauri kwamba tuendelee kupunguza, basi kwanza nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Spika, ukipitia rejea ya Bodi ya Mikopo ambayo mwanzoni ilikuwa inatoa tu kwa elimu ya juu, lakini kwa sasa tumeanza kushuka kwenda kwenye elimu ya kati, kwa hiyo, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anapata elimu kwa utaratibu wowote ule.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tutaangalia ushauri wake wa kwamba, je, ifutwe au tuipeleke kwenye ule utaratibu wa Bodi ya Mikopo na hawa wanafunzi wasiojiweza kwenye maeneo haya ya ufundi stadi, ili waweze kupata mikopo na waweze kuendelea na elimu yao. Nashukuru sana.
MHE. DKT.OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana na ninaishukuru Serikali kutupa Kituo cha Ndolage.

Wilaya ya Muleba ni miongoni mwa Wilaya kubwa hapa nchini yenye Majimbo mawili ya uchaguzi na ina shule nyingi za sekondari zaidi ya 67. Kila mwaka zaidi ya watoto 3,000 hawaendelei na Kidato cha Tano baada ya Kidato cha Nne. Ninaomba kupata commitment ya Serikali ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA chenye hadhi ya Wilaya kama zilivyo Wilaya nyingine? (Makofi)

Swali la pili, Serikali ina mkakati gani wa kutupatia Vyuo vya VETA ambavyo vinamilikiwa na Taasisi za Dini na watu binafsi kuvipatia ruzuku ya kujiendesha ili viendelee kuwasaidia na kuwaelimisha watoto wetu katika Wilaya zetu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Kikoyo, Mbunge wa Muleba Kusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu ya msingi kwamba Serikali inafanya ujenzi wa Vyuo hivi kwa awamu. Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Muleba Kusini kwamba katika bajeti ya Serikali imetengwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyuo 36 vya VETA katika Wilaya mbalimbali nchini. Kwa vile tunakwenda kuweka vigezo vya namna gani tunaweza kwenda kugawa vyuo vile 36, ninampa tu taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba Wilaya hii ya Muleba ina Majimbo karibu matatu na idadi ya wananchi ni kubwa na hivyo ni miongoni mwa vigezo ambavyo tutaviweka kulingana na ule uhitaji. Kwa hiyo nikuondoe wasiwasi katika mwaka ujao wa fedha kati ya vyuo vile 36 na Muleba itakuwa ni miongoni mwa hizo.

Mheshimiwa Spika, katika eneo lake la pili kuhusu vyuo vya binafsi kuvipa uwezo au ruzuku ya kujiendesha, utaratibu huu haukuwepo lakini Mheshimiwa Mbunge kwa vile ametoa hapa mapendekezo, naomba tuchukue mapendekezo haya tuende tukayafanyie tathmini ili tuweze kuangalia namna gani Serikali inaweza cheap in kwa sababu wanaosoma humu ni watoto wa Kitanzania.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. PHILLIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Songwe ni miongoni mwa Wilaya zenye stadi za kilimo, madini, uvuvi na ufugaji na inakidhi vigezo vyote vya kupata Chuo cha VETA kwa sababu tunalo eneo kubwa na tayari eneo hilo lina Hati Miliki ya chuo cha VETA toka mwaka 2011.

Je, katika bejeti hii iliyotengwa mwaka kesho Serikali itanipa chuo cha VETA Wilaya ya Songwe?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mulugo, Mbunge wa Songwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mulugo kwa vile tayari wananchi wameshajitolea au Halmashauri au Wilaya eneo na miongoni mwa vigezo au vielelezo ambavyo tutavizingatia kwenye yale maeneo ambayo tayari walishatenga maeneo, yameshapimwa na yana hati. Kwa vile, Mheshimiwa Mulugo wewe kwako tayari kuna eneo limeshapimwa na lina Hati, basi katika ugawaji wa vile vyuo 36 nadhani hiki kitakuwa ni kigezo muhimu kuhakikisha kwamba wananchi wa Songwe wanaweza kupata chuo hiki.

Nikuondoe wasiwasi vilevile katika bajeti yetu miongoni mwa Mikoa ambayo haina vyuo vya VETA ni pamoja na Mkoa wa Songwe. Kwa hiyo, tunakwenda kujenga vilevile chuo cha kikubwa sana pale Songwe ambacho kitaweza sasa kuchukua wanafunzi wote kutoka wilaya zile za Mkoa wa Songwe.
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniona niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Je, ni lini Serikali itafanya maboresho ya chuo cha VETA Gela kilichopo Wilaya ya Misenyi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante.
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Oliver, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni utaratibu wa Serikali kufanya ukarabati pamoja na upanuzi kwenye vyuo vile vya zamani, kazi hii tulianza na vyuo vyetu vya FDC. Tulikuwa na vyuo vya FDC 54 tumefanya upanuzi pamoja na ukarabati na ununuzi wa vifaa. Hivi sasa tunakwenda kwenye vyuo hivi vya VETA vya zamani, ukienda pale Karagwe tayari kazi hii tulishaianza Mheshimiwa Mbunge. Kwa hiyo, sasa kwenye vyuo vingine na tumetenga fedha kwa ajili ya kufanya ukarabati pamoja na upanuzi kwenye vyuo mbalimbali vya VETA vile vya zamani.
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa hii nami niulize swali la nyongeza.

Kwanza naishukuru Serikali kwa kutujengea chuo cha VETA Wilaya ya Namtumbo, pia mmetuletea vifaa vya kufundishia umeme, kompyuta, vifaa vya kushonea na mitambo lakini hatukupata vifaa vya kufundishia ufundi selemala.

Je, Serikali inaweza kutuletea pia vifaa vya kufundishia ufundi selemala? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Vita Kawawa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali tayari iko kwenye mkakati na kwenye bajeti yetu inayokuja mwaka wa fedha 2022/2023, tumetenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa. Tumeshafanya hivyo, tulitenga mwaka huu zaidi ya Bilioni 6.8 kwa ajili ya vyuo vya FDC, vilevile tumetenga kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwenye vyuo 25 hivi ambavyo tunakwenda kuvimalizia vilivyokuwa vinaendelea na ujenzi, vilevile kwenye vyuo vile vya zamani ambavyo vilikuwa bado havijapata vifaa tutapeleka vifaa vya kujifunzia na kufundishia vikiwemo na hivi vifaa kwa ajili ya uselemala.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza naishukuru Serikali kwa ujenzi wa chuo cha VETA Wilaya ya Rufiji na Wilaya ya Mafia.

Kwa kuwa, Serikali imetenga Bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya VETA kwa Wilaya 36; na kwa kuwa ndani ya Mkoa wetu wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo na Wilaya ya Mkuranga hakuna chuo cha VETA.

Je, Serikali inatuambiaje kama kuna uwezekano wa kupata chuo kutoka na vyuo 36 vitakavyojengwa?

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Subira Mgalu, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Pwani, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli anachozungumza Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mgao uliopita miongoni mwa wilaya za Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Mafia pamoja na Rufiji vilipata vyuo hivi lakini wilaya nyingine kama Mkuranga, Kisarawe pamoja na Bagamoyo bado havijapata vyuo hivyo.

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kama Wilaya hizi zitakuwa tayari zimetenga maeneo yaliyopimwa tayari yana Hati kama nilivyozungumza wakati najibu swali la Mheshimiwa Mulugo vitapata kipaumbele. Kwa hiyo, jukumu kubwa hapa ambalo ninakupa Mheshimiwa Mbunge ni kuhakikisha mnaweza kutenga maeneo kwa haraka ili kwamba wakati tunajaribu kutenga zile fedha maeneo haya yaweze kufikiwa kirahisi.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Kwa jinsi ambavyo mtiririko wa bajeti unaendelea kila mwaka na kwa kuwa kuna mahitaji makubwa ya ujenzi wa VETA, na kwa kuwa kuna baadhi ya Wilaya hapa nchini, kuna taasisi za dini zina vyuo vya ufundi. Je, Serikali sasa hamuoni upo umuhimu wa kuingia kwenye mfumo wa PPP na hizo taasisi ili wananchi wetu ambao wanahitaji ujuzi huo waweze kwenda VETA?(Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Cecilia Paresso, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza tumshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa mapendekezo au mawazo haya muhimu. Kimsingi utaratibu huu kwa hivi sasa Serikalini haupo au hatuna, kwa vile ni mapendekezo tunaomba tuchukue mawazo haya, tuende tukayafanyie kazi, tufanye tathmini ya kina, tuweze vilevile kukaa na wakuu hawa wa taasisi hizi, tuweze kuangalia namna gani tunaweza tukaendelesha vyuo hivi labda kwa mwendo ule wa PPP.

Mheshimiwa Spika, nakushuru sana.
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana; naomba kuuliza swali. Kwa kuwa chuo cha VETA kilichopo Temeke ni chuo cha Kimkoa kwa Mkoa mzima wa Dar es Salaam na sasa vijana ni wengi sana katika Mkoa wetu wa Dar es Salaam.
Je, mna mkakati gani wa kujenga vyuo vya VETA katika Wilaya zetu zote hasa katika Wilaya ya Temeke?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Dorothy Kilave, Mbunge wa Temeke, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu yangu ya msingi, kwamba Serikali inajenga vyuo hivi kwa awamu. Katika awamu zilizopita tumeshaweza kujenga katika Wilaya 77 nchini na Wilaya zilizobaki ni Wilaya 62.

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka ujao tunakwenda kujenga katika Wilaya 36. Tafsiri yake ni Wilaya zitakazobaki ni around kama Wilaya 25 au 26 hivi. Tunaamini katika mwaka wa fedha 2023/2024 tunakwenda kumaliza katika Wilaya zote. Kwa hiyo, nikutoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge hata kama hutakuwepo katika mgao huu wa hizi Wilaya 36 lakini tunaamini katika mwaka ujao 2023/2024 kwa vyovyote vile Wilaya zote tutakuwa tumekamilisha ikiwemo na Wilaya ya Temeke.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Je, ni lini Serikali itajenga chuo cha VETA kwa ajili ya Wilaya ya Mtwara kwa sababu kile kilichopo kilijengwa kwa ajili ya Mkoa wa Mtwara na Wilaya ya Mtwara ina Halmashauri Tatu na Majimbo Matatu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Abdallah Chikota, Mbunge wa Nanyamba kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli anachozungumza Mheshimiwa Mbunge, pale Mtwara kuna chuo cha Mkoa wa Mtwara ambacho kipo kwenye Wilaya ya Mtwara, katika chuo kile tafsiri yake ni kwamba kinahudumia Wilaya nzima ikiwemo Jimbo la Mtwara kwa maana ya Mtwara yenyewe, Manispaa pamoja na Jimbo la Nanyamba.

Mheshimiwa Spika, kwa vile sasa hivi mkakati wetu wa Serikali ni kuhakikisha kwamba tunakwenda kujenga kwanza kwenye kila Wilaya nchini, baada ya kukamilisha mchakato huu wa kujenga katika kila Wilaya sasa tunaweza kufikiria yale Majimbo au zile Wilaya ambazo zinakuwa na Majimbo mengi kuweza kufikia sasa yale Majimbo mengine ambayo yapo mbali na Makao Makuu ya Mkoa. Kwa hiyo, hili Mheshimiwa Chikota nakuomba tu nikuhakikishie kwamba tukamilishe kwanza ujenzi wa kila Wilaya ipate halafu baada ya hapo tutakwenda kwenye hizi Halmashauri au Wilaya ambazo zina Majimbo mengi.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Kwa kuwa, changamoto moja wapo ambayo inakabili hivi vyuo vya VETA ni upungufu mkubwa wa Walimu, kwa sababu tunategemea na vyuo vingi zaidi.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuandaa walimu kwa ajili ya vyuo hivyo na vyuo vya ufundi kwa ujumla?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Manyanya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli anachozungumza Mheshimiwa Mbunge kwamba, tuna changamoto kubwa sana ya Walimu, lakini sisi kama Serikali kama Wizara nimwondoe hofu Mheshimiwa Manyanya tayari tumeshaifanyia kazi. Kwanza, kwenye ajira hizi ambazo zimetangazwa/alizozitoa Mheshimiwa Rais hivi karibuni sisi Wizara ya Elimu tumepata ajira 2,035 na kati ya ajira hizi 2,035 ajira 1,000 tumesema ziwe za Walimu wa vyuo hivi vya ufundi. Kwa hiyo, tunakwenda kupunguza changamoto kwenye maeneo haya ambayo tunapeleka hivi vyuo vipya kwa kuhakikisha tunaajiri hawa Walimu wapya 1,000. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimwondoe wasiwasi vilevile Chuo chetu cha Walimu wa Ufundi pale Morogoro tumekikarabati na tumekiongezea miundombinu kwa kuhakikisha kwamba kinaongeza udahili wa Walimu hawa, ili kuhakikisha kwamba upungufu wa Walimu kwenye vyuo hivi unapungua.

Mheshimiwa Spika, naomba vilevile nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika mapitio ya mitaala tunayofanya sasa hivi tunakwenda kuongeza component kwenye hivi vyuo vya kawaida vya ualimu kuhakikisha kwamba tunakuwa na component vilevile ya ufundi, ili Walimu wale wasiwe tu wanakwenda kufundisha kwenye shule zetu, lakini vilevile waweze kwenda kufundisha kwenye vyuo vyetu hivi vya ufundi.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya swali la nyongeza. Jimbo la Kilwa Kusini halina Chuo cha VETA na hakuna mpango wa Serikali kujenga Chuo cha VETA badala yake tuna Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, lakini miundombinu yake ni chakavu na haitoshelezi. Tuna upungufu wa bwalo, viwanja vya michezo pamoja na maabara ya kompyuta. Nini mpango wa Serikali wa kukiimarisha Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Ally Kassinge, Mbunge wa Kilwa Kusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli anachozungumza Mheshimiwa Mbunge kwamba pale katika Jimbo la Kilwa Kusini tuna Chuo chetu cha FDC, tulifanya ukarabati kidogo, lakini bado kuna upungufu wa majengo haya aliyoyataja ikiwemo pamoja na bwalo. Nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Kassinge, katika mwaka ujao wa fedha tumetenga fedha kwa ajili ya kuongeza miundombinu au upanuzi wa vyuo hivi kikiwemo hiki chuo chako, lakini vilevile na chuo cha pale Kisarawe ambacho sasa hivi kinaendelea na ujenzi, pamoja na kule Kigamboni kwa Mheshimiwa Dkt. wa Kigamboni kule tunakwenda kuviongezea miundombinu hii ya majengo ili kuweza kudahili wanafunzi wengi, lakini kutengeneza mazingira mazuri na salama ya watoto wetu kuweza kusoma.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu ya Naibu Waziri yanayoonesha angalau matumaini, nina swali moja la nyongeza. Je, atatuhakikishia kwamba ukarabati utaendana sambamba na kuweka vifaa vya ufundishaji katika vyuo vyote ikiwemo vyuo vya kati? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Ntara, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyozungumza kwenye jibu la msingi kwamba, tumepata mkopo wa zaidi ya dollar milioni 425, matumizi makubwa ya mkopo huu ni kuhakikisha tunakwenda kuviongezea miundombinu vyuo vyetu hivi vikuu, lakini vilevile tunakwenda kuboresha mitaala na kuanzisha mitaala mipya na vilevile tunakwenda kusomesha Walimu/Wahadhiri kwa ajili ya vyuo hivi. Sambamba na hivyo tunakwenda kununua vifaa kwa ajili ya vyuo vikuu vyote vya umma nchini. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi hili eneo la vifaa nalo vilevile limezingatiwa. Kwa vile amezungumzia vilevile vyuo vya kati, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge vyuo vya kati navyo tumevitengenezea mkakati wake maalum kabisa.

Mheshimiwa Spika, kwanza tuna mradi wetu wa EASTRIP ambao zaidi ya Dollar za Kimarekani milioni 75 tumeweza kusaini kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivyo lakini vilevile kwa ajili ya ununuzi wa vifaa. Kwa hiyo, sambamba na huu mradi wetu wa HEET ambao utashughulikia vyuo vikuu, lakini tuna miradi mingine midogo midogo ambayo itashughulikia vyuo hivi vya kati kwa kuhakikisha kunakuwa na wahadhiri wa kutosha na vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwenye vyuo vyetu.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa vile Serikali ina mpango wa ukarabati wa vyuo vikuu hapa nchini. Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati vyuo vikuu vilivyopo kule Zanzibar? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Maryam Mwinyi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwenye majibu yangu ya msingi kwamba, mkopo huu wetu wa HEET (Higher Education for Economic Transformation) unakwenda kuboresha maeneo yote ya vyuo vikuu vya umma vikiwemo na vile vya Zanzibar. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi chuo chetu kile cha SUZA Zanzibar kimepata gawio katika gawio hili la mradi wetu wa HEET lakini taasisi yetu ile ya Marine Science ya Zanzibar ambayo inasimamiwa na Chuo chetu cha Dar es Salaam nayo vilevile sio tu inakwenda kuboreshwa bali inakwenda kujengwa upya. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi Zanzibar nayo tumeizingatia kwenye mgao huu na tutahakikisha kwamba kazi hii inakwenda kufanyika kwa haraka.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Waziri Chuo Kikuu cha Muhimbili majengo yake ni chakavu eneo ni dogo wanafunzi ni wengi kila mwaka. Je, Serikali inatoa kauli gani kuitanua Chuo Kikuu cha Madaktari Muhimbili ili kiweze kukidhi haja ya kututolea madaktari wengi nchini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Nahato, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwanza tukiri kwamba Chuo chetu cha Muhimbili eneo lake limebana sana, lakini sisi Serikali tayari tumeshaliona hilo na kwa kutambua hilo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika mradi wetu huu wa HEET tunakwenda kufanya mageuzi makubwa sana katika Chuo chetu hiki cha Muhimbili kwa kujenga campus au chuo kingine kipya kabisa katika eneo letu la Mloganzila ambalo litakuwa na fani au ndaki tofauti tofauti.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo haikutosha, tunakwenda tena kufungua campus nyingine mpya katika Mkoa wa Kigoma ambayo itasimamiwa na Muhimbili. Hiyo vilevile haitoshi, tena tunakwenda kufanya hivyo katika Mkoa wa Mbeya kwa kujenga campus nyingine hii ya Muhimbili. Kwa hiyo, mchakato huu umeshaanza, nimwondoe wasiwasi tutadahili pale wanafunzi wa kutosha kuhakikisha kwamba tunapata wataalam wa tiba hapa hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, taasisi binafsi zimekuwa wadau wakubwa katika suala zima la elimu ya ufundi na kuna uwekezaji mkubwa, je, Serikali haioni wakati umefika sasa wa kuwa na mikataba na waendeshaji wa vyuo hivi kama ilivyo hospitali binafsi kwenye mkataba wa DHH? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, Wilaya ya Kilosa ilitoa kwa makusudi Chuo cha VETA pale Mikumi kwa Serikali na toka nimekabidhi hakuna ukarabati wowote ambao umefanyika mpaka sasa; je, Serikali haioni wakati umefika sasa wa kurudisha chuo hiki kwa halmashauri ambayo ni miliki wa awali baada ya Serikali kushindwa kuwekeza chochote? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, nikijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Londo, Mbunge wa Mikumi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, Mheshimiwa Mbunge, anatoa ushauri kwamba, kwa nini sasa Serikali haioni umuhimu wa kuingia mikataba ya ubia juu ya uendeshaji wa vyuo hivi? Kwa vile huu ni ushauri ambao Mheshimiwa Mbunge anatupa kama Serikali, nimuahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba ushauri wake tumeupokea tutakwenda kuufanyia tathmini ya kina ili kuweza kuona maeneo gani ambayo Serikali inaweza ikaingia ubia pamoja na mashirika binafsi katika uendeshaji wa vyuo hivi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la pili, kuhusiana na Chuo hiki cha Mikumi nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge tumepeleka fedha katika mwaka uliopita wa fedha pale kwa ajili ya kufanya ukarabati, lakini na katika mwaka huu wa fedha 2023/2024 tumetenga fedha kwa ajili ya kuendelea na ukarabati pamoja na uongezaji wa majengo.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile mwakani 2024/2025 tumetenga fedha kwenye bajeti yetu kuhakikisha kwamba vyuo vyote vile vya zamani ambavyo tulivichukua kutoka kwa taasisi binafsi pamoja na halmashauri vinaenda kukarabatiwa, kuongezewa majengo, lakini vilevile kupeleka watumishi na vifaa kwa ajili ya mafunzo kwa vijana wetu. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali ina mpango wa kujenga VETA kila Wilaya sambamba na hilo, je, Serikali ina mkakati gani wa kuwapa vijana wanaosoma VETA mikopo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, safari ni hatua na tulishaanza utoaji wa mikopo kwanza kwa vijana wetu ambao walikuwa wanasoma elimu ya juu, lakini mwaka uliopita tumeanza kutoa mikopo katika elimu ya kati na kwa vile tunaendelea na utaratibu huu kwa kadiri ya upatikanaji wa fedha tunaweza tukafikia katika maeneo yote.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishe Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari Serikali imeshafanya kazi kubwa sana kwenye eneo hili la mafunzo ya VETA, kwa sababu ada ya vijana hawa au ada ya mafunzo kwa wale wanafunzi wa kutwa ni shilingi 60,000 na wale wanafunzi wa bweni ni shilingi 120,000. Serikali inachangia ruzuku kwa kila mwanafunzi zaidi ya shilingi 1,150,000 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka. Kwa hiyo, tutaendelea kutoa ruzuku hii na tutaangalia vilevile uwezekano wa kuweza kutoa mikopo katika kada hii muhimu.
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa hii nafasi, je, ni lini ujenzi wa Chuo cha VETA kinachojengwa Kata ya Uwiro, Arumeru Mashariki utamalizika? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nikiri kwamba kuna ujenzi ambao unaendelea katika Jimbo la Mheshimiwa Pallangyo, kule Arumeru na mimi mwenyewe nimeshafanya ziara zaidi ya mara mbili kwenye eneo lile kuangalia maendeleo ya chuo kile.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, malengo yetu ni kuhakikisha kwamba mpaka kufika mwezi Oktoba, mwaka huu vyuo hivi katika awamu ya kwanza viwe vimekamilika ili mwezi wa Novemba tuweze kuanza kutoa zile kozi za muda mfupi na Januari mwakani tuweze kuanza kutoa zile kozi za muda mrefu.

Kwa hiyo, hayo ndio malengo yetu tutahakikisha kwamba, ifikapo mwezi Oktoba, vyuo hivi vimekamilika, nakushukuru.
MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa TCU ni taasisi ya Muungano inayowakilisha Zanzibar na Tanzania Bara: Je, Mheshimiwa Waziri haoni kwamba ni busara kama kutakuwa kuna mkakati wa maana wa kuweza kuboresha na kupanua wigo wa uwakilishi wa Zanzibar ndani ya chombo cha TCU.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa TCU ni taasisi ya Muungano ambayo haina ofisi Zanzibar, kitu ambacho kinakwamisha na kuchelewesha kazi za vyuo vikuu pamoja na wahitimu wa vyuo vikuu kutoka Zanzibar: Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga ofisi Zanzibar pamoja na kuwa na Afisa Masuuli wa TCU ili kuimarisha uratibu kwa upande wa Zanzibar? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Soud, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge na nilithibitishie Bunge lako Tukufu kwamba kwa upande wa uwakilishi kwa maana ya ule wa kitendaji katika ngazi ya utendaji, taasisi yetu ina uwakilishi mzuri kutoka upande wa Zanzibar kwa sababu tuna Wajumbe wale wa Bodi ya TCU pamoja na Kamati zake, tuna uwakilishi wa kutosha kwa sababu baadhi ya Wajumbe wanatoka upande wa Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusiana na kuwa na ofisi, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sasa hivi utaratibu wa taasisi yetu jinsi unavyofanya kazi ni kwa njia ya mtandao. Kwa hiyo, haijalishi mtu yuko umbali gani awe Zanzibar, awe Mkoa wowote au hata nje ya nchi, bado anaweza aka-access mtandao huo na kufanya application na kufanya kazi zote kupitia mtandao.

Mhshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tumechukua wazo lake la kuweza kuwa na ofisi kule Zanzibar ili kurahisisha utendaji kazi wa taasisi yetu hii ya Muungano. Nakushukuru. (Makofi)
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi ya kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza nishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kweli inatusaidia sana. Tuliomba Chuo cha VETA Wilaya ya Kilombero tumepewa, tuliomba barabara ya lami tumepewa, Kiwanda cha Sukari shilingi bilioni 500 tumepewa, mradi wa maji shilingi bilioni 43 tumepewa, Hospitali ya Halmashauri tumepewa, kadhalika na kadhalika. Kwa kweli watu wanaochafua huko nje waache tunamshukuru sana Dkt. Samia kwa kazi kubwa anayoifanya. Naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, halmashauri ambazo zipo katika wilaya hazikupata Vyuo vya VETA, tulikubaliana kwamba, ziatapata shule maalum za ufundi. Je, ni lini ujenzi utaanza wa Shule Maalum ya Ufundi katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Ifakara kuna Chuo cha Ufundi vile vya FDC ambavyo vina eneo kati kati ya Mji wa Ifakara na eneo lile limekuwa likipata wavamizi mara kwa mara, je, Serikali haioni umuhimu wa kwenda kuzungushia fence katika chuo hicho ili kulinda eneo la chuo hicho? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Abubakari Damian Asenga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kupekee tupokee pongezi hizo za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, yeye ndio amewezesha hayo yote kutokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la kwanza kwa kupande wa shule zile za ufundi nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge ni kweli Serikali ina azma ya kujenga shule za ufundi katika majimbo yale ambayo hayakujengewa Vyuo vya VETA. Tunafahamu kwamba hivi Vyuo vya VETA vinajengwa katika wilaya pia tunafahamu kuwa zipo wilaya ambazo zina majimbo zaidi ya moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, iwapo kama VETA imejengwa katika Jimbo moja na wilaya hiyo ina majimbo zaidi ya moja, tafsiri yake shule hizi za ufundi tunakwenda kujenga kwenye yale majimbo ambayo yamekosa fursa za kujengewa vile Vyuo vya VETA.

Kwa hiyo, nikuondoe wasiwasi hivi sasa tupo katika maandalizi ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hizi zipo tayari. Tunafanya upembeuzi yakinifu pamoja na kufanya zile site visit kwa ajili ya kukagua yale maeneo ambayo zitajengwa shule hizi za ufundi na tunapofika Julai tunatarajia shule hizi ziweze kuanza kujengwa rasmi. Kwa hiyo, lini tunaanza? Tutaanza mwaka ujao wa fedha kwa maana Julai mwaka huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa pili kwenye vyuo vyetu vile vya FDC, ni kweli tuna vyuo vya FDC karibu 54 katika nchi yetu. Vilikuwa kwenye hali mbaya sana, vyuo hivi Serikali imeshafanya ukarabati, tumeongeza majengo kwenye baadhi ya maeneo ambako kulikuwa hakuna majengo, tumefanya ukarabati kwenye yale majengo ya zamani, tumenunua vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwenye vyuo hivi, kwa vile sasa shughuli hizi zote zilikuwa zinakwenda kwa awamu, awamu inayofuata sasa tunaangalia kwenye yale maeneo ambayo kuna uhitaji wa kujengewa uzio kwa ajili ya kujenga uzio.

Kwa hiyo, nikuondoe wasiwasi, tunaenda kwa awamu na uzio kwenye vile vyuo ambavyo viko mijini ambavyo tunaona kabisa kuna haja ya kujenga uzio tutakwenda kujenga uzio, ninakushukuru sana.
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Waziri, kwanza ninakushukuru kwa kunipa Chuo cha VETA Mbogwe, lakini kazi haifanyiki mpaka sasa hivi hata mafundi wametoka site. Mheshimiwa Waziri, shida ni nini? Kwa sababu wananchi walijua kwamba mwaka kesho tutaenda kuanza kukitumia hicho chuo. Ninahitaji majibu yako ili kusudi wananchi wa Mbogwe wajue, ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Maganga, Mbunge wa Mbogwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa vyuo hivi 64 vya wilaya pamoja na kile kimoja cha mkoa tunajenga kwa awamu na nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, baada ya kumaliza misingi kuna vifaa ambavyo inabidi tuagize. Tumefanya bulk purchase kutoka viwandani moja kwa moja. Katika zile karakana na majengo yale makubwa yote tunatumia Mfumo wa LGS (Light Gauge Steel), zile ni fabricated metals ambazo zinatoka kiwandani moja kwa moja. Kwa hiyo, unapoona ujenzi umesimama tayari tumesha-press order kwa ajili ya hizo fabricated metals na baada ya muda si mrefu zitakuja na zikishafika pale site ni kazi ya mwezi mmoja tu majengo yale yote yatakuwa tayari yameshanyanyuka.

Kwa hiyo, nikuondoe wasiwasi, kazi hiyo inaendelea, fedha zimeshalipwa kule ALAF na shughuli inaendelea kwa sababu zinakuwa imported. Mara baada ya kufika tutakuja hapo Mbogwe na kukamilisha hiyo kazi. (Makofi)
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Halmashauri ya Moshi ina vijana wengi sana ambao wanahitaji elimu ya ufundi. Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA katika halmashauri hiyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimwia Mwenyekiti, ninaomba nijibu swali dogo la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwisha kujibu kwenye maswali ya msingi kwamba kwa sasa baada ya kukamilisha ujenzi wa vile vyuo 25 vya awamu ya kwanza katika wilaya 25 na hivi 64, tutakuwa hatuna wilaya ambayo haina Chuo cha VETA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu kwamba kunawezekana kukawa na umbali wa namna moja au nyingine lakini ninaamini pale Moshi tuna Chuo cha VETA ambacho kiko pale Moshi, ni chuo cha mkoa, lakini vilevile kina-save kama chuo cha wilaya, lakini kwenye zile wilaya nyingine za pembezoni, ukienda Rombo, ukienda Hai, ukienda Siha, kote kule tumejenga Vyuo vya VETA na yale majimbo ambayo hayana vyuo tunakwenda kujenga shule za ufundi ku-complement pale ambapo Chuo cha VETA kimekosekana. (Makofi)
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ni miongoni mwa wilaya ambazo zimeanza ujenzi wa VETA eneo la Wilaya ya Tanganyika, lakini kwa bahati mbaya sana mpaka sasa tunavyozungumza ujenzi umekwama takribani zaidi ya miezi mitano. Ni lini Serikali itapeleka fedha kukamilisha ujenzi wa VETA Wilaya ya Tanganyika?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Kakoso, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali tumeshapeleka fedha na ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, pesa tulizopeleka hizi shilingi milioni 324.6 katika kila site, hizi zimekwenda kwa ajili ya zile local materials, kwa maana ya mchanga, kokoto, mawe, maji, lakini pamoja na gharama za kulipa mafundi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zile materials nyingine zote Wizara inanunua kwa mfumo wa bulk purchase kwa maana ya simenti, nondo, mabati pamoja na zile LGS (Light Gauge Steel) kwa ujumla wake. Kwa hiyo, iwapo kama misingi yote imeshakamilika na maboma yameshanyanyuliwa, tafsiri yake kinachosubiriwa sasa ni vile vifaa kutoka kiwandani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Kakoso, hivi sasa tayari vifaa hivi vimeshaagizwa na mara baada ya kufika tutavipeleka katika kila centre kuhakikisha kwamba majengo hayo yananyanyuka. Lengo letu ifikapo mwezi wa 10 vyuo hivi kwa awamu hii ya kwanza yale majengo tisa yawe yamekamilika ili mwezi wa 11 tuweze kuanza kutoa mafunzo rasmi, ninakushukuru sana. (Makofi)
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza nianze kwa kumshukuru sana Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha shilingi 2,400,000,000 kujenga chuo bora kabisa cha VETA Wilaya ya Ikungi. Sasa hivi tunavyoongea chuo kimeanza kazi chini ya Mkuu wa Chuo Ndugu Mathias Luhanga na wanafunzi wako darasani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka niombe tu Mheshimiwa Waziri kwamba kwa ajili ya mambo ya kiutawala chuo chetu kinahitaji usafiri. Ninaomba sana kujua ni lini Serikali itawaletea gari kwa ajili ya kufanya kazi za kiutawala katika Chuo chetu cha VETA Ikungi? Ahsante sana (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nikijibu swali dogo la Mheshimiwa Mtaturu, Mbunge wa Ikungi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwenye vyuo vyetu 25 tuna changamoto ya usafiri lakini nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, safari ni hatua na hatua tumeshaanza, kimsingi kwanza tulianza kujenga yale majengo, lakini baadaye tukajaribu kutafuta watumishi kwa ajili ya mafunzo hayo kuanza na hivi sasa mafunzo yameanza. Tumeanza kupeleka vifaa na hatua inayofuata ni kupeleka sasa vile vyombo saidizi kwa ajili ya kuhakikisha wataalamu wetu, walimu wetu na watumishi wetu wanafanya kazi zao kwa ufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi, katika bajeti yetu ijayo tumeweka fungu kwa ajili ya ununuzi wa magari, kwa ajili ya vyuo hivi vya VETA, FDC pamoja na vyuo vyetu vya ualimu. Tunaamini katika utekelezaji wa bajeti ya mwakani mambo hayo yatakwenda kufanyika.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, tunaishukuru Serikali kwa ukarabati mkubwa uliofanywa katika Chuo Tango FDC, Mbulu Mjini, je, Serikali ina mkakati gani sasa wa kumalizia yale majengo yaliyobaki kukarabatiwa ili chuo kile kiwe na hadhi?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nikijibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Zacharia, Mbunge wa Mbulu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli pale Tango tumefanya ukarabati mkubwa na baadhi ya majengo bado hatujakamilisha. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Zacharia, lakini ninakumbuka juzi ulikuja kwenye meza yangu tukalizungumza jambo hili pamoja na suala la kwenda kule Tango na nikakuahidi kwamba tusubiri tukamilishe shughuli za Bunge ili tuweze kwenda kuona hali halisi ilivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nikuondoe wasiwasi, katika Mradi wetu wa EP4R ambao tunataraji kuanza mwaka ujao wa fedha, tuna mpango wa kukarabati majengo yote katika vyuo vyote vya FDC ambavyo bado hatujafanya ukarabati. Kwa hiyo, kama nilivyokwisha kujibu kwenye swali moja la nyongeza hapa la FDC kule Ifakara, basi vilevile na Tango tutakwenda kufanya kama tutakavyofanya Ifakara. (Makofi)
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi na ninaipongeza Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan chini ya Wizara ya Elimu, Waziri na Naibu Waziri kwa kuanza ujenzi wa Chuo cha VETA ndani ya Wilaya ya Missenyi. Chuo hicho ni matarajio makubwa ya Wana-Missenyi na kimeanza lakini spidi yake kwa kweli hairidhishi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini sasa tutapata vifaa vya ujenzi ili tuweze kwenda kwa speed na tuweze kupata chuo hicho ambacho ni matarajio makubwa kwa Wana-Missenyi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kyombo, Mbunge wa Missenyi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwisha kujibu kwenye maswali mengine ikiwemo na hili la Mheshimiwa Kyombo kule Missenyi, sasa hivi tunachosubiri ni vile vifaa ambavyo ni imported materials, zile fabricated metals (LGS) kwa ajili ya majengo yetu yale makubwa, makarakana yale manne yote yale yanahitaji materials hizo, lakini pamoja na bati ambapo nimesema tayari tumesha-press order, tumeshalipa na vifaa hivyo viko njiani kuja. Mara vitakapofika mtashangaa ile speed yetu tutakayokwenda kule, ndani ya mwezi mmoja yale majengo yote na mazingira ya pale yatakuwa yamebadilika kabisa na tunaamini mpaka itakapofika mwezi wa 10, Missenyi tutakuwa tumekamilisha yale majengo makubwa na huduma pale zinaweza kuanza mara moja.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Mheshimiwa Waziri, kwanza niipongeze Serikali kwa ujenzi wa VETA nchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu, kutokana na kwamba dunia ya sasa mabadiliko ya teknolojia, maeneo mengi ya VETA ambazo zinajengwa, masomo yanayotolewa ni ya aina ile ile, ufundi ujenzi nyumba, ufundi cherehani na ufundi Seremala lakini soko la vijana nje linahitaji masomo mengine. Ufundi bomba, ufundi umeme wa magari, ufundi umeme wa majumba, lakini mitambo ya gesi kama usambazaji wa gesi unaoendelea nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni upi mkakati wa Wizara, wakati Mheshimiwa Rais anaendelea kujenga VETA nchini, ni upi mkakati wa Wizara kubadilisha syllabus ziendane na soko la sasa ili tuokoe vijana wengi wa Kitanzania wapate fursa hiyo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikijibu swali la Mheshimiwa Sanga kama ifuatavyo, Mheshimiwa Sanga anatoa ushauri kwa maana ya kubadilisha mtaala, lakini nikuondoe wasiwasi Mheshimiwa Sanga tayari Mheshimiwa Rais alishaliona hilo na alishaagiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeanza na maboresho makubwa ya mitaala yetu kuanzia shule za msingi, sekondari mpaka vyuo vikuu, lakini Mheshimiwa Rais aliagizwa kwamba, VETA hizi zinazojengwa, basi mitaala yake na masomo yake na kozi zake ziendane na shughuli za kiuchumi za sehemu husika, kwa maana tunakwenda kufanya customization katika vyuo hivi kwa lengo la kuhakikisha kwamba zile shughuli za kiuchumi zinazofanyika katika maeneo hayo ziweze kufundishwa katika vyuo hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, yale maeneo ambayo tunachimba madini tutakuwa na kozi za madini zinafundishwa kwenye vyuo hivi, yale maeneo ambayo tunashughulika na masuala ya uvuvi kutakuwa na kozi za uvuvi zinafundishwa kwenye maeneo haya, kule kwangu nako kimejengwa chuo kama hiki, kuna masuala ya utalii, lakini vilevile masuala ya hospitality yatafundishwa kwenye vyuo hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunakwenda kuhakikisha zile shughuli sasa za kiuchumi ndizo zitakazofundishwa, tukiongezea na hizi kozi nyingine za general ambazo kila mmoja wetu anapaswa kuzifahamu ili hata bomba likikatika pale nyumbani kwako huna haja ya kutafyta fundi, wewe mwenyewe unaweza kurekebisha kwa namna moja au nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, huo ndiyo mpango wa Serikali. Mheshimiwa Rais ameshatoa agizo na sisi kama Wizara ni lazima tutekeleze kwa kadri maagizo yalivyotolewa.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Chuo cha VETA kilichopo Manispaa ya Shinyanga ni chuo kongwe na kinahitaji ukarabati wa miundombinu. Ni upi mpango wa Serikali kukarabati Chuo cha VETA Manispaa ya Shinyanga? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nikijibu swali dogo la Mheshimiwa Dkt. Mnzava, ni kweli tuna vyuo vyetu, baadhi ya vyuo vyetu vya mikoa ni vya muda mrefu, majengo yake ni chakavu na miundombinu mingine ni chakavu, hata vifaa vilivyokuwa vinatumika ni vile vya muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Dkt. Mnzava, tuna miradi mbalimbali ambayo tumeshafanya maandiko yake na maandiko hayo yatakapokamilika na miradi hii kuanza tutakwenda kufanya ukarabati kwenye vyuo vyetu vyote kongwe kikiwemo na hiki Chuo cha Mkoa wa Shinyanga. (Makofi)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni kwamba katika Kata ya Mwika Kaskazini kwenye Jimbo langu la Vunjo kwenye Shule ya Msingi ya Lole kuna Chuo cha VETA ambacho kimetelekezwa kutoka mwaka 2000. Majengo yamechakaa, lakini kuna baadhi ya tools za kutumia kufundishia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kinachohitajika pale ni kukarabati yale majengo na kupata walimu wa kufundisha, basi pamoja na kuongeza hasa hivyo vifaa vya kufundishia. Je, ni lini Serikali itachukua hatua?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii sijui ni mara yangu ya tatu ninauliza swali hili, lakini nimeona nirudie kwa sababu wale wananchi wanateseka sana. Jimbo la Vunjo liko pacha na Jimbo la Moshi Vijijini kwenye halmashauri moja. Kwa hiyo, kuna disadvantages nyingi sana ambazo tunapata kwenye ku-allocate hizi facilities. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nikijibu swali dogo la Mheshimiwa Dkt. Kimei ni kuwa jambo hili ulilolizungumza ninaomba tu tutoe maagizo kwa Mkurugenzi wetu wa VETA, kwanza kwenda kuona hilo eneo, lakini Mheshimiwa Dkt. Kimei kama utaridhia ninadhani ni muhimu na sisi tukaenda tukaona, wazungu wanasema; “the seeing is believing.” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninadhani kuna umuhimu wa kupanga ratiba na sisi wenyewe kama Wizara, mimi binafsi niende nikaone tuweze kufanya tathmini ya kina ili tuweze kujua kitu gani, measures zipi tuweze kuchukua ili kama ni chuo ambacho kimeshakabidhiwa kwenye Wizara, basi tufanye ukarabati kama ulivyoshauri. Tupeleke vifaa pamoja na walimu ili mafunzo hapo yaanze kutolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuanzia tunaomba tumwagize Mkurugenzi wa VETA aweze kwenda eneo hilo kwa haraka na sisi tukimaliza Bunge hapa tutakwenda. Mheshimiwa Dkt. Kimei tutapanga na nitakuja hapo kwako tupange ratiba ya kwenda huko haraka iwezekanavyo. (Makofi)
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Wilaya ya Manyoni ina majimbo mawili. VETA inayoendelea kujengwa katika Manyoni iko katika Jimbo la Manyoni Mashariki. Unawaambiaje watu wa jimbo langu eneo la Itigi kuhusu ujenzi wa shule ambayo mmeitaja? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nikijibu swali dogo la Mheshimiwa Massare ni kwamba Mheshimiwa Massare anajua na tulishazungumza suala hili na alikuja ofisini na akaangalia orodha ya shule zitakazokwenda kujengwa za ufundi na Wilaya ya Manyoni, ilikuwa Manyoni imekosewa, Manyoni Kaskazini na Manyoni Kusini tukarekebisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Massare, shule yake ya Ufundi ipo, tumeshafanya marekebisho mwanzoni kulikuwa na typing error. Shule ile itakwenda kujengwa katika jimbo lake kama vile alivyoshauri yeye mwenyewe na kazi hii itaanza Julai mwaka ujao wa fedha. (Makofi)
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na kwanza niishukuru Serikali kwa majibu yake mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wana-Kyerwa wanapenda kufahamu fedha imetengwa tangu mwaka 2022/2023 lakini mpaka sasa hivi ujenzi unaenda kwa kusuasua. Tungependa kujua je, ni kwa nini? (Makofi)

Swali la pili, kwa kuwa vifaa vinatoka kwenye Wizara na hii inaweza ikawa sababu ya kuchelesha ujenzi huu, je, kwa nini fedha yote isipelekwe kwenye halmashauri ili ujenzi usimamiwe na halmashauri kama ilivyo miradi mingine kama hospitali za wilaya na vituo vya afya? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Bilakwate, Mbunge wa Kyerwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge, amekuwa akifuatilia ujenzi wa chuo hiki kwa muda mrefu na hata pale Serikali tulipokuwa hatujaanza ujenzi alifuatilia kuhakikisha kwamba chuo hiki kinajengwa kwenye eneo lake, lakini hata tulipoanza ujenzi mwishoni mwa mwaka 2022. Ujenzi huu ulianza mwezi Juni, 2022 ambapo ni mwishoni kabisa mwa mwaka wa fedha, alifuatilia mwenendo pamoja na maendeleo ya ujenzi huu. Kwa hiyo, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa ajili ya ufuatiliaji huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye jambo lake la kwanza kuhusiana na suala la ujenzi kusuasua, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, ni kweli Serikali ilitenga fedha na fedha hii ipo ingawa tunapeleka kule fedha hii kwa awamu. Kwa hiyo, nimhakikishie tu kwamba kuna vifaa vile ambavyo tunasema ni local materials ndizo hizi ambazo ni shilingi milioni 324 zimepelekwa kule kwa ajili ya ununuzi wa mchanga, maji, mawe na kulipa mafundi ambao wanahudumia kwenye hili eneo letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ujenzi huu haujasuasua sana, lakini tunajua kwamba unakwenda taratibu kutokana na ufuatiliaji wa karibu na kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawasawa. Kwa vile ametupa kama ushauri tutahakikisha katika kipindi hiki kifupi tuharakishe ujenzi ule ili Wana-Kyerwa nao waweze kupata chuo hiki kwa ajili ya mafunzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo lake la pili la vifaa kwamba tupeleke kule fedha kule kwa ajili ya vifaa. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu, kwa nini tumeamua kununua vifaa hivi kwa kutumia utaratibu wa ununuzi wa pamoja au bulk purchase?

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ununuzi wa pamoja (bulk purchase) tumepata faida nyingi sana. Kwanza tumetengeneza exemption ya zile kodi kwenye upande wa nondo, cement na vifaa vyote vile ambavyo vinatoka viwandani. Kwa hiyo, eneo lile ambalo tulipata exemption limetusaidia kwenda kufanya kazi zaidi ya pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ushauri wake huu wa kusema tupeleke fedha kule, tutapeleka fedha zile za local materials, lakini fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya viwandani tunadhani ni bora tununue moja kwa moja kwa sababu ina manufaa makubwa kuliko tungepeleka fedha hizi zote kule, matumizi yake yangekuwa makubwa na ile value for money tungeweza kuikosa, nakushukuru sana.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Halmashauri ya Ushetu tayari imekwishatenga eneo zaidi ya hekari 42 na lina hati na kila kitu, je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa shule hii ya ufundi katika Halmashauri ya Ushetu?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nijibu swali dogo la Mheshimiwa Cherehani, Mbunge wa Ushetu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Cherehani kwa kutenga eneo lile la Ushetu kwa ajili ya ujenzi wa shule zile za ufundi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana nilikuwa najibu swali hapa, azma ya Serikali ni kuhakikisha kwamba yale majimbo ambayo hatujajenga Chuo cha VETA tutakwenda kujenga shule ya ufundi. Kazi hii tunatarajia ianze mwaka ujao wa fedha wa 2024/2025. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Cherehani na wananchi wa Ushetu, Serikali ya Mama Samia iko kazini na mwezi Julai mwaka ujao wa fedha shule zile 100 za elimu ya amali tutakwenda kuanza ujenzi wake likiwemo na eneo la Ushetu.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, Wilaya ya Tarime ina halmashauri mbili, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Halmashauri ya Mji wa Tarime. Halmashauri ya Wilaya ya Tarime tumepata Chuo cha VETA, lakini Halmashauri ya Mji wa Tarime ambayo ni makao makuu ya wilaya hatujapata. Nataka kujua umesema hapo ujenzi wa shule za ufundi utaanza Julai, je, Halmashauri ya Mji wa Tarime nayo inaenda kujengewa hiyo shule ya ufundi?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nijibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Matiko, kama ifutavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Matiko kwa ufuatiliaji wa karibu kuhusiana na masuala ya elimu na taaluma kwenye mkoa wake pamoja na wilaya zake zote za Mkoa wa Mara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Matiko, azma ya Serikali ni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumejenga Vyuo vya VETA katika wilaya, tunafahamu kwamba kuna wilaya ambazo ni kubwa na zina majimbo zaidi ya moja. Kwa hiyo, kwenye maeneo yote au wilaya zote ambazo zina majimbo zaidi ya moja, tunaangalia ni eneo gani au jimbo gani limejengwa Chuo cha VETA. Kule ambako hakujajengwa Chuo cha VETA azma ya Serikali ni kupeleka shule ya amali au hizi shule za ufundi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hili Jimbo la Tarime Mji lina shule ya ufundi na ni miongoni mwa wilaya au majimbo ambayo ujenzi utaanza mwaka ujao wa fedha, ninashukuru sana.
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ili utekelezaji mahiri uonekane kiuhalisia Serikali inaonaje sasa kuvielekeza vyuo kuwa na jiji au halmashauri za kuzilea kama wafanyavyo wenzetu kule Japan, China na Indonesia.?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, wanafunzi wanapata shida sana unapokuja wakati wa kwenda field kupokelewa katika taasisi au idara mbalimbali. Je, Serikali ina mpango gani sasa kutoa mwongozo kwa idara na taasisi hasa za Serikali kupokea wanafunzi wa kufanya tafiti zao freely bila vikwazo vyovyote? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Dkt. Thea Ntara, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hakuna utaratibu wa vyuo vikuu kulea halmashauri au majiji katika nchi yetu. Utaratibu uliopo ni kwamba halmashauri hizi ziko huru kupata huduma katika vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki kwa kadiri ya chuo kikuu kilivyokuwa na wabobezi katika eneo fulani. Sasa kwa vile Mheshimiwa Mbunge ametoa ushauri hapa tuweze kuangalia jambo hili, basi ushauri wake tumeupokea na tunaenda kuufanyia tathmini kuweza kuangalia namna gani vyuo vyetu vinaweza vikashirikiana na halmashauri hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo la pili kuhusiana na suala la mwongozo, tunaomba nalo tulipokee. Tutakwenda kukaa na halmashauri zetu pamoja na taasisi nyingine ili kuweza kuona namna bora ya wanafunzi wetu wanapokwenda kufanya tafiti zao katika maeneo mbalimbali ya taasisi hizi nchini wasiweze kupata usumbufu wa aina yoyote, nakushukuru sana.
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi ya maswali ya nyongeza.

Swali la kwanza, Chuo hiki anachosema Mheshimiwa Naibu Waziri kimechukua muda mrefu ni zaidi ya miaka mitano sasa na wananchi wa Wilaya ya Sumbawanga na Mkoa wa Rukwa wanakisubiri kwa hamu kwa sababu wana uhitaji wa elimu hiyo ya VETA. Je, nili chuo hicho kitaanza kudahili wananfuzi kuanza mafunzo?

Swali la pili, facilities zilizoko kwenye chuo hicho ni ndogo zinaweza ku-accommodate wanafunzi 700 tu na uhitaji ni mkubwa sana.

Je, Serikali mmejipangaje kuhakikisha mnaongeza facility ili chuo hicho kiweze kudahili wanafunzi wengi zaidi?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Sangu, Mbunge wa Kwela kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli ninakiri mazungumzo au maelezo ya Mheshimiwa Mbunge kwamba Chuo hiki kimechukua muda mrefu, mwanzoni chuo hiki kilikuwa kinajengwa na kampuni moja ya Kichina, baada ya ku-default kwa maana baada ya kuleta changamoto kwenye ule mkataba, mkataba ulivunjwa. Kwa hiyo, ninamhakikishia tu Mheshimiwa Mbunge hivi sasa tumeshapeleka fedha zaidi ya shilingi bilioni 2.035 kwa ajili ya umaliziaji wa chuo kile. Nikupe taarifa tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, majengo mengi sana, tuna majengo zaidi ya 26 pale, majengo 22 mpaka kufika tarehe 30 Juni, 2022 yatakuwa yamekamilika isipokuwa majengo manne ambayo tumeyaongezea baada ya kuona capacity itakuwa ndogo. Tumeongeza mabweni mengine mawili, nyumba ya Mkuu wa Chuo, pamoja bwalo tumeliongezea ukubwa, haya yatachukua muda kidogo kukamilika. Nikuondoe wasiwasi chuo kile kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi wale wa muda mrefu zaidi ya 675 na zile kozi za muda mfupi zitakuwa zaidi ya wanafunzi 1,000 na tutakuwa tunaendelea kufanya hivyo kadri nafasi zitakavyotokea.(Makofi)
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi.

Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha Ufundi VETA Wilayani Hanang’?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Mbunge wa Hanang’ kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti yetu ya Serikali ambayo Mheshimiwa Waziri aliisoma hapa, kuna tengeo la zaidi ya vyuo 36. Ninamuahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwa vile tengeo lile lipo bado tutakuwa hatujamaliza kwenye Wilaya zote lakini Wilaya ya Hanang tutaipa kipaumbele. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Mbulu na Wilaya ya Mbulu haina kabisa Chuo cha VETA na kwa kuwa maelekezo yako ilikuwa tukupe ekari 50 na tumeshatenga tayari.

Je, ni lini utatuletea fedha za kujenga Chuo cha VETA Mbulu.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Flatei, Mbunge wa Mbulu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenye majibu yangu ya msingi kwamba sera ya Serikali ni kuhakikisha kwamba tunakwenda kujenga chuo katika kila Wilaya nchini. Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Flatei, kwa vile katika mwaka wa fedha ujao tunatengeo la vyuo karibu 36 katika Wilaya 36 tutaangalia zile Wilaya ambazo zina mahitaji makubwa ikiwemo na Wilaya ya Mbulu.
MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa kuwa, mpango wa kwanza wa Serikali ilikuwa ni kukamilisha Chuo cha VETA cha Wilaya ya Mkinga mwezi Mei, 2022, na kwa kuwa mpaka sasa chuo hicho hakijakamilika.

Je, ni lini Serikali itakwenda kukamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA katika Wilaya ya Mkinga?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Zodo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tulikuwa na ujenzi wa vyuo 25 katika wilaya 25 nchini ikiwemo na Wilaya hii ya Mkinga. Tayari Serikali imeshapeleka fedha zaidi ya Bilioni 20 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi huu, nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Zodo mpaka kufika mwisho wa mwezi huu vyuo hivi vyote 25 vitakuwa vimefika hatua ya mwisho kabisa ya ukamilishaji ili mwezi Julai tuweze kuanza udahili. (Makofi)
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Pamoja na kwamba Serikali tayari imepeleka fedha za awamu ya kwanza katika ujenzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mbulu, je, ni lini fedha za awamu ya pili zitapelekwa katika ujenzi wa Chuo cha Maendeleo TANGO FDC Mbulu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Issaay kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Issaay nadhani mimi na wewe tunazungumza mara kwa mara kuhusiana na chuo hiki; na nilikuomba kaka yangu kwamba kwenye ujenzi wa vyuo hivi vya FDC vilikuwa vyuo 54, na maeneo mengi sana tumefanya ujenzi pamoja na ukarabati. Nikakueleza kwamba katika mwaka wa fedha ujao tuna awamu ya pili ya ujenzi wa vyuo hivi kikiwemo na chuo hiki ulichokitaja. Kwa hiyo, nikuondoe wasiwasi katika mwaka wa fedha ujao tutazingatia yale maelekezo ambayo tulikuwa tumepewa na Mheshimiwa Rais kuhakikisha tunakamilisha ujenzi kwenye eneo hili. (Makofi)
MHE. MARTHA N. GWAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kuniona. Kwa kuwa, Wilaya ya Manyoni imeshatenga eneo la ujenzi wa chuo cha VETA katika Halmashauri ya Manyoni.

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa chuo hicho? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza kwenye majibu ya msingi kwamba ni sera ya Serikali kujenga chuo katika kila wilaya ikiwemo na Wilaya ya Manyoni. Na kwa vile katika mwaka ujao wa fedha tuna zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo 36 basi Wilaya ya Manyoni tutaipa kipaumbele. (Makofi)
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Msalala ina changamoto ya chuo cha VETA; na kwa kuwa tayari wananchi kupitia wadau wa Mgodi wa Bulyanhulu wametoa fedha, na tumeshajenga jengo la utawala na madarasa manne, sasa swali langu;

Je, ni lini sasa Wizara itakuja moja, ikague eneo lile ili iweze kutupatia kibali ili mwaka kesho tuanze kutoa huduma? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Mbunge wa Msalala kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nipongeze juhudi ambazo wananchi wamefanya pale Msalala kwa ajili ya kujenga mabweni pamoja na madarasa. Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, namuomba tu baada ya kikao hiki tukutane ili tuweze kuangalia ni namna timu yetu ya wataalam watakavyokwenda kufanya tathmini na kuangalia kama miundombinu iliyokuwepo pale inatuwezesha kuweza kuanza mafunzo katika eneo hilo. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona. Kwa kuwa Serikali inafufua kiwanda cha Machine Tools, Commonwealth Facility kiwanda kinajengwa pale Hai, lakini pia tumepata mdau anajenga kiwanda cha parachichi hivyo, mahitaji ya wataalam ni makubwa sana; na kwa kuwa tayari Serikali ilishaahidi kujenga chuo cha VETA pale Hai;

Je, ni lini sasa Serikali itatuletea fedha tuweze kujenga chuo hiki?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Hai kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza kwenye majibu ya msingi na kama ilivyoelekezwa/ilivyosomwa kwenye bajeti yetu ya Serikali, kwamba tumetenga zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo katika wilaya 36. Kwa hiyo, niumuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge tutakwenda kufanya tathmini ya kina ya uhitaji wa kila eneo na kuweza kuweka vipaumbele ni eneo gani la kuweza kwenda kujenga, lakini nikuondoe wasiwasi tutaizingatia sana haya maombi ya Hai. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, Serikali imetenga fedha ya kujenga vyuo vya VETA 36 katika wilaya ambazo hazina VETA sasa nataka kujua Wilaya ya Tunduru na sisi hatuna VETA je, na Wilaya ya Tunduru imo katika listi hiyo ya wilaya 36? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni ngumu sana kusema imo au haimo kwa sababu wilaya ambazo hazina vyuo vya VETA mpaka hivi sasa ni 62. Kwa hiyo, katika mwaka wa fedha ujao 2022/2023 tutakwenda kujenga kwenye wilaya 36, na mwaka 2023/2024 tutamalizia wilaya 27 zitakazokuwa zimebaki, lakini nikutoe wasiwasi kwa vile ukanda ule wa kusini bado maeneo yalikuwa ni machache sana yaliyofikiwa Tunduru itakuwa iko kwenye kipaumbele. (Makofi)
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Serikali, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Nafahamu kwamba kwenye Sera ya Elimu ya VETA, chuo kinajengwa kwenye Makao Makuu ya Wilaya. Kwa kuwa Jimbo la Kibaha Vijijini ni moja ya jimbo lililopo kwenye Wilaya yenye majimbo mawili, nataka nijue: Je, Serikali haioni sasa ni muda sahihi wa kutujengea Shule ya Sekondari ya Elimu Amali, ili kuendana na mbadala wa Chuo cha VETA?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa, nimeshaandika barua na nimefanya mawasiliano na Wizara ya Elimu mara nyingi na katika Bajeti ya Serikali ya 2023/2024, Waziri ametangaza uwepo wa shule 26 za elimu ya amali. Je, Waziri haoni sasa ni muda sahihi wa kumwagiza Mkurugenzi ili aandae eneo kwa ajili ya kunipatia shule moja kati ya hizo?
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Serikali, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Nafahamu kwamba kwenye Sera ya Elimu ya VETA, chuo kinajengwa kwenye Makao Makuu ya Wilaya. Kwa kuwa Jimbo la Kibaha Vijijini ni moja ya jimbo lililopo kwenye Wilaya yenye majimbo mawili, nataka nijue: Je, Serikali haioni sasa ni muda sahihi wa kutujengea Shule ya Sekondari ya Elimu Amali, ili kuendana na mbadala wa Chuo cha VETA?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa, nimeshaandika barua na nimefanya mawasiliano na Wizara ya Elimu mara nyingi na katika Bajeti ya Serikali ya 2023/2024, Waziri ametangaza uwepo wa shule 26 za elimu ya amali. Je, Waziri haoni sasa ni muda sahihi wa kumwagiza Mkurugenzi ili aandae eneo kwa ajili ya kunipatia shule moja kati ya hizo?
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Je, ni lini Serikali itajenga Shule Maalumu ya Ufundi niliyoiomba katika Kata ya Kisawasawa, Halmashauri ya Mji wa Ifakara?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba nijibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Asenga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Mwakamo, Serikali ina mpango wa kujenga zile shule 100 kwenye majimbo yote ambayo yalikuwa hayana Vyuo vya VETA. Miongoni mwa majimbo hayo ni Jimbo la Mheshimiwa Asenga kule Ifakara. Namwondoa wasiwasi, yeye shule yake iko katika mpango ule wa pili wa mwaka 2024/2025. Kwa hiyo, tutaanza kutekeleza kunako Julai, Mosi, 2024. Nakushukuru.
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imesema inaweka vifaa kwenye vyuo vyetu, lakini je, haioni haja sasa ya kuhakikisha vyuo vyote nchini vinakuwa na database ya tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanafunzi kwa ajili ya matumizi ya baadaye? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, ili kutengeneza mnyororo wa thamani wa matumizi bora ya tafiti na kuuchochea ubunifu na ugunduzi nchini.

Je, Serikali haioni haja sasa ya ku-pioneer kusimamia uanzishaji wa jamii za wanataaluma wa sekta mbalimbali na kuwaunganisha na wanafunzi wa vyuo ili kuchochea ubunifu na ugunduzi nchini? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nikijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Engineer Mwanaisha Ulenge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kuhusiana na suala la kuanziasha kanzidata, tayari Serikali imeshafanya kazi hii. Hivi sasa tunavyozungumza vyuo vingi sana vya elimu ya juu pamoja na taasisi zetu za elimu ya juu tayari zimeanza kuwa na hizi database au kanzidata ambazo zitakuwa zinahifadhi hizi soft copy au nakala laini za utafiti na ubunifu. Hivi sasa tumeanza kwa ngazi ile ya Shahada zile za Umahiri (Masters) pamoja na zile za Uzamivu (Ph.D) na tumeziagiza taasisi zetu zote ziweze kuanzisha kanzidata hizi ili kuhakikisha kwamba zile tafiti na bunifu ninaweza kutunzwa siyo hizi tu za sasa hata zile za miaka ya nyuma tumeanza ku-digitalize ili kuweza kuzitunza katika kanzidata hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la pili ambalo anataka kufahamu kama Serikali ina mpango gani juu ya uendelezaji, lakini kutengeneza linkage baina ya wanataaluma na wale ambao wanafanya kazi kule viwandani. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge pamoja na Bunge lako Tukufu, Serikali tayari imetoa mwongozo kwanza wa uanzishwaji wa vikundi hivi au kampuni hivi tunaziita kampuni tanzu katika Taasisi zetu za Elimu ya Juu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia mradi wetu wa mageuzi makubwa ya kiuchumi (HEET) pamoja na ule wa EASTRIP tumenzisha makampuni tanzu kwenye taasisi zetu za elimu ya juu kwa lengo la kutengeneza wigo wa wanataaluma wetu na watafiti kuwa na linkage na viwanda na maeneo mengine ya sekta binafsi ili kuhakikisha zile tafiti na bunifu zao zinapelekwa kule, lakini zinaweza kutumika katika maendeleo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari ukienda kwenye Taasisi yetu ya DIT, Nelson Mandela pale Arusha, lakini University of Dar es Salaam hata ukienda MUST kule Mbeya wana Makampuni haya ambayo yanatengeneza linkage baina ya taasisi zetu za kitaaluma na viwanda vyetu. Nakushukuru sana.
MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Spika, kwa maelezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri atakubaliana kabisa kwamba kwenye issue ya ufundi vitendo ni muhimu zaidi kuliko nadharia. Kwa Juni, 2023 tu zaidi ya watoto 37% ya zaidi ya wanafunzi 18,000 walishindwa kujiunga na VETA. Sasa kama focus ni vitendo hauoni sasa ni muhimu kwa wizara yake kupitia vigezo ili qualification iwe zaidi kwenye vitendo zaidi ya nadharia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, nijibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Tweve, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu ya swali la msingi kwamba kwa hivi sasa vigezo tunavyotumia ni hivi vya kuweka mtihani huu wa kuandika ili kupima zile stadi za KKK.

Mheshimiwa Spika, kama mnavyofahamu ni kwamba tuna maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi pamoja na umaskini na namna pekee ya kuondoa huu ujinga ni pamoja na kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge ametoa hili wazo hapa, naomba tuuchukue ushauri wake ili twende tukaufanyie tathmini na kuangalia namna bora ya kufanya hii mitihani, aidha kwa kuandika au kwa hiyo namna ambayo yeye amependekeza, nakushukuru.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, nilitaka kujua ni kwa nini Wizara imebadilisha vigezo vya wanafunzi wanaojiunga kwenye vyuo vya kati vya afya ambavyo vimesababisha kukosa wanafunzi wengi, na kwamba kwa vile vyuo kukosa wanafunzi itasababisha upungufu wa wauguzi katika zahanati na vituo vya afya vingi vilivyojengwa nchini.

Je, Serikali ina mpango gani wa kurudisha madaraja au zile credits za zamani?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, nijibu swali dogo la Mheshimiwa Jesca kuhusiana na suala la kubadilisha vigezo hasa kwa wale wanaojiunga na kada hizi za afya.

Mheshimiwa Spika, suala la vigezo vya kujiunga na shule siyo static, ni kitu ambacho kinatakiwa kibadilike kulingana na mwenendo wa elimu yetu jinsi ulivyo, lakini kwa vile ametoa ushauri hapa tuweze kwenda kuangalia upya, nimuahidi tu Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu kwamba tutakwenda kufanya mapitio ya hivyo vigezo ili tuweze kuangalia changamoto iko wapi. Ninajua kuna kigezo kimoja cha kwamba ni lazima mtu afaulu hesabu ndicho ambacho kimewaangusha wengi, lakini hivyo nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, ushauri wake tumeupokea na tutakwenda kuufanyia kazi na baadaye tutakuja na majibu sahihi, nakushukuru.
MHE. JACQUELINE K. ANDREA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali vitabu ambavyo vimesambazwa na ambavyo havijasambazwa ni sawa sawa na asilimia tisa; je, Serikali imejipanga vipi kukamilisha asilimia tisa zilizobaki?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kutokana na Jiografia ya Mkoa wetu wa Tabora na ukubwa na ni ya kwanza kwa ukubwa kwa nchi nzima. Je, Serikali ina mpango mkakati gani wa kuhakikisha mkoa huu unapata kipaumbele katika usambazaji wa vitabu? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, nikijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Jacqueline, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna baadhi ya mikoa ambayo vitabu hivi havijafika kwa 100% na naomba niitaje mikoa hiyo kama ifuatavyo: ni Mkoa wa Iringa, Katavi, Mara, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Rukwa, Shinyanga, Simiyu, Songwe pamoja na Tabora aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kazi ya upelekaji wa vitabu hivi vilivyosalia asilimia tisa inaendelea na tunakadiria mpaka kufika mwisho wa mwezi huu tutakuwa tumekamilisha usambazaji wa vitabu hivi kwa 100%.

Mheshimiwa Spika, katika eneo lake la pili kuhusiana na suala la Tabora kuipa kipaumbele, nimwondoe wasiwasi kwa vile tunatarajia ndani ya mwezi huu vitabu hivi viwe vimefika katika mikoa yote ukiwemo na Mkoa wa Tabora basi na Mkoa wa Tabora nao tutaupa kipaumbele kuhakikisha kwamba ndani ya Mwezi huu wa Tano vitabu hivi vyote vinafika kwa 100%, nakushukuru.

MHE. AMEIR ABDALLA AMEIR: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waiziri kwa ridhaa yako naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kwa pamoja kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Wizara ya Elimu ndiyo chemchem na chimbuko la wataalamu katika fani/stadi mbalimbali za kiuchumi na kwa kuwa Serikali imetumia gharama kubwa kufanya maboresho ya mabadiliko haya ya mitaala mipya.

(a) Je, ni kwa namna gani na kwa kiasi gani maboresho ya mitaala haya mapya yataleta mabadiliko katika kupunguza idadi ya utegemezi wa wataalamu wa stadi mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali nchini?

(b) Je, ni kwa kiasi gani maboresho haya ya mitaala yatatusaidia katika kupunguza ule mfumo wa wahitimu wetu wa vyuo mbalimbali kuweza kujiajiri badala ya kuajiriwa?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ameir, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu ya swali la msingi, kwanza kipekee tumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye amekuwa chanzo cha mabadiliko haya makubwa. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa maboresho ya mitaala haya ya mwaka 2023 katika ngazi mbalimbali za elimu yamezingatia mahitaji ya soko la sasa na baadaye. Kwa muktadha huo kozi mbalimbali zenye uhitaji mkubwa katika soko la ajira zimeweza kuanzishwa na Serikali hutoa mikopo katika maeneo hayo kwa vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini. Kwa kufanya hivyo tunaamini kabisa itaweza kupunguza utegemezi wa wataalamu katika sekta mbalimbali kwenye miradi yetu nchini.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la pili, maboresho ya mitaala ya mwaka 2023 yamelenga kutoa elimu ya ujuzi kwa kuanzisha mkondo wa elimu ya mafunzo ya amali ambapo katika ngazi ya elimu mhitimu atakuwa amepata maarifa, stadi na ujuzi utakaomwezesha kujiajiri au kuajiriwa. Kwa hiyo, dhana kubwa katika mfumo wetu huu na mitaala yetu ya sasa inalenga hasa kumwandaa kijana au mhitimu kuhakikisha kwamba anaweza kujiajiri au akaajiriwa mahala popote, nakushukuru.
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, shule hii ina tatizo la walimu, kwa hivi sasa ina walimu sita tu; je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza idadi ya walimu kuondokana na changamoto iliyokuwepo?

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la walimu limekuwa ni tatizo sugu Mkoani Mtwara kwa ujumla. Je, Serikali ni lini italichukulia tatizo hili kwa umuhimu unaostahili? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nikijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mchungahela, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tukiri kwamba kuna changamoto ya walimu katika Chuo hiki cha Kitangari na siyo chuo hiki tu bali karibu vyuo vyote kutokana na uongezekaji uliotokea baada ya kujenga vyuo vipya 25 vya wilaya na vile vinne vya mikoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tarehe 02/03/2024 tumepata kibali cha kuajiri jumla ya walimu 239. Kati ya hao, watumishi 72 ni watumishi mwega na watumishi 167 ni walimu. Tutahakikisha kwamba walimu hawa watakapopatikana tutakipa kipaumbele Chuo hiki cha Kitangari lakini tutawapa kipaumbele sana Mkoa wa Mtwara na vile vyuo vipya 25 vya wilaya na vile vinne vya mikoa, ninakushukuru.
MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kuniona.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaishukuru Serikali kwa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Kayenze huko huko Nyehunge. Swali langu ni kwamba, je, chuo hiki ujenzi wake utakamilika lini, maana kwa hivi sasa ujenzi huu unasuasua?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nikijibu swali dogo la Mheshimiwa Shigongo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa Serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo vya wilaya 64 pamoja na chuo kimoja cha mkoa ambacho ni Mkoa wa Songwe. Moja kati ya vyuo vinavyojengwa ni katika jimbo la Mheshimiwa Shigongo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Shigongo na Wananchi wake wa Buchosa; Serikali inaendelea na ujenzi huu kwa awamu na tumekuwa tukipeleka fedha. Tayari tumeshapeleka zaidi ya shilingi milioni 200 na kitu kwa ajili ya ujenzi na hivi sasa tunafanya ununuzi wa vifaa vya viwandani ambavyo ni zile LGS au Light Gauge Steel pamoja na mabati kwa ajili ya kupeleka kukamilisha ujenzi katika chuo hiki. Ni imani yetu itakapofika mwezi wa kumi au kumi na moja, ujenzi wa chuo hiki utakuwa umekamilika. (Makofi)
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Pamoja na hayo, kwa kuwa hadi sasa kuna vijana wanaomaliza darasa la saba hawajui kusoma na kuandika; na kwa kuwa hilo ni takwa maalum katika nchi yetu. Je, Serikali iko tayari sasa kurejesha ule mpango wa kutoa elimu na madarasa ya jioni kwa watu wazima ambao hawakufanikiwa kujifunza kusoma na kuandika katika shule ya msingi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, sambamba na elimu hiyo ya K.K.K, je, Serikali iko tayari kutoa mafunzo ya stadi za elimu ikiwepo kupika, kushona, kupasi kwa akina mama saa za jioni katika kata zetu na vijiji vyetu kupitia kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya mama yangu, Mheshimiwa Shally Raymond kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, ninaomba nimpongeze sana Mheshimiwa Shally Raymond kwa maswali yake na vilevile kwa juhudi zake kwa kuwasemea akina mama wa Kilimanjaro pamoja na Watanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la kwanza ambalo Mheshimiwa Mbunge anauliza kuhusiana na suala la maboresho ya elimu hii ya watu wazima katika kata zetu, ninaomba kwanza nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu. Katika matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, eneo hili vilevile limeangaliwa, la kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika taarifa za sensa za mwaka 2022 inaonyesha kwamba, sasa hivi katika nchi yetu 17% ya Watanzania hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu. Asilimia hii imeshuka kutoka 22% ya mwaka 2012. Kwa hiyo, imeshuka kwa kiasi fulani, lakini bado tunasema asilimia hii ni kubwa kulingana na maisha ya sasa hivi na karne ya sasa hivi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge. Katika maboresho ya Sera ya Elimu pamoja na mitaala tuliyofanya mwaka jana (2023), jambo hili limeingizwa. Hivi sasa katika halmashauri zetu zote tumeanzisha idara pamoja na vitengo vya elimu ya watu wazima, kwa maana ya elimu ya msingi na sekondari kwa kuteua Maafisa Elimu ya Watu Wazima ngazi ya msingi na Maafisa Elimu ya Watu Wazima ngazi ya sekondari. Sasa tunakwenda kuanzisha madarasa yale katika kata zetu na vijiji vyetu kule kote na hawa maafisa wetu ndio watakaokuwa wasimamizi wakuu katika eneo hilo. (Makofi)

Katika eneo la pili analolizungumza, kwamba sasa tuanzishe programu mbalimbali wa ajili ya akina mama, nimwondoe wasiwasi, Serikali yetu inatekeleza programu inayoitwa integrated approach. Katika programu hii ina elimu changamani ambapo stadi hii za K.K.K zinafundishwa pia zinachanganywa na stadi nyingine za ujasiriamali, stadi za maisha, upishi na masuala ya uhifadhi wa mazingira na maeneo mengine. Kwa hiyo, tayari Serikali inalifanyia kazi jambo hili na tunaendelea kulifanyia kazi kwa karibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. (Makofi)
MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; tunatambua kwamba Serikali ina mpango wa kujenga Shule za Ufundi katika Halmashauri zote ambazo hazijapata vyuo vya VETA. Je, ujenzi huu utaanza lini?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Chuo cha VETA kinachojengwa katika Wilaya ya Bagamoyo Halmashauri ya Chalinze mpaka sasa kinasuasua ujenzi wake na hatujui hatma yake ni lini kitamalizika. Je, Serikali ina kauli gani kumaliza chuo hiki ili wananchi wa Bagamoyo na wananchi wa Chalinze, wanafunzi wetu na vijana wetu wapate kusoma katika vyuo hivyo?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mkenge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake muhimu kwa Wanabagamoyo na Chalinze kwa ujumla na naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 87 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule hizi za amali kwa awamu. Kwa hiyo, katika kipindi hiki kwanza katika mwaka huu wa fedha tutajenga shule hizo 100, lakini ujenzi huu utaanza kwa awamu. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge tayari hivi sasa tumeshaanza kupeleka fedha ambazo ni kati ya shilingi milioni mia tano na ishirini na nane plus katika kila Halmashauri ambayo inataka kujengewa shule hizo.

Mheshimiwa Spika, ni matarajio yetu ndani ya quarter hii ya kwanza ya mwaka huu ujenzi huu wa shule hizi za sekondari za amali katika maeneo haya niliyoyataja uweze kuanza mara moja.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la pili, katika Chuo chetu cha VETA pale Chalinze na bahati nzuri na nilifanya ziara pale nimetembelea eneo lile kulikuwa na changamoto za design pamoja na wajenzi wetu wale tukajaribu kutatua. Nimwondoe hofu tayari tumeshazungumza na wenzetu wa Wizara ya Fedha, tulipokea mwanzoni shilingi bilioni 49 bado shilingi bilioni 51 hatujazipokea kwa ajili ya kuendelea na ujenzi.

Mheshimiwa Spika, tumekubaliana na Wizara ya Fedha ndani ya quarter hii ya kwanza tutahakikisha kwamba fedha zile shilingi bilioni 51 tumezipata ili kuendelea na ujenzi katika maeneo yote ya Wilaya hizi 64 ili kuhakikisha kwamba ujenzi huu unakamilika ndani ya mwaka huu ili mwakani vijana wetu waanze kupata mafunzo katika maeneo haya.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, uendelezaji wa ujenzi wa Chuo cha VETA katika Wilaya yangu ya Nanyumbu kwenye Kijiji cha Maneme umesimama kwa kipindi kirefu. Je, ni lini ujenzi huo utaendelea? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwishaeleza katika maelezo yangu ya jibu la mwanzo kwamba tunatarajia ndani ya quarter hii yaani mwezi huu Agosti na mpaka kufika mwezi Septemba tuweze kupata fedha hizi shilingi bilioni 51 ili ujenzi ule uweze kuendelea katika maeneo yote, katika Wilaya 64 na kile kimoja cha Mkoa wa Songwe, nakushukuru.
MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Serikali imekamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA cha Mkoa wa Geita, lakini kimejengwa very substandard. Sasa nataka kujua ni lini Wizara itapeleka Mkaguzi pale kuangalia kazi ilivyofanyika chini ya kiwango?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Kanyasu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nimeshafika Geita, Vyuo hivi vinne vya Mikoa ambavyo mwanzoni vilikuwa vinajengwa kwa ufadhili wa Benki ya FDB na baadaye mkopo ule ulisitishwa, Serikali ilikwenda kukamilisha ujenzi ule kupitia fedha za UVIKO-19 ambapo tulifanya ujenzi ule kwa njia ya force account, ujenzi umekamilika.

Mheshimiwa Spika, kwa vile Mheshimiwa Mbunge anazungumza kwamba umekwenda substandard, nitamwomba Mheshimiwa Mbunge aridhie baada ya Bunge hili tuweze kufanya ziara sote kwa pamoja, mimi na yeye twende tukabaini hayo maeneo ambayo anadhani kwa namna moja au nyingine labda yamejengwa kwa substandard ili tuweze kufanya maboresho na marekebisho, nakushukuru.
MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kile chuo chetu cha Musoma Mjini cha VETA ndicho chuo kinachohudumia vyuo vinavyoanzishwa vya Mkoani Mara kama Butiama pamoja na kule Rorya. Je, ni lini sasa chuo hicho kitapewa hadhi Mkoa pamoja na facilities zote kwa maana ya miundombinu inayolingana na hadhi ya Mkoa?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu dogo la Mheshimiwa Manyinyi. Nashukuru kwa maswali yake ya msingi, Mheshimiwa Manyinyi nitaomba na yeye vilevile aridhie baada ya Bunge hili labda tuweze kufanya ziara, twende pale tukafanye tathmini ya kuangalia mahitaji na mapungufu yaliyopo ili Serikali iweze kuyafanyia kazi tuweze kuongeza hiyo miundombinu ambayo inapungua ili kukipa hadhi chuo hiki kuwa Chuo cha Mkoa. Nashukuru sana.(Makofi)
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana Serikali kwa majibu. Idadi ya wanafunzi 22,844 ni idadi kubwa sana, je, nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba idadi hii inapungua, ili wanafunzi wasipate ujauzito tena? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, wanafunzi wanaonyonyesha utaratibu wao upoje wanapokuwa wanaendelea na masomo? Ahsante. (Makofi)
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana Serikali kwa majibu. Idadi ya wanafunzi 22,844 ni idadi kubwa sana, je, nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba idadi hii inapungua, ili wanafunzi wasipate ujauzito tena? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, wanafunzi wanaonyonyesha utaratibu wao upoje wanapokuwa wanaendelea na masomo? Ahsante. (Makofi)
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, je, Serikali ina mkakati gani wa kuwapatia posho japo kidogo kwa wanafunzi hawa ili kuhakikisha wanabaki shuleni? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninaomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Maryam Mwinyi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Maryam anashauri kwamba tuangalie namna gani ya kuweza kutoa posho kidogo. Hatuwezi kusema moja kwa moja jambo hili utekelezaji wake unakuwaje na kwa namna gani katika miongozo ya Serikali, lakini tubebe kama ushauri na twende tukaufanyie evaluation au tathmini tuweze kuangalia kama namna gani tunaweza kutekeleza au laa.
MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha wanafunzi hawa wanaorudi shuleni kwa mpango huu, wanaweza kumaliza masomo yao na kutimiza ndoto zao? (Makofi)
MWENYEKITI: Majibu, Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Sijasikia.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Munira, hebu rudia swali lako alipate vizuri.

MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha wanafunzi hawa wanaorudia masomo yao kwa mpango huu, wanamaliza masomo yao na kutimiza ndoto zao?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu ya swali la nyongeza kwenye mikakati mbalimbali ya Serikali, siyo tu kwa hawa ambao wanarudi hata kwa wale ambao wanaendelea na masomo, mikakati ni kama vile nilivyokwishaeleza awali kuhakikisha kwamba tunatengeneza mabweni, vilevile kutengeneza sheria zetu vizuri, kutoa elimu ile ya unasihi pamoja na nasaha mbalimbali ili kuhakikisha hawa sasa hawaingii tena kwenye changamoto hii ambayo ilikuwa imewapata hapo awali. (Makofi)
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa fursa, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, Serikali kwa ujumla wakawa tayari kuleta takwimu za wanafunzi walioolewa, waliopata mimba ili tujue ukubwa wa tatizo tujaribu kutafuta mipango mizuri ya kuzuia shida hii? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Waitara kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu hizi zipo na kama nilivyoeleza hapo mwanzoni kwamba mpaka kufika Machi, 2024 zaidi ya wanafunzi 22,000 waliweza kurejea shuleni kwa wale ambao walipata ujauzito kwa namna moja au nyingne. Hata hivyo, Mheshimiwa Waitara wewe unafahamu umeshawahi kuhudumu kwenye Serikali. Tuna takwimu zile ambazo tunazichukua za kila mwaka katika shule zetu zote. Kwa hiyo, tuna takwimu ya kila mwanafunzi mahali alipo na kama amekatiza masomo kwa namna moja au nyingine. Kwa hiyo, tupo tayari kuziwasilisha takwimu hizo kwa kadiri zitakavyohitajika.
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi, mimi nipo kwenye hiyo Kamati ya Elimu na kwa sababu tumeona kuna changamoto ya wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa watoto hawa ambao wanarudi shuleni baada ya Serikali kusema warudi shuleni.

Sasa Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba wazazi na walezi wanapewa elimu ya kutosha ili washirikiane na hawa watoto ambao wanarudishwa shuleni? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru na nimshukuru sana Mheshimiwa Nusrat Hanje nikijibu swali lake dogo na kwa vile yupo kwenye Kamati yetu ya Elimu, Utamaduni na Michezo na waraka huu unaeleza vizuri namna gani wazazi na walezi watashirikishwa kwenye malezi na makuzi ya watoto wetu ambao wanarejea shuleni. Kwa misingi hiyo, tuna Kamati Maalum katika kila shule za kuhakikisha kwamba wale watoto ambao wanarudi, Kamati ile iweze kushirikiana na wazazi na walezi kuhakikisha kwamba mtoto wetu anabaki salama, vilevile na makuzi ya mtoto aliyezaliwa yanakwenda katika hali ya usalama. Kwa hiyo, waraka wetu upo vizuri na unaelekeza mambo yote kwa ufasaha.
MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nilikuwa na maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali moja, kwa kuwa somo hili linatakiwa kufundishwa elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo vya ualimu tu. Je, Serikali sasa haioni umuhimu wa kufundisha somo hili la uzalendo katika vyuo vya kati na vikuu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kwa kuwa sera tayari imekubalika ya mtaala huu, je, sasa Serikali kupitia Mheshimiwa Waziri inaweza ikatuhakikishia kuwa ni lini litaanza kusomeshwa katika shule kwa mustakabali wa vijana wetu na nchi yetu? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Pondeza, Mbunge wa Chumbuni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la uboreshaji wa mitaala yetu ni suala ambalo ni dynamic siyo static. Ni mitaala ambayo inatakiwa iboreshwe kila wakati kulingana na mahitaji ya wakati huo. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako tukufu kuwa Serikali kupitia vyuo vyetu hivi alivyovitaja vya kati na elimu ya juu tunaendelea kufanya maboresho ya mitaala yetu yote ili kuhakikisha kwamba somo hili la uzalendo linakuwa ni sehemu ya masomo yatakayofundishwa katika vyuo vyetu vya kati na juu.

Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ushauri wake tumeupokea na wakati wa maboresho ya mitaala yetu katika vyuo vyetu vya kati utazingatiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili anauliza juu ya lini mtaala huu mpya na sera yetu mpya imeanza kutekelezwa. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako tukufu kuwa mtaala huu tayari tumeanza kuutekeleza kutoka mwezi Januari 2024, lakini tunatekeleza kwa awamu. Kwa hiyo, kwa awamu ya kwanza tunatekeleza kuanzia elimu ya awali, darasa la kwanza na darasa na la tatu. Vilevile kwa upande wa sekondari tumeanza kutekeleza mtaala mpya ambao unabeba masomo haya kwa kidato cha kwanza mwaka huu na kwa ule mkondo wa amali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa vyuo vya ualimu vilevile umeanza mwaka huu. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge mtaala huu tayari Serikali imeshaanza kuufanyia kazi na utekelezaji wake umeanza toka mwezi Januari, 2024. Ninakushukuru.
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na ninakushukuru na mimi kunipatia nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nauliza, Wizara ina mkakati gani kushirikiana na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuhakikisha vijana wetu wa Kitanzania wanapata elimu ya uzalendo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu ya swali la msingi kwamba elimu hii ya uzalendo tumekuwa tukiitoa kupitia makongamano pamoja na mitandao na vyombo vyetu vya habari. Pia nimezungumza kwa suala la ushirikiano Serikali tunafanya kazi kwa dhana ile ya collective responsibility, kwa maana Wizara moja inapokuwa na jambo kwenye Wizara nyingine lazima tuweze kushikiriana kuhakikisha kwamba tunatekeleza hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondoe wasiwasi kwa vile sasa masuala haya ya uzalendo na maadili yatakuwa yanafundishwa katika shule zetu kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu, bila shaka huko tunapokwenda ni kuzuri na kwa maana hiyo vijana hawa watakapotoka watakwenda kuhudumu kwenye maeneo mengine, katika Wizara nyingine ambayo bila shaka elimu hii watakuwa nayo toka wakiwa wadogo, ninakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa hali ya sasa ilivyo uzalendo kwa wananchi tulio wengi ni changamoto na Serikali imesema kwamba imekuwa ikitoa elimu hii kwa wananchi. Je, haioni sasa ni wakati wa kuongeza juhudi kuhakikisha elimu hii inawapata watu wote kwa ufasaha na kuweza kuwa chachu kwa kuelimika? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikijibu swali dogo la Mheshimiwa Mchungahela, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli jambo hili ni muhimu kwa wananchi wote, lakini nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, yeye ni Mbunge na vilevile ni Diwani kwenye halmashauri au jimbo lake, mambo haya yamekuwa ni ajenda muhimu hata katika Mabaraza yetu ya Madiwani. Kwa hiyo, tunachukua ushauri wake, vilevile tuweze kuhakikisha na sisi kama Wabunge kwenye Mabaraza yetu ya Madiwani kwamba elimu hii inawafikia Madiwani na wananchi wote katika maeneo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. (Makofi)
MHE. NORAH W. MZERU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali moja la nyongeza. Kwanza, nampongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa moyo wake wa huruma kwa kufanya maamuzi magumu kwa kuwarejesha wasichana waliopata mimba na kukatiza masomo yao. Je, Serikali imetekeleza mikakati gani, ili kuhakikisha wahanga wa ubakaji wanapata sauti na mifumo ya Sheria na haki inaboreshwa, ili kuzuia wasichana wasikatishe masomo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Norah, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwenye majibu ya swali langu la msingi, zipo jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuwalinda watoto wetu wa kike dhidi ya ubakaji na ukatili kwa ujumla. Jitihada hizo ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi wawapo shuleni, ujenzi wa mabweni pamoja na hosteli, kuanzisha madawati ya ushauri nasaha kwenye maeneo yetu ya shule na mpaka vyuoni kwa ujumla. Aidha, Serikali imeendelea na utoaji wa elimu kwa jamii, hususan dhidi ya vitendo hivi vya ukatili kwa watoto.

Mheshimiwa Spika, vitendo vya ubakaji ni kosa la jinai na adhabu yake inatolewa chini ya Sheria ya Adhabu, Kifungu Na. 16 ya Sheria yetu ya Bunge. Sheria hiyo inatoa adhabu kali ikiwemo kifungo cha miaka 30 au zaidi ya hapo. Kwa hiyo, hii ni mikakati ya Serikali kuhakikisha kwamba, vitendo hivi vinakomeshwa kwenye jamii yetu. Nakushukuru sana.
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Spika, Ahsante. Kumekuwa kuna unyanyapaa mkubwa sana kwa hawa wasichana ambao walipata mimba pindi wanapoamua kurejea kwenye shule zao walizokuwa wanasoma awali. Unyanyapaa huu unasababishwa kwanza na walimu wenyewe na pia, wanafunzi ambao wanasoma darasa moja.

Mheshimiwa Spika, je, sasa Serikali haioni sababu ya kutenga madarasa maalum kwa hawa ambao wanarudi mashuleni kwa sababu, ni watu maalum na wana mahitaji maalum? Kwa nini Serikali isione umuhimu wa kuanzisha hayo ma…?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Najibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Rehema Migilla, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Migilla anasema kuwarudisha kwenye shule hizo kunaleta unyanyapaa; kwanza tunapokea ushauri wa Mheshimiwa Migilla. Tutakwenda kufanya tathmini ya kina, lakini tunadhani kuwatenga na kuanzisha madarasa yao ndiyo unyanyapaa zaidi kuliko tutakapoanzisha ile elimu changamano.

Mheshimiwa Spika, lakini tumesema kwenye majibu ya swali la msingi, mwanafunzi huyu anapotaka kurudi shuleni ni ushauri wa mzazi au mlezi pamoja na mwanafunzi yeye mwenyewe kwamba, ni eneo gani anahisi kwa upande wake yeye litakuwa ni rahisi na jepesi kurudi bila kupata changamoto yoyote. Kwa hiyo, ngoja tukafanye tathmini ya kina kwenye maeneo hayo kwa sababu, waraka huu ni wa mwaka 2021 ndiyo tunaendelea kuutekeleza tuweze kuona performance yake halafu tukiona kwamba matokeo yake siyo chanya, tutafanya marekebisho na kufuata ushauri wa Mheshimiwa Migilla. Nakushukuru sana.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kuwa, kuna baadhi ya walimu wakuu wa shule huwawekea vikwazo watoto ambao walipata ujauzito kurudi shuleni kwa wakati. Nini kauli ya Serikali?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Najibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mnzava kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Waraka Na. 1 wa Mwaka 2021 unaelezea utaratibu mzima wa namna gani ya watoto hawa kurudi shuleni. Kwa hiyo, mwalimu mkuu hawezi kuwa kikwazo cha watoto hawa au huyu anayetaka kurudi shuleni, kurejea kama atafuata vizuri huo waraka.

Mheshimiwa Spika, nadhani wajibu wetu sisi ni kuhakikisha kwamba, waraka huu unaufikia umma, ili kujua ule utaratibu kwa sababu, kimsingi hatakiwi kuanzia pale shuleni moja kwa moja, anaanzia kwa Afisa Elimu na kama mwalimu mkuu ataleta changamoto yoyote, basi Afisa Elimu au Mkurugenzi au Mkuu wa Wilaya wa eneo husika anahusika moja kwa moja kuhakikisha kwamba, mtoto huyo anarudi shuleni bila kikwazo chochote cha mwalimu mkuu. Nakushukuru sana.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Sasa hivi takwimu zinaonesha kuna ongezeko kubwa sana la wavulana kuacha elimu ya msingi na elimu ya sekondari. Je, Serikali haioni ni muda muafaka sasa hivi kutenegeneza mkakati ambao pia, utawarejesha katika mfumo wa elimu wavulana hao ambao wameacha shule kwa sababu, ni haki yao ya msingi?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Abdallah Chikota, Mbunge wa Nanyamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli, kuna changamoto kwa upande wa watoto wetu wa kiume na wao vilevile wamekuwa wakikatiza masomo kwa namna moja au nyingine, lakini Waraka wetu huu Na. 1 wa Mwaka 2021 umeeleza wazi kwamba, utahusiana na watoto wetu wa kike waliopata ujauzito pamoja na watoto wengine waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, lakini namuondoa wasiwasi Mheshimiwa Chikota, hivi sasa pale Wizarani tumetengeneza timu ya kufanya utafiti wa kupata sababu hasa za msingi ni kwa nini kuna hii dropout au kukatiza masomo kwa wanafunzi wetu au vijana wetu wa kike na wa kiume. Baada ya utafiti huo tutapata kujua hasa sababu maalum zinazosababisha jambo hilo, lakini kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba, watoto wetu hawakatizi masomo.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu, kama mnavyofahamu kwamba, Sera yetu ya Elimu imepanua wigo wa elimu ya lazima kutoka miaka 7 kwenda miaka 10 kwa hiyo, ni lazima mtoto huyu atakapoingia darasa la kwanza akamilishe mzunguko wake wa miaka 10. Kwa hiyo, tunahakikisha tunatengeneza mikakati ya kuwa-retain wanafunzi hawa shuleni. Nakushukuru sana.
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi ya kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza nishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kweli inatusaidia sana. Tuliomba Chuo cha VETA Wilaya ya Kilombero tumepewa, tuliomba barabara ya lami tumepewa, Kiwanda cha Sukari shilingi bilioni 500 tumepewa, mradi wa maji shilingi bilioni 43 tumepewa, Hospitali ya Halmashauri tumepewa, kadhalika na kadhalika. Kwa kweli watu wanaochafua huko nje waache tunamshukuru sana Dkt. Samia kwa kazi kubwa anayoifanya. Naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, halmashauri ambazo zipo katika wilaya hazikupata Vyuo vya VETA, tulikubaliana kwamba, ziatapata shule maalum za ufundi. Je, ni lini ujenzi utaanza wa Shule Maalum ya Ufundi katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Ifakara kuna Chuo cha Ufundi vile vya FDC ambavyo vina eneo kati kati ya Mji wa Ifakara na eneo lile limekuwa likipata wavamizi mara kwa mara, je, Serikali haioni umuhimu wa kwenda kuzungushia fence katika chuo hicho ili kulinda eneo la chuo hicho? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Abubakari Damian Asenga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kupekee tupokee pongezi hizo za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, yeye ndio amewezesha hayo yote kutokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la kwanza kwa kupande wa shule zile za ufundi nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge ni kweli Serikali ina azma ya kujenga shule za ufundi katika majimbo yale ambayo hayakujengewa Vyuo vya VETA. Tunafahamu kwamba hivi Vyuo vya VETA vinajengwa katika wilaya pia tunafahamu kuwa zipo wilaya ambazo zina majimbo zaidi ya moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, iwapo kama VETA imejengwa katika Jimbo moja na wilaya hiyo ina majimbo zaidi ya moja, tafsiri yake shule hizi za ufundi tunakwenda kujenga kwenye yale majimbo ambayo yamekosa fursa za kujengewa vile Vyuo vya VETA.

Kwa hiyo, nikuondoe wasiwasi hivi sasa tupo katika maandalizi ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hizi zipo tayari. Tunafanya upembeuzi yakinifu pamoja na kufanya zile site visit kwa ajili ya kukagua yale maeneo ambayo zitajengwa shule hizi za ufundi na tunapofika Julai tunatarajia shule hizi ziweze kuanza kujengwa rasmi. Kwa hiyo, lini tunaanza? Tutaanza mwaka ujao wa fedha kwa maana Julai mwaka huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa pili kwenye vyuo vyetu vile vya FDC, ni kweli tuna vyuo vya FDC karibu 54 katika nchi yetu. Vilikuwa kwenye hali mbaya sana, vyuo hivi Serikali imeshafanya ukarabati, tumeongeza majengo kwenye baadhi ya maeneo ambako kulikuwa hakuna majengo, tumefanya ukarabati kwenye yale majengo ya zamani, tumenunua vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwenye vyuo hivi, kwa vile sasa shughuli hizi zote zilikuwa zinakwenda kwa awamu, awamu inayofuata sasa tunaangalia kwenye yale maeneo ambayo kuna uhitaji wa kujengewa uzio kwa ajili ya kujenga uzio.

Kwa hiyo, nikuondoe wasiwasi, tunaenda kwa awamu na uzio kwenye vile vyuo ambavyo viko mijini ambavyo tunaona kabisa kuna haja ya kujenga uzio tutakwenda kujenga uzio, ninakushukuru sana.
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Waziri, kwanza ninakushukuru kwa kunipa Chuo cha VETA Mbogwe, lakini kazi haifanyiki mpaka sasa hivi hata mafundi wametoka site. Mheshimiwa Waziri, shida ni nini? Kwa sababu wananchi walijua kwamba mwaka kesho tutaenda kuanza kukitumia hicho chuo. Ninahitaji majibu yako ili kusudi wananchi wa Mbogwe wajue, ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Maganga, Mbunge wa Mbogwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa vyuo hivi 64 vya wilaya pamoja na kile kimoja cha mkoa tunajenga kwa awamu na nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, baada ya kumaliza misingi kuna vifaa ambavyo inabidi tuagize. Tumefanya bulk purchase kutoka viwandani moja kwa moja. Katika zile karakana na majengo yale makubwa yote tunatumia Mfumo wa LGS (Light Gauge Steel), zile ni fabricated metals ambazo zinatoka kiwandani moja kwa moja. Kwa hiyo, unapoona ujenzi umesimama tayari tumesha-press order kwa ajili ya hizo fabricated metals na baada ya muda si mrefu zitakuja na zikishafika pale site ni kazi ya mwezi mmoja tu majengo yale yote yatakuwa tayari yameshanyanyuka.

Kwa hiyo, nikuondoe wasiwasi, kazi hiyo inaendelea, fedha zimeshalipwa kule ALAF na shughuli inaendelea kwa sababu zinakuwa imported. Mara baada ya kufika tutakuja hapo Mbogwe na kukamilisha hiyo kazi. (Makofi)
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Halmashauri ya Moshi ina vijana wengi sana ambao wanahitaji elimu ya ufundi. Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA katika halmashauri hiyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimwia Mwenyekiti, ninaomba nijibu swali dogo la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwisha kujibu kwenye maswali ya msingi kwamba kwa sasa baada ya kukamilisha ujenzi wa vile vyuo 25 vya awamu ya kwanza katika wilaya 25 na hivi 64, tutakuwa hatuna wilaya ambayo haina Chuo cha VETA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu kwamba kunawezekana kukawa na umbali wa namna moja au nyingine lakini ninaamini pale Moshi tuna Chuo cha VETA ambacho kiko pale Moshi, ni chuo cha mkoa, lakini vilevile kina-save kama chuo cha wilaya, lakini kwenye zile wilaya nyingine za pembezoni, ukienda Rombo, ukienda Hai, ukienda Siha, kote kule tumejenga Vyuo vya VETA na yale majimbo ambayo hayana vyuo tunakwenda kujenga shule za ufundi ku-complement pale ambapo Chuo cha VETA kimekosekana. (Makofi)
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ni miongoni mwa wilaya ambazo zimeanza ujenzi wa VETA eneo la Wilaya ya Tanganyika, lakini kwa bahati mbaya sana mpaka sasa tunavyozungumza ujenzi umekwama takribani zaidi ya miezi mitano. Ni lini Serikali itapeleka fedha kukamilisha ujenzi wa VETA Wilaya ya Tanganyika?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Kakoso, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali tumeshapeleka fedha na ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, pesa tulizopeleka hizi shilingi milioni 324.6 katika kila site, hizi zimekwenda kwa ajili ya zile local materials, kwa maana ya mchanga, kokoto, mawe, maji, lakini pamoja na gharama za kulipa mafundi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zile materials nyingine zote Wizara inanunua kwa mfumo wa bulk purchase kwa maana ya simenti, nondo, mabati pamoja na zile LGS (Light Gauge Steel) kwa ujumla wake. Kwa hiyo, iwapo kama misingi yote imeshakamilika na maboma yameshanyanyuliwa, tafsiri yake kinachosubiriwa sasa ni vile vifaa kutoka kiwandani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Kakoso, hivi sasa tayari vifaa hivi vimeshaagizwa na mara baada ya kufika tutavipeleka katika kila centre kuhakikisha kwamba majengo hayo yananyanyuka. Lengo letu ifikapo mwezi wa 10 vyuo hivi kwa awamu hii ya kwanza yale majengo tisa yawe yamekamilika ili mwezi wa 11 tuweze kuanza kutoa mafunzo rasmi, ninakushukuru sana. (Makofi)
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza nianze kwa kumshukuru sana Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha shilingi 2,400,000,000 kujenga chuo bora kabisa cha VETA Wilaya ya Ikungi. Sasa hivi tunavyoongea chuo kimeanza kazi chini ya Mkuu wa Chuo Ndugu Mathias Luhanga na wanafunzi wako darasani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka niombe tu Mheshimiwa Waziri kwamba kwa ajili ya mambo ya kiutawala chuo chetu kinahitaji usafiri. Ninaomba sana kujua ni lini Serikali itawaletea gari kwa ajili ya kufanya kazi za kiutawala katika Chuo chetu cha VETA Ikungi? Ahsante sana (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nikijibu swali dogo la Mheshimiwa Mtaturu, Mbunge wa Ikungi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwenye vyuo vyetu 25 tuna changamoto ya usafiri lakini nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, safari ni hatua na hatua tumeshaanza, kimsingi kwanza tulianza kujenga yale majengo, lakini baadaye tukajaribu kutafuta watumishi kwa ajili ya mafunzo hayo kuanza na hivi sasa mafunzo yameanza. Tumeanza kupeleka vifaa na hatua inayofuata ni kupeleka sasa vile vyombo saidizi kwa ajili ya kuhakikisha wataalamu wetu, walimu wetu na watumishi wetu wanafanya kazi zao kwa ufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi, katika bajeti yetu ijayo tumeweka fungu kwa ajili ya ununuzi wa magari, kwa ajili ya vyuo hivi vya VETA, FDC pamoja na vyuo vyetu vya ualimu. Tunaamini katika utekelezaji wa bajeti ya mwakani mambo hayo yatakwenda kufanyika.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, tunaishukuru Serikali kwa ukarabati mkubwa uliofanywa katika Chuo Tango FDC, Mbulu Mjini, je, Serikali ina mkakati gani sasa wa kumalizia yale majengo yaliyobaki kukarabatiwa ili chuo kile kiwe na hadhi?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nikijibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Zacharia, Mbunge wa Mbulu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli pale Tango tumefanya ukarabati mkubwa na baadhi ya majengo bado hatujakamilisha. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Zacharia, lakini ninakumbuka juzi ulikuja kwenye meza yangu tukalizungumza jambo hili pamoja na suala la kwenda kule Tango na nikakuahidi kwamba tusubiri tukamilishe shughuli za Bunge ili tuweze kwenda kuona hali halisi ilivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nikuondoe wasiwasi, katika Mradi wetu wa EP4R ambao tunataraji kuanza mwaka ujao wa fedha, tuna mpango wa kukarabati majengo yote katika vyuo vyote vya FDC ambavyo bado hatujafanya ukarabati. Kwa hiyo, kama nilivyokwisha kujibu kwenye swali moja la nyongeza hapa la FDC kule Ifakara, basi vilevile na Tango tutakwenda kufanya kama tutakavyofanya Ifakara. (Makofi)
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi na ninaipongeza Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan chini ya Wizara ya Elimu, Waziri na Naibu Waziri kwa kuanza ujenzi wa Chuo cha VETA ndani ya Wilaya ya Missenyi. Chuo hicho ni matarajio makubwa ya Wana-Missenyi na kimeanza lakini spidi yake kwa kweli hairidhishi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini sasa tutapata vifaa vya ujenzi ili tuweze kwenda kwa speed na tuweze kupata chuo hicho ambacho ni matarajio makubwa kwa Wana-Missenyi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kyombo, Mbunge wa Missenyi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwisha kujibu kwenye maswali mengine ikiwemo na hili la Mheshimiwa Kyombo kule Missenyi, sasa hivi tunachosubiri ni vile vifaa ambavyo ni imported materials, zile fabricated metals (LGS) kwa ajili ya majengo yetu yale makubwa, makarakana yale manne yote yale yanahitaji materials hizo, lakini pamoja na bati ambapo nimesema tayari tumesha-press order, tumeshalipa na vifaa hivyo viko njiani kuja. Mara vitakapofika mtashangaa ile speed yetu tutakayokwenda kule, ndani ya mwezi mmoja yale majengo yote na mazingira ya pale yatakuwa yamebadilika kabisa na tunaamini mpaka itakapofika mwezi wa 10, Missenyi tutakuwa tumekamilisha yale majengo makubwa na huduma pale zinaweza kuanza mara moja.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Mheshimiwa Waziri, kwanza niipongeze Serikali kwa ujenzi wa VETA nchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu, kutokana na kwamba dunia ya sasa mabadiliko ya teknolojia, maeneo mengi ya VETA ambazo zinajengwa, masomo yanayotolewa ni ya aina ile ile, ufundi ujenzi nyumba, ufundi cherehani na ufundi Seremala lakini soko la vijana nje linahitaji masomo mengine. Ufundi bomba, ufundi umeme wa magari, ufundi umeme wa majumba, lakini mitambo ya gesi kama usambazaji wa gesi unaoendelea nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni upi mkakati wa Wizara, wakati Mheshimiwa Rais anaendelea kujenga VETA nchini, ni upi mkakati wa Wizara kubadilisha syllabus ziendane na soko la sasa ili tuokoe vijana wengi wa Kitanzania wapate fursa hiyo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikijibu swali la Mheshimiwa Sanga kama ifuatavyo, Mheshimiwa Sanga anatoa ushauri kwa maana ya kubadilisha mtaala, lakini nikuondoe wasiwasi Mheshimiwa Sanga tayari Mheshimiwa Rais alishaliona hilo na alishaagiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeanza na maboresho makubwa ya mitaala yetu kuanzia shule za msingi, sekondari mpaka vyuo vikuu, lakini Mheshimiwa Rais aliagizwa kwamba, VETA hizi zinazojengwa, basi mitaala yake na masomo yake na kozi zake ziendane na shughuli za kiuchumi za sehemu husika, kwa maana tunakwenda kufanya customization katika vyuo hivi kwa lengo la kuhakikisha kwamba zile shughuli za kiuchumi zinazofanyika katika maeneo hayo ziweze kufundishwa katika vyuo hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, yale maeneo ambayo tunachimba madini tutakuwa na kozi za madini zinafundishwa kwenye vyuo hivi, yale maeneo ambayo tunashughulika na masuala ya uvuvi kutakuwa na kozi za uvuvi zinafundishwa kwenye maeneo haya, kule kwangu nako kimejengwa chuo kama hiki, kuna masuala ya utalii, lakini vilevile masuala ya hospitality yatafundishwa kwenye vyuo hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunakwenda kuhakikisha zile shughuli sasa za kiuchumi ndizo zitakazofundishwa, tukiongezea na hizi kozi nyingine za general ambazo kila mmoja wetu anapaswa kuzifahamu ili hata bomba likikatika pale nyumbani kwako huna haja ya kutafyta fundi, wewe mwenyewe unaweza kurekebisha kwa namna moja au nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, huo ndiyo mpango wa Serikali. Mheshimiwa Rais ameshatoa agizo na sisi kama Wizara ni lazima tutekeleze kwa kadri maagizo yalivyotolewa.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Chuo cha VETA kilichopo Manispaa ya Shinyanga ni chuo kongwe na kinahitaji ukarabati wa miundombinu. Ni upi mpango wa Serikali kukarabati Chuo cha VETA Manispaa ya Shinyanga? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nikijibu swali dogo la Mheshimiwa Dkt. Mnzava, ni kweli tuna vyuo vyetu, baadhi ya vyuo vyetu vya mikoa ni vya muda mrefu, majengo yake ni chakavu na miundombinu mingine ni chakavu, hata vifaa vilivyokuwa vinatumika ni vile vya muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Dkt. Mnzava, tuna miradi mbalimbali ambayo tumeshafanya maandiko yake na maandiko hayo yatakapokamilika na miradi hii kuanza tutakwenda kufanya ukarabati kwenye vyuo vyetu vyote kongwe kikiwemo na hiki Chuo cha Mkoa wa Shinyanga. (Makofi)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni kwamba katika Kata ya Mwika Kaskazini kwenye Jimbo langu la Vunjo kwenye Shule ya Msingi ya Lole kuna Chuo cha VETA ambacho kimetelekezwa kutoka mwaka 2000. Majengo yamechakaa, lakini kuna baadhi ya tools za kutumia kufundishia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kinachohitajika pale ni kukarabati yale majengo na kupata walimu wa kufundisha, basi pamoja na kuongeza hasa hivyo vifaa vya kufundishia. Je, ni lini Serikali itachukua hatua?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii sijui ni mara yangu ya tatu ninauliza swali hili, lakini nimeona nirudie kwa sababu wale wananchi wanateseka sana. Jimbo la Vunjo liko pacha na Jimbo la Moshi Vijijini kwenye halmashauri moja. Kwa hiyo, kuna disadvantages nyingi sana ambazo tunapata kwenye ku-allocate hizi facilities. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nikijibu swali dogo la Mheshimiwa Dkt. Kimei ni kuwa jambo hili ulilolizungumza ninaomba tu tutoe maagizo kwa Mkurugenzi wetu wa VETA, kwanza kwenda kuona hilo eneo, lakini Mheshimiwa Dkt. Kimei kama utaridhia ninadhani ni muhimu na sisi tukaenda tukaona, wazungu wanasema; “the seeing is believing.” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninadhani kuna umuhimu wa kupanga ratiba na sisi wenyewe kama Wizara, mimi binafsi niende nikaone tuweze kufanya tathmini ya kina ili tuweze kujua kitu gani, measures zipi tuweze kuchukua ili kama ni chuo ambacho kimeshakabidhiwa kwenye Wizara, basi tufanye ukarabati kama ulivyoshauri. Tupeleke vifaa pamoja na walimu ili mafunzo hapo yaanze kutolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuanzia tunaomba tumwagize Mkurugenzi wa VETA aweze kwenda eneo hilo kwa haraka na sisi tukimaliza Bunge hapa tutakwenda. Mheshimiwa Dkt. Kimei tutapanga na nitakuja hapo kwako tupange ratiba ya kwenda huko haraka iwezekanavyo. (Makofi)
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Wilaya ya Manyoni ina majimbo mawili. VETA inayoendelea kujengwa katika Manyoni iko katika Jimbo la Manyoni Mashariki. Unawaambiaje watu wa jimbo langu eneo la Itigi kuhusu ujenzi wa shule ambayo mmeitaja? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nikijibu swali dogo la Mheshimiwa Massare ni kwamba Mheshimiwa Massare anajua na tulishazungumza suala hili na alikuja ofisini na akaangalia orodha ya shule zitakazokwenda kujengwa za ufundi na Wilaya ya Manyoni, ilikuwa Manyoni imekosewa, Manyoni Kaskazini na Manyoni Kusini tukarekebisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Massare, shule yake ya Ufundi ipo, tumeshafanya marekebisho mwanzoni kulikuwa na typing error. Shule ile itakwenda kujengwa katika jimbo lake kama vile alivyoshauri yeye mwenyewe na kazi hii itaanza Julai mwaka ujao wa fedha. (Makofi)
MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza kabisa sina budi kuipongeza Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo inakuwa sikivu na ni mwaka jana tu tulishauri hapa Bungeni kuhusu elimu hii ya uraia na uzalendo na mwaka huo huo 2023 kazi imefanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maswali mawili ya nyongeza kwa lengo la kuboresha zaidi. Swali langu la kwanza je, mtaala huu umeshaanza kutumika ama unakaribia kutumika? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili ni kwamba, kama umeshaanza kutumika ama utatumika karibuni, kwa nini Serikali haioni umuhimu wa kurudisha vitabu vilivyokuwa vikitumika zamani? Kwa mfano, Msichana Jifahamu, vitabu ambavyo vina maudhui yanayomjenga kijana wa kiume na wa kike kuweza kujikinga na masuala ya mahusiano yasiyo rasmi wakati wa umri mdogo na yanayosababisha kuharibikiwa kimasomo pamoja na kupotoka kimaadili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Najma Giga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Giga, amekuwa akifuatilia kwa karibu kuhusiana na suala la maadili ya vijana wetu. Kwenye eneo lake la kwanza ambalo anahitaji kufahamu juu ya utaratibu wa mitaala na utekelezaji wake, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Giga na Bunge lako Tukufu kwamba mitaala yetu mipya imeanza kutekelezwa tokea Januari mwaka huu 2024 na tumeanza kutekeleza kwa awamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaanza na elimu ya awali wataanza na mtaala mpya, darasa la kwanza pamoja na darasa la tatu, vilevile kwa kidato cha kwanza. Kwa hiyo mtaala wetu kimsingi umeishaanza kutekelezwa hivi tunavyozungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo la pili kwenye masuala ya vitabu vile vya zamani. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba vipo vitabu vya zamani ambavyo tunaendelea kuvitumia mpaka sasa kama vitabu vya kiada na ziada, vilevile yapo maudhui ya vitabu vya zamani vile vitabu havitumiki lakini maudhui yake yameweza kuchomekwa kwenye vitabu vipya ambavyo vimetungwa hivi sasa ambavyo tunatumia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile stadi hizi unazozingumza za vijana wetu zimeendelea kufundishwa. Kwa upande wa elimu ya awali, tuna klabu mbalimbali za masomo wanafundishwa vijana wetu stadi mbalimbali zikiwepo na hizi za maisha. Upande wa Sekondari na Msingi stadi hizi za masomo zimeweza kuchomekwa kwenye masomo mbalimbali. Kwa hiyo, nikuondoe wasiwasi mambo haya yote Serikali imezingatia na tutatekeleza kwa kadri ninyi Wabunge mnavyoona inafaa, nakushukuru. (Makofi)
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kumwuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

(a) Kwa kuwa, majengo hayo yameanza kutumika na amekiri kwamba chuo ni kipya, je, Wizara ina mpango gani wa kuongeza fani zinazofundishwa katika Chuo cha Ufundi VETA – Chikundi hasa zitakazowajumuisha vijana wa kike ikiwemo upishi na ushonaji?

(b) Wizara ina mpango gani wa kuongeza majengo kwa ajili ya watumishi ili iendane na mafunzo yanatolewa na idadi ya watumishi ili waweze kufanya kazi zao vizuri? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Hokororo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoshasema kwenye majibu ya swali la msingi kwamba Chuo hiki kimeishafunguliwa na majengo yote yanatumika, nianze kwanza na swali la fani. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwa sababu chuo hiki ndiyo kwanza tumefungua na tunajua kwamba kuna mahitaji ambayo yanahitajika yakiwemo walimu. Kwa hiyo, nimwondoe hofu kwamba fani hizi zitakuwa zinaendelea kuongezeka kwa kadri mahitaji ya vifaa pamoja na wataalamu kwa maana ya walimu tutakapokuwa tunawapeleka pale, basi fani zitakuwa zinaendelea kuongezeka na tumesema fani ziendane na shughuli za kiuchumi eneo lile ambalo chuo hiki kimejengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa eneo la pili kuhusiana na uongezaji wa miundombinu kwa maana ya majengo, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu kwamba vyuo hivi vimejengwa 25 katika awamu ya kwanza katika Wilaya pamoja na Mikoa Minne na tunajenga kwa awamu. Kwa hiyo, awamu ya kwanza ilikuwa tujenge majengo ambayo yatawezesha chuo kuanza kutoa mafunzo, lakini awamu ya pili itakuwa sasa ni kuongeza miundombinu ikiwemo na nyumba za watumishi pamoja na miundombinu mingine ambayo itakuwa inahitajika kwa ajili ya kutoa mafunzo kwenye maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo niwaondoe wasiwasi, siyo tu hapa Chikundi lakini kwa vile vyuo vyote 25 ambavyo tumejenga na vile vinne vya mikoa na hivi sasa Mheshimiwa Rais ameishatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyuo 64 katika Wilaya 64 na Chuo kimoja cha Mkoa kule Songwe, tunaendelea na ujenzi huo na unakwenda kwa awamu, nakushukuru.(Makofi)