Primary Questions from Hon. Rose Vicent Busiga (3 total)
MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:-
Je, lini Serikali itapeleka fedha za kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya, Kata ya Nhomolwa – Mbogwe?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Nhomolwa kipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe. Kituo hiki kilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kwa kujenga jengo la kutolea huduma za nje (OPD) na majengo mawili ya wodi ya kulaza wagonjwa.
Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/2023 na 2023/2024, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mbogwe ilipeleka shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la wagonjwa wa nje na nyumba ya mtumishi ya two in one, ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje umekamilika na kituo kimeanza kutoa huduma mwezi Oktoba, 2023.
Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mbogwe imetenga shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo la maabara. Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa majengo ya Kituo cha Afya cha Nhomolwa. Ahsante. (Makofi)
MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:-
Je, lini Serikali itapeleka fedha za kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya, Kata ya Nhomolwa – Mbogwe?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Nhomolwa kipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe. Kituo hiki kilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kwa kujenga jengo la kutolea huduma za nje (OPD) na majengo mawili ya wodi ya kulaza wagonjwa.
Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/2023 na 2023/2024, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mbogwe ilipeleka shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la wagonjwa wa nje na nyumba ya mtumishi ya two in one, ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje umekamilika na kituo kimeanza kutoa huduma mwezi Oktoba, 2023.
Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mbogwe imetenga shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo la maabara. Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa majengo ya Kituo cha Afya cha Nhomolwa. Ahsante. (Makofi)
MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:-
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Bukombe hadi Katoro kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Barabara ya Bukombe – Katoro yenye urefu wa kilometa 58.20 kwa kiwango cha lami, unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Awamu ya kwanza inahusisha sehemu ya Bukombe (Ushirombo) hadi Bwenda (kilometa 5.3). Zabuni za kumpata mkandarasi zimefunguliwa tarehe 20 Januari, 2025 na kazi ya tathmini ya zabuni hizo inaendelea.
Mheshimiwa Spika, kwa sehemu ya pili ya kutoka Kashelo hadi Nyikonga (kilometa 10.4) pamoja na Daraja la Nyikonga iko katika hatua ya majadiliano. Mkataba wa kazi unatarajiwa kuwa umesainiwa kabla ya mwisho wa mwezi Februari, 2025. Kwa sehemu zilizobaki za Bwenda – Kashelo (kilometa 16.3) na Nyikonga – Katoro (kilometa 26.2), Serikali inaendelea kutafuta fedha, kwa ajili ya ujenzi.