Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Khadija Shaaban Taya (22 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
MHE. HADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa nafasi hii. Ikiwa leo ni siku ya kwanza nazungumza katika Bunge lako hili tukufu naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu sana, mwingi wa rehema na mwenye kurehemu amenijalia mimi kuwa hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia naomba kumshukuru Mheshimiwa Rais na chama chake, Chama Cha Mapinduzi, Wajumbe wa Baraza wa Dodoma hii Mkoa, Wajumbe wa Baraza wa Taifa, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ndugu Heri James na Umoja wa Vijana na Wazazi wote ahsante sana, muda hautoshi kushukuru wote, lakini naomba niishukuru familia yangu sana kwa support kubwa ambayo wamenionesha mpaka sasa kufikia hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ikiwa leo ni siku saratani duniani, mimi kama mtu mwenye ualbino nimeomba niongee leo ili niwaambie umma kwamba Mheshimiwa Rais amefanya kazi nzuri sana kwa watu wenye ulemavu au watu wenye ualbino, amefanya kazi nzuri sana. Amenunua mashine ambazo zinasaidia kuondoa tatizo la saratani. Hizi mashine ziko saba katika mikoa ya Singida, Iringa, Mara, Lindi, Zanzibar na kwingineko, lakini naomba nimuombe Mheshimiwa Rais kwa huruma yake, kwa uwezo wake, kwa kupenda kwake wanyonge, aongeze hizi mashine zitapakae mikoa yote kwa sababu hizi mashine mimi ni shuhuda wa hizi mashine. Nilikuwa na alama hapa shingoni kwangu ambayo ingeweza kunisababishia kupata saratani, hii mashine imenisaidia mimi kupona leo hii ninavyozungumza hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia naomba Serikali yako tukufu, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, naomba kwa sababu ni sikivu sana, iongeze idadi ya lotions kwa watu wenye ualbino. Hizi lotions zinatusaidia sana kuondoa tatizo la kupata mionzi ya jua, hili tatizo ambalo linatufanya sisi tusiishi kwa amani tupate saratani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, natamani kila Mbunge aliyekuwepo hapa aende Ocean Road aone jinsi gani saratani ya ngozi inavyotumaliza na namna gani saratani ya ngozi inavyotuua. Na hata life span yetu ni miaka 35. Hapa nipo nina miaka 33 naingia miaka 34 tarehe 7 Februari, keshokutwa nashukuru Mungu kwa sababu familia yangu imeweza kunitunza na labda pia wamekuwa na uwezo kwa muda mrefu kunipa haya mafuta, lakini si kila familia ina uwezo wa kupata haya mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pamoja na yote haya naomba nimshukuru Rais mara ya mwisho kabisa. Nimwambie Mheshimiwa Rais ahsante sana kwa miaka mitano aliyoingia yeye ameondoa lile janga kubwa lililokuwa linaumiza Watanzania, lililokuwa linawaumiza na kuwaliza, lilimliza Waziri wetu Mkuu katika Bunge hili tukufu, janga la kuwauwa watu wenye ualbino. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, imani ile potofu imeondoka na sasa hivi tunaishi kwa raha, tunaishi kwa amani, tunajidai.

Ahsante sana Mheshimiwa Rais, lakini naomba nikwambie tena umejali sana watu wenye ulemavu, sasa hivi kila shule inajengwa kwa kuzingatia mazingira mazuri kwa watu wenye ulemavu kupita, lakini Mheshimiwa Rais pia nakuomba uboreshe mazingira ya vyoo kwa ajili ya afya. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa Mzungumzaji)

MHE. HADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba niunge hoja, naungana na hoja, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Nimepata taabu kukatiza Mheshimiwa Keisha.

MHE. HADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, basi naomba niendelee.

SPIKA: Hapana, basi tena. Siku nyingine nitakufikiria leo muda umebana kidogo. (Kicheko)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kupata fursa hii leo kuchangia taarifa ya Kamati yetu ya Katiba na Sheria. Kwanza kabisa naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amenipa uhai mpaka sasa, na jana nimeongeza mwaka mwingine, mwaka ambao mwaka umeinifanya nitafakari mambo mengi sana, leo hii nataka nizungumze na Bunge hili Tukufu lakini na Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamu fika kwamba Tanzania yetu inachukua hatua mbali mbali za kusaidia watu wenye ulemavu. Nafahamu fika Serikali imeleta mwongozo mzuri juu ya kuimarisha, kusaidia hali ya watoto ya watu wenye ulemavu. Hata hivyo, naomba niliambie Bunge hili Tukufu hali ya watu wenye ulemavu ni ngumu zaidi kuliko tunavyofikiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika likizo ya ya mwezi wa 11 na wa 12, nilipata kufanya ziara kwenda katika vituo mbalimbali vya watu wenye ulemavu. Mambo niliyoyaona kule ni magumu sana hata kuayelezea. Mfano tu mzuri nichukue hapa Kongwa nilenda katika Kituo cha Mlali, nimekuta kuna watoto wenye ulemavu wa viungo wako pale wanalelewa na Kanisa Katoliki la pale Mlali. Hali niliyokuta pale inatia huruma sana sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watoto wamepelekwa pale kwa ajili ya kupata huduma ya afya ya kunyooshwa viungo mbalimbali lakini pia kupata huduma ile ambayo kuna madaktari wa KCMC na madaktari wengine kutoka nje ya nchi wanakuja pale kwa ajili ya kusaidia au wanajitoa. Wazazi wamekuwa wakipeleka watoto wao pale lakini wazazi wengine wameshindwa kwenda kuwaona watoto wao katika vile vituo kwa sababu kile kituo kina chaji shilingi 130,000 kwa ajili ya mtoto kupata huduma katika eneo lile. Sasa najiuliza, kwa Mtanzania wa kawaida anaweza kumudu hii shilingi 130,000 kwa ajili ya mtoto wake kupata huduma katika kituo kile? Mtanzania wa kawaida kila mwezi, 130,000 anaweza? Hilo ni swali la kujiuliza sisi Wabunge humu ndani ambapo katika maeneo yetu vituo kama hivi vipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuangalia tu, mzazi anayeshindwa kulipia hiyo anamwacha mtoto wake pale anaondoka harudi tena kumwona, watoto wanatelekezwa katika vituo vile kwa sababu huyu mzazi anaona fika kabisa kwamba mimi sina hii fedha, naendaje pale. Nitakabidhiwa huyu mtoto, nitawezaje kumhudumia? Ningeomba sana Serikali iangalie hili jambo kwa upande wa pili waone kabisa zaidi. Wazazi wanaozaa watoto, wenye watoto wenye ulemavu wanapata shida ngumu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka mama yangu aliwahi kuniambia wakati nazaliwa, kabla baba yangu hajaja kuniona hospitali. Kuna mtu aliwahi kumuuliza kwamba hivi, unafikiri Shabani ataweza kumpokea huyu mtoto? Atamkubali kweli? Hii ni changamoto ambayo wazazi wengi wanakutana nayo, lakini cha kushangaza baba yangu aliponiona alinifurahia na kunikumbatia na leo hii nimefika hapa nilipo. Kwa sababu familia yangu iliweza kunikubali na kunilea na leo hii mimi sijioni kama ni mtu mwenye ulemavu; na watu wengi humu ndani wananiambia kwamba wewe mbona siyo mlemavu? Ni kwa sabau nimelelewa vizuri na familia ambayo ilinikubali na changamoto zangu na kunilea hadi nilipofika hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tuangalie, ni familia ngapi zinamudu? Akina mama wengi wamekuwa wakitelekezwa na mababa kwa ajili ya kuzaa watoto wenye ulemavu na wanabaki na watoto wale wanawalea wenyewe. Wanapata shida nyingi mno. Leo hii Bunge hili, hapa akija mtu mwenye ulemavu wanatoa huduma ya msaidizi, kwa sababu wanafahamu fika kabisa huyu mtu mwenye ulemavua ana changamoto, hawezi kujihudumia mwenyewe lazima apate msaidizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tujiulize, yule mzazi ambaye yupo nyumbani, amezaa mtoto mwenye ulemavu, ni msaidizi gani, ni familia gani au ni ndugu ugani ambaye anaweza akakaa na huyu mtoto ambaye ana ulemavu atakulelea wewe? Ina maana huyu mzazi hana budi akae nyumbani, aweze kumlea huyu mtoto, amhudumie mwingine hawezi hata kujilisha mwenyewe. Hawezi hata kuoga mwenyewe. Je, Serikali inamfikiria vipi huyu mama ambaye hawezi kufanya shughuli nyingine zaidi ya kumlea mtoto wake?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilikuwa naona kabisa Serikali ione namna na haja ya kuona fika kabisa kwamba waone hawa wazazi either watafutiwe wasaidizi, kwamba Serikali ichukue jukumu la kulea au watafute namna ya kuwawezesha hawa wazazi waweze kupata fedha kupitia zile asilimia mbili. Asilimia mbili ile isaidie akina mama ambao wana watoto wenye changamoto ya ulemavu waweze kujikwamua kiuchumi ili tuone namna gani tuweze kuona hawa watu waweze kulea watoto wao, waone fika kabisa na wao ni part ya Tanzania hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri upo pale katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mtu mwenye ulemavu akifika pale anapata msaidizi kwa siku analipiwa shilingi 10,000. Anapata bajaji ya kwenda kumpeleka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Hivi vitu vyote tunafanya juu huku. Bunge linafanya, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinafanya; lakini vipi huku chini kwenye ngazi ya familia? Kwa sababu kama huyu mzazi ameweza kutelekezwa na mwanaume kwa ajili ya kulea, ndugu pia wanaweza kuona kwamba huu ni mkosi kwenye familia yetu. Analeaje huyu mtoto?

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamani, Bunge hili naamini kabisa, watu wote sidhani kama kuna mtu ambaye hajawahi kufuatwa na shida za watu wenye ulemavu; na ukiangalia fedha ya jimbo haiangalii kusaidia watu wenye ulemavu. Watu wanaingia kwenye mifuko yao kusaidia watu wenye ulemavu. Juzi tumepata takwimu ya sensa lakini bado majibu hatujayapata ya kujua idadi gani ya watu wenye ulemavu ambao wapo katika hii nchi ili Serikali sasa iweze kusaidia. Sasa tunahitaji zile takwimu ili tujue katika kila jimbo kuna watu wangapi wenye watoto wenye ulemavu wanawalea ili sasa Serikali ione haja na Bunge hili lishauri namna gani ya kusaidia hawa wazazi wenye hawa Watoto?

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii naamini kabisa jambo lolote likija whether kwa kukatwa tozo, whether kwa kukatwa mishahara yetu sidhani kama kuna mtu humu ndani ataweza kuwa na sauti ya kusema kwamba jambo hili hapana, wananchi watakasirika kwa ajili hawataki kuhudumia watu wenye ulemavu. Sasa hivi tumeona kabisa watu wanatafuta namna ya kujikwamua kiuchumi wanatumia watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kuna tamthiliya ya Juakali. Ukiangalia mazingira ya ile tamthiliya mule ndani Mtu ana NGO yake anaita watu wenye ulemavu anatengeneza story apate fedha halafu anajinufaisha yeye na familia yake. Yale ndiyo maisha halisi ya huku nchini, siyo tamthiliya ile. Kuna mzazi mwingine ana mtoto wake mwenye ulemavu amemficha ndani, anashindwa namna ya kutoka kwenye jamii, anaona ni aibu, anaona ni mikosi. Hivi vitu si kwenye tamthilia, ni maisha halisi ya Watanzania. Sasa Bunge hili lione namna halisi ya kusaidia watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi namshukuru sana Mheshimiwa Rais. Amekuja na huu mwongozo, ni mwanzo mzuri mno, Serikali mmeanza vizuri mno. Sasa kwa Serikali hii mama, kama Mheshimiwa Rais unanisikia, ninakuomba usije kuondoka katika Serikali hii kama haujatatua shida za watu wenye ulemavu kuona namna gani ya kusaidia. Kwa sababu ukiangalia idadi ya watu wenye ulemavu katika nchi hii ni wachache mno na Serikali hii ikiipa kipaumbele, hatushindwi kitu. Kuna kampuni nyingi tu ambazo zinafanya kazi katika nchi hii. Kuna fedha nyingi wanazo, CSR sijui nini na nini. Mfuko wa watu wenye ulemavu ni muhimu kulea watoto wenye ulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naomba Bunge hili Tukufu, endapo sheria hii itakuja muiunge mkono, kwa sababu naamini kila mtu hapa ni mlemavu mtarajiwa. Kwa sababu naamini kuna Wabunge humu ndani wamekuja wakiwa wazima na sasa hivi ni watu wenye ulemavu na leo hii sisi tuna watu tunawazaa humu ndani, tutazaa watoto wenye ulemavu. Leo hii tukitengeneza msingi mzuri au tathmini nzuri ya watu wenye ulemavu kuishi vizuri, tunajitengenezea sisi wenyewe na kizazi chetu cha baadaye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kusema hayo naunga mkono hoja nashukuru sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2021 (Toleo la Kiingereza)
MHE. HADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kupata nafasi hii ya kuzungumza leo mara ya pili.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nikupe pole wewe pamoja na Bunge lako Tukufu na Wabunge wote kwa kuondokewa na kipenzi chetu, rafiki yetu, Mheshimiwa Nditiye.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesimama hapa mbele kuzungumza juu ya hii sheria ambayo imekuja kuhusu kutumia Kiswahili katika Mahakama zetu. Mimi naona umuhimu wa hili. Nitashangazwa sana kama kuna mtu ataona hakuna umuhimu katika hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimekuwa msanii kwa muda mrefu sana na katika tasnia ya sanaa, kikubwa sana kilichokuwa kinatufanya tupoteze haki zetu ni kwa sababu ya kutokujua lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo ilikuwa inaandikwa katika mikataba yetu mingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, wengi sana wamepoteza haki zao, wengi sana wamepoteza uwezo, mpaka sasa ambapo tumeweza kuwa na uwezo wa kumiliki Wanasheria. Kwa muda huo tulikuwa hatuna uwezo wa kuwa na Mwanasheria, fedha hizo tulikuwa hatuna. Kwa hiyo, nafahamu umuhimu wa kutumia Kiswahili katika hizi Mahakama zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niongee jambo lingine kwamba tulipopata safari ya kwenda China kupata mafunzo ya Chama cha Mapinduzi, nilipendezwa sana na tabia za Wachina. Vile vikao vilikuwa vinaendeshwa kwa lugha ya Kichina japokuwa wanajua kuzungumza Kiingereza. Wanazungumza Kichina, anatokea mkalimani anazungumza Kiingereza, halafu sisi mwenzetu anazungumza Kiingereza halafu anatafsiri kwa Kiswahili. (Makofi)

Mheshimiwa naibu Spika, kwa hiyo, tunatakiwa tutambue umuhimu wa hii lugha kwa sababu itatuletea heshima kama Watanzania. Watanzania wengi wanakwenda China wanafanya biashara na Wachina wengi wanakuja Tanzania wanafanya biashara pamoja na kutokujua lugha lakini wanafanya biashara. Kwa hiyo, naomba Bunge hili Tukufu liunge mkono hoja hii kwa kutambua umuhimu wa uzalendo wa nchi yetu na Mheshimiwa Rais ameonyesha uzalendo wa nchi yetu kwa kuzungumza Kiswahili katika vikao vyake vyote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hii hatua ambayo tunakwenda kutumia Kiswahili katika Mahakama zetu ni heshima kubwa sana kwa Tanzania. Kama kuna mtu ambaye hawezi kufahamu hili, namshangaa kwa nini amekuja kuwa Mbunge kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi wake ambao wanazungumza Kiswahili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lugha ambayo tunatumia hapa Bungeni ni Kiswahili, nasi ndiyo watunzi wa hizi sheria. Kwa hiyo, nashangaa kwa nini mtu hawezi kuona umuhimu wa kutumia sheria ya Kiswahili au kutumia Kiswahili katika Mahakama zetu kwa ajili ya kutoa haki? Hatujakataza kutumia Kiingereza, endapo kutakuwa na uhitaji wa kutumia Kiingereza watatumia, lakini bado itatafsiriwa kwa Kiswahili ili iweze kutusaidia baadaye kwa ajili ya records. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naunga mkono hoja hii iliyoletwa na Mheshimiwa Waziri, kama Mwanakamati wa Katiba na Sheria na Mwanasheria mpya sasa. Nashukuru sana kwa kuchangia leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Awali ya yote, naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe wote ambaye ametufikisha hapa leo tukiwa na afya njema na uhai ambao ametupa.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo napenda nijikite katika mambo mawili, matatu. Mojawapo nataka nizungumze juu ya watu wenye ulemavu na ajira. Katika kusoma na kufuatilia hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu nimegundua kwamba ni msikivu sana, amefanya kazi nzuri sana, amefanya kazi ambayo Mungu anamtaka yeye afanye. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati yetu ilishauri mambo kadhaa wa kadha lakini nashukuru moja ambalo umesema unaenda kulitekeleza ni hili la kuleta data kamili ya watu wenye ulemavu. Data kamili ya watu wenye ulemavu itatusaidia katika utekelezaji wa majukumu ya watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hiyo data kamili ya watu wenye ulemavu, kutakuwa na wasomi, wafanyakazi, watoto wadogo na wagonjwa ambao tutawatambua ili kutekeleza kwa urahisi kabisa malengo ambayo tumejiwekea kwa watu wenye ulemavu. Naomba niseme kwamba hali ya watu wenye ulemavu ni ngumu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niweke msisitizo katika suala la ajira. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, ameendeleza yote mazuri yaliyofanywa na Awamu ya Tano. Katika kuchagua na kujali Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu, amechagua watu watano katika Baraza la Makatibu Wakuu, hii pekee inaonesha dhahiri anatuamini sisi watu wenye ulemavu. Naomba Serikali iangalie suala hili kuanzia hapo, kwamba tumejaliwa watu watano wenye ulemavu basi ishuke mpaka chini kwenye watumishi ili tuweze kuonekana na kuonesha uwezo wetu ambapo tunaamini kabisa uwezo tunao.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tuangalie lile suala la asilimia tatu, je, limetimizwa na kwa ukubwa gani? Kwa sababu nikiangalia private sector, hata humu ndani tu kuna Wabunge wana makampuni makubwa, je, wametimiza ule wajibu wa asilimia tatu? Hili suala tulifuatilie, tusiwe tunaweka sheria ambazo hatuwezi kuzifuatilia kama zinatekelezeka. Tuweke sheria ambazo tunaweza tukazifuatilia tukajua kabisa hii idadi ya watu wenye ulemavu ya asilimia tatu inatekelezwa Serikalini pamoja na private sectors. Kwa private sector, mtu amewekeza pale akiamini mtu mwenye ulemavu hawezi, basi tuangalie namna gani ya kuwapa hawa watu motivation au kuangalia namna yoyote ile hata ya kuwapunguzia kodi fulani hivi ambayo inaweza wao kuwafanya waendelee kuajiri watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nayasema haya kwa sababu nafahamu watu wanaoniomba kazi na wanataka ada ya shule na kadhalika. Kwa hiyo, hizi data zitatusaidia sana, nawaomba ushirikiano katika hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia naomba nishukuru baadhi ya Wabunge ambao tayari wameendelea kuzungumzia watu wenye ulemavu na wale ambao wameendelea kujitoa katika majimbo yao kama kutoa miguu kwa watu wenye ulemavu wa viungo, kwa mfano, namshukuru sana Mheshimiwa Antony Mavunde. Kwa hiyo, naomba Serikali iangalie watu wenye ulemavu kwa jicho pana zaidi. Kwanza, tupo wachache sana na sidhani kama Serikali hii chini ya Mheshimiwa mama Samia Suluhu Hassan itashindwa kulisimamia suala hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine nizungumze juu ya Jiji la Dodoma au Makao Makuu ya Dodoma. Sote humu ndani tunafahamu kwamba Bunge la Kumi na Moja liliazimia kuweka Sheria ya Makao Makuu, basi hii sheria isiwe tu kwenye makaratasi iendane na utekelezaji wake. Utekelezaji wake ni kuendelea kufufua vitu ambavyo vitaonyesha kweli hii ni Makao Makuu. Tuangalie Uwanja wa Msalato, ring road, upatikanaji wa maji. Hili la upatikanaji wa maji ni shida sana, kuna maeneo ambapo siku nne hakuna maji, tunaishije hapa na sasa hivi tuna kiwango kikubwa sana cha watu. Kwa hiyo, naomba sana Serikali hii itambue na iendeleze lile wazo la Mwalimu Julius Nyerere la kuhamia Dodoma ambalo lilitekelezwa Awamu ya Tano, tuendelee kutekeleza yale yote ambayo waasisi wetu wametuwekea katika mipango yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia niwashukuru Watanzania wote ambao wamejitokeza kwa wingi kuomboleza msiba wa kipenzi chetu. Hii imetuonesha kabisa kwamba Rais wetu alikuwa anakubalika, amefanya kazi kubwa kwa ajili wa Watanzania na kweli alikuwa ni Rais wa wanyonge. Kwa kuangalia hilo, naamini Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan Rais wetu mpendwa ataendeleza yote kwa sababu ni mwanamke shupavu na jasiri. Naomba wanawake wote tumsaidie kusimamia yale yote ambayo tumejiwekea katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa haya machache niliyozungumza, naunga mkono hoja hii ya Waziri Mkuu. Ahsante sana. (Makofi)
The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3) Bill, 2023
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii kuchangia Muswada huu. Kwanza naomba niungane na wenzangu kuwapongeza Mawaziri wote walioteuliwa, sana sana Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu. Lakini vilevile nimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuzidi kuwaamiani vijana katika majukumu makubwa kabisa ya nchi hii. Hii inaongeza chachu lakini inatupa moyo sana vijana, pia inatuamsha kuona kwamba tunaweza kushika nafasi kubwa especially ukimtaja Mheshimiwa Juduth Kapinga, kwa kweli hongera sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama unavyofahamu tuko hapa kwa ajili ya kubadilisha sheria tukiamini kwamba hizi sheria zinaenda kufanya kazi. Kwa hiyo kama sheria haitoweza kwenda kufanya kazi maana yake lengo kuu lazima tubadilishe au turekebishe ili tuweze kusaidia wananchi au tusaidie jamii yetu. Mheshimiwa Rais ameona fika kabisa, na juzi amebadilisha Mawaziri na ameweza kubadilisha Wizara na kutengeneza Wizara mpya ambayo ni Wizara ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji. Hii Wizara imepewa majukumu makubwa sana ya kufanya. Lakini kama unavyoweza kuona kwamba kuna baadhi ya majukumu yalikuwa yamebakia katika Wizara ya Viwanda na Biashara sasa leo hii wameona kuna umuhimu wa kubadilisha kuona EPZ ihamie kwenye Wizara ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu sote kwamba EPZ ni sheria ya uwekezaji ya masuala ya mauzo ya nje ya nchi. Kwa hiyo Mheshimiwa Rais anauwezo wa kuipeleka hii sehemu yoyote, na ndio maana lengo la Sheria hii kubadilishwa ni ili iweze kwenda katika Wizara nyingine yoyote. Kama leo hii EPZ ikiamua kwenda Wizara ya Viwanda na Biashara basi iweze kufanya kazi, ndilo lengo kuu la mabadiliko ya sheria hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naomba sana nimpongeze Mheshimiwa Rais, na pia niipongeze Serikali kwa kutuletea sheria hii ambayo inatupa flexibility, kwamba hatutakuwa tunabadili mara kwa mara; leo hii EPZ imeenda Wizara nyingine basi tubadilishe sheria kupeleka Wizara nyingine, lakini inatupa uwanja mpana wa kusema sasa EPZ ipo wizara fulani basi sheria hii iweze kwenda vizuri na iweze kwenda kufanya kazi katika Wizara yoyote ile.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kwa mabadiliko hayo tunaomba tuipongeze Serikali lakini tupongeze pia Kamati, kwa sababu Kamati katika mchango wake iliona pia kuna pengo la Katibu Mkuu kutokuwepo katika Kamati hii ya EPZ Katibu Mkuu wa Wizara rasmi, hivyo basi Serikali imetuahidi kwamba itaweza kuleta marekebisho mengine ambayo haya marekebisho yataweza kuja kusaidia ili Katibu Mkuu wa Wizara hii ambaye ndio permanent secretary wa Waziri aweze kujua vizuri masuala yote ya EPZ kuliko kwenda kumchukua Mheshimiwa Waziri awe kila siku anampelekea taarifa ya kikao cha Kamati ambayo mambo ambayo yameelezewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kwa kusema hayo nashukuru kwa kutoa mchango wangu huu, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Awali ya yote naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe wote ambaye amenipa uhai wa leo hii kusimama leo na kuzungumza sekta yangu na sekta ya maisha yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii naomba nizungumze na umma huu wa Wabunge pamoja na Taifa hili. Sanaa ni maisha yetu vijana na kama Serikali ina mpango mzuri wa kuongeza ajira kwa vijana basi sanaa ni sehemu nzuri sana ya kuongeza ajira. Msanii kama msanii anayeimba, kuna anaye-produce, kuna director, kuna mpiga picha, kuna kila aina ya kazi, sasa hivi hadi mabaunsa wamekuwa wanaajiriwa kupitia sehemu ya sanaa. Kwa hiyo sanaa ni jambo muhimu sana na tukilizungumza hapa tuzungumzie kwa u-serious wake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niende moja kwa moja kwenye upande wa mirabaha; mirabaha kwa wasanii ni jambo la muhimu sana, leo hii Keisha nitazeeka, siasa nitastaafu, lakini kupitia hii mirabaha tutaweza kupata pesa mpaka tunakufa na watoto wetu wataendelea kula hela, kama ambavyo mimi sasa hivi bado naendelea kula hela ya muziki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hii hela ya muziki tunayokula, tunakula kupitia caller tune, ringtones, lakini tunataka COSOTA wasimamie mirabaha. Hii mirahaba itatusaidia sisi ku-generate lot of money, yaani pesa nyingi sana ambazo hizi pesa zitatusaidia sisi wasanii kutengeneza kazi zenye ubora ili tuweze kushindina kimataifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mirabaha ninayoizungumiza hapa kuna sehemu za starehe nyingi sana ambazo wewe huwezi kwenda kwenye starehe kama hauwezi kusikiliza muziki, kwa hiyo mirabaha hii tunayoizungumza sehemu za starehe, sehemu za mabasi, sehemu za hotels hawawezi kupiga muziki wetu bila kulipia pesa, ina maana tunapata pesa nyingi sana, lakini vilevile na Serikali inakusanya mapato mengi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kuna mapato mengi ambayo yanakosekana kwa Serikali kwa sababu ya kutokusimamia vizuri mirabaha ya wasanii katika hii nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine naomba nizungumze juu ya masuala ya maadili, mimi ni mfuasi mzuri sana wa maadili ya wasanii. Ni mfuasi mzuri sana na ni mfano mzuri sana kwa maadili ya wasanii. Leo hii mimi nisingefika hapa kama ningekuwa sina maadili, lakini maadili gani tunayozungumza hapa, maadili ya kufungia nyimbo za wasanii bila kujua hawa wasanii wanatakiwa waimbe nini?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ningeomba Wizara iwaite hawa wasanaii, ikae nao, iseme wanataka nini katika hizi kazi, lakini siyo wasanii peke yao hata hivi vyombo vya televisions, media zote wawaite, media ziambiwe ni nyimbo gani na nyimbo gani zinatakiwa kupigwa kwa muda gani, kwa sababu kuna muda ambao Watoto wamelala, hawasikilizi nyimbo zingine, lakini kuna hata kwa hawa watu wa filamu wanaigiza filamu na zinawekwa masharti pale chini ya miaka 13 hapaswi kuangalia hii filamu, chini ya miaka 18 anapaswa kuangalia, hivyo, kwa hiyo tuweke utaratibu ambao hawa wasanii watajua ni namna gani wao wanapaswa kuongoza kazi yao ili waweze kufanya kazi zao za sanaa kwa uhuru vizuri. Kwa sababu mwisho wa siku utamfungia huyu msanii ana familia yake, ana maisha yake, ana ndugu zake wanamtegemea hebu tuangalie hili suala kama Wizara ione namna gani ya ku-deal na wasanii katika masuala haya especially masuala haya ya maadili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nimefurahi sana kuona kwamba katika hii hotuba ya Waziri imezungumza kuhusu masuala ya tuzo. Tuzo ni muhimu sana, mimi nimekuwa msanii kwa kipindi cha muda mrefu na nimekuwa nimeshika tuzo mbili za mwanamuziki bora wa kike Tanzania, lakini nimeshika tuzo ya albamu bora ya Zuku. Hizi tuzo zilinifanya mimi niwe motivated kufanya kazi sana. Kwa hiyo leo hii kama Wizara imeona umuhimu wa kuanzisha tuzo hizi basi ione umuhimu wa kuruhusu tuzo zingine za watu wengine kuendelea kufanya kazi kuliko kuwawekea vizingiti vingi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii mtu akianzisha tuzo anaambiwa kipengele fulani usiseme, kipengele fulani usiseme, sasa hizi tuzo zitaendeshwaje, hizi tuzo mnataka ziwe nyingi ili zi-motivate wasanii wetu. Wasanii wapo kila sehemu na wanafanya vizuri na kila msanii ana ubora wake na katika kazi yake.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nikwambie jambo moja ambalo wasanii wanahangaika, wasanii wamepata bima za afya, lakini wasanii wanataka bima ya maisha. Tunashukuru sana Wizara, wameweza kutuwezesha kupata bima za afya, lakini wanataka bima za maisha ili wajihakikishie maisha yao hawa wasanii, tunaomba sana sana hili jambo liendelee, liwekwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile naomba pia nizungumze juu ya masuala ya maadili ya mavazi, hili suala jamani naomba sasa Serikali ituambie ni mavazi gani msanii anapaswa avae. Je, akienda kufanya video kwenye swimming pool anatakiwa avae baibui au nikabu? (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, tujiulize ni mavazi gani haya ambayo yanahitajika kwa wasanii wavae? Je, tuangalie asili ya Mtanzania vazi lake ni nini? Turudi tena huko kwenye tamaduni zetu, tuangalie Mtanzania anapaswa kuvaa nguo ya aina gani, ili akifikisha ujumbe ajue anafikisha ujumbe kwa namna gani. Wenzetu tunawaona nje wanavaa swimming costumes kwenye swimming pool kwa sababu ndivyo utamaduni wao unavyosema. Basi na sisi tuangalie kwenye swimming pool tuvae nini, tuvae nikabu au tuvae skin tight au tuvae nguo gani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili ni suala la uhalisia, leo hii tutawalaumu wasanii wanaenda kurekodi nje South Africa wapi, kwa sababu wanafuata facilities, hizi facilities zinawasaidia wao kuonesha uhalisia katika kazi zao. Sasa leo hii kama facilities hapa Tanzania haturuhusiwi kutumia nguo za polisi, haturuhusiwi kutumia sijui mahakama, sasa tutafanyaje kazi kama wasanii? Uhalisia utatoka wapi? Tutashindana vipi kitaifa na kimataifa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunamshukuru sana Diamond kusema kweli, Diamond anatuwakilisha vizuri sasa hivi Diamond anagombea tuzo ya BET. Ningeomba Wabunge wote hapa wam-support Diamond kwenye ma- group yao ya maeneo yao wapige kura kwa ajili ya Tanzania. Diamond hayuko pale kwa sababu ya Diamond au kwa ajili ya Wasafi au kwa sababu ya Babu Tale hapana, Diamond yuko pale kwa ajili ya Watanzania na anawawakilisha Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, basi naomba Bunge hili wahamasishe wananchi wao huko wanakoenda, wampigie kura Diamond aweze kuleta tuzo hii Tanzania proudly kabisa na sisi tuone kwamba tumepata hii tuzo ya mwanamuziki ambaye anaiwakilisha vizuri Tanzania hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kusema hayo machache na Bunge lako hili Tukufu, nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Lakini naomba niunge mkono hoja endapo haya mambo yatatekelezeka, lakini nilisahau jambo moja la mwisho samahani kweli muda wangu haujaisha. Kuna suala hili la arena. (Makofi/Kicheko)

NAIBU SPIKA: Kengele imeshagonga

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, arena arena arena, Babu Tale umesahau kuwaambia kwamba…

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Keisha muda wako umekwisha.

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kupata nafasi hii kuchangia leo katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kwanza kabla ya yote naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu kutujaalia uhai.

NAIBU SPIKA: Ndiyo wewe au?

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya, leo hii nimesimama hapa kuchangia masuala ya elimu juu ya watu wangu ambao wamenileta hapa Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Rais, sana sana. Mama jana tumekusikia umezungumza kama Mama tena Mama yule ambaye ana viakiba vyake yupo tayari watoto wake wale hata ugali na mlenda kuliko kushinda na njaa. Kwa hiyo, tayari tumeona namna gani Mama anaguswa na Watanzania na wanyonge na tunakupongeza sana Mama, tunakupongeza sana Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichangie leo kwenye hii Elimu, Sayansi na Teknolojia juu ya masuala ya vipaji. Mimi ni muumini wa vipaji, kwa sababu nimepata kipaji changu, nilikuwa na kipaji changu lakini nimeendelezwa kupitia Shule ya Msingi. Nimefanya bands, nimefanya kwanya, nimeimba na nimefanya vitu vingi sana mashindano ya kwaya, bendi yakanijengea uwezo. Kwa hiyo ninaamini kabisa Wizara ya Elimu ikiangalia namna hii ya kuweza kukuza vipaji vya watu, leo hii tusingewaponda akina Diamond na wengine kwa sababu shamra shamra za shuleni za mashuleni zile za mashindano ya waimbani na vitu kama hivyo.

Kwa hiyo, naamini kabisa, Wizara ya Elimu ikiangalia namna hii ya kuweza kukuza vipaji vya watu, leo hii tusingewapata akina Diamond akina nani kwa sababu ya ile shamra shamra za shuleni zile za mashindano ya waimbaji ya nini na vitu kama hivyo. Kwa hiyo, naamini sio kipaji kimoja tu tunaweza tukakipata shuleni vipaji vingi tu tunaweza tukatengeneza watu wengi tu wacheza mpira, michezo, everywhere, kila sehemu tunaweza tukapata watu wa kuweza kuwakilisha hii nchi, lakini pia kuinua uchumi wa hii nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni muumini wa vipaji kwa sababu pia itaacha haya mambo ya kukaa vijiweni kuvuta bangi, kuvuta unga na panya road. Vipaji vitakuzwa kimaadili zaidi, tutaona kabisa umuhimu wa vile vipaji ambavyo tunavitengeneza kuanzia chini mpaka kwenda juu. Kwa hiyo, naiomba Wizara hii iangalie hilo kurudisha mambo ya muziki shuleni, mambo ya mpira michezo na vitu kama hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, cha pili naomba nichangie juu ya masuala ya lugha ya alama mashuleni. Juzi nimesema tunahitaji lugha ya alama mashuleni, ni muhimu sana. Tunafahamu kabisa lugha ni mojawapo ya sehemu ya mawasiliano, hatuwezi kuelewana kama hatutumii lugha ambayo tunaweza tukaelewana. Naomba tu niwaulize Wabunge leo hii Wabunge nyinyi humu ndani mnawawakilisha wananchi, watu wenye ulemavu huko chini katika Majimbo yenu, hivi ni wangapi humu ndani wanafahamu lugha ya alama ya kuwasiliana na viziwi? Wangapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, ni wachache sana, kama wapo basi ni mmoja, wawili au watatu, mimi mwenyewe sifahamu lugha ya alama na huwa najisikia vibaya sana. Kwa hiyo, ningeomba Wizara pia ilete semina hata ya wiki moja tufahamu tujifunze lugha ya alama, tujue numbers tujue vitu basic ambavyo vinaweza vikatusaidia kuwasiliana na hawa watu wasijione kama wanatengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo mpiga kura wako akija kwako anataka kuzungumza na wewe hawezi kuzungumza naye. Gharama za mkalimani ni kubwa sana, hawezi kumudu muda wote akawa anatembea na mkalimali ili akuelezee shida zake. Kwa hiyo, tunaamini kabisa watoto wetu mashuleni wakianza kujifunza lugha ya alama ina maana hata watu ambao wamezaliwa wana ulemavu wa kutokusikia, tayari itawasaidia wao. Kwa hiyo, naomba Serikali iangalie hili ni muhimu mno mno, ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, cha mwisho, naomba nichangie juu ya masuala ya elimu jumuishi, tunafahamu tuna Walimu katika mashule ya elimu jumuishi. Tunafahamu kwamba hawa Walimu wengine ni wachache mno, lakini wengine pia wame-specialize kwenye area moja lakini sasa kwa sababu tu ni walimu wa elimu jumuishi, wanakwenda mashuleni wanafundisha kila mtoto ambaye ana matatizo ya ulemavu, hapana. Tunatakiwa tujue kabisa huyu mwalimu ame-specialize kwenye viziwi peke yake, huyu mwalimu ame- specialize kwenye ulemavu wa akili, huyu mwalimu ame- specialize kwenye area hii na hii na hii. Kwa hiyo, tujue namna gani hawa watu wanaweza wakatusaidia tuongeze Walimu ambao wamebobea katika sehemu mbalimbali ili tuweze kuwafundisha hawa watu na vile vile kuwatengenezea mazingira mazuri ya wao kuishi katika hii dunia.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpongeze mama katika area moja. Ameongeza vyuo vya watu wenye ulemavu sasa hivi vimeongezeka. Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, amesema vyuo vilivyoongezeka kule Singida kesho kutwa tunakwenda kuzindua Tanga. Hii tayari ni hatua nzuri sana ambayo Serikali imefikia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi vyuo tuvitumie hivi vyuo viende kuamsha/kuondoa umasikini wa watu wenye ulemavu tuwatengenezee elimu, lakini pia tuwape nyanja tofauti tofauti tuwatengenezee ubora na uwezo ambao wanaweza wakafanya. Hivi leo hii wanaonaje Serikali wakawafundisha hawa watu wenye ulemavu ambaye yeye labda hawezi kutembea, tukamfundisha kutengeneza bahasha tu hizi, halafu leo tender za hizi bahasha tukazichukua kwa watu wenye ulemavu, ndio tukawa tunawalipa wale watu wenye ulemavu, hatuoni kama tutakuwa tumewasaidia hawa watu wenye ulemavu? Kwa hiyo, naomba Serikali itafute namna gani ya kuondoa umaskini wa watu wenye ulemavu, watu wenye ulemavu ni maskini sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumze, hawa watu ni masikini sana, kwa sababu kama mtu tu ana miguu yake na mikono yake na maisha ni magumu, fikiria mtu ambaye hana miguu, hana mikono, hawezi kusikia, ni namna gani ambavyo anaishi au na wale pia familia ambayo inawalea wanashindwa kuwalea vizuri. Kwa hiyo, naomba Serikali inapokuwa inafikiria mambo yake ya kimaendeleo, mambo ya kielimu, iangalie sana kundi hili ni muhimu mno. Mmii ni sauti ya watu wenye ulemavu hapa Bungeni, nitazungumza kila siku na mtanichoka lakini naomba Serikali iangalie namna gani ya kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kusema hayo machache naunga mkono hoja na nashukuru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kupata fursa ya kuzungumza, tena kwa ghafla, lakini umenipa fursa hii ya kuzungumza leo ili kuchangia hoja ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametukutanisha tena leo katika bajeti hii ya mwaka wa fedha 2024/2025.

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri sana ambayo anaifanya, especially kwenye eneo la watu wenye ulemavu. Mheshimiwa Rais watu wenye ulemavu tunamshukuru sana, tupo pamoja na yeye, tunampenda sana na tunamtakia kila la heri katika majukumu yake yote ambayo anayafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo nitachangia katika maeneo kadhaa, lakini eneo ambalo ni muhimu sana kwangu kuchangia kila ninapopata fursa ya kuzungumza na naomba msinichoke, ni juu ya masuala ya watu wenye ulemavu. Mheshimiwa Rais amefanya mambo mengi sana kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kufungua vyuo na kutengeneza miundombinu mbalimbali katika maeneo mengi. Sasa hivi ukienda katika shule unakuta miundombinu ya watu wenye ulemavu ipo, ukienda kwenye vyuo tayari kuna vyuo vya watu wenye ulemavu, lakini pamoja na hayo yote naomba kutoa ushauri wa kuboresha katika baadhi ya maeneo.

Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya hivi vyuo ambavyo vinafunguliwa vinakosa vifaa vya kufundishia kwa mfano, kwa wale ambao wanapika keki na vitu kama hivyo. Jambo hili nimelipata nikaona nije kulizungumza ili Serikali iendelee kuweka mkazo katika eneo hilo. Pia, naomba kushauri katika hivi vyuo watu wajifunze namna ya kutengeneza fimbo pamoja na wheel chairs, ili waweze kujisaidia wenyewe kwa sababu, inaonekana kuna uhaba wa vifaa hivi saidizi kwa watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo mengi sasa unasikia kuna harambee kwa ajili ya kupata vifaa vya watu wenye ulemavu. Naamini Serikali ya Awamu ya Sita haijashindwa kutengeneza mkakati mzuri ambao unaweza kusaidia kupata vifaa hivi vya watu wenye ulemavu katika maeneo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba kushauri, kama tunapeleka wanafunzi katika hivi vyuo, basi tuwatengenezee mkakati mzuri ili kujua mwanafunzi akitoka pale anaenda kufanya nini? Akitoka pale atawezeshwa namna gani? Akitoka pale tupate matokeo, ni kiasi gani watu wenye ulemavu wameweza kunufaika na vyuo hivi ambavyo wamepelekwa. Issue siyo vyuo, lakini issue ni hawa watu waweze kunufaika au kujikwamua kiuchumi wao pamoja na familia zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali itengeneze mkakati mzuri ambao utawawezesha watu wenye ulemavu baada ya kutoka kwenye vyuo hivi. Juzi nimemwona Mheshimiwa Waziri wa Fedha katika mitandao ya kijamii, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, akisema kuwa 10% imerudi. Kama hii 10% imerudi, basi Serikali ije ituambie kwa sababu, kwa watu wenye ulemavu hili ni eneo ambalo wanalitegemea sana kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi katika zile asilimia mbili ambazo zinatolewa na Serikali. Kwa hiyo, tunahitaji Serikali itusaidie kwenye eneo hili, ili watu wenye ulemavu waweze kujikwamua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2022 tumefanya sensa ya watu wote ikiwa ni pamoja na watu wenye ulemavu. Matokeo yamekuja 11.2% ya watu wote Tanzania Bara wana ulemavu na Tanzania Visiwani watu wenye ulemavu ni 11.4%. Hii ni asilimia kubwa sana, natamani sana kuona Serikali inaweka mkakati kwa ajili ya kuwakwamua watu wenye ulemavu ikizingatia idadi kubwa ya watu wenye ulemavu wanatoka katika familia maskini, nasisitiza wanatoka katika familia maskini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, natamani kuona Serikali ina mkakati gani wa kuondoa shida za watu wenye ulemavu. Watu hawa wapate shida ya maumbile yao, wapate shida ya changamoto zao za kimwili ila wasipate shida za kiuchumi kama ambavyo nchi nyingine ambazo zinafanya vizuri zina mkakati mzuri wa kunyanyua watu wenye ulemavu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naamini kabisa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, haiwezi kushindwa. Rais wetu anajali wanyonge, anajali watu maskini, anajali watu wenye ulemavu na ameonesha hilo kwa sababu, ameweza kuwaita watu wenye ulemavu Ikulu na kuzungumza nao, ameweza kutenga fedha kwa ajili ya mafuta, lakini pia ameweza kutenga shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuwezesha shughuli za watu wenye ulemavu katika Wizara ya Fedha. Mwaka jana tulipata hiyo bajeti na natumaini mwaka huu pia, tutaongezewa hiyo bajeti kwa sababu, shida za watu wenye ulemavu ni nyingi mno. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi kati niliangalia hizi takwimu na nilitamani sana kupata uelewa zaidi wa hizi takwimu especially kwa sisi watu wenye ulemavu, lakini ikipendeza Bunge zima lipate kujua hizi takwimu. Ni maeneo gani yenye watu wenye ulemavu na ni kiasi gani, au kuna aina gani ya watu wenye ulemavu na wingi wao katika maeneo yao tofauti tofauti kusudi Wabunge wanapokuja hapa kusaidia nchi yao na wananchi wao, watambue katika majimbo yao wana idadi kiasi gani ya watu wenye ulemavu na ni wa aina gani ili ifike mahali nipate kusikia hapa kila Mbunge akizungumzia masuala ya watu wenye ulemavu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kusema masuala ya watu wenye ulemavu, pia naomba nichangie eneo la masuala ya dawa za kulevya kwa sababu hata watu wenye ulemavu wanaguswa na masuala ya madawa ya kulevya. Naomba niipongeze Serikali ya Awamu ya Sita ya Mama Samia Suluhu Hassan. Imeweza kufanya kazi kubwa sana pamoja na Kamishna Mkuu wa Madawa ya Kulevya. Serikali tuendelee kumlinda yule baba ili aweze kufanya kazi nzuri ya kukomboa vijana wetu na watoto wetu kwa sababu Mama ameonesha nia ya dhati na thabiti ya kuhakikisha anasaidia vijana wake wasiingie au wasijihusishe sana na matumizi ya madawa ya kulevya au wasipate ule uwanja mpana sana wa matumizi ya madawa ya kulevya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kiasi kikubwa sana kimekamatwa mwaka jana Desemba, kiasi cha 3,182, kiasi kikubwa ambacho kwa historia hakijawahi kukamatwa au basi kama kimewahi kukamatwa, hatujawahi kutangaziwa kwamba kiasi kikubwa kama hiki kimeweza kukamatwa. Kwa hiyo, naomba niishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita ya Mama Samia Suluhu Hassan kwa sababu tunaona kabisa nia yake ya dhati ya kuhakikisha vijana, wanawake, watoto pamoja na watu wenye ulemavu wanajiepusha na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zinaharibu akili zetu, utendaji kazi wetu na inaondoa nguvu kazi. Kwa hiyo, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuzingatia hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo, naomba nichangie na kusisitiza pia kwenye eneo la vifaa saidizi pamoja na ofisi za watu wenye ulemavu. Mheshimiwa Waziri Mkuu katika kongamano langu la uzinduzi wa NGO yangu alitoa kauli akisema, kila halmashauri itenge chumba maalum kwa ajili ya SHIVYAWATA, wapate ofisi ili watu wenye ulemavu wajue eneo la kufika la kueleza shida zao kwa urahisi na kila halmashauri ipate kujua shida za watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningetamani sana kujua hili suala limefikia wapi kwa sababu namna ninavyosikia, bado kuna maeneo ambayo hawajatekeleza neno hili. Labda sasa tutafute namna ya kutengeneza kama sheria ili kila halmashauri kuwe na ofisi ambazo hazitakuwa zinachangiwa kiasi chochote cha pesa na wenye ulemavu waweze kupata huduma kwa urahisi zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia Serikali itengeneze mkakati mzuri wa kupata vifaa saidizi kama nilivyosema hapo awali. Ningetamani sana halmashauri ingetenga pesa ukiachana na hii asilimia mbili ambayo ni kwa ajili ya masuala ya uchumi, lakini nyingine kwa ajili ya kumwezesha mtu mwenye ulemavu. Sasa wheel chairs zimekuwa bei ghali, tunatamani sana kupata vifaa hivi kwa ajili ya watu wenye ulemavu. Tupate mafuta kwenye halmashauri zetu ili wafikiwe kwa urahisi zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kusema hayo, naomba nikushukuru sana, lakini namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anayofanya. Tuendelee kumtia moyo, tuzingatie uwezo wake, tufahamu na tuendelee kumsemea Mheshimiwa Rais wetu kwa sababu tunawiwa kufanya hivyo, kwa sababu tunawakilisha wananchi wale ambao wana shukurani kwa miradi ambayo imepelekwa kule chini, katika kila kata kuna miradi. Kwa hiyo, tumshukuru sana Mheshimiwa Rais na tuendelee kumsemea mazuri...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante.

MHE. KHADIJA S. TAYA: ... na mema.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana tena sana kwa kupata fursa ya kuchangia Bajeti ya TAMISEMI. Ni nadra sana kwangu kuchangia TAMISEMI, lakini leo inanipa fursa nzuri ya kutaka kuchangia, nawe umenipa nafasi hii ya kuchangia, nakushukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametuleta hapa leo tukiwa tuna uhai na uzima, tunapumua vizuri na Mwenyezi Mungu awajalie huko ambao wametangulia mbele za haki, awalaze mahali pema peponi.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo naomba nipongeze zaidi na kuomba machache. Naomba nimpongeze Mheshimiwa Rais. Kusema kweli katika kipindi ambacho bajeti ya TAMISEMI imekuwa ngumu, ni bajeti ya mwaka 2023/2024. Kwa sababu gani? Kwa sababu miundombinu mingi imeharibika, lakini pamoja na uchache wa bajeti, mmeweza ku-manage, hongereni sana, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuwa considerate. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba niwape pole sana waliopata maafa ya mafuriko na mengine mengi, lakini nikupe pole sana Mheshimiwa Waziri Mchengerwa kwa kukutana na majanga ya mafuriko katika Jimbo lako. Insha’Allah Mwenyezi Mungu awajalie wale waliopoteza maisha kwa wale watoto wetu wapendwa wa Mkoa wa Arusha, Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi, amina.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpongeze Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Rais ni mama, ni mzazi, ni baba yetu. Ni baba kwa cheo chake, kwa sababu gani? Kwa sababu katika kipindi chake cha miaka mitatu ameweza sana kujali maslahi ya watoto wetu wa Taifa hili ambao ndiyo msingi wa maendeleo ya baadaye. Amejali vipi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, amejali kwa kuhakikisha kwamba pesa nyingi ameipeleka chini kwenye huduma za jamii. Leo hii hapa Bungeni unaona kila mmoja anayesimama hapa hata kama atasema changamoto, lakini atapongeza. Hatupongezi kinafiki, hatupongezi kiuchawa, tunapongeza kwa sababu tumefanya ziara, tumeona mambo mazuri ambayo Mheshimiwa Rais ameyafanya huko chini.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaona hospitali zinazojengwa, tunaona shule za msingi ambazo sasa hivi watoto wetu wanakanyaga tiles na wana-slide madirisha ya vioo. Yote haya ni Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mwenyezi Mungu anasema asiyeshukuru kwa kidogo hawezi kushukuru kwa kikubwa kamwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kushukuru huko, nashukuru pia kwa TAMISEMI au Serikali kukubali kuhakikisha au kurekebisha sheria na kanuni zinazoendesha CSR. Naomba niwapongeze sana Serikali kwa sababu bei nyingi ambazo tunapewa na kwa vitu ambavyo vinatakiwa vifanyike, hazina uhalisia. Unaweza ukaambiwa pad shilingi 8,000 wakati mtaani tunafahamu pad ni shilingi 3,500 au 3,000 au 2,500. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwa kuwa mmeamua kwenda kuangalia, basi mkaangalie uhalisia au namna gani mtaweza kuunda vizuri sheria hizi au kanuni hii ya CSR ili iweze kunufaisha nchi yetu na Taifa letu kwa ujumla. Nataka niwaambie watu kwamba, nilipofika hapa Bungeni nilianza kuwa katika Kamati ya Katiba na Sheria. Mwenyekiti wangu alikuwa Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa. Kaka yangu umekuwa una-support kubwa sana na watu wenye ulemavu, naomba nikupongeze kwa hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimekuwa kila nikisimama kuzungumza masuala ya watu wenye ulemavu umekuwa ukikazia sana na kitu pekee pia ulikuwa unaomba zaidi ulikuwa unaomba takwimu za watu wenye ulemavu. Tunashukuru Sensa ya mwaka 2022 leo hii tuna takwimu za watu wenye ulemavu. Takwimu hizi zitaenda kufanya nini? Zinaenda kusaidia Serikali kutengeneza mikakati na mpango wa kusaidia watu wenye ulemavu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu kwamba sasa hivi watu wenye ulemavu ni asilimia 11 ya population yote. Ni watu wengi sana asilimia 11.2, watu wenye ulemavu ni wengi mno. Serikali lazima mjipange mjue namna gani ya kuweza kusaidia watu wenye ulemavu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana Mheshimiwa Mchengerwa kwa sababu ulikuwa Mwenyekiti na ulikuwa ukisimamia masuala yote ya watu wenye ulemavu, lakini leo hii wewe umepewa rungu sasa kusimamia, I mean kutenda. Sasa upo kwenye nafasi ya kutenda. Ninakuomba sana kaka yangu kwa mapenzi uliyonayo kwa watu wenye ulemavu, naamini kabisa unaenda kutenda haki. Unaenda kusimamia maslahi ya watu wenye ulemavu kwenye nyanja tofauti tofauti, tukianzia kwenye upande wa Ofisi za Watu Wenye Ulemavu katika Halmashauri zako. Hili jambo Mheshimiwa Waziri Mkuu alilitoa kama mwongozo. Sasa basi tengenezeni mwongozo wa maandishi. Serikali itambue kwamba kila halmashauri inapaswa kuwa na Ofisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mnaweza mkashangaa kwa nini tunalilia Ofisi? Tunataka watu wenye ulemavu wajue eneo lao la kupeleka malalamiko yao na changamoto zao na kupata maelekezo juu ya asilimia mbili na kutambua fursa zilizopo za watu wenye ulemavu. Tunahitaji Ofisi Mheshimiwa Mchengerwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais ametoa fedha kwa ajili ya mafuta ya watu wenye ulemavu, nataka nijue, usimamizi wa fedha zile uko vipi? Mpaka sasa bado sijapata majibu ya namna gani au mmeshatengeneza mafuta haya au vipi? Sijapata majibu. Ninaomba leo hii katika Wizara yako, basi nipate majibu mazuri ya watu wenye ualbino wanapata vipi mafuta katika halmashauri zao? Kwa sababu fedha zimetoka na nina uhakika mwaka huu pia mtatenga fedha kwa ajili ya kununua mafuta ya watu wenye ulemavu au kwa ajili ya kutengeneza kwa urahisi, kwa bei ya chini mafuta ya watu wenye ulemavu ili yaweze kupatikana kwa urahisi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninavyosema kuhusu mafuta, naomba mnielewe jamani. Sisi watu wenye ualbino ili tuishi, tutembee, tufanye kazi zetu tunahitaji kupaka mafuta, siyo tu baby care, tunahitaji kupaka mafuta ya kuzuia mwanga wa jua. Hii inatuboreshea afya zetu inatulindia ngozi zetu. Kwa hiyo, nawaomba sana mnielewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni bahati iliyoje, namshukuru Mheshimiwa Rais sana, sana, sana kwa kutambua tena umuhimu wa vijana, amemteua rafiki yangu Mheshimiwa Zainab Katimba. Mheshimiwa Zainab Katimba ni mfano mzuri wa binadamu ambaye anapenda watu wenye ulemavu. Mimi ni rafiki yake na anafahamu changamoto zetu nyingi kwa sababu nimekuwa nikizungumza naye mara kwa mara. Anafahamu na kujua changamoto na matatizo ya watu wenye ulemavu na ninaamini kabisa atakuwa msaada kwake tosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Rais hajakosea kwa sababu amemweka mtu ambaye ni mtendaji kazi mzuri, hodari na mchapakazi, mwenye huruma. Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais tunakushukuru sana kumteua rafiki yangu Mheshimiwa Zainab Katimba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nisipozungumza jambo hili nitakuwa sijatendea haki hii bajeti. Naomba pia niipongeze Serikali kwa miundombinu ya watu wenye ulemavu katika shule pamoja na vyoo vya watu wenye ulemavu shuleni.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. KHADIJA S. TAYA: … lakini ombi langu la mwisho kabisa kwa Serikali…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa…

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakuomba sana…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa…

MHE. KHADIJA S. TAYA: … ombi langu la mwisho, la mwisho kabisa…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, ngoja basi niseme.

MHE. KHADIJA S. TAYA: … ni kuongeza idadi ya…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, mimi nasemea hivi…

MHE. KHADIJA S. TAYA: …ya wafa…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, acha niseme basi.

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, sawa.

NAIBU SPIKA: Kwa vile hoja yako ni muhimu na umelia sana, nakuongeza dakika moja. (Makofi)

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Rais amejenga miundombinu ya shule pamoja na vyoo vya watu wenye ulemavu, tunaomba tuongezewe idadi ya walimu wanaofundisha watoto wenye ulemavu. Tunakuomba sana Mheshimiwa Mchengerwa liangalie hilo ili tusipate shida ya kutambua kwamba huyu amefaulu tumpeleke shule hii au tumhamishe huku. Shule hizi muhimu jumuishi zikipata walimu wazuri, watu wenye ulemavu wanaenda kuelimika na umasikini unaenda kwisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Afya
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kupata nafasi hii tena katika Wizara ya Afya kuchangia mambo mbalimbali. Kwanza naomba nikupongeze sana dada Ummy, Mheshimiwa Ummy anafanya kazi kubwa sana ndio maana leo hii Mheshimiwa Rais amemrudisha hapo, ameona kazi ambayo ameifanya. Leo hii anawasikia Wabunge wengi wakiomba vifaa tiba kwa sababu tayari kuna majengo, kwa hiyo Mheshimiwa Rais pamoja na Mheshimiwa Waziri wamefanya kazi kubwa sana kuleta fedha za UVIKO kujenga vituo vya afya vingi na ndio maana leo hii tunaomba vifaa tiba kwa sababu tunayo tayari majengo ambayo yanaenda kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo sana wa fadhila leo hii kama sitomshukuru Mheshimiwa Rais, kwa sababu Mheshimiwa Rais ni msikivu mno, mwaka jana nilisimama hapa ndani nilizungumza sana kuhusu masuala ya mafuta kwa ajili ya watu wenye ulemavu. Leo hii nasimama hapa kwa kujidai kwamba Mheshimiwa Rais amesikia kile kilio chetu. Aliwaita watu wenye ulemavu Ikulu na akaelekeza Wizara ya Mheshimiwa Ndalichako kwa ajili ya kutenga bajeti ya watu wenye ulemavu, ya kununua mafuta Sh.60,000,000. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naamini hii bajeti ya Sh.60,000,000 kwa mwaka 2022/2023, itaongezeka kutokana na idadi tutakayopata kutokana na sensa. Tukishafanya sensa tutajua idadi kamili ya watu wenye ulemavu wa ngozi ili tuweze kupata mafuta yanayotosheleza kabisa, lakini kwa kianzio tumeanza vizuri, Sh.60,000,000 imetengwa na utaratibu mzuri sana utafanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia naomba nimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kufanya mabadiliko ya MSD. MSD leo hii tumepata kiongozi mwingine mpya na leo hii kila mtu anasifia MSD, lakini naomba niwaambie MSD jambo moja, wasijisahau na hizi sifa. Hawa hawa watu leo hii wanaowasifia kesho watawasema humu ndani mtawashangaa. Kwa hiyo, kwa makosa ya huko nyuma waangalie kitu gani wenzao walikosea na wao wajitengeneze kwa namna gani ili waweze kuboresha. Tunawaamini sana MSD na sisi, wao ni kimbilio letu kwa sababu sisi tunawawakilisha wananchi, kwa hiyo wao ni kimbilio letu sisi. Kwa hiyo, tunawaomba sana sana katika jambo hili waangalie sana maslahi ya wananchi zaidi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii pia nina maombi kadhaa kwa Wizara hii ya Afya; leo namwomba Mheshimiwa Ummy, kuna jambo hili la mashine kwa ajili ya kuzuia kansa. Wanasema kinga ni bora kuliko tiba. Nawaambia kweli humu ndani Wabunge hawajawahi kuona mgonjwa wa kansa mtu mwenye ulemavu wa ngozi au mtu mwenye ualbino na kama wakitoka hapa wakaenda ocean road wakaona wagonjwa wa kansa watanielewa kwa nini kila siku nikisimama hapa nazungumzia suala la kansa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo, basi naomba hizi mashine zilizopo ziongezwe zipo kwenye mikoa saba, basi tuone namna gani ya kuongeza hizi mashine ili kila mkoa wapate hizi mashine, wasiweze kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kuzuia saratani ya ngozi. Pia naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Ummy amefanya kazi nzuri sana. Leo hii nimefurahi mno, nimefurahi sana sana kwa kuona kwamba kitengo cha mionzi kinahamia Dodoma. Kwa hiyo sasa Dar es Salaam pale ocean road kipo kitengo cha mionzi, lakini pia Mwanza pale kipo na sasa hivi Dodoma kipo, ina maana itawasaidia watu wanaotoka Singida, Manyara, Arusha hawatoenda mbali sasa hivi watakuja hapa Dodoma kwa ajili ya kupata mionzi kwa ajili ya saratani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimwombe pia jambo lingine Mheshimiwa Ummy, namwomba sana kitengo cha afya, huduma za afya kwa watu wenye ulemavu namwomba sana, leo hii tunazungumza kuhusu suala la afya ya akili, sisi walemavu mimi mwenyewe nawezakana sina afya ya akili, kwa sababu tukiudhiwa tunakasirika haraka sana, tuna mambo mengi sana ambayo yametuzonga, hiki kitengo kitatusaidia sana kwa huduma zake kwa ajili ya kushauri. Kwa hiyo naomba huduma ya utengemao ili iweze kutusaidia sisi tuweze kufanya majukumu yetu vizuri. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kupata fursa hii kuchangia katika Wizara hii ambayo na-declare interest kwamba nahusika, mimi ni mdau mkubwa wa hii Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa sababu katika Wizara ambayo anaonyesha mapenzi ya dhati kabisa, kuwapenda kabisa ni Wizara hii. Ndiyo maana sasa hivi naona hamasa kubwa katika hii Wizara, tayari ameishaonesha dira kabisa kwamba hii Wizara ni watoto wangu, wanahitaji kulelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tayari Mheshimiwa Rais ameshaonesha dhamira ya dhati katika Wizara hii, Mheshimiwa Waziri na Waheshimiwa Wabunge waanze kuangalia Wizara hii kwa mnajili mpya kabisa, tukianzia hasa kwenye masuala ya bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri. Kusema kweli, mimi ni kati ya watu ambao nilishangaa kumwona Bakhresa amekuja kwenye hii Wizara, Mama ana jicho la mbali sana, lakini naanza kuona sasa namna gani umeanza ku-cope vizuri na wanasanii na wanamichezo. Tayari tunaanza sasa kuona siku ile kwenye Tuzo tulikuwa tunacheza sana pale, tunaanza kuona sasa Wizara imempata mtu ambaye anaweza akaifanyia kazi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumpongeze Mheshimiwa Rais pia kwa kumchagua kaka yangu Kipenzi Mheshimiwa Hamis Mwinjuma tayari huyu ambaye ana-idea anajua kabisa, anajua shida na chnagamoto za Wizara hii naamini kabisa kwa sababu yeye ni mwanamichezo lakini pia ni mwanamuziki ataenda kuleta ukombozi katika wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumzie suala la bajeti. Kwa kuangalia zamani wakati nasoma tulifundishwa basic needs katika maisha na wakawa wanasema kwamba malazi, mavazi, usafiri ikawa ni kitu kama luxury sasa hivi usafiri siyo luxury tena ni lazima. Leo hii katika hii wizara tunaangalia kama entertainment kwamba hii Wizara ni kwa ajili ya entertainment hapana siyo kweli. Hii Wizara inaenda kuwa mkombozi mkubwa wa kupunguza ajira katika nchi hii. Kwa namna gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii Wizara ikiweka mikakati mizuri kama ambavyo alivyoweka mikakati kaka yangu Bashe katika BBT. Hii Wizara italeta heshima ya kupata bajeti kubwa sana na kuweza kuendeleza Wizara hii katika uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu niambie Waheshimiwa Mawaziri hao wawili ambao tayari wamepewa dhamna katika wizara hii muhimu sana katika nchi yetu waangalie namna gani ya kuja kuwa–convince wabunge hawa waangalie mikakati gani waipange katika nchi hii, ili iweze kuondoa hii isuue ya bajeti. Leo hii bilioni 35 ni bajeti ndogo sana, ni bajeti ya aibu najisikia vibaya kwa sababu hii wizara ambayo inanihusu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi Mheshimiwa Rais Wizara hii imeweza kutoa mikopo kwa badhi ya wasanii mnaweza kuona namna gani Mheshimiwa Rais anaipenda hii wizara, lakini leo hii Wizara ina bajeti ya bilioni 35, nazungumza hapa wasanii wakiwepo pale, nazungumza hapa wanamichezo wako humu ndani bilioni 35 inaenda kusaidia kitu gani katika hii Wizara? Tuangalie namna nyingine ya kufanya uwekezaji katika Wizara hii ili iweze kusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine Mheshimiwa Waziri mimi ni mmoja ya watu ambao tulikuja kwenye tuzo za wanamuziki pale the The Dom Masaki. Mheshimiwa Waziri na Wizara yako naomba niwapongeze sana mwaka jana hii shughuli imeanza na sasa hivi mwaka huu mmefanya kazi nzuri sana, lakini naomba niulize au niwaambie ni namna gani ya kufanya kwa namna moja ama nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri umewaandalia wasanii tuzo. Wasanii hawa ambao wameandaliwa tuzo. Tuzo zinatangazwa pale kwa ajili ya wasanii kupewa tuzo hawapo na wengine hawajaandaa hata wapokeaji wa tuzo hizi sasa unajiuliza ni kwamba lack of coordination ama ni shida iko wapi? Je, wasanii hawajazipokea hizi tuzo ama Mheshimiwa Waziri na jopo lako hamjaweza kuzitangaza hizi tuzo vizuri au kuwapa tarehe nzuri ya kujua tuzo ni tarehe fulani na wasanii wote wanapaswa kuwepo. Mimi sijawahi kuona huko nje kina Beyonce wakakosa kwenye tuzo, sijawahi kuona kina Rihanna wakakosa kwenye tuzo, kwa sababu ndiyo sehemu pekee ya kuonesha appreciation ya kazi yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii unaenda pale unakuta nusu ya wasanii ambao wanaenda kupewa tuzo hawapo hii inaondoa hamasa na Ladha ya tuzo zetu za Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri tafuta namna ya kukaa na wasanii wako. Wasanii ni wasikivu na wanakuheshimu, wanaheshimu Serikali ya Mama Dkt. Samia Suluhu Hassan. Fanya warsha mbalimbali, fanya semina mbalimbali, waelimishe mambo ambayo unataka kuwafanyia, waoneshe njia waoneshe upendo. Nina uhakika hao wasanii wako watakuwa wanashiriki kila tukio ambalo wewe na Wizara yako inaandaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu mimi nilijisikia vibaya naona hadi wasanii ambao juzi tu wametoka eti na yeye hayupo. Ukiuliza yuko wapi? hujui. Yaani haijulikani yuko wapi nasema sasa hii tuzo ameandaliwa nani? Kama siyo wasanii. Kwa hiyo, tuangalie either kama shida iko kwa wasanii basi zungumzeni nao, lakini kama shida iko kwene menejimenti ya Wizara basi fuatilieni hili jambo mjue namna gani ya kuweza kwenda kusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu nataka nizungumze kuhusu mmomonyoko wa madili. Naisema huku kwa sababu wizara hii au tasnia hii ni sehemu mojawapo ya mmomonyoko wa maadli katika Tanzania yetu. Nasema hivi kwa sababu nimetokea huko nafahamu vizuri jinsi gani mtu anaona kwa namna moja au nyingine kwamba ili mimi niwe msanii lazima nivute bangi, ili niwe msanii lazima ninywe madawa ya kulevya, ili niwe msanii lazima ninywe pombe, ili niwe msanii lazima nicheze uchi yaani kuna vitu vingi sana katika wizara hii ambavyo Mheshimiwa Waziri kwa weledi wako, kwa muonekano wako, kwa namna yako na uzoefu wako utawaweza Kwenda kuvifanyia kazi, ili hii wizara au hivi vipaji wazazi huko nyumbani waweze kuruhusu watoto wao kutaka kuwa wasanii tulinde utamaduni wetu. Tulinde asili yetu tulinde utanzania wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la utamaduni unaweza ukaona sasa hivi dunia ilivyo badilika masuala ya utandawazi mambo yamebadilika. Watu tumepita kwenye phases za kubadilisha nywele, phases za kuweka kope za kujichubua…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. KHADIJA S. TAYA: …lakini sasa hivi kuna phases ambayo ni mbaya sana ya kubadilisha maumbile.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. KHADIJA S. TAYA: Tunabadilisha maumbile yetu leo hii huyu mtu mwembamba hana shape lo hii kesho kutwa unamuona ana shape kubwa sana.

MWENYEKITI: Ahsante muda wako…

MHE. KHADIJA S. TAYA: Kwa hiyo naamini hii Wizara ya kuelimisha vijana wetu, watu wetu…

MWENYEKITI: Muda wako umeisha Mheshimiwa Khadija, ahsante sana.

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa fursa hii lakini Serikali iangalie namna gani ya kusaidia vizazi vyetu Tanzania inaenda kunagamia kwa namna hii. Ahsante sana nashukuru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. KHADIJA S. TAYA: Bismillah Rahman Rahim.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kupata nafasi hii. Kwanza naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amenipa leo afya njema ya kusimama katika Bunge lako tukufu kuzungumza masuala ambayo yanaenda kustawisha maisha ya vijana wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Rais sana na siyo kinafiki. Tuzungumze ukweli, Royal Tour siyo kitu ambacho kinaenda kunufaisha utalii peke yake, Royal Tour inaenda kunufaisha wasanii wa Tanzania hii. Mama alipoenda Marekani, alitembelea Paramount Studio. Katika hii studio amezungumza na watu masuala ya kuwekeza Tanzania kupitia hiyo hiyo Royal Tour.

Mheshimiwa Naibu Spika, mama alipoenda Los Angeles amekutana na wadau zaidi ya 15. Hawa wadau wamejadili mambo tofauti tofauti, wanakuja hapa Tanzania na amezungumza nao kabisa kuhusu fursa zinazopatikana hapa nchini. Leo hii mama anatuletea wasanii wakubwa ambao wanaweza kutuletea maendeleo katika hii nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiachana na hayo, mama pia katika mtu ambaye ametengeneza hii Royal Tour anaitwa John, yule jamaa Producer, amekuja Tanzania, amezungumza na wasanii, amefanya kikao na wasanii tarehe 29 Aprili, ameona changamoto gani ambazo wanapitia na kadhalika ili waboreshe kazi zao katika maeneo tofauti tofauti. Mama anaupiga mwingi sana. Jiulizeni sisi tunaupiga wapi? Umeuliza swali zuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuipongeza timu ya Serengeti Girls na pia niipongeze timu ya Tembo Warriors. Pia naomba niwaambie kwamba tunahitaji timu za makundi maalum ziendelezwe vizuri. Tunahitaji timu hizi za makundi maalum waanze kuwa na maslahi mazuri, kwa sababu katika upeo wangu sasa hivi naanza kuona hizi timu ndiyo zinazotutangazia nchi yetu vizuri, na sasa hivi tumesaini mkataba wa masuala ya usawa wa kijinsia. Tunaomba maslahi ya hawa wanatimu ambao wanaenda kwenye kutuwakilisha katika nchi nyingine huko, maslahi yawe sawa na hizi timu za wanaume ili tuweze kutimiza masuala ya usawa wa kijinsia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakienda kwenye hotels, wasifikie huko uchochoroni, Hapana. Waende kwenye hoteli, kama ni Four Stars au Serengeti Boys au Taifa Stars nao pia waende huko. Kuwe na bajeti nzuri ambayo itasaidia hawa vijana, kwani watajitoa sana na wanaumia sana. Kwa hiyo, naomba Serikali iangalie suala hili sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kuna timu hizi za watu wenye ulemavu, tunazisaidia vipi? Naomba nimwambie leo Waziri, kuna timu imekuja hapa Tembo Warriors tayari wanaenda kuwakilisha Kombe la Dunia, lakini kuna timu ya Albinism Sports Club ambao nao wanaenda Kenya keshokutwa hapa kwa ajili ya kuwakilisha nchi. Sasa tunazisaidiaje hizi timu? Tutafute namna yoyote ile ambayo Wizara na Bunge lako Tukufu zisaidie hizi timu ili ziweze kwenda kuwakilisha michezo hii ili tuweze kukuza hii nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumze kuhusu masuala ya muziki pia leo. Kaka yangu hapa Mheshimiwa Babu Tale amezungumza sana kuhusu BASATA na COSOTA. Naomba niwaambie jambo moja, msanii mpaka mnamwona amefika pale, amepitia mambo mengi sana; anapitia changamoto nyingi sana. Ukizingatia kwamba huyu msanii hana pesa, hana capital ambayo inamwezesha kufanya hizi kazi zake. Kwa hiyo, wanapitia kwenye changamoto nyingi hapa katikati kiasi kwamba zinaondoa yale maadili ya Kitanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa leo hii msanii ameshakuwa hivyo: Je, Serikali mnafanya nini? Kazi yenu kubwa ni kutoa elimu siku hadi siku ili hawa watu tuweze kuwa-shape, wajue sasa kwamba wanaenda kuwakilisha nchi. Tuwa-shape wawe wasanii wazuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii ukisema tu msanii amekosea, amevaa vibaya, hujamtengeneza au hujamkuza vizuri au hujamlea vizuri, hujampa elimu vizuri, unamfungia kazi yake. Hivi mnafahamu tunatumia gharama kiasi gani kutengeneza hizi video? Hivi mnafahamu tunatumia muda kiasi gani ku-invest kwenye hizi videos? Hivi mnafahamu vyote hivi? Hamfahamu! Sisi ndio tunafahamu ndiyo maana leo hii tulipambana kuja humu Bungeni tuwazungumzie wananchi wetu waliotuleta humu Bungeni, lakini tuzungumze juu ya masuala ya sanaa ya nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii umemsikia pale Mheshimiwa Riziki Lulida hajaniita Mheshimiwa Khadija, ameniita Mheshimiwa Keisha. Hilo ndiyo jina ambalo linatambulika katika nchi hii. Hili jina halikuja hivi hivi tu, limekuja kwa juhudi.

MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Taarifa.

T A A R I F A

MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Naibu Spika, natoa taarifa kwa mwongeaji kwamba mambo yote yanayotokea, kwa kweli wanatakiwa Wizara hii pamoja na yote waelezee kwamba wameshawatafutia masoko ya kazi zao wasanii hawa katika maeneo au nchi ngapi? Watupe idadi. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Taarifa hiyo.

MHE. KHADIJA S. TAYA: Sijaielewa taarifa. (Kicheko)

NAIBU SPIKA: Haya tuendelee. (Makofi)

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninachotaka kusema hapa ni kwamba wasanii tunatumia muda mwingi sana kutengeneza majina yetu ili tufike pale tunapopataka. Tunatumia investment ambazo hatujui hata namna ya kuzipata lakini tunazipata. Sijui mnanielewa! Hatujui hata namna tunavyozipata, lakini tunazipata.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwa kutumia hizi changamoto tunazopitia, sometimes tunakuwa frustrated, tunahitaji elimu, tunahitaji semina nyingi, nyingi. Kwa hiyo, naomba hii Wizara ikiwezekana, mwakani mwongeze bajeti ya kuwaelimisha wasanii, na sio wasanii kubwa peke yake, mwende Tanzania nzima kutoa elimu kwa wasanii ili wajue namna gani wanazifanya kazi zao vizuri katika maadili ya Kitanzania ili tuweze kutangaza nchi yetu Kimataifa vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu leo hii kuna wasanii jamani wanafanya kazi. Hii ni kazi kama kazi nyingine. Mfahamu hilo, hizi ni kazi kama kazi nyingine. Kuna wasanii wamesoma katika hii nchi. Kuna wasanii wamesoma; Nanji amesoma, Billnass amesoma, Zuchu amesoma India Advance Diploma ya Business, Saraphina amesoma Petroleum Chemistry Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na leo hii ni msanii pale amesimama, Mwana FA ana Masters ya Uingereza, ana Degree ya pale IFM, mimi nina degree ya pale CBE. Tumesoma, msitudharau. Msione kama vile katika hii nchi hatuna mchango wowote. Tuna mchango mkubwa sana, na leo hii tunazungumzia kila siku hapa masuala ya ajira, sijui ajira ndogo, ajira nini! Tukiweza kutengeneza vijana vizuri vijana humu ndani, nawambieni suala la ajira litakuwa ni historia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kila nyumba kuna msanii mmoja, katika kila nyumba, kuna wanamichezo, tunataka nini tena? (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante, kengele ya pili.

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kupata fursa ya kuchangia katika Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora. Awali ya yote naomba nimshukuru tena Mwenyezi Mungu kila siku kwa kutuamsha salama na tukiwa na afya njema.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, naomba nimshukuru Mheshimiwa Rais kwa muda wake anaoutumia angeweza kuwa na familia yake, lakini muda mwingi anafanya kazi kwa ajili ya Watanzania na sote tunaona na tuna-appreciate sana, atambue hilo. Kwa nafasi yake tunamheshimu sana na tunasema tena tunasimama na Mama Samia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nishukuru Mhimili wa Bunge; Mheshimiwa Spika na wewe Naibu Spika, nawashukuru sana kwa sababu mnaendesha Bunge letu vizuri, mnatupa nafasi na fursa vijana leo hii ni mara ya tatu nachangia. Ahsanteni sana na Mungu awabariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo kwenye Ofisi hii ya Utumishi na Utawala Bora au Wizara hii ya Utumishi na Utawala Bora nataka nichangie mambo kadhaa. Naomba kwanza niwapongeze sana, mmefanya kazi nzuri sana. Mimi nikiwa Mjumbe wa Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria, mna mipango mizuri sana kiasi kwamba natamani sana tupate pesa za kutosha. Tupate pesa za kutosha vipi? Tupate pesa za kutosha kwa ajili ya kutimiza yale ambayo tumeyapanga katika mipango yetu endelevu tunayoenda kuifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano tu TAKUKURU kwa mwaka 2023/2024 wameweza kujenga ofisi tatu za mikoa. TAKUKURU hao pia wameweza kujenga ofisi saba za wilaya katika kipindi cha Mama Samia. Ni kipindi cha mwaka mmoja tu, TAKUKURU hawa hawa wameweza kuajiri watu 350. Ni hatua kubwa sana hiyo ambayo Serikali inafanya na tunawashukuru sana kwa sababu hizi ajira ni za watu wetu, ni za wananchi wetu. Sisi kama Wabunge tunawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiachana na TAKUKURU kwa mambo ambayo imefanya, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeweza kusimamia promotions mwaka 2021/2022 watumishi 91,841 wamepata promotions. Mwaka 2022/2023 promotions 120,210. Mwaka 2023/2024 promotions watumishi 81,515 lakini mwaka 2024/2025 tunakadiria tutaweza kuwapandisha watumishi 219,000. Hizi zote gharama yake ni shilingi 789,615,000 na kuendelea. Hii ni hatua kubwa sana ambayo mmeifanya naomba niwapongeze sana Utumishi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo, mmeweza kuajiri katika hiyo miaka, mwaka wa kwanza ule 2021/2022 mmeajiri watu 32,000, mmeajiri tena watu 30,000 kwa mwaka unaofuatia, mmeajiri watu 47,000 na mmekadiria kuajiri watu katika mwaka huu wa bajeti 2024/2025 watu 45,000. Mwenyezi Mungu awatangulie sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana mwanzo nilianza kusema kwamba hizi pesa tunazopitisha hapa Bungeni zifike kwenye hii ofisi, kwa sababu tunaenda kuhakikisha ajira za Watanzania zinaenda kupatikana. Tumsaidie Mheshimiwa Rais, tuhakikishe vipaumbele vya ajira vinakuwepo kwa sababu nchi yetu hii changamoto kubwa iliyopo ni ya ajira. Ndiyo maana sasa hivi Serikali imekuja na utaratibu mzuri wa kuanzisha vyuo vya mafunzo ili watu waweze kujisimamia na kujiajiri ambayo ni hatua nzuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna watu ambao wamesoma maeneo mbalimbali na wameshatumia muda mrefu sana kusoma lakini ajira hakuna. Kwa hiyo, ajira hizi bado tunazihitaji pamoja na vile vyuo ambavyo vipo, tunavihitaji pia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka nigusie naomba zile rufaa zinazotolewa na watumishi mzifanyie kazi kwa haraka sana. Jambo lingine naomba Ofisi hii au Wizara hii ya Utumishi na Utawala Bora, hakikisheni mnafanya tathmini ya kujua ofisi gani kuna wafanyakazi kiasi gani na kuna uhaba wa kiasi gani? Kwa sababu kuna ofisi ambazo wafanyakazi ni wengi zaidi ya ofisi nyingine ili iwe rahisi ninyi ku-reallocate wafanyakazi waende kwenye maeneo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja hayo, nataka pia nigusie suala la uhamisho ambalo kila mtu hapa ameligusia na amelizungumzia. Kusema ukweli mimi kwenye hili nitakuwa tofauti na wenzangu, mnisamehe.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni mhubiri wa kutokuhamisha watu. Kwa sababu gani? Kwa sababu watu wanakosa ajira kwa muda mrefu, wanapopata ajira wanapangiwa maeneo ambayo kule kuna wananchi na hao wananchi wanahitaji huduma yetu. Hao wananchi wanahitaji huduma yetu jamani. Hivyo basi, kama wananchi wanahitaji huduma yetu, tunahitaji kuwatendea kazi, tunahitaji kuwatumikia, isipokuwa tu pale ambapo mtu atakuwa na sababu za msingi zinazomfanya ahame kutoka eneo moja kwenda eneo lingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani nitakuwa nimeeleweka kwamba, mimi siyo muumini wa kutaka watu wahamishwe maeneo kwa sababu ya matakwa yao, ila wahamishwe maeneo kwa sababu za msingi zinazowahitaji wao wahame. Kuna sababu za ugonjwa ambazo zinahitaji hospitali kubwa, basi mtu ahamishwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kushauri jambo kwamba katika zile ajira ambazo mnatangaza, kwa nini msiainishe kwamba ajira hizi ni za mikoa hii ili wale watu wanaoenda kuomba wajue kabisa wanaomba kwenda kwenye hiyo mikoa, wasiombe kwa ajili ya kutaka kuingia ili wahame? Waombe katika Mikoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia hata wale wenye matatizo, wanaotaka kuhama, kwa mfano juzi kati kulitokea kesi moja kuna mtu anataka kuhamia Manyara na mwingine anataka kuhamia Dar es Salaam, hawa watu wawili waliweza kuwasiliana wakabadilishana. Ikitokea fursa kama hiyo Utumishi, pitisheni tu kwa sababu hawahitaji gharama zenu, wanahitaji kuhama kwa matakwa yao basi, msiingie gharama kama Serikali ya kuwahamisha mtu kama huyo ambaye anataka kuhama kwenda sehemu nyingine ambayo yeye anaona kwamba inafaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kusema hayo, naomba pia niwashukuru sana Ofisi ya Utumishi na Utawala Bora kwa kuwa mmeweza kutengeneza utaratibu mzuri ambao unaenda kusaidia watu wenye ulemavu kwenye usahili kwa urahisi zaidi. Namaanisha nini? Pale mnapowaita watu wengi sehemu moja, mnatakiwa mtambue mahitaji ya watu wenye ulemavu. Tayari mmeweza kuainisha katika Kamati yetu kwamba mtaweka utaratibu maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu, kwanza wawe ni first priority kwenye interviews, pia kuwawekea maeneo maalum kwa wao kupumzika ili wasipate ile pressure kutokana na hali zao na ugumu wa mazingira kwao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba niwapongeze sana kwa kujali hilo, na kwa sababu hii ni Serikali ya Mama Samia, Serikali ya Mwanamke inatambua, inathamini watu wenye ulemavu, pia utu wa binadamu. Kwa hiyo, hongereni sana kwa hilo. Hongera sana Mheshimiwa Waziri Simbachawene kwa ushirikiano wako, umefanya kazi nzuri sana na unashirikiana vizuri na Kamati yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kupata nafasi hii ya kuchangia katika Bajeti Kuu ya Serikali hii. Awali ya yote, naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kunifanya kuwa mwenye afya njema, namshukuru sana kusema kweli na sote tunapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema. Jambo la pili naomba nimshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Rais, kwa jambo zuri alilolifanya, jambo ambalo linaenda kuondoa umaskini katika hii nchi na jambo ambalo linaenda kumwezesha mtoto wa maskini kupata elimu. Hili suala la elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka form six ni jambo la kiukombozi sana, sana. Watu wengi hawana uwezo wa kujisomesha, lakini leo hii wataweza kusoma bure mpaka form six. Hili ni jambo la kihistoria na ni jambo la kwenda kutangaza na kulisemea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, naomba niishukuru Serikali kwa kuongeza bajeti ya kilimo. Kilimo ni uti wa mgongo, kilimo ndio chenye kuondoa umaskini wetu. Kilimo ndio chachu ya uchumi wa nchi yetu. Sasa leo hii bajeti imeongezwa, inaenda kuongeza ufanisi na ubora katika kilimo chetu ili tuweze hata kuuza nje ya nchi. Naomba nishukuru pia nimshukuru au nimpongeze Mheshimiwa Mwigulu, bajeti hii imelenga hasa katika kubana matumizi. Tunaishukuru sana Serikali, tunawashukuru sana sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii naomba niongelee masuala ya wanawake au makundi maalum. Taasisi ya TWCC au Tanzania Women Chamber of Commerce, wakishirikiana na Trade Mark East Africa wamefanya tafiti ambayo hii tafiti imeonesha wanawake asilimia 40 na vijana asilimia 47 ndio makampuni yaliyosajiliwa katika nchi hii. Tukiangalia Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2006, ambayo imekuja kuwa amended mwaka 2011, sheria inataka Serikali katika mapato yake au katika manunuzi yake, asilimia 30 iende kwenye makundi maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kushangaza, ni asilimia moja tu imeenda kwa wanawake. Tukiangalia kwa tafiti za mwaka 2019/2020 tunaweza kuona kwamba Serikali ilitengeneza au ilitenga kiasi cha shilingi trilioni 25, ambapo asilimia 30 ni sawasawa na trilioni 8.0, katika hizo trilioni 8.0 ni asilimia moja tu, narudia tena asilimia moja tu ndio wanawake wameipata ambayo ni shilingi bilioni 80 tu, ni kiasi kidogo sana cha pesa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tukiachana na hilo juzi kati Naibu Waziri amejibu swali la Mheshimiwa mmojawapo hapa Viti Maalum, amesema kwamba, katika halmashauri 184 ni halmashauri 24 tu zimeweza kutenga vikundi au kuweka vikundi 88, hivi vikundi 88 kwa ajili ya kupata tenda za halmashauri. Vikundi 88 hivi ni vikundi vinne tu vilivyopata tenda za halmashauri na hii asilimia nne ni ya Mkoa wa Dodoma peke yake, ambayo ni Halmashauri ya Dodoma Jiji. Hawa vijana au hawa wanawake ndio wamepata hizi tenda za kupaka rangi, za TEHAMA na kadhalika. Sasa unaweza kuona ni kiasi gani hali ni ngumu katika nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii sasa tunaona katika bajeti kwamba wana- plan ya kuondoa asilimia tano iende kwenye kwa hawa machinga, ni wazo zuri sana na sitaki kwamba lisiende, lakini kwa nini tusiongeze? Kwa nini tusiongeze asilimia badala ya kupunguza asilimia ambayo haiwezi kutuwezesha. Ukiangalia katika vikwazo vya hawa watu kutokufikisha ni kwa sababu ya kukosa fedha, kwa sababu ya kukosa uelewa na haya mambo kama kuna hii sheria ipo, lakini pia ukiachana na hayo kuna masuala ya rushwa asilimia 10 ya wale wanunuzi wenzangu masuala ya procurements, lakini ukiachana na hayo kuna sababu nyingi tu ambazo zinakwamisha wanawake kwenye wasipate hizi tenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Serikali ninachosema hapa ni kwamba asilimia tano, asilimia mbili ya wanawake, asilimia mbili ya vijana, cha kusikitisha zaidi asilimia moja tu ya watu wenye ulemavu. Asilimia moja tu ya watu wenye ulemavu sijui aliyekuwa anafikiria alikuwa anawaza nini? Labda alikuwa anawaza ile asilimia mbili ya watu wenye ulemavu kuna mtu mwenye ulemavu ataenda kwa ajili ya wanawake, ataenda kwa ajili ya vijana, kwa hiyo asilimia moja inawatosha, seriously, hivi ndio tunavyotaka tujenge nchi? Hivi ndivyo tunavyotaka tuinue watu wenye ulemavu? Sio sawa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba leo niseme sio sawa kabisa na kama wanataka hii aslimia moja wanaweza hata wakachukua basi nayo pia kwa sababu tunakuwa kama vile tunafanyiana favor, asilimia moja ya watu wenye ulemavu? Kila siku napigiwa simu za kuombwa hela za watu wenye ulemavu na sio kwa sababu wanapenda kuomba ni kwa sababu hawana pesa. Sasa leo hii asilimia moja ya halmashauri inawatoshaje? Kwa nini Serikali isiangalie nyanja nyingine au namna nyingine ya kufanya ili wananchi au watu wenye ulemavu waweze kusaidika katika nchii hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan, namwomba Rais wetu aliangalie hili kwa jicho la pili. Wabunge wenzangu naamini hili jambo linaweza kwenda kutuondoa huko, tukisema tukubaliane na asilimia tano kukatwa kwa ajili ya kwenda kwa machinga wakati kuna makundi ya bodaboda, wakati kuna makundi ya akinamama ntilie, wanahitaji hizi pesa tunaenda kuumia. Mimi kama mtu mwenye ulemavu leo hii nitawaambia nini wenzangu kwamba nilikuwa Bungeni nilikubali asilimia moja ipitishwe. Sikubaliani na jambo hili! Naomba Serikali iangalie jambo hili kwa mapana ili iweze kusaidia wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiachana na hayo, kuna jambo la asilimia tatu, unaangalia kwenye masuala ya ajira asilimia tatu watu wenye ulemavu wanahitajika ili tu utekelezaji wake imekuwa ni ngumu, tena sio ngumu kidogo, ngumu sana. Sasa leo hii basi, haya mtu huyu hawezi kuajirika, anaamua kujikwamua aende halmashauri aombe mkopo, wanamwambia asilimia moja ya mkopo, tuwe wakweli jamani, tuwe serious na hii kazi. Sijaomba Ubunge kuja hapa kwa ajili ya kuja tu kukaa na kupiga makofi, nimekuja hapa kwa ajili ya kuwasemea wenzangu, lakini kwa asilimia moja nakataa na naomba Wabunge wenzangu waniunge mkono katika hili. Waone namna gani ya kwamba kama tunataka basi asilimia mbili ya watu wenye ulemavu, asilimia nne ya wanawake na asilimia nne ya vijana, halafu tuongeze asilimia tano iwe kwa ajili ya ya nini, kwa ajili ya machinga kwa sababu na wao pia tunawahitaji katika nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kupata fursa ya kuchangia bajeti kuu. Kwanza naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai na uzima aliotupa, pili naomba nimshukuru Mheshimiwa Rais, nikupongeze Mheshimiwa Rais, Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi zote ambazo umefanya, umeapa kushughulikia watanzania na kweli tunaona nia yako thabiti.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwapongeze Mawaziri wake pamoja na watendaji wote kwa kazi nzuri ambazo kusema kweli mnafanya, ambapo mnaleta maendeleo katika nchi yetu na tumeona baadhi ya mifano mizuri ya Mawaziri ambao wanachukua maamuzi magumu sana lakini yote kwa ajili ya wananchi wao. Kwa hiyo, niipongeze Serikali ya Mama Samia, nipongeze Awamu ya Sita ya Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wetu kipenzi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge lako Tukufu, Wabunge wako hawa wana uchungu, wanazungumza vitu vizuri wanatengeneza hoja nzuri za kupata mapato, tunatengeneza sheria humu ndani, tunatengeneza bajeti na tunapitisha bajeti. Hii yote ni kwa sababu ya wananchi ambao ndiyo wametupa kibali cha kuja kwenye nyumba hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nasema sisi ni wenye bahati sana, tuna bahati kwa sababu tumepata kuweza kufanya kazi, kazi ambayo ukiifanya vizuri utasifiwa na binadamu, lakini ukiifanya vizuri zaidi utaweza kupata thawabu kwa Mwenyezi Mungu ambaye ametuumba sisi wanadamu wake. Hilo ni jukumu kubwa sana lakini ni bahati kubwa sana na kuwa mtumishi wa umma na wewe una-responsibility the same kama Mbunge ambaye yupo kwa ajili ya wananchi wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema mwanzo, hawa Wabunge wako wanapitisha, Bunge hili linapitisha bajeti, bajeti kwa ajili ya wananchi. Tunawapa thamani au tunawapa watu ambao wanaenda kusimamia hizi hela zifanye kazi. Juzi tumesikia pale Arusha kwa Kaka yangu RC Makonda ambaye pia anafanya kazi nzuri, tumesikia kuna pesa ambazo zinaenda lakini hazifanyiwi kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi yetu sasa hapa ni nini, tunajukumu gani? Jukumu letu tushauri Serikali kitengo kile cha tathmini au monitoring and evaluation peke yake chini ya Waziri Mkuu bado naona hakitoshi, kwa sababu hiki kitengo hakina pesa ya kutosha. Kwa nini sasa tusitengeneze sheria ya kutengeneza mamlaka kamili ambayo hiyo mamlaka itaweza kuijisimamia kuanzia juu mpaka kwenye Halmashauri huku chini tukaweza kuzisimamia vizuri pesa zetu?

Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu kuna CAG ambaye anakuja baada tatizo limeshatokea. Kwa nini tusitengeneze mfumo mzuri, tunafahamu pesa kiasi gani imeengia Dodoma Mjini, ipo kwa malengo gani, kwa hayo malengo sasa tuone hiyo pesa inaenda kweli kwenye hilo eneo na je, zile criteria ambazo zimewekwa na wataalam wetu zinafuatwa? Unaenda hospitali katika vituo vya afya wamejenga tiles kabla ya kile kituo hakijatumika, tiles zimeanza kuonesha unyevu unyevu wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapoteza zile pesa ambazo tunazipitisha hapa lakini tunawalipisha kodi wananchi wetu. Tuangalie namna gani ya kuleta mamlaka rasmi ya kuhakikisha hizi pesa ambazo tunazitenga hapa zinaenda kufanya kazi inayotakiwa kufanya na zinaenda kusimamiwa inavyotakiwa kusimamiwa. Hili ni jukumu letu Wabunge tuhakikishe tunaleta hii sheria na tuitetee kwa nguvu yetu yote ili mamlaka rasmi ya tathmini na ufuatiliaji iweze kuundwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sijaishukuru Serikali ya Mama Samia. Juzi nizumezungumza masuala ya mtoto na mauaji ya watu wenye ualbino, Serikali imesikia, Mama Samia ametoa pole, Mheshimiwa Waziri Mkuu kaja hapa na mikakati mizuri ya kuondoa shida ya watu wenye ulemavu. Nasema ahsante sana Mama Samia, Nasema ahsante sana Mheshimiwa Waziri Mkuu lakini naomba kusisitiza mambo ambayo tumeyapanga, mikakati ambayo tumeipanga tuende kutekeleza na twende kuwakumbusha wananchi wetu huku chini kulinda watu wenye ualbino, lakini kuhakikisha tunaondoa zile hali za watu kuwa na uwoga. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa kengele yako ya pili.

MHE. KHADIJA S. TAYA: Ahsante Mheshimiwa, Daah! muda mfupi sana.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 2) wa Mwaka 2021 (Toleo la Kiingereza)
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa nafasi hii ambayo nimeipata leo ya kuchangia Muswada huu ambao tumeletewa, Muswada Na.2.

Mheshimiwa Spika, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Rais, kwa namna ambavyo anafanya kazi yake vizuri, anaongoza Taifa letu vizuri, anaonyesha ukomavu wa kisiasa na vile vile anaona kabisa namna gani ya ku-deal na masuala mbalimbali ya kitaifa ambayo kwa namna moja ama nyingine yeye anaona kwamba ni busara kunyamaza kimya na kufanya au kuachia vyombo vyake vifanye kazi.

Mheshimiwa Spika, nikupongeze pia kwa namna ambavyo unaendesha Bunge letu na kufuata Sheria zote na Kanuni zote za Bunge lako Tukufu ambalo leo hii sisi tunakuangalia kama kioo chetu na tunaangalia kama mfano mzuri wa uongozi, especially sisi vijana. Pia nikupe pole kwa changamoto ambazo unakutana nazo kwa sisi vijana ambao tumekuwa na mihemko ambayo tunaona kabisa haituletei afya kabisa katika Bunge letu na Taifa letu kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, leo hii nimekuja kuchangia mada tofauti tofauti ambazo kuna Sheria hii ya Mawakili, hii Sheria ya Mawakili katika Kamati yetu, tuliona kabisa Mawakili wanaapishwa na Jaji Mkuu wa Serikali. Tukaona kabisa kwa namna ambavyo sheria hii inatutaka tuwaweke hawa wawe wanajajiwa au wanatolewa na Mamlaka za Mkoa na si Taifa, hii ni kuondoa ile namna ya usomi wao au ni dharau kwao kwa kuona kwamba, yaani waondolewe kwa mamlaka ya chini wakati wao wameapishwa na mamlaka ya juu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo Kamati iliona kabisa kwamba kuna busara ya wao kuamuliwa na Kamati ya Kitaifa, lakini siyo Kamati ya Maadili ya Mkoa. Kwa hiyo naomba nikuhakikishie Kamati yako ipo makini sana na inafanya kazi kwa weledi na uamunifu wa hali ya juu.

Mheshimiwa Spika, kuna jambo lingine hili la masuala ya Sheria za Usajili wa Vizazi na Vifo; tuliona kwamba kwenye familia kuna mambo mengi sana ambayo yanatokea especially pale mtu anapofariki. Tumeona ni namna gani ambavyo famili zinakuwa na mkanganyiko. Watu wengi wanadhulumiwa mali zao na yote kwa sababu labda ya cheti na tukaona kabisa kwamba tuone namna wazazi I mean watoto wa familia au mwenza wa familia na au kama hao wote hawapo basi ndugu wapate hiki cheti ili kiweze kuwasaidia katika majukumu yao mengine.

Mheshimiwa Spika, hii Kamati yako haipo legelege kama watu wanavyofikiria, hii Kamati ya Katiba na Sheria ipo makini kuliko mnavyoweza kufikiria, kuna mambo ambayo yanaletwa katika Kamati yetu tunayarudisha kwenye Serikali na tunataka kuiomba Serikali iwe inaangalia mambo ya msingi ya kutuletea huku kwa maslahi ya Taifa letu. Nakupa tu mfano mzuri; tuliletewa issue ya Makatibu kwamba waendelee kufanya kazi endapo Bodi zinavunjwa.

Mheshimiwa Spika, sasa kitu kama hiki kwa maslahi ya Taifa mtu mmoja akaamua maamuzi ya wengi ambao hawa wengi walikuwa kwa ajili ya maslahi ya Taifa, sasa mtu mmoja kwa muda wa mwaka mmoja na zaidi ambao wao walikuwa wanataka tuwaongezee, tuwaongezee miezi mingine 12. Kwa kweli Kamati iliamua kwa pamoja kuondoa hii sheria, tukairudisha Serikalini. Kwa nilitaka kukuonyesha kwamba namna gani Kamati hii ipo makini na inajali maslahi ya Taifa lake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa yote ambayo tumeyapitisha hapo, naunga mkono hoja kwa kuona kabisa kwamba kila kitu tulichofanya tulifikiria mara mbili kwa kuangalia kwamba namna gani tunaweza kusaidia Taifa letu kupitia hizi sheria kwa sababu tunatengeneza sheria kwa ajili ya kutatua matatizo, hatutengenezi sheria kwa ajili ya kuendeleza matatizo ambayo yanatukuta katika jamii yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa kusema haya machache, nashukuru sana na Bunge lako hili Tukufu na Mwenyezi Mungu akujaalie uendelee kuwa na busara siku zote na hata pale utakapokuja kuombwa msamaha basi Mwenyezi Mungu busara ikuongoze na Mwenyezi Mungu akuongeze basi, uendelee kuwa na moyo huo huo wa kusamehe. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Khadija Shaabani Taya.

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 7) wa Mwaka 2021
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kupata nafasi hii ya kuchangia masuala haya ya sheria. Nami naweza kusema siku hizi naanza kuwa mwanasheria kidogo kupitia hii Kamati ya Katiba na Sheria wananifundisha mambo mawili matatu.

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba niungane na wenzangu wote kumpongeza Rais na Kamati Kuu kukuleta wewe kuwa Spika wetu. Tunakuamini sana na tunafahamu uwezo wako, kwa hiyo, tunakupenda sana na tunaamini kabisa utaleta mabadiliko mengi katika Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Rais na Serikali yake, imekuwa ni Serikali sikivu mno, ambayo inaleta tija. Mambo mengi sana ambayo tunayaomba, yanakuja. Leo hii nitawathibitishia Umma kwa namna moja ama nyingine kwamba mambo ambayo tunayasukuma kwenye Kamati, tunawasumbua Mawaziri, wameamua kuleta marekebisho leo.

Mheshimiwa Spika, leo hii ni siku ambayo watu wasioona wanapata ukombozi wa kupata elimu ambayo itawawezesha wao kujitambua na kujielewa vizuri zaidi. Leo hii tuna sheria ambayo ni ya Copyright and Neighboring Rights Act. Hii sheria inaruhusu Serikali kuweza kuchapisha vitabu ambavyo vitaweza kuwasaidia watu wasioona. Jambo hili ni kubwa mno katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata juzi niliuliza swali juu ya masuala ya vitabu vya nukta nundu. Leo hii Serikali inaenda kupata nafasi ya kwenda kuchapisha vitabu vyovyote vile ambavyo vinaletwa na watu, au vinachapishwa na watu. Kwa hiyo, ni mkombozi mkubwa sana kwa watu wenye ulemavu. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kutambua na kujali sana watu wenye ulemavu kwa kutuletea hii sheria.

Mheshimiwa Spika, katika hii sheria Ibara ya 20, pia tumeona kabisa kwamba wanaenda kudhibiti maudhui au vitu ambavyo vitaingia katika nchi hii ambavyo vinapingana mila na desturi zetu. Kwa hiyo, tayari tupo vizuri katika masuala ya desturi na tamaduni zetu, yaani Tanzania inaenda chini ya Mheshimiwa Mama Samia, tuko vizuri sana. Mama yetu anaupiga mwingi mno na we real appreciate. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sheria ya pili ni hii ya National Sports, mambo ya betting. Wapendwa hii sheria ni nzuri sana kwa sababu inaenda kidogo ku-discourage haka kamchezo kwa kutoa tozo kwa hii sports betting. Jamani vijana wengi sana wamejiingiza katika haya mambo. Naamini kabisa gharama inaenda kuwa kubwa kidogo ambapo watu wengi wataanza kufanya kazi. Mimi naamini kabisa vijana wanaenda kuanza sasa kufanyakazi zaidi na siyo ku-bett zaidi. Najua ni mambo ambayo mnapenda, lakini kidogo tu- discourage hivi vitu ili tuweze kuwa na Taifa zuri au vijana ambao wanaenda kufanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Spika, pia kingine, katika Kamati tumeshauri walete sheria nyingine ambazo zinaenda kuangalia kupata mapato sehemu nyingine pia. Siyo mchezo wa Sports Betting peke yake, basi hata michezo mingine au sehemu nyingine ambazo tunaona kabisa katika michezo, tutaweza kwenda kutengeneza michezo yetu na kulinda michezo yetu na kuimarisha michezo yetu.

Mheshimiwa Spika, kingine naomba pia nimpongeze Mheshimiwa Mchengerwa pale ambapo ameingia tu na masuala ya tuzo na masuala ya mirabaha; japo mimi mrabaha wangu sijapata, nashangaa sana kwa sababu Tanzania nzima inafahamu nyimbo zangu zimekuwa zikipigwa sehemu nyingi na tofauti tofauti. Ila naamini kabisa mwanzo ni mzuri, mmefanya kazi nzuri, tunaamini kabisa mnaenda kufanya mapinduzi ya hizi tuzo na hizi tuzo tunaambiwa kabisa hazitopendelea.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tayari tunaenda kutengeneza michezo yetu, sanaa yetu na utamaduni wetu. Kwa hiyo, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais na Serikali yake na tunashukuru pia kwa usikivu wa mambo na kuona namna gani ya kubadilisha sheria ambazo zinashindwa kutekelezeka zinakuja kubadilishwa ili ziweze kutekelezeka kwa urahisi zaidi. Hilo ndiyo lengo letu kuu la kubadilisha hizi sheria.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naishukuru sana Serikali na nakushukuru pia wewe kwa kunipa nafasi hii, japo nilisahaulika katika orodha, lakini umeni-consider ndiyo maana nasema unafaa sana na unaupiga mwingi sana. Ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Tume ya Mipango wa Mwaka 2023.
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kupata fursa hii ya kuchangia siku hii ya leo.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa viumbe vyote ambaye amenipa uzima leo nasimama hapa mbele kuchangia Miswada muhimu mitatu katika nchi yetu, ambayo hii miswada inaenda kuleta mapinduzi makubwa katika Taifa letu katika nyanja ya maendeleo na uchumi kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, naomba nimpongeze Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan sana kwa kufikiria kuleta Miswada ya aina hii ambayo sasa ameona ni namna gani inaweza kwenda kuchangia, kuchechemua maendeleo ya nchi yetu, lakini pia naomba nimpongeze kwa namna ambavyo anavyotembea usiku na mchana kwa ajili ya kutetea Taifa letu kuleta maendeleo na kusaidia jamii yake ya Tanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, pia naomba nikupongeze wewe kwa kuliongoza Bunge hili vizuri sana na kutupa sifa nzuri sana na keshokutwa hapo unaenda kuwa Rais, tunakuombea Mwenyezi Mungu akujalie uende kuwa Rais wa Bunge la Dunia. Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu tunaamini uwezo wako, tunaamini kabisa umaridadi wako, tunaamini kabisa weledi wako, kwa hiyo tunaamini kabisa unaenda kuwa Rais mzuri sana wa Bunge la Dunia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kuchangia Muswada wa Tume ya Mipango. Katika jambo ambalo Bunge hili tunapaswa ku-support leo hii ni hii Tume. Haya yamekuwa malalamiko ya muda mrefu sana kwa Wabunge wengi ambao mimi nimesikia michango yao humu ndani. Wanasema uratibu hakuna kwenye Serikali, wanasema juu ya mipango, leo hii tunaweza tukajenga shule lakini shule haina labda madawati, shule haina walimu, shule haina vitendeakazi vingi tu, Muswada huu unaenda kusaidia tatizo hilo.

Mheshimiwa Spika, Muswada huu unaenda kusaidia tatizo la kukosa vifaa vya hospitalini. Leo hii tunajenga majengo lakini hatuna vifaa ni kwa sababu tunakosa mipango thabiti katika nchi yetu. Leo hii Tume hii inaenda kusaidia upatikanaji wa vifaa vya hospitalini na upatikanaji wa vifaa vyote.

Mheshimiwa Spika, wakati mimi nasoma tulikuwa tunaambiwa sehemu ambayo tunataka tupeleke maendeleo, tupate mawasiliano, tupate maji, tupate umeme, tupate barabara nzuri. Nakumbuka tulikuwa tuna point zinasema lack of infrastructure, lack of transportation vitu vingi sana ambavyo tulikuwa tunajifunza mashuleni. Leo hii Tume hii inaenda kupanga mkakati mzuri sana. Tumeona barabara zetu watu wanajenga barabara baadae wanaenda kubomoa kwa ajili ya kupitisha mabomba ya maji. Tume hii inaenda kutatua tatizo hilo.

Mheshimiwa Spika, hii Tume imechelewa kuja kwa sababu tunaamini kabisa chini ya Mheshimiwa Rais hakuna Waziri atashindwa kupanga mpango mzuri wa watu wenye ulemavu. Tume hii inaenda kusaidia masuala yote ya watu wenye ulemavu. Tume hii inaenda kupanga mkakati mzuri wa watu wenye ulemavu wasaidiwe kwa namna gani katika nyanja ya elimu, katika nyanja ya afya, katika nyanja tofauti tofauti ya maendeleo na masuala mengine ya kimsingi.

Mheshimiwa Spika, Tume hii inaenda pia kusaidia kuna Sheria ya PPRA ya Manunuzi katika nchi hii, Wabunge wengi hawaifahamu hii sheria na hata watendaji wengine pia hawaifahamu hii sheria. Asilimia 30 ya manunuzi ya taasisi zote inatakiwa iende kwa makundi maalum. Sasa Sheria hii inaenda kusaidia utekelezaji wake wa hii Sheria, pia kusimamia Watendaji waweze kujua hii Sheria inapaswa kutekelezwa kwa namna gani. Kwa hiyo tunaenda kutengeneza mifumo mizuri ya utekelezaji, mifumo mizuri ya utendaji, kwa hiyo hii Sheria nawaomba Wabunge wenzangu leo hii tuipitishe kwa sababu ina umuhimu mwingi sana.

Mheshimiwa Spika, hii Sheria jamani inaenda kusimamiwa na Mheshimiwa Rais na Mawaziri wawili ambao ni Waziri wa Fedha na Waziri wa Mipango. Leo hii, hii sheria inaenda kuwa na tija kwa namna moja ama nyingine katika jamii yetu katika Taifa letu la Tanzania.

Mheshimiwa Spika, pia naomba nichangie juu ya Sheria ya Usalama wa Taifa. Katika pita pita zetu huko mitandaoni kuna watu wanasema kwamba kwa nini hii Sheria watu wanaenda kulindwa, wale wagombea Urais. Serikali imejipanga vizuri kulinda amani ya Taifa hili. Hii amani tunayojivunia ni kwa sababu Usalama wetu wa Taifa wanatusaidia sana. Sasa leo hii Wagombea wa Urais wanaenda kuomba nafasi ya Urais walindwe na nani? Je, leo hii wakipata shida yoyote huoni kama italeta machafuko katika nchi yetu? Kwa hiyo Sheria hii inaenda kuleta wapate mamlaka ya kwenda kusimamia viongozi wote ambao wanaomba nafasi ya Urais ili waweze kulindwa, kushauriwa namna ya kujilinda na namna ya kulinda na wajumbe wao ambao wanaenda kuwapigia kura.

Mheshimiwa Spika, vilevile kuna mtu alikuwa ananiambia kwamba hii Sheria inakwenda kuondoa madaraka ya Mheshimiwa Rais. Guys hii sheria inaenda kuongeza madaraka ya Mheshimiwa Rais. Ni nani ambaye anaweza kupinga mamlaka ya Mheshimiwa Rais wakati katika vitabu vyote vya dini vinatambua mamlaka za nchi, sasa ni nani ambaye anaweza kuondoa mamlaka ya Mheshimiwa Rais?

Mheshimiwa Spika, hii sheria inaenda kuongeza uwezo wa Mheshimiwa Rais kuchanganua mambo kuweza kulinda nchi yake vizuri, kuwasaidia Usalama wa Taifa vizuri, na Usalama wa Taifa wanaenda kumsaidia Mheshimiwa Rais katika mambo ya usalama wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kwa kusema hayo, naomba Bunge lako hili na Wabunge wako hawa, waweze kupitisha Sheria hizi tatu pamoja na Sheria ya Urekebu ambayo hii sheria ni muda mrefu sana miaka kadhaa haijafanyiwa marekebisho na leo hii tunaenda kufanya marekebisho ya Sheria hii ambayo inaenda kuleta mapinduzi ya kubadilisha Sheria mbalimbali za nchi hii.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kwa kusema hayo machache naomba niunge mkono hoja wa Miswada hii mitatu. Ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Yatokanayo na Urekebu wa Sheria wa Mwaka 2023 .

Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023.
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kupata fursa ya kuzungumza leo na kujadili miswada hii mitatu ambayo imeletwa mbele yetu katika Kamati yetu ya Utawala, Katiba na Sheria.
Mheshimiwa Spika, naomba nimpongeze Mheshimiwa Rais, nampongeza sana kwa sababu ameonesha nia ya dhati, ameonesha uthubutu wa hali ya juu, ameonesha namna gani anaguswa na demokrasia; ametuletea 4Rs, ambazo tunaenda kuzitekeleza katika Bunge hili. Bunge hili ndiyo litaamua kuwa 4R’s ziende ama zisiende. Bunge hili ndiyo litaamua tumwangushe Mheshimiwa Rais ama tusimwangushe.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze na Muswada wa Tume ya Uchaguzi. Kwanza kabisa wadau wamekuja, wamezungumza vizuri, wamechangia mno na Kamati tumesikiliza maoni yao na tumekubaliana nao katika jina la Sheria hii ya Tume ya Uchaguzi, jina la Tume ya Uchaguzi, tunahitaji Tume hii iitwe Tume huru ya Uchaguzi kwa sababu hakuna cha kukikwepa.

Mheshimiwa Spika, ndani ya Katiba imeshawekwa kwamba Tume hii itakuwa huru, kwa hiyo hakuna sababu yoyote ya kukwepa jina huru I mean katika Tume hii kuitwa Tume huru ya Uchaguzi. Kwa hiyo, naomba niipongeze sana Kamati pia naomba niipongeze Serikali kwa kulitambua hilo na kukubaliana na Kamati.

Mheshimiwa Spika, pili katika Muswada huu umesema kabisa kwamba kutakuwa na Kamati ya Usaili, ambapo Kamati ya Usaili tulitamani nayo iwe na ushirikishwaji au uwiano wa kijinsia katika ile Kamati ya Usaili, lakini kwa sababu nafasi nyingi zinaenda kwa advantage au kwa wale watu ambao tayari wana nafasi hizo jambo hilo tukaona kabisa tulipeleke katika Tume ya Uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, Tume ya Uchaguzi inasema kwamba Mjumbe mmoja atachaguliwa kutokana na nafasi yake, lakini tunasema kabisa katika hii Kamati ya Usaili izingatie uwiano wa kijinsia. Katika zile nafasi tano ambazo si nafasi mbili zile za Mheshimiwa Rais ambazo hatuwezi kuzigusa kwa sababu Katiba inatuongoza hivyo, nafasi ya Mwenyekiti na nafasi ya Makamu Mwenyekiti itateuliwa na Mheshimiwa Rais basi nafasi zile tano zilizobakia zizingatie uwiano wa kijinsia, kwa sababu huo ndiyo wimbo wa sasa especially tukiwa tunajua kabisa tuna Mheshimiwa Rais Mwanamke ambaye anahitaji kunyanyua wanawake katika maeneo tofauti tofauti.

Mheshimiwa Spika, katika Ibara ya 33 ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani inasema kupata wadhamini kwa ajili ya kukudhamini wewe kugombea nafasi. Naomba Bunge lako hili linisikilize vizuri sana. Hauwezi kuwa mgombea mzuri au huwezi kuwa kiongozi mzuri kama hujapeleka aina ya watu gani wanaonda kukudhamini. Muswada huu ulisema kabisa kwamba ni watu 200 tu bila kusema kwamba kuna issue ya gender. Kwa hiyo, tunachohitaji Muswada huu urekebishwe ili uweze kusema gender ambayo ni wanawake na wanaume ikiwezeakana na makundi maalumu ya watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Spika, wewe kuwa kiongozi mzuri ni pale ambapo unaona wale wanaokudhamini ni wanaume, wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ndiyo ita-determine uwezo wako wa uongozi na ndiyo itaweza kukusaidia wewe kujua namna gani ya kufanya kazi na kuwa mwajibikaji kwa kuamini kwamba waliokudhamini ni makundi yote, kwa sababu tunaweza tukaona kabisa hii kwa sababu tunalifumbia macho unakuta mtu anapeleka wanaume watupu wanaomdhamini hajali masuala mengine ya makundi maalumu, hatojali masuala ya kijinsia, kwa hiyo kwenye barua yako ya udhamini katika wale watu ambao unawaandika pale basi hakikisha kuna makundi. Serikali imekubaliana na hilo ina maana leo hii tutaweza kuwa na wanawake, watu wenye ulemavu pamoja na vijana. Mtu mwingine anaweza akasema kwamba hawafahamu wapi wanapatikana watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Spika, Serikali hii ina chama chake ambacho ni Chama cha (SHIVYAWATA) Shirikisho la Vyama Watu wenye Ulemavu, kila Mkoa kuna mwakilishi wa Mkoa, kuna mwakilishi wa Wilaya, katika Wilaya zenu kuna ofisi za watu wenye ulemavu utawapata huko kwa ajili ya kuwaandikisha watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Spika, katika Muswada huu wa Uchaguzi, nizungumze kama walivyozungumza wenzangu. Watu wanavyosikia ukatili wa kijinsia mawazo yao yanaweza yakaenda tu kwa ajili ya wanawake peke yake, naomba ni-declare interest. Mimi nina watoto watatu wa kiume, watoto watatu wa kiume sasa hivi kila ukienda kila semina tunayopata ni masuala ya wanawake, itafika kipindi wanaume watakuwa asilimia 20 tu, kuna umuhimu wa kuweka usawa wa kijinsia ili wanaume wasije kuzidiwa na wanawake.

Mheshimiwa Spika, nasisitiza tena sisi watoto wetu wanatuona sisi kama viongozi, wanatuona tumesimama katika Bunge hili wanatamani kuwa kama sisi, wanatamani kuchukua nafasi zetu na kama vile Daktari mtoto wake anavyotamani kuwa daktari na ndivyo hivyo Watoto wanatamani kuwa wanasiasa. Nami nimezaa watoto wa kiume na-declare interest natamani usawa wa kijinsia kwa sababu naamini watoto wangu hawataachwa nyuma.

Mheshimiwa Spika, yale mawazo ya kusema usawa wa kijinsia ni kwa wanawake tu au tunapambania wanawake peke yake muyaondoe. Usawa wa kijinsia na wanaume ifike kipindi tuangalie kabisa wanaume wawepo, wanawake wawepo wote wapate wawakilishi pamoja na watu wenye ulemavu bila kusahau watu wenye ulemavu, hii itasaidia sana uwakilishi na utekelezaji wa mambo yetu ambayo tunaenda kuyafanya.

Mheshimiwa Spika, kuna hili suala la unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa kijinsia hautokei tu kwa wanawake, unyanyasaji wa kijinsia hata kwa wanaume. Tunashuhudia ulimwengu wa sasa tunashuhudia kwenye mitandao ya kijamii wakisema kila mtu ni shoga uongo kweli? Kila mtu ushoga uwongo kweli? Ukitaka kujua wewe ni nani ongea, ukitaka kufahamu wewe unaonwajwe katika jamii ongea utatukanwa matusi yote. Mwanaume utapewa ushoga, mwanamke utapewa usagaji.

Mheshimiwa Spika, haya masuala tukemee, bila kuweka kwenye Sheria hii hatutaweza kamwe kusaidia jamii yetu na vizazi vyetu vijavyo. Tuangalie namna gani ya kuweka hili kosa kwa sababu kama tunaweka rushwa na kama rushwa ipo kwenye Sheria zingine kwa nini tusiweke ukatili wa kijinsia katika Sheria hii ya Uchaguzi ili kama tunahukumiana tuhukumiane papo hapo, hatuhitaji tena kwenda Polisi, kesi iwe ndefu, maana yake wewe umemtukana mwenzako unatenguliwa katika teuzi zako.

Mheshimiwa Spika, nakuomba sana katika Bunge lako hili tutatengeneza historia ya pekee kwa kipindi hiki ambacho Mheshimiwa Rais yupo Madarakani pale ambaye anapenda haki, anapenda usawa, tuhakikishe masuala haya tusiyaache. (makofi)

Mheshimiwa Spika, Sitafanya vyema kama sitozungumzia maswala ya Viti Maalum. Kuna vyama ambavyo havina utaratibu mzuri wa kuwapata Viti Maalum na sisi hapa ndani tunatengeneza sheria, tunanyanyasika, tunapata shida tunaonekana labda hivi viti ni vya kupewa tu wakati tunagombea wengine. Sasa leo hii tutengeneze sheria ya kufanya Tume ya Uchaguzi au Msajili wa Vyama vya Siasa, kati ya hawa wawili wasimamie, waelekeze katika vyama vingine watuambie wanapataje Wabunge wa Viti Maalum? Watuambie wanapatikana vipi Wabunge wa Viti Maalumu? Je, hakuna rushwa yoyote ya ngono ambayo inaendelea? Tuwe wawazi tuseme. Kwa sababu, wengine inasemekana hivyo maskini wa Mungu kwa sababu ya kutokuwa na utaratibu mzuri wa kupatikana kwa hivi viti. Kwa hiyo, mwisho wa siku kuna watu wanaweza kuweka wake zao, kuna watu wanaweza wakaweza watoto wao, sasa Tume iangalie na isimamie.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili siyo kwa sababu mimi nimesema hapa hata Katiba inasema. Ibara ya 81 imesema Tume itasimamia suala la uchaguzi wa Viti Maalum, ielekeze namna ya kupokea majina lakini pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kupata Viti Maalum. Hivyo basi naomba katika hizi Sheria tusiziache. Tutatengeneza historia ya kipekee katika Bunge hili na mimi nafurahi kuwa mmoja wa kuleta mabadiliko kwa ajili ya vizazi vyangu, watoto wangu ambao wangeweza kutamani kuwa kama mimi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo machache nashukuru sana na mbarikiwe mno. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa Mwaka 2023.

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023