Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Mustafa Mwinyikondo Rajab (2 total)

MHE. MUSTAFA MWINYIKONDO RAJAB: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kituo hiki kimejengwa kwa muda mrefu hivi sasa na kwa kuwa katika eneo hili kuna wananchi wamezunguka na sasa hivi wameshaanza ujenzi;

Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kufuatana nami kwenda kuhakiki mipaka ya ukubwa wa eneo hili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na napenda kumueleza Mheshimiwa Mbunge kuwa niko tayari. Tutaongozana ili kwenda kutatua tatizo la mipaka lililopo, ahsante sana.
MHE. MUSTAFA MWINYIKONDO RAJAB: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina masuali mawili ya nyongeza. Kwanza ninaipongeza Idara yetu ya Uhamiaji kwa kuwa na majengo mazuri na ya kisasa kwa upande wa Zanzibar. Swali langu la kwanza; ni lini sasa mpango huu utaanza?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; kwa kuwa tunaanzisha zahanati naamini kwamba kutahitajika wataalam wa kada za afya. Je, Idara ya Uhamiaji ina mpango gani kuwapata wataalam hawa kwa kipindi hiki?
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mustafa Mwinyikondo Rajab, Mheshimiwa Mbunge wa Diwani kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi ni kwamba, mara baada ya kupokea mwongozo kutoka Wizara ya Afya Zanzibar ndipo tutakapoanza ujenzi mara moja wa zahanati hii ya kuhudumia Askari pamoja na wananchi wanayoizunguka.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kuhusu wataalam, wataalam wapo, lakini Idara pia itaendelea kuajiri hatua kwa hatua kuhakikisha kwamba inakidhi mahitaji ya kutoa huduma katika zahanati ambayo itajengwa. Ahsante sana.