Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Answers to supplementary Questions by Hon. Exaud Silaoneka Kigahe (216 total)

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kwa kuwa ni zaidi ya miaka 30 sasa tangu wakulima wa chai wa Kilolo wapande chai yao na kujengewa kiwanda ambacho hakijawahi kufanya kazi; na kwa kuwa katika muda huo wako Mawaziri kadhaa na Manaibu wameenda kule wakapiga picha kwenye mandhari nzuri za mashamba yale na kuahidi wananchi wale kwamba shughuli hiyo itakamilika mapema iwezekanavyo na hawakurejea tena. Je, Serikali inatoa tamko gani kwa wananchi wa Kilolo kwamba sasa kiwanda kile kilichojengwa na hakikuwahi kufanya kazi, kitafanya kazi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa michakato mingi imepita ya kumpata mwekezaji na mchakato wa mwisho ulikuwa mwaka 2019 na wawekezaji walijitokeza na wakapatikana na wako tayari, na kwa kuwa uwekezaji huu haukukamilika kutokana na urasimu wa Serikali. Je, Serikali iko tayari kuwawezesha wale wawekezaji kwenda kuwekeza badala ya kuanza mchakato mwingine ambao unaweza ukachukua miaka mingine 30?Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Justin Lazaro Nyamoga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, Serikali imefanya jitihada nyingi sana kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi. Kwa taarifa tu ni kwamba katika miaka ya nyuma tayari kuna wawekezaji walikuwa wamejitokeza kwa ajili ya kuwekeza katika kiwanda hicho na mmojawapo ni Mufindi Tea and Coffee Company chini ya DL Group. Hata hivyo, baada ya kupitia mchakato wa upatikanaji wa mwekezaji huyo ilionekana kwamba kuna baadhi ya vipengele vilirukwa lakini pia baada ya kuwa na due diligence ya kutosha ilionekana kwamba mwekezaji huyo alikuwa hana uwezo wa kuwekeza katika kiwanda hicho.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, juhudi hizo bado zinaendelea na kama nilivyosema katika jibu la msingi kwamba sasa tunaandaa andiko maalum ambalo litaangalia namna bora ya uendeshaji wa kiwanda/shamba lile likihusisha ushirikishwaji wa wadau wote kwa maana ya wakulima wadogo, halmashauri ya Kilolo lakini pia na Msajili wa Hazina ambaye ndiye anasimamia kiwanda hicho. (Makofi)
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kama ilivyo kwa wananchi wa Kilolo, ni lini Serikali itakiamuru Kiwanda cha Chai cha Katumba kuongeza bei ya chai kwa wakulima wadogo wadogo katika Wilaya ya Rungwe?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, bei ya chai katika soko la dunia hivi karibuni iliyumba kidogo. Kwa hiyo, kampuni nyingi za chai zimekuwa na changamoto ya soko katika kuuza chai zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu bei kwa wakulima wadogo wadogo naamini baada ya kutengemaa kwa soko la chai duniani sasa hivi ni dhahiri shairi kwamba kampuni nyingi za chai ikiwemo hiyo ya Katumba, Mbeya na nyingine zitaweza kuwaongezea bei wakulima kwa sababu sasa kuna uhakika wa soko katika soko la dunia.
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwanza napenda kusema kwamba Serikali imepotosha Bunge lako Tukufu kwa kusema uongo ambao haukubaliki. Je, Waziri anajua kwamba TAMISEMI chini ya Waziri Jafo waliunda Kamati ya Uchunguzi (fraud) mwaka 2018 na Kamati hii ilitoa mapendekezo kuonesha jinsi SIDO ilivyowaibia wakulima pamoja na Halmashauri ambayo haikufanya kazi yake vizuri kuwasahauri wakulima na michango ambayo ilitolewa na Rais wakati huo Kikwete, karibu shilingi milioni 300 haikutumika vizuri na akaomba hatua madhubuti zichukuliwe na SIDO ilipe hela zile za wakulima?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, Mheshimiwa Waziri ana habari kwamba kutokana na kutofanya kazi kwa mitambo ile ndiyo maana sasa hivi PSSF imenunua mitambo mipya na inaifunga kwa kuona kwamba mitambo ile iliyofungwa ilikuwa batili? Inakuwaje Waziri…

NAIBU SPIKA: Umeshauliza maswali mawili tayari.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kaboyoka, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niseme hakuna uongo ambao umesemwa katika Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kama nilivyosema katika jibu langu la msingi kwamba SIDO baada ya kuingia mkataba ule na kuweza kufunga mtambo ule kulikuwa na changamoto mbalimbali na hasa kwenye upande wa ukaushaji katika mchakato ule. Baada ya kujadiliana na Halmashauri ya Same ikaonekana kwamba wakulima wale walikuwa hawaridhishwi na utendaji wa mitambo ile kwa hiyo SIDO ilishirikiana na mradi wa Market Infrastructure, Value Addition And Rural Finance - MIVARF kuagiza mtambo mpya ambao ulikuwa na gharama ya shilingi milioni 29 na SIDO walichangia katika mtambo huo mpya shilingi milioni 9 na ukafungwa kama nilivyosema tarehe 27/02/2015 na ukaendelea kufanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na hasara au gharama ambazo zilikuwa zimeingiwa na wakulima wale baada ya kuwa mtambo ule haufanyi kazi vizuri, kama nilivyosema tunaielekeza SIDO waweze kufanya mashauriano na Halmashauri ili waone namna gani ya kuwafidia wakulima wale ambao walipoteza mazao yao kipindi kile ambapo mtambo ule ulikuwa haufanyi kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mtambo uliopo sasa hivi unafanya kazi vizuri na yeye atakuwa ni shahidi. Wakulima wale wameridhika na wanaendelea kufanya kazi zao za kuchakata zao la tangawizi.
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri amekiri kwamba viwanda hivyo viwili anavyovisema, kimoja kinabangua tani 2,000 badala ya tani 5,000 na kingine hakibangui kabisa, kinafanya kufunga. Swali la kwanza; je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha viwanda hivi vinabangua kwa ule uwezo wake? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; katika Manispaa ya Mtwara Mikindani kuna kiwanda kikubwa cha kubangua korosho kinachomilikiwa na Kampuni ya OLAM. Kiwanda hicho kimefungwa. Kiwanda kile kilikuwa kinaajiri wafanyakazi wasiopungua 6,000 wakiwemo wanawake karibu 5,000. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha wanakaa na mwekezaji yule, kiwanda kile kiweze kufanya kazi ili wanawake wa Jimbo la Mtwara Mjini waweze kupata ajira wajikwamue kiuchumi?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kweli kabisa kwamba, kama nilivyosema katika jibu la msingi, kuna changamoto ya malighali kwa maana ya korosho ambazo zinahitajika katika viwanda vyetu mbalimbali vya kubangua korosho hapa nchini. Hivyo, kutokana na changamoto hiyo, Serikali kupitia Bodi ya Korosho, tumeandaa mwongozo ambao kwanza tunawapa kipaumbele wabanguaji wa korosho hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kuanzia msimu wa 2021 mwongozo huo unataka malighafi zinazopatikana katika mnada wa awali kupitia soko la awali la korosho, viwanda vyote vya ndani ambavyo vinabangua korosho, kwanza vipate korosho, vikishajitosheleza ndiyo sasa tunafungua ule mnada wa pili ambao sasa utahusisha wafanyabiashara wote ambao wako katika soko la korosho. Hii itapelekea kuhakikisha kwamba viwanda vyote vinavyobangua korosho vinapata malighafi kulingana na mahitaji yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kuhusu Kiwanda cha OLAM, ni kweli kiwanda hiki ambacho kilikuwa ni sehemu ya uwekezaji katika Manispaa ya Mikindani, changamoto kubwa iliyosababisha kufungwa kiwanda kile ilikuwa ni kutokana na kukosa malighafi ambazo zilitokana na ushindani wa wanunuzi wa korosho katika minada ambayo inafanyika kwenye maeneo hayo. Ndiyo maana tunapeleka mwongozo huu ambao sasa utahakikisha kwamba viwanda vya kubangua korosho vinapata malighafi kwanza, halafu sasa zile zinazobaki ndiyo zitaingizwa kwenye mnada ambao utajumuisha wafanyabiashara wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali tayari imeshaanza mawasiliano na Kampuni ya OLAM ambao waling’oa mitambo ile na kuipeleka nchi jirani Msumbiji ambako wao walikuwa na utaratibu mzuri wa kuhakikisha viwanda vinapata malighafi. Kwa hiyo, sasa tunataka warudi nyumbani kwa sababu nasi tayari tumeshaweka mwongozo huo ambao unawahakikishia malighafi viwanda vyote ambavyo vinabangua korosho hapa nchini. (Makofi)
MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Tunduru tuna Kiwanda cha Kubangua Korosho kilichojengwa miaka ya 1980 ambacho alipewa mwekezaji kwa muda mrefu na mwekezaji yule alikuwa anaendelea kubangua korosho bila kufikisha lengo la makubaliano na Serikali. Kufikia mwezi Agosti, 2020, kubangua korosho wamesimama kabisa na korosho za Tunduru zinalazimika kununuliwa na kupelekwa nje. Je, kwa nini Serikali haioni haja ya kumnyang’anya mwekezaji yule Kiwanda cha Tunduru cha Korosho na kupewa mtu mwingine ili uzalishaji wa korosho uendelee? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mpakate kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nia ya Serikali ni kuhamasisha uwekezaji wa viwanda mbalimbali hapa nchini ikiwemo viwanda vya kubangua korosho. Ni kweli kiwanda cha kubangua korosho cha Tunduru (Tunduru Cashew Factory) ambacho kilinunuliwa na Kampuni ya Micronics ambaye amewekeza katika maeneo mengi, bado kuna changamoto kidogo katika ufanyaji wake wa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema, lengo la Serikali ni kuona tunaendelea kuhamasisha uwekezaji katika viwanda. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mpakate kwamba tutakaa na mwekezaji huyu, tuweze kujadiliana naye, tuone ni changamoto gani ambazo alizipata katika uendeshaji wa kiwanda hicho.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, suala la kumnyang’anya kiwanda litakuwa baada ya kujihakikishia kwamba kweli ameshindwa kutekeleza kuwekeza katika kiwanda hicho halafu tuweze kuona namna bora ya kupata mwekezaji mwingine. (Makofi)
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza sina budi kuishukuru Wizara kwa jawabu zuri lenye mantiki ambalo linaeleweka na linalofahamika. Itakuwa ni hasa Watanzania wengi watalifurahia jawabu hilo kutokana na maelezo yake aliyojipanga.

Mheshimiwa Spika, lakini nina maswala mawili ya nyongeza. Kwa kweli matunda kama mananasi, matikiti, machungwa, embe n.k huwa yanazaliwa kwa wingi na yanakosa soko na yanaharibika mitaani. Je? Serikali inawaambia nini wananchi wa mikoa hiyo wanaozalisha matunda kwa wingi mbinu ya kunusuru matunda hayo ili yaweze kukaa kwa muda mrefu? (makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa tunazungumza Tanzania ya viwanda na ninakubaliana na maelezo yako, lakini ningeiomba Serikali ikawahamasisha wazawa wa Tanzania wa kila mkoa wakaweza kuanzisha viwanda ili kila mkoa ukawa na viwanda vya kusindika au cha kufanya juhudi yoyote ili mikoa inayozalisha matunda kwa wingi iweze kuyanusuru matunda yao na iweze kufanikiwa na wanachokilima kiwape faida yao? Naomba kuwasilisha.
NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Fakharia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli tunajua changamoto ya upotevu wa mazao yaani (post harass losses) kwa ujumla wake na hasa katika msimu ambao kunakuwa na mavuno mengi, kwa maana ya matunda mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango Madhubuti, kwanza wa kuhamasisha uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo ambavyo Waheshimiwa Wabunge kila mmoja maeneo yake anaweza kuwa na viwanda hivyo ambavyo vinaweza kuchakata mazao haya au matunda hayo kwa muda ambao yanakuwa yamezalishwa kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, lakini pili kupitia SIDO tuna teknolojia na viwanda vidogo vidogo vingi ambavyo vinachakata mazao ya matunda lakini pia teknolojia ya kukausha ili kuyatunza matunda hayo yasiweze kuharibika, yaweze kutunzwa ili yasiweze kupotea kabla ya kutumika.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hilo nashukuru kwa ushauri wa Mheshimiwa Mbunge; kwamba Serikali tunaendelea kuhamasisha kweli uanzishaji wa viwanda lakini pia na teknolojia nyingine ikiwemo kuwa na vyumba maalum cold rooms ambazo ni facility za kutunza matunda kabla ya kuuza yaweze kukaa kwa muda mrefu ili angalau yaweze kudumu yasiharibike haraka.

Mheshimiwa Spika, tunachukua ushauri wake lakini tunaendelea kuhamasisha uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo, lakini pia kupitia masharika yetu tuna teknolojia mbalimbali ambazo tunawakaribisha Waheshimiwa Wabunge kupitia SIDO na taasisi zetu nyingine waweze kupata teknolojia hizi ili ziweze kuwasaidia katika kutunza matunda ili yasiweze kupotea wakati wa mavuno mengi.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali la nyongeza. Ni kwamba, Serikali yetu sasa hivi imeingia kwenye mfumo wa Serikali ya viwanda na uhamasishaji huu umekuwa mkubwa sana. Katika Wilaya ya Liwale viko viwanda vidogo vidogo kazi yake ni kusindika korosho, lakini wananchi wale wanashindwa kupata mali ghafi kwa sababu ya kuwa na mitaji midogo. Tunafahamu kwamba korosho, zinazalishwa, zinauzwa kwenye minada; na kwa sababu wale wawekezaji ni wadogo wadogo hawawezi kuingia kwenye mnada matokeo yake anapoingia kwa wananchi kwenda kununua korosho anaoneka wananunua kangomba.

Mheshimiwa Spika, je, sasa Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wananchi wale wadogo wadogo kupata mali ghafi hii ya korosho ili vile vikundi vyao vya kubangua korosho viweze kubangua kwa msimu mzima au kwa mwaka mzima?
NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kutoka Liwale kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli usindikaji wa zao la korosho angalau sasa unaimarika kwa sababu sasa tumehamasisha uanzishaji na kufufua viwanda vingi vya kusindika korosho.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeshaweka utaratibu maalum baada ya kuona changamoto hiyo inayowapata wazalishaji au wabanguaji wa korosho wa viwanda vya ndani kutokana na ile changamoto ya kuweza kutokununua kwenye minada.

Mheshimiwa Spika, utaratibu uliopo ni kwamba wale wote wenye viwanda vya kuchakata au kubangua korosho ambao wanazalisha kwanza kabla ya kufungua msimu wa mnada huwa tunawapa kipaumbele wao kwanza, wanunue waweze kutosheleza mahitaji yao halafu zile korosho zinazobaki ndizo zitaingizwa kwenye mnada wa jumla. Lengo ni hilohilo kuwalinda, kulinda viwanda vyetu vya ndani ili viweze kupata raw material au malighafi ya kutosha kabla ya kuingia kwenye ile competition ya mnada mkubwa.

Mheshimiwa Spika, naomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge wa Liwale kwamba hilo tutalichukulia kwa umakini sana kuhakikisha viwanda vyetu vya ndani vinapata malighafi za kutosha ili waweze kuzalisha kadri ya uweze ambao viwanda hivyo vimesimikwa.
MHE. LUCY J. SABU: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Ninalo swali moja ambalo kwa kuwa NHIF na WCF walishaomba kibali hususani kwa ujenzi wa kiwanda hiki.

Ni lini sasa Serikali itatoa kibali cha ujenzi wa kiwanda hicho cha vifaa tiba Mkoani Simiyu? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Lucy John Sabu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama nilivyosema tayari mkakati huu wa kujenga kiwanda hicho upo na kweli WCF na NHIF ndiyo walikuwa wamepewa kazi hiyo kujenga kiwanda hicho.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Kamati Maalum ambayo inaratibu au inashughulikia sekta ya viwanda vya dawa na vifaa tiba ambao wanaendelea kuchanganua namna bora kama nilivyosema ya kutekeleza mradi huu. Kwa hiyo, kama nilivyosema tukishakamilisha taratibu hizo kiwanda hicho kitaanza kujengwa mara moja kupitia mifuko hii, lakini pia na MSD nao watashiriki kuhakikisha tunakidhi vigezo vya kutengeneza dawa zenye ubora unaotakiwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
MHE. JULIANA D. MASABURI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, napenda kuwashukuru Serikali kwa majibu yao mazuri, lakini je, Serikali imejipangaje hasa kuwachukulia hatua hawa wawekezaji ambao wanapewa hivi viwanda na wanavitelekeza na wanaenda mbali zaidi wanavichukulia mikopo na kuviacha hapo? Serikali imejipangaje kisheria kuwabana aina hii ya wawekezaji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Juliana Didas Masaburi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeshaanza kuchukua hatua na ndiyo maana tumeona katika viwanda vile 68 ambavyo vilikuwa haviendelezwi tayari hivi 20 vimesharejeshwa Serikalini. Lakini pia tunaendelea kuvitathimini na hivyo vingine.

Kwa hiyo niwahakikishie watanzania na Mheshimiwa Juliana Masaburi na Wabunge wote kwamba Serikali ipo makini kuona sasa wawekezaji wote watakaoingia mikataba ya kuviendeleza viwanda katika sekta zote pale ambapo watakiuka masharti ya mikataba tutakayoingia nayo sheria zitachukuliwa na hatua mahsusi ikiwemo kuwanyang’anya viwanda hivyo vitachukuliwa ili kuhakikisha sasa tunapata wawekezaji makini ambao kweli wataleta tija katika uendelezaji wa sekta ya viwanda nchini. Ahsante sana.
MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kuniona na mimi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kile Kiwanda cha MUTEX, Mheshimiwa Naibu Waziri amekubali kwamba aliyekuwa anakiendesha alinyang’anywa kwa sababu alikuwa hakiendeshi kwa tija na sasa yapata ni miaka mitatu kile kiwanda kimesimama.

Je, ni kwanini basi hata huyo, huyo asingepewa akakiendeleza kuliko ambavyo sasa kile kiwanda kimesimama na watu wanakosa ajira?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Vedastus Mathayo Manyinyi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati wa ubinafsishaji wa viwanda hivi kulikuwa na mikataba na katika mikataba hiyo kulikuwa na vigezo maalum na ndiyo maana tuliona sasa katika kuvunjwa kwa mikataba hiyo ndiyo maana imechukua muda mrefu ili kujihakikishia, ilikuwa mojawapo ni kumshawishi yule aliyepo kuona kama anaweza kuendeleza, lakini baada ya kujiridhisha kwamba ameshindwa ndiyo maana vimerejeshwa Serikalini.

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo ni kupata wawekezaji mahiri ambao kweli wapo makini na watawekeza kwa tija. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Vedastus Manyinyi, kwanza tuna dhamira ya dhati ya kupata wawekezaji sasa mahiri ambao watawekeza katika viwanda hivi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia tusingependa kuwaonea au kumpa mtu kwa upendeleo. Kwa hiyo tufuate utaratibu ambao utatangazwa na baadaye wawekezaji wengi watapatikana ambao watawekeza kwa tija.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye suala hili la viwanda tutakumbuka pia kulikuwa na viwanda vingi vya korosho vilivyopo maeneo ya kusini, Mtwara, Lindi, Masasi, Nachingwea na maeneo mengi. Serikali imesema imeamua kubinafsisha na kuna vingine vilikuwa vinatumika kama maghala ya kuhifadhia mazao badala ya kuviendeleza kuwa viwanda vya korosho ili kuweza kutoa ajira.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunataka tusikie commitment ya Serikali, ni lini zoezi hili wanalolifanya litakamilika ili kuweza kuvirejesha hivi viwanda, watu muda sahihi wa kukamilisha? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Cecil David Mwambe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi ni kweli kuna viwanda vingi ambavyo vimekuwa havifanyi kazi baada ya wawekezaji wengi kuvitelekeza au kutokuviendeleza au kuendeleza kwa kusuasua au kubadilisha matumizi ya viwanda hivyo ikiwemo wengine waling’oa hata mitambo ya viwanda hivyo na kubadilisha kuwa ma-godown.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Waheshimiwa Wabunge watuelewe kwamba Serikali ina nia ya dhati ya kuona sasa tunapata wawekezaji mahiri. Kwa hiyo hata viwanda vya korosho ambavyo vilikuwa vimetelekezwa kama nilivyosema tunaenda kutangaza utaratibu maalum wa kuweza kuwapata wawekezaji kwa njia ya wazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, baada ya hapo naamini wengi ambao wana nia ya kuwekeza katika viwanda hivi watapatikana na hakika tunaamini viwanda hivi vitaenda kufanya kazi kwa tija kama ambavyo Serikali imekusudia. Nakushukuru sana.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza kipekee nimshukuru Mkuu wa Wilaya mpya aliyekuja katika Wilaya ya Rungwe, jana ameweza kuwaita wadau wanaonunua zao la maziwa na kuhakikisha wanapatikana wengi na wala siyo mmoja tena.

Mheshimiwa Spika, swali langu la kwanza; Serikali haioni kuna haja ya kuleta Sheria Namba 3 ya mwaka 1977 ambayo ilikuwa inataka wakulima wote wanakaa katika mfumo wa kijiji. Sasa inawafanya Bodi ya Chai ambao ndiyo watoaji wa leseni hawawapi wakulima mmoja, mmoja kwa maana mkulima wa chai aweze kwenda kukopa benki, aweze kujua ni chai yake amuuzie nani na amkatae nani, sheria hii inawabana. Sasa kwa nini Serikali isilete marekebisho ya Sheria hiyo?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; Mrajisi wa Ushirika Wilaya ya Rungwe na sijui wilaya zingine alianzisha ushirika mpya na kuondoa ushirika wa kwanza bila kuwahusisha wakulima. Serikali inasemaje kwa hilo japokuwa jibu la msingi amesema ameweka, anasimamia na anafuatilia. Serikali ifuatilie kwa kina juu ya wakulima hawa ambao wao wanajua wapo RSTGA, lakini leo kuna kitu kinaitwa RUBUTUKOJE, wakulima wameachwa njia panda. Naomba Serikali ifuatilie kwa ukaribu suala hili. Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru sana dada yangu kwa ufuatiliaji wa karibu kuhusiana na maendeleo ya wakulima wa chai na maziwa katika Wilaya ya Rungwe.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kama nilivyosema kama kuna maendeleo ambayo anayaona kupitia Mkuu wa Wilaya kama tulivyosema tayari tumeshaanza kulishughulikia hili, ili kupata taarifa maalum kama nivyosema kwenye jibu la msingi kupitia Tume yetu ya Ushindani (FCC). Kwa hiyo hilo analolisema kuhusiana na Sheria Na.3 ya mwaka 1977, basi tutaangalia hilo pia, lakini tukipata taarifa maalum kulingana na ambavyo tumeomba kwa maana ya utaratibu wa ununuzi, namna bei zinavyopangwa katika soko, lakini pia na majina ya wanunuzi ambao wanashiriki katika ununuzi wa chai na maziwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Mrajisi katika Vyama vya Ushirika, naomba nalo tulichukue kama Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, tutafuatilia ili tuone ni namna gani tutatatua changamoto ambayo inawakabili wakulima wa chai na maziwa katika Wilaya ya Rungwe. Ahsante.
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, gesi asilia ninayozungumzia kwenye swali langu la msingi ni ile gesi ya Songosongo na eneo mahsusi ambalo nimeulizia ujenzi wa kiwanda ni katika Mji wa Kilwa Masoko, ambapo kimsingi tayari eneo la kutosha lipatalo ekari 400 lilishatengwa tangu mwaka 1989, lakini pia TPDC ilishalipa fidia ya eneo hili na ni eneo ambalo lipo huru na lina hati. Je, Serikali inathibitisha kupitia Bunge lako Tukufu kwamba kiwanda hiki cha mbolea kitajengwa mahsusi Kilwa Masoko na si kwingineko? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kwa ridhaa yako kuambatana nami baada ya Bunge hili kwenda Kilwa ili akajionee maendeleo na maandalizi ya eneo la kutosha la kiwanda hiki? Ikiwa ni pamoja na uwepo wa bandari, uwepo wa eneo la kutosha kwa ajili ya upanuzi wa bandari, lakini pia uwepo wa eneo la kutosha kwa ajili ya kutolewa malighafi hii, lakini pia atapata fursa ya kujionea Kiwanda cha Maji cha Swahili Water pale Nangurukuru. Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nipo tayari.

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ally Mohamed Kassinge Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi ni kwamba tunataka kuona tunatumia malighafi iliyopo ya gesi asilia na kimsingi kama alivyosema TPDC tayari walishakuwa na eneo na hata wawekezaji hawa tunaojadiliana nao wengi tunataka waeleke kujenga katika Mji huu wa Kilwa Masoko ambapo ndipo malighafi inatoka.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana kwa juhudi zake za kufuatilia suala hili na kama nilivyosema mwanzoni nitaambatana naye katika maombi yake ili tuweze kupitia kuona namna gani tunajionea, lakini pia kuona na viwanda vingine ambavyo vimewekeza katika Mkoa wa Lindi hususani Kilwa Masoko.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba niulize maswali madogo mawili ya nyongeza. Pamoja na uwepo wa viwanda hivyo 14 alivyovitaja, lakini bado Serikali inaagiza dawa na vifaa tiba kwa asilimia 80 kutoka nje. Je, tatizo ni ubora wa dawa zinazotolewa nchini ama ushindani wa kibiashara?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa Serikali imesema ifikapo mwaka 2025 itafikia asilimia 60, napenda kujua tu, sasa hivi tuko asilimia ngapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema, Tanzania bado hatujajitosheleza katika uzalishaji wa dawa kwa maana ya kuwa na viwanda vichache ambavyo vinazalisha dawa na vifaa tiba kwa ajili ya matumizi hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala siyo ubora, ni uwezo wetu ambao bado haujakidhi mahitaji ya ndani. Suala la ushindani ni suala lingine kwa sababu ushindani upo hata katika bidhaa ambazo tumejitosheleza, lakini specifically kwenye hili bado uwezo wetu wa kuzalisha ndani ni mdogo, ndiyo maana tumelenga kuhamasisha kupitia vivutio mbalimbali ili tuwe na wawekezaji wengi zaidi wanaowekeza katika viwanda vya kutengeneza dawa na vifaa tiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kiasi ambacho kinaagizwa sasa, ni kweli hatujafikia uwezo wa kutengeneza asilimia zote za dawa kwa maana ya asilimia 100, bado tunaagiza zaidi ya asilimia 80 kutoka nje. Kwa hiyo, bado lengo letu kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, ni kufikia asilimia ya uzalishaji ifikapo mwaka 2025.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nilikuwa naomba kuuliza; je, Serikali ina mpango gani ya kufufua Kiwanda cha Machine Tools, kiwanda ambacho kinatengeneza vipuri kwa ajili ya viwanda vingine na pia vinatengeneza na kuunda mashine za kusaidia viwanda vingine vidogo na vikubwa?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo mnajua, Serikali sasa ina mpango wa kuendeleza uchumi wa viwanda. Kiwanda cha (Kilimanjaro Machine Tools – KMTC) ni moja ya viwanda muhimu sana kwa maana ya basic industries katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeshaamua kufufua kiwanda hicho. Katika bajeti ya mwaka huu tumetenga zaidi ya shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya kujenga kinu cha kuyeyushia chuma (foundry).

Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Saasisha Mafuwe kwamba kiwanda hicho sasa kinaenda kufanya kazi kwa sababu tutakuwa na uwezo wa kuyeyusha chuma na kuzalisha vipuri ambavyo vinahitajika katika viwanda vingine kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Viwanda hapa nchini. (Makofi)
MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri ningependa kuzungumza kitu kimoja:-

Mheshimiwa Spika, sasa hivi ni mwaka wa 12 toka fidia ya mwanzo ilipofanyika na wengine mpaka sasa bado hawajafanyiwa fidia. Na lile eneo Serikali ilishatengeneza GN tayari kiasi kwamba, wananchi wanashindwa kufanya tena chochote katika maeneo yale. Na maeneo yamekuwa mapori, yamekuwa usumbufu, wafugaji wameingia pale inakuwa mgogoro kati ya wakulima na wafugaji. Je, Serikali inaweza ikafanya mpango wowote kuwarudishia maeneo yao hawa wahusika kama hawatakuwa tayari?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, kwa haya majibu yake Mheshimiwa Naibu Waziri, yuko tayari mimi na yeye tuongozane bagamoyo tukafanye mkutano wa hadhara Mlingotini, ili awaridhishe wananchi wa kule kwa hili janga ambalo lilewapata kwa miaka 12 sasa?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, kwanza fidia ya mwisho iliyolipwa kwa wananchi hao ilikuwa ni mwaka wa fedha 2017/2018 kwa hiyo, sio kweli kwamba, ni zaidi ya miaka 12 katika malipo ya mwisho yaliyolipwa fidia kwa wananchi hao.

Mheshimiwa Spika, maeneo ya uwekezaji kwa ajili ya maendelezo, hasa kwa sekta ya viwanda na uwekezaji mwingine ni muhimu sana. Kwa hiyo, niwaombe Waheshimiwa Wabunge na Mheshimiwa mkenge kwamba, si vema maeneo ambayo yameashaainishwa kwa ajili ya maendeleo ya viwanda na uwekezaji mwingine kurudishwa kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika jibu langu la msingi, Serikali inaendelea kuona umuhimu wa kulipa fidia hizo haraka iwezekanavyo, ili uendelezwaji wa maeneo hayo uweze kufanyika. Lakini pili tunaendelea kushauri Serikali za Mikoa na halmashauri kuona namna bora ya kuyamiliki maeneo ambayo Serikali Kuu kwa maana ya kupitia EPZA tutakuwa bado tunashindwa kuyalipa, ili nia ya Serikali ya kuwa na maeneo maalum ya uwekezaji na hasa kwa ajili ya maendeleo ya viwanda yaendelee kuwepo kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Mheshimiwa Mkenge niko tayari, tutaongozana na wewe na wataalamu wetu kutoka EPZA ili kuweza kuongea na wananchi wa Mlingotini kwa ajili ya kuona namna bora ya kuendeleza, hasa kulipa fidia maeneo haya ambayo yametwaliwa.
MHE. IRENE A. NDYAMKAMA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, ni lini Serikali inawahakikishia wananchi wa Mkoa wa Rukwa itawatafutia wawekezaji na kuwekeza kiwanda hicho cha sukari mkoani hapo?

Mheshimiwa Spika, swali jingine, kwa kuwa, Mkoa wa Rukwa ni tatu bora kwa kilimo nchini Tanzania. Ni lini Serikali itaangalia tena mkoa huu kwa kuwekeza viwanda vingine?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaendelea na kuhamasisha uwekezaji au viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika mpango wa miaka mitano ambao umeuona moja ya maeneo muhimu sana ambayo tumeainisha ni kuhakikisha tunatafuta wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, ikiwemo miwa na mazao mengine ambayo yanalimwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Rukwa.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, na yeye ni mmoja wa wadau muhimu sana ambao tunaweza tukashirikiana ili kuhakikisha tunawekeza viwanda vidogovidogo vya kati na vikubwa kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa wa Rukwa. Lakini pia nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, muda wowote Wizara iko tayari kushirikiana na kukushauri na kushauriana na wawekezaji wengine, lakini pia kuangalia vivutio maalum ambavyo vitasababisha wawekezaji wengi kuwekeza katika mikoa yetu ikiwemo Mkoa wa Rukwa.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwa kuwa Serikali inakiri kwamba, uwezo wetu wa kuzalisha sukari ndani hautoshelezi mahitaji ya ndani na tunaagiza kiasi cha takribani tani tani zaidi ya laki moja za sukari kutoka nje.

Mheshimiwa Spika, na kwa kuwa, miwa ya wakulima katika Jimbo la Mikumi ni zaidi ya tani laki nne zinateketea mashambani. Na kwa kuwa, kiwanda cha Ilovo wakati wanauziwa walikuwa na masharti ya kuongeza upanuzi wa kiwanda hicho na Serikali inasuasua. Je, ni lini Serikali inaenda kuhakikisha kwamba, upanuzi wa kiwanda hicho unakamilika na mazao ya wakulima ya miwa yanaenda kupata soko la uhakika?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kama nilivyosema mahitaji ya sukari hapa nchini ni makubwa ukilinganisha na uwezo wetu wa uzalishaji wa ndani. Suala la wananchi kukosa soko katika Wilaya ya Kilombero ni moja ya maeneo muhimu sana ambayo sisi kama Wizara ya Viwanda na Biashara tumeshayaona. Na moja ya mikakati ya Wizara ya Viwanda ni kuona namna gani sasa tunaongeza uchakataji wa miwa ambayo inakosa soko katika viwanda vilivyopo.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO), tunaenda kuleta mitambo midogo ambayo itaweza kusaidia kuchakata miwa kwa wakulima wadogowadogo ambao wanakosa soko katika viwanda vikubwa kwa sasa, ikiwemo maeneo ya Kilombero.

Mheshimiwa Spika, kuhisiana na viwanda vilivyopo tayari kuna mipango maalum, kwanza kuhamasisha kuongeza uwekezaji kwa kuongeza uzalishaji katika viwanda hivyo, lakini pia kuhakikisha na wao wanaingia sasa, kuna kitu tunaita quail farming, ili waweze kusaidiana na wakulima wadogowadogo kuzalisha miwa mingi, lakini pia na wao wenye viwanda kuwa na mashamba mengine ambayo yatatosheleza mahitaji ya uzalishaji katika viwanda vilivyopo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwanza tutahakikisha miwa ambayo inakosa soko tunaleta hiyo mitambo midogo ambayo itachakata miwa hiyo, ili angalao wakulima wale waweze kupata soko la uhakika.

Mheshimiwa Spika, la pili. Tunaendelea kushirikiana na viwanda vilivyopo ili kuhakikisha wanahamasisha wakulima wadogowadogo kwa maana ya kuingia quail farming katika viwanda vyao.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri na Serikali kwa ujumla kwa majibu mazuri na ya kina kuhusiana na swali hilo ambalo tumeuliza, lakini naomba niulize maswali mawili za ziada madogo. Swali la kwanza; kwa vile SIDO inalenga watu wa chini watu ambao wapo kwenye vijiji na kadhalika na hawa watu ni vigumu sana waweze kuelewa hivi vitu alivyovieleza kwa sababu hata mimi nilikuwa sivijui. Je, wana mpango gani wa kuiongezea SIDO uwezo wa kujitangaza na kutekeleza maonesho kwenye miji midogo midogo kama Mji wa Himo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni kuhusiana na mabanda ya viwanda au majengo ya viwanda. Kasi ya ujengaji wa majengo haya ni ndogo sana pengine tunaenda na too much sophistication, lakini tukienda kwa mtindo mwingine naamini tutaweza tukaharakisha sana ujenzi wa haya mabanda. Je, kama wakienda na kasi hii kweli ni lini wanafikiria watatufikia sisi kule kwenye Mji wa Himo, Uchira na miji midogo midogo kwenye mikoa yetu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali madogo mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Charles Kimei, Mbunge wa Vunjo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli uelewa wa wajasiriamali wengi kuhusu huduma zinazotolewa na Shirika letu la Kuhudumia Viwanda Vidogovidogo (SIDO) bado si wa kuridhisha sana kwa sababu taarifa nyingi haziwafikii wale wajasiriamali wadogo. Namshukuru Mheshimiwa Dkt. Charles Kimei kwa mawazo mazuri kwamba sasa tuone namna ya pekee ya kuliwezesha shirika letu la SIDO kujitangaza zaidi kwa wajasiriamali wadogo ili waweze kutambua fursa na teknolojia ambazo zinatolewa na shirika letu la SIDO.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Kimei kwamba tunaenda kuwezesha SIDO na tunaenda kuwatengea fedha zaidi kwa maana ya mwaka ujao wa fedha 2021/2022 kuwatengea fedha zaidi ikiwemo kwa ajili ya kujitangaza ili angalau wajasiriamali wengi waweze kujua fursa na huduma za teknolojia ambazo zinazotolewa na shirika letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu majengo ya viwanda, naomba niwahakikishie Wabunge na Watanzania wote hasa wajasiriamali ambao wanataka kuwekeza katika viwanda kwa maana ya viwanda vidogo vidogo kwamba, tunakwenda kuwaongezea SIDO uwezo ili waweze kujenga majengo mengi zaidi ambapo humo wajasiriamali wetu wataweka viwanda vyao vidogo vidogo au mashine zao ambazo wataweza kuchakata mazao ya kilimo mbalimbali kulingana na mikoa au mahitaji ya sehemu mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tunaenda kuwaongezea uwezo SIDO ili angalau waendelee kujenga majengo mengi zaidi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wajasiriamali. (Makofi)
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi kuuliza swali dogo la nyongeza. Uhitaji wa viwanda kwa ajili ya kuchakata muhogo katika Jimbo la Vunjo unafanana sana na uhitaji wa huduma hiyo katika Jimbo la Buyungu. Jimbo la Buyungu na Wilaya ya Kakonko kwa ujumla ni wakulima wazuri sana wa zao la Muhogo. Tatizo letu ni upatikanaji wa mashine hizo za kuchakata na kuweza kupata unga na kuboresha thamani ya zao hilo, lakini pia ni bei…

NAIBU SPIKA: Uliza swali Mheshimiwa.

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, swali, je, ni lini tutapata mashine hizo za kuchakata unga wa Muhogo katika Wilaya yetu ya Buyungu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Aloyce Kamamba, Mbunge wa Buyungu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza katika jibu langu la msingi kwamba kupitia shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo SIDO tayari tuna teknolojia mbalimbali na hasa za kuchakata mazao mbalimbali ikiwemo kuchakata muhogo. SIDO tayari kupitia ofisi za mikoa na hasa katika Mkoa wa Kigoma tayari tuna mashine hizo za kuchakata muhogo katika ofisi za Kibondo DC, Kakonko, Kasulu na Uvinza. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge kupitia Ofisi zetu za SIDO, Mkoa wa Kigoma aweze kuwasiliana nao ili kuona kama atapata mashine kulingana na mahitaji yake ambayo yeye anaomba katika Jimbo lake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekee kama katika mashine hizo ambazo zipo katika Mkoa wa Kigoma itakuwa kwamba hazitoshelezi mahitaji yake basi nimhakikishie SIDO tupo tayari kuwasiliana nae ili tuweze kutengeneza mashine zinazokidhi mahitaji ya Mheshimiwa Mbunge na wajasiriamali katika Jimbo lake la Buyungu. (Makofi)
MHE. ANTHONY P. MAVUNDE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kwa kuwa taasisi za SIDO na TEMDO zilizopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara zimeonesha ufanisi mkubwa kwenye kutengeneza mtambo wa destemming na crushing ya zabibu ambayo inapelekea kutengeneza mchuzi wa zabibu ambao umeonekana una tija kubwa sana kwa wakulima. Je, Serikali ina mpango gani sasa kuziwezesha taasisi hizi mbili ili zitengeneze mashine nyingi zaidi za kuchakata mchuzi wa zabibu ili wakulima waondokane na kuuza zabibu na badala yake wauze mchuzi wa zabibu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anthony Mavunde, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Serikali kupitia taasisi za SIDO na TEMDO tumekuwa tukiwawezesha ili waweze kubuni na kutengeneza teknolojia mbalimbali ambazo zinachakata mazao ya kilimo ikiwemo zao la zabibu. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali sasa imeamua kwa dhati, kwanza kuziwezesha taasisi hizi kifedha, lakini pia na kuongeza uwezo kwa maana ya Rasilimali watu ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka huu wa fedha 2020/2021, tayari tumeshawezesha SIDO kama nilivyosema zaidi ya bilioni nne lakini pia TEMDO zaidi ya milioni mia tano ili waweze kusanifu na kutengeneza teknolojia mbalimbali ikiwemo za kuchakata zabibu.

Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama nilivyosema kwa wengine kwamba kwa wale ambao wana hitaji teknolojia maalum kulingana na mahitaji ya mazao yao kama hili la zabibu, basi naomba nimkaribishe Mheshimiwa ndugu yangu Anthony Mavunde, katika ofisi zetu za SIDO ili tuweze kuona namna ya kukamilisha mahitaji yake ambayo yatafaa kwa ajili ya kukamua zabibu.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri wa Viwanda. Tunazungumzia uchumi wa kati ikiwemo kuondeleza viwanda vyetu, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, je, ni nini mpango wa Serikali katika kuongeza viwanda vingi ili hawa vijana wanaohitimu mafunzo haya waweze kupata ajira kwa sababu naona ni vijana saba tu ambao wameajiriwa na Serikali?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, ni nini mpango mkakati wa Serikali kufufua viwanda vyote ambavyo vilijengwa enzi za Mwalimu ili hawa vijana wetu akribani 228 waliohitimu mafunzo haya ambao hawajapata ajira waweze kuajiriwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Christina Mnzava, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Tanzania tupo katika mkakati wa kuwa na uchumi unaoendeshwa na viwanda na hasa tukiwa sasa tumefika katika uchumi wa kati. Mpango wa Serikali ni kuhakikisha tunaongeza viwanda vingi kwa kuhamasisha sekta binafsi kupitia kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya wadau wa viwanda kuwekeza katika viwanda vingi ambavyo hatimaye vinatumia vijana wetu wanaohitimu katika vyuo vingi ambavyo vinatoa elimu hususan inayolenga katika kuongeza ubora wa bidhaa zetu zinazozalishwa katika viwanda lakini pia lengo ni kuona sasa tunakuwa na viwanda ambavyo vitakuwa vinapata wataalam walio na utaalam mahsusi katika mahitaji wa viwanda hivyo. Kwa hiyo, Serikali inaendelea kuhamasisha sekta binafsi lakini pia mashirika na watu mbalimbali na wawekezaji kutoka nje ambao wanaweza kuwekeza katika viwanda hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, katika swali la pili ni kweli viwanda vingi vilivyokuwa vimejengwa wakati wa enzi za Nyerere lakini pia viwanda vingi ambavyo vilikuwa vimebinafsishwa havifanyi kazi. Serikali ina mkakati maalum kwanza kupitia viwanda vyote ambavyo havifanyi kazi, lakini hasa vile ambavyo vilikuwa vimebinafsishwa kwa watu ambao hawaviendelezi ili tuweze kuvifufua. Lengo ni kuona sekta ya viwanda inaendelea lakini wa kutumia miundombinu ya viwanda iliyokuwepo hapo kabla ili viweze sasa kuchukua wataalam wengi ambao wanasoma katika vyuo vyetu vingi ili waweze kuajiriwa katika viwanda hivyo.
MHE. HAMIS M. MWINJUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri kwa niaba ya Serikali na ambayo yananipeleka kwenye maswali mawili ya nyongeza. Miongoni mwa matatizo makubwa ya kilimo na biashara ya viungo Wilayani Muheza ni kukosekana kwa ardhi kubwa ya kulimia mazao hayo kule ambako yanastawi. Pia na viwanda vya kuyachakata kulekule kwenye Tarafa ya Amani, ili kuyaongezea thamani kwa vile kule hakuna kiwanda hata kimoja. Sasa kuna ekari 35,063 ambazo ziko chini ya Kampuni ya East Usambara Tea Company ambazo zilikuwa na viwanda viwili ambavyo kwa sasa ni magofu na zinazotumika ni ekari 4,909 tu kwa miaka mingi na viwanda hivi vimegeuka magofu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, je, Serikali haioni hivi sasa ni wakati wa kuvirudisha viwanda hivi kwenye umiliki wake, ili kuwasaidia wananchi ikiwa ni kwa kuwekeza yenyewe ama kwa kushirikiana na wawekezaji wapya serious ili wananchi wa Amani wapate kupata viwanda vya kuongeza thamani mazao yao ya viungo kule? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; tatizo la aina hii, Waheshimiwa Wabunge wanaweza kuwa mashahidi, limekuwa likitokea sehemu nyingi ambapo wawekezaji wamekuwa wakiomba kumilikishwa viwanda hivi kwa ahadi ya kuvifufua na kuzalisha ajira pamoja na kuliongezea pato Taifa, lakini badala yake wamekuwa wanaviuwa na kuvigeuza kuwa magofu. Je, Serikali haioni sasa ni wakati wa kuwa aidha na sheria kali zaidi ama kutunga sheria mpya ili tusiendelee kuchezewa na viwanda vyetu vifanye makusudio yaliyokuwepo wakati vinaanzishwa? Nakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Hamis Mohamed Mwinjuma, Mbunge wa Jimbo la Muheza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Hamis Mwinjuma kwa kufuatilia sana maendeleo, hasa sekta ya viwanda katika jimbo lake. Amenifuata mara nyingi kuhusiana na viwanda hivi, hasa vya chai hivi vya East Usambara Tea Company Limited, ambavyo viko pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kuhusu suala la ardhi. East Usambara Tea Company Limited ina ekari 35,000 kama alivyosema na katika ekari hizo ni ekari 2,027 tu ndio zimepandwa chai na ekari 600 zimepandwa miti, kwa maana ya miti ile inayotumika kama nishati, kuni kwa ajili ya kutumika katika viwanda hivyo. Pia eneo lingine maeneo yaliyobakia ambayo yanamilikiwa na kampuni hii yanatumika kwanza katika sehemu nyingine ni vyanzo vya maji, lakini maeneo mengine ni natural reserve kulingana na utaratibu wa UNESCO kwamba, huwezi kutumia mazingira yote kulima, kwa hiyo, maeneo mengine makubwa yako katika mazingira ya reserve.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kutokana na uhitaji wa wakulima katika Jimbo la Muheza, tutaona namna gani kushirikiana na wenye kampuni, ili tuone kama wanaweza kutoa sehemu kidogo ambayo inaweza kutumika na wakulima wadogowadogo kwa ajili ya kuzalisha viungo ambavyo vitatumika katika viwanda vya kuchakata viungo kama alivyoomba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu uwekezaji katika viwanda hivyo. Nimjulishe tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, pamoja na ufuatiliaji huo wote, lakini viwanda hivi sasa vinafanya kazi vizuri. Uwezo uliosimikwa kwa viwanda vile viwili ambavyo vinafanya kazi vya Bukwa na Kwamkoro vina uwezo wa kuchakata kilo 120 kwa siku, lakini sasa hivi vinaweza kupata raw material kwa maana ya malighafi zaidi ya kilo 90,000. Kwa hiyo, maana yake viwanda hivi vinafanya kazi vizuri, lakini kuna viwanda vile viwili ambavyo kutokana na mahitaji haya wenye viwanda, Kampuni ya East Usambara Tea Company Limited, walivigeuza kama ma-godown, ambavyo vilikuwa Viwanda vya Munga na Nderema, lakini pia baadaye, nimjulishe tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, kampuni hii ina mpango sasa wa kuanza ku-pack kwa maana ya blending ya ile chai wanayozalisha pale badala ya kwenda kuuza kwenye minada ya Mombasa na kwingine, wataanza kufanya blending pale. Kwa hiyo, tuna mpango wa kuwasaidia ili wafufue viwanda hivi viwili viweze sasa kufanya blending badala ya kuwa store au magofu kama yalivyo sasa.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Niseme tu kwa majibu pia ya Serikali ambayo ni fifty fifty hivi, wakulima hawa wameanza kusumbuliwa sana na TAKUKURU. Wanakamatwa kila mahali na sijui kwa nini? Kwa sababu ni mkataba; sijui kosa la TAKUKURU linakujaje hapo! Niseme tu Mheshimiwa Rais wetu hapendi sana wakulima waonewe. Kwa kuwa, sasa Serikali imesema ilipata mkopo wa miaka 30, kwa nini wakulima hawa msiwape muda wa miaka 15 ili waweze kurejesha mikopo hii? Kwa sababu naamini ilikuwa ni nia njema sana, nami nimefanya vikao na watu wangu tarehe 10 Januari, 2021 na watu wa URSUS na kuna Wabunge wengi sana hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Wizara hii, Waziri na Naibu Waziri ni wapya, kwa nini wasitengeze kikao cha pamoja na Wabunge na watu wote wenye matrekta ili tuanze kujadili namna bora ya kuwasaidia wakulima hawa? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa ufuatiliaji ambao anafanya ndugu yangu Mheshimiwa Olelekaita kuhusiana na wakulima wa Jimbo la Kiteto. Nachukua maoni yake mazuri, lakini kwanza kuhusu TAKUKURU kuwasumbua hawa wakulima waliokopa, naomba Serikali tuchukue nafasi hii kusema kuwa tutawasiliana kwanza na wenzetu kupitia NDC tuone ni nini kilikuwa kinatokea mpaka TAKUKURU wakaingizwa kwenye utaratibu wa kufuatilia mikopo hii ambayo iliingiwa na wakulima wale waliokopa matrekta na NDC?

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ulipaji wa mikopo hii kwa kuongezewa muda, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba nalo hili tutalijadili kwa sababu ni mikataba ambayo iliingiwa na wakulima na walitoa wao wenyewe nafasi ya kulipa kulingana na uwezo wao. Kwa sababu ni nia njema ya Serikali kuhakikisha wakulima wanawezeshwa ili tuweze kupata mazao na malighafi za viwandani, basi tutakaa pia kupitia ili tuweze kuona namna gani tunawawezesha walipe kwa unafuu zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kikao cha pamoja, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa tutakuja, tutakaa na ninyi, tutajadiliana na viongozi wote na hasa wakulima ambao wanatakiwa kusaidiwa kwa namna yoyote ile ili waweze kufanya kazi zao kilimo kiwe na tija.
MHE. ENG. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kuniona. Kwa kuwa, swali la msingi nami pia nina wakulima kwenye jimbo langu la Hanang wanasumbuliwa vivyo hivyo; na malalamiko makubwa ya wakulima hawa ni ubora wa matrekta ambayo wamepewa na pia kukosa usaidizi pale ambapo matrekta haya yanaharibika, kwa maana ya matengenezo na matengenezo kinga na vipuri:-

Je, sasa Serikali iko tayari kuwasimamia hawa NDC pamoja na URSUS, kampuni iliyouza matrekta kuhakikisha kwamba matrekta haya yanahudumiwa kadri ya mikataba ya wakulima?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kumekuwa na changamoto kidogo kwa baadhi ya wakopaji kwa wakulima ambao walikopa matrekta haya ya URSUS katika suala la ubora. Kweli suala la teknolojia ambayo ilikuja na matrekta haya kulikuwa kidogo kuna changamoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Wizara kupitia NDC tulishaligundua hilo na hivyo tumeshaanza kulifanyia kazi kuona namna gani tunaweza kuwa na utaratibu mzuri wa kuwasaidia ili matrekta hayo yanayopata changamoto ya ubora kwa maana ya utekelezaji wa dhana nzima ya kuhakikisha trekta lile linafanya kazi, tumeshaanza kuainisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nikuhakikishie kwamba wenzetu wa NDC wameshaweka utaratibu mzuri wa kuwa na mafundi maalum ambao watapita kuwasaidia wakulima wale.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na vipuri, ni kweli matrekta haya kidogo yalikuwa na changamoto ya vipuri kwa sababu ni mapya na ile kampuni ya URSUS ilikuwa bado inaendelea kuleta baadhi ya spare. Kwa hiyo, hili nalo tunalifuatilia kuhakikisha kwamba matrekta haya yanaendelea kuwa na vipuri ili pale ambapo yanapata hitilafu au yanaharibika, basi angalau vipuri vya kurekebisha hitilafu hizo vinapatikana.
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, asante kwa kunipa nafasi. Swali la kwanza; uthamini wa mali na fidia ulifanyika tangu mwaka 2015, takribani miaka sita sasa wananchi wa Kata ya Mkoma Ng’ombe, Lwilo, Iwela pamoja na Mundindi hawajalipwa fidia hii ya bilioni 11.

Je, Serikali haioni kwamba, kuchelewesha kulipa fidia kwa wananchi hawa kutaiingizia Serikali gharama kubwa kwa sababu, nina wasiwasi isije tathmini hii ikaja kushuka thamani kipindi hicho wao watakachokuwa wanataka kuwalipa wananchi hawa fidia hiyo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; kwa kuwa kumekuwa na uhitaji mkubwa sana wa makaa ya mawe na NDC wamechukua vitalu vyote vya makaa ya mawe. Je, Serikali haioni umuhimu wa kutoa baadhi ya vitalu kwa wananchi wachimbaji wadogowadogo wazawa ili waweze kuchimba na kuweza ku-stimulate uchumi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Neema Mgaya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, uthamini wa mali kwa ajili ya kulipa fidia ili kupisha kuendelea kutekeleza mradi huo ulifanyika mwaka 2015 na kweli wakati ule thamani ya fidia iliyokuwa imeainishwa ni bilioni 11.03.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi ni kwamba, utekelezaji wa mradi huu bado uko kwenye majadiliano. Moja ya vipengele ambavyo viko kwenye majadiliano ni kuona namna gani mwekezaji ambaye atapatikana ataweza kulipa fidia ambayo iliainishwa, lakini pia baada ya kupitiwa kutokana na hali halisi ya sasa itabainika. Kwa hiyo, ulipaji wa fidia huu nao ni sehemu ya majadiliano ambayo tunaona kwamba, mwekezaji ambaye atapata nafasi sasa kuwekeza katika eneo hili yeye pia atahusika katika kulipa fidia ambayo ilibainishwa kwa ajili ya wananchi kupisha mradi ule.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu vitalu vya makaa ya mawe ambavyo vinasimiwa na NDC; naomba niwahakikishie kuwa ni kweli vitalu hivi kwa ajili ya maendeleo ya nchi NDC ndio inasimamia uendelezwaji wa uchimbaji katika maeneo hayo, lakini kwa ajili ya maendeleo endelevu mambo haya au biashara hizi za uchimbaji zinakwenda kibiashara zaidi. Kwa hiyo, wananchi au ambao wana uwezo kama wafanyabiashara au wawekezaji ikiwemo wananchi wa maeneo hayo wanaweza kwenda kuomba nafasi ya kushiriki katika maendeleo au uendelezaji wa uchimbaji wa makaa ya mawe katika vitalu hivi kwa kushirikiana au kupata vibali kutoka Shirika letu la Maendeleo la Taifa (NDC).

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunawakaribisha na kama watakidhi vigezo na kuweza kuwa na mitaji stahiki ya kuwekeza katika maeneo haya, nadhani hakutakuwa na shida, tunawakaribisha na shirika letu liko kwa ajili ya kusaidia Watanzania.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa fursa hii. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza, moja hilo ambalo umelileta la TAKUKURU na hili la Mheshimiwa Kamonga ambalo ameliuliza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimepanga kutembelea mradi huu mara baada ya bajeti yetu, Ijumaa. Katika ratiba zangu moja ya weekend nitatembelea mradi huu na tutazungumza na wananchi kwa ajili ya kuwapa maendeleo. Kwa kweli, katika bajeti yetu ambayo tutaitoa wiki hii tutaeleza kwa kina zaidi hatua ambazo zimefikiwa katika utekelezaji wa mradi huu na lini hasa utaanza. Kwa hiyo, nitafurahi sana Mheshimiwa Mbunge tukifuatana tukaenda kuzungumza na wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili la TAKUKURU. Naomba nilichukue hilo, tulifanyie kazi, tupate details hasa TAKUKURU wanafuatilia nini na katika mazingira yapi, ili tuweze kutoa jibu ambalo linaeleweka. Kwa sababu, kwa kweli, sina details za kutosha kuhusu TAKUKURU wanawakamata wananchi na kuwahoji katika masuala yapi hasa. Kwa hiyo, tunaomba tupate nafasi tulifuatilie tupate details, ili tukitoa jibu hapa tutoe jibu ambalo linaeleweka. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa haya masoko yamesimama muda mrefu, kuanzia mwaka 2013 na maelezo ya Serikali kila siku ni wanatenga bajeti: Sasa swali, Kwa kuwa haya masoko ni strategic, Serikali haioni ni umuhimu wa kushirikisha wadau binafsi katika kuendeleza haya masoko? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa Serikali imesema tangu mwaka 2019/2020 kwamba itatenga shilingi bilioni 2.9 kujenga hayo masoko, nataka commitment ya haya masoko kuanza kujengwa.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, ni kweli ujenzi wa masoko haya umesimama kwa muda mrefu tangu mwaka 2013/2014 wa mwaka wa fedha huo, kama nilivyosema katika jibu la msingi kwamba ilitokana na changamoto za ufinyu wa bajeti.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, Mheshimiwa Innocent Bilakwate, ambaye amekuwa akiendelea kufuatia sana ujenzi wa masoko haya kwa muda mrefu na ndiyo maana tumesema tunatafuta wadau wengine ikiwemo na benki, lakini na wadau wengine ambao tulikuwa tunashirikiana nao katika kujenga masoko hayo na ndiyo maana mwaka wa fedha huu 2021/2022 unaokuja Serikali imetenga angalau shilingi milioni 500. Lengo ni kukamilisha ujenzi wa masoko hayo.

Mheshimiwa Spika, pili, ni kweli commitment ya Serikali ni kuhakikisha tunajenga masoko ya kimkakati ya mipakani kwa sababu tunajua lengo la Serikali sasa ni kuanza ku-access masoko ya nje baada ya bidhaa nyingi au mazao mengi ya kilimo Tanzania kuongezeka. Kwa hiyo, ni lazima tutafute masoko ya nje. Kwa hiyo, ni mpango mkakati wa Serikali kuhakikisha tunajenga masoko ya mpakani, lakini ku-access masoko ya nje kupitia fursa mbalimbali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana; Tokyo International Conference on African Development (TICAD) pamoja na mambo mengine inahusisha nchi zote za Afrika kupeleka vijana kwenda kusoma katika vyuo nchini Japan na kupata uzoefu kwenye kampuni kubwa za nchini Japan kwa lengo kwamba wanapotoka huko waje kufanya uwekezaji hapa nchini kwa kushirikiana na kampuni hizo za Japan. (Makofi)

Kwa nini mpango huu kwa Tanzania umekoma ilhali nchi nyingine za Afrika zinzendelea kupeleka vijana Japan kujifunza? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; vijana hawa ambao tayari tumebahatika kuwapeleka Japan na wamesharejea. Serikali imewatumiaje kwa kushirikiana na kampuni sasa walikopata uzoefu huko Japan kwa ajili ya uwekezaji hapa nchini?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Tanzania na Japan bado wanaendelea na mipango ya kuwapa mafunzo na pia kupata uzoefu wa kazi mbalimbali kupitia taasisi zake nyingi ikiwemo JICA, lakini pia kuna utaratibu maalum baina ya Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa vijana kwenda kupata mafunzo Japan. Kwa hiyo, sio kweli kwamba tumekoma au utaratibu huo umesitishwa kwa sababu hata mwaka 2019 ambayo ni TICAD ya mwisho iliyofanyika nchini Japan baadhi ya maeneo ambayo yaliongelewa ni kuendeleza au kukuza ushirikiano wetu ambapo Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, alikuwepo kule Tokyo moja ya maeneo yaliyoongelewa ni kuona namna gani kutumia vijana wetu katika miradi mbalimbali ikiwemo kuvutia kampuni mbalimbali za uwekezaji nchini kama vile TOSHIBA, ambayo yanaweza kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kielektronic, lakini kuhusu kuwatumia vijana ambao wamepata mafunzo au uzoefu mbalimbali nchini Japan.

Mheshimiwa Spika, Tanzania bado inaendelea kuwatumia vijana hao wengi, lakini pia kwa Taarifa yako na mimi ni mmoja wa vijana hao ambao nimeweza kupata mafunzo Japan na ninaendelea kutumikia Serikali ya Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika sekta ya viwanda. (Makofi)
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa katika majibu ya msingi Serikali imetenga shilingi bilioni moja kwa ajili ya kujenga kongano ya kubangua korosho katika eneo la Masasi, je, ni lini ujenzi huo utaanza? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, baadhi ya viwanda vya kubangua korosho vimekuwa vikinunua korosho katika minada ya awali ili kuwezesha viwanda hivyo kubangua korosho na kuongeza thamani. Hata hivyo, imeonekana pia vimekuwa vikibangua korosho kiasi kidogo na nyingine kuuzwa ghafi. Serikali ina utaratibu gani wa kudhibiti jambo hili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Agnes Hokororo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa kuwa mfuatiliaji sana kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya korosho na hasa katika uwekezaji kwenye viwanda vya kubangua korosho.

Mheshimiwa Spika, kama alivyosema ni kweli Wizara na jukumu la Serikali ni kuhakikisha mazao ya kilimo ikiwemo korosho yanapata soko lakini pia yanaongezewa thamani kwa kuchakatwa katika viwanda vyetu vya ndani.

Mheshimiwa Spika, moja ya changamoto kubwa iliyokuwepo ni kuona korosho hizo zinapata wanunuzi na ndiyo maana tumeanzisha kongano au cluster ya korosho ili kuwahusisha pia na wajasiliamali wadogo waweze kushirikki katika kuongeza thamani ya zao la korosho.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 ilikuwa tumetenga shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kongano hilo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mwaka wa fedha ujao 2021/2022 kazi hii ya ujenzi itaanza kwa sababu tayari fedha hizo zimeshatengwa kwa ajili ya kujenga kongano hilo la wajasiliamali kwa ajili ya kubangua korosho kwenye maeneo ya Masasi na Mtwara.

Mheshimiwa Spika, kuhusu viwanda na kupata korosho katika minada ya awali, ni kweli ni utaratibu ambao Serikali imeuweka baada ya kuona viwanda vingi vinakosa malighafi ambayo ni korosho kwa ajili ya kubanguliwa katika viwanda hivyo. Kwa hiyo, utaratibu sasa kama alivyosema ni kweli kuna minada ya awali ili angalau viwanda hivi visikose kupata malighafi. Baada ya viwanda hivi kununua korosho hatua ya pili ni mnada ambao sasa unashirikisha na makampuni mengine.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kudhibiti viwanda hivi inategemea kwa sasabu kama kiwanda kimeshatosheka na malighafi inayohitajika katika kuchakata korosho basi wana uhuru wa kuuza nje. Kama tunavyojua Tanzania tuna competitive advantage kwa maana ya kuzalisha zaidi korosho kuliko maeneo mengine. Kwa hiyo, tukitosheka sasa katika viwanda vyetu then korosho inayobaki inaweza kuuzwa kwenye minada ya nje ambapo wanaweza kusafirisha nje kama ambavyo wanafanya sasa.
MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, shughuli ya uchimbaji chumvi kwenye kata ya Ilindi imekuwa ni ya muda mrefu na Halmashauri tumepanga mwaka ujao wa fedha tuweze kutenga fedha kwa ajili ya kujenga jengo ambalo sasa tutahitaji tupate mashine kwa ajili ya kiwanda kianze.

Je, Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari aambatane na mimi baada ya Bunge hili ili kwanza akaone eneo lile na ikiwezekana kama alivyosema sasa SIDO waweze kutusaidia kiwanda kile kianze?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali la pili, Serikali imesema kwamba Kata ya Chali na Kata ya Ilindi ni kata ambazo zina chumvi pale, lakini pamoja na ile kumekuwa na tatizo la upatikanaji wa maji kwa sababu ya chumvi Kata ya Ilindi haina maji kabisa kila sehemu maji yana chumvi na Kata ya Chali nayo haina maji ina sehemu moja ambayo ina chanzo cha maji, lakini Serikali imekuwa inaahidi haijatekeleza mradi ule.

Je, Waziri wa Maji yuko tayari vilevile naye aweze kufanya ziara kwenye Kata ya Ilindi na Kata ya Chali ili aweze kuona shida inayowakabili wananchi wa kata hizi kutokana uwepo wa chumvi ya kutosha?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA. Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kenneth Nollo, Mbunge wa Bahi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema lengo la Serikali ni kuona tunahamamisha ujenzi wa viwanda vingi nchini ili kutumia malighafi tulizonazo, kwa hiyo, niko tayari kuambatana na Mheshimiwa Nollo ili twende kuangalia kwanza sehemu yenyewe ilivyo, lakini pia tuweze kupata taarifa sahihi na kuweza kuanza michakato ya kuona namna gani ya kuvutia wawekezaji katika kujenga kiwanda au viwanda katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la pili, ni kweli, kwa sababu kama alivyosema eneo lile lina chumvi kwa hiyo maana yake maji mengi yatakuwa ni ya chumvi. Serikali kupitia Wizara ya Maji najua wana mipango mingi, basi tutashirikiana na Wizara ya Maji ili kuhakikisha tunaona namna gani ya kuwasaidia ndugu zetu wa Bahi ili waweze kupata maji safi kwa ajili ya matumizi ya majumbani.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa nafasi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jimbo la Manyoni Mashariki chumvi inapatikana katika Vijiji vya Mpandagani, Majiri na Mahaka.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wananchi wa vijiji hivyo vitatu ili waweze kuwekeza katika viwanda vidogo vidogo? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Chaya, Mbunge wa Manyoni Mashariki, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli sisi Tanzania tumebahatika kuwa na madini ya chumvi mengi kwa maana ya maeneo mengi, lakini uzalishaji wetu bado ni mdogo, ni wastani wa takribani tani 330,000 ambazo tunazalisha kwa mwaka. Kwa hiyo, kama nilivyosema, lengo la Serikali ni kuona sasa tunahamasisha viwanda vingi ili tuweze kuzalisha zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, na takwimu zinatuonesha kwamba tunaweza kuzalisha mpaka uwezo wa tani milioni moja kwa mwaka. Kwa hiyo tani 330,000 ambazo zipo ni kidogo. Kwa hiyo, jimbo la Mheshimiwa Dkt. Chaya ambao nao pia wana deposit nyingi za chumvi, basi nako pia tutaona namna gani ya kuona sasa tunahamasisha viwanda vingi ili viweze kujengwa katika eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia nimpongeze sana Mheshimiwa Chaya kwa kuwa amekuwa akifuatilia sana suala hili na mimi nimuahidi kwa niaba ya Serikali kwamba tunafanya kila liwezekanalo ili tuweze kuwa na viwanda katika Mkoa huu wa Singida, Jimboni kwa Mheshimiwa Chaya kule Manyoni Mashariki. Ahsante sana.
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo lililopo Bahi linafanana kabisa na tatizo lililopo Mtwara; viwanda vingi vimekufa kikiwemo Kiwanda cha Kubangulia Korosho cha Olam ambacho kilikuwa kinatoa ajira kwa wnanachi wengi wa Mkoa wa Mtwara.

Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua viwanda hivyo?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shamsia Mtamba, Mbunge wa Mtwara Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Mkoa wa Mtwara ndiyo ambao unazalisha korosho nyingi hapa nchini kuliko mikoa mingine na pia kumekuwa na viwanda vingi sana vya kubangua korosho ambavyo kama nilivyosema kabla tulikuwa na viwanda 12 vya Serikali ambavyo baadaye vilibinafsishwa. Lakini kuna vingine ambavyo vimekuwa havifanyi vizuri sana na tumeweza kuvirejesha Serikalini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda hiki cha Olam anachokisema of course kimefungwa kutokana na changamoto mbalimbali, lakini moja ya changamoto kubwa ambazo zilikuwa zinakabili viwanda vyetu ilikuwa ni upatikanaji wa malighafi, kwa maana ya korosho ghafi kwa ajili ya kubanguliwa katika viwanda hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, na moja ya mikakati ambayo Serikali sasa imefanya ni kuona sasa viwanda hivi vinapata malighafi katika mnada wa awali, kwamba viwanda vile vya kubangua korosho vipate malighafi zinazotakiwa, halafu baadaye sasa korosho zinazobakia ziende kwenye mnada wa kawaida.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mikakati inayowekwa na Serikali viwanda vingi sasa vitarudi kufanya kazi kwa sababu vitakuwa na uhakika wa malighafi, lakini pia na mazingira wezeshi ambayo Serikali imeanza kuyaweka ili kuvutia wawekezaji zaidi katika viwanda mbalimbali vikiwemo viwanda vya korosho katika Mkoa wa Mtwara.
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Serikali iliahidi kujenga kiwanda cha kusindika chumvi Ziwa Eyasi, Nyalanja katika Jimbo la Meatu; je, ni lini Serikali itatekeleza hilo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Leah Komanya, Mbunge wa Meatu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, kama nilivyosema katika jibu la msingi kwamba tunahamasisha ujenzi wa viwanda mbalimbali hapa nchini ikiwemo viwanda ambavyo vinachakata chumvi. Katika jimbo la Mheshimiwa Komanya katika Halmashauri ya Meatu Serikali iliahidi kujenga kiwanda kwa ajili ya kuchakata chumvi iliyopo katika Mkoa huo wa Simiyu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Serikali kama Wizara tulipata andiko kutoka kwenye Halmashauri ya Meatu na andiko hilo tunalifanyia kazi. Lakini pia tunajua kwamba kuna taasisi moja ya Nutrition International ambayo yenyewe tayari imeshaanza kuongeza thamani chumvi inayochimbwa pale ambayo kweli soko lake lipo katika nchi za Rwanda na Burundi na maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaambie Waheshimiwa Wabunge kwamba sisi Tanzania ambao ndio tuko kwenye Ukanda huu wa Pwani pamoja na Kenya, ndio wenye deposit kubwa za chumvi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa hiyo, ni vyema sana na sisi kama Serikali tumelitambua hilo kutumia soko hili ili tuweze kuzalisha chumvi nyingi zaidi, tuweze kuuza katika masoko ambayo yanatuzunguka.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tutakamilisha hilo, na Serikali inaendelea kulitekeleza andiko hilo ili angalau tuweze kukamilisha ujenzi wa kiwanda hicho kwa kuwavutia wawekezaji wengi zaidi, lakini pia na taasisi za Serikali ambazo zinaweza zikafanya uwekezaji katika eneo la Meatu. (Makofi)
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; wananchi wa Ludewa wangependa kufahamu kwa kuwa wamesubiria fidia hizi kwa muda mrefu. Je, kwa nini Serikali isitenganishe majadiliano na mwekezaji na suala la fidia ili wananchi wa Jimbo la Ludewa waweze kulipwa fidia mapema?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ningependa kufahamu ni lini Serikali itaanza kutoa elimu ya kuandaa wananchi wanaoathirika na miradi ili waweze kunufaika na miradi hii? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Joseph Zacharius Kamonga, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli katika mradi huu fidia kwa wananchi iliyothaminiwa jumla ya bilioni 11.037 katika majadiliano au katika mkataba ambao tuliingia na kampuni hii Situan Honda ilikuwa yeye kama mwekezaji atakuwa na wajibu wa kulipa fidia eneo hilo ambalo atakuwa analitumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kama nilivyosema baada ya majadiliano na mwekezaji huyu tutaangalia sasa kama tutafikia muafaka maana yake yeye atakubaliana kulipa fidia, lakini utekelezaji wa mradi huu lazima uanze mwaka 2021/2022, aidha tumekubaliana na mwekezaji huyu au hatujakubaliana lakini mradi huu lazima uanze kutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameshaeleleza na ni utekelezaji ambao unaenda kufanyika katika mwaka wa fedha ujao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la elimu katika eneo hili, ni kweli Serikali imekuwa ikiweka fedha kwa ajili ya kuelimisha wananchi namna ambavyo watashiriki katika ujenzi wa mradi huu kwa maana ya local content kwamba wao watafanya nini au watashiriki vipi katika mradi huu mkubwa wa Mchuchuma na Liganga. Kwa hiyo fedha zinatengwa kila mwaka na elimu inaendelea kutolewa kwamba sasa mradi huu ukianza naamini elimu zaidi itatolewa ili wananchi wa eneo hili waweze kushiriki katika utekelezaji wa mradi huu kikamilifu.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Tume ya Ushindani, kama zilivyo mamlaka zote za udhibiti hapa nchini, zina mamlaka ya kimahakama quasi- judicial organs. Je, Serikali haioni kuunganisha ushindani na kumlinda mtumiaji zinafifisha dhana nzima ya ushindani na inafifisha dhana nzima ya kumlinda mtumiaji wa Tanzania?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Dhana ya mtumiaji hapa nchini inaakisiwa kwenye sheria mbalimbali ambazo hazina dhana nzima ya kumlinsda mtumiaji na kuakisi haki nane za mtumiaji kama zilizvyoainishwa na Umoja wa Mataifa. Je, Serikali haioni ni wakati muafaka sasa kutunga sheria, a standalone law ya kumlinda mtumiaji wa Kitanzania?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Oscar Ishengoma Kikoyo, Mbunge wa Muleba Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli FCC au Tume ya Ushindani inasimama kama tume ambayo inahusika kama ya kimahakama, kwa maana ya quasi-judicial organ na ndiyo maana katika majukumu yake yale mawili ya kulinda ushindani pamoja na ya kumlinda mlaji tumeamua sasa ile National Consumer Advocacy Council ambayo ilikuwa ni sehemu, kama section katika taasisi hii ikae sasa independent ili sasa tuwe na uhakika kwamba, mlaji anasimamiwa ipasavyo badala ya kuwa chini ya Tume hii ya Ushindani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, miongoni mwa majukumu ambayo tunaenda kufanya, sasa tunataka tuanze kutunga sera ya kumlinda mlaji; na ndani ya sera hiyo sasa tutatengeneza pia sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya pili, kama nilivyosema, pia ili kumlinda mlaji maana yake sasa tunataka tuwe na sheria ambayo yenyewe moja kwa moja itahakikisha inasimamia kumlinda mlaji tu ikiwa nje ya FCC ambayo inafanya majukumu mawili ya kusimamia ushindani, lakini pia na kumlinda mlaji.
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nashukuru kwa majibu mazuri sana ya Serikali, lakini pia labda nieleze kidogo; mnamo tarehe 1 mwezi wa Kumi mwaka jana 2020 tukiwa katika kampeni Waziri Mkuu aliahidi ujenzi wa soko hili pale Nyakanazi na tarehe 11 mwezi wa Pili wakati akijibu Maswali ya Papo kwa Papo, swali lililoulizwa na Mheshimiwa Neema Lugangira aliahidi pia ujenzi wa soko hili na akataja kabisa ni soko la kimkakati na akataja value yake kama ni 3.5 billion.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye majibu ya Serikali wanasema wanahamasisha Halmashauri ya Biharamulo ili iweze kufanya ujenzi wa soko hili; hili soko limetamkwa, ukisema 3.5 billion kwa Halmashauri ya Biharamulo wajenge soko hili, labda litakaa zaidi ya miaka kumi, kwa sababu uwezo huo hatuna; na ilitamkwa humu ndani ya Bunge: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nipate commitment ya Serikali kwanza nijue financing ya soko hili itafanyika vipi? Sisi uwezo huo hatuna. Kwa hiyo, nipate majibu ya Serikali kama Serikali kuu itafanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu soko hili ni muhimu kwa ajili ya kufungua ukanda wetu na ni soko la kikanda litakalohudumia nchi za Kongo, Burundi, Rwanda na nchi nyingine zote za Jirani: nipate majibu ya Serikali, ni lini ujenzi wa soko hili utaanza? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali ina mkakati na mipango mbalimbali ya kuhakikisha inatekeleza ahadi ambazo viongozi wa Serikali wanaahidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hii pia kumpongeza Mheshimiwa Chiwelesa kwa ufuatiliaji mkubwa anaofanya kwa ajili ya maendeleo katika Jimbo lake la Biharamulo Magharibi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli masoko haya ya kimkakati na hasa masoko ya pembezoni ambayo yako katika mipaka ya nchi za jirani na hasa hizi za Kongo, Rwanda na Burundi ni masoko ambayo yana umuhimu sana kuyaendeleza ili yaweze kuleta maendeleo ya nchi, lakini kuwapatia kipato wananchi wanaokaa katika maeneo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, kupitia programu ya ASDP II ambayo pia imeweka ule mfumo wa O and OD ambao ni fursa na vikwazo kupitia utaratibu huo, Halmashauri zinahamasishwa kuangalia vyanzo mbalimbali vya ku-finance mipango yao, mikakati yao katika kuendeleza sekta ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na TAMISEMI tuna mikakati mbalimbali ambayo pia kupitia humo tunaweza kujenga masoko haya kulingana na fedha zinazvyopatikana. Nakushukuru sana.
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, japokuwa majibu ya Serikali zijaridhika nayo sana, lakini kwa kuzingatia kuwa Kassim Faya Nakapala Mwenyekiti wa Halmashauri na Ebeneza Emmanuel Katibu wa CCM wa Wilaya wako hapa kufuatilia miongoni mwa mambo mengine jambo hili na Diwani wa Kata husika Fatma Mahigi wa Mang’ula “B” kwamba eneo hili sasa limekuwa hatarishi sana ni eneo ambalo lina ekari takribani 250 na akina mama wameshaanza kubakwa. Naomba kuiuliza Serikali maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza Serikali ipo tayari kuweka ulinzi wakati huu inatafuta mwekezaji wa kuwekeza katika Kiwanda hiki cha Machine Tools?

Lakini pili naomba kuiuliza Serikali sasa hivi tunajenga reli ya kisasa ya SGR na hii reli ya kisasa itahitaji mataruma na kadhalika, kwa nini wasikabidhi eneo hili na kiwanda hiki kwa SGR ili iendelee kutumia kuzalisha vifaa vya reli? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Abubakari Damian Asenga, Mbunge wa Kilombero kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza sana ndugu yangu Asenga kwa ufuatiliaji kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo lake na hasa katika sekta ya viwanda na kwa ajili ya ufufuaji wa kiwanda hiki cha Mang’ula Machine Tools.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli eneo hili limekuwa kwa muda mrefu halitumiki kama nilivyosema kwa sababu mwekezaji aliyepewa eneo hili kuliendeleza hajaliendeleza kwa muda mrefu, nichukue nafasi hii kumuahidi kwamba tutashirikiana na Halmashauri kuona namna bora ya kuweka ulinzi ili eneo hili lisiwe hatarishi kwa sasa ambapo bado hatujapata mwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali la pili kama nilivyosema tunaangalia matumizi bora ikiwa ni pamoja na kutafuta wawekezaji ambao wataweza kutumia eneo hili kwa ajili ya kuwekeza viwanda, tuchukue pia hoja ya Mheshimiwa Mbunge kwamba kama wenzetu wa reli ya kisasa watataka kutumia eneo hili kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kutumika katika SGR basi nao tutawakaribisha, ahsante sana.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kuniruhusu kuuliza swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa kiwanda hiki kipo katika eneo la kimkakati kwa sababu kimezungukwa na mashamba ya miwa ama eneo ambalo linalima miwa kwa wingi, na kwa kuwa kulikuwa na mpango wa ku-transform kiwanda hiki kwenda kuzalisha sukari.

Je, Serikali inatoa tamko gani ikizingatiwa kwamba sasa hivi kuna mpango wa kuboresha viwanda vidogo vidogo vya kuzalisha sukari?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Dennis Londo, Mbunge wa Jimbo la Mikumi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli ukanda huu wa Kilombero ni ukanda ambao tunaweza tukasema ni wa kimkakati kwa uzalishaji wa miwa na sukari kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya hapa nchini. Ni kweli ni moja ya azma ya Serikali kuhamasisha au kuvutia wawekezaji wengi katika kuchakata miwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi tunatafuta wawekezaji mahiri ambao watajitokeza kuwekeza katika eneo hili ikiwemo wale ambao watataka kuchakata miwa basi na sisi tutawakaribisha ili kutumia nafasi hiyo katika eneo hili la Machine Tools kama sehemu ya kuwekeza viwanda vya kuchakata miwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tupo tayari na tusaidiane na Wabunge ili tuweze kuwekeza katika maeneo haya kwa umahiri zaidi, ahsante sana. (Makofi)
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa kwenye jibu la msingi Naibu Waziri amesema kwamba magunia ya katani ni ya adimu na yanahitajika sana; na kwa kuwa Mkoani Kilimanjaro ikiwemo Same, Mwanga ni wakulima wazuri wa katani lakini katani hiyo haipati namna ya kuhifadhiwa. Je, ni kwa nini Serikali haioni uharaka sasa kuzungumza na Mohamed Enterprise ambaye pia alimiliki mashamba hayo na akamiliki kile kiwanda ili waweze kutengeneza magunia? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ametutajia kuwa kuna viwanda nane na vitatu ndiyo vipo active lakini magunia haya yanatumika kwenye kuweka kahawa na Mkoa wa Kilimanjaro unalima kahawa na magunia wanaagiza kutoka nje. Je, Serikali inasema nini kuhusu hilo?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shally Raymond, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema ni kweli kuna changamoto katika zao la mkonge kwa maana ya uchakataji. Sasa hivi Serikali inafanya juhudi kwanza kuongeza uzalishaji wa mkonge kwa maana ya malighafi, lakini pia kuhakikisha wazalishaji kwa maana ya wachakataji kwenye viwanda wanaendelea. Ndiyo maana tumesema moja ya kazi tunazozifanya ni kuwapa vivutio maalumu ikiwemo kuwalinda wazalishaji wa ndani.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimueleze tu Mheshimiwa Shally Raymond kwamba huyu mwekezaji METL kwa maana Mohamed Enterprise tayari tumeshaanza kumpa baadhi ya mikataba kwa ajili ya kuzalisha vifungashio kwa maana ya magunia hayo katika zao la korosho. Hii ni mojawapo ya mipango ambayo tunadhani kwa sababu ana uhakika wa soko maana yake atapata mtaji na kuendelea kuzalisha kwenye viwanda hivyo vingine. Kiwanda cha Morogoro tayari kinazalisha tunaamini ataendelea kuzalisha pia katika kiwanda hicho cha Moshi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pili, kama ambavyo nimesema tumeshaanza kuwapa vivutio maalum ikiwemo kuwapunguzia baadhi ya kodi kwa magunia haya ambayo yanaenda kufanya kazi kwenye vifungashio katika mazao ya kilimo. Kwa hiyo, ameanza na korosho tunaamini akiendelea kuzalisha sasa ataenda kwenye vifungashio kwa ajili ya zao la kahawa na mazao mengine. Nakushukuru.
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kupata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa kwenye Jimbo la Same Mashariki, Kata ya Ndungu pamoja na Kata ya Mahore kuna mashamba makubwa ya kilimo cha mkonge lakini anayemiliki mashamba hayo haonyeshi kujali zao lile.

Je, Serikali mnasema nini katika hilo?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anne Kilango Malecela Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema moja ya mikakati ya Serikali ni kujihakikishia kuwa tuna malighafi za kutosha ambazo zitaenda kuchakatwa kwenye viwanda vyetu ambavyo tunavihamasisha kuanza kuvifufa sasa.

Kwa hiyo, moja ya mikakati ambayo tumeshaweka kupitia Wizara ya Kilimo ni kuwapa mikakati au kuhakikisha hawa wakulima wanaendeleza sasa haya mashamba ya mkonge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo hata hawa wa Same nakuahidi na Wabunge wapo hapa tunaendelea kujadiliana nao lakini kuhakikisha wanaenda kufufua mashamba hayo ili aweze kutoa raw material au malighafi kwenye viwanda ambavyo tunaendelea kuvifufua.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
MHE. ASSA N. MAKANIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Nashukuru kwanza kwa majibu ya Serikali juu ya zao letu hili la mchikichi ambalo linazaa mafuta ya mawese. Kwa kweli mchikichi ni zao la kipekee sana Kitaifa na Kimataifa, na sisi pia tunategemea tukiona zao hili likiweza kuwanufaisha wananchi wa Kigoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, tarehe 19 Desemba, 2020 Mheshimiwa Waziri Mkuu alikaa na wadau wa zao hili pale Kigoma ndani ya Ukumbi wa NSSF. Mojawapo ya mambo watu hawa waliomwambia wanahitaji kuona yakifanyiwa kazi ni Bodi ya Mawese na vifungashio maalum.

NAIBU SPIKA: Uliza swali Mheshimiwa Makanika.

MHE. ASSA N. MAKANIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujua sasa ni nini mkakati wa Serikali ulipofikia katika kutekeleza mambo haya ambayo walimwomba Waziri Mkuu yafanyiwe kazi?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Assa Nelson Makanika, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema, moja ya mikakati ambayo tunatekeleza ni kuanza sasa kutatua changamoto hizo, lakini zaidi tumeshaunda timu ya wataalam baada ya maelekezo ya Waziri Mkuu, wakati huo tumeshaunda timu ya wataalam kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na Kilimo ambao sasa wataandaa guidelines kwa ajili ya vifungashio kwenye mazao haya ya kilimo na bidhaa zake, mazao yote ikiwemo ya mawese.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili la bodi, nadhani hili tunalichukua kama moja ya vitu vya kufanyia kazi kama Serikali ili tuweze kuona kama kuwepo kwa Bodi ya Michikichi ni moja ya suluhisho, basi nalo tutalifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Changamoto ya vifungashio ambayo ipo kwenye mawese ni sawasawa na changamoto ambayo ipo kwenye zao la viazi kule Makete, Mbeya na sehemu nyingine na Serikali ilituahidi.

Je, ni lini vifungashio rasmi vya viazi vitapatikana kwa wananchi wa Makete, Mkoa wa Njombe, Mbeya na sehemu nyingine ili tuondokane na changamoto ya lumbesa ambayo imekuwa ikisumbua kwa muda mrefu hadi sasa?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Festo Sanga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema hiyo timu ambayo tumeiunda tumeshawapa deadline, kama ambavyo pia umesema, ndani ya mwezi mmoja waje na mkakati au mpango ambao utaweza kutatua changamoto hii. Kama nilivyosema, si kwa zao moja tu la viazi au michikichi na mazao mengine yote. Kwa sababu changamoto ya lumbesa iko katika mazao mengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lumbesa ni tatizo pale ambapo inazidi vipimo ambavyo vimekubalika katika zao husika. Kwa mfano katika hali ya kawaida tunasema gunia moja liwe kati ya kilo 95 mpaka 105, kwa hiyo zaidi ya hapo inakuwa ni shida. Sasa inaweza kuwa kifungashio ni kidogo kiasi kwamba ikaonekana kama ni lumbesa lakini kiko ndani ya uzito unaokubalika. Hata hivyo, tunachukua changamoto hizi, kama nilivyosema, Kamati hii itakwenda kuweka sasa mkakati au guidelines maalum kwa ajili ya kupata vifungashio specific kwa mazao maalum likiwemo hili la viazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri, Tanzania Bureau of Standards na Bureau of Standards zote ulimwenguni kazi yake ni kulinda na kudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingia nchini na zinazozalishwa ndani ya nchi.

Je, utakubaliana nami kwamba, TBS haipimwi kwa kiasi cha pesa inazoingiza nchini, kutokana na jibu lako ulilonijibu katika swali langu la msingi?

Swali la pili; kuna wale ambao wanashindwa kulipia yale magari, kwa kushindwa huko kulipia yale magari inabidi yale magari mtueleze mnapeleka wapi yale magari? Hamuoni kwamba, Tanzania mnataka kuigeuza kuwa dumping area? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Neema Mgaya, Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Neema kwa ufuatiliaji wa siku nyingi kuhusiana na ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini. Ni kweli, kazi ya msingi ya TBS ni kuhakikisha na kudhibiti ubora wa bidhaa zote zinazoingizwa nchini ndiyo maana tumeamua sasa ili kuwa na ufanisi katika hilo kukagua sisi wenyewe kwa sababu kama nilivyosema katika jibu la msingi, baadhi ya mawakala huko nje walikuwa hawafanyi kazi ipasavyo na malalamiko bado yalikuwa mengi sana kwamba kuna baadhi walikuwa wanaletewa bidhaa ambazo hazina ubora lakini kwa sababu tayari mawakala walikuwa wamethibitisha kwa hiyo maana yake TBS ilikuwa haina namna ya kufanya.

Mheshimiwa Spika, lakini kwa sababu sasahivi tunathibitisha wenyewe, pia tumeshawaambia makampuni yanayoleta bidhaa nchini kuhakikisha wanaleta bidhaa ambazo zina ubora. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Neema kwamba kazi hiyo inafanyika na ndiyo maana tunaamua kujiimarisha sasa ili TBS waweze kufanya kazi hiyo kwa uthabiti.

Mheshimiwa Spika, pili, kuhusu ubovu wa bidhaa au magari yaliyotumika yanayoingizwa nchini, kama nilivyosema mpaka sasa zaidi ya wateja hao 13,968 ambao wameingiza magari nchini hakuna hata mteja mmoja ambaye amelalamika kuhusiana na ubovu wa magari au bidhaa zinazoingizwa. Kwa hiyo, tunaamini sasa mfumo huo utaenda kuboreshwa zaidi kwa maana ya kukagua kwa ubora zaidi na tunawaelekeza wateja wetu kuhakikisha wanaingiza bidhaa kupitia makampuni ambayo tumekubaliana ambayo yanatoa bidhaa hizo kutoka nje. Ninakushukuru.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru.

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Naibu Waziri, sijaridhika na majibu yake. Kwa taarifa rasmi zilizopo ni kwamba, viwanda hivi pamoja na mashamba viko chini ya Msajili wa Hazina. Msajili wa Hazina pamoja na Wizara ya Fedha ndiyo wanaotakiwa kuwalipa wafanyakazi hawa.

Mheshimiwa Spika, naomba kusikia commitment ya Serikali. Je, ni lini wafanyakazi hawa 502 watalipwa na Serikali? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; Viwanda hivi vinaenda sambamba na mashamba yale maua na mbogamboga. Mashamba haya na viwanda ni muhimu sana kwa uchumi wa wananchi wa Mkoa wa Arusha pamoja na sekta hii ya maua na mbogamboga.

Naomba kujua Serikali ina mikakati gani wa kuyafufua mashamba haya? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, napenda kuongezea majibu mazuri ambayo amejibiwa na Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, siyo sahihi kwamba Serikali ndiyo inapaswa kulipa madeni haya, kwa sababu kama ambavyo ameeleza Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwanda kwamba TIB ilipewa dhamana ya kuhakikisha kwamba inarudisha fedha ambazo Kiliflora ilikuwa imekopeshwa. Fedha hii ilirudishwa kupitia mnada ambapo Serikali ilinunua mashamba yale kihalali, lakini hawa ambao wanadai wanadai vitu viwili vikubwa: Kwanza wanadai malimbikizo ya mishahara kwa kampuni ambayo ilikuwa imewaajiri pamoja na mafao.

Mheshimiwa Spika, haya ni madai ambayo yanapaswa kulipwa na mwajiri ndiyo maana hata katika kesi waliyofungua walimshitaki muajiri na Mahakama kupitia Tume ya Usuluhishi wakatoa maamuzi kwamba, hii kampuni iwalipe kwa hiyo, maamuzi tayari yalishatoka kwamba, kampuni hii ndiyo inapaswa kuwalipa hawa wadai.

Mheshimiwa Spika, nawashauri hawa wadai kwamba pengine wangeweza kuwasiliana na vyombo vya dola ili waweze kuwasaidia kuwatafuta hawa wanaowadai waweze kuwalipa mali yao.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na namna ambavyo mashamba haya yataendelezwa kwa sababu, mashamba haya sasa hivi yapo tayari kwa Serikali, kuna mikakati mikubwa ya kuhakikisha kwamba tunaimarisha sekta ya kilimo kupitia rasilimali mbalimbali ambazo zinamilikiwa na Serikali, yakiwepo mashamba haya, lakini kwa kuwa, sasa hivi muda ni mfupi siwezi kueleza mikakati hiyo ambayo iko chini ya benki ya TIB kwa kirefu.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo Mheshimiwa Mbunge nitakupatia baadae. (Makofi)
MHE. NG’WASI D. KAMANI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, la kwanza; kwa kuwa, maelekezo haya yalikuwa ni maelekezo ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, katika hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge hili la 12 ilifanyika tarehe 13 Novemba, 2020 ni mwaka mzima sasa umepita na zaidi. Na kwa kuwa, katika majibu yake Mheshimiwa Waziri amesema wako katika hatua ya mwisho, swali langu; ningependa sasa Serikali itoe commitment ni lini hasa taarifa hii itakuwa tayari na kuletwa hapa Bungeni kwa ajili ya kuanza utekelezaji?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; pamoja na haja ya kuunganisha mifuko hii, lakini changamoto kubwa zaidi ya mifuko hii ni ukosefu wa fedha za kutosha kwa mifuko hii kujiendesha. Sasa ni nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba, mifuko hii inapokuja kuundwa sasa inakabiliana na changamoto hii na inakuwa na fedha za kutosha kwa ajilinya kukidhi uwezeshaji wa wananchi kiuchumi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ng’wasi Damas Kamani, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Ng’wasi kwa kuwa, ameendelea kuwasemea sana vijana katika maeneo mengi, ili kuwatetea na kuwawezesaha katika maendeleo ya nchi hii. Ni kweli kama anavyosema ni karibu zaidi ya mwaka sasa tangu maelekezo au jukumu hili tupewe kwa ajili ya kuunganisha mifuko hii.

Mheshimiwa Spika, lakini mtakumbuka kwamba, mifuko hii imegawanyika katika maeneo tofauti, ipo mifuko ile ambayo inatoa mikopo moja kwa moja, lakini ipo mifuko ambayo ni ya dhamana, mingine ni ya kutoa ruzuku na mingine ni ya uwezeshaji, lakini zaidi yah apo mifuko mingine ni ya sekta binafsi. Kwa hiyo, Serikali inafanya tathmini ya kutosha kujiridhisha ili tunapokuja kuona mifuko ipi iunganishwe iwe na tija kweli.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niwahakikishie Serikali inaliangalia kwa umuhimu sana na tukikamilisha taarifa hiyo, kama nilivyosema tutaileta hapa Bungeni ili tuweze kuendelea kuboresha mifuko hii.

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili la ukosefu wa fedha za kutosha; ni kweli baadhi ya mifuko imekuwa na changamoto ya kuwa na bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuhudumia wahitaji au kuwawezesha wanaokopa.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema na sisi tulikubaliana ndiyo maana tumesema tunataka kuunganisha mifuko hii ili iweze kuwa kwanza na fedha za kutosha ile ambayo inatoa huduma zinazofanana. Lakini pili mkakati wa Serikali ni kuona kuendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kwa mfano ile kwenye halmashauri ambako tunatoa 10% maana yake mapato yakiimarika yakiongezeka maana yake hata ile 10% itakuwa ni fedha za kutosha zaidi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hiyo ni mikakati ya Serikali kuhakikisha fedha pia zitaendelea kutengwa kwenye mifuko mingine ambayo itakuwa imeunganishwa hapo baadaye ili waweze kuwa na bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuhudumia wananchi.
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza kwenye Wizara ya Viwanda na Biashara. Kwa kuwa mifuko hii imeonekana haina tija ya kutosha kwa sababu zinatolewa fedha taslim, ni kwa nini sasa Serikali isije na mpango mbadala wa kutoa facilities (vitendea kazi) na kuwawezesha vijana badala ya kuwapa fedha taslimu ambazo pia zimekuwa hazirudi kwenye Serikali lakini pia haziwafikii vijana wa kutosha. Ni kwa nini sasa wasilete utaratibu wa kuwapa vitendea kazi ili waweze kufanya kazi na tuone kitu kinafanyika?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nusrat Hanje Mbunge kama ifuatavyo. Ni kweli kumekuwa na changamoto nyingi kama ambavyo nimesema kwa maana ya kutokuwa na fedha za kutosha mahitaji ya wananchi ambao wanataka kukopeshwa au kupata fedha kutoka kwenye mifuko hii. Lakini lengo la Serikali ni lile lile kuimarisha na kuwasaidia kwa ukaribu zaidi wananchi katika kuwawezesha.

Mheshimiwa Spika, moja ya mifuko ambayo inatoa mikopo hii ni NEDF kupitia SIDO pia tumekuwa tukiwapa ujuzi lakini na wengine vitendea kazi. Lakini sasa baada ya kuwa na lengo hili la kuona namna gani kuunganisha mifuko hii naamini taarifa hiyo ndiyo itakuja na utafiti rasmi wa namna gani ya kuboresha ikiwemo kama ni kuwasaidia vitendea kazi hasa vijana ambao wanakuwa wanakopa fedha hizo au wengine na kutokutimisha lengo la mikopo hiyo nakushukuru.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kama Mheshimiwa Waziri alivyosema kwenye jibu lake la msingi Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa, ambayo inaongoza kwa uzalishaji wa maziwa hapa nchini. Sio hayo tu maziwa yanayozalishwa katika Mkoa wa Arusha ni maziwa yenye viwango na ubora wa hali ya juu. Inasikitisha sana kuona bado Serikali hatujaweza kuwasaidia wafugaji na wazalishaji wa maziwa katika Mkoa wa Arusha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika lita alizotaja Mheshimiwa Waziri hapa, lita milioni 30 ni lita milioni sita tu, ambazo zinakwenda kuchakatwa kwenye viwanda vyetu ni sawa na asilimia 20 tu. Asilimia 80 ya maziwa yanayozalishwa katika Mkoa wa Arusha yote yanapotea kwa sababu hayapiti kwenye viwanda kwa ajili ya kuchakatwa. Hii hapa inasababishwa na ukosefu wa maeneo ya ukusanyaji wa maziwa haya kwa ajili ya kupeleka katika viwanda vyetu. Swali langu kwa Serikali; je, Serikali haioni umuhimu wa kuweka mipango madhubuti kwa ajili ya kuongeza hizi collection points hususani kwenye ngazi za chini ambazo uzalishaji ndio mkubwa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; katika Mkoa wa Arusha kuna Taasisi za Utafiti kama CAMARTEC na TEMDO. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongezea uwezo hizi taasisi kwa ajili ya kuendeleza sekta ya viwanda vidogo vidogo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Zaytun Seif Swai, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mpango madhubuti na ndio maana kila mwaka tunahakikisha tunaongeza bajeti kupitia Wizara husika, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, lakini pia na Wizara nyingine ili kuhakikisha tunaboresha sehemu za kukusanyia maziwa kwa maana ya collection centres.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni kweli Taasisi za CAMARTEC na TEMDO ni Taasisi ambazo zinasaidia sana, teknolojia ambazo zinakwenda kuwasaidia vijijini kwa maana ya wafugaji na wakulima. Kila mwaka tunaendelea kuwaongezea bajeti ili waendelee, kuzalisha mashine au teknolojia rahisi na stahiki kwa ajili ya kusaidia wakulima wa vijijini ikiwemo wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Spika, parachichi ni moja ya mazao saba ya kimkakati ambayo Serikali imeyatangaza, zao la pili kwa Mufindi Kusini ni chai.

Mheshimiwa Spika, naomba kufahamu commitment ya Serikali katika kusaidia wakulima ambao majani yao yanamwagwa wanakosa soko na viwanda havichukui.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ziko tetesi kwamba kiwanda hicho kimeuzwa atatusaidia Mheshimiwa Naibu Waziri kama atakuwa na majibu ipi commitment ya Serikali juu ya maslahi ya wafanyakazi kama kweli kiwanda hicho kimeuzwa Mufindi ya Kusini?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali madogo mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile, Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nishukuru na nimpongeze Mbunge mwenzangu kutoka Mufindi ambaye anafuatilia sana maendeleo ya wilaya hiyo.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema nia ya Serikali Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha tunaweka mazingira wezeshi kwa ajili ya maendeleo ya viwanda na hasa tukizingatia kuwa sekta binafsi iwe kiongozi kwa ajili ya kufikia uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Spika, moja ya mikakati ya kukwamua maendeleo katika sekta ya viwanda ni kuhakikisha viwanda vilivyopo vinaendelea, lakini pia kwa ufanisi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu viwanda vya parachichi; viko viwanda viwili katika mkoa wa Iringa; Kibidula Avocado Packiging Industry ambayo inafanyakazi vizuri, lakini pia na Kiwanda cha GBRI, Kampuni ya GBRI pale Iringa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Unilever kwa maana ya Kampuni ya Chai, sisi kama Wizara tumeshapata notice ya kuuzwa kwa kampuni hiyo na taarifa hizi ziliifikia Tume ya Ushindani mwaka jana mwezi Desemba kwa maana ya tarehe 17 Desemba, 2021 na hatua zinazochukuliwa kwa kampuni ambayo inauzwa huwa kwanza ni kutangaza notice ya siku 14 kwa wale ambao ni wadau au wanahusika katika mchakato wa kuuza. Kwa hiyo siku zile 14 ziliisha na hakukuwa na mtu yeyote mwenye maoni au malalamiko.

Mheshimiwa Spika, lakini pili sisi kama Serikali kupitia Tume ya Ushindani tunaendelea sasa kufuatilia hatua stahiki za uuzwaji wa kampuni hiyo. Kwa ruhusa yako labda nifafanue kidogo kama utaruhusu kampuni ya Unilever ina kampuni tanzu ya Ekaterra ambayo ndiyo inasimamia sekta ya chai, sasa wanauza kwa Kampuni ya Puchin Bidco ambayo yenyewe itachukua eneo hilo. Kwa hiyo, kwa sasa tumeshaiagiza FCC waendelee kufuatilia na kama kuna watu wenye malalamiko kuhusiana na mauziano haya walete maoni au malalamiko kwenye Tume ya Ushindani.

Mheshimiwa Spika, lakini tatu kuna masuala ya maendeleo ya wafanyakazi nayo yatazingatiwa katika mchakato huo, nakushukuru.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsante; zao la parachichi limekuweko nchini miaka nenda rudi na hata mikoa mingine likiwa ni chakula cha mbwa; hadi majuzi Serikali ilivyoanza kuona kwamba ni zao la kibiashara.

Mheshimiwa Spika, Serikali inatuambia nini sasa kujenga kiwanda cha kuchakata parachichi katika mkoa wa Kilimanjaro ambapo maparachichi mazuri sana yako kule Rombo, Mwika, Kahe na kwingine ambapo yanatupwa tu hadi leo?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shally Raymond, Mbunge kutoka Kilimanajro kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema mwanzo azma ya Serikali ni kuhakikisha tunaongeza ujenzi wa viwanda kwa kuweka mazingira wezeshi. Kilimanjaro ni moja ya maeneo ambayo yanalima kwa wingi sana parachichi hivyo basi ombi letu ni kuhakikisha na sisi kama wawekezaji tuanze kutumia fursa, kwanza tunaweka miundombinu kupitia SIDO changamoto kubwa tuliyonayo ni collection centers kutunza katika vyumba vya ubaridi matunda yale ili yaweze kuchukuliwa na wenye viwanda. Kwa hiyo kupitia SIDO tutaenda kuhakikisha sasa kunakuwa na ofisi katika ngazi za Halmashauri au Wilaya ili kupunguza upotevu wa mavuno ya matunda yanaposubiriwa kupelekwa kwenye viwanda ambavyo tayari viko nakushukuru sana.
MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, lakini napenda kumuuliza maswali yangu mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia soko lenye uhakika na tija nchini?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; je, Serikali ina mpango gani wa kuwaunganisha akinamama kwenye mitandao ya wafanyabiashara duniani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mwantumu Dau Haji, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Mwantumu kwa vile ambavyo anawasemea sana akinamama ili kuhakikisha nao wanajikomboa katika kufanyabiashara katika mazingira mazuri. Lengo la Serikali, kwanza ni kuhakikisha wafanyabiashara wote wakiwemo akinamama wanazalisha bidhaa zao katika ubora. Kwa hiyo, la kwanza tunalofanya kuhakikisha tunawapa mafunzo ili kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye tija.

Mheshimiwa Spika, pili, kupitia taasisi zetu tunawaunganisha kwenye masoko mbalimbali kupitia maonesho ambayo yanaandaliwa na TANTRADE. Pia kwenye kuhakikisha wanaingia kwenye mtandao wa wafanyabiashara duniani kwa kupitia chamber ya wafanyabiashara wanawake Tanzania Women Chamber of Commerce tumekuwa tukiandaa kwa kushirikiana na Serikali, ziara kwenye Maonyesho ya Kimataifa ikiwemo ile iliyofanyika mwaka 2018 kule China ili angalau kuwapa uelewa mpana kwa wafanyabiashara wetu akinamama katika masoko ya kimataifa.

Mheshimiwa Spika, pia zaidi sasa tumeanzisha biashara mtandao kupitia TANTRADE na Posta ili iwasaidie kufanya biashara kwenye mtandao na hivyo kujiongezea kipato. Nakushukuru sana.
MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Serikali ililipa eneo la Viwanda na Uwekezaji pale Bunda Mjini kwa muda mrefu na wananchi wakahama kwenye eneo lile, lakini leo wameanza kurejea kwenye eneo lile. Ni nini mpango wa Serikali katika kulitumia eneo lile?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Robert Maboto, Mbunge wa Bunda Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli eneo lile ambalo lilo pale, lipo chini ya EPZA kwa maana ya maeneo ya uwekezaji huru kwa ajili ya mauzo nje. Serikali tunaendelea kutafuta fedha ili tuweze kuyaendeleza maeneo yote ambayo yapo chini ya EPZA likiwemo eneo hili la Bunda Mjini.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutalitekeleza au tutaanza kulifanyia kazi hivi karibuni katika eneo hilo la Bunda Mjini. Nakushukuru.
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo nyongeza. Tuna Mifuko mingi sana ya uwezeshaji wanawake na vijana kiuchumi na mifuko hiyo imekuwa kwenye Wizara mbalimbali ndani ya Serikali: -

Kwa nini Serikali sasa isifikirie angalau kuwa na mifuko miwili ambayo itatosheleza mahitaji ya walengwa kwa maana ya wanawake na vijana? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Cecilia Paresso, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kumpongeza Mheshimiwa Paresso kwa sababu anauliza swali la msingi sana kuona namna ambavyo tunaweza kupunguza wingi wa Mifuko hii ambayo inahudumia wananchi kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Spika, tunalipokea wazo hili na Serikali ipo kwenye michakato kuona namna gani ya kuunganisha mifuko inayotoa huduma zinazofanana ili kuweza kuifanya iwe na tija kwa ajili ya kuwasaidia wananchi ikiwemo akina mama, vijana na walemavu. Kwa hiyo, tunachukua mawazo yake, nasi tunaendelea kuyafanyia kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. BAHATI K. NDINGO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Naomba kuiuliza Wizara, kutokana na athari za UVIKO-19 nchi yetu pia imekumbwa na ongezeko la mfumuko wa bei: -

Je, Wizara imefanya tathmini gani kuona athari ambazo wafanyabiashara wamepata; na wana mkakati gani kuhakikisha hali ya mfumuko wa bei nchini unakwenda kurekebishwa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bahati, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli sote ni mashahidi kwamba kumekuwa na athari kubwa kutokana na janga hili la ugonjwa wa UVIKO-19, katika bidhaa mbalimbali kwa maana ya kupanda bei. Serikali inafanya jitihada za makusudi kuona namna gani tunasaidia viwanda na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ndani ya nchi pamoja na kuweka vivutio na kupunguza gharama za wale ambao wanaingiza bidhaa mbalimbali zinazotumika kutoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, nadhani mtaona kwa makusudi Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuangalia hili, aliweza kuangalia pia eneo la mafuta ambayo ni sehemu nyeti sana inayoongeza gharama za bidhaa kwenye usafirishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, pamoja na mambo mengine tunaangalia kwa namna gani tutasaidia wazalishaji ili waweze kuzalisha kwa bei nafuu, na pia mnyororo mzima wa usafirishaji wa bidhaa za ndani na zile zinazotoka nje ya nchi. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana; pamoja na majibu ambayo nina uhakika hayatawafurahisha wala kuwaridhisha watu wa Korogwe naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza, jambo hili ni la muda mrefu sana na muwekezaji huyu hana uwekezaji wowote ambao ameufanya kwenye eneo lile, wapo wafanyakazi wa zamani wanadai, lakini pia wapo wawekezaji wengi wanajitokeza wanakitaka kiwanda hiki.

Nataka Serikali iniambie ni lini sasa zoezi la kurudisha kiwanda hiki rasmi itakamilika ili kuwezesha uwekezaji mwingine?

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili; kwa kuwa kuna malalamiko ya madai waliokuwa wafanyakazi kwenye eneo lile na kiwanda hiki ni muhimu kwa uchumi kwa watu Korogwe. Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari baada ya Bunge hili, Wizara ya Viwanda inayosimamia Sera, Ofisi ya Msajili wa Hazina na watu wa Maliasili waliokuwa wanakisimamia kiwanda hiki, tufanye ziara kwenda Korogwe tukazungumze kule namna nzuri ya kukikwamua kiwanda hiki kiweze kuwasaidia watu wa Korogwe? Nakushukuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Thimotheo Mnzava, Mbunge wa Korogwe Vijijini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Thimotheo Mnzava kwa vile ambavyo anafuatilia sana maendeleo ya jimbo lake hususan katika sekta ya viwanda.

Mheshimiwa Spika, ni kweli jambo hili limekuwa la muda mrefu kama alivyosema tangu mwaka 2018 na kimsingi kama unavyojua kwa viwanda vyote ambavyo vilikuwa vimebinafsishwa kulikuwa na mikataba ambayo lazima Serikali iwe na uhakika inavyofanya urejeshwaji wake ili kusiwe na matatizo mengine ya kuingia utata kati ya wawekezaji hawa. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba taratibu za kisheria zikikamilika mapema iwezekavyo uwekezaji mpya katika kiwanda hiki utafanyika.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la lake pili, nimuahidi Mheshimiwa Mbunge sisi kama Wizara ya Viwanda na Biashara, Serikali ina nia ya dhati kuhakikisha tunakwamua au tunaendeleza sekta ya viwanda. Tutaambatana baada ya Bunge hili tutawasiliana ili tuweze kufanya ziara na kuongea na wananchi wa Korogwe Vijijini ili tuone namna gani ya kusaidia kufufua kiwanda hiki muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo la Korogwe Vijijini. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa nafasi hii.

Mheshimiwa Spika, kiwanda kinachotajwa hapo malighafi yake inatoka katika Shamba la Misitu Shume ambayo ipo Lushoto na ninavyo fahamu mimi kiwanda hiki kwa sasa Msajili wa Hazina amekikodisha kwa mwekezaji mdogo wa pale Korogwe.

Je, kwa nini wasiboreshe mkataba ulipo sana na mwekezaji huyu mdogo ili angalau kuweza kuwasaidia wananchi wa Korogwe na Lushoto kwa ujumla?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika nakushukuru sana, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Rashid Shangazi, Mbunge wa Mlalo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali wakati inaangalia namna ya kuweza kukifufua kiwanda hiki ilikodisha kwa mwekezaji anayezalisha nguzo ambazo kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge zinatoka Lushoto.

Kwanza nia ni kuona kile kiwanda hakiharibiki kwa maana miundombinu ile iweze kuendelea kuwa bora. Lakini kama nilivyosema kwa sababu bado hatujamaliza mchakato wa kukirudisha rasmi Serikalini kwa hiyo hatuwezi kumpa mwekezaji mwingine mpaka tukamilishe taratibu za kisheria ili tusiwe na migogoro mingine na wawekezaji ambao wataingia katika kiwanda hivho. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ASYA MWADINI MOHAMMED: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Kwa mujibu wa majibu ya Mheshimiwa Waziri ni dhahiri kwamba Tanzania hakuna kiwanda kinachochakata vigae na ukizingatia vigae vingi tunaingiza kwanza chupa za pombe na mengineyo, lakini tunazalisha na hapa nchini maana yake uchafuzi wa kimazingira unaendelea. Nini mkakati wa Serikali kuanzisha kiwanda cha kuchakata vigae nchini?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; je, Serikali haioni sasa kupunguza kodi kwa bidhaa zote zinazochakatwa na taka ngumu ili kuweza kuwavutia wawekezaji waweze kuwekeza nchini lakini pia na kuyalinda mazingira yetu?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asya Mwadini Mohamed Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli bado hatuna viwanda vya kuchakata vigae kwa maana ya mabaki, lakini nia ya Serikali ni kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kuvutia wawekezaji ambao tunaamini wataendelea kuwekeza katika maeneo tofauti ikiwemo hili ambalo Mheshimiwa Mbunge amelitaja, kwa hiyo tunaendelea kutafuta na kuweka kuwavutia wawekezaji katika eneo hili.

Mheshimiwa Spika, lakini la pili ni kweli Serikali tunaendelea kufanya juhudi na kuona namna ya kuweka vivutio maalum katika maeneo mbalimbali ikiwemo hili la kupunguza kodi katika maeneo ya uchakataji au urejeshaji taka ambazo kwa kweli zinaharibu sana mazingira hapa nchini. Kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira tunaendelea na juhudi za kuhakikisha tunatunza mazingira kwa kuvutia wawekezaji wanaopunguza taka ambazo zimezagaa mjini nakushukuru.
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, ahsante, ni miradi mingapi ya uwekezaji kati ya hiyo 294 imeanza?

Lakini pili, je, Serikali haioni sababu ya kuanzisha Idara au Kitengo Maalum cha Ufuatiliaji na Ushawishi?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Issa Ally Mchungahela Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kweli katika miradi hii 294 sababu ni swali la takwimu naomba tutafute takwimu zaidi za uhakika na nitampa Mheshimiwa Mbunge ni miradi mingapi ambayo imetekelezwa kati ya hii 294.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili tayari tuna vitengo vya ufuatiliaji kwa maana ya Monitoring and Evaluation katika Wizara, lakini pia hata katika taasisi zetu ikiwemo Kituo cha Uwekezaji cha TIC; na kwa taarifa tu katika miradi ambayo imetekelezwa mwaka 2021/2022 miradi zaidi ya 1,200 imeshafanyiwa ufuatiliaji kwa maana ya kuhakikisha kujua kama inatekelezwa na kwa kiwango gani. Nakushukuru sana.
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, Wilaya ya Rory ana Tarime moja ya faida ambayo tunaipata kuwepo mpakani kati ya Tanzania na Kenya ni pamoja na unafuu wa bei ya bidhaa ambazo zinazalishwa maeneo ya mpakani.

Swali la msingi hapa lilikuwa linauliza Wizara haioni kuna umuhimu sasa wa kuwasaidia wale wachuuzi wadogo ambao unakuta bidhaa chache, kwa mfano mifuko miwili ya cement, mifuko mitano ya sukari ambayo wakikamatwa wakati mwingine hupewa kesi za uhujumu uchumi au hunyang’anywa pikipiki zao au kutaifishwa bidhaa zao zile chache. Mheshimiwa Waziri haoni kuna umuhimu wa kuwasaidia hawa wafanyabiashara wadogo ili kutengeneza mazingira rafiki angalau waweze kufanya biashara hizi bila usumbufu wanaopata?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili Wilaya ya Rorya tayari tuna eneo ambalo tumelitenga kwa ajili ya kuweka viwanda kwa mahitaji na muktadha wa bidhaa hizo hizo ambazo wananchi wetu wanavuka kwenda kuzifata Kenya.

Je, Wizara ina mpango gani wa kuhakikisha angalau inazungumza na wawekezaji wa bidhaa hizi hizi wanazozalisha Kenya kujenga kiwanda, kuja kuwekeza maeneo ya Rorya ili tuwasaidie hawa wananchi wanaovuka maeneo ya mpaka kwenda nchini Kenya? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Chege kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli moja ya mikakati ambayo tunayo Serikali ni kuona namna gani tunawasaidia wachuuzi au wafanyabiashara wadogo wadogo, wajasiriamali katika mikoa ya mipakani ambao wanafanya biashara kati ya nchi na nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya maelekezo ambayo tulishawaelekeza maafisa wetu wa taasisi zote zinazohudumia wafanyabiashara mipakani ikiwemo TRA, TBS na nyingine kuhakikisha kwanza wanatoa elimu kwa wachuuzi hawa wajasiriamali namna ya kufanya biashara kati ya nchi moja na nyingine. Lakini zaidi waendelee kuwasaidia kwa maana ya kuwapa muda fulani kama angalizo wakati wanaendelea kujifunza namna ya kufanya biashara kati ya nchi hizi mbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala la pili nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba moja ya mikakati yenu ni kuona tunawavutia wawekezaji katika kujenga viwanda maeneo ya mipakani ikiwemo katika eneo la Rorya. Kwa hiyo, hilo tutalifanya na tutachukua kwa uzito mkubwa nimwakikishie Mbunge tutalifanya hilo tutashirikiana naye, nitawasiliana naye baada ya kikao hiki. Nakushukuru sana.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru; ni kweli kumekuwa na kero kubwa sana kwa hawa wafanyabiashara wadogo wanaokutwa wanafata bidhaa upande wa pili Kenya. Ni kwa nini sasa Serikali isielekeze task force iache huu utaratibu wa kufukuzana na hawa wafanyabiashara wadogo ambapo wakati mwingine inapelekea vifo kwa kuwagonga ili kuwepo na utaratibu wa kiofisi kama mtu amekwepa kodi basi anafatiliwa kuliko wanavyofanya sasa hivi?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Esther Matiko kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali yetu ya Awamu ya Sita chini ya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan imeshasema na tumeshaelekeza kwamba tuwahudumie wafanyabiashara na hasa tukiwa na lengo la kujenga sekta binafsi yenye nguvu kuhakikisha kwamba wanafanya biashara zao vizuri bila kero. Kwa hiyo, nilichukue hili ili tuone kama kweli shughuli hizo zinafanyika, kero hizo au task force hizo ziweze kukomeshwa mara moja kuhakikisha wanawasaidia badala ya kuwa-harass wafanyabiashara.
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa Serikali ilitueleza kwamba kuna viwanda vya kuanzia 3,500,000 na katika Mkoa wetu wa Kagera kina mama wamekuwa wakikopeshwa mikopo isiyo na tija.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwakopesha hivyo viwanda badala ya pesa ili kutengeneza ajira nyingi mkoani kwetu Kagera? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Oliver Semuguruka, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Kagera kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa sababu amekuwa akifatilia sana kuhusiana na wafanyabiashara wakina mama wajasiriamali katika Mkoa wa Kagera. Nimshukuru sana kwa kazi kubwa anayoifanya Mheshimiwa Oliver. Lakini kuhusiana na mitaji hii ni kweli wajasiriamali wadogo hasa akina mama tunataka kupitia Shirika letu la Viwanda Vidogo kuwakopesha viwanda au teknolojia rahisi za kufanyia biashara zao badala ya kuwapa fedha ambazo wakati mwingine zinaweza kutumika katika malengo yasiyokusudiwa.

Kwa hiyo, moja ya mikakati ni hiyo kuwapa viwanda ili iwasaidie kuzalisha bidhaa ndogondogo pia waweze kukidhi mahitaji ambayo wameomba katika mikopo hii. Nakushukuru sana.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi.

Je, ni upi mpango wa Serikali kupitia Wizara hii ya Uwekezaji kuangalia yale makundi ya asilimia 10 ambayo hayana vigezo vya kukopeshwa. Kwa mfano wanaume ambao wamepita umri wa vijana kwa ajili ya kuwawezesha, lakini pia kwenye asilimia 10 zipo baadhi ya halmashauri hazina uwezo kukidhi makundi yote asilimia 10. Ipi kauli ya Wizara hii kuwawezesha makundi hayo ambayo yanabaguliwa?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Condester Sichalwe, Mbunge wa Momba kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mbunge kwa kufatilia kuhusiana na asilimia 10 za fedha zinazotengwa kwenye halmashauri zetu ili kuwasaidia akina mama, vijana na wenyeulemavu katika kufanya biashara zao ndogo ndogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya mikakati ya Serikali sasa ni kuona makundi haya kwanza yanapata elimu ya ujasiriamali kupitia wataalamu wetu wa Maafisa Biashara katika halmashauri pia kwa kushirikiana na Shirika letu la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) ili waweze kutimiza malengo ambayo wamekusidia katika mikopo hiyo. Lakini zaidi tutaangalia namna ya kuwezesha zile halmashauri ambazo kidogo zina mapato machache ili nao waweze kutosheleza mahitaji katika kuwakopesha vijana na akina mama ambao wanahitaji mikopo kwa ajili ya kufanya biashara zao katika halmashauri zetu na majimbo yetu. Nakushukuru sana.
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishukuru Serikali kwa majibu yake mazuri, lakini pia ninalo swali moja la nyongeza; kwamba, Uvinza ndipo kunapopatikana malighafi ya kutengeneza saruji. Sasa nataka nijue Serikali imejipanga vipi kuhakikisha kwamba, kiwanda hicho kinajengwa ili wananchi waweze kupata ajira ya muda mfupi, lakini na muda mrefu na ili tuweze kukamata soko la DRC na Burundi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nashon William, Mbunge wa Kigoma Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Mbunge kwa kufuatilia. Amekuwa anafuatilia sana kuhusiana na ujenzi wa kiwanda katika Wilaya ya Uvinza, lakini mkakati wa Serikali ni kuendelea kuboresha miundombinu wezeshi ili kuvutia wawekezaji zaidi katika ujenzi wa viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi ni mashahidi sasa hivi Kigoma itaenda kufunguka kwa sababu Mheshimiwa Rais wetu, Samia Suluhu Hassan, anaunganisha gridi ya Taifa ya umeme katika Mkoa huo. Maana yake hii ni miundombinu wezeshi ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya ujenzi wa viwanda. Kwa hiyo, tunaamini kwa uboreshaji wa miundombinu hii wezeshi, pamoja na barabara tutavutia wawekezaji zaidi ambao watakuja kujenga pia katika Wilaya ya Uvinza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tunaendelea kufanya juhudi za makusudi ili kuvutia wawekezaji zaidi ambao watajenga viwanda katika ukanda huo wa ziwa ili kushika soko katika nchi za jirani, kama alivyosema. Nakushukuru sana.
MHE. MOHAMED SAID ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri aliyonipatia kwenye swali langu hili la msingi, maswali yangu ni kama ifuatavyo.

Kwa vile amesema kwamba Serikali ina mpango wa kuondosha vizuizi vya biashara. Je, Serikali ina mpango gani wa kuviunganisha vyombo ambavyo vinazuia biashara kuwa na kasi kwa mfano, ZBS na TBS kuweza kuunganika na ikiwa mzigo umekaguliwa Zanzibar iwe imetosha ama mzigo ikiwa umekaguliwa Tanzania Bara iwe imetosha. (Makofi)

Swali la pili, kwa vile tunataka kuongeza mapato ya wananchi pamoja na Serikali; Je, sasa Wizara yako haioni ni wakati wa kukaa na Wizara ya Fedha ili kuiruhusu biashara kufanyika wakati wa siku za Jumapili kama zilivyo border nyingine ambazo zinafanyakazi siku Saba kwa wiki? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mohamed Said Issa Mbunge wa Konde, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli moja ya mikakati ambayo tunaiweka ni kuona namna gani tutaboresha kwa kuunganisha baadhi ya taasisi ambazo zinafanyakazi zinazofanana kati ya Tanzania Bara na Zanzibar ikiwemo hizi za ZBS na TBS. Lakini kwa sababu haya ni mambo ya Kimuungano naomba tuendelee kuyafanyia kazi ili tuweze kuona namna gani tutaendeleza mashirikiano kati ya mamlaka hizi mbili na mamlaka nyingine ambazo zinashirikiana katika kufanyakazi zinazofanana kati ya pande hizi mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ni kweli moja ya vitu ambavyo tunavifanya katika kuhakikisha tunaongeza mapato ni kuboresha au kurahisisha ufanyaji biashara kati ya Zanzibar na Tanzania Bara. Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara tunachukua ushauri huu ili tuweze kuona namna ya kukaa na wenzetu Wizara ya Fedha na Mipango kuboresha siku ambazo ni za sikukuu au Jumapili au weekend ambazo wakati mwingine kunakuwa na changamoto ya ufanyajikazi ili tuweze kuwahudumia wafanyabiashara vizuri waweze kufanya shughuli zao katika siku hizi za weekend.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. (Makofi)
MHE. CONSANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali iliahidi kwamba baadhi ya viwanda vitafufuliwa kwa ubia wa ushirika na mifuko ya jamii. Sasa ninataka kujua ahadi hiyo imefikia wapi.

MheshimiwaNaibu Spika, swali langu la pili, hivi karibuni nchi yetu ilikumbwa na uhaba mkubwa wa mafuta ya kupikia. Malighafi ya mafuta ya kupikia ni pamba ambayo ipo nyingi kwenye eneo hilo.

Je, ni mkakati gani sasa ambao Serikali inao kuhakikisha kwamba kiwanda hicho kinafanya kazi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Constantine Kanyasu Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza ni kweli, ni jitihada ya Serikali kuona viwanda vyetu vinafanya kazi/vinafufuliwa moja ya kimkakati ilikuwa ni kuhusisha mifuko yetu ya jamii kuona nayo inashiriki katika kuzalisha au kufufua kiwanda hiki cha Kasamwa, lakini kutokana na stadi iliyofanywa na wenzetu wa NSSF ilionekana kwamba wakati ule bado haina tija kwa wao kuwekeza kulingana na malengo ya mifuko hii ya jamiii. Kwa hiyo, hilo bado linafanyiwa kazi kuona kama kutakuwa na tija ili kuwekeza katika kiwanda hiki cha Kasamwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili mkakati wa Serikali ni kweli, moja ya maeneo ambayo Serikali imeweka mkazo ni kwenye sekta ya kilimo kuona tunaboresha kilimo ili tuwe na malighafi muhimu kwa ajili ya kuzalisha mafuta ya kula, mojawapo ni mafuta ambayo yanatokana na zao la pamba kwa maana ya mbegu za pamba. Kwa hiyo, uzalishaji utaongezeka na hivyo tunaamini viwanda hivi moja ya changamoto ilikuwa ni malighafi kwa hiyo vitakwenda kupata malighafi, ambayo itatumika pia kuzalisha pamoja na bidhaa nyingine na mafuta ya kula ambayo yanatokana na mbegu za pamba. Ninakushukuru.
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Pwani unaongoza kwa zao kubwa la korosho. Je, nini mkakati wa Serikali kufufua Kiwanda cha Korosho TANITA Kibaha?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo ambayo pia tunalenga katika kuhakikisha tunaongeza thamani ni kwenye zao la korosho. Viwanda vingi ambavyo vilikuwa havifanyi kazi, mkakati wa kwanza ni kuona vile inavyowezekana kurudisha katika mikono ya Serikali ili tutafutie wawekezaji wengine lakini pia pili, ni kuvutia wawekezaji wapya kuwekeza katika viwanda vipya ambavyo navyo vitaongeza kazi ya kuchakata zao la korosho ili kuziongezea thamani katika Mikoa ya Pwani na Mikoa ya Nyanda za Kusini ambao wanalima zaidi zao la Korosho. (Makofi)
MHE. CONDESTER MICHAEL SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Nimesikiliza majibu ya Serikali siyo mbaya, ni hivyo hivyo. naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba na kwamba wanatambua uzalishaji ambao upo vijijini Je, Serikali sasa haioni kwamba kuna haja ya kubadilisha Sheria ya Vilevi na Vileo (The intoxication Liquors Act) ambayo ni ya mwaka 1968 na marekebisho yake ya mwaka 1978. Hauni kuna haja; kwamba, sheria hii ikibadilishwa inaweza ikaendana na mazingira tuliyonayo sasa kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia wananchi waliopo kule vijijini? Kwasababu Sheria iliyopo sasa hivi inaongelea sana mambo ya leseni.

Mheshimiwa Spika, swali la pili kulingana na Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi kusisitiza uchumi wa viwanda Je, Wizara hii haioni sasa ipo haja kabisa ya kuwapa SIDO jukumu la kuwasaidia wananchi hawa wanawake wa vijijini na sehemu zote, kuwapa elimu, kupata takwimu halisi ili waweze kuwasaidia kuboresha hizo pombe zao za kienyeji na ziweze kuwa kwenye viwango na ziweze kuuzwa nje ya nchi? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Condester Sichalwe Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli, na ninadhani ni mawazo mazuri, kwamba tuangalie namna ya kupitia sheria zetu za vileo na vilevi ili iweze kuendana na uhalisia wa sasa. Nadhani hii kama Serikali tuichukue. Na kwasababu ni wajibu wetu kama Wabunge kutunga sheria hizi basi na sisi tutalifanyia mchakato ili tuweze kuona uhalisia kama kuna uhitaji wa kubadilisha sheria hizo.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni kweli kupitia SIDO Serikali inaboresha baadhi ya mitambo lakini pia na kuboresha mikopo kwa ajili ya wajasiliamali mbalimbali ikiwemo wanawake. Na sasa labda tutaangalia mahsusi kwa ajili ya hawa wazalishaji wa pombe za kienyeji ambao huenda watataka teknolojia mahsusi au mfuko maalum ili waweze kuwezeshwa kuzalisha pombe ambazo zina viwando badala ya kuendelea kuzalisha hizi pombe ambazo tunaita ni za kienyeji. Nakushukuru.
MHE. JULIANA D. MASABURI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu hayo ya Serikali ambayo bado hayaridhishi napenda kuiuliza Serikali; tangu nimeandika hili swali najua kuna shirika la TBS najua kuna Tume ya Ushindani; lakini bidhaa fake hasa vipodozi, vyakula vimezidi kuzalishwa nchini na kuingizwa kwa kasi ya juu. Naomba majibu sahihi ya Serikali nini wanapanga kudhibiti bidhaa fake? (Makofi)
NAIBU WAZIRI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Juliana Didas Masaburi Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli changamoto ya bidhaa fake ni ya kudumu. Na kwa namna ambavyo tunajua lazima tuendelee kudhibiti. Serikali inaendelea kufanya juhudi mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, mojawapo ya changamoto tuliyonayo ni upungufu wa watumishi katika taasisi zetu hizi za TBS na FCC. Hata hivyo tunaendelea kuboresha ili kupata watumishi wa kutosha. vilevile tunaweka nguvu au mkazo kwenye elimu kwa umma, kwasababu bidhaa fake au bidhaa hizo au vipodozi hivi vinavyoingizwa ni kwasababu ya mahitaji ambayo Watanzania wanahitaji. Kwa hiyo, tukiwapa elimu sahihi maana yake vitakosa soko au uhitaji wa bidhaa hizo. Kwa hiyo tutaendelea kutoa elimu pamoja kuimarisha zaidi kwa kuhakikisha tunapata watumishi wa kutosha ili wasaidie kudhibiti mianya ambayo inatumika kuingiza bidhaa hivi fake na vipodozi ambavyo vinakosa sifa za kutumika kwa ajili ya kudhibiti soko la Tanzania.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Mheshimiwa Spika, kwenye swali la msingi la vipodozi fake kweli ni janga la Kitaifa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba vipodozi vinapendezesha (beautifying) lakini kazi kubwa ya vipodozi ni za kiafya katika ngozi na mwili. Swali langu la msingi ni kwamba, ni lini Serikali itahamisha bidhaa za vipodozi kutoka Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara kwenda Wizara ya Afya ambapo kuna wataalam wa vipodozi hivyo ili tuweze kulinda afya ya jamii? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Florent Kyombo (Mb) kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika ni kweli vipodozi ni sehemu ya bidhaa ambayo ipo kwenye kundi la dawa. Sasa, kwasababu ni ushauri Serikali tunalichukua ili tuweze kuona namna gani tutaliweka hili suala liweze kutumiwa kwenye sehemu sahihi kama sio Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, nakushukuru.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwakuwa tumekuwa tukishuhudia kila mara vitu hivyo au vipondozi hivyo, vyakula hivyo vikichomwa katika maghara na kwa gharama kubwa sana. Je, ni nani anayegharamia, kwasababu yule aliyenyang’anywa tayari ameshafilisika?
NAIBU WAZIRI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shally Raymond (Mb) kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli, kwamba kwa utaratibu anayetakiwa kugharamia uharibifu wa bidhaa hizo fake au vipodozi ni yule ambaye ameingiza, kwa maana ya aliyekiuka sheria ya uingizaji wa bidhaa, kwasababu zidhaa zote ambazo zinaruhusiwa kuuzwa katika masoko ya Tanzania hasa vipodozi lazima viwe vimesajiliwa. Kwamba, kama vimeingizwa kinyume na sheria hiyo yeye ndiye atakayetakiwa kulipa ili kuhakikisha anafidia gharama hizo za kuharibu vipodozi, nashukuru.
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, nataka tu kujua Serikali ilipofanya tafiti imegundua ni kwanini wafanyabiashara wengi hasa wadogo wadogo wanafunga biashara zao hivyo kupelekea hali ya uchumi kudolora hususan Mkoani kwetu Mtwara?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, nataka tu kujua mkakati wa Serikali ukoje kuhakikisha unawaunganisha wananchi wa mkoa wa Mtwara na fursa ya masoko katika nchi ya Comoro?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Tunza Issa Malapo Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, moja ya mikakati tunayoifanya ni kuhakikisha tunafanya tafiti mbalimbali. Moja kwa kuwashirikisha taasisi za umma lakini pia na wadau wa maendeleo ambao wanafanya tafiti hizo kuhusiana na hali ya uchumi lakini pia na namna ya kufanya biashara nchini.

Mheshimiwa Spika, moja ya matokeo ambayo yanaonesha pamoja na kwamba kuna udolora wa wafanyabiashara wadogo lakini ni changamoto za maeneo. Ndiyo maana Serikali imekuja na mpango wa kuwapanga katika maeneo mahususi ili wawe na maeneo ambayo ni mazuri na rafiki kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ambao mara nyingine wakikaa maeneo ambayo si rafiki kunakuwa na ile changamoto zak ukimbizwa na baadhi ya mgambo na taasisi zingine ambazo wafanyabiashara wadogo wanakuwa wamevamia na kufanya biashara zao katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, ni kweli tunaendelea kutafuta, moja ya changamoto yao ya mitaji ambayo tunaifanyia kazi ili wafanyabiashara wadogo wadogo waweze kupata mitaji kwa njia rahisi. Lakini zaidi pia tutaendelea kuwatafutia maeneo ya kufanyia biashara katika Mkoa wa Mtwara kama ulivyosema lakini pia na maeneo mengine nchini, ili wafanyabiashara wadogo kwanza wapate mitaji lakini pili wawe na maeneo mahususi ya kufanya biashara bila kusumbuliwa.
MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa michikichi mkoani Kigoma, viwanda vidogo vidogo havitoshelezi kuchakata mafuta na bidhaa zinazotokana na zao la chikichi: Je, Serikali ina mikakati gani ya kuleta viwanda vya kati na vikubwa mkoanii Kigoma (secondary and tertiary industry)? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili: Serikali ina mipango gani ya kutenga maeneo ya viwanda vya kati na vikubwa katika wilaya zote za Mkoa wa Kigoma? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kavejuru Felix, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza namshukuru sana Mheshimiwa Kavejuru kwa ufuatiliaji mkubwa kuhusiana na zao la chikichi na mnyororo mzima wa thamani katika Mkoa wa Kigoma.

Mheshimiwa Spika, ni kweli jitihada zilizopo ilikuwa ni kuanza na viwanda hivi vidogo ambavyo vilikuwa vinakidhi mahitaji wakati ule uzalishaji wa michikichi ulipokuwa katika hali ya chini kwa maana ya malighafi. Sasa juhudi kubwa zimefanywa na Serikali, tunaamini tuna malighafi ya kutosha, kwa hiyo, mipango ya Serikali sasa ni kuanza kuvutia wawekezaji wakubwa ili waweze kuwekeza katika viwanda vitakavyochakata mnyororo mzima wa thamani wa mchikichi katika Mkoa wa Kigoma.

Mheshimiwa Spika, hii ni pamoja na kuboresha miundombinu. Waheshimiwa Wabunge ni mashahidi kwamba sasa tumeshapata umeme wa grid ya Taifa katika Mkoa wa Kigoma ambayo ilikuwa ni moja ya kikwazo, pia barabara zinaboreshwa ambavyo ni vitu muhimu sana kwa ajili ya kuvutia wawekezaji. Kwa hiyo, tunaendelea kuweka mazingira wezeshi na bora kwa ajili ya uwekezaji katika mikoa ya pembezoni ikiwemo Mkoa wa Kigoma.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kutenga maeneo ya uwekezaji kwenye kilimo pia na maeneo ya kujenga viwanda, kwanza nimshukuru sana kwa ushauri wake. Sisi kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo tunaendelea kutenga maeneo ya kilimo kwa ajili ya mashamba makubwa. Pia niwaombe Serikali za Mikoa na Halmashauri ili waendelee kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji, kwa sababu hii ni endelevu, tunatakiwa tuwe na maeneo sahihi na yenye miundombinu wezeshi ili wawekezaji wakubwa wanapokuja kuwekeza viwanda hivi wasihangaike tena kupata ardhi ambayo wakati mwingine inakuwa mgogoro mkubwa kwa ajili ya kuweka viwanda hivi vikubwa.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Serikali ina mkakati gani wa kujenga kiwanda cha kukamua mchuzi wa zabibu ili kuweza kuondoa adha ya wakulima wa zabibu wa Mkoa wa Dodoma wanaotembea na mabeseni barabarani wakitembeza zabibu na kuiuza bila faida yoyote? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kunti Majala, kuhusiana na sekta ya kilimo hasa kwenye zao la zabibu.

Mheshimiwa Spika, tayari tumeshaanza juhudi mbalimbali za kusaidia kuchakata zabibu ili ziweze kuwa katika hali ya mchuzi wa zabibu anaosema, ambapo tayari kuna wadau mbalimbali wameshaanza kuchukua, wakiwemo kiwanda cha Jambo ambao wapo Shinyanga. Vilevile wengine wameshaanza kuchukua zabibu hizo ambazo naamini wadau hawa ambao tumewahamasisha watapunguza adha ya kutembea kuuza zabibu ambazo hazijachakatwa ambazo wakulima wenzetu wa Mkoa wa Dodoma wanahangaika nazo. Nakushukuru.
MHE. HAMIS M. MWINJUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pia nashukuru kwa majibu ya Serikali kupitia kwa Naibu Waziri ambayo yananipeleka kwenye maswali mawili madogo ya nyongeza. La kwanza, wakati huu ambao taratibu mbalimbali zinaendelea za kutafuta masoko kwa ajili ya machungwa, lakini pia kutafuta uwekezaji kwa ajili ya kutengeneza viwanda cha kuchakata matunda: Serikali haioni sasa kuna umuhimu wa kutengeneza vituo vya ukusanyaji, uhifadhi na uuzaji wa machungwa ili kuwapa uhakika wa sehemu ya kuuzia machungwa yao wananchi wa Wilaya ya Muheza na pia kuepusha idadi kubwa ya machungwa yanayoharibika kila mwaka kwa kukosa uhifadhi mzuri?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Hamis Mohamed Mwinjuma, Mbunge wa Muheza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia sana kuhusiana na soko la machungwa katika Mkoa wa Tanga Wilayani Muheza. Niseme kweli, machungwa ya Muheza ni ya aina yake kwa maana ya ladha; ni matamu kuliko; kwa hiyo, unaweza ukayatenganisha kuliko ya maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali imeanza mpango wa kujenga maghala ambayo yatakuwa kama vituo vya kukusanyia matunda ili kuhakikisha matunda hayapotei. Siyo maghala tu, yatakuwa ni maghala ambayo yatakuwa na vyumba vya ubaridi (cold rooms) ambavyo vitawasaidia wakulima kutunza mazao yao, yakae kwa muda mrefu wakati wanatafuta masoko.

Mheshimiwa Spika, moja ya jitihada kama nilivyosema ni kujenga viwanda vya kuchakata matunda ya machungwa, lakini tunavutia viwanda vidogo na vikubwa. Tumeshaanza kujenga viwanda vidogo kupitia vikundi vidogo vidogo ambavyo vitaongeza thamani. Pia tumeshaanza kuongea na wawekezaji wakubwa ambao wataenda kuwekeza kwenye eneo la Muheza kwa kuwapa vivutio maalum maana wengi wanataka kuwekeza mjini badala ya mashambani ambako ndiko kwenye machungwa. Kwa hiyo, tutaweka mkakati maalum wa kuwavutia ili wapate vivutio vya kuwekeza katika Mkoa wa Tanga hususan Muheza. Nakushukuru.
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza. Pamoja na soko kutokuwa na uhakika, kumeibuka utamaduni wa wanunuzi kufika mpaka mashambani, wao ndio wanapanga bei na aina ya vifungashio ambapo kwa kiwango kikubwa inamuumiza mkulima.

Je, Serikali inasema nini kuhusiana na hili?

Swali la pili, je, Wizara ipo tayari sasa kwenda kukaa na wakulima hawa kusikiliza changamoto zao lukuki walizonazo ili waweze kupata ahueni na kuondokana na changamoto hiyo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Paresso kwa kufuatilia hili la mazao hasa kwenye zao la vitunguu. Ni kweli kumekuwa na changamoto hiyo ya wanunuzi wengi na wakati mwingine hata wa nje kufika kwa wakulima kule vijijini. Tumeshatoa maelekezo mara nyingi hasa kwa wenzetu wa halmashauri tuendelee kushirikiana kuhakikisha tunaendelea kujenga collection centers, yaani maeneo ya kuuzia kama masoko. Maeneo hayo ndiyo maalum kwa wakulima ili waweze kuuza kwa tija na kwa vipimo.

Mheshimiwa Spika, pia nichukue nafasi hii kusema kwamba Wakala wa Vipimo ambao wako chini yetu waendelee na waende eneo hili maalum wakaone changamoto hii iliyopo ili kukomesha ufungashaji wa mazao yetu kwa njia ambayo siyo sahihi. Maana tumeelekeza mazao yote yauzwe kwa vipimo, siyo kwa vifungashio. Pia kulikuwa na hii habari ya lumbesa, naamini tulishasema na ninarudia tena, kuhakikisha wanauza kwa vipimo na tuhamasishe halmashauri waweke collection centers ili wakulima wapate bei yenye tija kwa mazao yao.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kwenda kukagua; nitaenda, na niagize WMA waende kwanza, nasi tutaenda kuona changamoto hasa katika eneo hili Bonde la Eyasi ili tuweze kutatua changamoto hii ambayo nadhani ni sehemu zote nchini na tunaendelea kufanyia kazi hilo. Nakushukuru sana.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya swali la nyongeza. Mheshimiwa Waziri, kumekuwa kuna shida sana ya masoko kama alivyosema kwenye swali la msingi, lakini kumekuwa na matangazo ya uwongo redio wakisema zao la vanilla linauzwa kwa kilo moja Shilingi milioni moja: Unatoa katazo gani kwa watu wanaowadanganya wakulima katika zao hili? (Kicheko)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwa na matangazo ambayo wakati mwingine yanaleta taharuki na hasa kwenye hili zao la vanilla kwamba linauzwa bei kubwa na wakati mwingine nadhani hii imekuwa kama zile biashara za kwenye mitandao. Kwa sababu hiyo, Serikali na kwenye maeneo mahususi kwa mfano maeneo ya Njombe, kumeshatokea utapeli huo.

Mheshimiwa Spika, tumeshaelekeza wenzetu kwenye halmashauri waone namna gani kweli hawa ambao wanadhani wanataka kusaidia wakulima, washirikiane na halmashauri kuona kweli hilo zao kama ni vanilla au mazao mengine kweli yanaweza kustahili kulimwa lakini pia kuwa na njia sahihi kuhamasisha ulimaji huo badala ya kuwa na biashara mtandaoni ambazo mara nyingi ni utapeli.

Mheshimiwa Spika, naomba niseme, kwa kweli sisi kama Serikali tunaendelea kufuatilia matapeli wanaotumia biashara mtandao kutapeli wakulima au wananchi kutoa fedha ambazo mwisho wa siku haziwezi kuwa na tija kama ambavyo wamelenga. Nakushukuru.
MHE. KHALIFA MOHAMED ISSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza, kwa niaba ya Mheshimiwa Mohamed Said Issa.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; je, utekelezaji wa makubaliano hayo umefikiwa kwa kiasi gani?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, Serikali ipo tayari leo kutoa tamko kuwa bidhaa zilizotambuliwa na moja katika mashirika mawili hayo hutumika nchi nzima bila ya utambuzi wa Shirika lingine lolote nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Khalifa Issa Mohamed, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa makubaliano haya umeshaanza na unaendelea kama nilivyosema kwenye maeneo yale yote matano kwa maana viwango vile tunavyokubaliana vinatekelezwa, lakini pia na bidhaa zote zinatambuliwa katika pande zote mbili.

Mheshimiwa Spika, kwenye swali la pili, ndio hii moja ya vitu ambavyo tumesisitiza katika sehemu ya tano, kwamba lazima bidhaa zote ambazo zimethibitishwa na ZBS au na TBS kwa upande wa Bara zinatambuliwa katika pande zote mbili.

Mheshimiwa Spika, hii si kwa Tanzania tu ni kwa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki kwamba hata ukienda kwenye bidhaa ambazo zimetoka kwenye nchi hizi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo taasisi zao za udhibiti wa viwango zimethibitishwa, zikija huku kwetu zinatambuliwa. Kwa hiyo, si kwetu tu kwa maana ya Zanzibar na Tanzania Bara, lakini pia hata Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nakushukuru sana.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kutokana na majibu ya Serikali, kwa kuwa suala la kutoa elimu kwa wananchi limekuwa likifanyika mara kwa mara, lakini halijawa na tija ya kutibu tatizo la lumbesa. Ni upi mkakati wa Serikali kusimamia Sheria ya Vipimo, Sura 340, kuhakikisha kwamba suala la lumbesa linaisha kabisa nchini?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, Serikali haioni ni wakati muafaka kati ya Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda na Biashara kuanzisha selling point ili kuwekwe mizani katika maeneo hayo ili kudhibiti suala la lumbesa nchini kwenye mazao ya viazi, vitunguu na mazao mengine ambayo yamekuwa msiba kwa muda mrefu kwa mkulima ambaye amekuwa akinyonywa kwenye Taifa letu?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Festo Sanga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli moja ya changamoto tuliyonayo ni usimamizi wa kutekeleza hii Sheria na mkakati uliopo ni kupitia wenzetu Serikali za Mitaa kwa maana TAMISEMI, kuhakikisha wanasaidia kwanza maeneo yale ambayo kuna mauzo kuwe na mizani ambayo itatumika kuhakikisha wale wote wanaonunua wanapima au wananunua kwa uzito.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ambalo nalo linaendana na hili ni kwamba, hiyo ndiyo mikakati ya Serikali ambayo tunataka sasa tuhamasishe wananchi kujiunga katika vyama vya msingi au kuimarisha ushirika katika maeneo ya mashambani ili waweze kuwa na uwezo au nguvu ya ku-bargain. Moja, ili wapate bei nzuri na pili, ili sheria hii iweze kutumika ni lazima wawe na maeneo ya kuuzia.

Kwa hiyo, mpango uliopo kupitia Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara vile vile Kilimo na wenzetu wa TAMISEMI ni kuona tunawa-organize sasa wakulima wale wawe na maeneo mahususi ya kuuzia mazao yao ili tuwapatie uwezeshaji wa kuwa na vipimo, kwa maana ya mizani lakini pia wawe na nguvu ya kudai bei stahiki ya mazao yao. Nakushukuru.
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Pamoja na uwepo wa hiyo sheria Mheshimiwa Waziri aliyotuambia, lakini ni dhahiri kwamba watumishi tulionao hawatoshi, lakini pili miundombinu siyo rafiki. Huko vijijini ambako ndiko wakulima waliko, wakulima wetu wa mazao mbalimbali nchini wamekuwa wakiuza kwa lumbesa kwa sababu tu kwanza mtu anayeratibu ni wafanyabiashara kwa maana ya madalali, ndio wanaopanga wakulima wetu wauzaje na kwa uzito upi. Je, Serikali haioni sasa muda umefika kwa wafanyabiashara wa mazao kutoa maelekezo wanapokwenda vijijini kununua mazao, waende na mizani na wananchi wetu wapewe maelekezo pia na elimu kwamba wasiuze kwa mfumo wa lumbesa?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kunti Majala kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tuna changamoto ya watumishi katika maeneo yote ikiwemo hili la Wakala wa Vipimo kwa maana ya wanaosimamia mambo ya vipimo. Kwa kweli kazi kubwa inafanyika kwa kushirikiana na halmashauri kuhakikisha tuna washirikisha Maafisa Biashara ambao ndio wanaowasadia na pia Maafisa Ugani ambao wako katika maeneo hayo ili kuhakikisha tunawalinda wakulima katika maeneo yote.

Mheshimiwa Spika, sio katika lumbesa tu, kwa sababu lumbesa kama alivyouliza muuliza swali la msingi kwenye viazi, lakini pia hata katika maeneo mengine ambako wanatumia vitu kama ndonya, kangomba, bakuli na vitu kama hivyo. Kwa hiyo tunajitahidi kuhakikisha Maafisa Biashara na Maafisa Ugani hawa wanawasaidia wakulima ili kuhakikisha kwamba wanakuwa na maeneo ya kuuzia ambako watawasaidia.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kuwaelekeza Maafisa Biashara ambao tumekwishawapa nafasi ya kuwa wafanyakazi pia katika Idara za Uwekezaji, Viwanda na Biashara, wasaidie na wasimamie hili suala ili tuondokane na unyonyaji huu unaotumika wa kunyonya wakulima kwa kununua katika vifungashio au bila kutumia vipimo katika maeneo ya mashambani ili tuondokane na masuala haya ya lumbesa.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, inasikitisha sana, nashukuru sana ametoa majibu ya swali hilo. Hata hivyo inasikitisha sana kwamba mifuko hii inajikita kwenye majiji na kwenye manspaa ambazo zina uwezo mkubwa kwa zile asilimia zao 10 kutoa mikopo kwa vijana, wanawake na walemavu. Wamejikita huko sasa, ni ile ile dhana kwamba watu wanaohitaji zaidi ni vijijini lakini hii mifuko hailengi wale wa vijijini.

Je, Serikali haioni umuhimu wa kuhakikisha kwamba mifuko hii inabadilisha misimamo yake au mitizamo yake na kulenga zaidi Halmashauri kwenye wilaya za vijijini? Hilo ni la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, je, Serikali haioni umuhimu wa kuunganisha mifuko hii ili kupunguza gharama za uendeshaji na pia kutoa usawa zaidi na ufanisi katika kutoa mikopo yake?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Kimei, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katika moja ya mikakati ambayo tunaifanya Serikali ni kuona namna gani mifuko hii ya uwezeshaji itawasaidia zaidi wananchi walioko katika maeneo ya vijijini na ndio maana moja ya mifuko hii au pesa zinazotolewa kwa wajasiliamali ile asilimia 10 ina gusa katika Halmashauri zote ambazo zinagusa pia vijijini. Pia zaidi tutaangalia na hii mifuko mingine ikiwemo ya NEDF, SELFU na TAFF iweze kufika kule vijijini kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameshauri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la pili tayari tumeshaanza na kazi hiyo inafanyika, kuona namna ya kuunganisha mifuko inayotoa fedha au inahudumia shughuli zinazofanana na taarifa hiyo tayari inakamilika iko kwenye hatua za mwisho kuona mifuko ipi itaunganishwa ili kupunguza wingi wa mifuko hii, ambayo inahudumia watu wanaofanana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inaonesha kusua sua kwa ufanisi wa mifuko hii, na ni tangu Bunge la Kumi na Moja tumekuwa tukizunngumza kuhusu kuunganisha mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, mifuko ya ujasiriamali.

Je, ipi kauli ya Serikali, kwa kutumia muda mrefu kiasi hiki, wanasemaje kuhusiana na kuharakisha mchakato kwa sababu ni fedha za Serikali zinazoenda huko?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Nusrat Hanje, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema Serikali tumeshaanza na tumeshafika hatua ya mwisho. Naamini katika mwaka wa fedha ujao kutakuwa na taarifa kamili ya nini mfuko huu pia utapunguzwa. Kwa sababu tuna mifuko zaidi ya 72 lakini kati ya hiyo tisa ni ya sekta binafsi, 63 ndiyo ya Serikali. Kwa hiyo, tunaanza kwanza hii ya Serikali 63 tuone namna gani tunapunguza ili iweze kuwa na tija kama ambavyo Bunge lako limeendelea kushauri, nakushukuru.
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuwa usemi wa majadiliano unaendelea na umekuwa wimbo wa muda mrefu; na kwa kuwa mradi huu nji muhimu sana kwa Taifa letu ikiwa ni sambamba na kupata ajira 5,000 zilizo rasmi na zisizo rasmi 25,000 na vile vile tunatambua kwamba, baada ya miaka 15 makaa ya mawe yatakuwa hayana soko tena duniani kutokana na teknolojia zinazoendelea.

Je, Serikali inaweza ikatupa muda specific time lini mtamaliza majadiliano na muwekezaji huyu ili tuende awamu nyingne na mradi huu, uweze kutekelezeka kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Neema William Mgaya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mtakumbuka wakati tunawasilisha Taarifa ya Kamati kwenye Bunge lako tumeeleza kwa kirefu jinsi ambavyo Serikali imechukua jitihada za maksudi kuhakikisha tunakamilisha mapema majadiliano haya, lakini changamoto ilikuwa kwa upande wa wawekezaji hawa ambao tuliingia nao mkataba kabla. Hata hivyo tunaamini katika mwaka wa fedha ujao (2023/2024), In Shaa Allah, tutaweza kukamilisha kwa sababu tayari tuko kwenye hatua nzuri zaidi ili tuweze kufikia hatma ya majadiliano haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Ninalo swali dogo tu la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mpango huu wa blueprint ulitengeneza changamoto mbalimbali ambazo ziko kwenye Sheria mbalimbali na ucheleweshaji katika kuushughulikia imekuwa ni issue. Wizara ina mpango gani sasa kwamba makosa mapya hayajirudii kwenye sheria zinazotengezezwa mpya?
NAIBU WAZIRI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Napenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Olelekaita kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli moja ya changamoto katika mambo yaliyokuwa kwenye andiko hili la blueprint ilikuwa ni Sheria na Kanuni zipatazo 88 ambazo zilikuwa na changamoto mbalimbali. Mpaka sasa zaidi ya Sheria na Kanuni 40 zimeshafanyiwa kazi ambayo ni takribani asilimia 45 ya utekelezaji ya mpango huu wa kuboresha mazingira ya wafanya biashara nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tunaendelea kupitia na kuhakikisha Sheria na Kanuni ambazo bado ni kinzani kwa ajili ya kuweka mazingira bora ya ufanyaji biashara nchini tunaendelea kuzitatua na kupitia Bunge lako Tukufu ninaamini mengi tutaendelea kuyarekebisha kadri ya muda unavyokwenda, kwa sababu pia tunavyotatua baadhi ya changamoto kuna changamoto zingine mpya zinaibuka. Kwa hiyo, Serikali itaendelea kutatua kadri ambavyo hali halisi itakavyokuwa inajitokeza.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na maelezo aliyoyatoa Mheshimiwa Naibu Waziri, tumekaa hapa tunaongea lakini huko Halmashauri zetu wanatunga Sheria Ndogondogo ambazo zilizopo nyingi zinakwenda kupunguza attraction ya wawekezaji hasa wa ndani.

Je, ni mkakati gani wa sasa ambao Wazira inao kuhakikisha inaratibu zoezi hili ili liweze kuhakikisha kwamba Wawekezaji hasa wa ndani wanaweza wakafanya kazi bila ya kuwa na Sheria Ndogondogo hasa za tozo?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Napenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Deo Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli moja ya changamoto tulizonazo kwenye utekelezaji wa mradi wa blueprint au MKUMBI ni katika ngazi za Halmashauri. Wizara tumeshaanza kuliona hilo na moja ya utekelezaji tumeanzisha madawati au kitengo mahususi kinachoshughulikia masuala ya viwanda, biashara na uwekezaji katika ngazi ya Halmashauri. Tunaamini kitengo hiki kitasaidia moja, kuhakikisha tunaharakisha utekeklezaji wa yale maboresho ambayo tumeyafanya, lakini pili kuwaelimisha wenzetu wa Halmashauri ili wawe wanatunga Sheria au Kanuni ambazo si kinzani na nia hii ya Serikali ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara hapa nchini. Nakushukuru. (Makofi)
MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ni nchi ya 141 kati ya 190 kwa ugumu wa ufanyaji biashara. Majibu ya Mheshimiwa Waziri yananipa mashaka juu ya commitment ya Serikali juu ya kutumiza haja ya reforms katika regulations zetu. Hivi ni kwa nini hiyo taarifa ya utekelezaji msiilete Bungeni ili tuweze kuijadili, badala ya kuipeleka kwenye Kamati peke yake, tuleteeni Bungeni hapa tuijadili, tuna usongo na hali hii sisi, tunataka tumalize haya matatizo. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara napenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Abbas Tarimba Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira, ni moja ya Kamati ambazo zimetungwa na Bunge lako Tukufu. Kwa hiyo namini kwa utaratibu ule ule kwamba Kamati hizo zinawasilisha Bunge hili na kwa maelekezo yenu nadhani inawezekana kama kutatakiwa kuleta hapa, basi ni maelekezo ya Bunge lako Tukufu ili tuweze kufanya hivyo.
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mpaka sasa hivi Blueprint inaonekana ni document ya Serikali na watu hawaimiliki. Ni yapi sasa mafanikio mpaka sasa hivi tangu tufanye reforms kwenye blueprint, Serikali imefanikiwa nini kiuchumi ili at least sasa tuanze kuona value for money na hayo marekebisho ambayo tumeyafanya?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, napenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Nusrat Hanje, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafanikio yako mengi kama ambavyo nimesema. Moja ya maeneo ambayo yalikuwa yana angaliwa ni zile Sheria zilizoanishwa kwenye mpango ule au kwenye document hiyo, ambayo kimsingi iko public na kila mtu anaweza ku-access na sio ya Serikali. Ni zaidi ya sheria na kanuni 88, ambazo katika hizo sheria na kanuni 40 zimeklwisha ratibiwa na kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo katika mambo ambayo yalikuwa yameibuliwa ni mwingiliano kati ya taasisi za Serikali moja wapo mi TBS na TMDA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mengi yameweza kurekebishwa; lakini moja ni uanzishwaji wa mifumo ambayo ilikuwa na changamoto kwa wafanyabiashara kwa mfano Wafanyabiashara wakitaka kulipia ilikuwa ni changamoto kubwa. Kwa hiyo mifumo 42 imerekebishwa, moja wapo tunaona ni hii GEPG ambayo ni malipo ya Serikali na yameboreshwa na hii imepunguza sana manung’uniko kwa wananchi kupanga foleni Kwenda kulipa katika taasisi mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi katika utekelezaji huo ndiyo tunaona kwamba tumeanzisha idara hizi na vitengo ambavyo vitakuwa mahususi sasa kusikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara maeneo yote. Kuanzia wizarani kuna kitengo hicho lakini pia tunaenda kwenye halmashauri tunaweka kitengo ili kuhakikisha tunapunguza manung’uniko na changamoto ambazo wafanyabiashara wa Tanzania walikuwa wanakutana nazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo taarifa hizo au kitabu hicho au document hiyo ni ya wananchi wote. Kwa hiyo popote utakapotaka unaipata na taarifa hizi kama ulivyosema kama ukihitaji tutaileta hapa Bungeni; lakini Kamati yako ya Viwanda, Biashara na Mazingira wamekwisha ipata na wameijadili na mambo mengi yanaendelea kurekebishwa.
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwanza kabisa nimshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kufuta riba kwa mkopo wa asilimia 10 kwa wanawake.

Mheshimiwa Spika, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa wanawake wengi ni waaminifu sana katika masuala ya kurudisha mikopo, Je Serikali ina mpango gani wa kuongeza muda wa marejesho? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili kwa kuwa mahitaji ya mikopo ni mengi kwa wanawake, vijana na walemavu. Je, Serikali au Wizara ina mpango gani wa kuongeza asilimia 15, asilimia Saba wakopeshwe wanawake, asilimia Tano wakopeshwe vijana, asilimia Tatu watu wenye ulemavu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Esther Midimu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue nafasi hii kumshukuru sana na kumpongeza Mheshimiwa Esther Midimu kwa kufuatilia kwa makini sana kuhusiana na maendeleo ya wanawake na hasa kushiriki katika shughuli za kiuchumi kupitia ujasiriamali.

Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali kama nilivyosema kwa kuanzisha mifuko pia kwa kuweka mfuko maalum ambapo kuna Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, pia mfuko wa asilimia 10 zinazotengwa katika Halmashauri lakini pia kupitia taasisi za fedha nyingine zinazolenga kuhudumia makundi mbalimbali yakiwemo wanawake.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunaendelea kuongeza fedha kwa namna tofauti tofauti ili kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika kuongeza uchumi wa nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu hitaji la pili nipende kumshukuru Mheshimiwa Esther kwamba ametoa mawazo ya kuona namna gani Serikali itaongeza asilimia kutoka zile asilimia 10 zinazotengwa katika Halmashauri kwenda asilimia 15. Nadhani hili ni suala zuri tunalichukua ili kulifanyia kazi pamoja na wenzetu wa TAMISEMI. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza naomba ku-register masikitiko yangu kwa majibu waliyoyatoa Serikali.

Mheshimiwa Spika, tumekuwa tukishuhudia Serikali inakuwa na miradi ambayo haina mpango mkakati madhubuti ya kuonesha ukomo wa mradi. Mathalani hili Soko la Remagwe limetelekezwa tangu Awamu ya Nne, takribani miaka 10.

Je, ni kwa nini Serikali kwa takribani miaka 10 haikuweza kuwa inatenga walau bajeti kila mwaka ili kuhakikisha kwamba inakamilisha huu mradi ambao inakiri kwamba ni wa kimkakati? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Mkoa wa Mara unazalisha mazao ya kibiashara na ya chakula pamoja na mifugo ambapo hulisha ndani ya nchi lakini pia huenda kuuza nchi jirani ya Kenya, ambapo wakulima hawa wanauza kwa bei ‘chee’ baada ya kuwa wameishiwa na muda.

Ni kwa nini sasa Serikali isione umuhimu wa dharura wa kukamilisha soko hili la kimkakati la Kimaitaifa la Remagwe ili kutatua changamoto ya kimasoko kwa wakulima? (Makofi)
NAIBU WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Esther Matiko, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru kwa maswali hayo pia niwashukuru Wabunge wa kutoka Tarime, Mheshimiwa Mwita Waitara na Mheshimiwa Michael Kembaki ambao wamekuwa wakifuatilia sana maendeleo ya ujenzi wa soko hilo. Kama nilivyosema Serikali inajua umuhimu wa masoko haya na ndiyo maana tulianza kujenga katika mipaka yote ambayo ni masoko ya kimkakati. Serikali inaendelea kutafuta fedha kama nilivyosema ilikuwa chini ya ufadhili wa benki, ufadhili huo uliisha, kwa hiyo tunatafuta fedha nyingine zaidi ili tukamilishe kujenga majengo hayo.

Mheshimiwa Spika, zaidi tumeshawaambia wenzetu katika Halmashauri kuanza kutenga fedha kidogo kidogo katika bajeti zao kutokana na umuhimu wa masoko haya, kwa hiyo wanachokisema ndiyo Serikali inachokifanya na tunaendelea kufanya hivyo lakini kwasababu ni masoko ya kimkakati yana miundombinu muhimu, kwa hiyo ni lazima tupate fedha za kutosha ili tunapokuja kurudia sasa tukamilishe kwa pamoja kuhakikisha masoko haya yanakamilika katika viwango vinayotakiwa. Nakushukuru.
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, ahsante na naipongeza Serikali kwa majadiliano yanayoendelea kati yake na wawekezaji, japo nasikitika kwamba ni karibu mwaka sasa tangu mazungumzo hayo yameanza. Kwa hiyo, kwa umuhimu wa mahitaji ya mbolea nchini, naomba basi mchakato huu ufanyike kwa haraka ili tutatue tatizo kubwa la wakulima ambao wanakosa pembejeo za mbolea msimu mpaka msimu.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa Waziri mwaka 2021 kupitia Bunge hili aliahidi kuja Kilwa ili kuona mchakato wa uanzishwaji wa kiwanda hiki, lakini nadhani kutokana na majukumu alishindwa kupata nafasi hiyo. Sasa je, yupo tayari baada au ndani ya Bunge hili wakati mchakato wa majadiliano unaendelea, kufuatana nami kwenda Kilwa Masoko ili kuona maendeleo ya maandalizi ya kiwanda cha mbolea?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, naamini Serikali yetu ni sikivu chini ya Rais wetu Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, tutaharakisha majadiliano haya ili tuweze kufanikisha uwekezaji huu muhimu mapema.

Mheshimiwa Spika, nikijibu swali la pili, naomba nimwahidi, kwa kweli tangu mwaka 2021 hatujapata nafasi, lakini naamini mwaka huu nitakwenda. Nakushukuru sana.
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, kama ilivyo kwa Kiwanda cha Mbolea Kilwa, ni sawa kabisa na ilivyo na uhitaji wa Kiwanda cha Mbolea Mtwara, hususan Jimbo la Mtwara Mjini kwa sababu malighafi ipo. Sasa tu nataka kujua, ni lini Serikali itajenga kiwanda hicho kwa sababu kitaongeza ajira na wakati huo huo itawezesha nchi kupata mbolea kwa ajili ya kilimo?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tunza Malapo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi, Serikali ina nia njema kuhakikisha tunavutia wawekezaji wengi kuwekeza katika viwanda vingi ikiwemo viwanda vya mbolea.

Mheshimiwa Spika, pia hili la Mtwara nalo tunalichukulia kwa umuhimu wake kwamba tutaendelea kutafuta wawekezaji zaidi ili weweze kuwekeza Mtwara na maeneo mengine ambayo yana malighafi kwa ajili ya kuzalisha mbolea. Nakushukuru.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nashukuru kwa majibu yenye matumaini kutoka kwa Mheshimiwa Naibu Waziri. Maswali yangu mawili ya nyongeza ni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, imekuwa ni mtindo kabisa wa Wizara hii kuanzisha majengo na kutokumaliza kwa wakati kwa sababu ya kutokupata mgao unaotakiwa kutoka Serikali Kuu, kwa maana ya Wizara ya Fedha: Je, kwa mwaka huu wa 2022, hiyo shilingi milioni 100 iliyoahidiwa ni kweli itatolewa? Naomba commitment ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili ni kwamba, Wilaya ya Nyasa haina kabisa chuo chochote kinachotoa mafunzo kwa sasa hivi ikiwemo haya ya ujasiliaamali: Je, SIDO kwa kuwa jengo bado halijakamilika, mtaweza kwenda kutoa mafunzo hayo angalau kila mwezi mara moja wakati tukiendelea na huo ujenzi?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Stella Martini Manyanya, Mbunge wa Nyasa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa fedha kwa maana ya kukamilisha vituo vingi vya mafunzo na uzalishaji ambavyo vimeanzishwa katika wilaya na mikoa mbalimbali. Ni nia ya Serikali na sasa tunaamini tutapata hizo fedha ili kukamilisha kituo hiki na vingine ambavyo bado havijakamilika.

Mheshimiwa Spika, suala la pili, nachukuwa maombi ya Mheshimiwa Eng. Stella Manyanya kwamba tuanze sasa kuona namna ya kuanza kutoa mafunzo ya uzalishaji katika maeneo ambapo kuna wajasiliamali wengi ikiwemo katika Jimbo hili la Nyasa ambapo wajasiliamali hawa watapata mafunzo kupitia SIDO.

Mheshimiwa Spika, nawaagiza SIDO waanze sasa kupitia utaratibu ambao siyo rasmi, badala ya kusubiria majengo, waanze kutumia majengo ambayo Halmashauri zinaweza zikatupa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wazalishaji katika maeneo yote ikiwemo katika Jimbo la Nyasa.
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri yaliyotolewa na Serikali, ila nina swali moja dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imekuwa na dhamira ya kutengeneza ajira maeneo haya yenye uwekezaji kwa kutenga vitalu vya wachimbaji wadogo; na kwa kuwa katika eneo lile la Mkomang’ombe, eneo lote lenye makaa ya mawe limeshikiliwa na Serikali kupitia Wizara hii: Je, Serikali haioni haja ya kukaa na wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakiomba muda mrefu kugaiwa maeneo ya kuchimba makaa ya mawe ili nao waweze kutengeneza ajira?

Mheshimiwa Spika, ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Zachariuz Kamonga, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Zacharius kwa ufuatiliaji kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu katika Jimbolake la Ludewa. Ni kweli dhamira ya Serikali ni kuona sasa tunashirikisha wachimbaji wadogo katika maeneo yote au katika biashara zote ambazo zinafanyika kwenye maeneo husika.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, kwa sababu mradi huu ni mkubwa, kwa sasa bado tunakamilisha majadiliano na huyu mwekezaji mkubwa. Kwa hiyo, naamini atakapoanza kutekeleza na hao wengine wachimbaji wadogo nao naamini watashiriki katika kuhakikisha wanafaidika na uwepo wa mali asili au madini haya katika maeneo hayo ya ludewa.

Mheshimiwa Spika, tunalichukua hili kwa uzito wake ili kuhakikisha local content nayo inachukua nafasi yake.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
MHE. JUDITH S. KAPINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naishukuru Serikali kwa mujibu mazuri. Suala la ulinzi wa mlaji kwenye biashara za kimtandao hauwezi kusubiri Mpango Mkakati wa Miaka Mitano kwa sababu tayari tumechelewa na hivyo madhara makubwa yanaonekana kwa walaji pamoja na wafanyabiashara.

Je, Serikali haioni umuhimu wa kufanya utaratibu wa haraka labda kwa kuweka kanuni ili kuweza kumnufaisha mfanyabiashara huyu na mlaji katika mitandao hii ya kijamii? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Judith Kapinga Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia sana kuhusu biashara na hasa biashara mtandaoni. Ni kweli tuna mkakati huo lakini hatuwezi kusubiri mkakati ili tuweze kutelekeza majukumu ya kumlinda mlaji kwa sababu biashara mtandaoni ziandelea. Ndiyo maana sasa tunafanya marekebisho ya Sheria ya Ushindani Na. 8 ya Mwaka 2003 ambayo pia ina jukumu la kumlinda mlaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi tumeshachukua hatua zaidi, tumeanza kuhamasisha biashara mtandaoni na Waheshimiwa Wabunge watakumbuka mwaka 2021 wakati wa Maonesho ya Saba Saba tumefungua biashara mtandaoni kupitia Shirika letu la Posta; Posta hii ya commerce na mambo mengi yanafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hatuwezi kusubiri mkakati, kuna jitihada nyingi zinaendelea wakati pia na hili la mkakati linaendelea kufanyika ili kuhakikisha tuna uhakika wa kuwalinda walaji wanaotumia biashara mtandaoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Spika, natambua juhudi za Serikali katika kuendea suala zima la uwekaji mifumo ambayo itakuwa ni rahisi lakini utekelezaji ni mdogo sana na unachelewa sana. Andiko la Blue Print linaelekeza kwamba kutakuwa na mchanganuo wa jinsi gani ya kutekeleza na time frame.

Mheshimiwa Spika, swali langu, Je, Serikali iko tayari kuleta Bungeni mchanganuo wa jinsi gani changamoto hizi zinakwenda kutekelezwa na muda wake kwa maana ya time frame?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kwa kuwa Serikali ilidhamiria kujipima yenyewe kwa kutengeneza kitu kinachoitwa National Ease of Doing Business Report pamoja na kitu kinachoitwa Organizational Performance Index.

Je, Serikali imefikia wapi katika kutekeleza utaratibu huo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali madogo wawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Tarimba Abbas, Mbunge wa Kinondoni, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kazi kubwa anayofanya katika kuhakikisha biashara na mazingira ya ufanyaji biashara hapa nchini yanakua.

Mheshimiwa Spika, ni kweli Blue Print utekelezaji wake ambao tulianza mwaka 2018 tunaenda vizuri lakini bado changamoto chache ambazo ni endelevu. Nakubaliana na yeye kwamba lazima tuhuishe kwa sababu changamoto zilizokuwepo wakati ule na sasa ziko tofauti. Kwa hiyo, tunahuisha time frame ya kuendelea kutatua changamoto za utekelezaji wa Blue Print kila mwaka na tutafanya taratibu hizo kuona Wabunge wote wanapata time frame hiyo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu utaratibu wa kuwa na National Ease of Doing Business, Wizara tumeanza kutekeleza hilo na hivi karibuni tutakuwa na vitengo katika Mamlaka za Halmashauri ambavyo vitakuwa vina Watalaam wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambao watashirikiana na Mamlaka ili kuhakikisha tunaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, pia nichukue nafasi hii kuwaomba Waheshimiwa Wabunge ambao pia ni Madiwani tuendelee kushirikiana kwa sababu sisi ni sehemu ya Mabaraza ya Madiwani, tunapotunga zile Kanuni Ndogo (By Laws) basi tuangalie zisije zikawa nazo ni sehemu ya kuweka vikwazo vipya au kero mpya katika kutekeleza blue print. Nakushukuru.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi fupi kuuliza swali la nyongeza. Mifumo ambayo ni effective ni ile ambayo inatatua matatizo ya wawekezaji kwa muda na kwa haraka.

Mheshimiwa Spika, hii blue print tumeisikia muda mrefu sana. Ni lini hasa itatoka au ni document nyeti? Tunaomba kauli ya Serikali kwenye hilo. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Deo Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema blue print ni mfumo ambao unashughulikia au kurahisisha ufanyaji biashara hapa nchini. Tumeshaanza utekelezaji wake, hoja ya Mheshimiwa Mwanyika ni kwamba tayari kuna kero mbalimbali. Mwanzoni mpaka mwaka 2020 tulikuwa tumeondoa kero 232 lakini sasa tumeshafika 280. Lakini zaidi tumeshaanzisha mifumo ya kielektroniki ambayo inasomana kupunguza kero mbalimbali ambazo zilikuwa zimeainishwa katika matrix ile kwenye blue print.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunaendelea kutekeleza hatua kwa hatua. Ninyi ni mashahidi kwamba sasa tumepunguza baadhi ya kero ile ya kupanga foleni kwenda kulipa kwa mfano katika taasisi mbalimbali tunatumia kielektroniki lakini pia moja ya changamoto kubwa ambazo tulikuwa tunazishughulikia ni miundombinu wezeshi ambayo Serikari ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan tunatekeleza barabara na miundombinu mingine ambayo tunaamini hiyo itaongeza ufanisi katika ufanyaji biashara na uwekezaji hapa nchini.
MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali moja la nyongeza. Pale Mjini Musoma kuna Mwekezaji aliyenyang’anywa kiwanda cha MUTEX kwa sababu ufanisi wake haukuwa mzuri. Serikali ikaahidi kwamba ndani ya muda mfupi tutapata Mwekezaji mwingine.

Je, ni lini sasa huyo Mwekezaji atapatikana kwa sababu ni zaidi ya miaka mitatu toka mwekezaji yule aondolewe?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali tunahamasisha uwekezaji katika maeneo tofauti tofauti lakini Mbunge atakubaliana na sisi kwamba tayari kuna wawekezaji wengi sana ambao wameshaanza kuingia hapa nchini baada ya maboresho ambayo tunayafanya.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa tuna zaidi ya wawekezaji wa miradi 294 ambao wanategemea kuwekeza katika maeneo mbalimbali na tunategemea zaidi ya Bilioni Nane, Dola za Kimarekani ambazo zitawekezwa katika miradi hiyo ambayo tunaamini itaenda kutoa zaidi ya ajira 60,000.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Musoma nao katika eneo hilo la Mheshimiwa Mbunge miradi hii pia kwa kuwa tunashirikiana nae tutawasiliana tuone namna gani ya kuvutia wawekezaji hawa ambao wameonesha nia ya kuwekeza hapa nchini, waweze kuwekeza katika eneo la Musoma. Nakushukuru sana.
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa biashara ya parachichi hivi sasa ni kubwa for export, na kwa kuwa biashara hii inafanywa zaidi na Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwemo Mkoa wa Njombe pamoja na Mbeya.

Nataka kujua lini Serikali itaweka mfumo rafiki katika kuhakikisha kwamba wanaweka mfumo wa cold-room kwenye baadhi ya mabehewa ya TAZARA kama ilivyoainishwa kwenye blue print ili kuweza kuhakikisha kwamba parachichi zinafika Bandarini au Airport zikiwa na ubora? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Neema Mgaya, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli moja ya changamoto kubwa katika mazao au biashara ya matunda na mbogamboga ni hii mifumo ya cold-rooms ambayo ni changamoto kubwa. Sasa hivi tayari tumeshaanza kwenye ngazi za maeneo ambayo wanalima parachichi ikiwemo Njombe na Iringa kuwa na viwanda lakini pia na cold-rooms ambazo zitasaidia kutunza matunda hayo.

Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa hoja yake kwamba tuone sasa kwenye vyombo vya usafirishaji kwa maana miundombinu hii ikiwemo kwenye reli nao wawe na mabehewa maalum ya kuwa na cold-rooms ambazo zitasaidia kusafirisha parachichi ili zifike Bandarini au Airport kwa wakati bila kuharibika.

Mheshimiwa Spika, tunalichukua hilo wazo na tunalifanyia kazi kuhakikisha kwamba biashara hii inakuwa endelevu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. KABULA E. SHITOBELO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mheshimiwa Rais amefanya jitihada kubwa sana ya kuhamasisha wawekezaji kuja nchini. Mkoa wa Mwanza kuna eneo zuri sana na kubwa sana maeneo ya Nyamuhongoro lililopangwa kuwa industrial pack.

Je, Serikali ina mpango gani kuendeleza eneo hili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli lengo la Serikali sasa ni kuanzisha industrial pack nyingi katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo eneo hili la Mwanza. Katika Bajeti ya Mwaka huu tumeshaweka fedha kiasi kwa ajili ya kuanza kuweka maeneo haya ya industrial pack kwa ajili ya kuwezesha wenye viwanda kuwekeza katika maeneo ambayo yana miundombinu wezeshi ikiwemo majengo na barabara.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunalichukua eneo hili pia la Mwanza ambalo ni muhimu sana kwa ajili ya kuwekeza viwanda nalo pia tutaliweka katika mipango ili kuhakikisha tunafikisha azma ya kujenga viwanda maeneo yote katika nchi yetu. Nakushukuru sana.
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza naishukuru Serikali kwa majibu mazuri ambayo imeonesha kwa mara ya kwanza Serikali yetu imetenga pesa kwa ajili ya kuwezesha majukwaa haya.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mkoa wa Pwani unaongoza nchi nzima wa kusajili majukwaa 1,723 na kuyasajili 945 ambayo yamepelekea kuanzisha kampuni ya Go Mama Public Company Limited. Je, Serikali ipo tayari kutumia Milioni 200 zinazotengwa mwaka huu wa Fedha kwa ajili ya kuwezesha Mkoa wa Pwani kwa kuwa umeonesha dira umeanzisha kampuni ambayo inayo matarajio ya kujenga kiwanda cha vifungashio?

Swali la pili, kwa kuwa Serikali ina Mifuko mingi ya Uwezeshaji zaidi ya 72 ambayo ipo katika Wizara tofauti tofauti. Je, Serikali haioni ipo haja ya Mifuko hii kuwa chini ya chombo kimoja ili iwe fursa kwa majukwaa haya ya uwezeshaji badala ya majukwaa haya kutegemea asilimia 10 ya mikopo ya mapato ya ndani ya Halmashauri. Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nashukuru na naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Subira Khamis Mgalu, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Subira kwa kazi kubwa anayoifanya katika Mkoa wa Pwani kama ambavyo wamesema wameanzisha hiyo kampuni ya Go Mama ambayo wanasema ina nia ya kuanzisha kiwanda cha vifungashio ambayo italeta pato kubwa sana katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema Serikali imeendelea na itaendelea kusaidia na kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia fursa mbalimbali ikiwemo Mifuko hii ya kuwezesha wananchi kiuchumi. Kwa hiyo, kwa kazi hiyo wanayoifanya naamini tutaangalia katika bajeti hii ili tuone namna gani mahsusi kusaidia kampuni hii ambayo inaenda kusaidia kujenga viwanda katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili tayari Serikali tumeshaanza utaratibu wa kuunganisha Mifuko hii ambayo mingi ipo ndani ya Serikali katika Wizara mbalimbali, pia mingine kutoka sekta binafsi, kwa hiyo tunaifanyia kazi, naamini katika mwaka wa fedha ujao tutafanya hivyo ili kuhakikisha Mifuko hii inakuwa na tija kwa ajili ya kuwasaidia wanawake kiuchumi. Nashukuru. (Makofi)
MHE. ASYA SHARIF OMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza ninaishukuru Serikali kwa majibu yake mazuri.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa bado mahitaji ni makubwa ya wananchi hao wajasiriamali ambao wanajishughulisha na biashara ya ngozi ya mbuzi na ng’ombe, hasa tukizingatia kwamba wananchi wengi wana mahitaji makubwa lakini tunanunua nje. Kwa mfano, mikoba ya kike ambayo ni hand bag, viatu pia mikanda ya akina Baba.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza nguvu ya viwanda ili vifaa hivi sasa viwe vina ubora katika nchi yetu?

Swali la pili, pamoja na kuwa umesema mnatafuta uwekezaji labda mtuambie Serikali viwanda vingapi ambavyo kwa sasa vipo, katika nchi yetu vinavyojishughulisha na usindikaji wa ngozi ya mbuzi na ng’ombe?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asya Sharif, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli mahitaji ya ngozi ambazo zipo katika hatua ya mwisho kwa maana finished leather kwa ajili ya bidhaa za ngozi ikiwemo mikoba na viatu bado ni changamoto katika viwanda vyetu vya ndani. Moja ya mikakati tuliyonayo ni kuhakikisha tunawahamasisha kwanza wafugaji kuzalisha ngozi zinazokidhi mahitahji, ikiwa ni pamoja na kuchunga mifugo yetu katika hali nzuri, ikiwa ni pamoja na kutokupiga chapa kuharibu ngozi, pia kupiga fimbo au viboko, mbuzi na kondoo.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili tunahamasisha uwekezaji katika viwanda hivi ambavyo vitatumia malighafi yetu kuzalisha bidhaa za ngozi kwa maana ya ngozi hadi mwisho (finished leather) kwa hiyo ni moja ya mikakati ambayo Seriakli inaendelea kufanya, katika kuhakikisha tunakuwa na ngozi nzuri.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na takwimu, tutamletea takwimu sahihi ya viwanda kwa sababu bado tunaendelea kuhamasisha na kuna viwanda vingi vidogo ambavyo vinaendelea kuzalisha bidhaa za ngozi katika nchi yetu, vikitumia ngozi kutoka ndani ya nchi lakini nyingine kutoka nje ya nchi. Ninakushukuru.
MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Moja, kwa kuwa upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vya kuchakata na kusindika mazao ya uvuvi vimepungua; mazao hayo ya uvuvi na malighafi yanapungua, hayakidhi mahitaji ya viwanda: Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha vyombo na zana za uvuvi ili kuongeza ufanisi na tija? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa kuna upotevu mkubwa wa mazao ya uvuvi baada ya kuvunwa: Je, Serikali itasaidiaje kusambaza teknolojia rahisi za usindikaji wa mazao ya uvuvi ili kuyaongezea thamani kwa wavuvi wadogo wadogo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kavejuru Eliadory Felix, Mbunge wa Jimbo la Buhigwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli moja ya changamoto tuliyonayo katika sekta ya viwanda ni ukosefu wa malighafi ambazo zinahitajika katika viwanda ambavyo vimepelekea baadhi ya viwanda kufungwa. Moja ya mikakati ya Serikali ambayo inatekelezwa kwenye mipango hii niliyoitaja ni kuwawezesha wavuvi na wenye viwanda kutumia teknolojia nzuri ya kisasa ambayo itapelekea kuvuna Samaki wanaohitajika katika viwanda badala ya kuvuna na wale madogo kwa maana ya makokoro ambayo yanatumika kuvuna hata mazalia.

Mheshimiwa Spika, pili, tuna mikopo mbalimbali, moja ni hii ya Halmashauri na pia kupitia taasisi zetu kama SIDO ambayo inawawezesha wavuvi kupata mikopo hiyo ili waweze kupata teknolojia za kisasa za kuvuna au kuvua samaki katika maeneo hayo. Kwa hiyo, Serikali inaendelea kuwawezesha wavunaji au wavuvi ili waweze kupata teknolojia za kisasa kupitia mikopo.

Mheshimiwa Spika, pili, kwenye upotevu; ni kweli moja ya changamoto iliyopo ni upotevu wa mazao yanayotokana na uvuvi baada ya kuvunwa. Mara baada ya kuvua Samaki wanapotea au wanaoza. Moja ya maeneo, tunajenga industrial pack au kongani ambazo zitasaidia kuwa na maeneo maalum ya kutunzia Samaki ikiwa pamoja na kuvutia wawekezaji wa viwanda ili kuhakikisha mavuno yanayotoka baharini au kwenye maziwa yanaenda moja kwa moja kwenye viwanda ili kuchakatwa kabla ya kuharibika.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Jimbo la Bunda Mjini, limetenga eneo la Kata ya Mgeta kwa ajili ya Ukanda wa Uwekezaji, mpaka sasa hivi hawajawekeza; na Bunda pia tunavua: Kwa nini sasa Wizara isione kwamba kuna haja ya kujenga kiwanda kwa ajili ya vifaa vya uvuvi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA:
Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ester Bulaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi moja juu ya changamoto tulizonaao: Kwanza, ni mazao yenyewe yanayotokana na uvuvi kupungua; pili, kukosekana kwa viwanda ambavyo vinazalisha vifaa vya uvuvi ambavyo ndiyo teknolojia mahususi ambayo itapelekea kuvua kwa ubora zaidi mazao ya samaki.

Mheshimiwa Spika, katika mikakati ambayo tunaendelea nayo ni kuvutia wawekezaji kujenga viwanda vya kuchakata, lakini pia naamini tukifanikiwa hilo, hatua inayofuata nadhani ni kuweka sasa viwanda ambavyo vinazalisha vipuri vitakavyoweza kuzalisha zana za kuvuali Samaki katika sekta hii ya uvuvi. Kwa hiyo, nachukua hili kama sehemu ya changamoto na juhudi zetu kama Serikali, kuvutia zaidi wawekezaji katika viwanda vya kuzalisha vifaa vya kuvulia samaki katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Nakushukuru.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu ya Serikali ambayo ni majibu ya kawaida (generic answers). Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, Mkoa wa Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe ndiyo ina uzalishaji mkubwa sana wa zao la parachichi. Kwa bahati mbaya sana uzalishaji huo ni mkubwa lakini asilimia 90 mpaka 99 ya mazao ya matunda ya parachichi yote yanasafirishwa nje bila kuongezwa thamani kwa maana halisi ya uongezaji wa thamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali langu; Mheshimiwa Waziri anaweza kutoa commitment hapa leo kwamba watachukua suala la Mji wa Njombe na Mkoa wa Njombe kama special case ili waweze kuanzisha maeneo maalum kwa ajili ya uzalishaji na uchakataji wa parachichi tuache kupeleka maparachichi zikiwa ghafi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kama ataitoa commitment hiyo na atakubaliana nami na sioni kwa nini asikubaliane nami. Je, kuonesha umuhimu wa suala hilo, Waziri yuko tayari twende pamoja Njombe baada ya kusoma bajeti yake ili tukaanze majadiliano ya awali ya kuanzisha mchakato huo wa kuanzisha viwanda vya kuchakata parachichi badala ya kusafisha, kupaki na kusafirisha ambayo inatupotezea sisi mapato? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Deodatus Phillip Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli moja ya vigezo ambavyo vinatakiwa kwa ajili ya kuanzishwa maeneo ya uwekezaji kwa ajili ya kuzalisha bidhaa kuuza nje (Special Economic Zones) ni uwepo wa malighafi; pili ni uwepo wa ardhi; zaidi ni miundombinu wezeshi kwa ajili ya kuzalisha bidhaa hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe commitment ya Serikali na niwaagize Mamlaka ya EPZA waanze mchakato mara moja wa kuwasiliana na Mkoa wa Njombe, na kutafuta wadau wengine. Kwa sababu katika maeneo haya ya uwekezaji kwa ajili ya mauzo nje tunashirikiana pia na sekta binafsi ili kuhakikisha mkoa huu sasa unakuwa na eneo kwa ajili ya kuzalisha bidhaa au kuzalisha maparachichi ambayo yatauzwa nje ikiwa ni bidhaa zake au maparachichi yenyewe ili kuongeza uchumi wa Mkoa wa Njombe na azma ya kupunguza kuuza malighafi nje, yakiwemo na maparachichi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya commitment hiyo na EPZA wataanza kufuatilia, na mimi nikubaliane naye, nitakwenda Mkoa wa Njombe ili tuweze kuona namna ya kujadiliana na wadau ukiwemo mkoa, kupata ardhi na wadau wengine kwa ajili ya kuwekeza au kuanzisha maeneo huru ya uwekezaji katika Mkoa huo wa Njombe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana; Mkoa wa Kagera unafahamika kwa uzalishaji wa zao la kahawa, na ni zao la kimkakati, na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imejikita kuboresha na kuongeza thamani ya zao la kahawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya wabia wa Kiwanda cha TANICA Serikali ni mbia na kuna hisa za zaidi bilioni 8.6 ambazo hazijalipiwa. Je, Serikali ina mkakati gani kuhakisha kwamba hizo hisa ambazo hazijalipiwa za bilioni 8.6 zinalipiwa ?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Oscar Ishengoma Kikoyo, Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, Serikali iliunda kamati maalum kwa ajili ya kuangalia namna ya kukikwamua kiwanda hiki muhimu sana cha kuzalisha kahawa katika Mkoa wa Kagera; hivyo tuko katika hatua za mwisho za kuona namna gani ya kupata fedha hizo pia kuona wanahisa wanaongeza hitaji ili, moja, kupata hizo fedha ambazo ni mtaji muhimu pili, kupata teknolojia ya kisasa ambayo itasaidia uzalishaji wenye tija wa kiwanda hicho; kwa sababu moja ya changamoto tuliyonayo ni uchakavu wa mitambo au mashine zilizofungwa tangia mwaka 1967.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Serikali inafanyia kazi na fedha zitakazopatikana tutaweza kuboresha kiwanda hiki pia kuhakikisha uzalishaji unakuwa na tija kwa ajili ya manufaa Taifa hili na Mkoa wa Kagera, nakushukuru.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru tena kwa kunipa fursa ya kuweza kuuliza maswali mengine mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ambayo Serikali imetoa, majibu haya hayaendani na uhalisia wa sasa kwa namna ambavyo kiwanda kinaendelea. Haya ni majibu ya zamani kabisa. Pamoja na hivyo ninaomba niongeze maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kutokana na mradi huu ni mradi wa kimkakati, tunauliza ni lini Serikali itaanza kutupatia fedha kuendeleza mradi huu kuliko kuanza kutafuta wawekezaji wa kuanza kuwekeza maana yake tulikuwa tumesha ahidiwa kupewa fedha?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kupitia Wizara ya Madini, Waziri mwenye dhamana husika alipotembelea Momba alisema angetuma wataalamu wake waje kutuandikia andiko na kufanya utafiti ni kwa namna gani tuweze kuzalisha kiwango kingi cha chumvi na tuweze kuongezea fedha. Je, Serikali mmeshapata andiko hili la wataalam ili tuweze kuombea fedha ya ziada kutoka kile kiwango ambacho tulikuwa tumepewa?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA:
Mheshsimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Condester Sichalwe, Mbunge wa Momba kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tunajua changamoto ya kiwanda hiki na tathmini inaonyesha tunahitaji takribani shilingi milioni 535 ili kukamilisha ujenzi au uendelezaji wa kiwanda hicho lakini Waheshimiwa Wabunge tunajua kwamba Serikali haifanyi biashara tunachokifanya ni kuwawezesha kama hii mradi maalum wa wale wananchi ili waweze kuendeleza mradi huo.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema tunahamasisha pia wawekezaji wengine ambao wanaweza kuingia na kushirikiana nao wananchi ambao wameanzisha mradi huu wa chumvi ili uweze kuwa na faida kwa wananchi. Kwa hiyo, Serikali kimsingi haiwezi kufanya biashara lakini inawawezesha wananchi ili waweze kuendeleza shughuli zao za kiuchumi kupitia mradi huu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili la andiko ambalo linaweza kuonesha umuhimu wa kupata fedha kupitia Wizara ya Madini. Hili tutalifanyia kazi na tutawasiliana na Wizara ya Madini ili tuone tumefikia wapi na kumpa jibu kamili Mheshimiwa Mbunge.
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, nina maswali mawili ya nyongeza; miongoni mwa watu wanaolima chumvi kwa wingi ni wakazi wa Mkoa wa Mtwara, changamoto kubwa wanayoipata ni soko la uhakika. Nataka kujua mkakati wa Serikali ni upi kuhakikisha wakulima wale wa chumvi wanapato soko la uhakika?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, ili kuchochea uchumi wa bluu; uwepo wa dhana bora za uvuvi ikiwemo meli ya uvuvi ya kisasa ni jambo la muhimu. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuleta meli ya kisasa ya uvuvi katika Bahari ya Hindi iliyopo Mkoa wa Mtwara?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA:
Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Tunza Issa Malapo, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli moja ya changamoto kubwa tuliyonayo kwa wazalishaji wa chumvi hasa wadogo ni changamoto ya soko la uhakika kwa chumvi yao na hasa ambayo ni malighafi kwa maana ya kuwa siyo finished product.

Mheshimiwa Spika, moja ya mikakati ya Serikali tumeshaanza kutekeleza na kuzuia uingizaji wa malighafichumvi au chumvi ambayo inatumika kuzalisha chumvi ya kula kutoka nje. Hili tumeshalisema na tunaamini viwanda vya ndani vinavyozalisha chumvi vitatumia malighafi zilizopo kwa maana ya chumvi inayozalishwa na wakulima wadogo wadogo wakiwemo wa Mkoa wa Mtwara.

Mheshimiwa Spika, zaidi tunahamasisha katika masoko ya kikanda kwa maana ya Afrika Mashariki na SADC ili tuone nchi ambazo zinakosa au hazina malighafi ya chumvi zinatumia malighafi ya chumvi yetu ikiwemo inayotoka katika Mkoa wa Mtwara ambao tunaamini itakuwa ni chumvi ambayo inapelekwa kwenye masoko hayo ili waweze kunufaika zaidi na uzalishaji wa chumvi katika maeneo haya ya Mtwara.

Mheshimiwa Spika, kwenye upande wa meli ya kisasa ya uvuvi kama nilivyosema Serikali tunaedelea kuhamasisha uwekezaji katika maeneo yote ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha uchumi wa bluu ambayo nayo inahusisha kuwa na meli za kisasa ambazo zingeweza kusaidia kuwa na uvuvi wa kisasa zaidi wenye tija. Serikali pia kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendelea na mikakati mbalimbali ambayo mojawapo ni kuona namna gani ya kutafuta wawekezaji wengi ambao wanaweza kuvua kwa tija katika bahari yetu.
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Serikali ni vyema tutambue kwamba Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, anaweka jitihada kubwa sana kuimarisha mazingira wezeshi na kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi na hiyo imeenda sambamba kabisa na Mheshimiwa Rais kuamua kuchukua jukumu la uwekezaji na kuweka chini ya Ofisi ya Rais, pamoja na kuteua Katibu Mkuu wa Uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba niulize maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; Blueprint imeelekeza kwamba ili kuimarisha mazingira wezeshi lazima tuwe tuna ardhi inayojulikana kwa ajili ya uwekezaji kwa maana ya kwamba ardhi hiyo ipimwe na iainishe ni uwekezaji gani ambao uatafanyika sasa je, mpaka hivi sasa Serikali imepima kiwango gani cha ardhi na ramani ya ardhi hiyo kwa ajili ya uwekezaji inapatikana wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; pamoja na kwamba Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 2022 ilipitishwa ndani ya Bunge lako Tukufu kwenye blueprint imeelekeza zaidi ya sheria 20 ambazo zinatakiwa zifanyiwe maboresho.

Kwa hiyo ningependa kufahamu kutoka kwa Serikali, je, ni lini Serikali italeta hizo sheria zingine zaidi ya 20 ili zifanyiwe maboresho ili kuhakikisha kwamba tunaimarisha mazingira wezeshi hapa nchini na hivyo kuunga mkono na kutokufifisha jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha na kuleta wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Neema Kichiki Lugangira, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi tumeshaanza kutekeleza MKUMBI au Blueprint na moja ya utelekezaji huo ni kuhuisha au kutunga Sheria mpya ya Uwekezaji lakini pia ninyi ni mashahidi katika Bunge liliopita tumepitisha maboresho ya sheria mbalimbali zaidi ya 19 ambazo ziligusa sekta tofauti tofauti.

Kama nilivyosema utekelezaji wa MKUMBI au blueprint sio kitu cha siku moja, kwa hiyo tunaendelea kutekeleza moja ya maeneo ambayo Mbunge ameyasema ni hayo ya kupitia baadhi ya sheria na kanuni lakini pia kuboresha baadhi ya taratibu ambazo zipo na tunazoona ni changamoto au kero kwa ajili ya kuboresha uwekezaji hapa nchini, nakushukuru.
MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Pamoja na uwekezaji mzuri kufanyika wa kujenga Kiwanda cha Nguo cha MUTEX Musoma, lakini mpaka sasa kiwanda kile hakifanyi kazi. Je, ni upi mkakati wa Serikali kufufua kiwanda hicho?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA:
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli moja ya mikakati tunayoifanya Serikali ni kuona namna gani tunafufua viwanda ambavyo havifanyi kazi na sisi kama Serikali tumeshaanza kuona vile viwanda ambavyo vilikuwa vimepewa watu binafsi na hawaviendelezi kuvirudisha Serikalini na hatua ya pili sasa ni kuvitafutia wawekezaji ili waweze kuwekeza katika viwanda hivyo na kimojawapo ni kiwanda hiki cha MUTEX kilichopo kule Musoma, nakushukuru.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nataka nimhakikishie Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba eneo hili limepimwa na lina hati ya Kijiji kwa ajili ya shughuli hiyo, na tayari Katibu Mkuu alitembelea eneo hili kwa hiyo hakuna mgogoro wowote wa umiliki.

Swali langu, kwa kuwa ujenzi huu umesimama tangia mwaka 1974 na sasa ni miaka 47 haujaendelezwa; je, ni lini sasa Serikali itaanza ujenzi?

Swali la pili, kwa kuwa kuna kiwanda cha aina hiyo hiyo kimejengwa kata ya Rundugai na kimefadhiliwa na mradi wa TASAF; je, hatuoni iko haja ya Serikali kuchukua na kukiweka chini ya SIDO ili kiweze kutoa huduma?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana; kwanza niwapongeze sana wananchi wa Jimbo la Hai kupitia Mbunge mahiri, ndugu yangu Saashisha Mafuwe kwa ufuatiliaji lakini pili kwa kutenga haya maeneo mahsusi na kuanza ujenzi wa jengo hilo ambalo ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya Viwanda.

Mheshimiwa Spika, niwahakikishie wana- Hai na hasa wana- Lwosaa kwamba sisi kama Wizara tutahakikisha tunaendeleza jitihada hizi za wananchi katika kujiwekea maendeleo kupitia SIDO na taasisi zetu nyingine kuanza kukamilisha jengo hilo. Kama umiliki sasa ukihamishiwa kwenda SIDO maana yake tutakuwa na ule uhakika wa kuendeleza na kuwekeza zaidi katika ujenzi wa jengo hilo na kukamilisha kama ambavyo tumesema kwa sababu tathmini imeshakamilika.

Mheshimiwa Spika, lakini pili na hili jengo lingine ambalo katika kata hiyo mpya Mheshimiwa Mbunge amesema nalo sasa wakati wanakuja kufanya uhamisho wa umiliki wa eneo hili la Lwosaa nawaagiza SIDO watembelee na kukagua pia jengo hili ili nalo tuweze kuliwekea katika mipango la kuliendeleza na kuwajengea wananchi hawa chuo cha ufundi kupitia SIDO katika Jimbo la Hai.

Mheshimiwa Spika, pia nichukue nafasi hii kuwaomba Waheshimiwa Wabunge wengine wote na sisi wananchi tutenge maeneo kwa ajili ya maendeleo ya viwanda pamoja na masoko kwa ajili ya kujiletea maendeleo kupitia SIDO na taasisi nyingine.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru lakini sio mwiki ni mvuke. Maswali mawili ya nyongeza: -

a) Je, kwa nini SIDO na TBS isijielekeze katika kuboresha teknolojia za asili za watengenezaji wa pombe ya mvuke ya mabibo badala ya kuendelea kutoa mafunzo?

b) Je, kwa nini Serikali, isipitie watengenezaji wote wa pombe ya mabibo, badala ya kusubiri waombaji wachache wenye uwezo wa kuagiza mitambo kwa ajili ya kupata hizo ithibati za TBS na SIDO?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni kweli kabisa kwanza nimpongeze Mheshimiwa Agnes Hokororo kwa kuleta tena hili swali ambalo ni hoja muhimu sana kwa Watanzania wengi ambao wengi tumeendesha shughuli zetu za kusoma shule na mambo mengine kupitia pombe hizi za kienyeji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, kweli tunachofanya sasa ni kuboresha teknolojia zilizopo lakini pia kuna wakati mwingine tungependa kupata teknolojia rahisi lakini za kisasa zaidi. Ndiyo maana SIDO tunahakikisha tunawatembelea wazalishaji hawa na kuwasaidia. Kama ambavyo nimesema, tayari kuna haya maombi, maana yake hawa ni wale ambao wana uwezo wa kuomba; lakini ambao sasa hawana uwezo wa kuomba, kama ambavyo nimesema wale wazalishaji wa pombe hii ya mvuke kupitia mabibo, tumeshaamua sasa tutawatembelea wauzaji wote wa pombe za kienyeji ili tuwaelimishe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, tutawaelimisha kuhusu mazingira sahihi ya kuzalishia, kwa maana ya kuzalisha pombe, ambapo itakuwa na mazingira sahihi mazuri. Pili tuwasaidie teknolojia rahisi na kuzihuisha zile zilizopo ili ziwe katika mazingira ambayo yatapelekea kupata viwango sahihi vya pombe. Tatu, tuwasaidie kuhakikisha wanapata teknolojia ya kutunza, packaging ili zile pombe zisiharibike mapema au zipate shida ambayo itapelekea kuwa sumu kwa walaji katika mazingira mabayo si sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
MHE. SYLVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, ni ukweli usiofichika kwamba SIDO zetu nyingi zinafanya kazi chini ya kiwango na hiyo ndiyo maana unaona hata idadi ya wanufaika ni wachache. Je, nini mpango wa Serikali wa kuziwezesha SIDO hizi ili ziweze kuwanufaisha wajasiriamali wengi zaidi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa wajasiriamali wengi wanashindwa kumudu gharama za mafunzo haya. Je, Serikali iko tayari kuweka wazi na kutoa maelekezo kwa SIDO zote nchi nzima kutoa mafunzo haya bure na kuweka mwongozo wazi wa namna gani mafunzo haya yanafanyika katika SIDO zetu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Ni kweli, niungane na hoja ya Mheshimiwa Mbunge kwamba tuna changamoto ya bajeti kidogo kwa Shirika letu la SIDO lakini sasa ni mpango wa Serikali kuona baada ya kuongeza katika sekta nyingine, ni dhahiri tutakuja kwenye sekta hii ya viwanda ambapo SIDO ni wadau muhimu sana kuhakikisha wanaendeleza na kufanya kazi zao kwa weledi wakiwa na bajeti ya kutosha. Kwa hiyo, Serikali imejipanga kuongeza fedha ili waweze kuongezewa SIDO waweze kufanya kazi zao zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, ni kweli tungeweza kutoa bure mafunzo lakini lazima kuna gharama ndogo ambazo wajasiriamali wanatakiwa kuchangia. Hoja kubwa hapa ni kuona namna gani tunawawezesha SIDO ili wawe na fedha za kutosha na gharama za wajasiriamali kuchangia kupata mafunzo ziwe chini zaidi au hatimaye yaweze kutolewa bure kama alivyoshauri Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, pamoja na majibu ambayo ni mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, tatizo la kiwanda siyo tu wanahisa, tatizo la kiwanda ni deni la Benki yetu ya Kilimo.

Swali la kwanza, je, Waziri haoni haja sasa ya kuhakikisha kwamba anaratibu majadiliano akishirikisha Wizara ya Mifugo ambayo ndiyo inasimamia sekta hiyo kwa haraka sana? (Makofi)

Swali la pili, anawahakikishiaje Wananjombe na wafugaji wa Njombe kwamba majadiliano hayo sasa yatafanyika kwa haraka katika kipindi hiki cha Bunge au mara tu baada ya kuisha Bunge hili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA:
Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kama nilivyosema nia ya Serikali ni kuona kiwanda hiki kinafanya kazi na kwa taarifa tu kwa sababu ya umuhimu wake Wizara wenye dhamana ya kuhakikisha maendeleo ya viwanda nchini yanafanikiwa na kuwa na tija, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutaratibu majadiliano ya wanahisa kwa maana ya NJOLIFA, Njombe Wilaya, Njombe Mji, Roman Catholic ambao nao wanahisa na wengine. Muhimu zaidi kama nilivyosema moja ya sababu iliyopelekea kukwama kiwanda hiki ni mtaji ambao sasa kupitia Benki ya Kilimo (TADB) ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 1.6. Sasa tutaandaa kikao, tutawaita kabla ya kuisha Bunge hili ili wanahisa wote na wenzetu wa TADB tuje tukae hapa, tuone namna gani tunakwamua mkwamo wa kiwanda hiki ili kiendelee kuzalisha kwa tija lakini pia kupata manufaa kwa nchi katika sekta ya viwanda.
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Swali la kwanza, kwa kuwa Jimboni Kibaha Vijijini kuna kongani kubwa ya viwanda Kwara na viongozi wa eneo hilo hawana uelewa wa kutosha juu ya miongozo hiyo. Je, Serikali haioni ipo haja sasa ya kufika Jimboni Kibaha kuwapa mwongozo ili waweze kusimamia chanzo hiki cha mapato?

Swali la pili, kwa kuwa maeneo ya Kibaha Vijijini , viwanda vingi vitajengwa na vingine vitatumia Sheria ya EPZ. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kubadilisha sheria ili viwanda hivi vitakavyojengwa kwenye EPZ viweze kuchangia shughuli ya maendeleo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ni kweli Kibaha katika Mkoa wa Pwani ni moja ya maeneo ambayo kuna uwekezaji mkubwa sana wa viwanda hapa nchini. Kwa takwimu tulizonazo kwa Aprili tu takribani miradi saba imewekezwa katika eneo hili ambalo ni muhimu sana kwa wawekezaji wengi.

Mheshimiwa Spika, Wizara na Serikali kama nilivyosema, maeneo yote ya uwekezaji pamoja na eneo la Kwala Industrial Park ambalo linajengwa pale, tunawaelekeza wawekezaji kuhakikisha wanachangia maendeleo na miradi ya kijamii. Pili katika maeneo hayo tumeshaweka kwenye Serikali za Mitaa Idara Maalum ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambao kazi yao wao ni kuwaelimisha wawekezaji hawa kwa kushirikiana na TAMISEMI kuhakikisha wanachangia mapato wanayopata kutoka na uwekezaji huo.

Mheshimiwa Spika, pili, kwenye maeneo ya uzalishaji kwa ajili ya mauzo nje EPZ tumeshasema na tunao mpango wa kuweka utaratibu wa uwekezaji, ambao unaelekeza wawekezaji hawa ambao wanafaidika, wananufaika na vivutio maalum ambayo kimsingi ni kodi za Watanzania, kuhakikisha mapato wanaopata au faida wanazopata kutokana na uwekezaji huo waweze kurudisha kwa wananchi kupitia shughuli mbalimbali za kijamii, kama ni elimu, afya, maji au barabara kulingana na mahitaji ya maeneo husika ambayo wanawekeza wawekezaji hao, nakushukuru sana.
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; Serikali inakiri kwamba bado haijapata kutambua vizuri kundi hili na ilihali na yenyewe inatambua kwamba ilitoa vitambulisho;

Je, Serikali iko tayari kukiri kwamba vitambulisho vile havikusaidia kutambua kundi hili, haswa kwa teknolojia duni ambayo imetumika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Ili machinga atoke kwenye hali ya umachinga na Kwenda katika kundi la wafanyabiashara wagodo na wa kati, ni lazima apewe afua mbalimbali za kikodi;

Je, Serikali ina mpango gani sasa kuzibainisha hizo afua za kikodi ili hawa wamachinga waweze kuzitambua na waweze kuingia kwenye kundi la wafanyabiashara rasmi?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Ni kweli moja ya changamoto zilizojitokeza kwa vitambulisho vile vya awali vya kuwatambua wamachinga ilikuwa ni kwamba vinaweza vikatumika na mtu yoyote kwa sababu havikuwa vya kielektroniki. Moja ya kazi kubwa tunayofanya sasa katika bajeti inayokuja ni Serikali Kwenda kutoa vitambuilisho vya kielektroniki ambavyo vitasaidia kuwatambua wajasiriamali walipo, lakini pia pale ambapo watakuwa wamekua, kwa maana kutoka mitaji ile midogo ya 4,000,000 ambayo tunatambua kama wajasiriamali, kwenda juu tutawatambua kama wafanyabiashara halali na kuwarasimisha kwenye kundi halali la wafanyabiashara kutoka wajasiriamlali.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwenye swali la pili; Serikali inafanya kazi kubwa sana. Moja ni kurasimisha kuwatambua wajasiriamali hawa na Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan ametoa fedha 10,000,000 kuanzisha ofisi za wamachinga kila Mkoa. Sasa kupitia hizo tutawatambua na kuwasaidia kupata mikopo nafuu kwenye taasisi zetu za fedha, lakini pia utaratibu unaokuja ni kuona zile fedha asilimia 10 ambazo zilikuwa zinatolewa ziweze kuwa na manufaa kupitia benki ili wajasiriamali hawa wadogo ambao wanahitaji mitaji kwa ajili ya kuendeleza biashara zao wanufaike.
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kufanya ziara jimboni karibu mara mbili, ametembelea kiwanda cha Kilombero Sugar na Mang’ula Machine Tools pamoja na shamba hili la rubber.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza. Shamba hili ambalo lina ukubwa wa karibu hekari 1,678; sasa hivi kuna watu wachache kwa manufaa yao wanalikodisha kwa wananchi: Kwanini Serikali kupitia Serikali ya Kata isitoe uwazi eneo la shamba ambalo halijapandwa rubber, lilimwe na wananchi mpunga au miwa kwa uwazi tofauti na ilivyo sasa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Ili kuweka ulinzi wa shamba hilo, tuliwasilisha ombi letu kwa Mheshimiwa Waziri kutoa sehemu ya shamba kwa maslahi ya maendeleo ya wananchi kwa ujenzi wa kituo cha polisi, high school na kituo cha afya: Je, ombi letu limefikia wapi?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ni kweli kulikuwa na changamoto hizi za uvamizi katika shamba hili la mpira. Namshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa kuleta taarifa hii ambayo kimsingi hairuhusiwi watu kufanya shughuli nyingine nje ya shughuli tarajiwa katika shamba hili la mpira.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama kuna uvamizi huo, naomba niielekeze NDC waweze kufuatilia ili kama kweli kuna haja ya wananchi kutumia maeneo ambayo hayajaanza kuendelezwa kwa kupanda miti ya mpira, basi tuone namna ya utaratibu mzuri kama ambavyo ameshauri Mheshimiwa Mbunge kupitia viongozi wa Kata na eneo husika ili wananchi wa pale waweze kufaidika na kutumia eneo hilo ambalo ni la Serikali, kwa utaratibu kamili. Kimsingi, eneo hili ni la kuzalisha miti kwa ajili ya mpira.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili kama alivyosema Mbunge, Mheshimiwa Waziri amepitia katika shamba hili, tunaendelea kujadiliana tuone namna gani tunaweza kuwezesha huduma hizi za kijamii kwa maana ya shule, vituo vya afya au kituo cha polisi, tuone kama vinaweza kujengwa katika eneo hili la shamba ambapo kimsingi ni kwa ajili ya uzalishaji wa mpira, nakushukuru.
MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Je, ni nini mpango wa Serikali katika kufufua viwanda vilivyotelekezwa kwa muda mrefu kikiwemo kiwanda cha kuchambua pamba cha Nyambiti kinachopatikana katika Kijiji cha Mwabilanda katika Jimbo la Sumve?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Ni kweli moja ya maeneo ambayo Serikali tunaweka mkazo sasa ni kuona tunafufua viwanda ambavyo vilikuwa vimebinafsishwa, na baadhi ya maeneo au viwanda hivyo wale wawekezaji tuliowabinafsia hawajavifufua au kuviendeleza au wanafanya tofauti na mkataba tuliowapa. Pamoja na viwanda vingine, hiki pia kipo kwenye mpango huo ambapo tunaendelea kutafuta wawekezaji au kuhakikisha wale ambao tumewakabidhi kwa sasa, waweze kuviendeleza kulingana na mikataba ambayo tulikuwa tumeingia nao, nakushukuru.
MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza sikubaliani na majibu ya Serikali kwa sababu kila siku wanajipanga, wanajipanga; wanafanya utafiti, wanafanya utafiti; sikubaliana nayo, lakini nina swali moja la nyongeza. Kwa vile Jimbo la Mwibara linakabiliwa na upungufu wa chakula na mojawapo ya sababu ikiwa ni ukosefu wa skimu za umwagiliaji maji: Je, ni lini Serikali itaanza tena mpango wa kupeleka chakula cha msaada katika Jimbo la Mwibara? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Serikali inaendelea kufanya kazi kulingana na mipango kama nilivyosema, katika mwaka wa 2023/2024 kuna fedha nyingi zimetengwa kwa ajili ya skimu za umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na changamoto ya chakula katika Jimbo la Mwibara, utaratibu ni kwamba pale kunapokuwa na uhitaji wa msaada wa chakula katika maeneo husika, naomba viongozi ikiwemo kupitia Mbunge mweze kuandika barua ya maombi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu ili tuweze kuratibu namna ya kupeleka chakula cha msaada katika maeneo husika ili kufidia au kupunguza nakisi ya chakula na adha kwa wananchi katika jimbo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Mbunge ashirikiane na viongozi wengine ili kuandika barua na kupata maelekezo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi ili niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa Serikali mwaka juzi 2021 ilitenga shilingi milioni 100 kupeleka Skimu ya Lwafi – Katangoro, lakini mpaka sasa hakuna tija yoyote imeonekana kwenye hiyo fedha: Ni upi mkakati wa Serikali wa kuongeza fedha ili kumaliza skimu hiyo na ianze kufanya kazi?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, tayari katika mpango wa mwaka wa fedha huu tunaoenda nao, fedha nyingi zimewekwa kwa ajili ya kukamilisha skimu mbalimbali za miradi ambayo ni mipya na inayoendelea. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge awe na imani kwamba sasa huu mradi utaenda kukamilishwa kwa sababu tayari fedha zimetengwa katika mwaka huu wa 2023/2024 ili kutekeleza pamoja na skimu nyingine ikiwemo na hiyo skimu ya kwa Mheshimiwa Aida Khenani, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Skimu za umwagiliaji wa maeneo ya chai kwenye Tarafa ya Igominyi katika Jimbo la Njombe Mjini: Nini kauli ya Serikali kuhusu utekelezaji katika kipindi hichi cha bajeti? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA (K.n.y. WAZIRI WA KILIMO): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Skimu ya Igominyi na maeneo mengine kama alivyosema, ni skimu muhimu sana kwa ajili ya kuhakikisha kilimo cha chai kinaendelea kuchangia katika uchumi wa nchi. Ni nia ya Serikali kuona skimu zote ambazo ziko kwenye mpango wake zinatekelezwa. Kwa hiyo, fedha zitaendelea kupelekwa katika maeneo ambayo yamepangwa kulingana na mpango wa fedha katika mwaka wa fedha huu wa 2023/2024, nakushukuru. (Makofi)
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, tuna Skimu ya Udimaa na Skimu ya Ngaiti ambazo zimechakaa sana, lakini zipo kwenye bajeti ya mwaka huu: Je, ni lini Serikali itaanza utekelezaji wa kujenga hizi skimu mbili ambazo nimezitaja? Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Ni kweli tunajua katika baadhi ya maeneo skimu nyingi zimechakaa, kwa maana ni za muda mrefu. Ndiyo maana kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, tayari tumeshaweka fedha kwenye mwaka huu wa 2023/2024. Kwa hiyo, muda wowote tutaanza kutekeleza skimu hizo ikiwemo ya kwa Mheshimiwa Mbunge kule Manyoni ili kuhakikisha skimu hizo zinaboreshwa ili ziweze kutoa faida kwa wakulima na kuweza kuhakikisha kilimo cha kisasa kinaendelea, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Naipongeza sana Serikali kwa jitihada zake za kupanga mipango ya umwagiliaji. Kwa kuwa Serikali ndiyo yenye wataalam, wabobezi katika masuala haya ya umwagiliaji.

Je, ni lini Serikali itapanga mipango ya kuwasaidia wakulima kufanya levelling kufikisha maji kwenye mashamba yao badala ya kuwaachia kazi mkulima mmoja mmoja afanye jambo hilo ambapo hawana utaalamu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inge-copy mambo yanayofanyika Egypt. Egypt wanafanyakazi zote mpaka kuwapeleka watu mashambani, kwa sababu ninyi ndio mna kamera, ninyi ndio mna vifaa vya kupimia: Sasa Serikali mna mpango gani wa kushughulikia wakilima ili maji yaende kwa watu wote?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni mawazo mazuri kutoka kwa Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ndiYo yenye dhamana ya kuhakikisha skimu za umwagiliaji na kuhakikisha maji yanaenda katika mashamba na maeneo mbalimbali ambako wananchi wanafanya shughuli za kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mipango ya Serikali tumesema moja ya maeneo ambayo yameongezwa sana fedha ni kwenye maeneo haya ya umwagiliaji. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mipango ya Serikali ni thabiti na itaendelea kutekelezwa kulingana na fedha ambazo tunazipanga na kuhakikisha tunaenda na vipaumbele katika maeneo ambayo kuna mahitaji haya ya skimu za umwagiliaji. Hivyo, tuwaondoe hofu Waheshimiwa Wabunge na wananchi kwamba Serikali itatekeleza miradi yake na mipango yake kwa kadri ambavyo tunapanga kwenye mipango ya kila mwaka wa fedha wa bajeti, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Skimu ya Bukangilija na Masela ni lini itaanza kujengwa Wilaya ya Maswa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, skimu zote ambazo ziko kwenye mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 na pia hata hizo mpya ambazo tunaendelea kuzipata zitawekwa kwenye mipango ya bajeti na hivyo zitajengwa kwa kadri ambavyo tumepangia kwenye mipango yetu ya Serikali pamoja na skimu aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge, nayo pia itaweza kufanyiwa kazi kadri ambavyo Serikali itakuwa imejipanga, nakushukuru sana.
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi ya swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale Kijiji cha Makangaga, Kata ya Kiranjeranje Jimbo la Kilwa Kusini, kuna skimu ya umwagiliaji ambayo imetelekezwa kwa muda mrefu: Je, Serikali ipo tayari kupeleka wataalamu pale Makangaga ili wakafanye upembuzi yakinifu na hatimaye skimu hii iweze kufufuliwa mara moja?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Serikali itapeleka wataalam waweze kutathmini hiyo skimu na kuona gharama na mahitaji halisi ili iweze kuboreshwa na iweze kutoa tija kwa wakulima wanaotumia skimu hiyo, nakushukuru sana.
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Mkoa wa Rukwa, Wilaya ya Kalambo, Tarafa ya Mwimbi kuna mito mingi sana ya kutosha: Je, Serikali ina mpango gani wa kuendeleza kilimo cha umwagiliaji katika tarafa hiyo? Ahsante (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA (K.n.y. WAZIRI WA KILIMO): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Azma ya Serikali ni kutumia vyanzo vyote vya maji vilivyopo, ikiwemo mito ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya kuhakikisha skimu za umwagiliaji zinafanya kazi. Kwa hiyo, katika maeneo ambayo tutaendelea pia kuyafanyia kazi ni mito hiyo iliyopo katika Jimbo la Kalambo ili kuhakikisha nayo inatumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji katika eneo husika ambalo Mheshimiwa Mbunge amelitaja, nakushukuru sana.
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa Serikali ilishachukua vipimo vya kujenga Bwawa la Iyongoma na bwawa hili ni muhimu sana kwa ajili ya kumwagilia Skimu ya Ndungu ambayo kwa muda mrefu imekuwa na matatizo: Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga bwawa hili?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kama ambavyo yeye mwenyewe amesema kwamba tayari kuna mipango inaendelea kuhakikisha tunalijenga hilo bwawa na wataalamu kama walishakuja kuangalia. Moja ya maeneo ambayo tutaangalia ni haya ambayo tayari yameshafanyiwa usanifu yakinifu ili yaweze kuanza kutekelezwa kadiri ambavyo tumepanga kwenye bajeti zetu za Wizara na kuhakikisha pia kama kuna miradi mingine ambayo itapelekea kukamilisha mabwawa haya nayo pia tutaangalia. Kwa hiyo, hili bwawa nalo litawekwa katika kipaumbele katika mipango ya Wizara, nakushukuru sana.
MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na ucheleweshaji wa ukamilishaji wa miradi mingi ya kimkakati ambayo inakuwa imeandaliwa na Serikali. Swali la kwanza; nataka kufahamu ni nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha miradi hii ya kimkakati inaisha kwa wakati? Mfano mzuri ni Mradi wa Chumvi, Momba, mpaka leo haupelekewi fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; nataka pia, kufahamu, kwa kuwa, kumekuwa na miradi mingi ambayo inaibuliwa ambayo inatumia fedha nyingi za Serikali na haiishi kwa wakati na mingine imekuwa na poor designing na allocation ya miradi kwa hiyo, pesa nyingi zinaenda zinakuwa hazileti tija kwa wakati. Ni nini mkakati wa Serikali wa kupunguza hasara inayotokana na miradi hiyo ambayo inakuwa imebuniwa chini ya kiwango? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Miradi mingi inayotekelezwa na Serikali ni kweli mingine inaweza kuwa na changamoto katika utekelezaji wake kutokana na sababu mbalimbali, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, miradi ambayo imeshawekewa mikakati maalum na ikatengewa fedha kwa wakati husika, tunatekeleza kwa wakati. Pale kunapokuwa na changamoto basi zinakuwa ni zile ambazo ziko nje ya uwezo ambao tumeupanga.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, Mbunge ametoa mfano wa Mradi wa Chumvi, Momba ni kwamba, huu ulibuniwa na Halmashauri, lakini na sisi kama Serikali Kuu tutaweka fedha hapo kama tulivyosema hapo awali, ili waweze kutekeleza mradi huo, lakini kwenye miradi mingine ambayo inatekelezwa kwa muda mrefu, Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeshatoa maelekezo kwamba, miradi ambayo imewekwa kwenye mipango lazima tuikamilishe kulingana na wakati na fedha nyingi zitatolewa kadiri ambavyo Serikali inapata, ili kuhakikisha tunaondokana na ucheleweshaji katika miradi husika, nakushukuru.
MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Halmashauri ya Mji wa Mafinga imetenga eneo la ekari 750 kwa ajili ya Industrial Park ili tuweze kuwa soko la kimataifa la mazao ya misitu; je, Serikali iko tayari kushirikiana na sisi kupitia EPZA kufanikisha ndoto hiyo ambayo itakuwa ni chanzo cha mapato na chanzo cha ajira?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Chumi, lakini Halmashauri ya Mafinga kwa kutenga maeneo haya ambayo ni mumhimu sana kwa ajili ya uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali tunathamini na tutahakikisha tunapeleka wawekezaji, lakini pia kusajili eneo hili chini ya uwekezaji, EPZA, ili mazao au bidhaa zinazozalishwa pale ziweze kuuzwa nje, lakini na ndani ya nchi katika kujiletea maendeleo katika Halmashauri ya Mafinga, lakini nchi kwa ujumla, nakushukuru sana.
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niulize swali la nyongeza. Kuelekea mwishoni mwa mwaka jana Serikali ilichukua hatua za kuweka mipaka ya kudumu eneo linalozunguka Uwanja wa Kimataifa wa KIA kwa lengo la kuweka miradi ya kimkakati. Je, ni miradi mingapi ya kimkakati na ni ya namna gani ambayo itajengwa kwenye eneo lile kwa sababu imechukua eneo kubwa sana takribani square kilometer 110? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Ni kweli lengo la Serikali ya Awamu ya Sita, kama nilivyosema chini ya Rais wetu mpendwa, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuona tunaongeza uwekezaji, kuvutia mitaji katika uwekezaji, uwekezaji wa ndani, lakini pia uwekezaji kutoka nje. Jambo hili linataka maeneo mahususi ambayo yameshaandaliwa tayari ili kupunguza ukiritimba na urasimu wa kutokupata maeneo ya uwekezaji kwa wawekezaji katika maeneo mengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, eneo hili la KIA linafanyiwa tathmini ili kuona miradi mahususi ya kimkakati ambayo itawekezwa katika eneo hili ambalo mwanzoni lilikuwa kidogo na changamoto ya kuingiliwa na watu. Kwa hiyo, Serikali inaendelea kufanya tathmini ili kuona miradi mahususi ambayo itawekezwa katika eneo hili la KIA, nakushukuru sana.
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali moja la nyongeza. Je, Serikali haioni umefikia wakati wa kuhamasisha wawekezaji wa ndani ili kusudi waweze kuzalisha mafuta yanayotokana na alizeti, ufuta, karanga, pamba, pamoja na mafuta yanayotokana na mifugo?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Ni kweli moja ya maeneo ambayo Serikali imeweka kipaumbele ni kuhamasisha uzalishaji wa mafuta kwa wazalishaji wa ndani, pamoja na kukaribisha wawekezaji kutoka nje, lakini mkakati mkubwa ni kwa wazalishaji wa ndani.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili tunalifanya kupitia, mosi kama nilivyosema, kuwawezesha wakulima ili kulima mbegu zenye ubora na zenye tija. Pili, tunatengeneza teknolojia rahisi, viwanda vidogovidogo ambavyo vitapelekea wananchi hawa wazalishaji wa ndani kuzalisha mafuta mengi, lakini yenye ubora kwa sababu, changamoto hapa si tu upatikanaji wa mafuta, lakini pia tunataka mafuta yenye ubora ambayo yatakuwa hayana athari hasi kwa walaji. Kwa hiyo, tunaendelea kuhakikisha tunawezesha teknolojia rahisi ili kuzalisha zaidi mafuta ya kula hapa nchini.
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu ya Serikali, nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; moja ya njia ya kutoa bei nzuri isiyotetereka ya zao la mkonge ni kuwa na nyuzi bora, kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri. Je, ni lini sasa Serikali itatekeleza ahadi yake ya kununua mashine za kuchakata mkonge, ili mazao ya mkonge, nyuzi zinazochakatwa ziwe na ubora ukizingatia kwamba, tuna changamoto kubwa ya uhaba wa mashine?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; katika kuimarisha soko la ndani, kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri, Serikali ilitoa agizo la kuzuia uingizaji wa kamba na nyuzi za plastic, lakini mpaka leo hali bado sio nzuri. Je, ni nini kauli ya Serikali juu ya kudhibiti uingizaji wa nyuzi na kamba za plastic kwenye nchi yetu?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya maeneo ambayo tunatilia mkazo ni kuwa na teknolojia sahihi ya kuzalisha bidhaa mbalimbali, ikiwemo nyuzi zinazotokana na mkonge. Katika jitihada hizo tumeshaweka bajeti kwa ajili ya kununua mashine hizo za kisasa ambazo ziliahidiwa, lakini zaidi kupitia taasisi zetu za ubunifu, TEMDO, kuna mashine inaandaliwa ambayo nayo itasaidia kuchakata mkonge, ili kupata nyuzi bora na zenye tija kwa ajili ya kuhakikisha tunapunguza uingizaji wa nyuzi mbadala za plastic kutoka nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kuzuia uingizaji wa nyuzi za plastic kama unavyojua ni kweli, bado mahitaji ni makubwa zaidi ya bidhaa hii kuliko uwezo wa kuzalisha wa ndani, kadri tunavyoendelea kuimarisha uzalishaji wa nyuzi za mkonge naamini tutapunguza hilo gap na pale tutakapokuwa tumejitosheleza, maana yake hii marufuku itaisha ili kuhakikisha hatuagizi tena nyuzi za plastic kutoka nje, nakushukuru. (Makofi)
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha bei ya zao la kahawa kwa wakulima wanaolima kahawa aina ya Arabika na Robusta? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Prof. Ndakidemi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli moja ya maeneo ambayo Serikali inaangalia kwa ukaribu sana ni kuona namna gani tunaboresha bei ya mazao ya kilimo ikiwemo Kahawa katika nchi hii. Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunaendelea kuongeza uwekezaji. Mosi, uwekezaji wa viwanda vya kuchakata zao la Kahawa. Pili, kuona tunafungua masoko ili wananchi hawa ambao wanazalisha, hata wale ambao hawajaongeza thamani waweze kuuza popote. Kwa hiyo, maana yake kupitia hiyo najua bei yake itaongezeka kwa sababu mahitaji yatakuwa makubwa kwa hiyo bei nayo itapanda. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Iringa ni kati ya Mikoa iliyohamasisha kulima kwa wingi zao la parachichi, changamoto inayowakabili ni bei kubwa sana ya miche ya mbegu. Je, ni lini Serikali itaona umuhimu hata kuwapatia miche ya ruzuku ili wananchi waweze kulima kwa wingi zaidi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali yetu ya Awamu ya Sita kama nilivyosema, chini ya Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeongeza fedha nyingi sana kwenye sekta hii ya kilimo na ninyi ni mashahidi kutoka billioni 200 mpaka karibu trilioni moja sasa. Moja ya maeneo ambayo yameangaliwa ni kuongeza ruzuku kwenye uzalishaji wa miche ya mazao mbalimbali ikiwemo parachichi. Hii tayari tumeshaweka na kule Iringa tayari pale Kilolo kuna miche ambayo inazalishwa kwa ajili ya ruzuku.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni muda tu kwamba wakulima wawasiliane na Idara ya Kilimo katika Mkoa wa Iringa ili waweze kupata miche ya ruzuku kwa ajili ya kupanda zao hili la parachichi. Nakushukuru. (Makofi)
MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni muda mrefu sasa wastaafu hawa tokea waliostaafu kipindi cha miaka ya 2020 hadi 2021. Ni bajeti gani ambayo imepanga fedha hizo kupewa wastaafu hawa. Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, kama nilivyosema, wastaafu jumla walikuwa 624, ili kulipa madeni haya lazima kufanaya uhakiki. Kama nilivyosema, tumeshahahikiki tayari wastaafu 579 ambao ndiyo jumla ya fedha hizo ambazo zimepangwa katika mwaka wa fedha kulipwa, ambazo ni shilingi 806,067,788.02. Hao wengine waliobakia nao tunaendelea na uhakiki ili kujiridhisha kwamba tunalipa stahiki zao bila kumpunja mstaafu yeyote katika Jeshi la Polisi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Serikali inahakikisha itatenga hizi fedha ili kuwalipa baada ya uhakiki huu kukamilika. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na fedha za wastaafu lakini kumekuwa na changamoto kubwa kwa watumishi wanaofanya kwenye Wizara hiyo, wanapohama kutokulipwa madai yao ya uhamisho kwa wakati.

Je, Serikali ina utaratibu gani wa kuhakikisha inawalipa kwa haraka? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Ni kweli moja ya changamoto zinazotokea pale kunapokuwa na uhamisho ambao haukuwepo kwenye bajeti kwa mwaka husika. Nakuhakikishia kwamba, uhamisho wote ambao umefuata taratibu kamili, wote watalipwa na hasa hii inatakiwa baada ya kuhakiki gharama hizo na kuingiza kwenye bajeti ya mwaka husika, watumishi hawa wanaohama wanalipwa stahiki zao kama ambavyo wamestahili. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali la nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itakuja kumaliza migogoro iliyopo kati ya Gereza ya Urambo na wananchi wanaozunguka gereza hilo ambapo migogoro imedumu kwa muda mrefu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba hili lije kama swali au kama atataka takwimu tutampa.
MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Tunajua mtumishi kabla hajastaafu ana miezi sita ya kumwandaa kustaafu. Je, ni nini sasa tamko la Serikali kuandaa mapema hayo malipo ya kusafirisha mizigo ya wastaafu ili wasiendelee kunyanyasika kama ilivyo sasa hivi?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kama nilivyosema mwanzo ni kweli moja ya changamoto ambazo huwa zinakuwepo ni kwa wale ambao wanastaafu lakini bado kwenye bajeti yetu hatujaweka. Kwa sababu, ni kweli kwamba wanaostaafu wanajulikana, dhamira ya Serikali yetu ni kuhakikisha wote wanalipwa kwa wakati.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunahakikisha kila unapotokea mwaka husika ambao wanaastafu wanawekwa kwenye bajeti za Serikali ili kulipwa kwa wakati bila kufanya ucheleweshwaji wowote kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge amesema. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la watu wanaostaafu kuchelewa kulipwa mizigo ni kubwa, hata kwenye Ripoti za CAG ipo na tatizo la uhamisho na lenyewe ni kubwa. Kwa Mkoa wa Mara, kuna watu ambao hawajalipwa huu ni mwaka wa tatu mpaka wa nne mfululizo ikiwemo na Wilaya ya Bunda.

Je, ni lini Serikali mtalipa madeni ya mizigo na uhamisho kwa waataafu wa Mkoa wa Mara? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Ninaomba niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba Serikali ina dhamira njema ya kuhakikisha wastaafu wanalipwa stahili zao kwa wakati, ikiwemo usafirishaji wa mizigo na mafao yao ya kustaafu. Kwa hiyo, moja ya maeneo ambayo tunaweka msisitizo ni kuhakikisha kila mwaka wa bajeti tunaweka bajeti ya kutosha ili kufidia madeni ya nyuma. Pili, kuhakikisha wale wanaostaafu katika mwaka husika wanalipwa kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nawahakikishia Waheshimiwa Wabunge kwamba, Serikali itaendelea kuwalipa kwa wakati kadri ambavyo fedha zitapatikana katika bajeti ya kila mwaka. Nakushukuru sana.
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kutokana na changamoto ambayo imeendelea kujitokeza kwa Askari wetu wanapostaafu kucheleweshewa mafao yao, kwanini Serikali sasa isije na mpango wa kufanya uhakiki angalau mwaka mmoja kabla ili mtumishi au askari anapostaafu apate mafao yake pamoja na fedha za usafiri? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Sisi tunalichukua hili na ni maeneo ambayo tunayafanyia kazi kama nilivyosema kuhakiki mapema. Mosi, madeni na Pili, mahitaji ya mwaka husika ili kupunguza ucheleweshaji huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali tunalifanyia kazi hili kama ambavyo wamesema na tunahakikisha tunafanya hivyo ili kupunguza adha kwa wastaafu hawa katika maeneo yote. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

Swali la kwanza; kwa kuwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi unaongeza changamoto za kiusalama katika maeneo yetu na kwa kuwa tulikubaliana kuwa na Polisi Kata, Polisi Kata ambao hawana vituo itakuwa ni sawa na bure. Ni nini mkakati wa Serikali sasa kujenga Vituo hivi vya Polisi katika maeneo ya pembezoni, ikiwemo Mkiwa na Misughaa pamoja na Mungaa ili kuweza kusaidia ulinzi na kwa sababu wananchi wameshafyatua matofali 1000 katika Kata ya Mkiwa na mimi kwenye Mfuko wa Jimbo nimeanza kuwaunga mkono. Ni nini Serikali itafanya kwa ajili ya kutusaidia kumalizia ujenzi huo? (Makofi)

Swali la pili; Askari wetu wanafanya kazi nzuri sana na maeneo mengi hawana nyumba za kuishi, wanakaa mtaani. Ni nini mkakati wa Serikali hususan kwenye Wilaya ya Ikungi, ambayo hatuna nyumba hata moja ya Askari, hata Mkuu wa Polisi Wilaya anaishi mtaani.

Ni nini mkakati wa Serikali kuwajengea makazi Polisi wetu. Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, Nakushukuru. Naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema awali, tunapongeza sana juhudi za Mheshimiwa Mbunge lakini na wananchi wa Jimbo kwa kuanzisha ujenzi wa Vituo hivi vya Polisi katika Kata hizo ambazo amezitaja. Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha tunaunga mkono juhudi za wananchi ili kuhakikisha tunakamilisha ujenzi huo. Katika hili tuwasiliane na Wizara ili kuhakikisha tunakamilisha majengo hayo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja na wameanza kufanya kazi kwa ajili ya kujenga na kukamilisha vituo hivyo vya Polisi Kata. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, moja ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuimarisha ulinzi na usalama ni kuona Askari wanaishi katika maeneo stahiki na yenye tija au hali nzuri katika maeneo ya kazi. Kwa hiyo, moja ya maeneo ambayo inaangalia ni kujenga nyumba za Askari katika maeneo yote ikiwemo katika Kata hii. Kwa hiyo, katika mipango ya Serikali ni kuona tunaendelea kujenga makazi ya Askari Polisi na Watumishi wengine ambao wanastahili kupata nyumba hizo ili waweze kufanya kazi zao kwa ubora zaidi. Nakushukuru. (Makofi)
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona.

Kwa kuwa, Kituo cha Polisi cha Nyang’hwale hakina hadhi na ni kidogo na kimechakaa. Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi cha kisasa cha Wilaya hapo Nyang’hwale?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Ni kweli maeneo mengi vituo vya Polisi ikiwemo hiki cha Nyang’hwale ni vya muda mrefu, kwa hiyo vimechakaa. Kama nilivosema, moja ya maeneo ambayo Serikali tunaweka mkazo ni kuboresha vituo hivi vya Polisi, hicho ni mojawapo ya Kituo cha Polisi ambacho tutaangalia namna ya kukirekebisha, kukarabati kadri ambavyo fedha zitapatikana. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itajenga nyumba za Askari Wilaya ya Itilima, Mkoa wa Simiyu?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo umesema ni kweli Serikali inajua umuhimu wa kuwa na vituo hivi vya Polisi, kwa hiyo, katika bajeti zake tutaendelea kutenga fedha ili kuhakikisha maeneo haya yote yanajengewa vituo vya Polisi, kadri ya muda utakavyohitajika. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Kwanza nashukuru sana kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Swali la kwanza; kwa kuwa sasa Serikali imekiri kwamba gunia sio kipimo ni kifungashio. Je, Serikali iko tayari sasa kutoa waraka na kupeleka kwa Wakala wa Vipimo na Halmashauri zote nchini kuzuia tabia ya kushusha magunia katikati ya safari na kuanza kuyapima barabarani?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kuna mazao kama mbogamboga, matunda na viazi yamekuwa yakipimwa kwenye soko kwa kilo, lakini shambani yamekuwa yakipimwa kwa magunia. Je, Serikali iko tayari sasa kutoa kipimo cha awali kwa ajili ya mazao ya aina hiyo, namna ambavyo yanaweza kupimwa yakiwa shambani?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza namshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa kutoa concern ya wenzetu wa Halmashauri na Wakala wa Vipimo kukagua magunia au mazao yanayopita katika sehemu mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tumeshasema kwamba, kama wananchi wameuza kwa vipimo na kukawa na uthibitisho wa kwamba mazao yale kama either yamefungashwa katika magunia au katika vifungashio (vibebesheo) vyovyote kama vina uthibitisho kwamba yameuzwa kwa vipimo, wale wanaokagua aidha Wakala wa Vipimo au Halmashauri watumie zile risiti au vielelezo vyovyote (evidence) ili ziwe ni sehemu ya kupunguza usumbufu kwa wananchi, wakulima au wafanyabiashara wanaposafirisha mazao badala ya kupima kila gunia kwenye maeneo ya ukaguzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kuhusiana na suala la mbogamboga. Haya bado ni maelekezo, katika mazao yote kwamba, katika maeneo mengi tunahamasisha wakulima wajiunge katika Vyama vya Msingi au wauzie kwenye masoko ambako kule sisi tumeshaelekeza Wakala wa Vipimo wapeleke mizani ili itumike kupima uzito wa bidhaa inayouzwa badala ya kutumika vifungashio vya namna yoyote ile ambavyo havitumii vipimo sahihi, nakushukuru sana.
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Spika, majibu ya Serikali kidogo yana changamoto kwa wastaafu hawa wa Afrika Mashariki, kwa sababu wastaafu hawa wamefungua kesi na ni imani yangu kwamba Serikali inafahamu kesi ya wastaafu hawa.

Je, Serikali iko tayari kuwaeleza wastaafu hawa kwamba malipo yao yalishalipwa na waache kushughulikia kesi yao?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; wazee hawa wamekuwa wakihangaika kwa muda mrefu kufuatilia malipo haya lakini Serikali inasema imewalipa mpaka mwaka 2016 madeni haya yameshalipwa. Sasa Serikali hawa wazee wanadai kitu gani mpaka wamekuwa wakihangaika mpaka kufungua kesi mbalimbali katika mahakama tofauti ili wapate stahiki zao?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, ni kweli kama alivyosema wastaafu hawa ambao kwa kweli kimsingi kama nilivyosema kwenye jibu la msingi walishalipwa na imekuwa ni tendency au kawaida kila kunapokuwa na Serikali mpya au regime mpya wanafungua madai katika mahakama yetu kudai malipo, lakini kimsingi Serikali tumeshasema na tunaelekeza tena kwamba kwa kweli waelewe kwamba walishalipwa na hakuna kingine zaidi kwa sababu tayari tulishamaliza kama nilivyosema. Kwa hiyo, wasiendelee tena na madai ambayo kimsingi hayana ukweli.

Mheshimiwa Spika, wastaafu hawa hawadai chochote kama nilivyosema walishalipwa kila kitu na tunachoendelea kulipa sasa ni pensheni kwa wale wachache ambao wanastahili kulipwa pensheni, nakushukuru. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi ni kuweka tu msisitizo kwamba wananchi wetu wana haki ya kwenda mahakamani wanapoona wanaweza wakapata haki zaidi, lakini kwa maana ya Serikali ilishahitimisha mchakato huu kwa barua na waliandikiwa barua ya tarehe 31 Desemba, 2013 ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha wanayo, lakini hiyo haizuii wananchi kuwa na haki ya kwenda mahakamani. Kwa hiyo, Serikali haiwezi kuzuia wananchi kwenda mahakamani, lakini kwa maana ya mchakato ulishafanyika, ukahitimishwa kwa barua na iliandikwa, ahsante.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Spika, ahsante; je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia na kuharakisha malipo ya waliokuwa wafanyakazi wa mashamba ya maua ya P Floral ili kupisha mwekezaji mpya? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, nitamwona Mheshimiwa Zaytun Swai pia kama itakuwa kuna ulazima basi alete swali la msingi.

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Spika, ahsante, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa Mkoa wa Rukwa ukepakana na maziwa mawili likiwemo Ziwa Tanganyika na Ziwa Rukwa. Serikali ina mpango gani wa kuanzisha uvuvi wa vizimba katika maziwa hayo, ili kupata malighafi ya samaki kwa wingi?

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili; nilitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kukiendeleza Kiwanda cha SAAFI kilichopo Mkoa wa Rukwa ambacho kilianzishwa na Hayati Chrisant Mzindakaya? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, kwanza nimshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kutambua umuhimu wa ufugaji wa samaki kwa njia ya kisasa, kwa maana ya vizimba katika Maziwa ya Rukwa na Tanganyika.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi tayari imeshaanza zoezi hilo. Tumeanza katika Mkoa wa Mwanza kwa maana ya Ziwa Victoria, tayari tunafuga kupitia vizimba. Kwa hiyo, nitoe wito kwa wataalamu wetu waweze kutembelea kwenye maziwa haya kwa kushirikiana na Mheshimiwa Mbunge, ili waweze kuanzisha ufugaji wa samaki kupitia vizimba katika Ziwa Rukwa na Ziwa Tanganyika na ninakuomba Mheshimiwa Mbunge uweze pia, kushirkiana nasi ili uweze kuwa kinara katika ufugaji huu wa kisasa wa samaki.

Mheshimiwa Spika, pili; kuhusiana na kiwanda hiki cha Sumbawanga Agricultural and Animal Food Industries Limited kwa maana ya SAAFI, changamoto kubwa ilikuwa ni fedha na uendeshaji wa kiwanda hiki ambacho ni kiwanda cha kisasa sana hapa nchini. Serikali tayari imeshaanza kupitia Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIDB), kutafuta mwekezaji mpya baada ya changamoto zilizokuwepo kwa mwekezaji yule wa mwanzo.

Kwa hiyo, tumeshatangaza tayari kupitia gazeti mwezi wa Agosti, kupata mwekezaji mpya ili aweze kuingia ubia na waliopo ili kuhakikisha kiwanda hiki kinafufuliwa, nakushukuru.
MHE. ESTHER E. MALEKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, katika kutekeleza Sera ya Tanzania ya Viwanda, nini mkakati wa Serikali kufufua viwanda vilivyopo katika Mkoa wa Kilimanjaro ili kuwapatia wananchi wetu ajira, lakini pia kuongeza uchumi wa Mkoa wetu wa Kilimanjaro? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kama nilivyosema nia ya Serikali ni kuhakikisha tunaendelea kutekeleza sera ya kuwa nchi ya viwanda na kama tulivyosema tuwe na uchumi unaoendeshwa na viwanda hapa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, tumeendelea kutafuta wawekezaji kwa sababu, tunaondokana na uchumi hodhi, kwa maana ya Serikali kufanya biashara au kuendesha viwanda. Kwa hiyo, Mkoa wa Kilimanjaro na Mikoa mingine ambako kuna viwanda vyenye changamoto, vile ambavyo vitakuwa vimebinafsishwa, lakini havijaendelezwa au vingine ambavyo tunaona havifanyi kazi, tutaendelea kutafuta wawekezaji kwa kuweka kwenye masharti nafuu, pia vivutio mbalimbali ili kuvutia uwekezaji wa ndani, hata wawekezaji kutoka nje ili kuhakikisha viwanda hivyo vimefanya kazi na kupunguza nakisi ya bidhaa mbalimbali ambazo zinatumika nchini kuagizwa nje, lakini pia kutoa masoko kwa malighafi ambazo zinatumika kwenye viwanda hivyo ambavyo vinzalishwa hapa nchini, nakushukuru.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Nataka kumweleza Mheshimiwa Waziri kwamba suala la pombe za kienyeji ni kwa lengo la kulinda viwanda vyetu vya ndani pia kulinda ubunifu wa watu wetu, kuongeza ajira na kuongeza uchumi kwa ajili ya kulinda mawazo ambayo yamezalishwa na wananchi wetu. Naomba kuuliza maswali ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, toka nimechangia hoja yangu ni mwezi umepita sasa. Je, ni upi mkakati wa Serikali kwa mwezi huu mmoja mmeshaanza kuzipatia leseni zile pombe ambazo mmezikataza kutumika kwenye jamii, mfano gongo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Je, kwa nini Serikali isiongeze kodi kwenye pombe zote ambazo zinaingizwa kutoka nje mithili hiyo ya spirit na pombe zingine ili kuzipa thamani pombe zetu za ndani na kuwavutia wawekezaji wote waje wawekeze kwenye pombe zetu za ndani ili tulinde soko letu la ndani na mawazo ambayo yametokana na watu wetu wa ndani? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni kweli tunajua mchango mkubwa sana wa sekta hii ya pombe na hasa pombe za kienyeji ambazo akina mama wengi ndiyo wanashiriki huku kama wajasiriamali kutengeneza pombe hizi za kienyeji na ndiyo zimekuwa nguzo na msingi mkubwa kulea familia katika kaya nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mkakati madhubuti na ndiyo maana nimesema tumeshaweka mikakati mojawapo ni kuona namna gani tunawasaidia kuwafundisha na kuwawekea teknolojia sahihi ili waweze kuzalisha pombe za kienyeji zinazokidhi viwango na ambavyo vitakuwa havina madhara kwa wanywaji. Kupitia TBS kwa maana ya shirika la viwango na SIDO tumeshaweka fedha katika bajeti ambayo itatumika kama ruzuku kuwafundisha, kuwafuata kwanza wazalishaji wa pombe hizi za kienyeji kule waliko vijijini lakini kuwafundisha namna ya kuzalisha pombe ambazo zinakidhi viwango ili ziweze kuendelea kutumika katika maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia zile pombe ambazo zilikuwa na madhara ambazo ndiyo wanasema zimepigwa marufuku tunataka tuwasaidie ili athari ile isijitokeze na baada ya hapo zitaruhusiwa kuendelea na kupewa ithibati ya ubora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, Serikali inafanya juhudi mbalimbali na hili ni dhahiri kwamba katika kuhakikisha tunafungua uchumi wa nchi yetu ni pmoja na kuruhusu biashara huru kulingana na taratibu na kanuni zilizopo, kwa maana ya kurusu pia bidhaa kutoka nje ya nchi kama vile ambavyo sisi tunauza nje ya nchi bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vyetu. Kwa hiyo, tunaendelea kuweka mkakati madhubuti kulinda viwanda vya ndani pale ambapo tutaona kwamba vinatakiwa kufanya hivyo na tumeshaanza kufanya na katika sekta hii ya pombe pia tutafanya hivyo ili kuwasaidia wananchi kunyanyua kipato lakini kuinua uchumi wa nchi yetu. Nakushukuru.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri aliyoyatoa. Nilitaka tu nimpe uhakika Mheshimiwa Mbunge kwamba tumelipokea wazo lake la kuongeza kodi kwenye pombe na tutakamilisha kufanyia kazi na tutatoa majibu tutakapokuwa tunatoa kauli ya Serikali kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka huu. (Makofi)
MHE. MWANTUMU DAU. HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante. Nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake ya Serikali aliyoyatoa. Nina maswali yangu mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kilimo BBT kwa vijana, Serikali ina mpngo gani wa kuja na BBT kwa wanawake wasiyosijiweza? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili je, Serikali haina umuhimu wa kuhakikisha mikopo hii inawafikia wanawake hao? (Makofi)
NAIBU WAZIRI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mwantumu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli moja ya changamoto tulizonazo ni kuona namna gani ya kuwawezesha wanawake wawe na kesho nzuri kama ambavyo kuna programu hii ya kesho nzuri kwa vijana kwenye sekta ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani hili ni wazo zuri ili kuona namna gani tunawasaidia wanawake ambao ndio wana mchango mkubwa sana katika uchumi wa nchi hii. Nadhani kama Serikali tunachukua hili ili tuweze kuja na programu maalum yenye mlengo huo kwa ajili ya kuhakikisha wanawake wanakuwa na kesho nzuri kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la pili, ni dhahiri kweli Serikali tumeshaona changamoto zilizojitokeza kwenye mifuko mbalimbali ikiwemo ile 10% ilikuwa inatengwa na Halmashauri kwamba ilikuwa haiwafikii walengwa wakiwemo wanawake kutokupata kwa wakati na mambo mengine mengi. Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo tupitie upya namna ya kuhakikisha mifuko hii inawasaidia na hasa wanawake waweze kupata fedha zile kwa wakati, lakini kulingana na mahitaji yao. Sasa tunaangalia kwa namna ya pekee zaidi wanawake wasiojiweza ili waweze kupata mikopo au uwezeshaji huu kwa wakati kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameshauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Je, Serikali imefanya tathmini kujua kama majukwaa ya wanawake yanaleta tija katika wilaya zetu?

NAIBU WAZIRI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Komanya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, majukwaa haya ya wanawake katika mikoa yamekuwa na tija kubwa, kwa sababu ndio ambayo yamepelekea wanawake wengi kupata mikopo, lakini pia kuwa na elimu ya ujasiriamali katika maeneo tofauti tofauti. Changamoto tuliyonayo ni kuona sasa tunawezesha zaidi majukwaa haya ya wanawake ili kuweza kupata mikopo kwa wakati, lakini yenye kutosheleza mahitaji yao kadri ambavyo wanaomba. Kwa hiyo kuna tathmini ya kutosha ambayo tunaifanya ili kuona namna gani zaidi ya kuendeleza majukwaa haya ya wanawake katika mikoa.
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kuuliza swali moja la nyongeza ambalo linasema hivi, kwa wale wanawake wanaofanya kazi maofisini, lakini kipato chao kidogo. Je, mnawawezesha vipi katika na wao kufanikisha masuala yao ya kuweza kujinyanyua kiuchumi? (Makofi)

NAIBU WAZIRI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni kweli, kuna wanawake ambao wanafanya kazi maofisi lakini mishahara yao kidogo haitoshi na hii ni kwa watumishi walio wengi, Serikali na hata katika sekta binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna programu mahususi na Serikali wanafanya kwa wakati fulani kuhakikisha wanawapa upendeleo maalum kuwakopesha wakati mwingine mikopo ambayo haina riba. Pia kupitia ajira hizi watumishi hawa huwa wanapata kipaumbele kukopa katika taasisi za fedha, lakini pia wanaanzisha vikundi au SACCOS ambazo zenyewe zinawasaidia kujiwezesha kiuchumi au kupata fedha za ziada kwa wanawake ambao wanakuwa hawana uwezo au ambao mishahara yao ni kidogo katika maofisi yetu.
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Napenda kujua Serikali inawasaidiaje wanawake wa Mkoa wa Simiyu ambao hawajiwezi kiuchumi na ambao hawapo kwenye mpango wa TASAF?
NAIBU WAZIRI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni kweli, katika mikoa au majimbo mengi ikiwemo Simiyu kuna wanawake wengi ambao hawana uwezo, hawajiwezi, lakini hawako kwenye ule mpango wetu wa TASAF. Moja ya maeneo ambayo tunayaangalia sasa kama nilivyosema ni kupitia zile 10% ambazo tunaweza kuzifanyia kazi na kuunganisha baadhi ya mifuko ambayo ilikuwa haiwafikii walengwa, ili tuone hawa ambao hawako kwenye TASAF lakini wana uhitaji maalum kama swali la msingi ulilouliza waweze nao kunufaika na fedha hizi za Mifuko ambayo itawasaidia kuweza kuanzisha shughuli mbalimbali za kijasiriamali, lakini pia kuinuka kiuchumi katika shughuli zao za kila siku.

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri. Kwa kujua kwamba Wilaya ya Same ina madini mengi ya gypsum hasa kwenye Kata za Bendera na Makanya na kwa kujua kwamba gypsum inaweza kuwa na products nyingi ambazo zitatengeneza ajira kubwa katika viwanda hivyo. Je, Serikali ina mpango gani wa kusaidia wananchi wa Wilaya ya Same kupata wawekezaji ili waweze ku-process ile gypsum wa-add value? (Makofi)
NAIBU WAZIRI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Naghenjwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli moja ya maeneo ambayo tunayaangalia ni kuhamsisha uwekezaji katika sekta nyingi ikiwemo hii ya madini na hasa ya gypsum ambayo inatumika katika maeneo mengi kwenye ujenzi na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanawake najua ndio wanashiriki sana katika shughuli za kiuchumi kama nilivyosema tutaona namna ya kukaa na Mheshimiwa Mbunge ili tuone kama kunakuwa na andiko kwa ajili ya Wilaya ya Same ambayo litavutia mahususi uwekezaji wa viwanda katika sekta hii kwa maana ya kuzalisha gypsum na shughuli nyingine za kiuchumi au viwanda vingine katika Jimbo la Same.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri, je, SIDO imepotelea wapi kwa sababu kwenye Jimbo letu sijawahi kusikia SIDO, iko wapi?
NAIBU WAZIRI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Naomba nijibu swali la Dkt. Kimei, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, SIDO bado ipo na inaendelea kufanya shughuli zake, changamoto tuliyonayo ni mtaji mdogo wa kuweza kutoa huduma kama ilivyokusudiwa na shirika letu la kuendeleza viwanda vidogo na biashara ndogo Tanzania. Sasa tutakuja na sheria mahususi ili tuone namna gani ya kuiwezesha SIDO iweze kufanya shughuli zake kibiashara badala ya kutoa huduma ambayo inahitaji mtaji zaidi wa Serikali. Kwa hiyo tunadhani huu utakuwa ndio ufumbuzi ili waweze kuendesha shughuli zao kibiashara ili kuwafikia wajasiriamali wengi na wenye viwanda wengi zaidi kadri ambavyo uchumi wa sasa unataka.

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi. Wilaya ya Chemba ni Wilaya ambayo ina maeneo mazuri na ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji, lakini bahati nzuri sana tupo katikati ya Barabara ya c2c. Wizara ya Uwekezaji ina mpango gani wa kuwekeza kwenye Wilaya ya Chemba ambayo iko karibu kabisa na Makao Makuu ya Nchi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
NAIBU WAZIRI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mheshimiwa Monni ni kweli Chemba ni sehemu ya kimkakati kwa sababu iko katika barabara Kuu tunasema South – North Corridor ambayo tunaamini sasa kwa kufungua njia hizi kutakuwa na fursa nyingi za uwekezaji katika maeneo ya Chemba kama ilivyo Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie kwamba Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuwatafuta wawekezaji, lakini nitumie fursa hii kumwomba Mheshimiwa Mbunge kushirikiana na halmashauri kuanza kutenga maeneo mahususi kwa ajili ya uwekezaji ili tunapopata wawekezaji wasipate kikwazo kwa maana ya kupata ardhi ambayo iko tayari kwa ajili ya uwekezaji katika sekta mbalimbali katika Jimbo la Mbunge.
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Swali la kwanza; lini Serikali italipa fidia ya Mradi wa Makaa ya Magangamatitu na Katewaka, Wilaya ya Ludewa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Mheshimiwa Rais amefanya kazi kubwa sana ya kupitia upya Mradi huu wa Liganga na Mchuchuma, amekwenda mpaka China sambamba na kulipa fidia. Sisi tunataka kujua, majadiliano na mwekezaji yamefikia hatua gani, lakini tunataka kujua vile vile mkataba utasainiwa lini ili mradi huu uanze kufanya kazi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kuhusu suala la fidia kwa Mradi wa Magangamatitu na Katewaka kwa sababu tumeshaanza kulipa fidia kwenye mradi mkubwa, tukikamilisha zoezi hili maana yake zoezi litakalofuata ni kuangalia tena miradi hii ya Magangamatitu na Katewaka ili kuona nako fidia zinalipwa kwa wananchi wanaopisha miradi hiyo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, Serikali inatambua umuhimu wa Mradi huu mkubwa wa Liganga na Mchuchuma ambao kwa kweli utakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa letu. Kama alivyosema Mbunge, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafanya kazi kubwa sana, Rais Samia Suluhu Hassan, kupitia Diplomasia ya Kiuchumi tumeweza kufikia hatua nzuri sana kuweza kukamilisha majadiliano na hawa wawekezaji ambao mwanzoni walikuwa hawaji kwenye majadiliano.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nimhakikishie kwamba juhudi zinazochukuliwa na Rais wetu mpendwa, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha mradi huu unaanza mapema ziko kwenye hatua nzuri na tunaamini majadiliano haya sasa yatakamilika mapema kwa sababu nao wameanza kuonesha nia ya kutekeleza mradi bila kuleta vikwazo au vivutio vile ambavyo walikuwa wanadai mwanzo ambavyo vina hasara kwa Taifa letu, nakushukuru.
MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ikiwa haya ndiyo majibu ya Serikali.

Je, Serikali iko tayari sasa kutengeneza kitu kinachoitwa Program and Plan of Action kikionesha tarehe na miezi na mwaka kuelekea kuanzishwa kwa mradi huu badala ya kusema tu majadiliano yanaendelea? Watupe commitment ya Serikali. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kama nilivyosema ni kweli tumekuwa na majadiliano ya muda mrefu na sababu kubwa ilikuwa ni upande wa pili kwa maana ya huyu mwekezaji ambaye kidogo alikuwa haji kwenye majadiliano kwenye vikao. Sasa kama nilivyosema, Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshaweka mahusiano mazuri na nje wanakotoka wenzetu wawekezaji hawa. Kwa hiyo tunaamini sasa kwa sababu wameshaanza kuja maana yake tutafikia muafaka karibuni, halafu tutatoa hiyo programu kwamba schedule ya utekelezaji wa mradi huu itakuwaje, nakushukuru.

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuniona. Naomba tu nimuulize Mheshimiwa Waziri. Kwa kuwa Mradi huu wa Liganga na Mchuchuma awali ulikuwa unaipa Serikali ya Tanzania 20% na 80% ilikuwa inakwenda kwa mwekezaji wakati uwekezaji wake ulikuwa ni dola milioni 600 tu kati ya dola bilioni tatu zilizokuwa zinahitajika. Je, Serikali imeweka mkakati gani wa dhati wa kuhakikisha kwamba sisi tunanufaika zaidi ukizingatia kwamba chuma cha Liganga ni jiwe ambalo liko juu wala huchimbi unafanya kukata tu kama keki ya harusi? (Kicheko)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ni kweli mradi huu gharama yake jumla kwa tathmini za wakati ule ilikuwa ni bilioni tatu, mwekezaji huyu katika mkataba ule wa awali alikuwa awekeze kwa maana ya fedha kianzo dola milioni 600.

Mheshimiwa Spika, tunaamini katika majadiliano ambayo tunaendelea nayo sasa tutaona namna gani sasa kuhakikisha mwekezaji huyu anaweka fedha au mtaji wa kutosha ili sisi kama nchi tuweze kunufaika, zaidi katika mkataba huu hatuweki fedha yoyote lakini zaidi kupitia sheria zetu tutakuwa wanufaika wakubwa kwa sababu zile asilimia 20 ni interest ambayo sisi kama nchi hatuwekezi fedha bali kutokana na utekelezaji wa mradi huu sisi hizo ni asilimia ambazo tayari Serikali tunapata bila kuingiza mtaji wowote katika mradi huu.
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, majibu ya Waziri yananipa wasiwasi, kwa sababu mimi nimekuwa Mjumbe wa Kamati ya Viwanda na inavyosemekana kwamba huyo mwekezaji wa kwanza ana matatizo na Serikali, inaonekana kwamba uwezo wake haupo. Sasa majibu ambayo anatupa Waziri ni ya Mkandarasi mwekezaji mpya au mwekezaji wa kwanza?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ni kweli Mkandarasi huyu baada ya kutokutekeleza mradi huu kwa wakati kulingana na mkataba ule wa awali, Serikali tuliweza kufanya ufuatiliaji wa uwezo wa mkandarasi huyu. Kweli katika moja ya vitu ambavyo vilionekana ni kwamba alikuwa na uwezo mdogo, lakini baada ya majadiliano ya hivi karibuni amesema anaweza kufanya lakini bado tunaendelea kuona kama kuna mwekezaji mwingine ambaye anaweza kuwekeza baada ya kumalizana na huyu aliyeko mwanzo kama atashindwa.

Mheshimiwa Spika, katika majadiliano haya mojawapo ni kuona na kutathmini uwezo wa mwekezaji huyu wa mwanzo Sichuan Hongda na tukiona kwamba hana uwezo kulingana na taarifa ambazo tumezipata na vyanzo vya kutoka nchini kwake then tunaweza kutafuta sasa mwekezaji mwingine kulingana na utaratibu wa mkataba wa awali ambao lazima tuuvunje au tutafute namna nyingine ili kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa manufaa ya nchi. Kwa hiyo, haya yote katika majadiliano haya ya sasa hivi yanazingatiwa. Nakushukuru sana.
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa majibu ya Serikali, lakini nina ushahidi kupitia kwa Mwenyekiti na Katibu wa Wastaafu hawa, na pia wamepeleka vielelezo vyao kwa Waziri Mheshimiwa Ndalichako kwamba mpaka sasa hawajalipwa stahiki zao;

Je, nini kauli ya Serikali kuweza kuwalipa wastaafu hawa haki zao?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, hii Kampuni ya Magunia mwaka 1996 baada ya kuona haiendeshwi kwa faida iliamua kuwapumzisha au kuwastaafisha wafanya kazi hao lakini pia mwaka huo huo iliingia mkataba wa hiari kwa watumishi hao baada ya kukubaliana kustaafu kwa maana ya kupata mshahara wa mwezi mmoja, malimbikizo ya likizo, malimbikizo ya mishahara, gharama za kusafirisha mizigo na malimbikizo ya michango mingine baada ya kuingia mkataba wa hiari kwamba watalipwa kama vibarua kwa siku shilingi 1,000 na wangelipwa marupurupu mengine kama kiwanda kingepata faida.

Mheshimiwa Spika, lakini kiwanda hiki baada ya kuona kinashuka faida mwaka 1998 kilibinafsishwa kwenda kwenye kampuni ya TPM ambayo ni Kampuni tanzu ya Mohamed Enterprises. Kwa hiyo, maana yake madai haya nadhani ndio hayo ambayo walidhani watalipwa kama kiwanda hiki kingeweza kupata faida kwa wakati huo, nakushukuru.
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, na ahsante sana Serikali kwa kunijibu swali langu vizuri, nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, napenda kuiuliza Serikali; kwa kuwa biashara ya wazalishaji wetu wa chumvi katika Mkoa wetu wa Lindi imekuwa ikiathiriwa na waagizaji wa chumvi kutoka nje ya nchi.

(a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia hawa wafanyabiashara wadogo wadogo waanze kufanya biashara ya chumvi kwa ufanisi?

(b) Je, Serikali sasa haioni wakati umefika wa kuweza kuwa na bei elekezi kwa zao hili la madini ya chumvi kwa Mkoa wetu wa Lindi ili kuhakikisha kwamba hawa wafanyabiashara wa chumvi katika Mkoa wetu wananufaika na biashara hii?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, ni kweli kwamba kumekuwa na changamoto katika sekta hii ya chumvi kwa maana ya baadhi ya viwanda kuagiza malighafi ya chumvi kutoka nje badala ya kuchukua chumvi inayozalishwa hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, tulishatoa maelekezo na hili ni agizo la Serikali, kwamba wenye viwanda wote wanaozalisha chumvi hapa nchini watumie malighafi kwa maana ya chumvi inayozalishwa nchini, kwa hiyo tulishatoa marufuku kuagiza chumvi kutoka nje ya nchi kwa ajili ya viwanda vya ndani.

Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu bei elekezi, tunashukuru kwa sababu tunadhani biashara zinatakiwa ziende kwa uhuru, kwa maana ya supply and demand, lakini pale inapotokea hoja mahsusi muhimu kama hii tutangalia ikiwa kuna ulazima wa kuweka bei elekezi kwa ajili ya kuona wananchi wa Tanzania, na hasa wanaozalisha chumvi ghafi, waweze kupata bei nzuri inayouzwa kwenye viwanda vya Tanzania, nakushukuru sana.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Swali la kwanza; kumekuwepo na uingizaji wa nguo hasa vitenge na kanga kwa njia za magendo kutoka nje ambavyo vinapelekea ukwepaji wa kodi na hivyo kupoteza mapato, lakini pia vinasababisha viwanda vyetu nchini kutokuwa shindani. Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba inatokomeza biashara hii ya magendo ili kuweza kusababisha viwanda vyetu viweze kuzalisha kwa tija? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; nchi yetu imekuwa na viwanda maarufu sana Afrika Mashariki na Kati, kama vile Kilitex, Urafiki, Mutex, Mwatex, lakini viwanda hivi vimeshindwa kufanya kazi kwa changamoto mbalimbali ikiwepo mitaji. Ningependa kujua Serikali ina mkakati gani angalau kuweza kutoa dhamana za mikopo kwa viwanda hivi ili viweze kujiendesha kwa tija pia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Esther Nicholas Matiko, Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli sekta ya nguo na mavazi nchini imekuwa na changamoto kubwa ikiwemo hiyo ya kuingiza bidhaa hizo kwa njia ya magendo. Tunajua na tulishaanza kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kudhibiti mipaka au zile sehemu ambazo wanaingiza kiholela katika maeneo ya bandari bubu, lakini pia na mipaka ya kutoka nchi za jirani. Pia kwa sasa kumekuwa na tabia ya kuingiza, kupitisha nguo hizo kwenda nchi za jirani halafu kurudisha nchini. Kwa hiyo tumeshaanza kuchukua hatua ikiwemo kudhibiti kwenye sehemu zote zinazoingiza bidhaa, lakini kuongeza watumishi kwenye Taasisi zetu ikiwemo TBS, FCC na wengine, kuhakikisha tunaongeza udhibiti katika mianya ambayo wanaingiza bidhaa hizo bandia hasa bidhaa za nguo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu viwanda ambavyo havifanyi kazi, ni kweli kuna viwanda ambavyo vimesimama ikiwemo kama alivyotaja ya Urafiki, lakini anajua Serikali tumekuwa na mkakati mara nyingi kuhakikisha tunavisaidia kwa kuweka dhamana na kuweza kuweka ruzuku mbalimbali ili viweze kufanya kazi. Ndiyo maana hivi viwanda tisa ambavyo vinaendelea kufanya kazi sasa, ni kutokana na juhudi hizi za Serikali mpaka vimefikia idadi hiyo kutoka vitatu mpaka tisa, nakushukuru.
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, mwaka 1998 Serikali ilitaifisha viwanda vikiwemo vya nguo na vingine. Mwaka 2017 viwanda hivi vilirejeshwa Serikalini katika Bajeti ya Viwanda na Biashara ya mwaka jana, Waziri alisimama hapa akasema viwanda hivi vitatangazwa kwa wawekezaji wenye uwezo ili waweze kuvifufua. Wananchi wetu na hasa vijana wanalalamika ajira, kwa nini Wizara iko kimya mpaka leo?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza ya Mheshimiwa Lucy, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli viwanda ambavyo vilikuwa vimebinafsishwa na vikawa havifanyi kazi jumla viwanda kama 20 vilikuwa vimerejeshwa Serikalini. Kati ya hivyo 10 tutavitangaza, notice ilishatangazwa mwaka jana, lakini sasa tunaendelea na mchakato wa kupata wawekezaji.

Mheshimiwa Spika, vingine ambavyo tunadhani ni muhimu kama Serikali tuendelee kuviendeleza, vitakuwa chini ya Mashirika mbalimbali ya Serikali ikiwemo NDC, maeneo yale ya uwekezaji kwa ajili ya wananchi EPZA, na kadhalika. Kwa hiyo, Serikali inaendelea na mchakato wa kuona tunapata wawekezaji mahiri, hatutaki tena kwenda haraka tukapata wawekezaji ambao badala ya kuendeleza viwanda watavidhoofisha zaidi kama ambavyo ilitokea huko nyuma. Kwa hiyo tunaendelea na mchakato huo kuhakikisha tunavitangaza viwanda hivyo kwa wawekezaji wenye tija na wenye nia ya kuendeleza viwanda hivyo. (Makofi)
MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa asilimia 75 ya mafuta ya kupikia yanatoka nje ya nchi na kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kupikia kilichopo katika Kata ya Wazo kinaitwa Family kimefungwa.

Je, Mheshimiwa Waziri ataambatana pamoja na mimi baada ya hapa ili kujua ni sababu gani kiwanda hicho kimefungwa?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swali la nyongeza ya Mheshimiwa Mchungaji Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali sasa hivi mkakati wetu ni kuhakikisha tunajitolesheza kwenye mafuta ya kula. Kwa hiyo kama kweli kuna kiwanda ambacho kimefungwa na mimi kama Naibu Waziri kwenye sekta inayohusu viwanda, nitaambatana na Mheshimiwa Mbunge ili tuweze kuona changamoto gani zinakikabili hicho kiwanda ili kiweze kuendelea kuzalisha mafuta ya kula ili kupunguza changamoto hii ya mafuta ya kula nchini, nakushuru sana.

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona. Kwa kuwa Serikali inayo dhamira ya dhati ya kufufua Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools na tayari wameshaanza kuleta mitambo mbalimbali. Swali langu, Serikali iliahidi kutupa bilioni 1.6 kwa ajili ya kujenga foundry machine yaani kinu cha kuyeyusha chuma. Je, ni lini Serikali itatuletea fedha hizo ili kiwanda kiweze kufanya kazi kwa asilimia mia moja?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Kilimanjaro Machine Tools ni moja ya viwanda ambavyo vilikuwa vinazalisha vipuri kwa ajili ya kulisha viwanda vingine ambavyo vinazalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo viwanda vya nguo na kadhalika. Lengo la Serikali kama nilivyosema ni kufufua viwanda vyote na kuhakikisha vinapata vipuli. Sasa hivi Serikali imeshatoa milioni 700, kwa hiyo bado milioni 800 na kidogo ambazo zitaenda kukamilisha ujenzi wa foundry hiyo katika kiwanda cha KMTC. Kubwa zaidi commitment imeshatoka, Wizara ya Fedha itatoa fedha hiyo ili foundry hiyo iweze kujengwa. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba nia ya Serikali na lengo la Serikali ni kulitimiza kadri ambavyo tumepanga kwenye bajeti zetu, nakushukuru.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri. Uzoefu unaonesha kwamba taasisi nyingi ambazo ziko chini ya NDC hazifanyi vizuri kutokana na ukosefu wa fedha kwa mfano General Tyre, Kilimanjaro Machine Tools na kadhalika.

Swali langu katika bajeti ya mwaka huu 2022/2023 Wizara imeanza kutenga fedha zozote kwa ajili ya kuendeleza kiwanda hicho cha Mang’ula Machine Tools?

Kwa kuwa kiwanda kile kimenyofolewa maeneo muhimu karibu yote kwa mfano sehemu za foundry imenyofolewa kiasi kwamba ni ngumu kukirudishia kama kilivyo na kitahitaji gharama kubwa sana. Kwa nini kwa sababu kuna majengo ambayo yanawezesha kukaa wanafunzi eneo hilo lisitumike kwa ajili ya kuendeleza taasisi za kiufundi?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Stella Manyanya, Mbunge kama ifuatavyo:-

Kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Stella Manyanya kwa kazi kubwa anayoifanya kufuatilia maendeleo ya sekta ya viwanda kwa sababu na yeye amekuwepo kwenye sekta hiyo kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ni kweli Shirika letu la Maendeleo la Taifa (NDC) lina miradi mingi ambayo kidogo ina changamoto lakini tumeshaanza kuyafanyia kazi ikiwemo Kilimanjaro Machine Tools ambako tumepeleka fedha ya kutosha kwa ajili ya kuihuisha ili kutengeneza foundry ambayo inafanana fanana na ile iliyokuwepo kule Mang’ula.

Kwa hiyo tumeshaanza kutengea fedha, lakini kwenye hii mahsusi ya Mang’ula baada ya kuona uhitaji huu tunafanya utafiti wa kuona nini kitafanyika halafu baada ya hapo sasa ndiyo tutakuja na bajeti yenye uhalisia. Kwa hiyo, tuko kwenye hatua za awali za kufanya utafiti wa nini kitafanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuhusu mitambo iliyokuwepo ni kweli na ndiyo maana tunataka tukihuishe kwa maana tuone sasa nini kitafanyika kwa sababu mwekezaji aliyekuwa amepewa mara ya kwanza ni kweli aling’oa mitambo mingi ikiwemo ya foundry, ya forging na fabrication na kuuza. Kwa hiyo, kimsingi tutaanza kama upya lakini kwa sababu nia ya Serikali nia ya kuona tunahuisha viwanda hivi kwa hiyo Serikali imeweka mkazo na tutakifanyia kazi na kutenga bajeti ya kutosha ili tuhakikishe tunarudi kwenye uhalisia wake wa awali, nakushukuru.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza.

Je, Mheshimiwa Waziri atakubali kuongozana nami kutembelea eneo hili ili aone umuhimu wake na fursa zilizopo kwa kuongeza ajira na biashara kwenye ukanda huu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki?

Mheshimiwa Spika, la pili; kwa vile Serikali imeanza sasa kuboresha mazingira ya machinga huku mjini kwa kuwajengea maeneo mazuri na kuwawekea mapaa kwenye biashara zao.

Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwezesha wanawake, akinamama, mabinti zetu kule kwenye vijiji ambao wanaenda kwenye magulio kama yale ya Mwika, Kisambo, Marangu, Lyamombi, Kinyange wakinyeshewa mvua mazao yao yakiharibiwa kwakati mvua zinaponyesha ni pamoja na kupigwa na jua kali. Je, Serikali haioni haina mkakati wa kuwajengea mapaa angalau kwenye maeneo machache kwenye masoko haya? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali madogo mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Charles Kimei, Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Dkt. Kimei kwa ufuatiliaji kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo la Vunjo amekuwa akifuatilia sana kuhusiana na ujenzi wa masoko.

Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu kuongozana nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba baada ya Bunge hili tutapanga na tutaongozana ili tuweze kutembelea maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo katika Jimbo lake.

Mheshimiwa Spika, lakini la pili ni kweli Serikali inapambana kuhakikisha tunaweka miundombinu wezeshi ikiwemo masoko, maeneo ya kuuzia bidhaa mbalimbali hasa kwa wanawake, vijana na wamachinga na hii Serikali imeshaanza kupitia TAMISEMI kujenga mabanda na kuezeka maeneo mbalimbali ambayo yanatumika kama masoko ili kuhifadhi bidhaa wakati wa mvua na jua ili wakinamama wafanyabiashara waweze kufanyakazi. Naomba halmashauri waweze kufanya hivyo ili kuhakikisha bidhaa hizo zinatunzwa na kuuzwa katika mazingira mazuri, nakushukuru.
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, lakini kuna maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa sasa tunakaribia kwenda kusaini mkataba mkubwa wa uchakataji wa gesi asilia wa LNG kule Kusini na sehemu ya uzalishaji wa malighafi za gesi kuwa pia inatengeneza mbolea.

Je, ni upi mkakati wa Serikali kufungamanisha uchakataji wa gesi asilia na uanzishaji wa Kiwanda cha Mbolea katika eneo la Kusini?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Mkoa wa Tanga ndiyo tutakaopokea hifadhi ya mafuta ghafi kutoka Uganda.

Je, Serikali haioni kwamba tunaweza tukatumia eneo la Chongoleani ikiwa ni sehemu pia ya usafishaji ghafi; kwa sababu mafuta haya pia ni malighafi kwa ajili kutengeneza mbolea tukapata Kiwanda kingine cha Mbolea katika Mkoa wa Tanga kama kile kilichokuwepo miaka ya nyuma? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shangazi, Mbunge wa Mlalo, kama ifutavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Shangazi kwa kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa viwanda hasa vya mbolea katika nchi hii na hasa katika Mkoa wa Tanga. Serikali ina mpango wa matumizi ya gesi asilia ambao unatekelezwa kupita Shirika letu la Maendeleo la Petroli (TPDC) lakini pia kwa kushirikiana na Kituo chetu cha Uwekezaji cha (TIC). Kwa hiyo, katika mpango huo tumeshaendelea kuvutia wawekezaji na zaidi ya kampuni tatu ambazo zimeonesha utayari wa kuwekeza katika kuzalisha mbolea kwa kutumia gesi asilia kampuni hizo ni pamoja na Helmik na Ferosta kutoka Ujerumani lakini pia tunayo Polyserve kutoka Misri, lakini zaidi na wengine wanaendelea kufanya tathmini na namna ya kutumia gesi asilia ikiwemo Kampuni ya Dangote.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, katika mpango huo tumeshaendelea kuvutia wawekezaji, na zaidi ya kampuni tatu zimeonesha utayari wa kuwekeza katika uzalishaji wa mbolea kwa kutumia gesi asilia. Kampuni hizo ni pamoja na Helium na Feroster kutoka Ujerumani na pia tunayo Polysafe kutoka Misri. Vile vile na wengine wanaendelea kufanya tathmini ya namna ya kutumia gesi asilia ikiwemo Kampuni ya Dangote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni sahihi kabisa, ni mawazo mazuri kuona namna gani Tanzania inatumia fursa ya mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda ambayo yatakuja Tanzania, tuone namna gani ya kutumia mafuta hayo ghafi kuzalisha mbolea ili tukidhi mahitaji makubwa ya nchi hii kutokana na upungu au nakisi ya mbolea kwa ajili ya sekta ya Kilimo. Nashukuru. (Makofi)
MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa kuwa changamoto ya mbolea bado ni kubwa sana nchini; na kwa kuwa Tanga tulikuwa na Kiwanda cha Mbolea na sasa hivi hakifanyi kazi: Je, Serikali haioni haja sasa yakutafuta mwekezaji kwa ajili ya kwenda kuwekeza kwenye kiwanda kile ili kutatua changamoto kubwa ya mbolea tuliyonayo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zodo, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama nilivyosema tuna changamoto kubwa sana ya mbolea, zaidi ya tani 600,000 zinahitajika katika kukamilisha mahitaji ya tani 700,000 kwa mwaka ambazo zinatumika katika nchi hii. Kwa hiyo, Serikali ina mpango wa kuendelea kufufua viwanda ikiwemo na hiki ambacho anasema Mheshimiwa Mbunge kule Tanga. Tutaona namna ya kutafuta wawekezaji ili waweze kuwekeza katika kiwanda hicho ili kuendelea kuzalisha mbolea kama ilivyokuwa hapo awali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kuniona. Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi sana kununua viuatilifu hasa vinavyotumika katika zao la korosho, na mnunuzi mkubwa ni maeneo yote ya Mtwara na Lindi: Je, Serikali haioni sasa ni wakati muhimu wa kujenga viwanda vya viuatilifu ambavyo vinaendana na material hii ya gesi?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mchungahela Mbunge wa Lulindi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tuna changamoto kama ilivyo kwenye mbolea, lakini pia kwenye viuatilifu ambavyo kwa kiasi kikubwa tunaingiza kutoka nje. Serikali imeshaanza mipango hiyo ikiwemo kuzalisha kupitia kile kiwanda chetu cha viuwadudu pale Kibaha, lakini tutaona pia namna ya kutumia gesi kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, ambapo nayo ikianza kuchakatwa inaweza kuzalisha viuatilifu mbalimbali ambavyo vinaweza kutumika katika sekta hii ya kilimo hasa kwenye mikorosho na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kiwanda cha LOSAA, kiwanda ambacho ni cha ufundi wa ufumaji na Seremala; kilisimama kwenye ujenzi wake tangu mwaka 1973. Tukazungumza na Mheshimiwa Waziri akamtuma Katibu Mkuu wa Wizara yako, ametembelea pale na akaahidi kiwanda kile kitamaliziwa na kuanza kufanya kazi: Je, ni lini Serikali itaanza umaliziaji wa kiwanda hiki?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Serikali tuna mpango wa kufufua viwanda vyote ikiwemo kiwanda ambacho anakisema Mheshimiwa Mbunge. Kweli Serikali tumeshachukua jitihada ikiwemo kutuma wataalamu wetu na Katibu Mkuu alishaenda pale kuweka tathmini ya kuona mahitaji halisi ya gharama ya kukiendeleza kiwanda kile.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali katika fedha za mwaka huu ambazo zimepitishwa hapa, mojawapo tutaangalia namna ya kuanza hatua za awali kukifufua kiwanda hicho ili kiweze kuendelea kufanya kazi na wananchi wa Jimbo la Hai weweze kunufaika na nchi nzima tuweze kutapa faida ya uwekezaji katika viwanda vyetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali ya nyongeza. Kwa kuwa tafiti zimeonesha kwamba Gypsam au jasi inatoa mbolea ikichakatwa na kwa kuwa Wilaya ya Same ina jasi nyingi katika Kata ya Bendera na Makanya: Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka viwanda katika sehemu hizo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kaboyoka, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katika malighafi ambazo zinatumika katika kuzalisha mbolea, mojawapo ni Gypsam, na kwa sababu Mheshimiwa Mbunge amesema kuhusiana na Jimboni kwake, Mkoani huko, basi tutaona namna gani ya kuvutia pia wawekezaji waweze kuona namna ya kutumia malighafi zilizopo pale ili kuanzisha viwanda vya mbolea kama ambavyo tunavutia maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu aliyoyatoa, nina maswali mawili ya nyongeza.

Ningependa nimwambie Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba kule Njombe tuna Kiwanda cha Maziwa ambacho kimefungwa kwa muda mrefu na kiwanda kile kina wadau mbalimbali ambao wanahusika na kina changamoto nyingi sana.

Swali la kwanza je, Mheshimiwa Waziri anaweza kuniambia Wizara hii ambayo kazi yake ni uratibu; je, anaweza sasa kuchukua hilo jukumu la kufanya uratibu ili wadau mbalimbali wa kiwanda kile waweze kukutana na kutatua hizo changamoto?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa Waziri au Naibu Waziri anaweza kutoa commitment hapa sasa kwamba yeye pamoja na hao wadau watakuja Njombe ili kukaa na wakulima ambao wanaumia sana kutokana na kiwanda kile kutokufanyakazi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Deodatus Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Deodatus Mwanyika kwa kufuatilia sana kuhusiana na viwanda katika Mkoa wa Njomba na hasa Kiwanda hiki cha Maziwa ambacho muda mwingi anafuatilia.

Mheshimiwa Spika, ni kweli viwanda vingi havifanyikazi kutokana na changamoto mbalimbali na Serikali kama nilivyosema kupitia mpango wa kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara tunapitia mojawapo ni kuhakikisha tunatatua changamoto zinazokabili viwanda hivyo, ikiwemo kiwanda hiki cha maziwa cha Njombe; tutafanya tathmini tuone nini changamoto zilizowasibu mpaka kisiwe kinafanyakazi hivi sasa na hatimaye Serikali tutachukua hatua.

Mheshimiwa Spika, la pili; kwa sababu kweli kiwanda kinahusisha sekta tatu kwa maana ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara lakini tutashirikiana na wenzetu Wizara ya Kilimo, lakini Mifugo na Uvuvi ili tuweze kukitembelea kama nilivyosema kubaini changamoto ambazo zinazikabili kiwanda hiki ambacho kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge hakifanyikazi. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza katika Wizara hii ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Kwa muda mrefu Serikali kupitia TPDC imetenga eneo la kujenga Kiwanda cha Mbolea Kilwa Masoko itakayotokana na malighafi ya gesi asilia; na kwa mara ya mwisho tumepewa taarifa kwamba Serikali iko katika mazungumzo na mwekezaji.

Swali; mazungumzo kati ya Serikali na mwekezaji yamefikia hatua gani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, napenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Ally kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli adhma ya Serikali ni kuona tunajitosheleza katika uzalishaji au mahitaji ya mbolea nchini ambayo ni takribani ya tani 700,000. Uzalishaji tulionao sasa si zaidi ya tani 100,000. Lakini mipango hiyo pamoja na mingine ni kuona gesi asilia katika Mkoa wa Mtwara inatumika kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge amesema na TPDC kweli kuna eneo limetengwa na kwa kweli kama nilivyosema swali hapa Bungeni kuna wawekezaji wameshajitokeza ambao watakuja kuwekeza katika viwanda vya kuzalisha mbolea kwa kutumia gesi asilia.

Mheshimiwa Spika, nimuhakikishie Mbunge kwamba Serikali inafuatilia sana jambo hili ili kuhakikisha majadiliano hayo yanakamilika mara moja na kwa kweli tunafanya majadiliano kwa ajili ya kuona namna ya kuwavutia. Kwa sababu kilichopo hapa ni namna ya kuwavutia ili waweze kuwekeza katika kutumia gesi hiyo ikiwemo pamoja na mambo ya bei na mambo mengine/vivutio maalum ambavyo wanahitaji wawekezaji hao. Kwa hiyo, tutakamilisha na kuanza kuzalisha mbolea kupitia gesi asilia, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwenye Jimbo langu la Nachingwea kuna viwanda viwili ambavyo kwa muda mrefu havifanyikazi; Kiwanda cha Lindi Pharmacy lakini pia Kiwanda cha Mafuta Ilulu.

Nini mpango wa Serikali kufufua viwanda hivi ili viweze kuzalisha ajira kwa vijana wetu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Nachingwea kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali kupitia ubinafsishaji tulibinafsisha viwanda 156 lakini katika viwanda hivyo viwanda 88 ndiyo vinafanyakazi vizuri, 68 vilikuwa havifanyikazi vizuri na moja ya maeneo ambayo tumekwishayafanyia kazi ni kuvirudisha baadhi ya viwanda ambavyo vipo 20, mojawapo vikiwa hivi viwanda viwili ambavyo alivitaja Mheshimiwa Mbunge, Kiwanda cha Mafuta Ilulu na kile kingine cha kubangua korosho cha Nachingwea.

Mheshimiwa Spika, lakini katika hatua za awali tumeshafanya tathmini viwanda hivi ni kati ya viwanda ambavyo tutaviweka katika maeneo ya uwekezaji kwa ajili ya kuzalisha bidhaa kwa ajili ya mauzo nje (SEZ).

Kwa hiyo, tayari tumeshachukua hatua mbalimbali na sasa tunaendelea kutafuta wawekezaji ambao tutashirikiana nao, ili wazalishe bidhaa aidha za mafuta au kubangua korosho kama ilivyokuwa awali kwa ajili ya kuuza nje. Kwa hiyo, tayari tumeshachukua hatua kwamba hivi vitakuwa chini ya maeneo huru ya uwekezaji kwa ajili ya mauzo nje na hivi viwanda vitafufuliwa tutakapopata mwekezaji mapema iwezekanavyo. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. JERRY W. SILAA: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi; masuala ya uwekezaji wa viwanda si tu yanaleta tija kubwa kwenye ajira na kusaidia upatikanaji wa bidhaa kwenye soko la ndani yakiwemo mafuta ya kupikia na bidhaa nyingine.

Nini mkakati wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha kuisaidia Benki ya Rasilimali Tanzania (Tanzania Investment Bank Development) kupata mitaji ya uhakika kwa ajili ya viwanda? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jerry Silaa, Mbunge wa Ukonga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli azma ya Serikali ni kuona namna gani tunawasaidia wawekezaji hasa wa ndani kupitia kuwasaidia kwenye changamoto ya mitaji ya rasilimali fedha. Kwa hiyo, mojawapo ni kupitia mabenki yetu yanayosaidia wawekezaji ikiwemo Benki hii ya Rasilimali na mabenki mengine. Lengo la Serikali ni kuhakikisha tunaweka mazingira wezeshi ikiwemo hiyo ya kuwapa mitaji au kuhakikisha wawekezaji ambao wanataka kuwekeza kwenye viwanda hivi wanapewa huduma hiyo ya kifedha.

Kwa hiyo, Serikali itaendelea kufanyakazi kuona kila namna inayowezekana kuwezesha benki zetu ambazo zinakopesha wafanyabiashara au wawekezaji katika sekta ya viwanda. Nakushukuru sana.
MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pale Musoma Mjini tuna tatizo kubwa sana la ajira kwa sababu viwanda vingi vimekufa; vilikuwepo viwanda vya samaki vimekufa, Kiwanda cha Nguo cha MUTEX kimekufa, Kiwanda cha Maziwa kimekufa, Kiwanda cha Mkonge kimekufa. Sasa ni zaidi ya miaka kumi kila siku Serikali inaahidi kutafuta wawekezaji. Sasa tunapenda kujua, ni lini sasa itatusaidia kupata hawa wawekezaji ili watu wetu waendee kupata ajira? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, napenda kujibu swali la nyongeza dogo la Mheshimiwa Vedastus Manyinyi, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kama nilivyosema, tulipofanya tathmini ya mwaka 2017 kuhusiana na viwanda vilivyobinafsishwa, viwanda vingi zaidi ya 68 vilikuwa havifanyikazi vikiwemo viwanda ambavyo viko katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge kule kule Musoma. Kama nilivyosema katika tathmini hiyo tumeshavigawa vingine tunavitafutia wawekezaji, lakini vingine tutaviweka katika mashirika maalum ikiwemo maeneo huru ya uzalishaji kwa ajili ya mauzo ya nje (SEZ), lakini vingine katika taasisi zetu kama Shirika la Maendeleo la Taifa – NDC na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, lakini katika kutafuta wawekezaji kuna hatua mbalimbali kwa sababu tusingependa kurudia tena makosa tuliyoyafanya huko nyuma kutafuta/kupata wawekezaji ambao siyo mahiri. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wote kwamba Serikali inajitahidi kuhakikisha kuweka mazingira wezeshi, ili kuvutia wawekezaji ambao tunajua watakuwa ni makini na wenye nia thabiti ya kuvifufua au kujenga viwanda vingine ambavyo vitakuwa na tija kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii. Nakushukuru sana.
MHE. KHAMIS MBAROUK AMOUR: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na nimshukuru Waziri kwa majibu yake mazuri, kimsingi nina swali moja tu la nyongeza.

Je, Serikali ipo tayari kuwatambua hawa wajasiriamali wamachinga, nakusudia wa Tanzania nzima, wawe wa Tanzania Bara na Visiwani, halafu wakawaandalia mazingira ya kukopesheka benki? Je, Serikali ipo tayari kufanya hivyo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Khamis Mbarouk Amour, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tayari Serikali imeshaanza kutambua wamachinga Tanzania nzima ikiwemo Visiwani, lakini kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge kwa sababu anafuatilia sana suala hili, tutaongeza juhudi na kuweka mipango stahiki ya kuwatambua na kuwawezesha wamachinga wote ikiwemo upande wa Zanzibar ambao tunaamini wanatakiwa kupewa fursa sahihi ili waweze kuendelea kufanya biashara zao kwa ukamilifu na kwa ufanisi. Nakushukuru.

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kati ya changamoto kubwa zinazowapata wafanyabisahara wadogo hawa tunaowaita machinga ni uwezo wa kupata mikopo kwenye hizi financial institutions zetu, na sababu kubwa ni kutokidhi vigezo, hasa dhamana na wale wachache ambao wanapata mikopo haswa kwenye hizi micro-finance riba ni kubwa sana hivyo inasababisha wao kushindwa kuendeleza biashara zao.

Je, Wizara imejipanga namna gani ili kuweza kuwasaidia watu hawa kwenye sekta hii niliyoitaja? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Alfred Kimea, Mbunge wa Korogwe Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli, changamoto kubwa ambayo inawakumba wajasiriamali ikiwemo wamachinga ni changamoto ya kupata fedha au mitaji kwa ajili ya kufanya shughuli zao. Serikali inachukua jitihada mbalimbali ikiwemo kuweka fedha mahususi kwa ajili ya kuwasaidia wamachinga, kama ile asilimia 10 ya mikopo kupitia Halmashauri zetu, lakini pia zaidi kupitia taasisi zetu kama SIDO ambayo inahudumia viwanda vidogo na wafanyabiashara wadogo, tumeshaweka mahususi kwanza fedha, lakini pili tumekubaliana kupunguza ile riba ambayo mwanzoni ilikuwa ni kubwa kwa hiyo, itakuwa chini ya asilimia 10, lakini zaidi tunaendelea kuongea na taasisi za kifedha za binafsi na ninyi ni mashahidi, tarehe 11 Aprili Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, alifungua ile kampeni ya teleza kidijitali ambapo mfanyabiashara au mmachinga mdogo anaweza kupata fedha bila kuwa na dhamana au kwenda benki kupitia simu ya kiganjani, wanasema Mshiko Fasta kuanzia shilingi 50,000 mpaka 500,000.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hii ni jitihada kuhakikisha tunamkomboa mfanyabiashara mdogo au mmachinga kupata fedha kirahisi zaidi. Nakushukuru.
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, pamoja na majibu mazuri ya mwisho ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nilitaka kumuuliza tu swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa tunazungumzia sana asilimia kumi kama kuwafikia vijana, na tunatambua vijana wanaozungumzwa kwenye asilimia 10 zile asilimia nne zao ni vijana wanaoishia miaka 35 na machinga wengi wanazidi miaka 35.

Je, ni upi sasa mkakati wa Serikali katika kuwafikia machinga walio wengi zaidi ya hawa wa miaka 35? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Issa Mtemvu, Mbunge wa Kibamba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli, asilimia 10 zile zimelenga zaidi akinamama, vijana na wale wenye ulemavu, lakini kwenye kundi hili la vijana ni kweli wakishavuka ule muda wao maana yake wanakuwa hawawezi kukopesheka.

Mheshimiwa Spika, lakini kama nilivyosema Serikali inaendelea na juhudi mbalimbali ikiwemo kupitia taasisi za kifedha ili kuhakikisha wamachinga hawa, hawa wajasiriamali ambao watakosa fursa kwenye ile asilimia 10 ambayo inatengwa katika Halmashauri, basi wapate fedha kupitia taasisi nyingine kama nilivyosema SIDO na taasisi za kifedha nyingine ambazo zinatoa mikopo kwa wajasiriamali. Nakushukuru sana.
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Spika, nikushukuru na napenda kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, maeneo mengi kwenye Halmashauri wametenga maeneo kwa ajili ya wamachinga, namaanisha wamewajengea vibanda na vibanda hivi wanakwenda kuwapangisha. Hawa wamachinga mtaji wao ni kuanzia shilingi 20,000 mpaka shilingi 4,000,000; je, Halmashauri ziko tayari kuwapatia bure hivi vibanda kwa ajili ya kufanya biashara zao?
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli katika mikakati ya kuhakikisha tunawezesha wajasiriamali na hasa wamachinga ni kuwatengea maeneo, lakini pia kuwawekea miundombinu wezeshi ikiwemo vibanda hivyo ambavyo vinasaidia kufanya biashara zao katika mazingira mazuri, lakini kama ulivyosema katika Halmashauri huenda wanakusanya fedha kidogo kwa ajili ya kuvikarabati au kuhakikisha vile vibanda vinakaa muda mrefu viweze kuwasaidia wajasiriamali au wamachinga hao. Kwa sababu ametoa wazo hilo nadhani tutaongea na wenzetu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ili kuona namna gani ya kuwasaidia vizuri zaidi wajasiriamali au wamachinga ambao hawana uwezo wa kulipia vibanda hivyo kutokana na hali halisi na maeneo husika. Nakushukuru sana.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri japo yamekaa kiujumla mno, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Je, ni upi mkakati wa muda mfupi wa Serikali wa kuwasaidia wafugaji wa Mkoa wa Arusha kuweza kusindika maziwa yao ambayo kwa sasa kiasi kikubwa yanapotea? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Mkoa wa Arusha ulikuwa ni miongoni mwa Mikoa inayoongoza kwa viwanda hapa nchini, kama General Tyre, Kiwanda cha Kiltex na viwanda vya kusindika vyakula mbalimbali ambavyo kwa sasa vimetelekezwa. Je, ni upi mpango wa Serikali wa kufufua viwanda hivi ambavyo ni chanzo kikibwa cha ajira kwa wananchi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, ni kweli Mkoa wa Arusha ni moja ya Mikoa ambayo inazalisha maziwa kwa wingi na ndiyo Mkoa ambao unaoongoza kwa kuwa na viwanda vingi sana vya kusindika maziwa kwa maana ya kuwa na viwanda 18. Kama tunavyojua Tanzania ina mifugo mingi hasa ng’ombe kwa maana nchi kama ya tatu katika Afrika. Sasa, changamoto kama alivyosema, ni kweli kuna upotevu wa maziwa mengi ambayo yanazalishwa katika mkoa huu na mikoa mingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali uliopo sasa hivi, moja, ni kuona tunakuja na uwekezaji katika maeneo ya utunzaji (storage facilities) ambayo yatasaidia kuhakikisha viwanda hivi vinapata maziwa katika ubora wake. Kwa sababu mpaka sasa, viwanda vilivyopo katika Mkoa wa Arusha na hata viwanda vingine bado vinazalisha chini ya uwezo wake uliosimikwa. Maana yake ni nini? Ni kwamba katikati hapa kutoka kwa wafugaji ambao wanaleta maziwa viwandani, kuna uharibifu wa upotevu wa maziwa kiasi kwamba viwanda vyenyewe havipati maziwa ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa pili kama tulivyosema, tunaendelea kuhakikisha sasa wafugaji na pia hata wanunuzi wanaendelea kuchukua, kusaidiana, kuwe na mikataba kati ya wenye viwanda na wafugaji ili kuhakikisha maziwa yote yanayozalishwa yanapata soko kwenye viwanda hivi vilivyopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na maendeleo ya viwanda ambavyo vilikuwepo na vingine vilibinafsishwa ambavyo havifanyi kazi, Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara tumeshapitia na kufanya tathmini ya namna ya kuvifufua viwanda hivyo. Vingine vilikuwa vimebinafsishwa na wawekezaji ambao wamevitelekeza, lakini hata vingine ambavyo havifanyi kazi ili tuweze kuhakikisha navyo vinaendelea kufanya kazi na kuleta viwanda vingine vipya, nakushukuru.
MHE. JACQUELINE K. ANDREA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi. Kwa kuwa Mkoa wetu wa Tabora una maeneo mengi ya kutosha na wafugaji ni wengi; nini mpango wa Serikali kutenga fedha kwa ajili ya kuwekeza kwenye viwanda vya maziwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kweli kama nilivyosema Tabora pia ni eneo ambalo kuna wafugaji wengi na ng’ombe wengi, kama nilivyosema hamasa kubwa ni kuona tunaendelea kuhamasisha uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani pia hata wa nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kuwaomba watanzania wenzangu hata Wabunge wenzangu kuendelea na kushiriki, kutumia fursa hizi zilizopo katika maeneo yetu. Bahati nzuri, Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa kodi nyingi kwenye maeneo haya kwenye viwanda vya maziwa, kwenye storage facilities. Kwa hiyo, tutumie fursa hii kuwekeza huko ili tuweze kukwamua au kuwasaidia wafugaji ambao wanakosa soko la kuuza maziwa yao ambayo naamini tukizalisha bidhaa zinazotokana na maziwa tutapata fursa kubwa ya kuuza ndani ya nchi pia nje ya nchi kwa sababu tayari bidhaa hii inahitajika sana, nakushukuru sana.
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru nataka kujua Serikali imefikia hatua gani katika uwekezaji wa kiwanda cha mbolea katika Mkoa wa Mtwara kwa sababu sisi tuna malighafi ambazo zinaweza kuzalisha mbolea?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, ni kweli moja ya maeneo ambayo tunaangalia kwa uzito sana ni uwekezaji viwanda vya mbolea hapa nchini na ninyi mashahidi sasa tumeendelea kufanya hivyo na sasa kiwanda kikubwa ambacho kipo hapa Dodoma kinaendelea INTRACOM.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Mtwara ni maeneo mahususi ambako tunategemea kuwekeza viwanda vinavyotumia gesi. Kwa hiyo, mchakato uliopo bado tunaendelea kuongea na wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza katika maeneo haya na hasa kule Kilwa ambapo tutatumia gesi ile kuzalisha mbolea. Kwa hiyo, mipango ya uwekezaji bado ipo katika sekta ya mbolea, ahsante sana.
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza swali la nyongeza kwamba Wizara imeanzisha ujenzi wa vituo vya maziwa, ikiwemo kituo kidogo cha maziwa katika Kata Oltrumet ambayo imefikia eneo la lintel mpaka sasa vituo hivyo havijamalizika. Je, Serikali inatoa kauli gani juu ya kumalizia vituo hivyo vya maziwa?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, ni kweli Serikali ya Awamu ya Sita imeweka nia ya dhati na haya ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwamba tuone namna gani tunapunguza upotevu wa maziwa na hivyo vituo hivi vinavyojengwa ni utekelezaji wa mpango BBT mifugo ambayo Wizara ya Mifugo inasimamia. Naamini vituo hivi vitakamilika hasa tukijua kwamba Mheshimiwa Rais ameshaongeza fedha nyingi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Mwenyekiti nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba vituo hivi vitakamilika mara moja ili viweze kusaidia wananchi.
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naomba niulize swali la nyongeza kwamba kwa sababu ili Serikali iweze kuweka uvutiaji wa wawekezaji katika sekta ya maziwa ni wajibu wake pia kujenga vituo vya kukusanyia maziwa. Ni nini mpango wa Serikali kujenga vituo vya kukusanyia maziwa katika Mkoa wa Singida ili iwe rahisi wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta hiyo?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, ni kweli kama nilivyosema kwenye majibu ya nyongeza, kwamba; moja ya maeneo ambayo Serikali ya Awamu ya Sita inaweka msisitizo sana ni maeneo ya vituo vya kukusanya maziwa na hasa na kuweka storage facilities ambazo zitasaidia kutunza maziwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mtaturu kwamba, eneo hilo pia nako tutakuja kuweka vituo hivi vya kukusanyia maziwa na hasa vifaa hivi vya kutunzia maziwa ili yasiharibike wakati yanasubiri kwenda kwenye viwanda.
MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru.

Mheshimiwa Spika, ni kwamba kwa kuwa viwanda vya Nyakarilo, Buyagu na Nyamirilo havifanyi kazi leo, takribani miaka 21. Huu mpango unaopangwa na Serikali hauoni kama ndio unafifisha zao letu la pamba kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi katika Ilani yake imesema ya mwaka 2025 tunakwenda kuzalisha pamba tani milioni moja na tutaboresha viwanda. Leo tunakwenda mwaka wa tatu hakuna kiwanda chochote katika Wilaya ya Sengerema kilichoboreshwa.

Mheshimiwa Spika, haoni kwamba Serikali tayari tena ina mpango wa kupingana na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi? Swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali letu la pili ni kwamba kwa kuwa, viwanda hivi vipo na vinasimamiwa na vyama vya ushirika chini ya Wizara ya Kilimo na ninyi Wizara ya Viwanda ni sehemu ya Serikali. Mko tayari kufuatana na mimi kwenda Sengerema kukagua hivyo viwanda na kuwaeleza wananchi, lini mtaviboresha?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, ni kweli kabisa kwamba, kumekuwa na changamoto katika sekta ya viwanda hasa viwanda vya pamba katika maeneo mengi kwamba ni viwanda vya siku nyingi na hivyo vimechakaa, na kama alivyosema Mheshimiwa Tabasam, ni kweli Serikali imeshaweka mkakati maalum.

Mheshimiwa Spika, kwanza changamoto iliyokuwepo kabla ilikuwa ni changamoto ya malighafi kwenye viwanda ambavyo vinafanya kazi, lakini sasa kwa sababu ya uzalishaji mkubwa ambao Mheshimiwa Rais ameshaweka fedha nyingi kwenye sekta ya kilimo, tunaamini kweli kutakuwa na uzalishaji mkubwa kulingana na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo sasa pamba hii inatakiwa kulishwa kwenye viwanda vyetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sisi kama Wizara ya Viwanda na Biashara, lakini kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo tutahakikisha tunapitia na kuona viwanda hivi viaenda kufufuliwa na kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu ziara, ni kweli nitafanya ziara ili nijionee na mimi kama Wizara ya Viwanda tunaoratibu viwanda, lakini kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, ili tuhakikishe sasa mkakati tuliouweka wa kupata mitaji kupitia Benki ya Kilimo, viwanda hivi viweze kufufuliwa ili wananchi wa Sengerema na wengine wanaofanya kazi waweze kunufaika na uwepo wa viwanda hivi, lakini pia kuchochea kilimo cha pamba, nakushukuru.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri japo yamekaa kiujumla mno, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Je, ni upi mkakati wa muda mfupi wa Serikali wa kuwasaidia wafugaji wa Mkoa wa Arusha kuweza kusindika maziwa yao ambayo kwa sasa kiasi kikubwa yanapotea? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Mkoa wa Arusha ulikuwa ni miongoni mwa Mikoa inayoongoza kwa viwanda hapa nchini, kama General Tyre, Kiwanda cha Kiltex na viwanda vya kusindika vyakula mbalimbali ambavyo kwa sasa vimetelekezwa. Je, ni upi mpango wa Serikali wa kufufua viwanda hivi ambavyo ni chanzo kikibwa cha ajira kwa wananchi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, ni kweli Mkoa wa Arusha ni moja ya Mikoa ambayo inazalisha maziwa kwa wingi na ndiyo Mkoa ambao unaoongoza kwa kuwa na viwanda vingi sana vya kusindika maziwa kwa maana ya kuwa na viwanda 18. Kama tunavyojua Tanzania ina mifugo mingi hasa ng’ombe kwa maana nchi kama ya tatu katika Afrika. Sasa, changamoto kama alivyosema, ni kweli kuna upotevu wa maziwa mengi ambayo yanazalishwa katika mkoa huu na mikoa mingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali uliopo sasa hivi, moja, ni kuona tunakuja na uwekezaji katika maeneo ya utunzaji (storage facilities) ambayo yatasaidia kuhakikisha viwanda hivi vinapata maziwa katika ubora wake. Kwa sababu mpaka sasa, viwanda vilivyopo katika Mkoa wa Arusha na hata viwanda vingine bado vinazalisha chini ya uwezo wake uliosimikwa. Maana yake ni nini? Ni kwamba katikati hapa kutoka kwa wafugaji ambao wanaleta maziwa viwandani, kuna uharibifu wa upotevu wa maziwa kiasi kwamba viwanda vyenyewe havipati maziwa ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa pili kama tulivyosema, tunaendelea kuhakikisha sasa wafugaji na pia hata wanunuzi wanaendelea kuchukua, kusaidiana, kuwe na mikataba kati ya wenye viwanda na wafugaji ili kuhakikisha maziwa yote yanayozalishwa yanapata soko kwenye viwanda hivi vilivyopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na maendeleo ya viwanda ambavyo vilikuwepo na vingine vilibinafsishwa ambavyo havifanyi kazi, Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara tumeshapitia na kufanya tathmini ya namna ya kuvifufua viwanda hivyo. Vingine vilikuwa vimebinafsishwa na wawekezaji ambao wamevitelekeza, lakini hata vingine ambavyo havifanyi kazi ili tuweze kuhakikisha navyo vinaendelea kufanya kazi na kuleta viwanda vingine vipya, nakushukuru.
MHE. JACQUELINE K. ANDREA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi. Kwa kuwa Mkoa wetu wa Tabora una maeneo mengi ya kutosha na wafugaji ni wengi; nini mpango wa Serikali kutenga fedha kwa ajili ya kuwekeza kwenye viwanda vya maziwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kweli kama nilivyosema Tabora pia ni eneo ambalo kuna wafugaji wengi na ng’ombe wengi, kama nilivyosema hamasa kubwa ni kuona tunaendelea kuhamasisha uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani pia hata wa nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kuwaomba watanzania wenzangu hata Wabunge wenzangu kuendelea na kushiriki, kutumia fursa hizi zilizopo katika maeneo yetu. Bahati nzuri, Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa kodi nyingi kwenye maeneo haya kwenye viwanda vya maziwa, kwenye storage facilities. Kwa hiyo, tutumie fursa hii kuwekeza huko ili tuweze kukwamua au kuwasaidia wafugaji ambao wanakosa soko la kuuza maziwa yao ambayo naamini tukizalisha bidhaa zinazotokana na maziwa tutapata fursa kubwa ya kuuza ndani ya nchi pia nje ya nchi kwa sababu tayari bidhaa hii inahitajika sana, nakushukuru sana.
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru nataka kujua Serikali imefikia hatua gani katika uwekezaji wa kiwanda cha mbolea katika Mkoa wa Mtwara kwa sababu sisi tuna malighafi ambazo zinaweza kuzalisha mbolea?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, ni kweli moja ya maeneo ambayo tunaangalia kwa uzito sana ni uwekezaji viwanda vya mbolea hapa nchini na ninyi mashahidi sasa tumeendelea kufanya hivyo na sasa kiwanda kikubwa ambacho kipo hapa Dodoma kinaendelea INTRACOM.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Mtwara ni maeneo mahususi ambako tunategemea kuwekeza viwanda vinavyotumia gesi. Kwa hiyo, mchakato uliopo bado tunaendelea kuongea na wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza katika maeneo haya na hasa kule Kilwa ambapo tutatumia gesi ile kuzalisha mbolea. Kwa hiyo, mipango ya uwekezaji bado ipo katika sekta ya mbolea, ahsante sana.
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza swali la nyongeza kwamba Wizara imeanzisha ujenzi wa vituo vya maziwa, ikiwemo kituo kidogo cha maziwa katika Kata Oltrumet ambayo imefikia eneo la lintel mpaka sasa vituo hivyo havijamalizika. Je, Serikali inatoa kauli gani juu ya kumalizia vituo hivyo vya maziwa?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, ni kweli Serikali ya Awamu ya Sita imeweka nia ya dhati na haya ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwamba tuone namna gani tunapunguza upotevu wa maziwa na hivyo vituo hivi vinavyojengwa ni utekelezaji wa mpango BBT mifugo ambayo Wizara ya Mifugo inasimamia. Naamini vituo hivi vitakamilika hasa tukijua kwamba Mheshimiwa Rais ameshaongeza fedha nyingi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Mwenyekiti nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba vituo hivi vitakamilika mara moja ili viweze kusaidia wananchi.
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naomba niulize swali la nyongeza kwamba kwa sababu ili Serikali iweze kuweka uvutiaji wa wawekezaji katika sekta ya maziwa ni wajibu wake pia kujenga vituo vya kukusanyia maziwa. Ni nini mpango wa Serikali kujenga vituo vya kukusanyia maziwa katika Mkoa wa Singida ili iwe rahisi wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta hiyo?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, ni kweli kama nilivyosema kwenye majibu ya nyongeza, kwamba; moja ya maeneo ambayo Serikali ya Awamu ya Sita inaweka msisitizo sana ni maeneo ya vituo vya kukusanya maziwa na hasa na kuweka storage facilities ambazo zitasaidia kutunza maziwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mtaturu kwamba, eneo hilo pia nako tutakuja kuweka vituo hivi vya kukusanyia maziwa na hasa vifaa hivi vya kutunzia maziwa ili yasiharibike wakati yanasubiri kwenda kwenye viwanda.
MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

(i) Je, ni maeneo yapi ambayo Serikali imeyaainisha katika Mkoa wa Kigoma kwa ajili ya uwekezaji?

(ii) Je, ni shughuli zipi za kipaumbele zilizoainishwa kutangazwa katika maeneo hayo? (Makofi)
NAIBU WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza. Mkoa wa Kigoma ni moja ya Mikoa ya kimkakati hapa nchini, hivyo maeneo ambayo tunaazimia kuyawekea uwekezaji wa kutosha ni kwenye uongezaji thamani katika mazao ya kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, azma hiyo, inadhihirika pale ambapo Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameendelea kuboresha miundombinu wezeshi ikiwemo barabara za lami lakini pia, kupeleka umeme wa Gridi ya Taifa ili kuona namna gani tunaweza kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari pale Kigoma tumeshaweka kiwanda kikubwa cha kuchakata chikichi lakini pili, kuna kiwanda kikubwa kinaenda kujengwa cha kuchataka sukari.

Mheshimiwa Naibu Spika, shughuli muhimu ambazo zinaweza kufanywa katika Mkoa wa Kigoma, mahsusi Buhigwe ambako Mheshimiwa Mbunge anatoka, na kwa kuwa tunajua wako mpakani na kuna masoko ya DRC na Burundi, kwa hiyo, tunataka tuone mazao ya tangawizi, kahawa, ndizi, parachichi na mazao mengine yanastawishwa na kuwekezwa katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie nafasi hii kuwaomba Halmashauri zote katika Mkoa wa Kigoma kutenga maeneo ya uwekezaji ili kuweza kufanikisha lengo na azma ya Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuuweka Mkoa wa Kigoma kuwa Mkoa wa kimkakati, nakushukuru sana.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, na ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa sasa Serikali imeridhia kwamba taasisi zake zikanunue vyuma pamoja na vipuri kwenye kiwanda hicho;

Je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kuweka mpango mzuri wa kutumia chuma cha Liganga ambacho Serikali inaendelea na mchakato wa kuzalisha ili chuma hicho kitumike kuzalisha vyuma kwa ajili ya taasisi zetu za Serikali?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; Halmashauri ya Wilaya ya Hai imepeleka maombi ya kupewa eneo kwa ajili ya kuanzisha Mji Mdogo wa Kibiashara Njia Panda ya kwenda Machame. Ninaomba kufahamu, Serikali imefikia wapi katika mpango huo wa kutupa eneo la kibiashara Njiapanda ya Machame?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, ni kweli moja ya mikakati ya Serikali ni kuona rasilimali zetu nchini zinatumika kuzalisha bidhaa ambazo tunahitaji kuzitumia na hasa kwenye hizi bidhaa za chuma ambazo tunatumia fedha nyingi sana kuagiza chuma kutoka nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango wa Serikali tunavyoendelea kutimiza na kukamilisha uanzishwaji na utekelezaji wa Mradi wa Liganga na Mchuchuma tunaamini hii ndio itakuwa malighafi itakayotumika na kiwanda hiki cha KMTC.

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari kuna hatua zimeshafanyika ikiwa ni pamoja na kulipa fidia kule Mchuchuma na Liganga, na sasa tunakamilisha majadiliano na wawekezaji ili tuanze kuchimba chuma na kuhakikisha inatumika katika viwanda vyetu kikiwemo KMTC.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuhusu swali la pili; ni kweli Mheshimiwa Mbunge amekuwa akifuatilia sana kuhakikisha eneo hili la KMTC ambalo ni eneo kubwa wenzetu wa Halmashauri ya Hai wanapata eneo la kujenga Mji Mdogo katika eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari Serikali tumeshaanza kujadiliana na kupitia NDC ambao wameshaweka master plan ili kuona namna ya kua-accommodate maombi hayo ya Mheshimiwa Mbunge na wana Hai. Katika mpango huo tutaona nini tutawapa na wafanye shughuli gani zinazoendana na mahitaji mahsusi ya Kiwanda hiki cha KMTC, nakushukuru sana.
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kumshukuru Mheshimiwa Waziri na Serikali kwa ujumla kwa majibu mazuri sana na pia kwa mikakati mizuri kuhakikisha eneo hili linatumika kiuchumi kwa nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa vile hili eneo liko mkabala na TAZARA na uwanja wa kimkakati wa Songwe na barabara ya TANZAM, je, Serikali ina mpango gani wa kutenga eneo kwa ajili ya bandari kavu na kujenga bandari kavu katika eneo hilo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ajili ya umuhimu wa eneo hilo, je, ni lini Serikali itaanza upimaji na kutenga maeneo ya eneo hili muhimu?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni kweli Mkoa wa Mbeya ni moja ya mikoa ya kimkakati ambayo Serikali inauangalia kuhakikisha unawekezwa vizuri, kwa maana ya miundombinu wezeshi. Kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, ni kweli eneo hili ni la kimkakati kwa sababu linapitiwa na barabara kuu inayoenda Zambia. Pia, kuna uwanja wa ndege na reli ya TAZARA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya maeneo ambayo Serikali inaweka mkazo ni kuweka miundombinu wezeshi yote. Hili suala la bandari kavu ambalo litasaidiana na miundombinu hii mingine nalo ni moja ya maeneo ambayo tunayaangalia ili kuboresha eneo hili ili liwe sehemu ya kusaidia kukuza biashara, kuuza nje lakini pia kuingiza bidhaa ambazo zinatoka maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana tunasema eneo hili ni kwa ajili ya uwekezaji mauzo nje kwa sababu tunategemea baada ya miundombinu kukamilika na bandari kavu pia itasaidia kuuza nje, kwa maana ya kuuza bidhaa zinazozalishwa katika eneo lile kwenda nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu upimaji, katika bajeti hii inayokuja tunayoenda nayo ni moja ya maeneo maalum ambayo tutaangalia namna ya kuyapima ili yaweze kutumika kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na miundombinu mingine ikiwemo bandari kavu katika eneo hili la Mbeya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa swali la nyongeza. Kumekuwa na mpango wa muda mrefu wa Serikali kujenga kiwanda cha mbolea kinachotokana na gesi asilia ya Songosongo pale Mjini Kilwa Masoko. Kauli ya mwisho ya Serikali ni kwamba iko kwenye mazungumzo na mwekezaji. Nataka kufahamu na wana-Kilwa pia wanataka kufahamu;

Je, mpango wa kujenga kiwanda cha mbolea Kilwa-Masoko bado uko pale pale au umesitishwa?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni sahihi kabisa moja ya mipango ya Serikali ni kuhakikisha tunajenga viwanda vingi vya kutosheleza mahitaji ya mbolea nchini. Ninyi ni mashahidi, tumeshaanza kujenga hicho cha Intracom hapa Dodoma lakini pia tunacho kile cha Minjingu ambacho kinaboreshwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiki cha Kilwa-Masoko ni mahsusi kwa sababu hawa watatumia gesi asilia ambayo nayo ni muhimu sana kwa ajili ya kuzalisha mbolea ambazo zinahitajika hapa nchini. Kwa hiyo, mpango wa Serikali ni kuhakikisha tunaendelea kutafuta wawekezaji na kukamilisha mipango hiyo. Ujenzi wa kiwanda hiki cha mbolea katika eneo hili la Kilwa-Masoko utatekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Spika, Serikali inahitaji fedha kwa ajili ya miradi yake. Sasa ni kiasi gani cha fedha ambacho kinatokana na uwekezaji huo wa Serikali kwenye mashirika hayo ambacho kimeenda katika Mfuko Mkuu wa Hazina kwa sababu hiyo ni book value na what we need is actual cash.

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili, kwa kuwa bajeti yetu ni trilioni 40 na ushee na uwekezaji wetu una thamani zaidi ya trilioni 76, nini mkakati wa Serikali kutumia hisa hizo ama kuongeza mtaji ili tukopee kwa ajili ya ku-finance miradi yetu ya kimkakati? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Londo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika takwimu au hesabu za kiuhasibu kwa mwaka 2022/2023 Serikali iliweza kukusanya mapato ambayo siyo ya kikodi kutokana na gawio na michango ya mashirika haya ambayo imeenda kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali zaidi ya trilioni 1.008 lakini lengo lilikuwa ni kupata bilioni 931. Kwa hiyo, tumeweza kufanya vizuri kwa zaidi ya asilimia 108. Hizo fedha zote zaidi ya trilioni moja zimeingia katika Mfuko Mkuu wa Serikali kwa maana ya kuchangia katika bajeti.

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili la Mheshimiwa Londo, moja ya mikakati ya Serikali ambayo inaendelea sasa? Mosi, ni kufanya mageuzi katika mashirika ya umma na taasisi za Serikali ambazo Serikali imewekeza fedha huko ili ziweze kuwa na tija zaidi.

Mheshimiwa Spika, lakini pili, moja ya maelekezo ni kuona ni tunakuwa na sheria ambayo itampa mamlaka makubwa zaidi Msajili wa Hazina ili aweze kusimamia vizuri taasisi hizi ili ziweze kutoa gawio au kufanya vizuri ili fedha hizo sasa ndizo ambazo zuitaingizwa au zitaongezwa kwenye Bajeti Kuu ya Serikali kama ambavyo ulivyosema ambayo ni zaidi ya trilioni 40. Kwa hiyo, moja ya mikakati ni hiyo kwamba tuhakikishe tunasimamia vizuri ili michango na gawio zinazotokana na uwekezaji wa Serikali katika makampuni na taasisi hizi za Serikali yaweze kuwa na tija au yaongezeke zaidi, nakushukuru.
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza ni kwamba Sheria ya Kodi na Sheria za Uwekezaji hazisomani, kwa maana miradi mingi inafunguliwa lakini wawekezaji hawafanyi hivyo kwa sababu hakuna vivutio. Je, ni lini Serikali italeta hapa sheria hizo ili ziweze kupitiwa upya na ziweze kusomana? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili. Shirika la UNDP limewezesha mikoa mbalimbali kuanzisha miongozo ya uwekezaji, na kule Tanga tumeanzisha na tumeanza kuzindua miongozo ile ya uwekezaji. Ni nini sasa Serikali inafanya baada ya miongozo ile kuenea Tanzania nzima ili dhamira ile ya kuanzisha viwanda iweze kutimia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli bado kuna changamoto kwenye baadhi ya sheria na pia kwenye sera za uwekezaji. Serikali imeishaanza kupitia sheria mbalimbali za taasisi zetu, sheria za kodi, na vile vile tumeanza kuboresha au kuhuisha sera zetu mbalimbali ikiwemo Sera ya Uwekezaji, Sera ya Viwanda na Sera ya Biashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, haya niliyosema ndiyo ambayo Serikali tunafanya sasa ili kuhakikisha sera zetu na sheria zetu zinaendana na mahitaji sahihi kulingana na uhalisia wa sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kama nilivyosema, tumeshaanza kutengeneza miongozo mbalimbali ya uwekezaji na miongozo hii au makongamano haya yamekuwa yakifanyika katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Tanga. Matokeo haya katika Mkoa wa Tanga mahususi ni kutengwa kwa maeneo. Kwa mfano, maeneo yale kongwe ya maeneo ya uwekezaji 68, haya yamewekwa kwa ajili ya kujenga viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, miongozo hii sasa imeshaanza kuzaa matunda, na wawekezaji wengi wameshaanza kuonesha nia ya kuwekeza katika nchi yetu, na pia katika Mkoa wa Tanga ambako Mheshimiwa Mbunge ameuliza. Nakushukuru sana.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika, sana. Jibu la Serikali linatia matumaini. Naomba kufahamu katika mwendelezo huo wa kufufua viwanda, je, Viwanda vya Losaa Kilimanjaro, Kilimanjaro Machine Tools, Moshi Leather na Kilimanjaro Utilization viko katika mpango huo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katika mikakati ambayo tumeiweka ni pamoja na kufufua viwanda. Kiwanda hiki cha Losaa ambacho tayari tumeshapeleka Shirika letu la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Tanzania (SIDO), wameshaenda kufanya tathmini ya namna ya kufufua kiwanda kile.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Kilimanjaro Machine Tools tayari tumeshaweka mitambo mipya mbalimmbali ambayo inafanya kazi, na tunaendelea kuongeza kwa kuweka bajeti katika mwaka huu ili kununua mitambo mingine ya kuyeyusha chuma katika kuhakikisha vipuri mbalimbali vinatengenezwa katika viwanda hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunaenda hatua kwa hatua kuhakikisha kuwa viwanda vyote ambavyo vilikuwa vimekufa vinafufuliwa na hasa katika Mkoa wa Kilimanjaro. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waziri wa Mipango, Ofisi ya Rais.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka tu niongezee kwenye majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri pale kwa Mheshimiwa Eng. Ulenge kwamba, sasa hivi katika reform za Mashirika ya Umma, tunaunganisha taasisi ambazo zinahusika na uwekezaji kwa maana ya TIC na EPZA. Kwa kufanya hivyo, tutazipitia upya sheria zote husika na yale Mheshimiwa Mbunge aliyoyasema tutayaangalia. Nashukuru sana. (Makofi)
MHE. JANETH E. MAHAWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; je, Serikali haioni umuhimu wa kuwasaidia wanawake wajasiriamali wanaofanya biashara pembezoni mwa barabara hususan wale wanaokuwa na watoto wadogo kwa kuwatafutia maeneo ya muda wa kati wanasubiri kuwatengea maeneo husika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; je, ni lini sasa kituo cha uwekezaji kitaona umuhimu wa kuwasaidia kutengeneza program ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali wadogo hususan wanufaika wa mikopo ya Serikali ili fedha zile ziweze kurudi kwa kuwekezwa sehemu sahihi na kuwaonesha fursa zinazowazunguka katika maeneo yao?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuna changamoto kubwa ya maeneo ya ufanyaji biashara hasa kwa akinamama wajasiriamali wadogo na vijana ambao wanauza biashara ndogondogo na wengi wanatumia maeneo ya barabarani au kando ya barabara kuuza bidhaa zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeshaanza kutenga maeneo kwenye halmashauri na miji ambako tunahamasisha hawa akinamama na wengine ambao hawana maeneo maalum ili waweze kufanya biashara zao katika maeneo hayo ambayo ni salama na sahihi kulingana na ubora hasa kwenye vyakula.
Mheshimiwa Naibu Spika, kituo chetu cha uwekezaji kimekuwa kikitoa vivutio maalum kwa Watanzania na hasa kikilenga wajasiriamali au wafanyabiashara wanawake na vijana. Ndiyo maana kupitia program hii ya kuwezesha akinamama na vijana, Mheshimiwa Rais ameanza kuja na mpango maalum ambao kupitia mikopo hii ya 10% itakuwa ni sehemu ya kichocheo cha kuwasaidia akinamama hao ili wapate fursa za kuwekeza na kukua zaidi katika biashara zao. Nakushukuru.
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE: Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, kwa kuwa viwanda hivi tayari vilipata wawekezaji ambao walishindwa kuendeleza kama mkataba ulivyodai, je, ni hatua gani zimechukuliwa na Serikali kwa wawekezaji hawa ambao walishindwa kufanya kazi iliyokusudiwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, zao la korosho ni zao la kibiashara na linatuingizia kama Taifa fedha nyingi za kigeni, kwa kufufua viwanda hivi vya kubangua korosho tutakuwa tunaongeza thamani ya zao lenyewe, lakini pia tutakuwa tunainua uchumi wa wakulima na kuongeza pato la Taifa. Ni mkakati gani wa Serikali kuhakikisha korosho haziuzwi zikiwa ghafi badala yake kufufua viwanda vingi vya kubangua korosho ili tuweze kuinua ubora wa zao hilo na kuongeza thamani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, kwanza nachukua nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Chinguile kwa ufuatiliaji kuhusu uongezaji thamani wa mazao mbalimbali ikiwemo korosho katika Mkoa wa Mtwara.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya hatua ambazo Serikali imechukua kwa swali lake la kwanza, ni kupitia kama nilivyosema na kufanya tathmini ya viwanda vyote ambavyo vilibinafsishwa na havifanyi kazi. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuvirejesha na ndiyo maana viwanda zaidi ya 20 vimesharejeshwa na vingine tunaendelea utaratibu kukamilisha urejeshwaji, zaidi ya viwanda 33 na hiyo ndiyo hatua ya kwanza kwamba wale ambao wameshindwa kuviendeleza viwanda hivi, vyote vitanyang’anywa ili tuweze kutafuta wawekezaji wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pili, katika hilo tunataka wale ambao sasa huenda walifanya hujuma kwenye viwanda vile ambavyo walipewa vilikuwa labda na mitambo na vifaa mbalimbali vya mashine za viwanda hivyo ambavyo either wameng’oa au wamefanya hujuma yeyote, basi nao kulingana na mikataba ile nao watachukuliwa hatua mbalimbali za kisheria kulingana na mikataba ambayo tuliingia nao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la pili, ni kweli Serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha bidhaa, mazao ya kilimo yanaongezwa thamani ikiwemo korosho ambayo inaingizia Serikali fedha nyingi za kigeni. Lengo sasa ni kuhakikisha korosho inaanza kuuzwa ikiwa imebanguliwa badala ya kuwa ghafi na ndiyo maana tumeanza moja, kurejesha hivi viwanda na kuvifufua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, Wizara kupitia taasisi zetu, tunaandaa mashine, teknolojia rahisi ya viwanda vidogo vidogo ambavyo vitawasaidia wakulima wadogo wadogo na wajasiriamali waweze kubangua katika ngazi ya chini ili tuhakikishe tunauza korosho ambayo imebanguliwa badala ya kuendelea kuuza korosho ghafi, nakushukuru. (Makofi)
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, pale Njombe tuna kiwanda cha kuchakata maziwa ambacho kimefungwa kwa miaka saba na nimeuliza mara nyingi hapa ndani. Serikali inachukua hatua gani kuratibu ili kiwanda hiki kifunguliwe?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, kwanza nachukua nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Mwanyika, Mwenyekiti wangu wa Kamati ya Viwanda na Biashara ya Bunge lako Tukufu kwa kufuatilia kuhusiana na maendeleo ya viwanda katika Mkoa wa Njombe mahususi kiwanda hiki cha maziwa ambacho kwa kweli amekuwa akifuatilia na tumeshafanya hatua mbalimbali, moja, ni kujadiliana na wenzetu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia tumekaa vikao na benki kwa maana ya wadau mahususi, Benki ya Kilimo - TIDB na tumeshakubaliana kwa hatua za awali kwamba kiwanda hiki tunawatafutia wawekezaji na mwekezaji ambaye atakuwa tayari ataweza kupewa mkopo ili kuhakikisha anakifufua lakini pia kuhakikisha na viwanda vingine vya namna hii vinafufuliwa katika Mkoa wa Njombe na maeneo mengine hapa nchini, nakushukuru.
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa na mimi swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha Chai cha Chivanje kilichoko Wilayani Rungwe kimefungwa na mwekezaji. Wakulima wa Chai wa Wilaya ya Rungwe wanasumbuka sana mahali pa kupeleka hiyo chai.

Sasa je, ni lini Serikali itafungua kiwanda hicho ili wananchi na wakulima wa Wilaya ya Rungwe waendelee kupeleka chai kwenye kiwanda hicho?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na namshukuru sana Mheshimiwa Suma Fyandomo ambaye kwa kweli pamoja na mambo mengine, amekuwa akifuatilia sana kuhusiana na viwanda vya chai ambavyo vimekuwa na changamoto si tu katika Mkoa wa Mbeya kule Rungwe, lakini na maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeshaanza kufanya kazi ya kufuatilia viwanda vyote vya kuchakata chai hapa nchini ikiwemo kiwanda hiki ambacho amekisema Mheshimiwa Mbunge ili kuhakikisha, kwanza, wawekezaji hawa ambao kama wameshindwa, tuwatafute wawekezaji wengine, lakini pia kuhakikisha wakulima hawa ambao wamelima chai ambayo kwa kweli isipovunwa na kupelekwa kiwandani, inaharibika na ni hasara kubwa kwa Taifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imeshaanza kufanya kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, tunataka kuona wawekezaji hawa ambao walikubali kuchukua viwanda hivi wanafanya kazi na kuviendeleza viwanda hivi kulingana na mikataba ambayo Serikali imeingia nao.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza natoa pole nyingi kwa wananchi wa Hai kwa kuondokewa na Katibu wa Kata ya KIA.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya Serikali kufufua Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools, walituahidi eneo la Njiapanda Machame wataanzisha centre kwa ajili ya kusaidia kiwanda hiki na wananchi wanaotumia njia ya Machame, je, mchakato huu umefikia wapi?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na pia nampongeza Mheshimiwa Saashisha Mafuwe kwa ufuatiliaji wa kuendeleza eneo hili ambalo lilikuwa ni eneo la Kilimanjaro Machine Tools kwa maana ya kuhakikisha wananchi wa pale wanafaidika na uwekezaji wa kiwanda hiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa faida ya Bunge lako, lakini pia kwa Mheshimiwa Saashisha Mafuwe na wananchi wa Hai kwamba tayari tuna mkandarasi ameshapewa kazi ya kufanya tathmini na kuanza michoro kwa ajili ya eneo hili la Njiapanda ambalo tumelenga ambayo ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba tuwe na mitaa ya biashara na mitaa ya viwanda ambapo hapa sasa kunakuwa na eneo hili kwa ajili ya biashara mbalimbali ikiwemo kama vituo vya mafuta na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari kazi inafanyika na mkandarasi yuko tayari kuandaa michoro ya eneo hili kwa ajili ya eneo la kibiashara katika Halmashauri hii ya Hai.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja dogo la nyongeza lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuruhusu vyakula kutoka nje kuingizwa ndani ya nchi?

(b) Kwa kuwa chakula cha mifugo ni ghali sana jambo ambalo limekuwa ni changamoto sana kwa wafugaji; je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza kodi kwa uingizaji wa vyakula hivyo ikiwa pamoja na kupunguza tozo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, kwanza, nimpongeze sana Mheshimiwa Msongozi kwa ufuatiliaji kuhusiana na sekta hii ya mifugo hasa vyakula vya mifugo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa tumekuwa na changamoto ya vyakula vya mifugo vinavyozalishwa kwa maana ya kusindikwa hapa nchini ukiacha vile vya kawaida kwa maana ya nyasi na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba tuna nakisi kubwa ya uzalishaji wa vyakula vya mifugo katika viwanda vyetu na hasa katika maeneo mengine. Ni 55% tu ya vyakula vingi vinavyozalishwa kwenye sekta hii katika kulisha mifugo kwa maana ya kuku, lakini maeneo mengine bado tuna changamoto hiyo.

Kwa hiyo, mpaka sasa tayari Serikali inaruhusu vyakula vingi vilivyosindikwa kwa ajili ya mifugo vinaagizwa kutoka nje. Kwa hiyo, tunaendelea kufanya hivyo, lakini jitihada ni kuona tunazalisha sisi wenyewe ndani. Kwa hiyo, tayari hilo tunalifanya, kwa sababu tuna nakisi hiyo ya vyakula vya mifugo vinavyosindikwa katika viwanda vyetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na la pili, ni kweli tuna haja na tunaendelea kutoa vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi kwenye viwanda vinavyozalisha vyakula vya mifugo kwa sababu kama nilivyosema asilimia zaidi ya 60 tunaagiza kutoka nje.

Kwa hiyo, Serikali tunaendelea kuweka mipango Madhubuti ya kusaidia viwanda vya ndani na kutoa vivutio zaidi kwa wale wanaoingiza kwa sasa, lakini pia kwa wale wanaozalisha kwenye viwanda vyetu vya ndani, kwa sababu ndio haja kubwa kuona vyakula hivi vinasindikwa katika nchi yetu. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, vile viwanda ambavyo viliuzwa na Serikali kwa dhamira ya kuendeleza ubanguaji na walionunua viwanda hawakufanya ubanguaji na badala yake wamefanya maghala.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuvirejesha viwanda vile kwa sababu havijafanyiwa kazi iliyokusudiwa?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwanza nishukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo kuhusiana na uongezaji thamani kwenye sekta hii ya korosho. Kimsingi ni kweli viwanda vingi ambavyo vilikuwa vimebinafsishwa wakati ule ambavyo viko kwenye sekta ya korosho, walionunua wengi/waliobinafsishiwa hawakuviendeleza na moja ya anachokisema Mheshimiwa Katani ni kweli na tumeshasema tayari Serikali imeshaanza mchakato wa kuvirejesha viwanda vyote ambavyo viliuzwa au vilibinafsishwa na havifanyi kazi na walionunua hawajaviendeleza. Kwa hiyo, naomba tu watupatie nafasi tukamilishe mchakato huu ili tuvirejeshe Serikalini na kuwatafutia wawekezaji wengine.
MHE. MICHAEL M. KEMBAKI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Serikali ambayo bado mimi sijaridhika nayo, ukienda katika maduka mengi ukitafuta bidhaa genuine huwezi kuipata. Je, maana yake ni kwamba Serikali haioni bidhaa hizi katika maduka yetu na katika soko ambalo lipo katika mitaa yetu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kumekuwa na viwanda vingi bubu ambavyo vipo katika mitaa yetu, vingine vinatengeneza oil chafu ambayo tunatumia kuweka kwenye magari yetu. Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba viwanda hivi ambavyo vinatengeneza bidhaa ambazo hazikidhi viwango vinadhibitiwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza namshukuru sana Mheshimiwa Kembaki kwa kufuatilia masuala yanayohusiana na bidhaa bandia au bidhaa ambazo hazikidhi mahitaji katika soko letu. Ni kweli bado tuna changamoto ya bidhaa bandia, lakini siyo kweli pia kwamba hakuna bidhaa genuine katika maduka yetu kama ambavyo amesema Mheshimiwa Mbunge. Bidhaa zote zipo na niseme kuna watu ambao wanatumia nafasi hii moja kuingiza bidhaa hizi ikiwa ni sehemu ya kukwepa kodi na kufanya mambo mengine ambayo hayafai.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, bidhaa genuine zipo lakini pia na bidhaa bandia zipo na ndiyo maana tuna Sheria ya Ushindani ili kuhakikisha tunafuatilia na kukagua kwenye maduka ili tubaini. Hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa kwenye bidhaa ambazo ni bandia na tunashukuru kwamba wafanyabiashara na wazalishaji wanashirikiana na Serikali ili kutambua bidhaa ambazo siyo genuine katika maduka yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na swali la pili, viwanda bubu ambavyo vinaingiza na kuzalisha bidhaa bandia tayari hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa, moja ikiwa ni kuwakamata na kuchukua hatua kali dhidi yao. Haya yamekuwepo siyo tu katika bidhaa alizozitaja Mheshimiwa Mbunge, lakini pia hata kwenye vinywaji.

Kwa hiyo, kuna wengine wanachukua vifungashio vya viwanda fulani halafu wanaweka bidhaa humo na kuanza kuuza mitaani. Kwa hiyo hatua zimekuwa zikichukuliwa ili kukabiliana na changamoto hii ya viwanda bubu, nakushukuru sana.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, naomba ufafanuzi zaidi kwenye jibu lako, hapo ulipoanzia; “Aidha, kwa wale waliokwishaanza wenyewe na kuwa na changamoto ya mikopo tunahimiza wawasiliane na Mfuko wa Pembejeo.” Sijaelewa connection yake na swali langu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni kwa nini Serikali kupitia Wizara ya Kilimo isione umuhimu kwamba wale vijana wanaopata mafunzo ya BBT wawe wanafundishwa na wanakuwa attached kule walikotoka kwenye halmashauri zao ili waweze kueneza ule ujuzi kwenye halmashauri badala ya kuwabeba na kuwapeleka kwenye block farming?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Jesca, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza sana kwa kufuatilia mpango huu wa kujenga kesho iliyobora kwa vijana katika sekta ya kilimo. Katika BBT kuna maeneo manne ambayo Serikali inayafanyia kazi. Moja, ni hayo ya block farming ambalo liliulizwa kwa maana ya mashamba makubwa; sehemu ya pili ya financing kwa maana ya mikopo kwa wale ambao wanakuwa wamepata mafunzo hayo; sehemu ya tatu ni ya ugani ambayo nayo pia tunaiangalia; na sehemu ya nne ni ya kuhakikisha maji yanapatikana kwenye mashamba hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kuhusiana na ufafanu wa eneo la kwanza ni kwamba kulingana na swali lake kwamba tumefanya makubaliano na JKT, lakini kuna vijana wengine ambao walipita JKT hawatakuwa kwenye huu mpango. Kwa hiyo, tunasema wale ambao watakuwa wamepita BBT lakini hawapo kwenye huu mpango ambao tumekubaliana MOU na JKT maana yake na wao tunachukulia wameshapata ujuzi. Sasa kwa sababu kwenye mpango huu hawa watapata fedha kwa maana ya ukopeshwaji watakapokuwa wamepita kwenye block farming hizi, sasa wale ambao hawako kwenye utaratibu huu maana yake tunawashauri wapate financing kupitia Mfuko huu wa Pembejeo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na sehemu ya pili, kama nilivyosema ni kwamba tayari tunawaandaa vijana kulima kisasa kwenye mashamba haya ya block farming. Wengine ambao watapenda kwenda zaidi ni wale ambao watapata mafunzo ya ziada ya ugani na hawa tutawaelekeza warudi kwenye maeneo waliyotoka kwa wakulima. Pia, hata wale wengine ambao wanaweza kuwa hawajapata mafunzo haya mahususi ya ugani pia tunachukua wazo hili kwamba nao wakipata nafasi sasa badala ya kukaa kwenye mashamba haya ya block farms kubwa wanaweza wakarudi wakashirikiana na wakulima kule vijijini walikotoka ili kueneza ule ujuzi walioupata kuwasaidia wakulima wengine, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ABDUL YUSUF MAALIM: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa kiasi gani TARI (Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Bara) na ZARI (Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar) zinashirikiana katika kutatua changamoto za kilimo kwa pamoja kupitia TEHAMA? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni tafiti za aina gani mpaka sasa zimefanyika katika teknolojia ya habari na mawasiliano ili kutoa matokeo chanya? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nijibu maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia kuhusiana na matumizi ya TEHAMA na hasa ushirikiano wa taasisi zetu za utafiti kwenye kilimo kwa maana ya TARI kwa upande wa Tanzania Bara na ZARI kwa upande wa Zanzibar. Taasisi zetu, ikiwemo hizi zimekuwa zikishirikiana sana katika maeneo mbalimbali katika utafiti, kupeana na kujengana uwezo kati ya wataalamu kutoka ZARI na TARI.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikijibu maswali hayo kwa pamoja, hivi karibuni mwaka 2022 taasisi hizi zilifanya tafiti kwa ushirikiano katika mazao ya mihogo na mpunga ambapo moja kupitia Wakala wa Kimataifa wa Atomiki waone namna gani tunaweza kupunguza athari ya maradhi ya mihogo kwa maana ya michirizi kahawia ambayo inaathiri sana zao la muhogo ambalo linalimwa Tanzania Bara lakini pia na kule Visiwani.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia katika mpunga (mchele) ambapo wameweza kufanya utafiti ili kuona namna gani ya kuongeza uzalishaji wa mpunga (mchele) ambao unalimwa kati ya Tanzania Bara na kule Visiwani ili kupunguza baadhi ya athari au kuboresha mavuno yanayotoka katika maeneo haya ya kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo moja, tunashirikiana sana kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa taasisi zote kama nilivyosema TARI na ZARI. Pili, tafiti zote ambazo zinatumia TEHEMA zimefanyika kwa kushirikiana na tutaendelea kuboresha ushirikiano huu kadiri muda unavyoendelea, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nilitaka niulize swali kuhusiana na hiyohiyo TEHAMA, katika Halmashauri ya Masasi hususan katika Jimbo la Lulindi kuna maeneo mengi ambayo wakulima wanapata tofauti. Mtu ana ekari 100 lakini ukienda kwenye kompyuta anaonekana hana shamba na mwingine hana shamba lakini ukifika kwenye kompyuta anaonekana ana ekari labda 50. Je, ni lini Serikali itahakiki upya maeneo hayo ili kila mmoja ajue umiliki wake? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: nakushukuru sana. Namshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia taarifa hizi ambazo wakati mwingine kweli kutokana na changamoto za kiteknolojia kuna wakati inawezekana kweli taarifa za mtu mmoja zinahamia kwa mtu mwingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tumeanza kuboresha TEHAMA kwenye sekta ya kilimo na maeneo mengine. Changamoto hizi ndogondogo tunaendelea kuzifanyia kazi na tuendelee kupewa taarifa na nitaonana naye baada ya hapa ili aweze kutupa taarifa mahususi ili wataalamu wetu waweze kufuatilia na kuweza kurekebisha changamoto hiyo, nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Kilimo.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Nataka tu niwaombe Watu wa Lindi, Pwani, Ruvuma na Mtwara, changamoto iliyojitokeza kama wiki moja iliyopita kwenye Mfumo wa Ugawaji wa Ruzuku ya Pembejeo. Tumeshawaagiza watu wa eGA wana-update na kuzi-retrieve data za mwaka jana na watagawiwa wakulima kutokana na data base ya mwaka jana na update iliyofanyika mwaka huu itaendelea kufanyiwa cleaning. (Makofi)
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali kwa niaba ya Mheshimiwa Esther Malleko. Pamoja na mipango ambayo ameeleza hapa ya Serikali, Serikali inachukua hatua gani za haraka sasa kuhakikisha kwamba tunapata masoko nje ya nchi ikizingatiwa kwamba Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa wingi wa mifugo ili nyama yetu iweze kupata bei iliyo nzuri kwenye masoko ya dunia.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Serikali ilituelekeza Jimbo la Hai kuhakikisha tunaanza kuwekeza pesa kidogo kwa ajili ya kujenga machinjio ya kisasa pale KIA. Je, Serikali ipo tayari sasa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Hai kujenga machinjio ya kisasa ili sasa nyama iweze kutengenezwa pale KIA na ipakiwe na ndege kwa Mikoa yote ya Kanda ya Kaskazini.
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kuendelea kufuatilia kuhusiana na sekta hii ya mifugo hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli moja ya hatua tunazozifanya kama Serikali ni kutafuta masoko nje ya nchi na kupitia Taasisi yetu ya Maendeleo ya Biashara Nje (TANTRADE), tumeshaanza kuongea na kuingia makubaliano na baadhi ya nchi nje kwa ajili ya kupata masoko ya nyama ikiwemo Saudi Arabia, Qatar, Iran, China na nchi nyingine. Ambazo hizo kwa mfano, Saudi Arabia tu wanahitaji tani laki saba za nyama ya Ng’ombe kwa mwaka, kwa hiyo tumeshakubaliana nao tutaanza kuendelea kufanya hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Iran wanataka tani 70,000 kwa kila wiki, sasa tunachokifanya ni kuhakikisha tunawawezesha wananchi wetu wafuge kisasa ili nyama hizi zipate ithibati ili ziweze kuingia kwenye masoko hayo, lakini pia kwenye soko letu la Afrika tayari nako tumeshaanza kuingia ili kupata masoko ya nyama kwa maana ya kuuza nyama ambayo imechinjwa badala ya kuuza mifugo.

Kuhusu suala la pili ni kweli moja ya maeneo ambayo tunayafanyia kazi ya kimkakati ni kuongeza miundombinu wezeshi ambayo itafanya nyama yetu iwe na ubora unaotakiwa. Moja, ni majosho lakini kama nilivyosema ufugaji wa kisasa na machinjio ya kisasa. Sasa tumeshaanza kukaribisha wawekezaji kwenye machinjio ya kisasa lakini nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa sababu tayari katika Jimbo lake la Hai wameshaanza mchakato wa kujenga machinjio hayo ya kisasa, Serikali italeta fedha ili kuunga mkono machinjio hayo ili yaweze kukidhi ubora wa kutoa nyama yenye ubora kuingia kwenye masoko ya kimataifa, nakushukuru. (Makofi)
MHE. AMEIR ABDALLA AMEIR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri kwa ruhusa yako ningeomba kuuliza suala moja la nyongeza lenye kifungu (a) na (b) kama hivi ifuatavyo:-

(a) Kwa kuwa moja kati ya majuku ya msingi sana ya TBS na ZBS ni kulinda usalama wa chakula kwa mlaji. Swali langu ni kwamba je, tathimini ikoje sasa juu ya huu uwepo wa vifaa vyenye teknolojia ya kisasa vyenye uwezo wa kuchambua sampuli kwa uharaka sana wa vyakula vyetu ili kumuhakikishia Mtanzania kwamba anakula chakula chenye usalama na uhakika?

(b) Swali langu la pili ni kwamba je, kuna jitihada gani zozote au viashiria vyovyote vya mafanikio mpaka sasa kwa wafanyabiashara ambao wana-standard mark ya ZBS kuweza kupata soko la biashara zao kikanda na Kimataifa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na kwanza na mimi nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge Mheshimiwa Ameir kwa kufuatilia sana kuhusiana na mashirikiano na ubora wa bidhaa kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuhakikishie wewe, lakini na Bunge lako Tukufu kwamba Tanzania imekuwa kati ya nchi ambazo zina maabara ya kisasa sana ya kupima ubora na viwango kwa ajili ya usalama katika chakula na bidhaa nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa yako tu wakati Kamati yako ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma ilipotembelea TBS ilijionea dhahiri maabara ya kisasa katika jengo ambalo tumejenga kwa zaidi ya shilingi bilioni 20 na maabara ya kisasa ya zaidi ya shilingi bilioni 500 ambazo hizi zinatumika kupima ubora kwa ajili ya kuhakikisha bidhaa na hasa chakula zinakuwa na usalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tuna teknolojia za kisasa na vifaa vya kisasa kabisa ambavyo vina hithibati ya Kimataifa vinavyopima ubora kwa ajili ya usalama wa chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la pili kuhusiana na bidhaa zenye ubora ambazo kutokana na ushirikiano wa ZBS na TBS ambazo zinazaliwa kutoka kule Zanzibar, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwanza kwamba sisi kama nchi ni Wajumbe wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afika (SADC) ambapo kule kuna tuzo za Kimataifa kwa maana ya Kanda hiyo SADCAS na katika tuzo hizo za ubora tumekuwa tukishirikisha ZBS na TBS na wajasiriamali na wazalishaji wengi kutoka Zanzibar wamekuwa vinara wa kuonesha bidhaa bora zinazokidhi matakwa na soko la Kimataifa lakini la kikanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano katika tuzo hizo moja ya kampuni ambazo zimepata tuzo ni Kampuni ya Zanzibar Milling Cooperation kupitia unga wake maarufu sana wanasema special boflo ambao umekuwa ukipata tuzo karibu miaka yote kwenye mashindano hayo. Hata wajasiriamali wadogo wa kawaida kwa mfano Zanzibar Zaidat Product amekuwa pia naye anapata tuzo nyingi za uzalishaji kwa bidhaa zake katika tuzo hizo ambazo zinashirikisha mataifa mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ZBS na TBS wanashirikiana kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa Tanzania Bara, lakini na Zanzibar zinakuwa na ubora kwa ajili ya kupata soko la Kimataifa, lakini na ndani ya nchi, nakushukuru.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali lililotangulia lilikuwa linahusu masuala ya watumiaji na mikopo. Sasa ni lini Serikali kutokana na umuhimu wa watumiaji itatenganisha masuala ya ushindani na masuala ya watumiaji ili tuweze kuwalinda watumiaji wa Tanzania?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Tanzania tunazalisha bidhaa. Ili kuuza ile bidhaa, watumiaji inabidi wanunue. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhamasisha watumiaji wa Tanzania wanunue na kutumia bidhaa na huduma zilizozalishwa hapa nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba sheria hii tuliyoitaja inasimamia ushindani wa haki pamoja na kuwalinda walaji. Uzoefu unaonesha kwamba nchi nyingi duniani zinatumia sheria hii moja ambayo inachukua maeneo mawili kwa maana ya ushindani wa haki katika soko, lakini pia kupitia humo kumlinda mlaji, kwa sababu tunapitia sheria hii, pale ambapo tunaona kuna haja ya kutenganisha kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameshauri, basi Serikali haitasita kufanya hivyo na tunachukua ushauri wake, lakini pia na wadau wengine ambao watatoa maoni wakati tunaihuisha au tunarekebisha Sheria hii Na. 8 ya Mwaka 2003.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili, ni kweli sisi kama Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, tayari tuna mikakati mbalimbali. Moja ya kaulimbiu yetu katika kuhakikisha tunakuza Sekta ya Viwanda na Uzalishaji nchini ni, “Nunua Tanzania, Jenga Tanzania,” kwa maana ya nunua bidhaa zilizozalishwa Tanzania ili uweze kuijenga nchi yako Tanzania.

Mheshimiwa Spika, tunaendelea kufanya hivyo, lakini kwa kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zina ubora unaotakiwa ili ziweze kushindana na bidhaa zinazotoka nje, kwa sababu ili kuhakikisha Watanzania wanapenda bidhaa zao za ndani, lazima ziwe na ubora ule ambao unalingana na bidhaa nyingine kutoka nje ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunaendelea kuhakikisha tunatangaza hilo, lakini kuhakikisha bidhaa zetu zinazalishwa katika ubora unaotakiwa, nakushukuru.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Serikali ilifanya Sensa ya Makazi na Watu mwezi Agosti mwaka 2022 na takribani shilingi 350,000,000,000 zilitumika kwa shughuli hii. Sasa nataka kumuuliza Mheshimiwa Waziri, ni takwimu gani ambazo wanazihitaji kuzifanya nje na takwimu ambazo Sensa ya Makazi ilizifanya? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Mji huu wa Mtambaswala umeunganishwa na Mji wa Msumbiji kwenye Daraja la Umoja na Daraja hili lilikuwa kwenda sambamba na ujenzi wa bandari kavu katika Mji wa Nangomba. Je, ni lini bandari kavu hii itajengwa ili kuchochea uchumi wa mji huo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Ally Yahya Mhata kwa kuwa amekuwa akifuatilia sana suala hili la mpakani kwa maana ya mpaka ule wa Tanzania na Msumbiji kupitia pale Mtambaswala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana tumesema takwimu hizi ambazo zipo ikiwemo za sensa ambayo imefanyika hapa nchini na tafiti nyingine tunataka tuone katika mipaka yote ikiwemo Mtambaswala tunajenga kitu kinaitwa One Stop Border Post (vituo vya mpakani). Hivi vituo sasa ndiyo lengo baada ya kuona takwimu sahihi ambazo tunazo kupitia mpaka huu tunajenga hicho kituo OSBP pale ili kuchangamsha uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo takwimu hizo ndizo zinatusaidia kufanya maamuzi au utekelezi wa mipango ya Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ni kweli katika Halmashauri ya Nanyumbu kuna Daraja lile la Umoja ambalo linaunganisha kupitia pale Nangomba na kwenda Msumbiji. Ndiyo maana tunasema moja ya mambo ambayo tunayafanya ni kuongeza kwanza biashara katika mpaka ule na huo ndiyo sasa utatupelekea kujenga na hii ambayo tunalenga kuwa na bandari kavu ambayo itasaidia sana kuhakikisha uchumi kwa sababu mahitaji makubwa kwa wenzetu pale ni kuchukua bidhaa kutoka kwetu. Kwa hiyo tutumie fursa hii ili tuweze kufaidika na soko zuri lililopo kwa majirani zetu pale Msumbiji kwa maana ya kupitia mpaka huu wa Mtambaswala. Nakushukuru.
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE: Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, kwa kuwa viwanda hivi tayari vilipata wawekezaji ambao walishindwa kuendeleza kama mkataba ulivyodai, je, ni hatua gani zimechukuliwa na Serikali kwa wawekezaji hawa ambao walishindwa kufanya kazi iliyokusudiwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, zao la korosho ni zao la kibiashara na linatuingizia kama Taifa fedha nyingi za kigeni, kwa kufufua viwanda hivi vya kubangua korosho tutakuwa tunaongeza thamani ya zao lenyewe, lakini pia tutakuwa tunainua uchumi wa wakulima na kuongeza pato la Taifa. Ni mkakati gani wa Serikali kuhakikisha korosho haziuzwi zikiwa ghafi badala yake kufufua viwanda vingi vya kubangua korosho ili tuweze kuinua ubora wa zao hilo na kuongeza thamani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, kwanza nachukua nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Chinguile kwa ufuatiliaji kuhusu uongezaji thamani wa mazao mbalimbali ikiwemo korosho katika Mkoa wa Mtwara.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya hatua ambazo Serikali imechukua kwa swali lake la kwanza, ni kupitia kama nilivyosema na kufanya tathmini ya viwanda vyote ambavyo vilibinafsishwa na havifanyi kazi. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuvirejesha na ndiyo maana viwanda zaidi ya 20 vimesharejeshwa na vingine tunaendelea utaratibu kukamilisha urejeshwaji, zaidi ya viwanda 33 na hiyo ndiyo hatua ya kwanza kwamba wale ambao wameshindwa kuviendeleza viwanda hivi, vyote vitanyang’anywa ili tuweze kutafuta wawekezaji wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pili, katika hilo tunataka wale ambao sasa huenda walifanya hujuma kwenye viwanda vile ambavyo walipewa vilikuwa labda na mitambo na vifaa mbalimbali vya mashine za viwanda hivyo ambavyo either wameng’oa au wamefanya hujuma yeyote, basi nao kulingana na mikataba ile nao watachukuliwa hatua mbalimbali za kisheria kulingana na mikataba ambayo tuliingia nao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la pili, ni kweli Serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha bidhaa, mazao ya kilimo yanaongezwa thamani ikiwemo korosho ambayo inaingizia Serikali fedha nyingi za kigeni. Lengo sasa ni kuhakikisha korosho inaanza kuuzwa ikiwa imebanguliwa badala ya kuwa ghafi na ndiyo maana tumeanza moja, kurejesha hivi viwanda na kuvifufua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, Wizara kupitia taasisi zetu, tunaandaa mashine, teknolojia rahisi ya viwanda vidogo vidogo ambavyo vitawasaidia wakulima wadogo wadogo na wajasiriamali waweze kubangua katika ngazi ya chini ili tuhakikishe tunauza korosho ambayo imebanguliwa badala ya kuendelea kuuza korosho ghafi, nakushukuru. (Makofi)
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, pale Njombe tuna kiwanda cha kuchakata maziwa ambacho kimefungwa kwa miaka saba na nimeuliza mara nyingi hapa ndani. Serikali inachukua hatua gani kuratibu ili kiwanda hiki kifunguliwe?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, kwanza nachukua nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Mwanyika, Mwenyekiti wangu wa Kamati ya Viwanda na Biashara ya Bunge lako Tukufu kwa kufuatilia kuhusiana na maendeleo ya viwanda katika Mkoa wa Njombe mahususi kiwanda hiki cha maziwa ambacho kwa kweli amekuwa akifuatilia na tumeshafanya hatua mbalimbali, moja, ni kujadiliana na wenzetu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia tumekaa vikao na benki kwa maana ya wadau mahususi, Benki ya Kilimo - TIDB na tumeshakubaliana kwa hatua za awali kwamba kiwanda hiki tunawatafutia wawekezaji na mwekezaji ambaye atakuwa tayari ataweza kupewa mkopo ili kuhakikisha anakifufua lakini pia kuhakikisha na viwanda vingine vya namna hii vinafufuliwa katika Mkoa wa Njombe na maeneo mengine hapa nchini, nakushukuru.
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa na mimi swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha Chai cha Chivanje kilichoko Wilayani Rungwe kimefungwa na mwekezaji. Wakulima wa Chai wa Wilaya ya Rungwe wanasumbuka sana mahali pa kupeleka hiyo chai.

Sasa je, ni lini Serikali itafungua kiwanda hicho ili wananchi na wakulima wa Wilaya ya Rungwe waendelee kupeleka chai kwenye kiwanda hicho?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na namshukuru sana Mheshimiwa Suma Fyandomo ambaye kwa kweli pamoja na mambo mengine, amekuwa akifuatilia sana kuhusiana na viwanda vya chai ambavyo vimekuwa na changamoto si tu katika Mkoa wa Mbeya kule Rungwe, lakini na maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeshaanza kufanya kazi ya kufuatilia viwanda vyote vya kuchakata chai hapa nchini ikiwemo kiwanda hiki ambacho amekisema Mheshimiwa Mbunge ili kuhakikisha, kwanza, wawekezaji hawa ambao kama wameshindwa, tuwatafute wawekezaji wengine, lakini pia kuhakikisha wakulima hawa ambao wamelima chai ambayo kwa kweli isipovunwa na kupelekwa kiwandani, inaharibika na ni hasara kubwa kwa Taifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imeshaanza kufanya kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, tunataka kuona wawekezaji hawa ambao walikubali kuchukua viwanda hivi wanafanya kazi na kuviendeleza viwanda hivi kulingana na mikataba ambayo Serikali imeingia nao.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza natoa pole nyingi kwa wananchi wa Hai kwa kuondokewa na Katibu wa Kata ya KIA.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya Serikali kufufua Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools, walituahidi eneo la Njiapanda Machame wataanzisha centre kwa ajili ya kusaidia kiwanda hiki na wananchi wanaotumia njia ya Machame, je, mchakato huu umefikia wapi?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na pia nampongeza Mheshimiwa Saashisha Mafuwe kwa ufuatiliaji wa kuendeleza eneo hili ambalo lilikuwa ni eneo la Kilimanjaro Machine Tools kwa maana ya kuhakikisha wananchi wa pale wanafaidika na uwekezaji wa kiwanda hiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa faida ya Bunge lako, lakini pia kwa Mheshimiwa Saashisha Mafuwe na wananchi wa Hai kwamba tayari tuna mkandarasi ameshapewa kazi ya kufanya tathmini na kuanza michoro kwa ajili ya eneo hili la Njiapanda ambalo tumelenga ambayo ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba tuwe na mitaa ya biashara na mitaa ya viwanda ambapo hapa sasa kunakuwa na eneo hili kwa ajili ya biashara mbalimbali ikiwemo kama vituo vya mafuta na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari kazi inafanyika na mkandarasi yuko tayari kuandaa michoro ya eneo hili kwa ajili ya eneo la kibiashara katika Halmashauri hii ya Hai.