MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kuanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya kimkakati ya Kyazi Kayanga – Missenyi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kujenga Barabara ya Kyazi Kayanga – Missenyi kwa kiwango cha lami ili kuboresha usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Kata za Bwanjai, Kitobo, Bugandika na maeneo jirani. Hivyo, katika mwaka wa fedha 2026/2027, Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kuifanyia usanifu na kupata gharama za kuijenga kwa kiwango cha lami. Pindi gharama za ujenzi kwa kiwango cha lami zikijulikana, Serikali itaanza ujenzi huo kwa bajeti zinazofuata.
Mheshimiwa Spika, katika kuiwezesha barabara hiyo kupitika na kurahisisha usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa kata hizo, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imetenga shilingi milioni 59 kwa ajili ya kuifanyia matengenezo.