Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 33 | Industries and Trade | Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara | 288 | 2022-05-30 |
Name
Dr. Charles Stephen Kimei
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. CHARLES S. KIMEI aliuliza;
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa soko la Kimataifa katika eneo la Lokolova mpakani mwa Tanzania na Kenya?
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA, alijibu:-
Mheshimiwa Spika, nakushukuru na kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Charles Stephen Kimei, Mbunge wa Vunjo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Moshi imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 140 katika eneo la Lokolova kwa ajili ya ujenzi wa soko la mpakani. Hatua inayofuata ni kupata hati miliki ya eneo hilo na hatimaye kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya soko hilo, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved