Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 37 | Foreign Affairs and International Cooperation | Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki | 328 | 2022-06-03 |
Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini Pakistan?
Name
Amber. Mbarouk Nassor Mbarouk
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanza kufanya utafiti wa kuangalia uwezekano wa kufungua Ubalozi nchini Pakistan. Utafiti huo unahusisha kuangalia faida za kiuchumi zilizopo nchini humo ambazo Tanzania inaweza kunufaika nazo ikiwa ni pamoja na kuainisha gharama za ufunguzi wa Ubalozi huo na uendeshaji wake.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved