Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 38 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 337 | 2022-06-06 |
Name
Elibariki Emmanuel Kingu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Magharibi
Primary Question
MHE. ELIBARIKI I. KINGU aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itawasilisha Muswada wa Sheria unaozuia Polisi kukamata na kuwashikilia watuhumiwa kabla ya kukamilisha upelelezi?
Name
Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Songea Mjini
Answer
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Elibariki Immanuel Kingu, Mbunge wa Singida Magharibi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura Na. 20 kupitia Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 1 ya mwaka 2022 mwezi Machi, 2022, ambapo kwa sasa Sheria imeweka masharti ya kutofungua mashtaka mpaka upelelezi utakapokamilika, isipokuwa kwa makosa makubwa tu.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved