Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 38 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 339 | 2022-06-06 |
Name
Maimuna Salum Mtanda
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Newala Vijijini
Primary Question
MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga mabweni pamoja na miundombinu mingine katika Chuo cha VETA Kitangali?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maimuna Salum Mtanda, Mbunge wa Newala Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimwa Naibu Spika, Serikali inatambua mahitaji ya miundombinu ya kufundishia na kujifunzia ikiwemo mabweni katika Chuo cha VETA Kitangali ambapo mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali ilitoa Sh.299,267,002.00 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, jengo la utawala na vyoo na ukarabati wa karakana ya ushonaji, umeme pamoja na uwekaji wa samani na vifaa.
Mheshimwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na jitihada za kutafuta fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya miundombinu ikiwemo mabweni, bwalo, nyumba za Walimu na uzio katika Chuo cha VETA Kitangali.
Mheshimwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved