Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 13 | Sitting 10 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 152 | 2023-11-10 |
Name
Amina Ali Mzee
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AMINA ALI MZEE aliuliza: -
Je, Serikali ina mkakati gani wa kuliwezesha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kujiendesha kibiashara?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linatekeleza majukumu yake kikamilifu kama chombo cha utangazaji cha umma. Serikali ipo katika mkakati wa kukamilisha utungaji wa Sheria ya TBC ya mwaka 2023, itakayowezesha kuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato. Aidha, TBC inazo chaneli za kimkakati kwa ajili ya kuongeza mapato ikiwemo TBC2, TBC Online, TBC FM na Radio za Jamii Dodoma na Arusha, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved