Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 13 | Sitting 10 | Lands, Housing and Human Settlement Development | Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi | 153 | 2023-11-10 |
Name
Jafari Chege Wambura
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Rorya
Primary Question
MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:-
Je, lini Serikali itafanya maboresho ya Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995?
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jafari Wambura, Mbunge wa Rorya, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, rasimu ya Sera ya Taifa ya mwaka 1995, Toleo la 2023 liliwasilishwa na kujadiliwa katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri, tarehe 18 Agosti, 2023. Aidha, Wizara imekamirisha maboresho ya rasimu ya sera kwa kuzingatia maoni ya Baraza la Mawaziri.
Mheshimiwa Spika, hatua inayofuata ni rasimu hiyo ya sera kujadiliwa katika Mkutano wa Kazi wa Baraza la Mawaziri kwa tarehe itakayopangwa, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved