Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 49 | Information, Culture, Arts and Sports | Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo | 433 | 2022-06-22 |
Name
Antipas Zeno Mgungusi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Malinyi
Primary Question
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza:-
Je, kwa nini Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania hawafundishi nje ya nchi hata katika Ukanda wa Afrika Mashariki au Nchi za SADC?
Name
Pauline Philipo Gekul
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Tanzania ina makocha 19 wenye viwango vya CAF A Diploma ambao wanakidhi viwango vya kufundisha nje ya nchi. Hata hivyo, makocha hawa hawafanikiwi kupata fursa za kufundisha nje ya nchi kutokana na historia ya elimu walizonazo. Hivyo basi, Wizara kwa kushirikiana na TFF wanaratibu mpango wa kutoa mafunzo ya Ukocha kwa wanafunzi wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya michezo ikiwemo Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, Butimba na Vyuo Vikuu nchini ili kupata Makocha wenye sifa.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved