Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 69 2024-04-15

Name

Vincent Paul Mbogo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA K.n.y MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itazigawa Kata za Chala, Kala na Ninde Nkasi kwa kuwa ni kubwa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, uanzishwaji wa maeneo mapya ya utawala huzingatia Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka za Wilaya, Sura ya 287 na Mamlaka za Miji, Sura ya 288, pamoja na Mwongozo wa Uanzishwaji wa Maeneo ya Utawala wa Mwaka 2014.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua uhitaji wa kugawa baadhi ya maeneo mapya ya utawala, lakini kwa sasa Serikali imetoa kipaumbele katika kuboresha na kukamilisha miundombinu kwenye maeneo ya kiutawala yaliyopo ili yaweze kutoa huduma kwa ufanisi zaidi na baadaye kuendelea na maeneo mengine kwa kufuata taratibu na vigezo vilivyoainishwa. Ahsante.