Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 9 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 145 2024-02-09

Name

Dr. Josephat Mathias Gwajima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kawe

Primary Question

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA aliuliza: -

Je, nini maandalizi ya Serikali kuhusu teknolojia ya kutengeneza watu wenye akili bandia na kulinda maadili ya Kitanzania?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia napenda sasa kujibu swali la Mheshimiwa Askofu Josephat Mathias Gwajima, Mbunge wa Kawe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia ikiwemo matumizi ya akili bandia na teknolojia nyingine zinazoibuka. Katika kuendana na mabadiliko hayo, Serikali imeandaa mwongozo wa matumizi ya teknolojia mpya na zinazoibukia pamoja na kuanza mapitio ya Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka, 2003 ili kuweka usimamizi na mazingira thabiti ya ulinzi wa Taifa dhidi ya matumizi ya teknolojia zinazoibukia ikiwemo matumizi ya akili bandia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuwekeza katika miundombinu na vifaa stahiki pamoja na kuandaa wataalamu katika ngazi mbalimbali. Kwa mfano, imeanza maandalizi ya ujenzi wa Vyuo Mahiri viwili vya TEHAMA ambapo kimoja kitajengwa Eneo la Nala hapa Jijini Dodoma na kingine Eneo la Buhigwe, Mkoani Kigoma. Vilevile inaendelea na taratibu za kuanzisha Kituo cha Umahiri katika utafiti na ubunifu ikiwemo teknolojia ya akili bandia na teknolojia nyingine zinazoibukia katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, katika mitaala ya elimu iliyoboreshwa, wanafunzi wataanza kufundishwa masuala ya TEHAMA kuanzia elimu ya msingi. Pamoja na jitihada hizo, Serikali inaendelea kusimamia maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa ujumla wake, kwa kuweka mazingira yenye kuhakikisha kuwa haiathiri maadili ya kitanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)