Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 14 | Sitting 13 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 217 | 2024-02-15 |
Name
Agnes Elias Hokororo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani kwa watumishi wanaokaimu nafasi kwa muda mrefu katika Vyuo vya FETA ikiwemo Mtwara?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibuĀ¬: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Agnes Elias Hokororo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kutokana na changamoto za kimuundo (organization structure) ya Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Fisheries Education and Training Agency - FETA) watumishi wengi waliokuwa wanakaimu kwa muda mrefu walishindwa kuthibitishwa katika nafasi zao. Changamoto hiyo ya kimuundo imeisha baada ya Muundo mpya wa FETA kuidhinishwa mwezi Oktoba, 2022.
Mheshimiwa Spika, hivi sasa Serikali inaendelea na taratibu za kujaza nafasi za uongozi katika Muundo huo mpya ikiwemo kuwafanyia upekuzi wote wanaokaimu ili wakikidhi vigezo wathibitishwe katika nafasi hizo au kama hawakidhi vigezo wateuliwe watumishi wengine kujaza nafasi hizo.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved