Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 52 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 461 | 2022-06-27 |
Name
Dr. Thea Medard Ntara
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:-
Je, kuna mpango gani wa kukarabati Chuo Kikuu cha Dodoma na Vyuo vingine ambavyo vilijengwa na kuonekana vina dosari?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Thea Medard Ntara, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Vyuo Vikuu nchini huanzishwa kwa kuzingatia taratibu na miongozo maalum inayotambulika na Sheria ya Vyuo Vikuu nchini.
Mheshimiwa Spika, kupitia utekelezaji wa Mradi wa Higher Education for Economic Transformation (HEET), Serikali itaboresha miundombinu kwa kujenga na kukarabati Taasisi 23 za Elimu ya Juu ikiwemo Vyuo Vikuu vya Umma ambapo Chuo Kikuu cha Dodoma ni miongoni mwa vyuo hivyo.
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved