Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 43 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 562 2024-06-07

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza: -

Je, lini Serikali itawapatia mbegu bora za ufuta wananchi wa Wilaya ya Kilwa waweze kuzalisha ufuta mwingi kwani wanatumia mbegu za asili?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuwahamasisha wakulima wa zao la ufuta katika Wilaya ya Kilwa kutumia mbegu bora ili kuongeza uzalishaji. Katika msimu wa mwaka 2023/2024 Serikali ilisambaza bure jumla ya tani 10 za mbegu bora ya ufuta kwa wakulima wa Kilwa na kuweka mashamba ya mfano ya kilimo bora cha ufuta katika Kata za Likawage na Mandawa. Aidha, Serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imetoa elimu kwa wakulima katika Kata za Miguruwe na Mandawa kuhusu umuhimu wa matumizi ya mbegu bora na kanuni za kilimo bora cha zao la ufuta ili kuongeza tija. (Makofi)