Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 42 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 542 2024-06-06

Name

Athumani Almas Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Kaskazini

Primary Question

MHE. ATHUMAN A. MAIGE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaipatia Hospitali ya Wilaya ya Uyui gari la wagonjwa?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imepeleka magari mawili ya kubebea wagonjwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mwezi Februari, 2024. Magari hayo yamepangwa katika Hospitali ya Wilaya Uyui na Kituo cha Afya Igalula.

Mheshimiwa Spika, magari hayo yanatumika kutoa huduma kwa mfumo wa Kaskedi ambapo Vituo vya Afya vya Loya, Tura, Upuge na Mabama pamoja na zahanati ambazo hazina magari ya kubebea wagonjwa vitahudumiwa.