Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 46 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 595 2024-06-12

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga vituo vya afya katika Tarafa ya Negezi ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi kwani tarafa hiyo ina kituo kimoja tu cha afya?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tarafa ya Negezi ina kata nane ambapo kata mbili kati ya hizo zina vituo vya afya. Vituo hivyo ni Kituo cha Afya Negezi kilichopo Kata ya Negezi ambacho kilipokea shilingi milioni 500 mwaka 2021/2022 na Kituo cha Afya Nhobola kilichopo Kata ya Talaga ambacho ni cha muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya kwenye kata za kimkakati kote nchini zikiwemo kata zitakazokidhi vigezo katika Tarafa ya Negezi.