Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 19 Good Governance Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 245 2024-05-06

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI K.n.y. MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: -

Je, ni kwa nini wanufaika wa TASAF wanalazimika kufuata fedha benki hata fedha hiyo ikiwa ni kidogo?

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa malipo kwa wanufaika wa TASAF unafanyika kwa njia kuu tatu: kwanza, kupitia akaunti ya Benki; pili, kupitia akaunti ya simu ya mkononi; na tatu, kwa malipo taslimu kupitia kwa wakala au katika kituo cha malipo. Uamuzi wa njia gani ambayo mlengwa atapenda kulipwa, unabaki kuwa wa kwake mwenyewe mlengwa ambaye anatambulika wakati wa uandikishaji wa daftari la walengwa.