Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 19 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 255 2024-05-06

Name

Abeid Ighondo Ramadhani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kukomesha mapenzi ya jinsia moja nchini pamoja na ukatili dhidi ya watoto?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara za kisekta inaratibu utekelezaji wa mikakati ya kukabiliana na tatizo la mmomonyoko wa maadili na ukatili dhidi ya watoto. Mikakati hiyo ni pamoja na:-

(i) Kusimamia utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto pamoja na kuanzisha na kuimarisha madawati ya ulinzi na usalama wa mtoto katika shule za msingi, sekondari na vyuo; na

(ii) Kusimamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) pamoja na Mpango wa Taifa wa Kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana Balehe (NAIHA). Aidha, Wizara itaendelea kutoa elimu kwa umma na kuongeza afua za malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto pamoja na kuimarisha taasisi za familia kwa lengo la kupunguza au kumaliza kabisa changamoto ya mmomonyoko wa maadili nchini, ahsante.