Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 30 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 394 2024-05-21

Name

Yustina Arcadius Rahhi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. YUSTINA A. RAHHI aliuliza: -

Je, kuna mbwa wangapi nchini?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa taarifa ya sampuli ya Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mwaka 2020, nchi yetu ilikadiriwa kuwa na mbwa 2,776,918. Aidha, kupitia taarifa hiyo mikoa iliyoongoza kwa mbwa wengi ni Geita 302,879, Mwanza 287,270 na Tabora 243,768.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inaendelea kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kuhakikisha takwimu sahihi za mifugo ikiwemo mbwa zinapatikana kwa wakati ili kuwezesha mipango ya Serikali ya kuendeleza Sekta ya Mifugo.