Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 9 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 145 2024-09-06

Name

Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza:-

Je, lini Serikali itachakata tafiti zinazofanywa na wanafunzi ili kuchochea ugunduzi na ukuaji wa teknolojia katika sekta mbalimbali nchini?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kufanya utafiti na kutumia matokeo ya utafiti ili kuongeza maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini, pamoja na juhudi nyingine, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu, kuweka vifaa na vifaa stahiki pamoja na kuandaa wataalamu wa utafiti kwa kuwawezesha kupata mafunzo ya muda mfupi na mrefu ili tafiti zinazofanyika vyuoni zikiwemo tafiti za wanafunzi ziwe na mchango katika maendeleo ya teknolojia na ubunifu nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imewezesha kuanzishwa kwa vituo atamizi vipya 17 kwa ajili ya kukuza na kuendeleza ubunifu unaozalishwa nchini. Vituo atamizi vilivyopo katika Taasisi za Elimu na Mafunzo vinasaidia kuendeleza ubunifu na matokeo ya utafiti yanayotokana na kazi zinazofanywa na wanafunzi katika taasisi hizo. Hivyo, wanafunzi wanapata fursa ya kutumia elimu wanayoipata kwa maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla. Mafanikio yaliyotokana na kuanzishwa kwa vituo hivyo ni pamoja na kuanzishwa kwa makampuni mapya 94 yanayotokana na ubunifu na hivyo kutoa ajira za moja kwa moja kwa vijana takribani 600. Nakushukuru.