Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 9 | Home Affairs | Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi | 153 | 2024-09-06 |
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza: -
Je, lini Vituo vya Kipolisi Wilaya za Kipolisi Tarime, Sirari, Utegi na Nyamwaga vyenye hadhi kama Kituo cha Mtumba Dodoma vitajengwa?
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inajenga kituo cha Polisi Daraja “A” Tarime ambacho kitagharimu kiasi cha fedha shilingi 1,200,000,000 na katika mwaka wa fedha 2024/2025 zimetengwa fedha kiasi cha shilingi 350,000,000 kuanza ujenzi huo. Aidha, Serikali itaviboresha Vituo vya Polisi Sirari, Utegi, na Nyamwaga ili viwe na hadhi ya Vituo vya Polisi vya Wilaya kwa kuweka mifumo na miundombinu ya kisasa ili kurahisisha utekelezaji wa kazi za polisi kwa mujibu wa matakwa ya haki jinai na kuzingatia mahitaji ya msingi ya makundi yote ya binadamu na tathmini kwa ajili ya utekelezaji huo umeshaanza kufanyika. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved