Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 38 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 494 2024-05-31

Name

Rose Cyprian Tweve

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ROSE C. TWEVE aliuliza: -

Je, kigezo cha mtihani wa kuandika kabla ya kujiunga na Vyuo vya Ufundi (VETA) ni cha lazima kwa wanafunzi wa mafunzo kwa vitendo?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inatoa mafunzo ya ufundi stadi kwa nadharia kwa 30% na vitendo kwa 70%.

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa stadi za kuandika, kusoma na kuhesabu katika utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) hutoa mitihani ya majaribio (aptitude test) wa kujiunga kwenye vyuo vyake. Hii ni kwa sababu kuna umuhimu wa kubaini endapo wanaotaka kujiunga na vyuo vya VETA wanamudu stadi za KKK ikiwa ni kigezo cha kujiunga na vyuo vya ufundi stadi na pia kwa ajili ya muendelezo wa kielimu kwa hapo baadae pindi mwanafunzi akihitaji kujiendeleza zaidi. Ninakushukuru sana.