Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 38 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 500 | 2024-05-31 |
Name
Najma Murtaza Giga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza:-
Je, kwa nini Serikali isiweke kwenye mpango wa maendeleo wa kila mwaka kipaumbele cha kudhibiti vitendo vya udhalilishaji watoto nchini?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imejumuisha masuala yote ya ukatili na udhalilishaji wa watoto katika Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ambapo tathmini ya utekelezaji wa mpango kazi wa kwanza inaonesha jumla ya shilingi bilioni 30.5 zimetumika katika utekelezaji wa afua za kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na huku Serikali ikiwa imetumia shilingi bilioni 25 na wadau wa maendeleo wametumia shilingi bilioni 5.5 za fedha hizo. Aidha, Serikali itaendelea kutenga fedha za utekelezaji wa Mpango Kazi wa Pili wa MTAKUWWA ikiwa ni jitihada za kuendelea kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto hapa nchini, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved