Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 1 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 9 2024-08-27

Name

Ameir Abdalla Ameir

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. AMEIR ABDALLA AMEIR aliuliza:-

Je, maboresho mangapi ya mitaala ya elimu yamefanyika katika vipindi tofauti na nini matarajio ya mitaala mipya katika ubunifu na uvumbuzi?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya mitaala nchini yamefanyika katika vipindi sita tangu tupate Uhuru. Aidha, kutokana na dira na malengo ya elimu katika ngazi mbalimbali, maboresho ya mitaala ya mwaka 2023 yamejikita katika ujenzi wa umahiri wa msingi katika kuwasiliana, kushirikiana, ubunifu, fikra tunduizi na utatuzi wa matatizo, ujuzi wa kidijitali, maadili na uzalendo. Hizi zote ni stadi za karne ya 21 kwa kuzingatia falsafa ya elimu ya kujitegemea. Hivyo, maudhui ya ngazi mbalimbali ya elimu yamejikita pamoja na masuala mengine kujenga ubunifu na uvumbuzi miongoni mwa wanafunzi, nakushukuru.