Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 50 2024-08-30

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

Ujenzi wa Barabara ya Kisomboko hadi
Zahanati ya Mawela – Moshi

MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Barabara ya kutoka Kisomboko kwenda Zahanati ya Mawela – Moshi Vijijini kwa kiwango cha changarawe?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Kisomboko – Mawela Zahanati inakadiriwa kuwa na kilomita tatu, barabara hiyo ambayo haijasajiliwa katika mtandao wa barabara zinazohudumiwa na TARURA ni mpya. Barabara hii ni moja kati ya barabara zinazoelekea katika Zahanati ya Mawela ikiwa ni pamoja na Barabara za Uru Seminari – Kifumbuni ambayo ni kilomita 4.5 na Molangi – Kisarika High School – AMCOS kilomita tatu ambayo kwa mwaka 2024/2025 itafanyiwa matengenezo ya kawaida kwa gharama ya shilingi milioni 900.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2024/2025 Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika itahakikisha Barabara ya Kisomboko – Zahanati ya Mawela inafanyiwa matengenezo ili iweze kupitika na kutoa huduma kama inavyokusudiwa. (Makofi)