Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 5 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 110 | 2024-07-29 |
Name
Iddi Kassim Iddi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Msalala
Primary Question
MHE. IDDI K. IDDI aliuliza:-
Je, lini Serikali itatenga fedha kumalizia bweni la wasichana Shule ya Sekondari Jana katika Halmashauri ya Msalala?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa bweni katika Sekondari ya Jana ambapo imeendelea kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo kutatua changamoto hiyo. Ujenzi wa bweni la wasichana katika shule hiyo umefikia hatua ya kozi za juu ya lenta ambapo jumla ya shilingi milioni 47 kutoka kwenye Mfuko wa Jimbo na CSR kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu zimekwishatumika. Kazi hiyo imefanyika chini ya usimamizi wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Jana.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imetenga shilingi milioni 50 za mapato ya ndani kwa ajili ya kuanza ukamilishaji wa bweni hilo. Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga na kukamilisha miundombinu ya elimu yakiwemo mabweni kadiri ya upatikanaji wa fedha. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved