Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 2 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 22 2024-08-28

Name

Ally Juma Makoa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kondoa Mjini

Primary Question

MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka fedha za ujenzi wa uzio wa Shule ya Wasichana Kondoa ili kuimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, mwaka 2021/2022 mpaka 2023/2024, Serikali Kuu imepeleka shilingi milioni 600.8 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo vyumba vya madarasa nane, mabweni mawili, matundu ya vyoo 14 na vitanda 660 katika Shule ya Wasichana Kondoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa uzio kwa ajili ya ulinzi wa mali na wanafunzi wa bweni. Hata hivyo, kwa sasa kipaumbele cha Serikali Kuu ni ujenzi wa miundombinu ya msingi inayowezesha kuongeza nafasi za udahili wa wanafunzi.