Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 2 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 29 | 2024-08-28 |
Name
Leah Jeremiah Komanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Meatu
Primary Question
MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga jengo la kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Meatu?
Name
Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilosa
Answer
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania imeendelea kuimarisha majengo ya Mahakama katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kujenga majengo mapya na ya kisasa na kukarabati majengo chakavu. Wilaya ya Meatu ni moja ya wilaya ambazo zina majengo ya Mahakama lakini jengo lake ni chakavu na siyo la kisasa. Kwa mujibu wa mpango wa ujenzi wa majengo ya Mahakama, Wilaya ya Meatu itajengewa jengo la kisasa katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved