Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 53 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 679 2024-06-25

Name

Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. MARYAM AZAN MWINYI aliuliza:-

Je, lini Serikali itaweka vifaa tiba katika majengo ya huduma za mama na mtoto kwenye halmashauri mbalimbali nchini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali za halmashauri. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 hadi 2023/2024, jumla ya shilingi bilioni 186.3 zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vikiwemo vifaa vya huduma ya mama na mtoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2024/2025, Serikali imetenga shilingi bilioni 66.7 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba ambapo kipaumbele kimewekwa kwenye vifaa tiba vya huduma za mama na mtoto kwenye vituo vyenye upungufu mkubwa zaidi kote nchini. Ahsante.