Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 1 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 4 | 2024-10-29 |
Name
Anastazia James Wambura
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA aliuliza:-
Je, lini Serikali itapeleka Walimu wa kutosha wa Shule za Msingi na Sekondari Mkoani Mtwara?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikiajiri walimu wa shule za msingi na sekondari kila mwaka kulingana na upatikanaji wa fedha. Katika kipindi cha mwaka 2020/2021 hadi 2022/2023, Serikali iliajiri walimu 29,879 wakiwemo walimu 16,598 wa shule za msingi na walimu 13,281 wa shule za sekondari. Mkoa wa Mtwara ulipangiwa walimu 968 wakiwemo walimu 502 wa shule za msingi na walimu 466 wa shule za sekondari.
Mheshimiwa Spika, tarehe 20 Julai, 2024 Serikali ilitangaza ajira za walimu 11,015 ambapo mchakato wa ajira ukikamilika watapangiwa vituo vya kazi. Mkoa wa Mtwara utapata walimu 502 wakijumuisha walimu 184 wa shule za msingi na 318 wa shule za sekondari.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved