Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 1 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 19 2024-10-29

Name

Maimuna Ahmad Pathan

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: -

Je, lini wananchi waliowekewa alama ya X kwenye barabara ya Masasi mpaka Liwale watalipwa fidia?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuwalipa wananchi wote ambao wamewekewa alama ya X kwenye barabara ya Masasi mpaka Liwale. Serikali itahakikisha inalipa fidia kwa mujibu wa sheria kabla ya ujenzi wa barabara hiyo kuanza, ahsante.