Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 7 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 115 | 2024-09-04 |
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza:-
Je, nini kimesababisha Mradi wa Maji Mbangara –Lulindi kutoanza licha ya kutengewa fedha kwa misimu mitatu mfululizo?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekamilisha usanifu wa kina wa Mradi wa Maji Kijiji cha Mbagara kilichopo Jimbo la Lulindi, Wilayani Masasi. Kazi zinazotarajiwa kutekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya kuendeshea mitambo (pump house), ujenzi wa matanki sita yenye jumla ya ujazo wa lita 800,000, ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 165, ujenzi wa vituo 24 na vioski 51 vya kuchotea maji. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha za utekelezaji wa mradi huo.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika jitihada za muda mfupi, Serikali imekarabati pamoja na kufanya upanuzi wa Skimu za Maji za Lupaso na Lulindi na hivyo kuboresha huduma ya maji safi na salama katika vijiji 38 vya Jimbo la Lulindi.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved