Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 88 2024-11-05

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA K.n.y. MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza:-

Je, Halmashauri ya Mtwara Mikindani ilikusanya kiasi gani cha ushuru wa magari yanayosafirisha Makaa ya Mawe kwa mwaka 2022/2023?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushuru wa makaa ya mawe katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara, Mikindani, hutozwa kwa makaa ya mawe yanayosafirishwa nje ya nchi tu kwa kiwango cha shilingi 20,000 kwa tani 30. Ushuru huo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara, Mikindani, ulianza kutozwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 ambapo jumla ya shilingi milioni 754 zimekusanywa. Ahsante.