Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 5 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 69 | 2024-11-04 |
Name
Francis Isack Mtinga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Mashariki
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaigawa Kata ya Mwangeza kuwa Kata za Ikulu, Mwangeza na Dominila na Vitongoji vya Midimbwi, Nyeri na Mulumba kuwa Vijiji?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa kuanzisha maeneo mapya ya utawala upo kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa Sura ya 287 na 288 pamoja na Mwongozo wa Uanzishwaji wa Maeneo ya Utawala wa Mwaka 2014. Aidha, utaratibu umeainishwa kwa kuanza na vikao vya ngazi za vijiji, Baraza la Madiwani, Kamati ya Ushauri ya Wilaya na Kamati ya Ushauri ya Mkoa kisha kuwasilishwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa tathmini ya vigezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kwa sasa Serikali imetoa kipaumbele kuboresha na kukamilisha miundombinu msingi kwenye maeneo ya kiutawala yaliyopo ili yaweze kutoa huduma kwa ufanisi zaidi na baadaye kuendelea na maeneo mengine kwa kufuata taratibu na vigezo vilivyoainishwa.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved