Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 6 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 96 | 2024-11-05 |
Name
Ussi Salum Pondeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chumbuni
Primary Question
MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu ya uzalendo kwa wananchi wakati Taifa lipo katika mageuzi makubwa ya uchumi?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Serikali imekuwa ikitoa elimu ya uzalendo kwa wananchi kupitia majukwaa mbalimbali kama vile vyombo vya habari na matamasha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, Serikali kwa kutambua umuhimu wa kutoa elimu ya uzalendo kwa kizazi cha sasa na baadaye, ilifanya maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 pamoja na Mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu wa mwaka 2023 ambapo katika maboresho hayo elimu ya uzalendo imetiliwa mkazo na itakuwa ikifundishwa katika Somo la Historia ya Tanzania na Maadili kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita. Somo hili litabeba maudhui yanayolenga kumjenga Mtanzania kuwa mzalendo na mwajibikaji anayefahamu historia, desturi, mila na maadili ya nchi yake.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved