Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 6 Finance and Planning Wizara ya Fedha 99 2024-11-05

Name

Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza kodi ya uingizaji wa vyakula vya samaki nchini?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Jacqueline Msongozi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, vifaa vinavyoagizwa kutoka nje na watu wanaojihusisha na ufugaji wa samaki na kilimo ambavyo Kamishna ameridhika kuwa ni kwa matumizi katika sekta ya ufugaji wa samaki, vimeondolewa Ushuru wa Forodha kwa mujibu wa kifungu cha 15(a) cha Sehemu B ya Jedwali la Tano ya Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani imetoa msamaha wa VAT kwenye uingizwaji wa vyakula vya mifugo ikiwemo vyakula vya samaki vinavyotambulika kwa HS Code 23.09, chini ya utaratibu wa utozaji ushuru wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.