Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 5 Finance and Planning Wizara ya Fedha 76 2024-11-04

Name

Salum Mohammed Shaafi

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Chonga

Primary Question

MHE. SALUM MOHAMMED SHAAFI aliuliza: -

Je, akaunti ya fedha ya pamoja ya Muungano imeshafunguliwa?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali mbili zinaendelea na mashauriano juu ya mapendekezo yaliyowasilishwa na Tume ya pamoja ya fedha kuhusu utaratibu wa kudumu wa kuchangia matumizi na kugawana mapato ya Muungano. Uamuzi wa pamoja utakapofikiwa na pande zote mbili za Muungano ndiyo utakaowezesha kufunguliwa kwa akaunti ya fedha ya pamoja, ahsante.