Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 5 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 86 | 2024-11-04 |
Name
Conchesta Leonce Rwamlaza
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanzisha Maabara ya kupima Sampuli za Magonjwa ya Mifugo Mkoani Kagera?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, uanzishwaji wa Maabara ya Kupima Sampuli za Magonjwa ya Mifugo Mkoani Kagera lipo kwenye mpango wa muda mrefu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kama ilivyo pia katika Mikoa mingine. Aidha, utambuzi wa sampuli za magonjwa ya mifugo kwa Mkoa wa Kagera kwa sasa unafanyika kupitia maabara ya Kanda iliyopo Mkoani Mwanza ambayo ni miongoni mwa maabara 11 zilizopo nchini na zinamilikiwa na Serikali, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved