Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 25 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 325 | 2024-05-14 |
Name
Justin Lazaro Nyamoga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilolo
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza:-
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara kutoka Kijiji cha Idete hadi Mgeta?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Idete - Mngeta ni barabara inayojumuisha barabara za Idete - Itonya kilometa 9, Itonya - Mhanga kilometa 4.5 na Mhanga - Mngeta kilometa 17 hivyo kufanya barabara ya Idete - Mngeta kuwa na urefu wa kilometa 30.5.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuifanyia matengenezo barabara hiyo ambapo katika mwaka 2022/2023 kilometa 13 zimetengenezwa katika kipande cha Mhanga - Mgeta kwa gharama ya shilingi milioni 282.5. Kwa mwaka 2023/2024 zimetengwa shilingi milioni 100 kwa ajili ya kuendelea kukiimarisha kipande cha Mhanga - Mngeta. Aidha, imetengwa shilingi milioni 456.4 kwa ajili ya matengenezo ya kipande cha Kimala – Idunda - Mhanga - Itonya (kilomita 22) na sasa Mkandarasi yupo uwandani anaendelea na kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuhudumia miundombinu ya barabara za Wilaya ya Kilolo ili kuhakikisha inaendelea kuwa katika hali nzuri kwa kuendelea kutenga fedha kulingana na bajeti.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved