Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 135 2024-11-08

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza: -

Je, lini Barabara ya Getifonga – Mabogini hadi Kahe itajengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imefanya usanifu wa Barabara ya Getifonga – Mabogini hadi Kahe, urefu wa kilometa 31.25 ambapo mpango uliopo ni kuanza na ujenzi wa kilometa 12.0 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi bilioni 15.9. Juhudi za kupata fedha kwa ajili ya ujenzi huo zinaendelea kufanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia fedha za Mradi wa RISE kwa ajili ya kuondoa vikwazo, shilingi milioni 780 zilitengwa katika mwaka 2023/2024 ili kufanya maboresho ya kilometa 1.2 iwe tayari kupokea matabaka ya lami. Kwa sasa kazi hii inaendelea na imefikia 42% ya utekelezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika mwaka 2024/2025, Serikali kupitia fedha za mafuta (tozo) imetenga shilingi milioni 775 kwa ajili kujenga kwa kiwango cha lami mita 800 ambapo kwa sasa kazi hizi ziko katika hatua ya ununuzi.