Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 136 2024-11-08

Name

Bahati Keneth Ndingo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbarali

Primary Question

MHE. BAHATI K. NDINGO aliuliza: -

Je, Serikali ina mikakati gani kuhakikisha barabara za vijijini ndani ya Wilaya ya Mbarali zinajengewa mitaro ili kuzuia uharibifu?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa mifereji ya maji ya mvua kwenye barabara zikiwemo za Wilaya ya Mbarali ambapo katika mwaka 2019/2020 mifereji ilijengwa katika Barabara za Rujewa Mjini ambazo ni NMB, Mbarali – Mferejini (mita 180) kwa shilingi 9,000,000, CCM Wilaya – Rujewa (mita 280) kwa shilingi 14,000,000, Kenny – Mferejini (mita 340) kwa shilingi 17,000,000, Amini – Posta (mita 200) kwa shilingi 10,000,000. Aidha, Barabara za Igawa Mjini ambazo ni Oleneno – Shule ya Msingi Igawa (mita 200) kwa shilingi 10,000,000, Mlidi – Minzi (mita 150) kwa shilingi 7,500,000 na Pangamawe – Tankini (mita 250) kwa shilingi milioni 12.5.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2024/2025 TARURA Wilaya ya Mbarali inatarajia kujenga mifejeji yenye urefu wa mita 1,000 kwa gharama ya shilingi 65,000,000 kwenye barabara ya Komba – Machicho iliyopo Igawa inayojengwa kwa kiwango cha lami.