Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 137 2024-11-08

Name

Geoffrey Idelphonce Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Masasi Mjini

Primary Question

MHE. GEOFFREY I. MWAMBE aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Miradi ya TACTIC kwenye Halmashauri ya Mji wa Masasi?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa TACTIC umegawanyika katika makundi matatu na Halmashauri ya Mji wa Masasi ipo katika kundi la tatu ambalo utekelezaji wake utaanza kwa usanifu kufanyika mwezi Novemba, 2024 kwa kipindi cha miezi nane. Baada ya usanifu, zabuni ya kumpata mkandarasi itatangazwa mwezi Julai, 2025 na baada ya kumpata mkandarasi, ujenzi utaanza mwezi Oktoba, 2025.