Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 21 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 278 2024-05-08

Name

Ng'wasi Damas Kamani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza:-

Je, Serikali imefikia hatua gani katika kuwapatia vijana 400 vifaa vya kutengeneza vihenge visivyoruhusu hewa kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya 2020 - 2025?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC) imewapatia vijana 420 vifaa vya kutengeneza Vihenge vya Chuma visivyopitisha hewa vyenye thamani ya shilingi 548,479,105 ambapo kila kijana alipatiwa seti moja iliyojumuisha Arc Welding Machine, Angle Grinder Machine, Portal Grilling Machine, Steel Divider, Tape Measure, Try-square, Centre Push, Hand Hacksaw na Safety Goggles.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Vifaa hivi vilizinduliwa na kugawanywa kwa vijana 420 na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane tarehe 08/08/2023 katika viwanja vya maonesho vya John Mwakangale, Mbeya. Ahsante sana.