Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 49 2024-11-01

Name

Aziza Sleyum Ally

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AZIZA S. ALLY aliuliza:-

Je, Vibali vya Ujenzi hutolewa baada ya muda gani tangu mwombaji aombe kupewa kibali?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa vibali vya ujenzi unasimamiwa na Mwongozo wa Utoaji wa Vibali vya Ujenzi na Usimamizi wa Ujenzi wa Majengo wa Mwaka 2018. Mwongozo huo umeweka muda na taratibu za utoaji wa vibali kulingana na aina ya jengo linaloombewa kibali.

Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha Mfumo wa Kielektroniki wa Utoaji wa Vibali vya Ujenzi wa TAUSI na umeanza kutumika Julai, 2024 kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambapo halmashauri 47 tayari zinatumia katika kutoa vibali vya ujenzi na halmashauri nyingine zitaanza kutumia. Kupitia mfumo huo, muda wa kutoa vibali umepungua, ambapo kwa sasa kibali kinaweza kutolewa ndani ya siku moja.