Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 33 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 428 2024-06-03

Name

Abdallah Jafari Chaurembo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia ujenzi wa Mfereji wa Shegho ambao unaathiri Wakazi wa Kata ya Kiburugwa Jimbo la Mbagala?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfereji wa Shegho una urefu wa kilomita 4.645 ambapo ulianza kujengwa kilomita 3.345 za awali katika awamu ya kwanza, kuanzia mwaka 2015 na kukamilika 2023. Kipande cha urefu wa kilomita 1.3 kufika Mto Mzinga hakikujengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa kipande kilichobaki cha kilomita 1.3 utatekelezwa kupitia Mradi wa DMDP, awamu ya pili, ambao hatua za kumpata mshauri mwelekezi atakayesimamia ujenzi huu zinaendelea. Serikali itaendelea kuihudumia miundombinu ikiwemo mifereji, Wilaya ya Temeke, kulingana na upatikanaji wa fedha.