Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 34 Water and Irrigation Wizara ya Maji 445 2024-05-27

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Mabwawa ya Maji ya Salama A, Rakana, Mihingo, Tingirima, Kambubu na Nyaburundu – Bunda?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere, Mbunge wa Jimbo la Bunda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 imetenga fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa bwawa la Mihingo ambapo hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 95. Vilevile, Serikali inakarabati Bwawa la Salama A sambamba na kufanya usanifu wa kina wa Bwawa la Tingirima.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mabwawa ya Kambubu, Nyaburundu na Rakana, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali itafanya mapitio ya usanifu zilizowahi kufanyika katika mabwawa hayo pamoja na kufanya tathmini ya athari za kimazingira na kijamii. Lengo ni kujiridhisha na mawanda ya mradi na kulipa fidia kwa waathirika watakaopitiwa na miundombinu ya mradi kabla ya kuanza utekelezaji wake.

Mheshimiwa Spika, mapitio hayo ya usanifu yatasaidia kubainisha kama maeneo hayo yanafaa kujengwa bwawa kati ya moja au mawili makubwa yatakayohudumia vijiji vyote kwa kutumia mitambo iliyonunuliwa na Serikali.